Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Bondo Mocks 2021 Exams

Share via Whatsapp

MASWALI
LAZIMA 

  1. Kumekuwa na janga la ugonjwa wa korona lililoathiri sekta ya elimu nchini Kenya kwa kipindi kirefu, mwandikie barua nduguyo anayeishi ughaibuni ukimjulisha kuhusu athari za ugonjwa huu kwa wanafunzi nchini. (alama 20) 
  2. Mitandao ya kijamii ina faida nyingi kuliko hasara, jadili. (alama 20) 
  3. Andika kisa kinachoafiki methali:…. Nazi mbovu harau ya nzima. (alama 20) 
  4. Andika kisa kitakachokamilika kwa maneno yafuatayo: 
    … hivyo ndivyo ukurasa mpya katika kitabu cha maisha yangu ulivyofunguka. (alama 20) 


MWONGOZO WA MASWALI 

  1. Hili ni swali la barua ya kirafiki, 
    • Kuwe na anwani moja ambayo ni ya mwandishi (mtahiniwa) - Anwani ifuatwe na tarehe na mamkizi  kv kwa ndugu mpendwa nk 

      Baadhi ya maudhui. 
    • Vifo vya wazazi  
    • Shule kufungwa 
    • Mimba za mapema 
    • Kujiunga na magenge ya majambazi 
    • Matumizi ya dawa za kulevya 
    • Ukosefu wa mahitaji ya kimsingi kwa sababu ya wazazi kupoteza ajira 
    • Kubaki mayatima kwa kupoteza wazazi wao 
      KADIRIA HOJA ZA MTAHINIWA 
      TNB 
    • Asiyezingatia sura ya barua ya kirafiki aondolewe alama 4S baada ya kusahihisha. 
  2. FAIDA 
    • Kupasha habari kwa muda mfupi 
    • Burudani 
    • Nyenzo ya kuelimisha 
    • Kuunganisha watu 
    • Kwa kufanya biashara 
    • Kubuni nafasi za kazi kwa vijana 
    • Ushuru kwa nchi 
    • Kwa kufanyia utafiti 

      HASARA
       
    • Kueneza ugaidi 
    • Kueneza wizi 
    • Huathiri utamaduni 
    • Hufuruga maadili ya kijamii 
    • Hueneza maovu kama vile ponokrafia 
    • Hupelekea kuvunjika kwa ndoa kakika jamii 
      TANBIHI 
      KADIRIA HOJA ZA MTAHINIWA 
    • Mtahiniwa arejelee pande zote mbili za swali yaani faida na hasara na atoe msimamo wake,pia msimamo wake unaweza kudokezwa na idadi ya hoja anazotoa katika kila upande 
    • Asiyerejelea pande zote mbili akadiriwe katika kiwango cha C+ alama 10 yaani alama zisizidi 
    • kutegemea lugha na maudhui. Rejelea mwongozo wa kudumu 
  3. Hii ni insha ya methali 
    • Mtahiniwa abuni kisa kinachoafiki maana ya methali hii. 
    • Kisa kinaweza kuhusu mhusika fulani aliyepotoka kitabia kisha akawaathiri wenzake anaoingiliana nao. 
      AU 
    • Kitu kilichoharibika au kuoza na kuathiri vingine vilivyo karibu nacho 
    • Kisa lazima kirejelee sehemu mbili za methali yaani, 
    • Mtu aliyepotoka kimaadili na jinsi alivyowapotosha wenzake AU 
    • Kitu kilichoharibika na jinsi kilivyoharibu vitu vingine vilivyo karibu nacho TANBIHI 
    • Mtahiniwa anayerejelea sehemu moja ya methali ,insha yake  ikadiriwe chini ya alama 10 yaani kiwango cha C+ 
  4. Hii ni insha ya mdokezo ambapo mtahiniwa lazima ahitimishe kisa chake kwa dondoo hili. 
    • Kisa kionyeshe mhusika anayeingia katika hali nyingine au maisha kuchukua mkondo mpya.Kisa kinaweza dhihirisha hali kama vile: 
    • Msimulizi amepita mtihani au amefuzu na anaelekea kiwango kingine 
    • Amepata kazi baada ya kuitafuta kwa miaka mingi na akaanza maisha mapya 
    • Amejipata gerezani n.k 
    • KISA KISIMULIWE KATIKA NAFSI YA KWANZA

MWONGOZO WA VIWANGO
Karatasi hii imedhamiria kutahini uwezo wa mtahiniwa wa kuwasiliana na msomaji na kuwasilisha ujumbe kimaandishi, wenye utiririko mzuri kimawazo, lugha ya kuvutia na yenye mawazo asilia. Ubainifu mwingi na hati nadhifu. Kutegemea maagizo ya swali lenyewe na umahiri wa lugha, ni lazima kutilia mkazo mtindo, mada na uwezo wa mtahiniwa kufuata maagizo vilivyo.
Mtahini lazima asome insha yote ili aweze kukadiria viwango mbalimbali vilivyopendekezwa, yaani A, B, C ama D kutegemea mahali popote pale pafaapo kuikadiria insha ya mtahiniwa.
VIWANGO MBALIMBALI

KIWANGO CHA D
MAKI 01 – 05

  1. Insha ya aina hii haileweki kwa vyovyote, ama uwezo wa mtahiniwa wa kutumia lugha ni hafifu sana hivi kwamba mtahini lazima afikirie kile anachojaribu kuandika.
  2. Mtahiniwa hana uwezo wa kutumia maneno ya Kiswahili kwa njia inayofaa.
  3. Lugha imevurugika, uakifishaji usiofaa na insha ina makosa ya kila aina ya kisarufi, kimaendeleo, kimtindo n.k.
  4. Kujitungia swali na kulijibu
  5. Insha ya urefu wa robo ikadiriwe hapa

NGAZI MBALIMBALI ZA KIWANGO CHA D
D- ( Kiwango cha chini ) Maki 01 - 02

  1. Insha haina mpangilio maalum, na haieleweki kwa vyovyote vile. Kwa mfano, kunakili swali au 2. kujitungia swali na kulijibu.
  2. Kuandika lugha isito Kiswahili au kuchanganya ndimi
  3. Kunakili swali au maswali na kuyakariri
  4. Kunakili swali au kichwa tu

D (Wastani )
Maki 03

  1. Mtiririko wa mawazo haupo, na insha haieleweki.
  2. Mtahiniwa amepotoka kimaudhui
  3. Matumizi ya lugha ni hafifu mno
  4. Kuna makosa mengi ya akila aina

D+ (D YA JUU) MAKI 4 – 05

  1. Insha ya aina hii huwa na makosa mengi ya kila aina. Lakini unaweza kutambua kile ambacho mtahiniwa anajaribu kuwasilisha.
  2. Hoja hazikuelezwa kikamilifu / mada haikukuzwa vilivyo.
  3. Mtahiniwa hana uhakika wa matumizi ya lugha.
  4. Mtahiniwa hujirudiarudia.
  5. Insha itakayozingatia sura lakini ikose maudhui ikadiriwe hapa.

KIWANGO CHA C KWA JUMLA MAKI 06 – 10

  1. Mtahiniwa anajaribu kuishughulikia mada japo hakuikuza na kuiendeleza vilivyo.
  2. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe kwa njia isiyovutia / hana ubunifu wa kutosha.
  3. Mtahiniwa anaakifisha sentensi vibaya.
  4. Mtiririko wa mawazo unaanza kujitokeza japo kwa njia hafifu.
  5. Insha ina makosa mengi ya sarufi, ya msamiati na ya tahajia (hijai)
  6. Insha yenye urefu wa nusu ikadiriwe hapa.

NGAZI MBALIMBALI ZA KIWANGO CHA C
C- ( C YA CHINI ) MAKI 06 – 07

  1. Mtahiniwa ana shida ya kuwasilisha na kutiririsha mawazo yake.
  2. Mtahiniwa hana msamiati wa kutosha wala miundo ya sentensi ifaayo.
  3. Mtahiniwa anafanya makosa mengi ya sarufi, ya hijai na ya msamiati na insha yake haieleweki kwa urahisi.

C WASTANI MAKI 08

  1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe lakini kwa njia hafifu.
  2. Dhana tofautitofauti hazijitokezi wazi.
  3. Mtahiniwa hana ubunifu wa kutosha.
  4. Mtiririko wa mawazo ni hafifu na hana ufundi wa lugha unaofaa.
  5. Amejaribu kuishughulikia mada aliyopewa.
  6. Mtahiniwa ana shida ya uakifishaji.
  7. Mtahiniwa anafanya makosa mengi ya sarufi, ya hijai na msamiati lakini bado insha inaeleweka.

C+ (C YA JUU) MAKI 09 – 10

  1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri akizingatia mada lakini kwa njia isiyo na mvuto.
  2. Dhana tofauti tofauti zimejitokeza japo kwa njia hafifu.
  3. Kuna mtiririko wa mawazo japo hana ufundi wa lugha unaofaa.
  4. Misemo na methali zimetumika kwa njia hafifu.
  5. Ana shida ya uakifishaji.
  6. Kuna makosa ya sarufi, ya msamiati na ya hijai yanayoathiri mtiririko wa mawazo.

KIWANGO CHA B KWA JUMLA MAKI 11-15

  1. Katika kiwango hiki, mtahiniwa anaonyesha hali ya kuimudu lugha.
  2. Mtahiniwa anatumia miundo tofautitofauti ya sentensi vizuri.
  3. Mtahiniwa ana uwezo wa kutumia lugha kwa ufasaha.
  4. Mada imekuzwa na kuendelezwa kikamilifu.
  5. Insha ya urefu wa robo tatu ikadiriwe katika kiwango hiki.

NGAZI MBALIMBALI ZA KIWANGO CHA B
B- (B YA CHINI) MAKI 11-12

  1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri kwa kueleza hoja tofautitofauti akizingatia mada.
  2. Mtahiniwa ana mtiririko mzuri wa mawazo.
  3. Mtahiniwa anatumia mifano michache ya msamiati unaovutia
  4. Makosa yanadhihirika / kiasi

B WASTANI MAKI 13

  1. Mtahiniwa anadhihirisha hali ya kuimudu lugha.
  2. Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika akizingatia mada.
  3. Mtahiniwa anateua na kutumia mifano michache ya msamiati mwafaka.
  4. Sarufi yake ni nzuri.
  5. Makosa ni machache / kuna makosa machache.

B+ (B YA JUU) MAKI 14 – 15

  1. Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika waziwazi.
  2. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe kwa njia inayovutia na kwa urahisi akizingatia mada.
  3. Mtahiniwa ana mchanganyiko mzuri wa msamiati unaovutia.
  4. Sarufi yake ni nzuri.
  5. Uakifishaji wa sentensi zake ni mzuri.
  6. Makosa ni machache ya hapa na pale.

KIWANGO CHA A KWA JUMLA MAKI 16-20

  1. Mtahiniwa ana ubunifu wa mawazo yanayodhihirika na kutiririka akizingatia mada.
  2. Mtahiniwa anadhihirisha ujuzi wa lugha yenye mnato.
  3. Ana uwezo wa kutumia tamathali za usemi ili kutoa hisia zake kwa njia bora na kwa urahisi.
  4. Umbuji wake unadhihirisha ukomavu na ukakamavu wake kimawazo.
  5. Insha ina urefu kamili.

NGAZI MBALIMBALI ZA KIWANGO CHA A
A- (A YA CHINI) 16 – 17

  1. Mtahiniwa anadhihirisha ukomavu wa lugha.
  2. Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika na anaishughulikia mada.
  3. Ana mtiririko mzuri wa mawazo.
  4. Msamiati wake ni mzuri na unaovutia.
  5. Sarufi yake ni nzuri.
  6. Anatumia miundo tofautitofauti ya sentensi kiufundi.
  7. Makosa ni machache yasiyokusudiwa.

A WASTANI MAKI 18

  1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri kulingana na mada.
  2. Anajieleza kikamilifu akitumia lugha ya mnato.
  3. Anatoa hoja zilizokomaa.
  4. Anatumia msamiati wa hali ya juu na unaovutia zaidi.
  5. Anatumia miundo tofautitofauti ya sentensi kiufundi.
  6. Makosa ni nadra kupatikana.

A+ (A YA JUU) MAKI 19-20

  1. Mawazo yanadhihirika zaidi na mada imeshughulikiwa vilivyo.
  2. Anajieleza kikamilifu akitumia lugha ya mnato.
  3. Hoja zake zimekomaa na zinashawishi.
  4. Msamiati wake ni wa hali ya juu na unaovutia zaidi.
  5. Sarufi yake ni nzuri zaidi.
  6. Anatumia miundo tofautitofauti ya sentensi kiufundi.
  7. Makosa yote kwa jumla hayazidi matano.

VIWANGO MBALIMBALI KWA MUHTASARI
 

KIWANGO NGAZI MAKI
A+
A
A-  
19 – 20
18
16 – 17 
B B+
B
B- 
14 – 15
13
11 - 12 
C+
C
C- 
09 – 10
08
06 – 07 
D+
D
D- 
04 – 05
03
01 – 02 

USAHIHISHAJI NA UTUZAJI KWA JUMLA
Mtahini ni sharti aisome insha yote akizingatia vipengee muhimu. Vipengee hivi ni maudhui, msamiati, mtindo, sarufi na hijai.
MAUDHUI

  1. Maudhui ni hoja au mambo yanayozungumziwa, kuelezewa au kuhadithiwa kwa mujibu wa mada iliyoteuliwa.
  2. Maudhui ndio hasa uti wa mgongo wa insha yoyote ile.
  3. Ubunifu wa mtahiniwa hukisiwa kwa kutathmini uzito wa maudhui yake kulingana na mada teule.

MSAMIATI
Msamiati ni jumla ya maneno yatumiwayo katika lugha husika. Mtahiniwa anatarajiwa kutumia msamiati unaooana na mada teule. Kutegemea ukwasi wa lugha alionao, mtahiniwa anatarajiwa kuikuza mada kwa kuifinyanga lugha kiufundi. Ni muhimu kuelewa
kwamba kutokana na maendeleo na ukuaji wa teknolojia na mawasiliano, maneno mapya yanaibuka kila uchao.

MTINDO
Mtindo unahusu mambo yafuatayo:

  • Mpangilio wa kazi kiaya
  • Mtiririko na mshikamano wa mawazo kiaya na katika insha nzima.
  • Hati nzuri na inayosomeka kwa urahisi.
  • Matumizi ya tamathali za usemi, kwa mfano, methali, misemo, jazanda na kadhalika.
  • Kuandika herufi vizuri kwa mfano Jj, Pp, Uu, Ww na kadhalika
  • Sura ya insha
  • Unadhifu wa kazi ya mtahiniwa.

SARUFI
Sarufi ndio msingi wa lugha. Ufanisi wa mawasiliano hutegemea uwezo wa mtahiniwa wa kutunga sentensi sahihi zenye uwiano wa kisarufi. Mtahini ataonyesha makosa yote ya sarufi yaliyo katika insha anayosahihisha. Makosa ya sarufi huweza kutokea katika:

  1. Matumizi ya alama za uakifishaji.
  2. Kutumia herufi kubwa au ndogo mahali pasipofaa.
  3. Matumizi yasiyofaa ya ngeli na viambishi, viunganishi, nyakati, hali, vihusiano na kadhalika.
  4. Mpangilio wa maneno katika sentensi.
  5. Mnyambuliko wa vitenzi na majina.
  6. Kuacha neno linalohitajika au kuongeza neno lisilohitajika katika sentensi.
  7. Matumizi ya herufi kubwa :
  1. Mwanzo wa sentensi
  2. Majina ya pekee
    1. Majina ya mahali, miji, nchi, mataifa na kadhalika.
    2. Siku za juma, miezi n.k.
    3. Mashirika masomo, vitabu n.k.
    4. Makabila, lugha n.k.
    5. Jina la Mungu.
    6. Majina ya kutambulisha hasa wanyama wa kufugwa, kwa mfano yale ya mbwa – Foksi, Jak. Popi, Simba,Tomi na mengineyo.
    7. Majina halisi ya watu k.m Maria, Rutto

MAKOSA YA HIJAI / TAHAJIA
Haya ni makosa ya maendelezo. Mtahini anashauriwa asahihishe huku akiyaonyesha yanapotokea kwa mara ya kwanza tu. Makosa ya tahajia huweza kutokea katika:

  1. Kutenganisha neno kwa mfano ‘aliye kuwa’.
  2. Kuunganisha maneno kwa mfano ‘kwasababu’
  3. Kukata silabi visivyo afikapo pambizoni kama vile, ‘ngan-o’
  4. Kuandika herufi isiyofaa kwa mfano ‘ongesa’ badala ya ‘ongeza’.
  5. Kuacha herufi katika neno kwa mfano ‘aliekuja’ badala ya ‘aliyekuja’.
  6. Kuongeza herufi isiyohitajika kama vile ‘piya’ badala ya ‘pia’.
  7. Kuacha alama inayotarajiwa katika herufi kama vile J, I
  8. Kukosa kuandika kistari cha kuendelezea neno afikiapo pambizoni au kukiandika mahali pasipofaa.
  9. Kuacha ritifaa au kuiandika mahali pasipofaa, kwa mfano ngombe, ngom’be, ng’ombe, ngo’mbe n.k.
  10. Kuandika maneno kwa kifupi kama vile k.v., k.m., v.v., n.k. na kadhalika
  11. Kuandika tarakimu kwa mfano 27-08-2013

ALAMA ZA KUSAHIHISHIA
=Hupigwa chini ya sehemu ambapo kosa la sarufi limetokea kwa mara ya kwanza tu.
—Hupigwa chini ya sehemu au neno ambapo kosa la hijai limetokea kwa mara ya kwanza tu.
√ Hutumiwa kuonyesha hoja inapokamilika pambizoni kushoto.
٨ Hutumiwa kuonyesha kuachwa kwa neno / maneno.
√ Hutumiwa kuonyesha msamiati bora. Alama hii hutiwa juu ya neno lenyewe.
X Hutumiwa kuonyesha msamiati usiofaa. Alama hii hutiwa juu ya neno lenyewe.
Maelezo mafupi yanahitajika kuhusu tuzo lililotolewa . Kila ukurasa uwe na alama ya √ chini katikati ili kuthibitisha kuwa mtahini ameupitia ukurasa huo.

UKADIRIAJI WA UREFU WA INSHA
Maneno 9 katika kila msitari ukurasa mmoja na nusu.
Maneno 8 katika kila msitari ukurasa mmoja na robo tatu.
Maneno 7 katika kila msitari kurasa mbili.
Maneno 6 katika kila msitari kurasa mbili na robo.
Maneno 5 katika kila msitari kurasa mbili na robo tatu.
Maneno 4 katika kila msitari kurasa tatu na robo tatu
Maneno 3 katika kila msitari kurasa nne na nusu.
Kufikia maneno 174 Insha robo.
Maneno 175 – 274 Insha nusu.
Maneno 275 – 374 Insha robo tatu.
Maneno 375 na kuendelea Insha kamili 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Bondo Mocks 2021 Exams.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest