INSTRUCTIONS TO CANDIDATES
- Andika insha mbili.
- Insha ya kwanza ni ya lazima kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia
- Kila insha isipungue maneno 400
- Kila insha ni alama 20
- Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili
- Wewe ni mwandishi wa habari. Umemwalika mwenyekiti wa tume ya utangamano na uwiano wa kitaifa nchini studioni ili kuangazia kwa kina swala la ukabila ambalo limekita mizizi katika taifa. Andika dayolojia kati yenu.
- Nchi imekumbwa na mizozo mingi ya kijamii hivi karibini. Huku ukipendekeza suluhisho, jadili vyanzo vya mizozo hiyo.
- Andika kisa kitakachodhihirisha maana ya methali: Nyumba njema sio mlango, ingia ndani uone.
- Tunga kisa kitakachoanza kwa maneno yafuatayo: Giza lilikuwa limechukua milki ya viumbe wote duniani. Nyota zilitoa mwanga hafifu na mwezi ulikuwa ushatua. Katika giza hilo la kaniki.
MARKING SCHEME
- Hii ni insha ya dayolojia, sura ya dayolojia izingatiwe
Kuwe na kichwa na kitaje neno dayolojia mf
Dayolojia kati ya mwandishi na waziri kuhusu…
Kichwa kiandikwe kwa herufi kubwa, kipigiwe mstari
Kuwe na utangulizi mfupi kuhusu mada mabanoni
Mtindo wa kitamthlia ufuatwe
Koloni zitumiwe kutenga majina ya wahusika na maneno wasemayo
Wahusika wote wawili wachangie hoja
Kwa kila hoja kuwe na suluhu mwishoni mwa aya
Maelezo katika mabano yawe kwa uchache sana
Baadhi ya hoja;
Mapendeleo kazini kwa misingi ya kikabila
Kuchagua viongozi kufuatia misingi ya kikabila
Kuchukia wasio wa kabila lako
Kudharau mila na desturi za kabila jingine
Kuzuka kwa makundi haramu ya kikabila
Matumizi ya lugha za kienyeji katika taasisi za umma
Kufurusha watu kutoka katika maeneo yanayoaminika kuwa ngome ya kabila fulani
Ukatili dhidi ya watu wa kabila jingine n.k
Suluhu
Kuhubiri Amani hasa katika maeneo ya kazi
Watu waajiriwe bila kuzingatia misingi ya kikabila
Kuchagua viongozi kulingana na utendakazi sio ukabila
Wanaochochea watu kufurushwa makwao kuchukuliwa hatua za kisheria
Kuheshimu mila, desturi za jamii nyingine n.k - Mizozo ya kijamii
Umiliki wa rasilimali muhimu kama maji, mashamba nk
Imani potovu zinazodunisha baadhi ya jamii
Uchochezi wa kisiasa
Mila kinzani
Mipaka ya kihistoria iliyowekwa na wakoloni
Mfumo wa elimu unaotweza baadhi ya mila na kulemeza nyingine
Migao ya nyadhifa na kazi isiyo sawa
Kutweza matumiza ya lugha za makabila mbalimbali katika vyombo vya habari
Suluhu
Ugavi sawa wa rasilimali
Utangamano wa jamii kupitia asasi mbalimbali kv dini
Kudhibiti kampeni za kisiasa
Kuchochea mwingiliano wa jamii kupitia ndoa
Kuwa na mipaka mipya ya maeneo mbalimbali isiyotenganisha jamii kikabila
Migao ya nyadhifa na kazi iwe sawa
Tumia lugha rasmi nay a taifa katika vyombo vya habari - Methali
Mwanafunzi atunge kisa kimoja kitakachoafiki maana ya matumizi ya methali hii
Kisa kiwe cha kuvutia
Mapambo ya lugha yaonekane
Makossa ya sarufi na hijai yaepukwe
Mtahiniwa aeleze pande zote mbili za methali
Uzuri wa nyumba huwezi kuujua kwa kuangalia tu ukiwa nje. Lazima uingie ndani.
Tabia za mtu si mavazi au umbo lake la nje ila ni matendo yake.
Huwezi kueleza uzuri wa kitu au mtu kwa kumwangalia umbo au mavazi. Lazima utangamane naye ujue tabia yake - Hii ni insha ya mdokezo
Mtahiniwa sharti aanze kwa maneno hayo
Asipoanza kwa maneno hayo, ataadhibiwa kimtindo
Mtahiniwa atunge kisa kitakachooana na maneno hayo
Kisa kiwe cha kushtua, kuhuzunisha na kudhihirisha hali fulani ya hofu
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Joint Pre-Mock Exams 2021/2022.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students