Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Mathioya Mock 2021 Exams

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  1. Jibu maswali manne pekee
  2. Swali la kwanza ni la lazima
  3. Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki.
  4.  Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
  5. Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
  6. Watahaniwa wahakikishe kwamba kurasa zote zimepigwa chapa sawasawa na maswali yote yamo.


MASWALI

SEHEMU A: FASIHI SIMULIZI

  1. “Magwiji wa uwanda mpana wa tamaduni za Kiafrika: wazee walioila chumvi wakabobea katika falsafa za turathi zetu, maghuluma wenye misuli tinginya na vifua vya mfumbata vinavyostahimili hujuma za kila nui na malaika wa kike uliosheheni mizinga na chemichemi ya urembo, nawasabahi. Wa zamani waliamba kuwa mwacha mila ni mtuma. Turathi zetu ni uhai. Turathi zetu ni msingi wa ubinadamu wetu. Turathi zetu zinabeba mustakabali wetu. Tuzienzi kama tuenzivyo asali.”
    Maswali
    1.                            
      1. Tambua kipera cha utanzu wa mazungumzo kinachohusishwa na kifungu hiki. (alama 1)
      2. Thibitisha jibu lako katika (i) kwa mifano yoyote mitatu. (alama 3)
    2. Iwapo umehudhuria utendaji wa kipera hiki nyanjani eleza sifa tano za mtendaji utakazoziona zisizojitokeza kwenye kifungu. (alama 5)
    3. Taja na kueleza miktadha minne ambamo kipera hiki kinaweza kutumiwa katika jamii ya kisasa. (alama 4)
    4. Andika sifa zozote nne za jamii ya nafsi neni katika utungo huu. (alama 4 )
    5. Eleza njia tatu za ukusanyaji wa data unazoweza kutumia kukusanya data kuhusu kipera hiki. (alama 3)

SEHEMU B USHAIRI
Jibu swali la 2 au la 3
2. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yafuatayo.

LONGA
Longa longea afwaji, watabusarika
Longa uwape noleji, watanusurika
Longa nenea mabubu, sema na viduko

Longa usichachawizwe, tamka maneno
Longa usitatanizwe, mbwa aso meno
Longa usidakihizwe, kishindo cha funo

Longa yote si uasi, si tenge si noma
Longa pasi wasiwasi, ongea kalima
Longa ukuli kwa kasi, likate mtima

Longa zungumza basi, liume ja uma
Longa japo ni kombora, kwa waheshimiwa
Longa liume wakora, kwani wezi miwa

Longa bangu na papara, hawakuitiwa
Longa bunge si kiwara, si medani tawa
Longa ni simba marara, wanaturaruwa.

Maswali

  1. Tambua na ueleze nafsi neni katika shairi hili. (alama 1)
  2. Onyesha vile kibali cha utunzi wa mashairi kilivyotumika kukidhi mahitaji ya kiarudhi.(alama 4)
  3. Kwa kutoa maelezo mwafaka, tambua bahari nne zilizotumika na mtunzi kwenye shairi hili. (alama 4)
  4. Eleza aina tatu za urudiaji katika shairi. (alama 3)
  5. Tambua na kueleza toni ya shairi. (alama 2)
  6. Eleza maana ya msamiati ifuatayo kama ilivyotumika katika shairi. (alama 2)
    1. Afwaji
    2. Tenge
  7. Eleza umbo la shairi hili. (alama 4)

3. Soma shairi lifuatalo kisha uyajibu maswali.
Jiji Juani
Jiji
Lililojaa fahari na vinyume

Maghorofa
Yatishayo kupasua ngozi ya mawingu
Viumbe na magari
Waliobanana barabarani.

Jiji la
Waliostaarabika
Ya kidunia
Mafukara.

Lililojaa mfano na mwambatano
Wa majalala ya taka na waokotezaji
Wa ombaomba na waliotakata
Wa polisi na dereva
Wa waliopujuka na wanaostahi.
Jiji la :
majengo ya aushi na mioyo ya mawe
jua linalooka viumbe
jua linalotekenya ngozi za watalii – wakimbiao ganzi ya
maji baridi
jua lichomalo wavuja jasho
Huku wakizumbua riziki.

La viwanda
Vijazavyo vibeti vyenye mimba vya wenye viwanda
Vinavyofuka moshi kwenye Madongoporomoka
Vinavyosumu maisha machanga na kuua wasiozaliwa.

Jiji
La wazururao na manamba
Wanaotia kitanzi staha
Wanaotoa kauli na maneno
Yanayouma na kukereketa.

La wazee na vijana
Ambao taadhima yao
Imemezwa na jiji juani.
Jiji litandalo mashariki na magharibi
Kaskazini na kusini
Mbuga zitandazo
Katikati ya tanuri hili.

Litengalo sehemu kwa baadhi
Majumba vilimani
Vyumba visivyodari
Na mabanda yaso dirisha
Kusugua mikono laini ya mwenye nyumba.

Maswali

  1. Fafanua maswala matatu makuu aliyoyashughulikia mshairi tungoni. (alama 6)
  2. Jadili jinsi mtunzi alivyotumia jazanda kufanikisha ujumbe wake. (alama 6)
  3. Mishata ni nini ? Bainisha matumizi mawili katika shairi. (alama 4)
  4. Shairi hili ni la kukatisha tamaa. Dhihirisha. (alama 4)

SEHEMU C. RIWAYA YA CHOZI LA HERI ( swali 4 na 5)
4.

  1. ‘’Sasa anakumbuka vyema. Anakumbuka ku ;pepesa kwa jicho lake la kulia kwa muda wa wiki mbili mtawalia. Anakumbuka anguko ambalo aliangika sebuleni…Anakumbuka mavune yaliyowandama mwili wake na kuunyong`onyeza kwa muda hata pasi na kuudhili kwa kazi yoyote ya haja. Anakumbuka jeshi la kunguru lililotua juu ya paa la maktaba yake… Anakumbuka mlio wa kereng`ende na bundi usiku wa kuamkia siku hii ya kiyama… milio hii ni kama mbiu ya mgambo, huenda kukawa na jambo. ``
    1. Eleza muktadha wa dondoo hli. Alama 4
    2. Jadili aina tatu za taswira katik;a dondoo hili. Alama 3
    3. Bainisha vipengele vingine vitatu vya kimtindo. Alama 3
  2. Kwa kutolea mifano, eleza mchango wa serikali katika kuimarisha maisha ya wananchi wake. Alama 10.

5. `` Mama mtu alikuwa ameamua kwamba hapa hapam weki tena. Alikuwa amehudumu katika afisi za umma kama mhazili mwandamizi kwa miaka mingi mpaka kazi hii akaiona inamfanya kusinyaa, hana hamu tena.

  1. Eleza umuhimu wa mrejerewa katika kukuza riwaya ya Chozi la Heri. Alama 4
  2. Huku ukitoa mifano jadili changamoto zinazokumba asasi ya ndoa kwa mujibu wa riwaya hii. Alama 8
  3. Jadili umuhimu wa mandhari katika kuijenga riwaya hii kwa kurejelea; Alama 8
    1. Shule ya Tangamano
    2. Hoteli ya majaliwa.

SEHEMU YA D TAMTHILIA YA KIGOGO ( swali la 6 na 7)
6. ``Dalili ya mvua ni mawingu, lazima tuwe macho.``

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. alama 4
  2. Bainisha vipengele viwili vya kimtindo alama 4
  3. Fafanua umuhimu wa mzungumzaji katika kuvijenga vipengele vifuatavyo vya tamthilia hii. Alama 12
    1. Ploti
    2. Maudhui
    3. Wahusika wengine

7. “Hatuwezi kukubali kutawaliwa kidhalimu tena!”

  1. Huku ukitoa mifano kumi, jadili namna wanasagamoyo walilemaza juhudi zao za kujikomboa. (al. 10 )
  2. Fafanua jinsi udhalimu unavyoendelezwa sagamoyo. (al. 10)

SEHEMU YA E HADITHI FUPI YA TUMBO LISILOSHIBA ( swali la 8)
Robert Oduori: Kidege
8.

  1. Changanua mtindo katika dondoo lifuatalo: alama 12
    ‘‘ Ndege akaamua kuwafunganisha ndoa. Ndiyo, ndoa hufunganishwa mbinguni. Kama mbingu ni huko juu, basi ndipo alipotua huyo Chiriku – ndege mdogo mwenye rangi ya kupendeza na mwenye nyimbo za peponi. Ukimlinganisha na tai, basi yeye ni kidege tu chenye madaraka madogo ya kuwafunganisha ndoa Joy na Achesa huko mbinguni juu ya mtu kulikotua. Kwa makini alidondosha kitone cha majimaji. Kikalenga kwenye pua, chwa! Achesa na Joy walishtuka. Wakatazama juu. Ndege akaruka. Mose alicheka sana pale alipokuwa. Waliokuwa wakilishana huba walitazamana. Wakabaki wanachekana, ama wanachekacheka ovyo tu.
    Wengi kamka hao walizoea bustani hii. Walizuru hasa baada ya shughuli nyingi za mchana kutwa. Shughuli za kujenga na kubomoa. Kubomoa , hili hawalipendi baadhi ya binadamu ingawa wengine wanalipenda sana. Hata yule anayejua kwamba anabomoa atasema anajenga. Mimi nikubali hivyo. Au wewe waonaje?
    Ali Mwalimu Rashid: Mkubwa
  2. “… Basi niache nitafute pesa. Muhimu mniunge mkono…”
    Fafanua athari ya vitendo vya mzungumzaji wa maneno haya katika jamii (alama 8)


Mwongozo wa kusahihisha karatasi ya tatu

FASIHI SIMULIZI
JIBU la 1

  1.                  
    1. ulumbi
    2.                          
      1. Matumizi ya lugha yenye mnato/ iliyojaa tamathali ya usemi kwa mfano methali: mwacha mila ni mtumwa.
      2. Taswira – ya urembo, misuli tinginya.
      3. Takriri – turathi zetu
      4. Anasema moja kwa moja mbele ya hadhira “nawasabahi’
      5. Anafahamu sifa zinazobainisha hadhira yake (kufahamu utamaduni wake) kama katika: ‘malaika wa kike mliosheheni mizinga na chemchemi ya urembo!’
        (za kwanza 3 x 1 = 3)
  2.                          
    1. Kuzusha na kupandisha toni kutegemea uwasilishaji wake.
    2. Kupaza sauri ili asikike kwa hadhira yake.
    3. Huenda akavaa maleba yanayoona na masimulizi hayo.
    4. Matumizi ya ishara kama vile mikunjo ya uso na viashiria mbalimbali kwa kutumia viungo mbalimbali.
    5. Miondoko jukwaani – mtendaji atatembea jukwaani kwa malengo maalum.
    6. Kutua kidrama katika utendaji wake (na zana hai/ halisia.
    7. Huenda akaimba, akauliza maswali au akaruhusu hadhira kuuliza maswali kwa dhamira ya kuihusisha katika utendaji.
      (za kwanza 5 x 1 = 5)
  3.                                    
    1. Asasi ya ndoa – mijadala ya mahari, utatuzi wa migogoro au kuchumbia
    2. Maabadini
    3. Asasi ya sharia/ mahakama
    4. Asasi ya siasa
    5. Asasi ya elimu
    6. Muktadha wa upatanishi
      (za kwanza 4 x1 = 4)
  4.                                              
    1. Jamii hii inauenzi uzee kwa kuwa wazee wana busara / falsafa.
    2. Inauenzi urembo miongoni mwa wasichana.
    3. Wavulana wanastahili kuwa na nguvu. (wenye miili iliyojengeka vizuri)
    4. Utamaduni unaenziwa na wale wasiouenzi wanakashifiwa.
    5. Ni wafugaji wa nyuki wanazalisha asali.
      za kwanza 4 x 1 = 4)
  5.                      
    1. Kutumia vinasa sauti
    2. Kutumia kanda za kunasa video
    3. Kuandika mazungumzo ya mtendaji
    4. Kusikiliza kwa makini
      (za kwanza tatu 3 x 1 = 3)

Majibu ya 2/3

SEHEMU A: USHAIRI
Swali la 2

  1. Mwananchi/ raia/mzalendo/mtetezi wa haki za binadamu. – aweze kueleza. (1 x 1 = 1)
  2. Kibali cha mshairi
    1. Tabdila – wanaturaruwa – wanaturarua ; ili kuleta urari wa vina.
    2. Inkisari – aso badala ya asiye, ili kuleta muwala wa mizani
    3. utohozi – noleji kutokana na neno knowledge ili kuleta urari wa vina na muwala wa mizani. (ataje na kueleza 2 x 2 = 4)
  3. Bahari nne
    1. Sakarani – lina mseto wa bahari – tathlitha, ukaraguni na mathnawi.
    2. Kikwamba – neno longa limetumiwa kuanzia beti zote kisha maneno yanayofuata yanatumiwa kueleza maana sawa ya neno longa.
    3. Ukaraguni – vina vya ukwapi na utao vinabadilikabadilika.
    4. Mathnawi – shairi limegawika katika vipande viwili ; ukwapi na utao
    5. Kikai – ukwapi una mizani 8 na utao una mizani 6
    6. Sabilia – shairi lina kitua. Mshororo wa mwisho unabadilika badilika katika kila ubeti.
      Zozote 4 x 1 = 4)
  4. Aina tatu za urudiaji
    1. Urudiaji wa neno – Longa
    2. Urudiaji wa visawe – longa ni sema, zungumza, ongea, kuli, tamka
    3. Urudiaji wa dhamira/ lengo – kusisitiza haja ya kuwasuta wabunge walafi/ wenye kuzua balaa.
      3 x 1 = 3
  5. Toni
    Ghadhabu/hasira – aweze kueleza (1 x 2 = 2)
  6. Maana ya misamiati
    1. Afwaji – kaumu/ halaiki/umati wa watu/kikundi/kigaro
    2. Tenge – Fujo/ ghasia/ kondo
      2 x 1 = 2
  7. Umbo la shairi
    1. Lina beti nne
    2. Kila ubeti una mishororo mitatu isipokuwa ubeti wa nne
    3. Kila mshororo una vipande viwili
    4. Lina kimalizio
    5. Kila mshororo una mizani 8 katika ukwapi na 6 katika utao
    6. Vina vya kati na vya mwisho vinatofautiana katika kila ubeti
      Zozote 4 x 1 = 4

Swali la 3 

  1.                                    
    1. Utabaka – jiji linaelezwa kuwa la waliostaarabika na la mafukara.
    2. Kutowajibika – mji unasemekana kujaa majalala ya waokotezaji
    3. Ukatili – viwanda vinafukiza moshi katika vitongoji duni hivi kuwaathiri maskini kiafya.
    4. Ubinafsi – wenye viwanda wameneemeka – vibeti vyao vina mimba – ilhali faida hiyo haiwafikii wafanyakazi wanaosalia masikini.
    5. Umaskini – mji waelezwa kujaa ombaomba.
      Hoja 3 x 2
  2.                      
    1. Majengo ya aushi yenye kusitiri mioyo ya mawe – maelezo haya yanadhihirisha kule kukosa utu kwa waishio mjini.
    2. Jua lichomalo – ni jazanda ya ugumu wa maisha mijini.
    3. Vibeti vyenye mimba – kutononoka kihali kwa wamiliki viwanda
    4. Kutiwa kitanzistaha – kuumbuliwa kwa mwanadamu.
    5. Maghorofa yatishayo kupasua ngozi ya mawingu – ufanisi mkubwa uliofikiwa mijini.
    6. Majalala ya taka- ni kiashiria cha uozo uliojaa mijini. Uozo huu ni pamoja na kutowajibika.
      Zozote 3 x 2 = 6
  3. Mshata ni mstari ambao haujakamilika kimaana. Unahitaji msaada wa mstari mwingine ili kukamilika.

    Mifano :
    Lililojaa na mwambatano
    Wa majalala ya taka na waokotezaji

    Jua lichomalo wavuja jasho
    huku wakizumbua riziki

    jiji
    la wazururuao na manamba
    Wanaotia kitanzi staha

  4.                  
    • Mji umewakosesha watu utu – mioyo ya mawe.
    • Ingawa wamiliki wa viwanda wanaendelea kunawiri waajiriwa wamesalia kuwa masikini
    • Heshima imewatoka wazee kwa vijana kule mjini.
    • Mji umezama katika taka na hapama dalili za kuondolewa kwazo.
    • Viwanda vinaathiri afya ya wakazi wa vitongoji duni na hata kusababisha kufa kwa wana wangali mimbani.
      Jibu la 4/5 Riwaya ya Chozi la Heri

4.

  1.                      
    1.                                  
      • maelezo ya mwandishi/ msimulizi
      • Anamrejelea Ridhaa
      • Ridhaa yuko nyumbani kwake/ganjo/gofu lake
      • Anapokumbuka yaliyompta kabla ya kuchomewa nyumba yake
    2.                    
      • Taswira mnuso – mavune yaliandama mwili wake
      • Taswira hisi – anguko ambalo alianguka sebuleni
      • Taswira sikivu – mlio wa kereng`ende na bundi
      • Taswira mwendo – jeshi la .ku8nguru kutua juu ya paa
    3.              
      •  Tashhisi – mavune yaliuandama mwili wake
      • Takriri/uradidi – anakumbuka
      • Methali – mbiu ya mgambo ikili a huenda kuna jambo.
  2.                
    • mchango wa serikali ;katika kuimarisha maisha ya wananchi wake.
    • Inawasaidia watoto ;ombaomba kwa kuwapeleka katika shule za ufundfi k.m Hazina
    • Kumwokoa Hazina na ,wenzake kutoka kwa uvutaji gundi na matumizi ya mihadarati na kisha wanawaelimisha
    • Imeanzisha elimu bila malipo kwa shule za msingi – Ridhaa kwa Tila
    • Inawajengea wanyonge makao – Hazina
    • Inazindua hazina ya kufadhili masomo ya watoto[ wahitaji.
    • Wizara yia elimpu inlamsaidia Ummu kwa kumhamisha hadi ,shule ya lupili ya lTangamasno.
    • Sauna na .Bi Kangara wanatiwa mbaroni.
    • Inawahukumu Sauna na Kangara miaka kadhaa na kazi ngumu.
    • Mwangeka anapata nafasi ya kuenda mashari kiu ya kati kudumisha amani.
    • Inawahamazisha wakimbizi baada ya vita kuzuka huko msitu wa Mamba.

5.

  1. umuhimu wa mrejelewa ; ( Annete- mkewe kiriri)
    • Kielelezo cha malezi mabaya
    • Anaonyesha ubinafsi
    • Usaliti – anapomwacha mumewe
    • Kuonyesha mgogoro katika ndoa
    • Ukengeushi
    • Uhusiano uliopo baina ya wazazi nas wanao
    • Madhara ya kuvunjika kwa ndoa
    • Sifa/ tabia za Kiriri
  2. changamoto zinazokumba asasi ya ndoa
    • Vifom - Teerry, Lily
    • Ukosefu wa watoto – Mwangemi na Neema
    • Ukabila/ ukoo – Lucia, Subira, Selume
    • Wazazi kukataa wanao kuolewa – Rehema
    • Ukosefu wa uaminifu – Bw. Tenge
    • Chuki – Pete kuonewa na wake wenza
    • Vita katika ndoa – mamake Sauna anadhulumiwa na Maya
    • Migogoro katika ndoa – babake Pete anamkataa
    • Pombe/ ulevi – babake mzazi Sauna
    • Umaskini – Naomi kumwacha Lunga
    • Upweke – Lunga
    • Uhasama katika ndoa – Mzee Mwimo
    • Wazee kuoa wasichana wadogo – mzee Funfo anamuoa Pete
    • Tofauti za kisiasa – Seleume na mumewe
    • Malezi ya watoto – Annete anaenda ughaibuni na watoto
    • Ndoa za kujaribisha – Nyangumi na Pete
    • Kudanganywa – Pete anadanganywa na mwanamme
    • Wanandoa kutoacha nasaba zao baada ya kuolewa – Naomi
    • Maonevu/ kutengwa – Subira
    • Usaliti – Billy na Sally
  3. umuhimu wa mandhari
    1. shule ya Tangamano
      • Kuonyesha masaibu lyanayoikumba familia ya ummu
      • Matatizo wanayokumbana lnayo wakimbizi – Kairu
      • Kuonyesha umaskini – familia ya Kairu
      • Ubaguzi wa kiokoo – mamake mwanaheri
      • Matatizo ya vijana wa kike katika umri mdogo – Zohali , Rehema
      • Jukumu la familia kusambaratisha watoto – Chandachema
      • Uwajibikaji wa vijana – Chandachema
      • Nafasi ya dini
      • Ukosefu wa uaminifu katika ndo/ uasherati – BW.Tenge
      • Ukatili wa Bw. Tenge
    2. hoteli ya majaliwa
      • Kukutanisha watoto wa Lunga.
      • Kuonyesha malezi mema – mwangeka na mwangemi
      • Uhafidhina wa babu
      • Taasubi ya kiume ya babu
      • Msamaha – Naomi / watoto wake

SEHEMU YA D TAMTHILIA
6. 

  1.                        
    • Msemaji – kenga
    • Msemewa – majika
    • Mahali – ofisini mwa majika
    • Kenga anamtahdharisha kuwa sharti harakati za Tunu zishughulikiwe kwa haraka
  2.                        
    • Methali – dalili ya .mvua ni mawingu
    • Msemo - tuwe macho
    • Jazanda/ istiari – mvua ( hatari)
  3. umuhimu wa Kenga katik ;a kuijenga ;
    1. ploti ;
      • Anachimuza ubadhurifu wa viongozi – anapojaribu kutumia vishawishi kwa Sudi
      • Kupitia kwake tunaona kufumanishwa kwa Ashua na Husuda ofisini mwa majoka.
      • Kupitia kwake tunafahamishwa kuhusu kifo cha Jabali ambach wahusika walikuwa ni m ;ajoka
      • Yeye pamoja na majoka wanapanga mauaji ya Chopi
      •  Aidha, alihusika ;katika mpango wa kumuumiza Tunu
      • Mabadiliko – anapojiunga na watetezi na kumuacha Majoka
    2. maudhui ;
      • Kuonyesha ubarakala – anafaidika na .uongozi wa Majoka
      • Kielelezo cha viongozi badhirifu – wanaponda mali ya ummma anapoahidiwa kipande cha ardhi
      • Ushauri mbaya – anamp[otosha majoka
      • Ubinafsi – anatumia wadhifa wake kutimiza maitakwa ya kibi na fsi
      • Anaonyesha mabadiliko –m anapojiunga na akina Tunu
      • Ukatili – anahusika katika mauaji ya Jbali
    3. wahusika;
      • Anakuza sifa za Majika kama katili – wanapopanga na ye mauaji ya Jabali
      • Anaonyesha ujinga wa Boza – anamdharau anapochonga ki9nyago
      • Ujasiri wa Sudi – anapokataa vishawishi vyake

7. 

  1.                                
    • Askari kuwapiga waandamanaji / Ashua jelani.
    • Vijana/ wahini kutumiwa katika mauaji
    • Kuwachagua viongozi waba ya
    • Wengine ka Kengak kutoa ushauri mbaya ili wafaidike
    • Kuuza pombe haramu inayodhuru – mama pima
    • M,ajoka kufunga soko
    • Vyombo vya habari kueneza propaganda
    • Viongozi kueneza ukabila/ vijikaratasi
    • Majoka/ viongozi kufuja pesa za umma
    • Kubomoa vibanda vya wafanya ,biashara
    • Majoka kutoa kibali cha ukataji miti
    • Kutosafisha soko ilhali kodi inalipwa
    • Vijana kujituma katika ulevi/dawa za kulevya
  2.                          
    • Kufungwa kwa soko la sagamoyo ni dhuluma kwa wafanya biashara.
    • mauji ya Jabali na waandamanaji
    • Ashua kuzuiliwa bila sababu.
    • Ashua kufanyiwa uhuni na majoka.
    • Ashua kupigwa kwenye seli
    • Mazingira machafu na wanasagamoyo walipa kodi
    • Kuvamiwa na kupigwa kwa Tunu
    • Majoka kukataa kutoa msaada wa chakula kwa wahitaji
    • Kutoa kodi ya juu
    • Kufunga vyombo vya habari mf. Runinga ya mzalendo.
    • Kutumia vitoa machozi kuwatawanya waandamanji
    • kukosa haki mahakamani.
    • Kuruhusu pombe haramu
    • Kuvivig’oa vibande vya wanasagamoyo
    • kujenga kiwanda cha sumu ua kuwa watu

8. SEHEMU LA E HADITHI FUPI

  1. MBINU ZA KIMTINDO
    • Msemo – funganisha ndoa
    • Chuku – kama mbingu ni huko juu basi ndiko alikotua huyo chiriku
    • Ulinganishaji/ urejeleaji – ukimlinganisha na tai, basi yeye ni kidege tu
    • Stihizahi – yeye ni kidege tu
    • Tanakali ya sauti – chwa !
    • Nidaa – chwa !
    • Lakabu – Mose
    • Taswira oni – walitazamana
    • Tasfida – walilishana huba
    • Tanakuzi – kujenga / kubomoa
    • Takriri – kubomoa
    • Ukinzani wa kauli – hata yule anayejua kwamba anabomoa atasema anajenga
    • Kinaya - hata yule anayejua kwamba anabomoa atasema anajenga
    • Swali balagha – au wewe waonaje ?
  2. Athari ya vitendo vya mzungumzaji wa maneno haya na wenzake katika jamii (alama 8)
    Mzungumzaji ni Mkubwa. Vitendo vyake vinajikita katika ulanguzi wa dawa za kulevya. Dawa hizi zinaiathiri jamii (vijana) kwa njia zifuatazo.
    • Huwafanya vijana kutojielewa. Mkubwa akielekea pwani kununua pweza, aliwakuta vijana waliokuwa wamelaliana kutokana na kutumia unga. Walikuwa kama kuku na vifaranga walioona mwewe (uk 142).
    • Huwafanya vijana kupotoka kimaadili. Mmpjawapo wa vijana waliotumia unga anamtisha Mkubwa kwa upyoro wake. Anamuuliza kama wanakula kwake na kumuita ‘makande’. Mkubwa anakupuka mbio.
    • Huwafanya vijana kuwa na hisia zisizo za kawaida. Kijana mmoja anamtusi Mkubwa na kumlaumu kwa kumwangusha na ndege. Anasema kuwa alikuwa anakata kona anaenda kwa Obama.
    • Tamaa ya mali inawafanya viongozi kuwaonga wapiga kura ili wachagulie, bila ya kujali kiwango chao cha elimu. Mkubwa anauza shamba ilia pate milioni kumi za kuwaonga wapiga kura.
    • Vijana wanaoshikwa baada ya kutumia dawa walizouziwa na wakubwa wanateswa. Wakiwa ndani hawana haki. Kula ni kifo, malazi ni kifo,kukoga ni kifo, kufua ni kifo, kila kitu ni kifo.
    • Dawa hizi zinasababisha ubaguzi mkubwa katika jamii. Viongozi matajiri wanaachiuliwa kwa ulanguzi wa dawa huku vijana maskini wakiendelea kukaa ndani. Mkubwa anafanya mazungumzo na mkuu wa polizi, Ng’weng’we wa Njagu na kesho yake Mkumbukwa anaachiliwa.
    • Dawa za kuelvya huwafanya watu kuwehuka. Katika ndoto yake, Mkubwa anawaona vijana wachafu wakifanyiana vitendo vichafu. Anawaona watu wamehamaki hawana raha. Wizi umezidi mitaani. Miongoni mwa viajana wale ‘wala unga’ ni watoto wake wa kiume. Anatoka mbio. Kawa chizi.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Mathioya Mock 2021 Exams.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest