Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Mathioya Mock 2021 Exams

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  • Andika jina na nambari yako kwenye nafasi ulizoachiwa hapo juu.
  • Tia sahihi yako kisha uandike tarehe ya mtihani.
  • Jibu maswali yote.
  • Andika majibu yako katika nafasi ulizoachiwa katika kijitabu hiki cha maswali.
  • Majibu yako yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili

KWA MATUMIZI YA MTAHINI PEKEE

SWALI

ALAMA

TUZO

1

15

2

15

3

40

4

10

JUMLA

80

MASWALI

SEHEMU A : UFAHAMU
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.
Zena alikuwa tayari ashayavulia nguo na alijua kuwa hana budi kuyaoga.Alijua wazi kuwa huu ndio wakati aibu zake zote, za kweli na za uongo,zitatolewa.Huu pia ndio wakati atakaotukanwa asibakishwe na watu wanaomjua na hata wasiomjua hapo mjini.Huu ndio wakati wema wake na uovu pia utatambuliwa na kuhadithiwa watu wote hadharani na kwa siri.
Huu ulikuwa wakati wa Kampeni za kumchagua mbunge wa wilaya ya mtondo Kaskazini.Kwa mara ya kwanza katika sehemu hiyo mwanamke amejitolea kupigania kiti hicho.Hapo mjini tayari moto ulikuwa unawaka na midomo inatamba kuhusu hili.Mwanamke huyo hakuwa mwingine ila ni yeye:Zena Saidi.
Zena alitoka katika familia iliyokuwa ikijulikana hapo mjini.Ilikuwa ni aila ambayo tungeweza kusema kuwa ilikuwa imeendelea.Kwa kiasi Fulani binti ya Mzee Saidi wameiona milango ya shule ijapokuwa kwa taabu mno.Wakati huo wasichana walikuwa hawasomeshwi sana na kama ulibahatika basi ulifika darasa la nne au la tano na ukatolewa mara kukitokea mume wa kukushika mkono au wazazi waonao kuwa kifua kimeanza kuinua nguo.Ilikuwa aibu kwa msichana kuonekana barabarani akienda au akitoka shule.Zena na wenzake walibandikwa majina mengi kama ‘makafiri’,Malaya na mengine mengi yasiyotajika.Zena aliendelea na kufikia darasa la saba.
Hakupita vizuri na hili halikuwa ajabu ukifikiria ule mzigo wa kazi zote alizotarajiwa afanye na asome wakati huohuo.Baba yake hakuwa na moyo wa kumwendeleza kwa sababu hakupata nafasi katika shule ya upili na pia alikuwa na wengi wa kumuingia kama umungu.Hivyo punde alipotokea mume wa kumuoa ilimbidi Zena aolewe maana wakati huo hangeweza kukataa.
Baada ya harusi hata haikuchukua muda kwa zena angali arusi kutambua kuwa hakupata mume bali dungudungu.Huyo mumewe hata hakustahi muda upite kabla kuonyesha makucha yake.Alianza kumuonyesha makruhu ya kila aina.Alibakisha tu Zena kumfumania juu chini na hili kwa hakika huyo Ali hakulijali.Alianza kurudi nyumbani akiwa amechelewa nusu saa,ikenda saa,saa mbili na hata usiku mzima.Akiulizwa kisingizio ni kazi.Zena toka mwanzo ni bunga mpaka akafahamikiwa.Toka Zena akivumilia mpaka akawa hana budi kumwelezea mamake.
Mama mtu aliyasikiliza kwa makini lakini hakuwa na suluhisho.”pengine mwanangu hutimizi wajibu wako”alitanguliza.Zena alinyamaza kwa kijitambo huku fikira zikimpita.Kama ni usafi wa nyumba na mwili anayatimiza,kama ni kupika apika akipua na kama ni kujipamba anafanya yote kumfurahisha Ali lakini wapi?Alivuta kauli,”Mama nayatenda yote lakini hata hajali,sijui nifanye nini?”Basi mama mtu alimshauri bintiye amsaili mumewe kwa upole huku akimpembeja kujua ukweli.Bwana mtu alipoulizwa alifoka kuja juu.Alitoa maneno mengi pima na mkono.”We mwanamke!We!Unanataka kunitawala?Nimekuoa au Umenioa?Huniamini nikikwambia ni kazi?”Ali alisema.Hapo basi akamwambia kuwa sasa atafanya zaidi.
Zena alikuwa tayari anajua kuwa mumewe ana mtu mwingine nje;hakuwa anahitaji udhibitisho wowote.Maana lisemwalo mjini lipo na alikuwa ashapata kidudu mtu aliyemnong’onezea hili.Lakini Ali akazidi na akawa hata siku nyingine harudi usiku kucha.Na aliporudi,nguo zote zikawa zinanukia oto la udi wa kupikwa na hata wa mawaidi na haliudi za nje.Ilikuwa ni kama huyo mwanamke mwingine anajuza kihila.Zena alipoteta basi akaanza kutiwa mkononi.
Haya yote aliyastahamili kwa shida.Maana alijua akienda kwao atakumbushwa jinsi mama yake alivyostahamili miaka rudi na kuishi na mumewe.Jambo lililomshinda Zena kumweleza mamaye ni kuwa yeye hakuwa na mateso ya kipigo na matusi.Kama ni kustahamili umaskini,kazi za nyumbani,ulezi na mengine,hayo hayangemshughulisha.Mamake alivumilia hali ya umaskini na ulezi wa mwana bila kunung’unika hadi mumewe alivyoafiki.Mungu alipopenda ,milango ya heri ilifunguliwa na wakaupa umaskini kisogo.

  1. Ni changamoto zipi mwanamke anakabiliana nazo katika jamii hii ya akina Zena (al 5)
  2. Mwanamke anatarajiwa kutekeleza majukumu gani ili kudumisha ndoa yake kulingana na mujibu wa kifungu. (al 3)
  3. Jamii hii imetawaliwa na taasubi ya kiume fafanua kwa mujibu wa taarifa. (al 3)
  4. Kwa nini Zena aliamua kuishi katika ndoa yenye dhuluma ( al 1)
  5. Ni vipi ndoa ya Zena ilikuwa tofauti na ya mamake. ( al 1)
  6. Eleza maana ya ( al 2 )
    1. kutiwa mkononi
    2. makruhu

SEHEMU YA B : UFUPISHO
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.
Miongoni mwa starehe ambazo waswahili wamezihifadhi mpaka leo ni kutoleana hadithi na kutegeana vitendawili.Starehe hizo ambazo kwa kawaida hufanywa nje huwa njiani au uani ,ama ndani chumbani au ukumbini,aghalabu hufanywa wakati wa magharibi au usiku baada ya kila mtu kumaliza kazi zake za nyumbani,dukani ,shambani ,ofisini na kadhalika .Haya yakitazamwa sana itaonekana kuwa hayakufanywa na wala hayafanywi vivi hivi.
Tangu zamani wazee wa Kiswahili waliwakataza wana wao kucheza mchana .Hawakupenda vijana wajizoeshe uvivu kwa kupiga malapa.Walisadiki kuwa mwana ambaye hakukanywa dhidi ya utiriri huu asingeweza kujifaa yeye mwenyewe na wala hata watu wengine .Isitoshe ,nani asiyejua kua ajizi ni nyumba ya njaa?Vijana walihimizwa kusaidia katika kazi mbalimbaliu zifanywazo ,majumbani,mashambani au mahali popote palipohisiwa kuwa mtu angalijifanyia jambo la kumpa riziki .Ndiposa ungesikia wazee wakiwaambia Watoto wao, ‘’ukisimulia hadithi mchana utaota mkia’’.Ingawa kwa watu wazima maneno haya yangekua masihara ,kwa Watoto yaliaminika sana na kwa hivyo wazazi wakapata mradi wao.Hii ndiyo maana waswahili husimuliana hadithi na kutegeana vitendawili jioni au usiku usiku .
Wazazi ambao hawataki Watoto wao watembeetembee au wacheze michezo ambayo itawafanya wakimbiekimbie na kujihasiri huwaita ndani ili wawe nao kuanzia magharibi.Waswahili wana itikadi nyingi zinazohusiana na wakati wa magharibi.Si ajabu kuwasikia wakisema kuwa magharibi ina nguvu.Ili kuwaepusha vijana wao na baa ilo la magharibi huwaleta Pamoja na kuwatolea hadithi .Na hata kama si hivyo hii huwa fursa nzuri kwa wazazi kuzungumza na Watoto wao ambao kutwa nzima huwa hawakupata nsafasi kuwa nao .
Starehe hizi pia huongeza elimu ,na kama wahenga wasemavyo ,elimu ni mwanga uangazao.Kwa mfano,ikiwa Watoto watategewa vitendawili ,jambo hili litawafanya wafikiri .Na kufikiri huku kutawafanya wavumbue mambo mengi ambayo pengine hapo awali hawakuyajua na kuyadhamini.Vile vile,huwafunza werevu wa kufumba na kufumbua ambayo ni elimu inayohitaji kiwango kikubwa cha busara.
Kutoleana hadithi ni miongoni mwa starehe ambazo kwazo Watoto hujifunza mambo mengi sana .Katika hadithi,Watoto wanaweza kujifunza mambo yanayohusu mila na desturi .Katika mambo haya watu hujifunza tabia nzuri,heshima ,uvumilivu na kadhalika.Pia,katika hadithi mtu anaweza kujifunza mambo ya historia na ya mazingira aliyoyazoea hata ambayo hayajui.
Aidha,hadithi ni chombo ambacho wazee hukitumia kuwafundisha Watoto mbinu za kuzungumzia.Wazee wenye busara angalabu huwapa nafasi Watoto wao wabuni na wasimulie hadithi zao.Wakati mwingine jamaa mbili Jirani huweza kukutana kufanya mashindano ya kutambiana hadithi.Mazoezi kama haya huwawezesha vijana kufikia viwango vya juu vya ufasaha wa matumizi ya lugha na ujasiri na ukakamavu na kuweza kusema mbele ya hadhara kubwa kubwa katika Maisha yao .Baadhi ya watambaji wakubwa waliopata kusifiwa haikosi mwanzo wao ulikua wa namna hii.
Hadithi pia huwafundisha watu kuhusu Maisha duniani.Zinaweza kuwafunza jinsi ya kuishi na ndugu,majirani, marafiki,wake au waume.Ulimwenguni huu tunamoishi,mna mambo mengi yanayomtatiza binadamu kwa namna mbali mbali.Hadithi zinaweza kupendekeza mambo ya kufanya na kuonyesha njia zenye mapito mema tunapofikiwa na adha kadha wa kadha.Zinaweza pia kukanya na kuonyesha faida ya kutosema uongo ama kuishi katika Maisha yasiyo muruwa,yaliyojaa kiburi na majivuno .Hapana shaka hadithi zinaweza kuongoza na kuwafanya watu wawe watiifu na raia wema katika nchi zao.

  1. Kwa maneno 50 fupisha aya mbili za kwanza. Al 5 ( mtiririko 1)
    Matayarisho
    .........................................................................................................................................................................

    Jibu

  2. Eleza umuhimu wa starehe kulingana na kifungu. (maneno 35) Al 4 (mtiririko 1)

  3. Kwa kuzingatia aya tatu za mwisho eleza dhima ya hadithi. (Maneno 50) al 6 ( mtiririko 1)

SEHEMU YA C : SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA

  1. Taja sifa mbilimbili za sauti zifuatazo. Alama 2
    1. /o/
    2. /ny/
  2.                            
    1. Eleza dhana ya mofimu. Alama 1
    2. Bainisha mofimu katika neno; kijakazi alama 1
  3. Bainisha miundo miwili katika ngeli ya: U-ZI Alama 2
  4. Tunga sentensi ukitumia aina zifuatazo za maneno.
    1. kiunganishi cha kinyume alama 1
    2. kitenzi kishirikishi kipungufu alama 1
  5. Zingatia maagizo uliyopewa
    Tutaenda kucheza uwanjani . ( Badilisha iwe katika nafsi ya tatu huru hali isiyodhihirika.) alama 2
  6. Andika sentensi hii katika ukubwa alama 2
    Mvulana mweusi alicheza ngoma karibu na mto Kiberenge.
  7. Eleza dhima ya sentensi ifuatayo. Alama 1
    Uchaguzi utafanyika mwaka ujao.
  8. Mwalimu alimshikisha mwanafunzi kitabu.
    Anza kwa: Kitabu… alama 2
  9. Taja matumizi mawili ya kinyota. Alama 2
  10. Alikula,akanywa,akasherehekea ujana wake. ( Andi ka upya katika wakati ujao hali ya kuendelea.) alama 1
  11.                    
    1. Eleza maana ya sentensi ambatano. Alama 1
    2. Tunga sentensi iliyo na muundo ufuatao. alama 2
      S- KN (W+V)+KT(T+N+S̅)
  12.  Ainisha virai vilivyopigiwa mstari. Alama 2
    Mama mwenye bidii sana alipata faida baada ya uchuuzi.
  13. Tunga sentensi moja kubainisha maana mbili za neno lifuatalo:
    changu Alama 2
  14. Yakinisha sentensi ifuatayo alama 1
    Asingalifika mapema asingalimpata angali hai.
  15. Unganisha sentensi hizi kwa kutumia kirejeshi. Alama 1
    Waathiriwa walipokea msaada kutoka jkwa serikali.
    Waathiriwa walikuwa wamevamiwana njaa.
  16. Fafanua maana tatu za sentensi ifuatayo. Alama 3
    Chakula kingine kimepakuliwa.
  17. Eleza matumizi ya kiambishi ji katika sentensi ifuatayo. Alama 2
    Mchezaji alijishindia tuzo la shaba.
  18. Andika katika usemi halisi. Alama 2
    Mbunge wa Kasarini aliwaambia wafuasi wake kuwa angewajengea barabara iwapo wangemchagua mwaka ambao ungefuata.
  19. Ukipigia mstari, tunga sentensi moja iliyo na vingele vifuatavyo: kipozi,kitondo, ala na kiima. Alama 2
  20. Jibu kwa kutumia neno mwafaka. Alama 3
    1. Thurea ni kwa nyota, …………………………………….ni kwa nywele.
    2. Barabara ni kwa njia, …………………………………..ni kwa ukuta.
    3.  Asante ni kwa kushukuru ,………………………………….. ni kwa kufariji.

SEHEMU D : ISIMUJAMII
Wewe ni muuzaji wa bidhaa za rejareja katika soko la Madongoporoma. Hivi maajuzi idadi ya wateja wako imepungua sana. Fafanua sifa kumi za lugha ambayo ungetumia kuwavutia., alama 10

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. Ni changamoto zipi mwanamke anakabiliana nazo katika jamii hii ya akina Zena (al 5
    • Kusemwa vibaya –Kusemwa kwa siri na wazi
    • Kutopewa nafasi ya kuongoza-Kwa mara ya kwanza mwanamke amejitolea kupigania kiti
    • Kutusiwa-kama makafiri na malaya
    • Kazi nyingi za nyumbani-mzigo wa kazi zote alizotarajiwa azifanywe
    • Kuozwa mapema
    • Wanaume kutoajibika katika kazi zao-Ali hakujali
  2. Mwanamke anatarajiwa kutekeleza majukumu gani ili kudumisha ndoa yake kulingana na mjibu wa kifungu.(al 3)
    • Kudumisha usafi wa nyumba
    • Kupika na kupakua
    • Kujipamba ili kumfurahisha mwanaume
    • Kumsaili mumewe kwa upole
  3. Jamii hii imetawaliwa na taasubi ya kiume fafqanua kwa mujibu wa habari (al 3)
    • Mwanamke hakupewa nafasi uongozini-Wanaume waongoza+
    • Mwanamke anaozwa mapema na baba
    • Mwanamke akiwa hawajibiki mumewe anatoka nje ya ndoa
  4. Kwa nini Zena aliamua kuishi katika ndoa yenye dhuluma( al 1)
    • Alijua akirudi kwao atakumbushwa jinsi mamake alistahimili kuishi na mumewe
  5. Ni vipi ndoa ya Zena ilikuwa tofauti na ya mamake.( al 1)
    • Mamake hakuwa na mateso ya kipigo na matusi
  6. Eleza maana ya ( al 2 )
    1. Kutiwa mkonono
    2. Makruhu

2.

  1. Kwa maneno 50 fupisha aya mbili za kwanza. Al 5
    jibu
    1. Miongoni mwa starehe za waswahili ni kutoleana hadithi na kutegeana vitendawili
    2. Starehe hizo hufanywa nje na ndani.
    3. Hufanoywa magharibi au usiku baada ya kumaliza kazi.
    4. Wazee wa waswahili waliwakataza watoto wao kucheza mchana.
    5. Wazee hawakupenda vijana wajizoeshe uvivu.
    6. Vijana walihimizwa kusaidia katika kazi.
    7. Walisadiki mwana ambaye hakukanywa dhidi ya kutiriri asingeweza kujifaa mwenyewe.
    8. Wazee waliwasambia watoto wao kuwa ; ukisimulia hadithi mchana utatoa mkia.
  2. Eleza umuhimu wa starehe kulingana na kifungu. (maneno 35) Al 3
    jibu
    1. Huwaleta pamoja
    2. Huongeza elimu
    3. Huwafanya wafikiri
    4. Huwafunza werevu
    5. Wazazi hupata nafasi ya kuzungumza na watoto wao
  3. Kwa kuzingatia aya tatu za mwisho eleza dhima ya hadithi. (Maneno 50) al 5
    jibu
    1. Hujifunza mambo yanayohusu mila
    2. Hujifunza tabia nzuri
    3. Hujifunza mambo ya historia
    4. Hujifunza mbinu za kuzungum za
    5. Huwezesha vijana kufuikia viwango vya juu vya ufasaha wa matumizi ya lugha
    6. Huwafunza kuhusu maisha duniani
    7. Huwafunza jinsi ya kuishi na wengine
    8. Hupendekeza mambo ya kufanya
    9. Huonyesha faida ya kutosema uongo
    10. Huongoza na kufanya watu wawe watiifu.

SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA

  1. Taja sifa mbilimbili za sauti zifuatazo. Alama 2
    /o/-nyuma ,wastani,viringwa
    /ny/-kaakaa gumu ,nazali,ghuna
  2.                        
    1. Eleza dhana ya mofimu. Alama 1
      Ni kipashio kidogo sana katika neno
    2. Bainisha mofimu katika neno; kijakazi alama 1
      ki-jakazi
      ki-umoja/udogo/muundo wa ngeli ya a-wa
      jakazi-mzizi
  3. Bainisha miundo miwili katika ngeli ya U-ZI Alama 2
    Uzi – Nyuzi U-NY
    Wembe – Nyembe W-NY
    Uteo – Teo U-Ɵ
    Ulimi – Ndimi U-ND
    Ubao – Mbao U-MB
  4. Tunga sentensi ukitumia aina zifuatazo za maneno.
    1. kiunganishi cha kinyume alama 1
      alimchapa lakini/ila/ hakulia
    2. kitenzi kishirikishi kipungufu alama 1
      yu,ni,li,tu,u,m,ki,li,vi
  5. Zingatia maagizo uliyopewa
    Tutaenda kucheza uwanjani . ( Badilisha iwe katika nafsi ya tatu huru hali isiyodhihirika.) alama 2
    Wao waenda kucheza uwanjani
  6. Andika katika ukubwa alama 2
    Mvulana mweusi alicheza ngoma karibu na mtoi Kibarenge.
    Vulana jeusi lilicheza goma karibu na jito Kiberenge
  7. Eleza dhima ya sentensi ifuatayo. Alama 1
    Uchaguzi utafanyika mwaka ujao.
    Sentensi ya taaarifa
  8. Mwalimu alimshikisha mwanafunzi kitabu. Anza kwa kitabu alama 2
    Kitabu kilishikishwa mwanafunzi na mwalimu
  9. Taja matumizi mawili ya kinyota. Alama 2
    Kuonyesha neno limeendelezwa vibaya/makosa
    Kuonyesha sentensi iliyo na makosa
    Kuonyesha jambo la faragha
  10. Alikula,akanywa,akasherehekea ujana wake. ( Andioka upya katika wakati ujao hali ya kuendelea.) alama 1
    Atakula,akinywa,akisherehekea ujana wake
  11.                        
    1. Eleza maana ya sentensi ambatano. Alama 1
      Ina vishazi huru viwili
    2. Tunga sentensi iliyo na muundo ufuatao alama 2
      S- KN (W+V)+KT(T+N+-S)
      Yule hodari alilima shamba kuliponyesha.
  12. Ainisha virai vilivyopigiwa mstari. Alama 2
    Mama mwenye bidii sana alipata faida baada ya uchuuzi.
    RV RH
  13. Tunga sentensi moja kubainisha maana ya neno lifuatalo ; changu. Alama 2
    Kitoweo cha samaki
    kimilikishi
  14. Yakinisha alama 1
    Asingalifika mapema asingalimpata angali hai.
    Angalifika mapema angalimpata angali hai.
  15. Andika ikiwa sentensi moja ukitumia kirejeshi. Alama 1
    Waathiriwa walipokea msaada kutoka jkwa serikali.
    Waathiriwa walikuwa wamevamiwana njaa.
    Waathiriwa ambao walikuwa wamevamiwa na njaa walipokea msaada kutoka selikali.
    Tanbihi.Kirejeshi tamati kisitumike
  16. Fafanua m,aana tatu za sentensi ifuatayo. Alama 3
    Chakula kingine kimepakuliwa.
    Ziada
    Sehemu ya
    tofauti
  17. Onyesha matumizi ya kiambishi ji katika sentensi ifuatayo. Alama 2
    Mchezaji alijishindia tuzo la shaba.
    Unominishaji
    Kirejeshi cha mtendwa
  18. Andika katika usemi halisi. Alama 2
    Mbunge wa kasarini aliwaambia wafuasi wake kuwa angewajengea barabara iwapo watamchagua mwaka ambao umefuata.
    “ Nitawajengea barabara iwapo mtanichagua mwaka ujao.’’ Mbunge wa Kasarini aliwaambia wafuasi wake.
  19. Tunga sentensi moja ukitumia kipozi, kitondo, ala na kiima.. Alam 2
    Mama alimpikia mgeni chai kwa sufuria
    Mama – kiima
    Mgeni – kitondo
    Chai – kipozi
    Sufuria - ala
  20. Jibu kwa kutumia neno mwafaka. Alama 3
    1. Thurea ni kwa nyota, shungi ni kwa nywele.
    2. Barabara ni kwa njia, kiambaza ni kwa ukuta.
    3. Asante ni kwa kushukuru ,Hamadi/makiwa/pole ni kwa kufariji.

ISIMU JAMII
Wewe ni muuzaji wa bidhaa za rejareja katika soko la Madongoporoma. Hivi maajuzi idadi ya wateja wako imepungua sana. Fafanua sifa kumi za lugha ambayo ungetumia kuwavutia., alama 10

  • Lugha ya chuku-mali safi ya bure,mali safi.
  • Matumizi ya ala za muziki-kupiga ngoma
  • Tanakali za sauti-
  • Uradidi/Takiriri/urudiaji-mia mia
  • Kutumia utohozi-soksi
  • Matumizi ya nyimbo
  • Matumizi ya viziada lugha na miondoko
  • Istilahi maalumu za kibiashara
  • Lugha ya kushawishi
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Mathioya Mock 2021 Exams.

Tap Here to Download for 50/-

Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students

Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest