Kiswahili Paper 3 Questions - Maranda Mocks 2021/2022 Exams

Share via Whatsapp

KISWAHILI (FASIHI)
Karatasi ya 3

Maagizo

  • Jibu maswali manne pekee.
  • Swali la kwanza ni la lazima.
  • Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki Riwaya, Ushairi, hadithi Fupi na Fasihi Simulizi.
  • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.


Maswali

SEHEMU A: TAMTHILIA
Pauline Kea: Kigogo

  1. Lazima
    “Nimekuja kuwakomboa. Si kuwaumbua. Hali hii si hali. Kuna leo na kesho. Na kesho hujengwa na leo.”
    1. Weka dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)
    2. Bainisha mitindo minne ya lugha inayojitokeza katika dondoo. (alama 4)
    3. Eleza michango kumi na miwili ya msemewa katika kudidimiza kauli iliyopigwa mstari kwa kurejelea tamthilia Kigogo. (alama 12)

SEHEMU B: RIWAYA
Assumpta K. Matei: Chozi la Heri
Jibu swali 2 au 3

  1. “Unajua kwamba mimi sikuumbiwa ujalaana, walimwengu ndio walionifinyanga upya, wakanipa moyo wa ujabari.”
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
    2. Changanua mtindo katika dondoo. (alama 4)
    3. Kwa kurejelea wahusika wowote kumi na wawili katika riwaya Chozi la Heri, thibitisha ukweli wa kauli iliyopigwa mstari. (alama 12)
  2.         
    1. Kwa kutolea mifano katika riwaya Chozi la Heri, jadili jinsi mwandishi alivyotumia migogoro ya kisiasa kufanikisha ploti. (alama 10)
    2. Kwa kurejelea barua ya kumstaafisha Lunga, jadili jinsi mwandishi alivyofanikisha maudhui katika riwaya. (alama 10)

SEHEMU C: USHAIRI
Jibu swali 4 au 5

  1. Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata

    Jogoo anapowika, ana jambo atangaza
    Atangaza kuamka, limeshatanduka giza,
    Giza limeshaondoka, uache kujidumaza,
    Mwanamke amka!

    Jogoo anapowika, mwanamke amjuza
    Amjuza kuamka, amulikwe na mwangaza,
    Mwangaza umeshafika, aache kujilegeza,
    Mwanamke amka!

    Jogoo anapowika, mwanamke ahimiza,
    Ahimiza kutimka, mbio ili kujikuza,
    Kujikuza si dhihaka, elimu kuitukuza,
    Mwanamke amka!

    Jogoo anapowika, mwanamke amkuza,
    Amkuza kuzizika, tamaduni za kuviza,
    Kuziviza kwa haraka, mila zinazopumbaza,
    Mwanamke amka!

    Jogoo anapowika, mwanamke atukuza,,
    Atukuza amefika, kupokea yake tuza,
    Tuza ya kurevuka, muamko kutangaza,
    Mwanamke amka!

    Jogoo anapowika, mwanamke akataza,
    Akataza kutotaka, minyanyaso ya kuliza,
    Kuliza na kuudhika, hakiye kugandamiza,
    Mwanamke amka!

    Jogoo anapowika, mwanamke amwongoza,
    Amwongoza umefika, muda wa kuongoza,
    Kuongoza kwa hakika, umma pasi kujitweza,
    Mwanamke amka!

    Jogoo anapowika, mwanamke azoweza,
    Azoweza kurauka, kwa bidii kujikaza,
    Kujikaza na kutoka, jikoni kulomviza,
    Mwanamke amka!

    1. “Mtunzi wa shairi hili ananuia kumzindua nafsinenewa.” Jadili. (alama 7)
    2.  Ainisha bahari sita za shairi hili. (alama 6)
    3. Onyesha mbinu tatu alizozitumia mshairi kukidhi mahitaji ya kiarudhi katika shairi hili. (alama 3)
    4. Andika ubeti wa mwisho kwa lugha tutumbi. (alama 4)

  2. Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata
    Kiza nene kimetanda
    Ukungu na umande
    Zinashindana
    Umweso unamulika
    Radi nayo inapiga
    Kimya!

    Bundi na milio yao
    Ama kweli, kimila si mazuri mambo.
    Mebainika usiku, usiku mkuu, wa kiza nene.
    Kiza! Kiza! Kiza!
    Balaa! Balaa! Balaa!
    Beluwa! Beluwa! Beluwa!
    Sinyaa! Sinyaa! Sinyaa!

    Kabla,
    Inajipenyeza kwa umbali
    Kwa umbali hakika
    Inuka! Zungumza! Wamefika!
    Hakika, sina cha kuwaeleza!
    Hakika, zaidi ya kuwakemea, kuwakemea, kuwakaripia, kuwafokea,
    Hakika, hakuna kutia, hakuna kutoa
    Hakika, Hisabati kueleweka hakupo.
    Haki, ukiukaji, melandana kama ulimi na mate!

    Dovu hili dovu kubwa!
    Lima hili, pandikizi
    Uzito wa nanga, kukwepa hakukwepeki.
    Wanasema faraghani, kwa mihemko!
    “Watatu maghulamu,
    Zao la ushuhuba, kando na mkataba.”
    Ingawa, kwangu mimi, maana yaniambaa.

    Kabla,
    Najua fika kuwa,
    Tumbo ndilo kisukumo, chanzo hasa.
    Uki ulioacha, ndicho chanzo cha migogoro.
    Migogoro isiyo ukomo
    Kutokomea tokotoko.
    Kwangu mezaa madhara.

    Lakini.

    Kabla ya Kabla,
    Hafifu maninga yanatazama
    Mwanga ukinyemelea,
    Ishara kuwa,
    “Yamekwisha!”
    Tetesi zimekuwa feki! Kwa vile,
    Nijuavyo,
    Hata wawili wetu mabanati,
    Hakika,
    Ni zao la takrima ya akraba yako mnuna.
    Hakika,
    Ulikuwa ardhi tambarare.
    1. Kwa kutolea mifano, fafanua masuala makuu sita anayoyazungumzia mshairi. (alama 6)
    2. Onyesha vipengele vifuatavyo vilivyotumika katika shairi. (alama 6)
      1. Aina za taswira
      2. Taashira
      3. Aina za usambamba
    3. Huku ukitolea mifano, bainisha nafsineni katika shairi hili. (alama 2)
    4. Fafanua toni inayojitokeza katika ubeti wa mwisho. (alama 2)
    5. Pambanua muundo wa shairi hili. (alama 4)

SEHEMU D: HADITHI FUPI
Jibu swali 6 au 7
Alifa Chokocho na Dumu Kayanda: Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine
Eunice Kimaliro: Mtihani wa Maisha

  1.               
    1. Onyesha jinsi mwandishi alivyotumia uzungumzinafsi kukuza wahusika katika
      hadithi Mtihani wa Maisha. (alama 8)

      Salma Omar Hamad: Shibe Inatumaliza
    2. “Lakini nakwambia tena, kula kunatumaliza.”
      “Lakini kula kunatumaliza vipi?”
      1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 5)
      2. Jadili jinsi mandhari ambamo mazungumzo haya yamejikita yanafanikisha maudhui katika hadithi hii. (alama 7)

        Alifa Chokocho: Tulipokutana Tena
    1.  “Kwa nini walinitoa na kunisabilia kuwa mbali na wao? … Nilihisi kwamba waliniuza au walinitupa.”
      Tumia usimulizi wa msemaji kutathmini ukweli wa kauli iliyopigwa mstari. (alama 9)
      Ali Abdulla Ali: Ndoto ya Mashaka
    2. Jadili mbinu-ishi zinazoibuliwa na wahusika mbalimbali katika hadithi hii. (alama 6)
    3. Changanua mtindo: (alama 5)
      “Siku zilijumuika zikawa majuma, majuma yakaungana na kuunda miezi na miezi ikaunda miaka. Nakumbuka siku moja … siku hiyo hatuna hili wala lile. Tulikuwa ndani tukipiga gumzo. Mimi na Waridi. Si unajua tena mambo ya utoto? Mimi nilikuwa barobaro zima na Waridi, mwanamwari. Ghafla tulisikia teke puu … na kilango ng’waa … kikasalimu amri!”

SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI

  1. Soma utungo ufuatao kisha uutumie kujibu maswali yanayofuata

    Jua limechomoza leo likiwa kali angani
    Majira ni ya asubuhi rafiki,
    Akilini sijasahau
    Aliyonipitishia, akishatindiika,
    Aibu ikanitwaa na wahaka kunivaa.

    Kadamnasi alifika hadharani kumimina
    Cheche moto za matusi ziso mithilika.

    Ila leo nasema kwa alofanya,
    Amani nawe na muwe ardhi na mbingu
    Pamoja nawe jamaa zako wakuandame
    Katika uchochole ulitima wa kimawazo
    Mazao yako na yanyaukie kondeni!
    Mifugo wako na wafie malishoni!
    Uhangaishwe nao mara elfu na elfu!
    Ujinga na daima urithishwe kimapokeo.
    Utulivu na ukugure daima dawamu!

    1. Tambua kipera cha mazungumzo kinachorejelewa. Thibitisha jibu lako kwa mifano mitatu. (alama 4)
    2. Kwa kutolea ithibati, taja shughuli zozote mbili za kiuchumi zinazotekelezwa na jamii inayorejelewa katika kipera hiki. (alama 2)
    3. Fafanua umuhimu wa nidaa katika kufanikisha uwasilishaji wa kipera hiki. (alama 3)
    4. Onyesha matokeo matatu ya kutenda kinyume na matarijio ya jamii inayorejelewa katika kipera hiki. (alama 3)
    5. Kwa hoja nane, eleza namna shule yako inavyochangia kukuza vipera mbalimbali vya fasihi simulizi. (alama 8)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions - Maranda Mocks 2021/2022 Exams.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest