Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Mwakican Joint Pre Mock Examination 2021

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  • JIBU MASWALI MANNE
  • SWALI LA KWANZA NI LA LAZIMA
  • JIBU MASWALI MATATU KUTOKA KWA SEHEMU ZILIZOBAKIA
  • USIJIBU MASWALI MAWILI KUTOKA SEHEMU MOJA

SEHEMU A USHAIRI

  1. LAZIMA:
    Kila nikaapo hushika tama
    Na kuliwazia hali inayonizunguka.
    Huyawazia madhila
    Huziwazia shida
    Huiwazia dhiki
    Dhiki ya ulezi
    Shida ya kudhalilishwa kazini
    Madhila ya kufanyiwa dharau
    Kwa sababu ya jinsia yangu ya kike.
    Hukaa na kujidadisi
    Hujidadisi kujua kwa nini
    Jamii haikisikii kilio change
    Wezangu hawanishiki mikono
    Bali wananidharau kwa kuukosoa utamaduni
    Hukaa na kuhiuliza
    I wapi afua yangu dunia hii
    I wapi raha yangu ulimwengu huu
    I wapi jamaa nzima ya wanawake?

    Maswali
    1. Shairi ulilosoma ni la aina gani? (alama 2)
    2. Toa anwani faafu ya shairi (alama 2)
    3. Eleza dhamira na maudhui ya shairi(alama 3)
    4. Taja na ueleze tamathali tatu za fani ambazo zimetumiwa katika shairi hili.(alama 6)
    5. Andika ubeti wa tatu katika lugha ya nathari.(alama 4)

SEHEMU YA B
KEN WALIBORA, KIDAGAA KIMEMWOZEA

  1. Jibu swali la 2 au la 3
    Kidagaa kimemwozea ni Anwani mwafaka ya riwaya ya’’ kidagaa kimemwozea’’Eleza(alama 20)
  2. “ hata haramu huhalalishwa ati…..Hutegemea mtendaji ni nani na mtendwa ni nani.”
    1. Fafanua muktadha wa dondoo hili.(alama 4)
    2. Eleza tamathali kuu katika maneno ya swali.(alama 2)
    3. Thibitisha ukweli unaotokeza katika dondoo.(alama 6)
    4. Eleza sifa za wahusika wafuatao
      Imani
      D.J (alama 8)

SEHEMU C TAMTHILIA
TIMOTHY AREGE: MSTAHIKI MEYA
JIBU SWALI LA 4 AU 5

  1. Si nyingi nd’o mjuao…….! Mimi sifahamu ila nikiona afadhali.
    1. Fafanua muktadha wa dondoo hili.(alama 4)
    2. Fafanua maisha ya msemaji.(alama I0)
    3. Taja tamathali iliyotumiwa katika dondoo hili.(alama 2)
    4. Kwa undani, fafanua maudhui yanayoendelezwa na msemaji.(alama 4)
  2. Kupitia mifano, eleza mbinu zozote kumi zilzioendelezwa na utawala wa Sosi ambao ni utawala Dhalimu.(alama 20)

SEHEMU YA D
DAMU NYESUSI NA HADITHI NYINGINE –KEN WALIBORA NA S.A MOHAMED.
JIBU SWALI LA SITA AU LA SABA

  1. GILASI YA MWISHO MAKABURINI (S.A MOHAMED )
    “una nini Msoi? Ama kweli itikadi na ushirikina vimekudhibiti kweli kweli.
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili.
    2. Eleza maudhui makuu ya hadithi (alama 16)
  2. Ndoa ya samani: Omar Babu(Abu marjan)
    Ukirejelea hadithi ya Ndoa ya Samani jadili maudhui ya Ndoa, mali na mapenzi.(alama 20)

SEHEMU E
FASIHI SIMULIZI

  1. Eleza sifa za malumbano ya utani katika jamii.(alama 10)
  2.    
    1. nyiso ni nini?(alama 2)
    2. eleza sifa nne za nyiso.(alama 8)


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. Swali la lazima.
    shairi huru (alama 2)
  2. jinsia ya kike/mwanamke (alama 2)
  3. kuonyesha uonevu na udhalilishaji unaofanyiwa kina mama kwa sababu za kijinsia tw-ati wao ni wanawake tu.(alama 3)
  4. Jazanda-kushika tama-
    1. kumanisha kuhuzunika, majonzi.
    2. Balagha-I wapi jamaa nzima ya wanawake?
    3. Takriri-kurudia mifano
      I wapi…? (alama 6)
  5.    
    1. kunyimwa raha na walimwengu
    2. kilio chake kutosikilizwa
    3. kudharauliwa kwa kuukosea utamaduni.(alama 3)
  6. hukaa nikijichunguza niweze kujua kwa nini jamii haisikii kilio change na kwa nini wenzake hawamuungi mkono badala yake wanamdumisha kwa kuukosoa utamaduni.

KIDAGAA KIMEMWOZEA
SWALI 2

  1. kidagaa kumwozea mtu ni jambo kumharibikia mtu kinyume na matarajio kwa mfano ,mwalimu majisifu maji marefu kulewa ovyo na kujiletea aibu.
  2. Dagaa ni samaki mdogo sana na hawezi kuharibika kwa urahisi kwa hivyo akiharibika ni lazima awe amehifadhiwa katika hali mbaya . samaki huyu hudharauliwa na kuhusishwa na watu maskini. Siku hizi samaki amegunduliwa kuwa na vitubishi vingi sna kumwita kidagaa ni kumdunisha zaidi.(ki-ya udogo)
  3. Mtu maskini-maana ya pili ni mtu maskini zaidi baada ya kuongeza “ki” maskini ako katika hali mbaya sana.
  4. Kulinganisha –mtu kuonekana kukosa maaana kama vile Amani, imani, matuko (kidagaa kimemwozea) mwisho huwa na manufaa kwa umma. Maskini hawa ndio hunifanikisha kuondolewa kwa matajiri (virutubishi) au tajiri ambaye huonekana anavyo, mwisho huambulia patupu kwa kuondolewa na maskini .
  5. Anwani hii imerejelewa mara nyingi katika riwaya hii ya kidagaa kimemwozea. Hii ni kwa sabau ya kutaka kisisitiza ujumbe wake,
  6. Riwaya iliyoandikwa na Amani ilikuwa inaeleza mashaka yanayowapata Waafrika baada ya uhuru kupatikana
  7. Riwaya hii ambayo majisifu aliiba mswaada ya Amani ni mojawapo ya sabau zilizomfanya Amani kuja sokomoko na kufanya uongo na wizi wa majisifu kujulikana.
  8. Riwaya hii aliyoiiba majisifu na miswaasa mingine ndiyo ilimfanya majisifu kupatwa na pigo la kupata watoto walemavu. Kwa hivyo kidagaa kilimwozea Majisifu. Mwisho anapata aibu aliposhindwa kutoa hotuba kule wangwani. Alilazimika kutoroka . Amani alimwarifu majisifu kuwa mswaada ni wake.
  9. Kuchomwa kwa nyumba kidagaa kina mwozea Imani wakati walipoteza mali yao yote. Alikosa mahali pa kwenda na alikuwa anataka kujitosa majini.
  10. Kutimuliwa chuoni. Kidagaa mwozea Amani alipokuwa chuop kikuu na kusingiziwa kasha anafungwa jela. Aliporudi alipata mamake mzazi amefariki. Mswaada wake kuibwa na majisifu. Kupoteza mali yao yote kwa kutapeliwa na saba Bora. Kupigwa risasi karibu aage dunia.
  11. Nasaba kujitia kitanzi kidagaa kinamwozea Nasa Bora mwisho wa riwaya wakati ouvu wake unafichuliwa na kulazimika kutoa stakabdhi za hatamiliki. Alilala tajiri kuamka maskini. Aliamua kijinyonga. Zozote 10 10x2=20

SWALI LA 3 KIDAGAA KIMWEMWOZEA

  1. Haya ni maneno ya Imani akimjibu DJ. Ukingoni mwa mto Kiberenge Imani alikuwa akiyanywa maji yam to. Jambo hili lilikuwa haramu. Alama 4)
  2. Haramu kuwa halali
    1. Nasaba Bora kunyakua mashamba ya Hamadi na mwinyihatibu na kuwaua kasha anabadilisha halimiliki mashamba yakawa yake.
    2. Nasaba kumwachia Amani motto mchanga na kusisitiza ni wake. Alifanya hivi na motto alikuwa wake.
    3. Nasaba kuwafungia Amani na Imani jela kwa mauaji ya motto ilhali motto alifariki kwa kukosa matibabu na lishe.(alama 6)
  3. Amani (alama 8)
    Maskini-mkoba ulisheheni mali yake yote kazi duni-kuchunga ng’ombe ukamaji, kuishi kibanda hafifu.
    Mvumilivu- kutembea mwendo mrefu kwa miguu bila maji na chakula, bidii ya kufika sokomoko uk.3. hakulalamika kufanya kazi ngumu na mhsahara duni kwa maozi.
    Mkarimu na mwenye upendo-alimpa DJ shati lake baada ya kupoteza lake ndani mwa kinywa cha fihali. Alimvalisha. Aligawa shamba lake na kuwapa maskini wa sokomoko. Alikarabati nyumba ya majununi/Nasaba na kumpa matuko.
    Mwenye heshima na adabu-uk 23 anamjibu Zuhura kwa staha na heshima.
    Mnyenyekevu-alikubali kufanya kazi ngumu na kuchunga mifugo na kuwakama ng’ombe kwa mshahara duni na hata kuishi katika kibanda kibovu.
    Alikuwa msafiri-kama kaburi. Alikuwa mnyamavu. Alipenda kusikiliza kuliko kusikizwa na kuambiwa kuliko kuamba
    Mwenye huruma- alimtuliza imani alipokuwa analia baada ya kumjulisha kuwa hana kwao wala kwake nk. Zozote 4 kutja ½ kueleza ½, ½=8/2=4

BOB.DJ
Sifa zake

  1. Mchungaji, ingawa umri wake ulikuwa mdogo.
  2. Alikuwa mototo wa mjane aliyepika pombe haramu kwenye mtaa wa Madongoporomoka mjini Songea.
  3. Aliwajali wengine-alikubali kuwapeleka Amani na Imani kutafuta ajira kwa Nasaba na Majisifu.
  4. Sheng-alitumia lugha ya sheng katika mawasiliano yake. Kwa maoni ya Amani ingeweza kuwaliza walimu machozi kikombe tele wakichelea wanafunzi wao kumwiga.
  5. Mwaminifu-aliaminiwa hadi mke wa maozi alimwamini na kumchukua kama motto wake.
  6. Msiri- alificha siri ya urafiki kati ya Lowela na Nasaba.
  7. Mwenye huruma-alimhurumia mbwa Jimmy ambaye alikuwa amefunngwa kwa nyororo ilhali alikuwa mgonjwa.
    Kutaja ½. Kueleza ½ 8/2=4
  1. Wazimu –kidagaa kinamwozea mashaka baada ya kuachwa na Ben Bella. Aliacha shule na kushikwa na wazimu. Alipelekwa kwa hospitali ya wazimu.
  2. Seli- matuko alitupwa seli baada ya kutoa hotuba ya kumkashifu nasaba. Alipigwa mateke na askari seli ilikuwa choo hapo zamani. Pia Imani na Amani.
  3. matuko: kupigana vita vikuu vya dunia. Alirudi akiwa wazimu. Alokosa heshima na usaidizi badala yake alirandaranda mitaani na kula kwa pipa. Hakuwa na mke watoto wala jamii.
  4. soka.chwechwe mwanasoka mashuhuri aliyeheshimwa, kidagaa kilimwozea wakati alivunjika fupaja na kusahaulika. Alibaki kuishi maisha ya huzuni. Hakuweza kucheza mpira tena na jina lake likafikia.
  5. talaka-zuhura aliachwa peke yake na Nasaba. Hadhi yake ilishuka kwani kwa wengi ilikuwa ni kupatikana katika chumba cha kulala na Amani, kabla ya hapo motto wake mashake alishikwa na wazimu, madhubuti alikataa kuishi kwa nyumba ya wazazi wake; pia alikataa chochote kilichomhusu babake baada ya kutoka urusi. N.K zozote 10 x 2=20

SWALI 4. MSTAHIKI MEYA TIMOTHY AREGE

  1. Maneno haya yanasemwa na mamake Dadavuo, alikuwa akinjibu waridi, pale hospitalini kutibiwa kwa sababu alikuwa anaendesha.(alama 4)
  2. Masiha ya msemaji(alama 10)
    1. Yeye ni mfanyikazi wa Meya Sosi wa mji wa Cheneo.
    2. Kama wafanyakazi wengine analipwa mshahara duni, wakati mwingi mshahara hucheleweshwa kwa miezi kadhaa. (5x2)
    3. Hana chakula bora na kwa hivyo hula chakula cha mbwa au kilichobaki pale kwa meya.
    4. Umaskini wake unamzuia kupasha moto chakula kwa sabau hana pesa za kunua mafuta. Kuni hazipatikani kwani ukataji wa miti umepigwa marufuku.
    5. Yeye na watoto wake hula chakula kilichoharibika, Dadavuo ana utapia mlo
  3. Tamathali ya usemi ni Nidaa(!)
  4.    
    1. umaskini
    2. matatizo yanayowakumba wafanyakazi.
    3. ukosefu wa Elimu.(alama 4)
  1. vitisho –anatishia kuwafuta kazi wafanyikazi, kukata mshahara wa siku ambazo waikuwa wamegoma, anamtisha siki na kumwambia kuwa asije kwake ama angemchukulia hatua.
    Askari –alimwita askari kumwondoa siki kwa nymba yake. Askari watumiwa kuwapiga wafanyakazi.
    Ahadi za uongo-kuwadanganya watu kuwadawa zingefika baada ya siku tatu, eti ziko melini kumbe hakuna chochote. Aliwahadaa wafanyikazi warudi kazini eti angeshughulikia shida zao.
    Propaganda –anamtumia kinara wa uhusiano bora kutumia vyombo vya habari kuendeleza uzalendo kwa kucheza nyimbo za kizalendo zilizopitwa na wakati.
    Mkutano-kuandaa mkutano kati yake na viongozi wa wafanyikazi (tat, Beka, Medi0 kuwafunga macho wananchi kwa baraza lilikuwa halina fedha za kuongeza mishahara au kuwashughulikia wafanyikazi.
    Tenga utawale- anamtenga Diwani 111 na siki kwa sababu hawakuliunga baraza mkono.
    1. Kuwaweka wanachi katika hali ya unyonge, kwa mfano mamake Davaduo, hadi wanaogopa kuomba chochote.
    2. Uwezo wa kisheria: kulikuwepo na mayors Act iliyompa Meya nguvu za kufanya lolote.
    3. Kipaliliza haki-alitaka kuuibia mji wa cheneo kwa kukubali kuwa alimkosea mwana kandarasi na kasha kumlipa huku akiiba pesa nyingi.
    4. Washauri wabaya-Bili na Diwani 1 na 11 walimshauri kuiba mali ya umma na kujinufaisha.
      Damu nyesusi na hadithi nyingine
  2.    
    1. maneno ya Sekwa, akimwambia Msoi nje ya nyumba ya Msoi kwa lazima waende Baa ya makaburini. Msoi alikuwa amepatwa na mikosi kama kuvunja bakuli la maua, kujikwa karibu aanguke na kujibana kidede kidogo alipokuwa anafunga mlango wa gari. (alama 4)
    2. maudhui makuu
      utabiri na unavyotekelezwa.
      1. Msoi ni mtabiri wa mambo ambayo yatatokea kabla yatokee.
      2. Kuna ishara zinazotangulia ndoto hizi kama malaika kusimama mwilini na mwili kutetemeka.
      3. Kuna dalili ambazo hutangulia tukio baya kama aliligonga bakuli la maua ambalo lilivunjika, karibu aanguke na mlango wa gari ulimbana mkono. Hali ya anga ilibadikika, kukawa na wingu jeusi.
      4. Wafu engi hasa vijana katika karne hii(semkwa, Asha na Josefina) hawakuamini katika maono (utabiri) yake waliamini katika maono (utabiri) yake waliamini yalitokea kisadfa tu.
      5. Ndoto ya Msoi ya vizuu ilikuja kuwa halisi wakati wimbo wa Michael Jackson wa Thriller ulipokuwa unaimba kufanya lolote, kwa mfano starehe ya kunywa, kula na kucheza katika Baa ya makaburini.
        Marafiki wa Msoi Semkwa Asha na Jospina hawakuamini hadi tukio lilipotokea na wakavamiwa na majambazi.
  3. Ndoa ya mali na mapenzi.
    1. Desturi za kuposa na kuolewa zilifuatwa mara ya kwanza msimulizi alipoposa aliandamana na mjomba wake. Mara ya pili pia alifuata sheria za ndoa ya Kiswahili alipeleka posa na ikakubaliwa.
    2. Mama zenu alipomwona binti yake wa pekee Amali alivyokuwa mrembo sana aliamua kumtumia kama kitenga uchumi.
    3. Msimulizi alipokuja na mjomba wake kama mila ilivyohitaji, mama zena alimdharau na kusema eti binti yake hawezi kuolewa na mtu ambaye hana chochote.
    4. Kukataliwa kwa msimulizi kulimfanya atie bidii kwa kufanya kazi mbalimbali na kubahatika kuenda Arabuni kufanya kazi hadi anapotajirika.
    5. Jamaa ya msimulizi ilimshihi amuoe aliporudi Arubani. Walifikiri kuwa bado alimpenda kama zamani, alikubali shingo upande.
    6. Mara ya pili alipopeleka mahari kwa akina Amali, Msimulizi alikubaliwa nafasi ya kumwuoa Amali.
    7. Wazazi wa Amali na hasa mamake alitka vitu kadhaa (samani) kabla ya ndoa kufungwa. Pia alitaka shere zifnyike kwake badala ya kwa bwana harufi.
    8. Msimulizi aligundua kuwa Amali na failia yake, hawakumpenda bali walipenda mali yake. Aliamua kutofunga ndoa na Amali. Alimwachia mali aliyokuwa amemnunulia.
    9. Kama msimulizi angekubaliwa pale mwanzo kumuoa Amali pengine wangekuwa mke na mume.
    10. Msimulizi aliwepanda wazazi wake ndugu ,jamaa na marafiki na kuwasaidia kujikimu kiuchumi. Alimnunulia ndugu yake gari la matatu. Jamaa wengine aliwatafutia kazi kule Arabuni.
    11. Ndoa kati ya tabaka la maskini 9msimulizi) na tajiri (amali) alikuwa ni vigumu kufanyika.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Mwakican Joint Pre Mock Examination 2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest