Kiswahili P3 Questions and Answers - Nambale Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

 MAAGIZO KWA MTAHINIWA

  1. Jibu maswali manne pekee
  2. Swali la kwanza ni lazima
  3. Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki.
  4. Usijibu maswali mawili kutoka shemu moja.

Kwa matumizi ya mtahini pekee

Swali

1

2

3

4

5

6

7

8

JUMLA

                   


MASWALI

SEHEMU A: HADITHI FUPI

SHIBE INATUMALIZA NA SALMA OMAR HAMAD
1. SWALI LA LAZIMA

“… Na ati tuliopewa hatupokonyeki…”

  1. Yaweke maneno haya katika muktadha wake. (al 4)
  2. Taja mbinu mbili za sanaa zilizotumika katika dondoo hili (al 4)
  3. Fafanua sifa zozote nne za mzungumzaji (al 2)
  4. Kwa kurejelea hadithi ‘shibe inatumaliza’ tathmini jinsi ubadhirifu wa mali ya umma umesawiriwa katika hadithi hii (al 10)

SEHEMU YA B
RIWAYA: CHOZI LA HERI: ASSUMPTA MATEI

2. “…liandikwalo ndilo liwalo? since when has man ever changed his destiny?”

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (al 4)
  2. Bainisha mbinu tatu za kimtindo zinazojitokeza katika dondoo hili. (al 6)
  3. Kwa kuzingatia hoja kumi, jadili jinsi ambavyo hali ya, liandikwalo ndilo liwalo”, inavyojitokeza katika Chozi la Heri. (al 10)
    Au

3. Maovu yametamalaki katika riwaya ya Chozi la Heri. Thibitisha (al 20)

SEHEMU C
TAMTHILIA: KIGOGO

4. “na uuchunge sana ulimi wako usikutome kwenye bahari mchafukoge usi…”

  1. Fafanua muktadha wa dondoo hili. (al 4)
  2. Eleza sifa mbili za msemaji (al 2)
  3. Eleza umuhimu wa msemewa katika kazi hii (al 2)
  4. Kwa kurejelea dondoo hili na tamthilia kwa jumla, eleza jinsi msemewa na wenzake walitiwa katika bahari mchafukoge. (al 12)
    AU

5. Tamthilia ya Kigogo ni ya kisasa. Thibitisha ukweli wa kauli hii. (al 20)
6. SEHEMU YA D: USHAIRI
Jibu swali la sita au la saba
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yafuatayo.

Msambe naja kuteta, nina wema wa kalima,
Moto wanikatakata, maini yangu yachoma,
Ili nipate takata, ukweli wote ‘tasema,
Anayekataa pema, pabaya panamuita.

Bahati ni kama nyota, humemeta na
Kuzima, Sikimbilie
mafuta, ukatae Kula
sima, Anayekataa pema,
pabaya Panamuita.

Haraka zina matata, angaza mbele na
Nyuma, Tenda mambo kwa kusita,
Usije ukalalama, Keti
pako ukipata, Kwa muradi
wa uzima, Anayekataa
Pema, pabaya panamuita.

Pema si penye mafuta, au pa wali
Na nyama, Pema watu hutafuta,
Utulivu na hekima, Si hoja penye
Ukata, pa watu hali ya nyuma,
Anayekataa pema, pabaya
Panamuita

Mahali pema ambata, kwa vitendo na huduma,
Sikae penye matata, palipojaa hasma,
Lau kama pamemeta, hapafai kwa daima,
Anayekataa pema, pabaya panamuita
Maswali

  1. Lipe anwani mwafaka shairi hili. (alama 1)
  2. Bainisha bahari mbili za shairi hili. (alama 2)
  3. Eleza muundo wa shairi hili. (alama 4)
  4. Fafanua dhamira ya mshairi. (alama 1)
  5.  Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari. (alama 4)
  6. Onyesha jinsi mshairi alivyotumia uhuru wake. (alama 3)
  7. Kwa kutoa mifano, bainisha tamathali mbili za usemi zilizotumika katika shairi hili. (alama 2)
  8. Eleza maana ya msamiati ufuatao. (alama 3)
    1. Kalima
    2. Mafuta
    3. Ukata

7. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

  1. Mbiu naipuliza, kwawa hapana ng’ambo,
    Kwa aningoja ‘mesikia, inaumiza matumbo,
    Kwa upole sitafyoa, hata kamna kwa
    kimombo, Yafaa jihadharia, maisha ya s’ende kombo.
  2. Maisha ya s’ende kombo, kututoa yetu ari,
    Zingatia haya mambo, wetu wale
    zimukiri, Kuwa wana kwa viambo,
    huwa Baraka na kheri watunzeni
    na maumbo, msie zusha hatari.
  3. Msije zusha hatari, na nyingi hizi zahama,
    Wazazi haya si siri, mawi mnayoandama
    Twaelezea kwa uzuri, matendoyo
    yatuuma Watoto tunayo mori, ni lini
    mtaja koma?
  4. Ni lini mtaja koma, na pombe siso halali?
    Sio baba sio mama, mbona ny’
    hamtajali? Mwafa ja nzi twasema,
    mwatua chabi la hali Hangaiko acha nyuma,
    kwani hamuoni hili?
  5. Kwani hamuoni hili, kila saa mwapigana Nyumbanizo hatulali, jehanamu tumeona
    Mwatusumbua akili, twaumia ten asana Achene na ukatili, kwani upendo hamna.
  6. Kwani upendo hamna, kamam mbwa mwatuchapa
    Mwatuchoma sisi wana, mio yetu yatupapa
    Pa kujificha hatuna, tumebaki tukitapa
  7. Tumevujwa na mifupa, hata leo uke wetu,
    Mwatubaka na kuapa, kutung’ata nyi’ majitu,
    Hayo makeke na pupa, mtakoma utukufu
  8. Mtakoma utukufu, nakutumia miki
    Na tabia zenye kutu, tumechoka nayo chuki
    Hatutakubali katu, kutendewa yenye siki Serikali fanya kitu,
    kwani nasi tuna haki

Maswali

  1. Fafanua tamathali nne za usemi zilizotumiwa katika shairi hili. (alama 2)
  2. Taja nafsi nne katika shairi hili. (alama 1)
  3. Eleza bahari mbili zinaowakilishwa katika shairi hili. (alama 4)
  4. Andika ubeti wa nne kwa lugha ya nathari. (alama 4)
  5. Eleza maudhui matatu yanayojitokeza katika shairi hili. (alama 3)
  6. Eleza umuhimu wa mbinu mbili amabazo mshairi ammetumia kutosheleza mahitaji ya kiarudhi. (alama 4)

SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI
8. Hamkuona jinsi tulivyowapiga magoli
Hamkuona vile tuliwala chenga kila mara
Itakuwaje timu mbovu kama hii
Kuchezea miamba kama sisi
Niliwafunga baada ya sekunde wakati ule nitashindwaje leo?
Maswali

  1. Tambua kipera kinachodokezwa na maelezo haya na ukifafanue (al 2)
  2. Fafanua umuhimu wa kipera cha fasihi ulichotambua katika (a) (al 8)
  3. Fafanua sifa zozote tano za mawaidha (al 5)
  4. Ni changamoto zipi zinazoweza kumkumba mtafiti akifanya utafiti wa soga nyanjani(al 5)


MWONGOZO

1. SEHEMU A
“… Na ati tuliopewa hatupokonyeki…”

  1.                              
    1. Haya ni maneno yake mbura
    2. Alikuwa katika uwanja wa sherehe ya mzee mambo ya kusherehekea mwanawe kuingia nasari. Anajihisi ya kwamba
    3. amezinduka na kugundua jinsi walivyokuwa wakiwanyanyasa wananchi ambao wangezinduka. (al 4)
  2.                      
    1. Yaweke maneno hayakatika muktadha wake.
    2. kejeli – matumizi ya neno ati
    3. kinaya- tuliopewa ni kinaya kwa kuwa walikuwa wamenyakuwa kutoka kwa wananchi kimabavu (al 4)
  3. Fafanua sifa zote nne za mzungumzaji.
    Mzungumzaji ni mbura
    1. ni mlafi-wanaunga foleni na kula sana
    2. Mwenye mapuuza-ingawa wanafahamu uzembe uliopo na unyakuaji wa mali ya umma na hawafanyi kitu
    3. Mbadhirifu-wamehusika katika kufisidi hazina ya taifa
    4. Ni mkweli/ aliyezinduka -anatambua makosa yao kama viongozi
    5. Ni mbinafsi- anakula chakula bila kujali wananchi wengine
    6. (zozote nne) (al 4)
  4. Kwa kurejelea hadithi ‘Shibe inatumaliza’ tathmini jinsi mwandishi amelishughulikia suala la ubadhirifu wa mali ya umma. (al 8)
    1. Sasa na mbura kulipwa mshahara kwa kushikilia wizara ambayo ingefanywa na mtu mmoja
    2. Sasa na mbura kula kwa niaba ya watu wengine
    3. Dj kuuza dawa ambazo zilipaswa kutumika na wananchi katika hospitali za kiserikali
    4. Dj kutolipia huduma za umeme na maji.
    5. Dj kulipwa mabilioni kutumbuiza watu katika sherehe za kibinafsi
    6. Mzee mambo kulipwa mshahara mwingi bila kazi
    7. Magari ya serikali kutumika katika sherehe za kibinafsi kubeba Watoto
    8. Watu wanakula kupita kiasi katika sherehe ya mzee mambo -sasa na mbura
    9. Vyombo vya Habari kupeperusha sherehe ya kibinafsi

SEHEMU YA B- CHOZI LA HERI
2.Eleza jinsi maovu yametamalaki katika riwaya ya Chozi la Heri.

  • katika jamii hii kuna biashara haramu kama ile ya uuzaji wa dawa za kulevya. Dick alipotekwa nyara alilazimika kuuza dawa za kulevya kwa muda wamiaka kumi
  • kuna ukabila, suala la ukabila linajitokeza wakati kulizuka vita vya baada ya kutawazwa kwa mwekevu
  • usaliti mzee kedi anamgeukia Ridhaa na aila yake
  • malezi mabaya-mamake sauna kuficha tendo la babake sauna kumpachika mimba
  • uuzaji wa Watoto-mtandao wa walanguzi wa bi kangara
  • kutupa mtoto baada ya kujifungua -Riziki immaculate
  • wizi na uporaji wa mali yaw engine- wakati vita vya baada ya kutawazwa kuzuka , watu walionekana kupora maduka ya kihindi,kiarabu n ahata waafrika wenzao
  • wanawake kuavya mimba katika jamii hii- sauna anaavya mimba ya babake
  • ndoa za mapema- wasichana kuozwa kwa vikongwe kama pete
  • matumizi ya pombe haramu – vijana wa vyuo vikuu wanabugia na kufariki
  • kutowajibika kwa wasimamizi wa hospitali -ukosefu wa dawa
  • visingizio- Lemi anasingiziwa
  • Dhuluma kwa wafanyikazi kv Naomi na mwajiri wake
  • kuna mauaji- watu wengi walipoteza wapendwa katika ghasia za baada ya uchaguzi
  • ubakaji- lime na mwanaheri wanabakwa
  • Wanawake wanawacha waume na aila zao- umulkheri wanaachwa
  • wazazi wanahusiana kimapenzi na wana wao mfano ni Sauna
  • wazazi wa zohali wanamwachia kazi zote hii ni ajira kwa watoto
    (Zozote 20x1=10)

3. “….liandikwalo ndilo liwalo? Since when has man ever changed his destiny”

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili.
    • Maneno ya Terry
    • Akimwambia Ridhaa
    • Nyumbani kwao
    • Baada ya kugundua kuwa anaamini ushirikina
    • Ni mawazo ya Ridhaa akikumbuka maneno aliyoambiwa na mkewe Terry
    • Kwa sababu ya kuamini kuwa milio ya bundi na kerenge’nde huashiria jambo Fulani lingefanyijka.
    • Yuko kando ya vifusi vya nyumba yake iliyochomwa
    • Baada ya familia yake kuchomewa ndani.
  2. Bainisha mbinu tatu za kumtindo zinazojitokesa katika dondoo hili. (al 6)
    • Methali –liandikwalo ndilo liwalo
    • Kuhamisha ndimi/msimbo-kauli ya kutumia sentensi nzima kwa lugha nyingine.
    • Since when has man ever changed his destiny?
      Tanbihi: mbinu hii si kuchanganya ndimi. Atakayeandika hivi asituzwe.
    • Swali la balagha – “liandikwalo ndilo liwalo?
      Since whaen has man ever changed his destiny?”
      3x2
  3. Kwa kuzingatia hoja kumi, jadili jinsi ambavyo hali ya, “liandikwalo ndilo liwalo”, inavyojitokeza katika Chozi la Heri. (al 10)
    • Neema na Mwangemi wanajitahidi kupata mtoto lakini hawafanikiwi na wanaishia kumpanga Mwaliko.
    • Wafuasi wa Mwanzi wanajaribu kushinda wa mwekevu lakini wanashindwa.
    • Kaizari anajitahidi kuzuia wahuni wasiwabake binti zake lakini wanamzidi nguvu na kuwabaka.
    • Lunga anajitahidi kumrithia na kumpendekeza mkewe Naomi lakini hatimaye anamtoroka na kumwachia Watoto
    • Kiriri anampinga Annette asiende ughaibuni lakini anampuuza na kuhamia huko.
    • Kiriri anawasihi wanawe warudi nyumbani lakini waliendelea kuishi ughaibuni hata baada ya kukamilisha masomo yao.
    • nyanyake Pete anajizatiti kupinga ndoa ya Pete lakini hatimaye Pete anaozwa.
    • Kipanga anataka kuambiwa babake halisi baada ya aliyemdhania kuwa babake kumkana lakini mamake hakumwambia.
    • hata baada ya mabwanyenye kutoa hongo ili nyumba zao zisibomolewe katika mtaa wa Tononokeni, zilibomolewa.
    • Dick anakataa kutumiwa na Buda kulangua dawa za kulevya lakini anamtishia na baadaye kuuza dawa za kulevya.
    • Naomi alimtoroka Lunga kwa sababu ya umaskini lakini anaishia kuteseka Zaidi na baadaye kufa
    • Amize Lucia wanajizatiti kupinga ndoa ya Lucia lakini baadaye Lucia anaolewe.
    • Wanaume wanatishia kumtusi Mwekevu anapojitosa siasani ili kumvunja moyo lakini anavumilia mpaka anachaguliwa kuwa kiongozi wa Wahafidhani.
    • Pete anakunywa dawa ya kuua panya ili afe lakini anapelekwa kituo cha afy cha Mwanzo Mpya na kuendelea kuishi.
    • Pete anajaribu kuavya mimba ya mtoto wake wa pili na wa tatu lakini anaishi kuwazaa watoto hawa.
      (zozote 10x1=10)

SEHEMU C: TAMTHILIA YA KIGOGO
4. “Na uuchunge sana ulimi wako usikutome kwenye bahari mchafukoge usi…”

  1. Fafanua muktadha wa dondoo hili. (al 4)
    • Maneno haya yanasemwa na Kenga. Anamzungumzia sudi, wakiwa katika karakana yao kwenye soko la Chapakazi. Kenga anamwita Tunu hawara jambo linalomkasirisha Sudi baada ya kukataa kumchongea ngao kinyago
  2. Eleza sifa mbili za msemaji. (al 2)
    1. Katili - Anamwambia Majoka aache moy wa huruma ili polisi watumie nguvu zidi kuwatawanya waandamanaji
      • Anashirikiana na Majoka kupanga kifo cha Jabali
      • Anapanga mauaji ya Tunu.
      • Anapanga kifo cha Chopi.
    2. Kibaraka - Ni kibaraka wa Majoka. Anataka kujua kama shujaa anayechongwa na Sudi anatambuliwa na Majoka.
      • Anakubali yote anayoambiwa na Majoka.
    3. Mshauri mbaya - anamshauri Majoka kulifunga soko.
      • Anamshauri pia atangaze kuwa maandamano ni haramu
      • Anakubali pendekeso la Majoka la kufunga runinga ya mzalendo
    4. Mwenye mapuuza/asiyewajibika
      • Anasema kuwa ‘Tunu hawezi kupigiwa kura hata!’
      • Anapoona kinyango cha mwanamke kikichongwa, anasema, “Tena ni wa kike? Sagamoyo ishawahi kuwa na mashujaa wa kike kweli?” Anakataa kufuatilia ili ajue ni nani hasa anayechongwa, na anavyoathiri utawala wa Majoka.
    5. Mwenye taasubi ya kiume
      • Anauliza, “Tena ni wa kike? Sagamoyo ishawahi kuwa na mashujaa wa kike kweli?
    6. Mpyaro
      • Anamwita Tunu haware anaposema, “umelishwa kiapo na huyo hawara wako, sio?’
        (zozote mbili)
  3. Umuhimu wa sudi
    • ni kielelezo cha watu wazalendo wanaojitolea kupigania haki katika jamii
    • ni kielelezo cha watu wenye ujuzi katika jamii kwa sabu alikuwa mchongaji Hodari
    • ni kielelezo cha watu waliosoma katika jamii kwa kuwa alifanya uanasheria

(d)JINSI SUDI NA WENZAKE WALITIWA KATIKA MCHAFUKOGE

  1. Kutiwa jela- ashua anatiwa jela
  2. Kutishwa-hashima wanatupiwa vikaratasi wahame
  3. Kufungiwa soko-wasifanye biashara
  4. Kuuliwa- jabali kuuliwa na majoka na vijana kuuwawa
  5. Kuongezwa mshahara na kupandishiwa kodi-walimu na madaktari
  6. Kupewa ahadi hewa-sudi kuahidiwa kupelekwa ughaibuni
  7. Matumizi ya vyombo vya dola-polisi wanawaua vijana
  8. Kunyakuliwa ardhi- ya soko la chapakazi ili majoka ajenge hoteli ya kifahari
  9. Kuvunjwa miguu-tunu
  10. Kupigwa-tunu na waandamanaji
  11. Kusimangwa-tunu anasimagwa na walevi
  12. Fumanizi- majoka kumwita Ashua ili amfumanishe na mkewe
  13. Ubaguzi – kandarasi kutolewa kwa vikaragosi
    AU

5. Tamthilia ya Kigogo ni ya kisasa . Thibitisha ukweli wa kauli hii. (al 20)

  1. Kuwepo kwa migomo katika tamthilia. Nchi nyingi duniani zinakumbwa na migomo ya wafanyakazi.
    Hii ni kama ilivyo katika Kigogo ambapo walimu na madaktari wanagoma kwa kuwa wanalipwan mishahara duni.
  2. Kuwepo kwa urithishaji wa uongozi. Viongozi wengi duniani hurithisha wanao au watu wa koo zao uongozini. Majoka anamwambia Kenga kuwa alikuwa na azma ya kumtangaza Ngao Junior kama mrithi wake wa kisiasa katika sherehe za kuadhimisha kuzaliwa kwake.
  3. Kuwepo kwa maandamano ya wanaharakati. Utawala wa kiimla utokeapo katika nchi mbalimbali duniani, hutokea wanamapinduzi ambao huwa na lengo la kuzikomboa nchi zao kutokana na tawala hizo. Tunu, Sudi na wafuasi wao wanashirikiana kumwondoa Majoka mamlakani.
  4. Utegemezi wa mikopo na misaada kutokana ughaibuni. Sagamoyo, kama nchi nyingine zinazoendelea duniani, inategemea mikopo na misaada kutoka nchi za ughaibuni. Mikopo yenyewe italipwa kwa kipindi cha miaka mia moja.
  5. Baadhi ya washauri wa viongozi wengi duniani huwapotosha. Kenga anmpotosha Majoka kwa ushauri mbaya kisha mwishowe anamsaliti.
  6. Wananchi kulipa kodi bila kupata huduma wanazostahili. Baadhi ya serikali katika nchi mbalimbali hukusanya kodi na kukosa kuwapa wananchi huduma muhimu. Serikali ya Majoka inakusanya kodi yay a juu lakini haidumishi usafi wa mazingira. Soko la chapakazi lina uvundo na maji-taka. Hii ni licha ya wanasagamoyo kulipa kodi ambayo ingesaidia katika uzoaji wa taka hizi. Tunu analalamikia kutokuwepo kwa huduma za matibabu, usafiri, maji safi, nguvu za umeme, elimu na kadhalika.
  7. Sera mbaya za uongozi zinazosababisha umaskini. Nchi nyingi duniani zimekumbwa na umaskini kutokana na ser mbovu za uongozi. Majoka na vikaragosi wake wanafunga soko la chapakazi linilotegemewa na watu wengi. Hali hii inasababisha umaskini. Wahusika kama vile Ashua wanashindwa kukidhi mahitaji ya familia zao.
  8. Utabaka. Utabaka huwepo katika nchi nyingi duniani. Huwa pana mpaka mkubwa baina ya matajiri na maskini. Hii ni kama ilivyo katika Sagamoyo.
  9. Viongozi mashuhuri kuidhinisha biashara haramu. Katika baadhi ya nchi duniani, viongozi mashuhuri ndio wanaoidhinisha biashara haramu. Mamapima anamweleza Tunu kuwa alikuwa na kibali cha uuzaji wa pombe haramu kutoka kwa Majoka.
  10. Viongozi wengi katika baadhi ya nchi duniani husahau wanachi waliowachagua. Viongozi kama hawa huendelea kujilimbikizia mali. Majoka anaendelea kujinufaisha kwa mali ya uuma akiwa na vikaragosa wake huku wananchi wakihangaika.
  11. Viongozi katili kuwaangamiza wapinzani wao. Katika nchi zinazoongozwa na viongozi wa kiimla, wapinzani huuawa huku wengine wakijeruhiwa vibaya. Jabali anauawa kwa amri ya Majoka huku Tunu akijeruhiwa vibaya.

6. SEHEMU YA D: USHAIRI

  1. Lipe anwani mwafaka shairi hili (al 1)
    Anayekataa pema, pabaya pamuita
  2. Bahari mbili za shairi hili (al 2)
    1. sakarani
    2. Masivina – halina urari wowote wa vina
  3. Muundo wa shairi hili (al 4)
    1. Beti nne
    2. Lina kibwagizo ‘Anayekataa pema, pabaya pamuita’.
    3. Halijazingatia mtoshelezo wa mishororo ktk kila ubeti
    4. Halina urari wa vina
  4. Dhamira ya shairi ni kuhimiza kuhusu umuhimu wa uadilifu na mienendo inayofaa. (al 1) hakiki
  5. Mahali pema si pale ambapo pana vizuri bali palipo na utulivu na hekima. Hata kama pana umaskini, mtu anapokataa mahali pema huitwa na pabaya. (al 4)
  6.                      
    1. Inkisan - Tasema
      - sikimbilie
    2. Msamiati wa kale- mato badala ya macho
    3. Kuboronga sarufi – keti pako ukipata
    4. Tabdila – muradi (zozote 3)
  7. Tamathali mbili za usemi (al 2)
    Tashbihi – Bahati ni kama nyota.
    Jazanda - mafuta, wali na nyama zimetumika kijazanda (zozote 2)
  8. Maana ya
    1. Kalima – usemi
    2. Mafuta – mng’aro
    3. Ukata - umaskini

7. USHAIRI

  1. Maswali balagha- na pombe siso halali?
    Mbona ny’ hamtajali.
    Isitiari- kutang’ata nyi majitu
    Tashbihi- kama mbwa mwatuchapa
    Mwafa ja nzi. (zozote 1x4)
  2. Mtoto (mwana)
  3. Lina mishororo mine hiyo ni Tarbia.
    Kina cha kubwagiza kimechukuliwa ili kuwa mwanzo wa ubeti unaofuata hivyo huitwa pindu au mkuju/nyoka.(zozote 1x2)
  4. Nilini wazazi wataacha kutumia pombe haramu na kuwajali watoto wao kwani wanakunywa na kuwaachia mateso na mahangaiko mengi bila kujali. (alama 4)
  5. Ukatili, malezi, ulevi. Mwanafunzi aeleze ipasavyo. (alama 3)
  6. Mazida –mshairi amerufusha baadhi ya … ili kuafikia urari wa k.m. nyumbanizo, matendoyo
    Liksani- mshairi amefupisha baadhi ya maneno pia kuafiki urari wa viua- mio, ny’
    Kuburanga sarufi- kwani upendo kamua badala ya kwani hamna upendo-ili kuleta urari wa viua katika mishororo. (mwanafunzi ataje mbili na kueleza.( zozote alama 2x2

8. SEHEMU YA E

  1. Majigambo
    Kipera hiki kinahusisha mhusika akijigamba kuhusu timu yake ambayo anaisifu kwa kufunga kwa sekunde (1x2)
  2. Umuhimu
    Hukuza ubunifu.kadiri mtu anavyotunga na kughani ndivyo anyokuwa mahiri
    Hukuza ufasaha wa lugha. Watunzi wengi wa majigambo huwa walumbi
    Ni nyenzo ya burudani. Huongoa wanaokuja kwa sherehe
    Hudumisha utu na utambulisho wa wanaume katika jamii
    Hufanya watuwaheshimiwe katika jamii
    Huhifadhi na kuendeleza Amani turathi na utamanduni wa jamii.
    Kitambulisho cha jamii.
    (zozote 1x8)
  3. Sifa za soga
    Huwasilishwa mbele ya watu
    Hugusia takriban vipengele vyote vya maisha ya binadamu
    Huibua maadili yanayohitaji kuzingatiwa
    Hujenga maudhui maalumu na ya aina nyingi kutegemea jinsia umri
    Hutumia lugha ya kuathiri hisia
    Aghalabu hutolewa na watu wenye umri mkubwa
    Hutolewa katika miktadha rasimu au iso rasimu
    Huwa na ufasaha mkubwa wa lugha (alama 5)
  4. Changamoto za utafiti nyanjani.
    Miundo misingi.
    Mawasiliano ya lugha/utofauti wa lugha
    Mtazamo hasi wa jamii husia.
    Ukeosefu wa usalama.
    Wahojiwa kudai kulipwa.
    Miundo misingi.
    Vizingitti vya kididni.
    Mwalimu ahakiki.(zozote 1x5)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili P3 Questions and Answers - Nambale Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest