MAAGIZO
- Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima
- Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
- Kila insha isipungue maneno 400.
- Kila insha ina alama 20
- Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili
MASWALI
- Lazima
Umealikwa katika jopo lililoteuliwa kuchagua kiongozi wa masuala ya watoto wanaorandaranda mitaani katika kaunti yenu. Andika tawasifu utakayowasilisha katika jopo hilo kuonyesha ufaafu wako. - Mitandao ya kijamii ina faida nyingi katika jamii. Thibitisha
- Andika kisa kinachothibitisha ukweli wa methali “kutangulia si kufika”
- Andika kisa kinachoanza kwa maneno yafuatayo.
Nilishusha pumzi kutokana na ufanisi niliopata baada ya masaibu tele
MWONGOZO
- TAWASIFU
Umealikwa katika jopo lililoteuliwa kuchagua kiongozi wa masuala ya watoto wanaorandaranda mitaani katika kaunti yenu. Andika tawasifu utakayowasilisha katika jopo hilo kuonyesha ufaafu wako.
SURA- Atumie nafsi ya kwanza
- Atumie aya kuwasilisha hoja zake
- Maisha ya kuzaliwa, kukua na elimu ichukue nafasi ndogo katika tawasifu
- Mtahiniwa ashughulikie ufaafu wake.
BAADHI YA MAUDHUI- Yeye mwenyewe kwa mtoto wa kurandaranda
- Aokolewa na ajiunga na elimu
- Kuwa kiongozi wa shirika la kusaidia watoto shleni – aelezee shughuli walizohusika nazo
- Shahada yake ni kuhusu nini?
- Baada ya kuhitimu ameshughulikia mradi ipi?
- Je kuna masuala aliyochangia kimaadhishi
- Je amehusika na makao mangapi ya watoto wanaorandaranda
Tanbihi
- Akitumia mtindo wa hotuba kama vile salamu hana sura – 4mm ( sura)
- Lazima atumie nafsi ya kwanza
- Akikosa – 4 mm (sura)
- Mitandao ya kijamii ina faida nyingi katika jamii. Thibitisha
SURA- Hili ni swali elekezi kila hoja itajwe, ifafanuliwe na ikamilike
- Ikiwa hoja haijakamilika isituzwe
- Lazima mtahiniwa awe na hoja zaidi ya saba kuhitimisha maudhui
- Lazima atumie hoja mufti
BAADHI YA HOJA- Hufanikisha mawasiliano miongoni mwa watu
- Hufanikisha biashara
- Hufanikisha elimu
- Hukuza utangamano
- Kuboresha mahusiano
- Kuboresha usalama
- Huburudisha – husaidia watu kukabiliana na matatizo k.v msongo wa mawazo n.k
- Andika kisa kinachothibitisha ukweli wa methali “kutangulia si kufika”
- kisa kinafaa kioana na methali
- Mwanafunzi azingatie methali husika
- maana ya hiyo iwe anayekutangulia si lazima akamilishe mkondo anaweza kukosa kufika
- mtahiniwa atunge kisa kimoja
- aonyeshe sehemu zote mbili za methali
- dhana ya kutangulia ionekane vizuri
- dhana ya kutofika ijitokeze hata kama ni aya chache au sentensi moja - Andika kisa kinachoanza kwa maneno yafuatayo
Nilishusha pumzi kutokana na ufanisi niliopata baada ya masaibu tele.
Jibu- Mtahiniwa ajikite katika kisa ambacho kinaelezea mambo magumu ambayo yamezunguka maishani hadi kufikia upeo wa ufanisi
- Mtahiniwa pia aeleze namna ambavyo amefanikiwa maishani baada ya masaibu mengi
- Kisa kisimuliwe katika nafsi ya kwanza
Please download this document as PDF to read all it's contents.
Why PDF Download?
- You will have the content in your phone/computer to read anytime.
- Study when offline.(No internet/data bundles needed.)
- Easily print the notes to hard copy.
Either
Click here to download the pdf version of "Kiswahili Karatasi ya Kwanza Maswali na Majibu - Kassu Jet Joint Exams 2020/2021", and read the full contents of this pageOR
OR
