Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Kigumo Mocks 2021 Exams

Share via Whatsapp

Maagizo.

  1. Andika jina lako na nambari yakoya mtihani katika nafasi Zilizoachwa hapo juu
  2. Tia sahihi yako kisha uandike tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
  3. Andika insha mbili: insha ya kwanza ni ya lazima
  4. Kisha chagua Insha ngingine moja kutoka kwa zile zilizobaki
  5. Insha yako isipungue maneno 400
  6. Kila insha ina alama 20.
  7. Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya kiswahili


MASWALI

  1. Lazima
    Andika barua kwa mhariri wa gazeti la mzalendo ukieleza athari za mabadiliko ya tabianchi na upendekeze namna ya kukabiliana na hali hii
  2. Andika kuhusu umuhimu wa vijana katika kuimarisha mshikamano wa kitaifa.
  3. Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali ifuatayo.
    Bahati ni chudi
  4. Tunga kisa kitakachokamilika kwa kauli ifuatayo:
    “…niliipapia ile bilauri ya maji kwa pupa. Sikuwa na uhakika kuwa kiu yangu ingekatika. Nikapiga mafunda mawili, matatu. Baada ya kugumia bilauri yote, ndipo nilipotambua kuwa kweli maji ni uhai.”


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA 

  1. Swali la kwanza
    Hii ni insha ya barua kwa mhariri
    1. Barua iandikwe kwa muundo wa barua rasmi.
      • Anwani ya mwandishi juu mkono wa kulia
      • Tarehe chini ya anwani ya mwandishi
      • Anwani ya mhariri upande wa kushoto
      • Mtajo
      • Mada
      • Maudhui
      • Jina la mwandishi
      • Sahihi
    2. Mwili (hoja)
      • athari
        1. Kukauka kwa mito
        2. Uhaba wa mvua
        3. Njaa / kiangazi
        4. Kutotabirika kwa misimu
        5. Magonjwa
        6. Mioto katika misitu
      • Mapendekezo
        1. Kutokata miti
        2. Upandaji wa miti
        3. Uhifadhi wa chemichemi za maji
        4. Kilimohifadhi
        5. Kudhibiti uchafu na gesi kutoka viwandani (Alama 20)
  2. Swali la pili
    Hii ni insha ambayo inamhitaji mtahiniwa kufafanua au kujadili mawazo yake au mtazamo wake kuhusu nafasi ya vijana katika utangamano wa kijamii.
    • Baadhi ya hoja ni kama zifuatazo:
      1. Vijana ndio wengi hivyo wanaweza kuwafikia raia wengi.
      2. Vijana wanathaminiana na kuaminiana, kwa hivyo ni rahisi kuwashawishi wenzao kutangamana.
      3. Ikiwa vijana wanafunzwa maarifa au mbinu za kukabiliana na matatizo au changamoto, wataweza kuziwasilisha mbinu hizi kwa wenzao.
      4. Ni muhimu vijana kuepuka kutumiwa na viongozi kama vyombo za kuvulia na kupalilia uhasama miongoni mwa raia.
      5. Kwa kuwa kundi la vijana ndilo lenye nishati Zaidi, linaweza kutumia nishati hii katika shughuli zinazoleta utangamano kama vile michezo.
      6. Vijana wanaweza kujisajili katika vyuo vilivyo katika maeneo mbalimbali nchini ili kutagusana na raia wa makabila tofauti tofauti.
      7. Vijana wanastahili au wanaweza kutumia lugha yao kwa mfano ‘Sheng’, kama kiungo cha kuwaunganisha na kueneza hisia za kizalendo.
      8. Vijana wanaosajiliwa katika vikosi vya kulinda usalama wanaweza kueneza siasa au sera ya kudumisha usalama kwa njia ya Amani badala ya vita.
      9. Viongozi wanaweza kuwahamasisha vijana kutoka makabila mbalimbali ili kupalilia mwtazamo wa kitaifa badala wa ule wa kieneo, kikabila au kinasaba.
      10. Kushiriki katika shughuli za kiusomi kama vile makongamano kunawawezesha vijana kuja pamoja kwa kujihisi kama raia wenye maazimio sawa, hivyo kuhimizana mshikamano.
      11. Mradi wa kazi wa vijana kwa mfano, uliwaleta vijana wa usuli tofauti pamoja.
    • Tanbihi.
      1. Mtahiniwa anaweza kuchukua mwelekeo wa kuonyesha mambo ambayo vijana wanaweza kufanya ili kuleta mshikamano wa kitaifa.
      2. Mtahiniwa pia anaweza kuonyesha au kujadili hatua ambazo vijana wamechukua kuleta mshikamano wa kitaifa.
      3. Mtahiniwa pia anaweza kuchanganya mielekeo yote miwili akataja hoja na kuitolea ufafanuzi kwa kuonyesha hatua ambazo vijana tayari wamechukua kuhusiana na suala hili.
        (Alama 20)
  3. Swali la tatu.
    1. Bahati ni chudi
      1. Chudi ni bidii
      2. Maana ya methali hii ni kuwa ili kufanikiwa katika jambo fulani ni sharti mtu afanyie jambo hilo bidii kubwa.
      3. Methali hii hutumiwa kuwahimiza watu wazidishe bidii kazini mwao ili waweze kufanikiwa.
      4. Kisa lazima kioane na maana ya methali hii
      5. Pande zote mbili za methali zidhihirike
        (Alama 20)
  4. Swali la nne.
    Insha ya mdokezo wa kumalizia.
    1. Lazima mtahiniwa amalizie kwa maneno aliyopewa.
    2. Asiongezee maneno yoyote baada ya mdokezo.
    3. Anakili kimalizio kizima jinsi kilivyo.
    4. Mawazo katika kisa cha mtahiniwa lazima yalingane na mdokezo.
    5. Azingatie nafsi na wakati (Alama 20)

VIWANGO MBALIMBALI
KIWANGO CHA D KWA JUMLA MAKI 01-05

  1. Insha haieleweki kwa vyovyote vile ama uwezo wa mtahiniwa wakutumia lugha ni hafifu sana hivi kwamba mtahini lazima afikirie kile mtahiniwa anacho jaribu kuwasilisha.
  2. Mtahiniwa hana uwezo wa kutumia maneno ya Kiswahili kwa njia inayofaa
  3. Lugha imevurugika ,uakifishaji na insha ina makosa ya kila aina.
  4. Kujitungia swali na kulijibu
  5. Insha ya urefu wa robo ikadiriwe hapa

NGAZI MBALIMBALI KIWANGO CHA D
D-(D YA CHINI) MAKI 01-02

  1. Insha haina mpangilio maalum na haieleweki kwa vyovyote vile
  2. Kujitungia swali tofauti na kulijibu
  3. Kuandika kwa lugha isiyo Kiswahili au kuchanganya ndimi.
  4. Kunakili swali au maswali na kuyakariri
  5. Kunakili swali au kichwa tu

D WASTANI MAKI 03

  1. Mtiririko wa mawazo haupo
  2. Mtahiniwa amepotoka kimaudhui.
  3. Matumizi ya lugha ni hafifu mno
  4. Kuna makosa mengi ya kila aina 3

D+ (D YA JUU) MAKI 04-05

  1. Insha ya aina hii huwa na makosa mengi ya kila aina .Lakini unaweza kutambua kile ambacho mtahiniwa anajaribu kuwasilisha
  2. Hoja hazikukuelezwa kikamilifu / mada haikukuzwa vilivyo.
  3. Mtahiniwa hana uhakika wa matumizi ya lugha.
  4. Mtahiniwa hujirudiarudia
  5. Insha yenye urefu wa robo ikadiriwe hapa.

KIWANGO CHA C KWA JIJMLA: MAKI 06-10

  1. Mtahiniwa anajaribu kuishughulikia mada japo hakuikuza na kuiendeleza vilivyo.
  2. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe kwa njia isiyovutia /hana ubunifu wa kutosha.
  3. Mtahiniwa anaakifisha sentensi vibaya.
  4. Mtiririko wa mawazo unaanzakujitokeza japo kwa njia hafifu.
  5. Insha inamakosa mengi ya sarufi, ya misamiati na ya tahajia (hijai.)
  6. Insha yenye urefu wa nusu ikadiriwe hapa.

NGAZI MBALIMBALI ZA KIWANGO CHA C
C-(C YA CHINI) MAKI 06-07)

  1. Mtahiniwa ana shida ya kuwasilisha na kutiririsha mawazo yake.
  2. Mtahiniwa hana msamiati wa kutosha wala miundo ya sentensi ifaayo.
  3. Mtahiniwa anafanya makosa mengi ya sarufi, ya hijai na ya msamiati na insha yake haieleweki kwa urahisi

C WASTANI MAKI 08

  1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe lakini kwa njia hafifu,
  2. Dhana tofautitofauti hazijitokezi wazi.
  3. Mtahiniwa hana ubunifu wa kutosha.
  4. Mtiririko wa mawazo ni hafifu na hana ufundi wa lugha unaofaa.
  5. Amejaribu kuishughulikia mada aliyopewa
  6. Mtahiniwa ana shida ya uakifishaji.
  7. Mtahiniwa anafanya makosa mengi ya sarufi ya hijai na ya msamiati lakini bado insha inaeleweka. 4

C+(C YA JUU) MAKI 09-10

  1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri akizingatia mada lakini kwa njia isiyo na mvuto.
  2. Dhana tofautitofauti zinajitokeza japo kwa njia hafifu.
  3. Kuna mtiririko wa mawazo japo hana ufundi wa lugha unaofaa.
  4. Misemo na methali zimetumika kwa njia hafifu.
  5. Ana shida ya uakifishaji.
  6. Kuna makosa ya sarufi, ya msamiati na ya hijai yanayoathiri mtiririko wa mawazo.

KIWANGO CHA B KWA JUMLA: MAKI11-15

  1. Katika kiwango hiki, mtahiniwa anaonyesha hali ya kuimudu lugha.
  2. Mtahiniwa anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi vizuri.
  3. Mtahiniwa ana uwezo wa kutumia lugha kwa ufasaha.
  4. Mada imekuzwa na kuendelezwa kikamilifu.
  5. Insha ya urefu wa robo tatu ikadiriwe katika kiwango hiki.

NGAZI MBALIMBALI ZA KIWANGO CHA B
B-(B YA CHINI): MAKI 11-12

  1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri kwa kueleza hoja tofautitofauti akizingatia mada.
  2. Mtahiniwa ana mtiririko mzuri wa mawazo.
  3. Mtahiniwa anatumia mifano michache ya msamiati unaovutia.
  4. Makosa yanadhihirika/kiasi

B WASTANIMAKI 13

  1. Mtahiniwa anadhihirisha haliya kuimudu lugha
  2. Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika akizingatia mada.
  3. Mtahiniwa anateua na kutumia mifano michache ya misamiati mwafaka.
  4. Sarufi yake ni nzuri.
  5. Makosa ni machache/kunamakosa machache

B+ (B YA JUU) MAKI 14-15

  1. Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika na anajieleza waziwazi.
  2. Mtahiniwa anawasiliha ujumbe kwa njia inayovutia na kwa urahisi akizingatia mada.
  3. Mtahiniwa ana mchanganyiko mzuri wa msamiati unaovutia.
  4. Sarufi yake ni nzuri.
  5. Uakifishaji wa sentensi zake ni mzuri. 5
  6. Makosa ni machache ya hapa na pale.

KIWANGO CHA A KWA JUMLA MAKI16-20

  1. Mtahiniwa ana ubunifu wa mawazo yanayodhihirika na kutiririka akizingatia mada.
  2. Mtahiniwa anadhihirisha ujuzi wa lugha yenye mnato.
  3. Ana uwezo wa kutumia tamathali za usemiilikutoa hisia zake kwa njia bora nakwaurahisi.
  4. Umbuji wake unadhihirisha ukomavu na ukakamavu wake kimawazo
  5. Insha inaurefu kamili

NGAZI MBAL1MBALI ZA KIWANGO CHA A
A-(YA CHINT) MAKI 16-17

  1. Mtahiniwa anadhihirisha ukomavu wa lugha.
  2. Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika na anashughulikia mada.
  3. Ana mtiririko mzuri wa mawazo
  4. Msamiati wake ni mzuri na unaovutia.
  5. Sarufi yake ni nzuri.
  6. Anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi kiufundi.
  7. Makosa ni machache yasiyokusudiwa

A WASTANI MAKI 18

  1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri kulingana na mada.
  2. Anajieleza kikamilifu akitumia lugha ya mnato/kunasa.
  3. Anatoa hojazilizokomaa.
  4. Anatumia msamiati wa hali yajuu na unaovutia zaidi.
  5. Anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi kiufundi.
  6. Makosa ni nadra kupatikana

A(AYAJUU)MAKI 19 -20

  1. Mawazo yanadhihirika zaidi na mada imeshughulikiwa vilivyo.
  2. Anajieleza kikamilifu akitumia Iugha ya mnato.
  3. Hoja zake zimekomaa na zinashawishi.
  4. Msamiati wake ni wa hali ya juu na unaovutia zaidi
  5. Sura yake ninzuri zaidi/kabisa
  6. Anatumia miundo tofauti tofauti ya sentesi kiufundi.
  7. Makosa yote kwa jumla hayazidi matano. 6
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Kigumo Mocks 2021 Exams.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest