Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Royal Exam Series Post Mock Trial Exams 2022

Share via Whatsapp

KISWAHILI
KARTASI YA 3
FASIHI

MAAGIZO

  • Jibu maswali manne pekee.
  • Swali la kwanza ni la lazima.
  • Maswali mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu zilizosalia yaani.
  • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
  • Kila swali lina alama ishirini (20)
  • Majibu yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.


Maswali

SEHEMU YA A: TAMTHILIA
Kigogo
(P.Kea)

  1. Lazima
    1. Jadili jinsi kumi ambazo maudhui ya ukatili yanajitokeza katika Tamthilia ya Kigogo (alama 10)
    2. Eleza mifano kumi ya matumizi ya kinaya katika Tamthilia ya Kigogo. (alama 10)

SEHEMU YA B: RIWAYA: |
Chozi la heri
(Assumpta K. Matei)

Jibu swali la Pili au la Tatu

  1. “Watu husema kuwa binadamu hawawi sawa ila kifoni...”
    1. Eleza muktadha wa maneno haya. (alalama 4)
    2. Tambua mbinu moja ya lugha iliyotumiwa katika dondoo hili. (alama 2)
    3. Eleza sifa na umuhimu wa mzungumzaji wa maneno haya. (alama 6)
    4. Thibitisha kuwa hakuna usawa baina ya wanadamu. (alama 8)

      Au
  2. Jadili nafasi ya sehemu zifuatazo katika riwaya ya Chozi la Heri
    1. Hotuba (alama 10)
    2. Uozo katika jamii (alama 10)

SEHEMU C:HADITHI FUPI

  1. Mtihani wa Maisha
    "Leo mwalimu mkuu atajua kwamba mdharau biu hubiuka‟
    1. Eleza muktadha wa maneno haya. (Alama 4)
    2. Taja mbinu ya lugha iliyotumika katika muktadha huu. (Alama 6)
    3. Eleza wasifu wa mzungumzaji wa maneno haya. (Alama 2)
    4. Jadili maudhui ya elimu kama yanavyojitokeza katika hadithi hii. (Alama 8)

  2. Ndoto ya mashaka
    (Ali Abdulla)
    ‟Kusema kweli lakini hata mimi sikuwa na nadhari katika kumpenda msichana huyu ...Nilimpenda kufa! Lakini! Kwao bure tu!‟
    1. Eleza mkutadha huu. (Alama 4)
    2. Taja mtindo wa lugha uliotumika katika mkutadha huu. Alama 4
    3. Taja sifa mbili za mzungumzaji. (Alama 2)
    4. Onyesha maudhui ya umaskini katika hadithi fupi ya Ndoto ya mashaka.

SEHEMU YA D:USHAIRI

Jibu swali 6 au 7

  1. Ushairi
    Soma shairi lifuatalo kasha ujibu maswali

    Daima alfajiri na mapema

    Hunipitia na jembe na kotama

    Katika njia iendayo kondeni
    Kama walivyofanya babuze zamani;
    Nimuonapo huwa anatabasamu
    Kama mtu aliye na kubwa hamu

    Kushika mpini na kutokwa jasho
    Ili kujikimu kupata malisho.
    Anapotembea anasikiliza
    Videge vya anga vinavyotumbuiza

    Utadhani huwa vimemngojea
    Kwa usiku kucha kuja kumwimbia;
    Pia pepo baridi kumpepea

    Rihi ya maua zikimletea
    Nao umande kumbusu miguu;
    Ni miti yote hujipinda migongo

    Kumpapasa, kumtoa matongo;
    Na yeye kuendelea kwa furaha

    Kuliko yeyote ninayemjua

    Akichekelea ha hahahahahaha ...
    Na mimi kubaki kujiuliza
    Kuna siri gani inayomliwaza?
    Au ni kujua au kutojua?
    Furaha ya mtu ni furaha gani

    Katika dunia inayomhini?
    Ukali wa jua wamnyima zao

    Soko la dunia lamkaba koo;
    Dini za kudhani za msonga roho

    Ayalimia matumbo ya waroho;
    Kuna jambo gani linamridhisha?
    Kama sikujua ni kutokujua

    Laiti angalijua, laiti angalijua!

    1. Eleza matatizo manne yanayompata mzungumziwa. (Alama 4)
    2. Eleza mtindo wa lugha uliotumiwa na mshairi na utoe mifano. (Alama 8)
    3. Taja nafsineni katika shairi hili. (Alama 1)
    4. Eleza toni ya shairi hili. (Alama1 )
    5. Taja mbinu mbili za uhuru wa kishairi uliotumika na utoe mifano. ( Alama 2)
    6. Andika ubeti wa kwanza kwa lugha ya nathari. (Alama 4)

  2. Soma shairi lifuatalo kasha ujibu maswali.

    Leo kitaka nifike, natamani, ila wauma mwili
    Kwa kazi nihusike, samahani, unahili kimwili
    Napenda nihesabike, makundini, ila huwezi mwili

    Vitisho pamwe kelele, ninavicha, kwa nafsi na mwili
    Ila ugonjwa utimile, umechacha, na kuudhili mwili
    Msikose simile, magalacha, si gurudumu mwili.

    Vingekuwepo viraka, kuutia, ngeushuruti mwili
    Kifundi kivipachika, kuingia, hata kuridhi mwili
    Upya ukaungilika, kuvutia, roho na wake mwili.

    Lakini kamwe haiwi, kuvipata, vipande vyake mwili
    Si hofu kupata mawi, sitajua, kupigania mwili
    Hata kufutwa sikawi, nitakita, kidete nao mwili.

    Kazi ninaithamini, ni hakika, akilini na mwili
    Ila kamwe siamini, kusagika, damu, jasho na mwili
    Uwele hususani, kioneka, nguvu hitishi mwili.

    1. Liweke shairi hili katika bahari tatu. (Alama 3)
    2. Eleza dhamira ya mshairi. (Alama 2)
    3. Elezamuundowashairihili. (Alama 4)
    4. Toa mifano ya uhuru wa kishairi uliotumika. ( Alama 4)
    5. Eleza kwa kifupi maudhui matatu yanayojitokeza katika shairi hili. (Alama 3)
    6. Andika ubeti wa kwanza kwa lugha ya nathari. (Alama 4)

SEHEMU E

  1. FASIHI SIMULIZI
    1.        
      1. Miviga ni nini? (Alama 2)
      2. Eleza sifa nane za miviga. (Alama 8)
    2.        
      1. Ulumbi ni nini? (Alama 2)
      2. Eleza sifa nane za ulumbi


Mwongozo Wa Kusahihisha

SEHEMU YA A: TAMTHILIA
P.Kea:Kigogo

  1. Swali la Lazima
    1. Jadili jinsi kumi ambazo maudhui ya ukatili yanajitokeza katika Tamthilia ya Kigogo
      1. Majoka analifunga soko la Chapakazi ambalo ni tegemeo la raia wa Sagamoyo.
      2. Majoka anawaita viongozi wa vyama pinzani ambao wanaupinga uongozi wake. iii)Majoka anawatuma wahuni ili wamshambulie Tunu.
      3. Majoka anamweka korokoroni Ashua kwa kuwa alikataa vishawish ivyake vya kimapenzi. v)
      4. Kuruhusu upikajipombe haramu kwa mamapima pasipo kuhofu madhara yake.
      5. Kuwaingiza vijana katika matumizi ya mihadarati katika Majoka na Majoka Academy.
      6. Kuwatishia kifo wanaokiuka amri na njama zake mbovu k.v Chopi.
      7. Kuamrisha waandamanaji wapigwe risasi na askari.
      8. Kutisha kumfuta kazi Kingi kwa kukosa kutekeleza amri yake.
      9. Kukataa kutoa msaada wa chakula kwa watoto wa Ashua.
      10. Kujaribu kumshawishi Ashua ashirik inaye mapenzi kama kisasi.
      11. Kumwinjikia kisasi Sudi alipokataa kuchonga kinyago ch aMarara (za kwanza10x1=10)

    2. Matumizi ya kinaya
      1. Mjumbe katika matangazo anarejelea ufanisi ambao umepatikana tangu uhuru ilhali raia wa Sagamoyo wanaish maisha ya dhiki(hawana maji, elimu duni)
      2. Mjumbe kudai utumwa uliondolewa ilhali wanajamii wanaish ikatika utumwa wa kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa mfano , soko linafungwa, dhuluma ya kutiwa kizuizini bila sababu naTunu kuvunjwa mguu.
      3. Mjumbe kudai hawatakubali kutawaliwa kimabavu ilhal iMajoka anawadhulumu –anafunga soko akiwa na nia ya kujitwalia na kujenga mkahawa.
      4. Majoka kusifiwa kuwa kiongozi shupavu ilhali anawaumiza wapinzani wake na hata kuwaua.
      5. Badala ya Majoka kuwalinda Wanasagamoyo kama kiongozi , anatumia vyombo vya dola kuwajeruhi na kuwaua raia wanaondamana.
      6. Majoka kudai Sagamoyo inajiweza huku raia wake wanaselelea katika uhitaji kwa nyenzo zao za kiuchum ikudhibitiwa na uongozi wa Majoka kwa mfano Soko la Chapakazi.
      7. Majoka kumwambiaTunu kwamba kosa halilipwi kwa kosa na yeye anaendeleza kisasi dhidi ya Sudi kwa kumuoa Ashua ambaye alimtamani.
      8. Majoka kuona kuwaTunu amenaswa na utandabui wa kikoloni ilhali anautumia ukoloni mamboleo kuwagandamiza wenyeji wa Sagamoyo– anajinufaisha kwa mali ya umma kama vile Soko la Chapakazi.
      9. Ni kinaya kuwa Ashua anadai kuwa kizuizin ikuna amani kuliko nyumbani anakoteswa na Sudi ilhali Sudi anajitahidi awezavyo kuikimu jamii yake wala hamtesi mkewe kama kizuizini
      10. Ni Kinaya kwamba Majoka anapanga sherehe ya maadhimisho idumu kwa mwezi mmoja ilhali wananchi / wafanyibiashara hawana chakula kwa kuwa Soko la Chapakazi limefungwa(Ashua na watoto hawana chakula)
      11. Ni kinaya kwamba kifo cha Ngurumo hakimsikitishi Majoka ilhali alikuwa kibaraka wake badala yake anaagiza azikwe haraka.
      12. Kenga na Kingi wanatusiwa na Majoka na kuitwa wasaliti ilhali Majoka mwenyewe ndiye msaliti wa Wanasagamoyo kwa kuwanyima ulinzi, chakula na kazi zao.
      13. Majoka anamsaliti mkewe Husda kwa kumtamani Ashua.
      14. Boza anadai kulipa kodi na kujenga nchi na kujitegemea lakini hiyo wanayolipa inamfaidi Majoka. Anatumia vyombo vinavyonunuliwa na kudumishwa na kodi ya wananchi kuwadhulumu.
      15. Madai ya Majoka kwamba anamheshimu Sudi ni kinaya kwani Majoka hamheshimu yeyote.
      16. Madai ya Majoka kuwa uchafu / taka ingeharibu jina zuri laSagamoyo ni kinaya kwani Sagamoyo haisifiki kwa lolote zuri.
      17. Ashua alimlaumu Sudi kwa kosa la yeye kutiwa kizuizini ilhali kosa lilikuwa la Majoka.
      18. Ngurumo anadai kwamba Sagamoyo ni mahali pazuri tangu Soko la Chapakazi lifungwe lakini hili ni kinaya kwani mahangaiko yamekithiri.
      19. Ngurumo kudai pombe ni starehe ilhali pombe inaangamiza Wanasagamoyo na hata wengine bkuwa vipofu.
      20. Ni Kinaya kwamba Majoka na vibaraka wake walitarajia uwanja wa ikulu ufurike watu kusherehekea siku ya uhuru lakini ni watu kumi tu waliohudhuria.
      21. Ni kinaya kwamba ukoloni ulidaiwa kung’olewa lakini hasa unaotawala n iukoloni kupitia kwa Majoka. (Hoja 10 ×1=10)

  2. “Watu husema kuwa binadamu hawawi sawa ila kifoni...”
    1. Eleza muktadha wa maneno haya (alalama 4)
      1. Haya ni maneno ya Kaizri. Anamwambia Ridhaa. Wapo katika Msitu wa Mamba. Ni baada ya kufurushwa kutoka Mlima wa Simba baada ya vita vya baada ya uchaguzi kuzuka. Anarejelea usawa kiasi uliokuwa ukionekana kuwepi pale kambini. (4×1= 4)

    2. Tambua mbinu moja ya lugha iliyotumiwa katika dondoo hili (alama 2)
      1. Kinaya- watu hawawi sawa ila kifoni
        (1×2= 2)

    3. Eleza sifa na umuhimu wa mzungumzaji wa maneno haya (alama 6)
      • Sifa za Kaizari.
        1. Ni mwenye busara. Anaelewa kuwa hakuna usawa wakati wa kifo kati ya maskini na matajiri ikizingatiwa wanavyokufa na wanavyozikwa (uk 14- 15).
        2. Ni maskini. Matone mazito ya mvua yalianguka kwenye ngozi ya wanawe, Lime na Mwanaheri. Hana uwezo wa kuwasaidia. Hata tambara hana (uk 15- 16).
        3. Ni mcha Mungu. Anamshukuru Mungu kuwa wangali hai licha ya hali ngumu (uk 16).
        4. Mwenye huruma. Aliwahurumia vijana waliouwawa kwa risasi na polisi wa Penda Usugu Ujute (uk 24).
        5. Mzalendo. Aliihurumia nchi yake ambayo ilielekea kushindwa kuwashawishi watu wake kuelewa umuhimu wa usalama (uk 24- 24).
        6. Mwenye mapenzi ya dhati. Alijaribu sana kuwaokoa wanawe waliokuwa wakibakwa ila akashindwa (uk 25).
        7. Mwenye tahadhari. Siku za kwanza kambini hakuweza kutumia vyoo vya kupeperushwa (uk 29).
        8. Mshawishi. Aliwasihi wakimbizi wenzake kuchimba misala (long drop) (uk 29). (3×1= 3)
        9. Kila sifa ifafanuliwe. Sifa zisianze kwa vinyume kama: hana utu, si mwenye tahadhari n.k.

      • Umuhimu wa Kaizari
        1. Anawakilisha watu wenye busara katika jamii.
        2. Ametumiwa kuonyesha matatizo wanayokumbana nayo wakimbizi.
        3. Anawakilisha athari zinazotokana na vita vya kikabila.
        4. Ametumiwa kuwajenga wahusika wengine kama Ridhaa.
          (3×1= 3)

      • Thibitisha kuwa hakuna usawa baina ya wanadamu (alama 8)
        1. Sheria za kikoloni zilimpa mzungu kibali cha kumiliki mashamba katika sehemu zilizotoa mazao na umilikaji wa ardhi na Waafrika sehemu hizi kupigwa marufuku (uk 7).
        2. Hata katika kifo hamna usawa. Kuna wanaokufa wakipepewa na wauguzi katika zahanati za kijijini. Wengine hulala maumivu yao yakiwa yamefishwa ganzi kwenye hospitali za kifahari (uk 14).
        3. Pia kuna tofauti katika mitindo ya mazishi ya matajiri na maskini. Matajiri huvishwa mavazi ya kifahari tofauti na maskini (uk 15).
        4. Mwalimu aliwaambia kina Tila kuwa utawala huteuliwa maksudi kuendeleza mfumo uliopo wa kiuchumi kwa maslahi ya watawala na tabaka ambalo linazimiliki nyenzo za uzalishaji mali (uk 39).
        5. Bwana Kangata na jamii yake walilowea kwa shamaba la mwajiri wao ambaye alikuwa akiishi jijini (uk 64).
        6. Kimondo alimweleza Lunga kuwa kuishi kwao wanyonge kuliamuliwa na matajiri (uk 69).
        7. Waafrika wafanyakazi maskini walinyimwa matibabu kwa kukosa Medical Scheme kama alivyoeleza daktari mwafrika (uk 70).
        8. Baada ya wakimbizi kuishi katika Msitu wa Mamba kwa kipindi fulani, jamii ilianza kutwaa uchangamano wa mtu kutambua kuwa yeye alitokana na ukoo mtukufu na jirani yake alikopolewa na ukoo wa mlalaheri (uk 75).
        9. Katika wimbo wake, Shamsi anaeleza kuhusu matajiri wanaomchungulia na kumcheka wakiwa kwenye roshani zao wakipunga pepo baada ya kujaza matumbo yao (uk 130).
        10. Ridhaa alihamia mtaa wa Afueni. Mtaa wa watu wenye kima cha juu kiuchumi. Daraja kubwa limeutenga mtaa huu na mtaa wa Kazikeni, mtaa wa watu wenye maisha ya kubahatisha (uk 137- 138).
          (8×1= 8)

          Au

  3. Jadili nafasi ya sehemu zifuatazo katika riwaya ya Chozi la Hari:
    1. Hotuba (alama 10)
      • Hotuba ni maelezo maalumu yanayotolewa na mtu mmoja mbele ya watu. Pia huitwa hutuba. Mwandishi wa riwaya hii ametumia hutuba kwa ustadi mkuu kupitisha ujumbe mbalimbali.
        Hotuba hizi ni:
        1. Hotuba ya Racheal Apondi kwa maafisa waliohudhuria warsha kuhusu jukumu la vikosi vya askari katika kudumisha usalama, amani na maridhiano nchini (uk 112- 113). Katika hotuba hii, Racheal Apondi anasisitiza kuwa:
          • Suala la usalama haliwezi tena kupuuzwa. Usalama umekuwa mojawapo ya mahitaji ya kibinadamu.
          • Anasema kuwa bila usalama, binadamu hawezi hata kushiriki katika shughuli za kuzalisha mali, hivyo hata mahitaji yake mengine ya kimsingi kama vile chakula, malazi na makazi hayawezi kukidhiwa.
          • Kila binadamu ana jukumu la kudumisha amani na usalama.
          • Wafanyakazi wa umma, hasa polisi na wanajeshi wana jukumu kubwa zaidi la kudumisha usalama na amani.
          • Kila mmoja wetu anastahili kuhakikisha kuwa ameepuka vitendo vya kihalifu
          • Ni vyema mtu kuwaangaza wahalifu wakati wote.
          • Vikosi vya polisi na wanajeshi vimefunzwa maarifa ya kukabiliana na kadhia za jinai na upelelezi.
            (4×1= 4)

        2. Hotuba ya Lunga Kiriri- Kangata kwa walimu na wanafunzi gwarideni (uk 68-69).
          • Hotuba hii ilisisitiza umuhimu wa kuhifadhi mazingira. Anasisitiza kuwa:
          • Suala la uhifadhi wa mazingira ni jukumu la kila mmoja wetu.
          • Misitu ilikuwa imevamiwa na viongozi wenye mate ya fisi.
          • Baadhi ya vinara wa taasisi mbalimbali za umma wamewaacha wanyama kama mayatima kwa kuwapoka makazi yao.
          • Maelfu ya maekari ya misitu yamefyekwa na kujengwa viwanda.
          • Badala ya mibambakofi na miti mingine inayosafisha hewa, michai imetwaa nafasi yake.
          • Wanaohusika na matendo haya wanapoulizwa hudai kuwa michai si adui ya mazingira!
          • Wengine wanasema kuwa misitu haina budi kukatwa ili kupanda mimea inayotoa chakula, kwani jamii lazima ijitosheleze kwa chakula.
          • La kuhuzunisha ni kwamba hawa hawa wanaosema hivyo ndio wanaokita majengo ya kifahari katika sehemu ambazo zinastahili kutengewa upanzi wa chakula!
          • Wengine wamediriki kunyakua hata madhabahu kwenye Mlima wa Nasibu ili kujenga hoteli kubwa za kitalii.
          • Wazee wetu hata hawana mahali pa kuchomea kafara!
          • Tunakata miti bila kupanda mingine.
          • Hata mabustani ya maua tunashindwa kuyastawisha.
          • Tukiendelea kuharibu mazingira sehemu yetu itazidi kuwa jangwa.
            (2×1= 2)

        3. Hotuba ya Umu katika hoteli ya Majaliwasiku yake ya kuzaliwa.
          • Umu anawashuku Mwangeka na Apondi kwa kuwa wazazi wake wema.
          • Anawashukuru kwa kumsomesha.
          • Anawashukuru kwa kumsaidia Dick kujiendeleza kimasomo.
          • Mwangeka na Apondi wanamshukuru Umu kwa kuwapa furaha.
          • Apondi anamshukuru kwa kumlea mdogo wao kwa maadili bora.
            (2×1= 2)

        4. Hotuba ya Dick katika hoteli ya Majaliwa siku ya kuzaliwa kwa Umu.
          • Dick anamshukuru Umu kwa msaada wake na ahadi ya kumlea.
          • Anamkumbusha siku walipokutana katika uwanja wa ndege na ilivyokuwa muhimu kwake.
          • Anamshukuru Umu kwa kumwelekeza kwa wazazi wao wale.
          • Anawashukuru Apondi, Mwangeka na wanawe kwa ushauri wanaompa.
            (2×1= 2)
          • Mtahiniwa ataje hotuba kisha aeleze masuala muhimu yanayoibuliwa na kila moja.

    2. Uozo katika jamii (alama 10)
      • Uozo ni hali ya kuzorota na kutozingatiwa tena kwa maadili mema katika jamii. Ni hali ambapo milazote na desturi njema huvurugwa na wanajamii wanaofanya mambo yaliyo kinyume nahali halisi ya maisha. Mwandishi amejadili suala hili kwa undani kama ifuatavyo;
        1. Jamii inaendeleza ubakaji. Genge la mabarobaro watano lilifululiza hadi walipokuwa maskini Lime na Mwanaheri na kuwabaka mbele ya baba yao (uk 25).
        2. Kuna ulanguzi wa dawa za kulevya. Dick alipotoroshwa na Sauna alipelekwa kwa tajiri mmoja aliyemwingiza katika kusafirisha dawa za kulevya kutoka nchi moja hadi nyingine (uk 119- 120).
        3. Wanajamii wanaendeleza uporaji na wizi wa mali. Vijana wanawavamia watu, kuwaua na kupora katika maduka ya kihindi, kiarabu na ya waafrika wenzao.
        4. Jamii inaendeleza ufuska/ ukahaba. Sauna aliiba watoto na kuwapeleka kwa mama mmoja aliyewatumia kwa biashara ya nipe nikupe (uk 84).
        5. Biashara haramu inaendelezwa. Bi. Kangara alifanya biashara ya kuwauza watoto na vijana- Safari yake ilipata mkondo mwingine baada ya polisi kupata fununu kuhusu njama ambazo yeye na Bi. Kangara walikuwa wakiendesha. Mabibi hawa walikuwa na mtandao ambao kazi yake ilikuwa kuwauza watoto na vijana (uk 84).
        6. Kuna tatizo la mimba za mapema. Vijana wana mazoea ya kukumbatia mtafaruku wa kuhisia unaowapata na mara hujipata wameambulia ujauzito kama alivyofanya Zohali (uk 98).
        7. Baadhi ya wanajamii wanaendeleza uavyaji mimba. Sauna alijaribu awezavyo kuavya mimba na mwishowe, baada ya kushindwa, anaamua kujiua.
        8. Kukiuka maadili ya kikazi. Fumba (mwalimu) anakiuka maadili ya kazi na kujihusisha kwa mapenzi na mwanafunzi wake, Rehema, na hatimaye kumpachika ujauzito (uk 102).
        9. Wazazi wanawabaka wana wao. Babake Sauna anafanya mapenzi na mwanawe kila apatapo nafasi, na mwishowe, Sauna anapata mimba.
        10. Starehe na anasa kwa vijana. Vijana wa vyuo vikuu wameshindwa kutofautisha usiku na mchana. Tindi anasahau kumrejesha Lemi nyumbani kutokana na muziki (uk 121).
        11. Wazazi wanakwepa malezi na kuwatupa wanao wakiwa wachanga. Neema anampeleka mtoto aliyemwokota kwa polisi (uk 162).
        12. Vijana kuwaiga wazee. Mwangemi na Mwangeka walikuwa na tabia mbovu ya kumuiga babu yao (uk 186).
          (10×1= 10)
          Mtahiniwa afafanue kwa mifano kutoka katika riwaya.
    3.             
    4.                 
      1. Haya ni maneno ya Boza akimwambia Sudi wakiwa sokoni chapakazi. Ni wakati Kenga alikuja kuangalia kama kinyago cha majoka kinachongwa halafu akawapa keki. (4x1)
      2.            
        • Ni muuaji – Aliua jabali.
        • Ni dikteta – Hakusikiliza washauri wake.
        • Ana taasubi ya kiume – Alisema mwanamke hawezi kuwa kiongozi.
        • Ni fisadi – Anataka kuchukuwa soko la chapa kazi.
        • Ni mkware – Anatafuta uhusiano wa kimapenzi na Ashua.
        • Ni mwongo - Alisema alisaidia Tunu katika masomo yake.
        • Ni katili – Alisema ngurumo azikwe juu ya miili mingine. (zozote 6x10
      3.       
        • Alisababisha mauaji ya wapinzani kama Jabali.
        • Alitoa hongo kama kumpa sudi likizo ughaibuni ikiwa atatengeneza kinyago.
        • Anatumia propaganda / uongo. Anasema wanasagamoyo wanajivunia kuwa na kampuni kubwa ya uzalishaji sumu.
        • Alitumia vitisho. Alitoa vijikaratasi vya kutisha kwa akina siti na Hashima.
        • Alifunga Runinga ya wazalendo ili isieneza kuhusu maandamano.
        • Alitumia tenga-tawala. Alitenganisha Tunu na Sudi walipomtembelea
        • Anatumia nguvu/udikteta. Anatoa amri kama ya kufunga soko.
        • Aliajiri watu wa ukoo wake ili wajilinde kwa mfano kenga.
        • Alitumia sheria vibaya – Aliamrisha Ashua kuwekwa ndani. (zozote 10x1)
  4.            
    1. Haya ni maneno ya Samueli matandiko anayejizungumzia. Yuko ofisini ya mwalimu mkuu. Amekuja kuchukua matokeo ya mtihani. (4x1)
    2.                 
      • Uzungumzaji nafsi - Samueli anajizungumzia.
      • Kinaya - Ni Samueli aliyeaibika si mwalimu.
      • Methali - mdharau biu hubiuka (3x2)
    3.        
      • Ni mwongo - Alimdanganya Nina kuwa ni mwerevu shuleni.
      • Ni mwoga - Alitaka kutorokea babake.
      • Hana matumaini - Anataka kujiua.
      • Hana bidii - Anashindwa na masomo (2x1)
    4.       
      • Babake Samueli anauza mali yake ili asomeshe watoto.
      • Babake Samueli anathamini elimu ya Samueli kuliko dada zake kama mwajuma na Bilha.
      • Samueli anatembea muda wa kilomita sita ili atafute elimu.
      • Samueli anaogopa kuzungumza na babake kuhusu matokeo yake.
      • Mwalimu mkuu alimdharau Samueli kwa kumrushia matokeo yake.
      • Samueli hakutaka kuonyesha matokeo yake kwa wenzake alipoanguka.
      • Samueli hakutia bidii masomoni mwake kwani hata majibu yake si sahihi.
      • Samueli alipoanguka mtihani wake alikosa matumaini na kutaka kujiua. (zozote 8 x 1)
  5.        
    1. Haya ni maneno ya msimulizi ambaye ni mashaka anayejizungumzia. Anakumbuka maisha yake ya awali na waridi. Mawazo haya yako akilini mwake. ( 4x1 )
    2.      
      • Kinaya - Alipenda waridi lakini wazazi hawakupenda.
      • Chuku - Nilimpenda kufa.
      • Uzungumzi nafsi - Anajizungumzia mwenyewe. (3x2)
    3.       
      • Ni maskini - Waridi alimtoroka.
      • Ni mwenye mapenzi ya dhati - Alipenda waridi.
      • Mwenye bidii - Alifanya kazi kama mlinzi (2x1)
    4.         
      • Nyumba ya mashaka ni yenye paa la debe linaloingiza mvua .
      • Nyumba yake imepakana na choo.
      • Aliishi kwa chumba ndani ya nyumba.
      • Alikuwa na watoto saba na wavulana waliishi kwa jirani.
      • Alifanya kazi duni ya ulinzi katika zuia wizi security(zws)
      • Hakuwa na samani ndani ya nyumba yake.
      • Waridi alimuacha kwa sababu ya umaskini.
      • Wazazi wake walifariki akiwa mchanga.
      • Alilewa na Bi, Kidebe aliyekuwa na maumivu.
      • Alilazimishwa ndoa na mzee Rubeya.
      • Alifanya vijikazi ili kusaidia Bi Kidebe kujikimu. (8x1)
  6.                    
    1.           
      • Ukali wa jua unaharibu zao.
      • Soko la dunia ni mbaya.
      • Dini za kudhani zamsonga roho.
      • Analimia waroho au wenye pupa. (4x1)

    2.      
      • Tashbihi
        • Katika njia iendayo kondeni
        • Kama walivyofanya babuze zamani.
      • Balagha
        • Kuna jambo gani linamridhisha
        • Kuna siri inayomliwaza.
      • Tanakali za sauti – Alichekelea ha ha ha ha ...
      • Taswira - videge vya anga vinavyotumbuiza
      • Tashihisi – Nao umande kumbusu miguu.
      • Msemo - kumkaba koo – kuumiza.
      • Takriri - Laiti angalijua, laity angalijua. (4x2)
    3. Mkulima (1x1)
    4. Malalamishi/huruma (1x1)
    5. Kuboronga sarufi
      • Kama mtu aliye na hamu kubwa.
      • Lahaja - kotama. (2x1)
    6. Kila asubuhi anapita akiwa na jembe akielekea shambani. Kama walivyofanya babu zake.Ninapomuona huwa ana furaha kama mtu aliye na tamaa kubwa ya kulima na kutokwa na jasho ili apate kujilisha. (4x1)
  7.          
    1.      
      • Ukawafi
      • Tathlitha
      • Ukara (3x1)
    2. Anaonyesha vile mfanyakazi mwenye bidii ambaye anaugua na kushindwa kufanya kazi. (1x2)
    3.          
      • Lina mishororo mitatu kila ubeti
      • Lina beti tano
      • Kila mshororo umegawa vipande vitatu
      • Vina vya kati havifanani lakini vya mwisho vinafanana.Lina silabi hizi 8,4,7 (4x1)
    4.         
      • Inkisari – ngeushuruti
      • Tabdila - Utimile
      • Kufinyanga lugha - lakini kamwe haiwi. Zozote (2x2)
    5.     
      • Magonjwa
      • Kazi
      • Bidii
      • Dhuluma kutoka kwa waajiri. (3x1)
    6.       
      • Ningetaka kufika leo lakini mwili una maumivu.
      • Niweze kufanya kazi lakini mwili unakataa.
      • Ningependa kuwa mmoja wanaohusika lakini mwili umeshindwa. ( 4x1)

  8.           
    1.      
      1. Miviga ni sherehe za kitamaduni ambazo hufanywa na jamii yoyote katika kipindi maalum cha mwaka.
      2.      
        • Miviga huandamana na matendo au kanuni Fulani.
        • Miviga hufuata utaratibu maalum.
        • Miviga huongozwa na watu mahususi katika jamii.
        • Miviga huandamana na utoaji mawaidha.
        • Maleba maalumu huvaliwa na wanaohusika.
        • Miviga hufanyiwa mahali maalum.
        • Miviga huenda na wakati maalum.
        • Huhusisha imani ya dini husika. (8x1)
    2.           
      1. Ni uhodari wa kutumia lugha kwa ufundi wa kipekee.
      2.    
        • Hutumia lugha kwa njia inayovutia na kushawishi.
        • Hutumika katika miktadha kama kutoa hotuba kwa jamii.
        • Hukuza ukakamavu wa kuzungumza hadharani.
        • Hutumia tamathali za usemi kama vile jazanda.
        • Ulumbi huwa na urudiaji mwingi wa maneno.
        • Walumbi hutumia chuku kwa ufanisi.
        • Mlumbi huelewa utamaduni wa jamii.
        • Ulumbi hutumika katika shuguli za jamii.
        • Ulumbi hutumia viziada lugha. (8x1)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Royal Exam Series Post Mock Trial Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest