Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Nyeri Mocks 2021 Exams

Share via Whatsapp
Download PDF for future reference Join our whatsapp group for latest updates

MAAGIZO:

 1. Andika jina lako na nambari yako katika nafai ulizoachiwa hapo juu
 2. Andika tarehe ya mtihani na utie sahihi yako katika nafasi ulizoachiwa hapo juu
 3. Jibu maswali yote katika nafasi zilizoachwa0
 4. Karatasi hii ina sehemu nne.
 5. Sehemu ya kwanza ni ya ufahamu - alama 15
 6. Sehemu ya pili ni ufupisho - alama 15
 7. Sehemu ya tatu ni sarufi - alama 40
 8. Sehamu ya nne ni isimu jamii - alama 10
 9. Watahiniwa wahakikishe kuwa sehemu zote zipo na alama zote zipo

KWA MATUMIZI YA MTAHINI PEKEE

Sehemu

Upeo

Alama

A.     Ufahamu

15

 

B.     Ufupisho

15

 

C.     Matumizi ya lugha

40

 

D.    Isimu jamii

10

 

Jumla

80

 

MASWALI

 1. UFAHAMU
  Soma makala yafuatayo kasha ujibu maswali
  Hakuna ndakika inayopita bila kisa cha kuchelewa. Mikutano karibu yote huchelewa kuanza kwa sababu wahusika hawafiki wakati ufaao. Ibada nazo hucheleweshwa kwa uzembe wa waumini. Na mazishi je?Taratibu hucheleweshwa vilevile.Ingawa hapa yaweza kufikiriwa kuwa pengine wampendao marehemu hawataki kuharakisha safari yake ya kwenda kuzimuni. Lakini hata arusi ambazo huwa na misururu ya mikutano ya maandalizi, siku itimiapo shughuli huchelewa. Si ajabu sherehe kuendela mpaka usiku ambapo ratiba ilionyesha zingekomea masaa ya alasiri.
  Uchunguzi unabainisha kuwa watu huchelewa kwa sababu mbalimbali. Sababu mojawaponi kutowajibika; yaani, watu wengi hawaoni umuhimu wa kuzingatia muda. Huu ni upuuzi mtupu. Wazee wetu walizingatia muda ipasavyo tangu jadi ingawa hawakuwa na saa wala kalenda. Hii ndiyo sababu walipanda mimea walipohitajika, wakavuna na hatimaye wakapika na kuandaa ipasavyo. Wahenga hawa walituachia methali nyingi kama funzo, kwa mfano; ‘Chelewachelewa utakuta mwana si wako’, na hata wakasindikiza kuwa, ‘Ngoja ngoja huumiza matumbo’.
  Watu wengine huchelewa kwa sababu ya kutojiandaa kwa yale yatakoyojiri. Watu wasiopanga shughuli zao na badala yake kuzifanya kwa kushtukia aghalabu hushindwa kuhudhuria hata mahojiano ya kuajiriwa kazi kwa wakati ufaao. Hawa huwa neema kwa washindani wao, Kujitayarisha si jambo gumu. Anachopasa kujua mhusikani saa ya miadi hali ya usafiri.
  Hivi viwili vitamwezesha kujua muda wa safari na hivyo kukadiria wakati wa kuondoka. Ni wangapi wameiona milolongo ya watu nje ya mlango ya benki wakiwasihi mabawabu na
  pengine kuwahonga wawaruhusu kuingia? Hawa huwa si wageni.Ni wateja wanaojua ratiba ya kazi lakini hushindwa kupanga mwenendo wao barabara.
  Mikutano, sherehe na shughuli nyingi huchelewa kuanza kwa masaa mengi kwa sababu eti mgeni mashuhuri amechelewa kufika. Muda wa kungoja huwa mrefu zaidi kutegemea ukubwa wa cheo cha mhusika. Watu hawa huchelewa makusudi kwa sababu pengine ya kiburi. Majivuno haya huwafanya wafurahi wanaposubiriwa na watu wadogo. Wakubwa hawa wanapofika badala ya kuomba msamaha, hujigamba kuhusu majukumu yao mengi na makubwa.
  Aidha kuna watu ambao hupenda kutekeleza mambo mengi, kwa wakati mmoja. Tujuavyo ni kuwa mambo mawili yalimshinda fisi. Pia watu wanaposhika mengi, mahudhurio yao katika baadhi ya mambo hutatizwa na hivyo huchelewa. Isitoshe, kuna watu wa aina hii hata wanapopewa ratiba ya mapema, hujikokota na hivyo kupitwa na wakati.
  Ingawa sababu tulizozitaja hutokana na watu wenyewe, kuna zile zinazosababishwa na dharura nyingine. Hizi ni pamoja na misongamano ya magari, kuchelewa kwa vyombo vya usafiri na hata kuharibika kwa vyombo. Hii ndiyo sababu inashauriwa kuwa mtu anapoamua kutekeleza jambo, atenge muda takribani wa dakika 30 kwa ajili ya dharura Fulani. Kwa hivyo hata anapopata tuseme pancha njiani bado atafika kwa wakati ufaao.
  Kuchelewa hauudhi tu watu wanaocheleweshwa bali huwa na matokeo mengine mengi. Mara nyingi watu waliochelewa huharakisha mambo ili kufidia muda walioupoteza. Kama wanaendesha gari, kwa mfanom basi huzidisha kai matokeo huweza kuwa ajali ambayo mara nyingine huleta ulemavu au vifo.
  Ratiba ya mambo ichelewapo watu waliofika mapema hupoteza muda kusubiri. Muda huu wangeutumia kwa harakati muhimu. Mfano wa uchumi wa kisasi unahitaji mamilioni ya watu kukurubiana, kutagusana na kuendesha shughuli zao kwa ujima. Aidha, watu hawana budi kubadilishana bidhaa na huduma. Mambo haya yanapocheleweshwa basi gharama huwa kubwa. Tatizo hili hubainika sana katika ofisi za umma.
  Ni kawaida watu kufika kazini dakika nyingi baada ya wakati wa kufungua milango ya kazini. Ajabu ni kuwa wafanyakazi wawa huwa wa kwanza kufunga kazi kabla ya kipindi rasmi. Inakisiwa Kenya hupoteza shilingi bilioni 80 kila mwaka kupitia uzembe wa kutozingatia wakati.
  Jambo la kwanza ni kuweka sera ya kitaifa inayolenga kuwaelimisha wananchi umuhimu wakuzingatia saa. Halikadhalika kanuni iwekwe ya kuwafungia nje watu wanaochelewa kuhudhuria shuguli za mikutano au hafla. Wananchi nao wazinduliwe kuwa ni haki yao kufumkana muda washughuli unapowadia kabla mgeni wa heshima kufika. Nchi ya Ekwado (Ecuador) imefanikiwa kutekeleza haya. Kenya pia haina budi kuandamana mwelekeo huo. Hii ndiyo njia mojawapo ya kufufua uchumi na kuhakikisha taifa linapiga hatua kimaendeleo.
  Maswali
  1. Kipe kifungu hiki anwani mwafaka. (alama 1)
  2. Taja watu watatu walio na mazoea ya kuchelewa katika shughuli walizoalikwa. (alama 3)
  3. Taja sababu zinazofanya watu kushindwa kutimiza miadi. (alama 4)
  4. Taja na ueleze njia nne zinazoweza kuondoa tatizo la kuchelewa. (alama 4)
  5. Eleza maana ya maneno haya kama yaliyotumiwa katika taarifa. (alama 3)
   1. ujima
   2. Miadi
   3. Pancha
 2. UFUPISHO (ALAMA 15)
  Soma makala yafuatayo kasha ujibu maswali yote
  Takriban kila siku vyombo vya habari hueleza kuhusu mateso ya watoto, cha kusikitisha zaidi ni kwamba mbali na visa vinavyoripotiwa, kuna vingine chungu nzima ambavyo havijaripotiwa . Mateso kwa watoto hawa ni ya aina mbalimbali. Mwezi wa Julai, 2005 wavamizi walipowaua watu zaidi ya sabini Kaskazini mwa Kenya walianza kwa kuwauwa watoto katika shule ya msingi ya Mabweni. Waliwauwa watoto ishirinina wawili huku mamia wakijeruhiwa.
  Kuna wazazi ambao huwapiga watoto wao mithili ya kumpiga nyoka. Utaona watoto wakiwa na majeraha yanayofanya malaika kusimama wilini. Visa vingi vimeripotiwa ambapo wazaziau walevi huwakata au kuwadhuru watoto sehemu Fulani za mwili kama vile masikio, miguu na mikono. Vilevile kumetokea visa vya kuwachoma watoto na wengine kuwachwa bila chakula.
  Kenya ni mojawapo ya nchi zilizotia sahihi mkataba wa kulinda haki za watoto. Serikali yetu ina idara katika ofisi ya makamu wa rais inayoshughulikia maslahi ya watoto.Mwezi wa Julai 2005, Serikali ilianzisha kampeni kabambe za kukomesha mateso dhidi ya watoto. Ajabu ni kwamba watu wengi na hata watoto, wenyewe hawajui haki zao. Sheria ya watoto ilipitishwa ili kutetea haki za watoto katika nchi ya Kenya.
  Baadhi ya haki za watoto ni kama vile kulindwa kutokana na ubaguzi wowote, kutunzwa na wazazi na kupewa elimu. Watoto wana haki ya elimu ya kiakademia na dini. Vilevile wana haki ya kulindwa kiafya. Watoto hawatakikani kunyanyaswa kiuchumi au kwa njia nyinginezo kama vile kusajiliwa kupigana katika vita. Kila mtoto akiwemo mlemavu, ana haki ya kuheshimiwa katika jamii.
  Hata hivyo sharti pia watoto wawajibike ipasavyo kwa wazazi, walezo na jamii kwa jumla. Mtoto anapaswa kuheshimu wakuu wake na kuwasaidia panapo haja. Watoto wana jukumu la kudumisha na kuimarisha umoja wa jamii na raia kuendeleza maadili mema katika jamii.
  Maswali
  1. Fupisha aya ya kwanza nay a pili kwa maneno 60-80 (ala 6, mtiririko 1)
   Matayarisho
   _____________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________
   Jibu
   _________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________
  2. Bainisha mambo muhimu aliyoyajadili mwandishi katika aya tatu za mwisho.
   (maneno 100 – 120) (ala 20, mtiririko 1)
   Matayarisho
   __________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________
   Jibu
   _______________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)

 1. Andika sifa zozote mbili za sauti zifuatazo (alama 2)
  1.  /u/
  2. /ch/
 2. Bainisha mofimu za neno ‘kilichonywewa’ (alama 3)
 3. Onyesha maumbo mawili ya silabi funge kwa kutolea mifano katika maneno. (alama 2)
 4. Andika upya sentensi kwa kutumia ‘o’ rejeshi tamati. (alama 2)
  Gari lililoanguka si lile unalolizungumzia.
 5. Badilisha katika usemi halisi (alama 3)
  Afisa wa usalama alisema kuwa wangemsaidia ikiwa angeshirikiana nao.
 6. Pambanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha vishale. (alama 4)
  Letu lililopaliliwa limetuleta mazao mengi.
 7. Andika sentensi ifuatayo upya ukibadilisha neno lilopigiwa mstari kuwa kivumishi. (alama 2)
  Msichana amepigwa vibaya
 8. Ainisha yambwa na chagizo katika sentensi ifuatayo. (alama 4)
  Wanafunzi walimwatikia mwalimu mkuu miche ya matunda kwa ustadi wakitumia vijiti.
 9. Andika visawe viwili vya neno ‘vurumai’ (alama 2)
 10. Ainisha virai vyovyote vitatu. (alama 3)
  Mwanafunzi yule mtoto hupenda kutembea katikati ya barabara kila wakati.
 11. Andika sentensi hii katika udogo wingi. (alama 2)
  Mtoto amefunga mlango wa nyumba yao.
 12. Onyesha matumizi mawili ya alama ya vifungo katika sentensi. (alama 2)
 13. Eleza maana ya kishazi (alama 1)
 14. Nyambua vitenzi vifuatavo kama ulivyoelekezwa. (alama 2)
  1. Suka (kauli ya kutendata)
  2. pa (kauli ya kutendeka)
 15. Tofautisha maana ya sentensi zifuatazo (alama 2)
  1. Alipokelewa mgeni
  2. Alipokezwa mgeni
 16. Yakinisha (alama 2)
  Usiponiita sitaandamana nawe.
 17. Tunga sentensi moja kutofautisha vitate vifatavyo. (alama 2)
  1. Chaka
  2. Shaka 

ISIMU JAMII

 1. Taja sababu sita zinazosababisha watu kubadili na kuchanganya ndimi. (alama 5)
 2. Hakiki sifa zozote tano za sajili ya kituo cha polisi. (alama 5)

MWONGOZO WA LUGHA

SEHEMU A. UFAHAMU (alama 15)

 1. Kipe kifungu hiki anwani mwafaka. (alama 1)
  Kutuza muda/wakati/kuchelewa
 2. Taja watu watatu walio na mazoea ya kuchelewa katika shughuli walizoalikwa. (alama 3)
  1. Waumini katika ibada
  2. Waombolezaji kwa mazishi
  3. Wanaohudhuria harusi na maharusi
  4. Wateja wa benki
  5. Wanaohojiwa kwa kutafuta kazi
  6. Wageni mashuhuri katika mikutano
 3. Taja sababu zinazofanya watu kushindwa kutimiza miadi. (alama 4)
  1. Uzembe
  2. Kutowajibika/mapuuza/kisigizio
  3. Kutojiandaa kwa ipasavyo/kutopanga
  4. Kutekeleza mambo mengi kwa pamoja
  5. Kuharibika kwa vyombo vya usafiri
  6. Kiburi
 4. Taja na ueleze njia nne zinazoweza kuondoa tatizo la kuchelewa. (alama 4)
  1. kujitayarisha /kujiandaa mapema/mf. Kupanga mwenendo wa barabara
  2. kuwajibika katika kuzingatia wakati/ratiba
  3. Kuweka sera za kuwelimisha watu kuhusu umuhimu wa kuzingatia saa
  4. Kuweka kanuni za kuwafungia nje wanaochelewa
  5. Wananchi wazinduliwe kuwa wana haki ya kufumukana muda wa shughuli unapokwisha.
 5. Eleza maana ya maneno haya kama yaliyotumiwa katika taarifa. (alama 3)
  1. ujima - ushirikiano
  2. Miadi - ahadi ya kukutana kwa sababu maalum
  3. Pancha - mpasuko kwa gurudumu

SEHEMU YA B: UFUPISHO

 1. Kila siku vyombo vya habari hueleza kuhusu mateso ya watoto
  • Kuna vingine ambavyo havijaripotiwa
  • Watoto huuawa na wavamizi vitani
  • Kuna wazazi wanaowapiga watoto kinyama
  • Kuwachoma
  • Kuachwa bila chakula
 2. Kenya ni mojawapo ya nchi zilizotia sahihi mkataba wa kulinda haki za watoto
  • Ina idara katika ofisi ya makamu wa rais inayoshughulikia maslahi ya watoto
  • Serikali ilianzisha kampeni kabambe za kukomesha mateso dhidi ya watoto
  • Watu wengi na hata watoto wenyewe hawajui haki zao
  • Sheria ya watoto ilipitishwa ili kutetea haki za watoto katika nchi ya Kenya
  • Watoto wanafaa kulindwa kutokana na ubaguzi/kutunzwa na wazazi na kupewa elimu ya kiukademia na dini /kulindwa kiafaya/kuheshimiwa katika jamii.
  • Watoto wenyewe wanapaswa kuwasaidia wazazi wao inapostahili.
  • Watoto wenyewe wnapaswa kuwasaidia wazazi wao inapostahili.
  • Watoto wanafaa kuadumisha umoja wa jamii na kuendeleza maadili katika jamii.
   (alama 8 + 1 ya mtiririko)
   Adhabu
  • Adhibu kosa la sarufi litokeapo kwa mara ya kwanza hadi 6 x ½ = 3
  • Adhibu kosa la hijai litokeapo kwa mara ya kwanza hadi 6 x ½ = 3

MAJIBU

 1. /u/ Sauti huwa nyuma
  Ulimi huwa juu 2 x ½ = 1
  Midomo huviringwa
  /ch/ ni kipasua kawamizo
  Ni ya kaka ngumu 2 x ½ = 1
  Ni hafifu/sighuna
 2. Ki – li -oho - nyw ew - a 6 x ½ = 3
  Ngeli wakati kirejeshi mzizi kauli kiishio
 3.                        
  1. K - m – la – ngo, m – tu, la – b – da
  2. IK – Al - ha - mi - si, Al – fa - ji - ri
  3. KIK - Mak – ta – ba, nak – ta – ri 2 x ½ = 1
 4. Gari liangukalo si lile ulizungumzialo 2 x 1 = 2
 5. Tutakusaidia ikiwa utashirikiana nasi afisa wa usalama akasema. 6 x ½ = 3
 6. S → KN + KT
  KN → W + S
  W → Letu
  S → lililopaliliwa
  KT → T + N + V
  T → limetuletea
  N → mazao
  V → mengi
  8 x ½ = 4
 7. Msichana mbaya amepigwa
  1 x 2 = 2
 8. Kipozi/yambwa tendwa - miche ya matunda
  Kitanda/yambwa tendewa - mwalimu mkuu
  Yambwa ala - vijiti
  Chagizo - kwa ustadi. 2 x1 = 2
 9. Ghasia, fujo, zogo, vurugu, kizaazaa, rangaito, kivangaito, tandabeluwa. 2 x 1 = 2
 10. Yule mtoro - kirai kivumishi
  Katikati ya barabara - kirai kihusish
  Kila wakati - kirai kielezi
  Mwanafunzi yule mtoro - kirai nomino.
  3 x 1 = 3
 11. Kitoto kimefunga vilango vya vijumba vyao. 1 x 2 = 2
 12.                    
  1. kufunga maelezo ya ziada/pembeni
  2. kufungia herufi na nambari
  3. Katika tamthilia kufungia maelekezo
  4. Kufungia neno ambalo ni kisawe
  5. kufungia neno ambalo ni kisawe
  6. kufungia maelezo ambayo ni ufagfanuzi wa jambo lililotajwa. 2 x 1 = 2
 13. Fungu la maneno lenye muundo wa kilima na kiarifa ambalo limo ndani ya sentensi.1 x 1 = 1
 14.                        
  1. sokota
  2. peka (2 x 1 ) = 2
 15.                  
  1. Mgeni alipokelewa kwa niaba yake.
  2. Aliletewa mgeni ampokee.
   2 x 1 = 2
 16. Ukiniita nitaandamana nawe. 1 x 2 = 2
 17. Chaka - mwitu/eneo lenye miti mingi
  Shaka - wasiwasi
  Sentensi moja na maana zidhihirike

SIMU JAMII

 1.                    
  1. Kuwa na umilisi wa lugha mbili au zaidi.
  2. Kukosa msamiati mwafaka wa kutumia katika lugha anayotumia wakati huo.
  3. Ili kujitambulisha na kundi moja la watu
  4. Ili kuficha maana kutoka kwa kundi la watu.
  5. kuonyesha ubingwa na umahiri wa lugha mbalimbali
  6. Kuonyesha hisia Fulani
  7. Kutaka kueleweka zaidi
  8. Kutoka kushirikisha watu katika mazungumzo.
  9. kutokana na maoea ya mtu
   Sifa za sajili katika kituo cha polisi
 2.                    
  1. Matumizi ya msamiati maalum vile ndani, afande, pingu n.k
  2. Matumizi ya misimu kama vile ndani kwa maana ya seli.
  3. Matumizi ya sentensi fupi ili kurahishisha mawasiliano.
  4. Lugha ya kuhaji/kudadisi
  5. Polisi hutumia lugha ya kuamuru. Kwa mfano, fanya upesi.
  6. Mshukiwa / mfungwa hutumia lugha ya unyenyekevu / heshima / upole
  7. Kushanganya ndimi /msimbo kama vile utafanyiwa booking vipi?
  8. Matumizi ya toni kali kwa washukiwa / wafungwa.
   Zozote 5 x 1 = 5

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Nyeri Mocks 2021 Exams.


Tap Here to Download for 50/-


Read 3176 times Last modified on Tuesday, 17 May 2022 13:21

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.

Print PDF for future reference