Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Mathioya Mock 2021 Exams

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  • Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima
  • Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia
  • Kila insha isipungue maneno 400
  • Kila insha ina alama 20
  • Kila insha lazima iandikwe ;kwa lugha ya Kiswahili
  • Insha zote sharti ziandikwe katika kijitabu cha majibu ulichopewa


MASWALI

  1. Serikali ya Kenya kupitia Wizara ya Elimu imeanzisha mfumo mpya wa elimu almaarufu CBC . Mwandikie barua mhariri wa gazeti la Taifa Leo ukitoa maoni yako kuhusu changamoto zinazotokana na mfumo huu.
  2. Magonjwa ya kuambukizana yanaleta hasara kubwa katika nchi na jamii kwa jumla. Fafanua.
  3. Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali ifuatayo.
    Mwana hutazama kisogo cha nina.
  4. Anza kwa kifungu kifuatacho. Ni kweli mama ana haki ya kusamehewa , kwani hakuna binadamu hata mmoja aliyekamilika… 


Mwongozo wa kusahihisha karatasi ya kwanza

Swali 1
Changamoto za CBC

  1. Walimu wengi wangali wanatatizika jinsi ya kuendeleza mafunzo hayo kwa wanafunzi.
  2. Mtaala wa CBC unawahitaji wanafunzi watumie asilimia kubwa ya muda uliotengewa somo wakijifunza kwa vitendo wakiwa pamoja hivyo muda mwingi hupotezwa
  3. Changamoto nyingine ni ile ya kutathmini kazi ya kila mwanafunzi katika kila kipindi. Wanafunzi wanashindwa kutekeleza hilo kwani muda ulioratibiwa kwa somo unaonekana mfupi kuliko mafunzo yanayohitajika kukamilishwa.
  4. Masomo kama vile muziki, sanaa ya uchoraji, somo la kilimo na mkengine ambayo yanatoa changamoto Nyingi kwa walimu kwani hawajazoea kuyafunza.
  5. Aidha mbinu zinazo pendekezwa kutumiwa na walimu ni ng`eni na walumu hawana uzoefu wa kutosha.
  6. Mtaala huu ni ghali mno na unaegemea sana vifaa halisi vya kufunzia.
  7. Baaadhi ya wazazi hawajasoma. Hawana uwezo wa kuwasaidia wanao.
  8. Wazazi wanaona kama usumbufu kuambiwa wagharamie vifaa vya kufundishia kila mara.
  9. Kazi Nyingi ya mtaala huu imeachiwa wazazi.
  10. Shule za mjini ambako hakuna shamba limekabiliwa na changamoto ya ufunzaji wa somo la kilimo.
  11. Masomo ni mengi zaidi takribani kumi na tatu kwa mwanafunzi wa gredi ya nne.
  12. Kuna mzigo mkubwa sana kwa watoto hawa.
  13. Itakuwa vigumu sana kukadiria viwango vya kufunzu kutoka darasa moja hadi lingine.
  14. Katika kuanzisha mtaala huu raia hawakutayarishwa kupitia vikao vya umma.
  15. Wazazi wengi ;hawana vifaa ;kama simu zenye uwezo wa kuchukua picha katika baaadhi ya vipindi ili kuvipeperusha mtandaoni.
  16. Uchache ;au u haba wa vitabu katika masomo mbalimbali.
  17. Idadi kubwa ya wanafunzi katika madarasa ni changamoto kwa walimu wanaoutekeleza mtaala huu
  18. Kuna uhaba wa madarasa yenye mazingira au vifaa vinavyofaaa kufunzia mtaala huu.

Swali 2.

  1. Vifo
  2. Kupoteza kazi
  3. Uchumi kuharibika
  4. Kuwapoteza watu wenye uwezo wakuzalisha uchumi wa jamii na inchi kwa jumla.
  5. Kupelejkea kutumia fedha Nyingi katika shughuli za matibabu.
  6. Watu huingia katika madeni.
  7. Inasababisha msongo wa mawazo na mfadhaiko wa mawazo.
  8. Huhatarisha maisha ya watu wengine katika jamii, hasa watoto na walio na magonjwa sugu kama kansa.
  9. Husababisha uwoga.
  10. Husababisha unyanyapaa.
  11. Walio wagonjwa huwa na mkabala hasi kujihusu na kuhusu maisha kwani huona kama watakufa.
  12. Hafanya watu kutengwa na jamii yao hata ile ya kimataifa.
  13. Inapunguza kinga mwilini na hivyo kumweka mgonjwa katika hatari ya kifo.

Swali 3
Mwanafunzi aandike kisa kitakacho onyesha kuwa katika maisha wale wadogo/wachanga huwafuata wakuu wao/walezi/waelekezi/vielelezo
Visa vinaweza kulenga:

  1. Mtoto atakayefuata mienendo ya wazazi wake
  2. Wafanyikazi wadogo watakaofuata mienendo ya wakuu wao.
  3. Mwanafunzi anayefuata mwalimu wake.
  4. Viongozi wa chini kama vile wabunge, watakaofuata Rais

Swali la nne
Kisa kilenga muktadha wa familia ilioachana kwa sababu fulani lakini wameafikia makubaliano ya kusameheana.
Tanbihi: insha ya 3 na 4 …kisa cha mwanafunzi ndicho maudhui hivyo mwalimu akitathmini kikamilifu.

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Mathioya Mock 2021 Exams.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest