Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Samia Joint Mock Examination 2021/2022

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  1. Andika Nambari yako ya usajili na darasa katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
  2. Tia sahihi yako kishauandike tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu
  3. Jibu maswali yote.
  4. Majibu yote yaandikwe katika nafasi ulizoachiwa katika kijitabu hiki cha maswali.
  5. Majibu yote lazima yaandikwe katika lugha ya Kiswahili.
  6. Karatasi hii ina kurasa 12 zilizopigwa chapa.
  7. Hakikisha kuwa kurasa zote zimepigwa chapa

 

  1. UFAHAMU (ALAMA 15)
    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuatia.
    Nchi yetu imeraukia mawio ya machafuzi ya kisiasa baada ya shughuli za uchaguzi zilizogonga mwamba mkuu. Hili lilijiri baada ya Tume ya uchaguzi kukosa kuendeleza uchaguzi kwa njia inayostahili. Jambo hili lilizaa msukosuko wa kisiasa usiomithilishwa katika historia ya taifa letu.
    Hivi sasa wakenya wanaishi kwenye kambi za watu wasio na makazi. Hiki ni kinaya kikuu kwani matukio haya yamezuka baada ya miongo minne ya uhuru. Vilio vya wakenya vimeshamiri na kupaasa sauti vikalalamikia kukosa makazi, lishe na ndoa kusambaratika. Ndoa zimevunjika baada ya’wenyeji’ kuwatimua ‘wageni na damu kumwagika.
    Kenya imekuwa miongoni mwa mataifa yanayowapa faraja wakimbzi kutoka nchi jirani zinazokumbua na vita vya wenyewe. Vita katika Somalia vimesababishwa na koo mbali zinazopigania uongozi hali ambayo imekwamisha shughuli zote za kiuchumi.
    Hali ya sasa ya Kenya imechochewa na msururu wa sababu; ukabila na tama ya uongozi zilionekana wazi katika miundo ya vyma viku vya kisiasa na katika kampeni zao. Wakenya walipiga kura kwa misingi ya kikabila upande ukitazamia mtu wao kushinda uchaguzi huo.
    Kwa upande mwingine , viongozi hao kutokana na tamaa ya uongozi walikuwa wamesmua kushinda uchaguzi huo kwa vyovyote vile. Leo tunavuna matunda ya siasa za ukabila na tamaa ya mamlaka.
    Maelfu ya wakenya ni makimbizi nchini na katika nchi jirani ya Uganda. Wakenya hao wanahitaji msaada wa chakula na mahitaji mengine ya kimsingi. Serikali na shirika la msalaba mwekundu zimefanya juhudi kuwasaidia wahasiriwa lakini kuna tetesi kwamba ubaguzi umejipenyeza katika ugawaji wa msaada huo.
    Waliopewa jukumu la kugawa msaada huo ni sharti waelewe kuwa waathiriwa ni wakenya wenzao na hawafai kubaguliwa kwa misingi ya makabila yao. Matukio kama hayastahili asilani katika taifa hili.
    Twahitaji zao aali la viongozi wasiojitwika ubabe bali wawe watumishi wa wananchi wanastahili kutupilia mbali tamaa za kujilimbikiza mali na kung’ang’ania uongozi. Pia katiba inafaa irekebishwe. Wakenya wanastahili kuelimishwa kuhusu undugu na utaifa. Fauka ya haya masuala yanayohusiana na hatimiliki za ardhi yanafaa kutandaraukiwa kwa dhati.
    1. Taja madhara manne ya ukabila. (al.4)
    2. Shughuli za ugawaji wa misaada zimekumbwa na changamoto gani. (al.2)
    3. Eleza tofauti ya chanzo cha vita nchini Somalia na Kenya. (al.2)
    4. Mwandishi anatoa mapendekesho gani ya kutatua tatizo hili la ukabila. (al.3)
    5. Eleza kinaya cha maisha ya wakenya kwa sasa. (al.2)
    6. Eleza maana ya maneno haya yalivyotumika katika kifungu cha ufahamu. (al.2)
      1. Mawio.
      2. Tandaraukiwa kwa dhati.
  2. UFUPISHO
    Soma makala haya kishaujibu maswali yanayofuata.
    Tangu asili –na jadi nasikitika kusema kuwa tumekuwa tukiwakandamiza mabanati wetu na kuwateka bakunja ilhali wameonyesha kuwa mikono miepesi. Siku mojanilikuwa nikitembea na babu yangu mkongew tulipoliona tapo lawanawake kwambali. “ Funika kombe mwanaharamu apite!” akininong’onezea, wanahusudu uwezo tu. “ Kwa uchungu watu wa fikira sikuelewa yakini alichotazamia lakini hii leo nang’amua. Basi imenibidi kutupilia mbali dhana hiyo hafidhina kwani asifuye mvua aghalabu imemnyea.
    Jina nzuri hung’aa gizani na bila shaka majina ya wanawake watu yameremeta kama nyota.
    Kwanza, wamejitolea mhanga katika nyanja za masomo. Si baba ambao wamehitimu kutoka vyio vikuu vya humu nchini na vile vile vya ughaibuni na kujipa shahada kadha wa kadha. Wamepata ujuzi wa kutosha katika maswala tatizo kama vile udaktari na uanasheria. Hivi ni kumaanisha kuwa tuna madkari shupavu, basi tuwape nafasi tusiendelee kuwa nyuma mithili ya koti katika kipengele hiki muhimu cha maisha. Ni wanawake ndio, lakini mgalla muue na haki umpe!
    Vile vile wanawake wenu wamejitokeza kifua mbele katika hatamu za uongozi. Mfano mwafaka
    katika serikali yetu, ambapo mawaziri ni wanawake. Nani asiyewafahamu, Cecily Kariuki, Racheal Omamo na Amina Mohamed? Wote wanafanya bidii za mchwa kustawi maisha ya wananchi. Ingekuwa ida na inadi kama tungewanyima viongozi hawa nafasi hizo na bila shaka jambo hili lingeathiri sana ujenzi wa taifa kwani ujuzi ndio nguzo ya kila kitu.
    Kwa upande mwingine wanawake ni walezi waliomakinika.Kama tujuavyo udongo hupatilizwa ungali maji na usipoziba ufa huna budi kujenga ukuta. Nani ndio wamepokezwa jukumu mahiri la malezi? Nina zetu hujitolea kwa hali na mali kuwakuza watoto kwa tajriba zinazofaa na kuwafunza maisha ndiposa wasifunzwe na ulimwengu. Aliyemakinika atakubaliana name kuwa malezi si jambo la kufanyiwa mzaha katika harakati za ujenzi wa taifa. Na huu wajibu wote ni wa mwanamke.
    Siwezi kuwasahau wanamke wanamuziki. Sote twaelewa kuwa kwa uchumi kama wetu, kutengemea kazi ya kuajiriwa ni kutaka muhali, chambilicho wahenga mchagua jembe si mkulima. Nashukuru wanadada wetu kwa kutia bidii katika uwanja wa mziki badla ya kuwa viruka njia. Kupitia kwa sauti nyororo kama kindanda wameweza kuwavutia hata watalii kuitembelea nchi yetu na kutuachia pesa za kigeni. Nawahimiza wengi kama iwezekanavyo wajaribu bahati yao………….jambo hili linajuza sana katika ujenzi wa taifa imara.
    Katika kitengo cha spoti, waawake wamejizatiti vilivyo na kutokea wanashati kweli kweli.
    Wamezika katika kaburi la sahau kuwa mchezo ni uawala wa wanaume. Kwa mfano katika michezo ya Olimpiki au jimuiya ya madola timu zetu za wanawake zimefanya vyema na kurudi nyumbani na nishani chungu nzima.Kwa wale wasiohusika katika michezo ningewasihi wajikakamue kisabuni basi wasiwaonee kijicho wenzao, kwani nyote ya mwenzio usilalie mlango wazi. I wapo tutazingatia ufanisi katika michezo, taifa hili halina budi kuendeleza uchumi wake.
    Kwa kukunja jamvi, ningetaka kusisitiza kuwa hata ingawa jitihada haziondoi kudura, wanawake wetu wamefanya bidii za kutosha na inafaa wapewe nafasi sawa na wanaume katika ujenzi wa taifa.
    Ningewahimiza wanaume wasiwe na kinyongo dhidi ya wamawake bali chanda chema huvishwa pete. Huu ndio wito wangu na kama tujuavyo kuro hasemi uongo na mbiu ya mgambo ikilia haikosi ina jambo.
    MASWALI
    1. Fafanua dhima ya mwanamke kulingana na makala haya. (maneno 70-80) (al.6)
      Nakala safi..................
    2. Bila kubadilisha maana fupisha aya ya pili nay a tatu. (maneno 50- 55) (al.7)
      Nakala safi......................
  3. MATUMIZI YA LUGHA
    1. Andika maneno yanayoafiki maelezo haya: (al.2)
      1. Nazali ya midomoni, kipasuo sighuna cha midomoni, kiyeyusho, irabu ya chini kati.
      2. Kipua ghuna cha kaakaa laini, irabu ya chini kati, kimadende ghuna cha ufizi, irabu ya chini kati.
    2. Ainisha mofimu kwa kurejelea majukumu ya kisarufi katika neno hili. (al.3)
      Alijipelekea
    3. Tunga sentensi ya swali ukitumia kiwakilishi nafsi ambata nafsi ya pili wingi. (al.2)
    4. Kwa kutolea mifano, andika miundo miwili ya ngeli ya LI-YA. (al.2)
    5. Andika sentensi ifuatayo kwa udogo wingi. (al.2)
      Mtoto mkaidi aliiba kitabu cha mwenzake.
    6. Tunga sentensi ukitumia nomino dhahania katika wakati ujao hali ya kuendelea. (al.2)
    7. Andika katika usemi halisi mtindo wa kitamthilia. (al.4)
      Khaemba Ouma alitaka kujua ni kwa nini Wandera Otieno alipenda Hisabati, Wandera Otieno akamweleza alipenda Hisabati kwa kuwa babake alikuwa mwalimu wa somo hilo.
    8. Unda nomino tatu kutokana na kitenzi safari. (al.3)
    9. Tunga sentensi moja kutofautisha maana ya daka na taka. (al.2)
    10. Tunga sentensi mbili tofauti kuonyesha matumizi ya lama za mtajo. (al.2)
    11. Yakinisha katika umoja. (al.1)
      Msipofanya bidii hamtapita mtihani.
    12. Tunga sentensi ukitumia ka kuonyesha mfulilizo wa matukio ya matukio ya wakati uliopita.(al.2)
    13. Unda sentensi changamano kutokana na tungo zifuatazo: (al.2)
      Mtoto alikuja nyumbani jana.
      Mtoto ndiye huyu.
    14. Jibu swali kulingana na agizo. (al.2)
      Halima alimbebea mwalimu mzigo kwa gari. (Anza kwa yambwa tendewa)
    15. Changanua sentensi ifuatayo kwa kielezo cha visaduku. (al.5)
      Kile kizuri kilikuwa kikitumika ba baba Yule
    16. Tunatumia shabaha tunapofurahishwa na jambo…………………………..tunapokula kiapo na yarabil…………………… (al.2)
    17. Andika maana ya maneno yafuatayo: (al.2)
      1. Kula kalenda
      2. Kula njaro.
  4. ISIMUJAMII. (al.10)
    Janga tandavu la korona limeathiri maisha ya kila mtu duniani, umepewa nafasi kama muuguzi kuzungumza na wanafunzi kuhusu suala hii. Andika sifa za lugha utakayotumia katika hotuba yako.


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

UFAHAMU

  1.        
    • Ubaguzi wa kikabila
    • Njao
    • Ukimbizi
    • Uchumi
    • Ukosefu wa makazi (al.4)
  2. Ubaguzi umejipenyeza katika ugawaji kwa misingi ya kikabila. (al.2)
  3.      
    1. Nchini Somalia vita vilisababishwa na uhasama na kiukoo/ koo mbalimbali zinazopigania uongozi.
    2. Nchini Kenya vita vilisababishwa na ukabila, tama za uongozi/ mamlaka, ubinafsi na viongozi. (al.2)
  4. Marekebisho ya katiba.
    • Viongozi wawe na maadhili mema
    • Wakenya wanastahili kuelimishwa kuhusu umoja/undugu/utaifa
    • Viongozi wawe watumishi wala sio wababa/watawala.
    • Masuala yanayohusiana na ardhi yafaa yashughulikiwe/yapewe kipao mbele
  5.      
    • Vita vya kikabila kuzuka Kenya, miongoni mwao baada ya uhuru.
    • Kisiwa cha amani kugeuka na kuwa uwanja wa vita/kuwa makao ya wakimbizi.
  6.      
    1. Mawio – Matokeo /athari/maafa.
    2. Tandarakiwa kwa dhati- Kupewa kipao mbele /kushughulikiwa

UFUPISHO

  1.        
    • Mwanamke ameelimika sawa na mwanamume.
    • Mwanamke ni kiongozi shupavu.
    • Mwanamke ni walezi walioaminika
    • Wanashiriki katika sanaa ya muziki.
    • Baadhi ni wanaspoti maarufu.
  2.      
    • Tangu jadi mabinti kuwatesa
    • Kuwadanganya.
    • Wao wana mikono miepesi ya kazi.
    • Wahafdhina hudai kuwa wao ni viumbe duni.
    • Majina yao yameng’ara kotekote.
    • Wengi wamesoma hadi vyuoni.
    • Wamehitimu katika taaluma tatizo

MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)

  1.      
    1. Mpya au mpwa. (al.2)
    2. Ng’ara
  2. A- Mofimu ya nafsi tatu umoja/ ngeli ya A – WA
    li- Mofimu ya wakati uliopita.
    Ji – Mofimu rejeshi ya mtenda
    Pelek- Mzizi
    e – Mofimu ya kauli ya kutendea
    a – kiishio (6 x ½ )(al.3)
  3. Mmelala nini leo? (al.2)
    (Nafsi ya pili (M)
  4.            
    1. Baadhi ya nomino huanza kwa umbo lolote katika umoja na kwanza kwa ‘ma’ katika wingi.
      Gari- Magari
      Jembe – Majembe
      Tunda - Matunda
    2. Baadhi ya nomino huanza kwa ‘ji’ katika umoja na ‘me’ katika wingi
      Jiko – Meko
      Jino –Meno
      Jingi – Mengi. (al.2)
  5.        
    • Vitoto vikaidi viliiba vijitabu vya vyenzao.
    • Vijitoto vikaidi viliiba vijitabu vya vyenzao. (al.2)
  6. Huzuni ilikuwa ikitanda sana wakati wa maambukizi ya korona. (al.2)
  7. Kaemba Ouma: Ningependa kujua sababu yako ya kupenda sana Hisabati /kwa nini unapenda Hisabati?
    Wandera Otieno: Ninapenda sana Hisabati kwa kuwa babangu alikuwa mwalimu wa Hisabati
  8.      
    • Msafara
    • Usafiri
    • Masafiri
    • Safari
  9. Daka – Nafsi ichimbayo ukutani kuweka vitu.
    • Kushika kitu kwa mikao mikono wakati kimetupwa.
    • Kabla ya kitu kwangura.
      Taka –Kuwa na hamu ya kitu
    • Uchafu
  10.      
    • Kuonyesha maneno mageni ya lugha nyingine.
    • Kunukuu maneno/usemi halisi
    • Kubainisha anwani kama vile ya vitabu, filamu majarida au vipidi vinapotajwa katika sentensi.(al.2)
  11. Ukifanya bidii utapita mtihani. (al.2)
  12. Alilala akaamka, a kakoga, akanywa chai na kuondoka. (al.2)
  13. Mtoto aliyekuja nyumbani jana ni huyu. (al.2)
  14. Mwalimu alibebewa mzigo na Halima kwa gari. (al.2)
  15.    
    S      
    KN   KT    
    W V T T H N U
    Kile Kizuri Kilikuwa Kikitumika na Baba Yule
  16. Wallahi /Billahi tunapokula kiapo na Yarabi! Tunapohuzunika na jambo. (al.2)
  17.      
    1. Kifungo/ kufungwa.
    2. Kutokuwa na kazi ya kufanya. (al.2)

ISIMUJAMII (al.10)

  • Lugha ya ucheshi
  • Msamiati maalum.
  • Kubadilisha msimbo
  • Matumizi ya sheng’
  • Kuchanganya ndimi
  • Matumizi ya lugha ya hisia.
  • Lugha inayohusisha tarakimu
  • Lugha agizi/maagizo
  • Lugha ya kitaaluma.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Samia Joint Mock Examination 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest