Kiswahili P1 Questions and Answers - Nambale Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  1. Andika insha mbili . Swali la kwanza ni la lazima.
  2. Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
  3. Kila insha isipungue maneno 400.
  4. Kila insha ina alama 20.

KWA MATUMIZI YA MTAHINI PEKEE

SWALI

UPEO

ALAMA

1

20

 
 

20

 

JUMLA

40          

 


MASWALI

  1. LAZIMA
    Vijana wana nafasi kubwa katika kuimarisha mshikamano wa kitaifa. Andika tahariri kwa gazeti la KIU kuunga mkono kauli hii.
  2. Pendekeza njia mbalimbali zinazoweza kutumiwa kukabiliana na baa la njaa nchini.
  3. Andika insha itakayothibitisha ukweli wa methali ifuatayo:
    Epuka maovu nayo yakuepuke.
  4. Andika kisa kinachomalizikia kwa maneno yafuatayo.
    ……………. Sasa ninaelewa maneno yake kuhusu kufanya maamuzi ya hekima au busara. Sasa nimepata baraka za wazazi na ridhaa ya kuishi pamoja.


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

1. Swali la lazima
Hii ni insha ya tahariri
Tahariri kwa Gazeti la Kiu

  1. SURA
    1. Kichwa – Jina la gazeti, tarehe na mada
  2. Utangulizi
  3. Mwili au maelezo kiaya
    Yanaweza kuwa ni maoni au msimamo wa mhariri au msimamo wa gazeti.
  4. Iwe na hitimisho k.m. jina la mhariri na wadhifa wake.

MAUDHI:

  1. Ujana ndio wakati ambao watu huwa na nguvu/nishati nyingi
  2. Vijana ndio wengi zaidi kwa hivyo wanaweza kuwafikia raia wengi.
  3. Vijana wanathaminiana na kuaminiana, kwa hivyo ni rahisi kwao kuwashawishi wenzao.
  4. Wanaweza (kujisajili kusoma katika vyuo vilivyo) katika maeneo mbalimbali (nchini) ili kutagusana na raia wa makabila tofautitofauti.
  5. Kushiriki shughuli za kimasomo k.v makongamano ambako kunawawezesha vijana kuja pamoja.
  6. Vijana wanaweza kuhimizana kuchagua viongozi kutoka makabila mbalimbali na kupalilia mwelekeo wa kitaifa.

2. Njia tofautitofauti za kukabiliana na baa la njaa

  1. Kuthibiti bei ya bidhaa za kimsingi ili isizidi uwezo wa kifedha/mapato ya wananchi wengi. 
  2. Kuthibiti bei ya mafuta na umeme ambazo kwazo gharama ya uzalishaji au kufanya biashara hutegemea kwa kiasi kikubwa.
  3. Usambazaji wa miradi ya unyunyiziaji maji katika maeneo kame na maeneo mengine nyakati za kiangazi.
  4. Kuimarisha usalama kote nchini ili wananchi waendelee na shughuli mbalimbali za uzalishaji
  5. Kuboresha miundomsingi/sekta ya uchukuzi ili kurahisisha usafirishaji.
  6. Kuhimiza wakulima kupanda mimea ya kiasili hasa katika maeneo ya mashambani. Baadhi yavyo havihitaji mbolea na hustahimili kiangazi.
  7. Kutoa mafunzo kwa wakulima kuhusu mbinu bora za kilimo, uhifadhi wa mavuno, matumizi wekevu ya mavuno/chakula, n.k. kupitia idara husika na hata mashirika yasiyo ya kiserikali yahusishwe.
  8. Kufadhili wasiojiweza kwa kuwapa pembejeo.
  9. Kuwa na sera madhubuti ya umiliki wa ardhi.
  10. Upanzi wa miti uanzishwe/uendelezwe ili kuboresha hali ya anga hasa mvua.
    TANBIHI: Mtahiniwa afafnue mawazo/hoja zake kiaya kuhusu njia kadhaa zinazoweza kutumiwa kukabiliana na baa la njaa.

2. Maana: Mtu anapoepuka mambo mabaya hawezi kufikwa na ubaya wowote Tunafunzwa na methali hii kwamba tujienge na mambo mabaya yanayoweza kutuletea madhara.
Ruwaza ijitokeze kama ifuatavyo:
Mhusika avutiwe na jambo baya, alishiriki kisha apatwe na madhara au jambo baya limvutie na afanye jitihada aepukane nalo.
Mtahiniwa aandike kisa kitakachooana na methali hii. Baadhi ya visa ambavyo vinaweza kusimuliwa ni kama vifuatavyo:

  1. Mhusika ajiingize katika vitendo vya wizi, asiache licha kuonywa kwa kukera wengi, baadaye akamatwe na hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yake.
  2. Mhusika aanze hulka ya uasherati/uzinzi/uzinifu, lakini asizingatie mawaidha anayopewa, aambukizwe ugonjwa wa zinaa.
  3. Mhusika ashiriki utumizi wa dawa za kulevya. Akose kutambua kuwa jambo hili litamletea madhara, baadaye aathirike mno.
    n.k.

4.Hii ni insha ya mdokezo. Mtahiniwa ajihusishe na kisa (nafsi ya kwanza).Ruwaza ya kisa idhihirishe kwamba mhusika alikuwa anapotoka na kuvuruga uhusiano na wazazi wake lakini alipata mawaidha/mwelekeo/wosia kutoka kwa mhusika mwingine na uhusiano mwema ukarejeshwa baina yake na wazazi wake. Baadhi ya visa ni:

  1. Mhusika anayetoroka nyumbani kwa kukosana na wazazi, apewe ushauri kasha aamue kurudi na kuomba msamaha na kuendeleza maisha pamoja na wazazi wake.
  2. Mhusika anayetamauka kimasomo kwa sababu Fulani, jambo hili livuruge uhusiano na wzazi wake, apewe ushauri na mwalimu au mwanafunzi mwenzake, asome afaulu na kufurahisha wazazi.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili P1 Questions and Answers - Nambale Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest