Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Asumbi Girls High School KCSE Mock 2021

Share via Whatsapp

Maswali

MAAGIZO

  • Jibu maswali yote.

 

  1. UFAHAMU: (ALAMA 15)
    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali:

    Takwimu zilizothibitishwa zaonyesha kuwa kila sekunde nane mtu mmoja hufa duniani kutokana na utumiaji wa tumbako. Kwa siku basi, watu 10,800 hufa. Wengi wa wavuta sigara huanza katika umri kati ya miaka kumi na mitatu hadi kumi na tisa. Takwimu zaonyesha kuwa mtu akivuta sigara kwa zaidi ya miaka ishirini huupunguza umri wake kwa kati ya miaka 20 hadi 25 zaidi ya ambaye hajawahi kuvuta. Hii ni kwa kuwa tumbako ina zaidi ya kemikali 4,000 zinazodhuru afya.

    Mojawapo ya madhara makuu zaidi yanayosababishwa na sigara ni saratani. Kunayo saratani ya ngozi – vidonda visivyopona huchubuka ngozini na baada ya muda hugeuka na kuwa kansa. Iri ya mapafu hutokea vifuko vya hewa vinapopasuka na hivyo kutatiza uvutaji wa oksijeni na utoaji wa kabondayoksaidi. Moshi pia husababisha madhara kwa njia ya kupitisha hewa, yaani umio, ambapo njia hii yaweza hata kuzibika hivyo kulazimu tundu kutobolewa kooni ili mgonjwa aweze kupumua. Kabla ya kufika kooni na mapafuni, moshi hupitia mdomoni. Saratani ya mdomo na ulimi basi hupatikana zaidi miongoni mwa wavuta sigara. Pia kidonda chochote, kwa mfano baada ya kung’olewa jino, huwa vigumu kupona kwa mvutaji sigara.

    Kwa wanawake, kuna hatari ya kupatwa na iri ya fuko la uzazi. Madhara kwenye njia nzima ya uzazi huifanya iwe vigumu kwa wanawake wavuta sigara kuhimili. Ni rahisi pia kuzaa njiti. Mtoto wa mvutaji huzaliwa akiwa mwepesi zaidi ya kawaida. Hii husababishwa na kabonimonoksaidi kutoka kwa sigara inayomdhuru mtoto tumboni. Saratani hii husababisha hata kifo cha mtoto aliye tumboni. Wengine wazaliwapo huwa na hatari ya kupatwa na saratani zaidi ya waliozaliwa na akina mama wasiovuta sigara.

    Aina zaidi za saratani zinazowakumba wavuta sigara ni kama vile saratani ya pua, ya tumbo, ya figo, ya kibofu cha mkojo, ya kongosho, ya njia ya kinyesi na hata saratani ya matiti inayowaathiri zaidi wanawake.

    Shida za sigara sio saratani pekee; sigara husababisha shida za macho na masikio kwa kiasi kikubwa. Mboni ya jicho yaweza kufunikwa na utando, hali inayoweza kusababisha hata upofu. Macho yaweza kuwashwa na moshi mkali wa sigara au mishipa ya macho iathirike na kemikali zinazofika kwayo kupitia kwa mishipa mapafu yanapoathirika. Masikio nayo huathiriwa na uchafu wa tumbako unaoganda kwenye mishipa hadi sehemu za ndani za masikio. Damu hupunguza mwendo ufaao masikioni hivyo yanaugua. Moshi na kemikali za tumbako pia hujeruhi sehemu za ndani na athari hii yaweza kuenea hadi ubongoni na kusababisha utando unaofunika ubongo. Hali hizi zaweza kusababisha uziwi.

    Mifupa na meno huathirika pia. Mifupa huwa myepesi, hukosa nguvu na kuwa rahisi kuvunjika. Mvuta sigara akivunjika mfupa huchukua muda wa asilimia themanini (80%) kupona zaidi ya mtu asiyevuta. Meno nayo hutatizika katika ukuaji wake kutokana na kugandwa na moshi wenye kemikali. Hali hii husababisha harufu mbaya, uchafu pamoja na kuoza kwa meno.

    Ngozi ya mvuta sigara hukaushwa na kemikali kwa sahabu uwezo wake wa kujirekebisha na kujilainisha hupunguzwa pakubwa. Hali hii husababisha ukavu unaoonekana pamoja na makunyanzi yanayomfanya mvuta sigara aonekane mzee zaidi ya umri wake. Vidole navyo vilevile hugandwa na kutu ya sigara, nazo kucha na vidole hugeuka rangi vikawa vya manjano, hudhurungi au maji ya kunde. Vidole pia hukaushwa na moto na kemikali ya sigara. Nywele za mvuta sigara pia huathirika kwa kuwa kemikali huipunguza kinga ya mwili hivyo mizizi ya nywele kukosa nguvu. Nywele za mvuta sigara zaweza kung’oka mapema.

    Sigara husababisha magonjwa ya moyo na vidonda vya tumbo. Kwa moyo, sigara husababisha shinikizo la damu na hatimaye mshtuko wa moyo waweza kutokea na kusababisha hata kifo. Kwa tumbo, sigara hupunguza uwezo wa kinga zake wa kuikinga dhidi ya asidi zinazosaga chakula. Pia hupunguza uwezo wa mwili wa kujikinga dhidi ya vidonda vya tumboni. Vidonda vya tumbo vya mvuta sigara huwa vigumu kupona na, ni rahisi kutokea tena baada ya kupona.

    Kwa mwanamume, mpigo wa damu kwenye sehemu za uzazi huathiriwa. Hali hii ikizidi husababisha hata upungufu wa nguvu ya mbegu kwenye shahawa. Hata ugumba waweza kutokea. Pia watoto wa mwanamke mvuta sigara waweza kuzaliwa wakiwa na kasoro. Mimba zingine zilizotungwa na wanawake wavuta sigara pia hutunguka. Na si hayo tu; madhara ya sigara ni mengi zaidi.

    Maswali
    1. Yape makala haya kichwa. (alama 2)
    2. Mbali na athari kwa uzazi kwa wanawake na wanaume na sura/umbo la binadamu, taja madhara mengine ya uvutaji sigara kwa binadamu. (alama3)
    3. Kwa kurejelea kifungu onyesha kwamba sigara kwa wanawake hasa ni hatari mno. (alama 4)
    4. Je, ni kweli kuwa vifo vingi hutokea kwa sababu ya uvutaji sigara? Toa sababu. (alama 2)
    5. Eleza namna ambavyo uvutaji sigara huathiri sura ya mhusika. (alama 3)
    6. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa kwenye taarifa. (alama 1)
      Gandwa _______________________________________________________________________
  2. UFUPISHO: (ALAMA 15)
    Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali:

    Biashara ya kimataifa ni muhimu sana katika ukuaji wa uchumi wa nchi yoyote ile. Nchi mbalimbali zimekuwa zikitegemeana kwa namna moja au nyingine. Kwa mfano, nchi ya Kenya imekuwa ikiuza maua na mboga katika nchi za ng’ambo na kupata fedha za kigeni ambazo hutumiwa humu nchini kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

    Biashara ya kimataifa huziwezesha nchi ambazo hazizalishi bidhaa na hata huduma mbalimbali kupata bidhaa hizo kutoka nchi nyingine zinazohusiana nayo katika biashara. Mathalan, Kenya ni nchi ambayo imekuwa ikitegemea kilimo lakini haijaendelea katika sekta ya viwanda. Kenya huagiza bidhaa kama vile vipuri vya magari na hata magari yenyewe kutoka nchi kama vile Japan. Nayo Kenya huuza mazao ya shambani kama vile pareto, chai na kahawa ng’ambo.

    Kupitia kwa biashara ya kimataifa, nchi hupata masoko kwa bidhaa zake. Kwa vile biashara ya kimataifa huziwezesha nchi husika kuzalisha bidhaa mahususi ambazo hazitaigharimu nchi pesa nyingi kuzalisha, nchi hizo aghalabu huzalisha kiasi kikubwa cha bidhaa kuliko mahitaji yake ya nyumbani. Nchi basi hulazimika kutafuta masoko nje ya mipaka yake. Kwa njia hii uchumi wa nchi huendelea kuimarika.

    Aidha, biashara ya kimataifa huwezesha nchi kupata huduma za kitaaluma ambazo hazipatikini katika nchi husika. Kuna nyanja za kiuchumi ambazo huhitaji wataalamu mahususi. Kwa mfano, katika sekta ya matibabu nchini humu tumepata kwamba kuna baadhi ya magonjwa ambayo yanahitaji matibabu maalumu. Wanaougua magonjwa haya huagiziwa madaktari kutoka ng’ambo au hata kupelekwa ng’ambo kwa uchunguzi na matibabu zaidi.

    Biashara ya kimataifa hukuza ushirikiano wa kimataifa. Nyakati za majanga ya kimaumbile na hata mengine yanayosababishwa na kutowajibika kwa binadamu, nchi hupata usaidizi kutoka nchi za ng’ambo. Kwa mfano wakati wa mkasa wa bomu wa 1998, Kenya ilipata msaada wa kukabiliana na janga hili kutoka Israeli, Marekani na hata Ujerumani ambako baadhi ya waathiriwa wa mkasa huo walipelekwa kwa matibabu zaidi. Ushirikiano huu wa kimataifa huwezesha wananchi kutoka nchi fulani kwenda kusomea na hata kufanya kazi katika nchi nyingine. Katika miaka ya hivi karibuni Wakenya wengi wamekuwa wakienda kusomea vyuo vikuu vya ng’ambo. Wengine wamediriki kupata kazi katika mashirika ya kimataifa katika nchi mbalimbali kama vile Afrika Kusini, Rwanda, Msumbiji na kadhalika.

    Biashara ya kimataifa husaidia kukuza ushindani kati ya nchi husika. Ushindani huu ni hakikisho la uzalishaji wa bidhaa za thamani bora. Kila nchi itafanya juu chini kuzalisha bidhaa ambazo zinaweza kukubalika katika soko la kimataifa. Pia wananchi wa nchi husika hupata aina tofauti za bidhaa badala ya kutegemea aina moja tu ya bidhaa zinazozalishwa nchini mwao.

    Biashara ya kimataifa huleta ushirikiano wa kisiasa na uelewano zaidi kati ya madola mbalimbali. Mathalan muungano wa nchi za Afrika Mashariki – Kenya, Uganda na Tanzania, hauchangii tu kuleta manufaa ya kiuchumi bali huleta ushirikiano zaidi wa kisiasa.

    Ingawa biashara ya kimataifa ina natija, biashara hii huandamana na hasara mbalimbali. Biashara hii imesababisha kuwapo kwa masoko huru ambayo yameleta ushindani mkubwa kwa wafanyibiashara wadogo wa humu nchini. Baadhi ya wafanyibiashara wamelazimika kufunga biashara zao baada ya kufilisika. Ushuru mkubwa unaotozwa baadhi ya bidhaa nchini huwafanya wananchi wengi kutofaidika kwa bidhaa na huduma kutoka nje. Aidha, kuna ucheleweshaji wa bidhaa zilizoagizwa. Bidhaa hizi mara nyingi huchukua muda kabla ya kutoka nchini, kwa hivyo wafanyibiashara wengi hulazimika kungojea kupata bidhaa hizi na kuwauzia wateja wao.

    Vilevile, kutokana na biashara ya kimataifa, bidhaa duni huweza kupenyezwa katika mataifa yanayoendelea. Pia baadhi ya wafanyibiashara wa kimataifa huchukua fursa hii kulangua dawa mbalimbali za kulevya ambazo huwaathiri vijana wa nchi husika. Wengine huhusika katika vitendo vya kigaidi kama vile uchomaji wa majengo mbalimbali kwa bomu na mauaji ya ananchi wasio na hatia.

    Ni kweli kuwa biashara ya kimataifa ina hasara zake. Hata hivyo mhimili mkubwa wa uchumi wa mataifa machanga.
    1. Kwa maneno yasiyozidi themanini, eleza umuhimu wa biashara ya kimataifa.(alama 7)
      Matayarisho
      Nakala safi
    2. Kwa maneno yasiyozidi 40, eleza ujumbe wa aya tatu za mwisho. (alama 6)
      Matayarisho
      Nakala safi
  3. MATUMIZI YA LUGHA
    1. Sahihisha sentensi: (alama 2)
      1. Mitume hiyo siyo ambayo tunaijua.
      2. Wasikilizaji sasa wanaburudika na muziki kutoka idhaa la taifa hii.
    2. Ikanushe sentensi hii katika umoja. (alama 2)
      Wasingecheza kiustadi wasingeshinda katika michezo ile.
    3. Tambulisha nyakati na hali katika sentensi: (alama 2)
      1. Wachezaji walikuwa wanafanya mazoezi.
      2. Nkirote alipoingia alitukemea.
    4. Eleza maana za sentensi. (alama 2)
      1. Kwa nini wasililie hapa?
      2. Kwa nini wasilie hapa?
    5. Toa mifano miwili miwili ya sauti zinazotamkiwa katika : (alama 2)
      1. ufizi …………………………………………………………………
      2. meno ……………………………………………………………………
    6. Andika udogo na ukubwa wa neno ‘kidole’. (alama 2)
    7. Tunga sentensi mbili tofauti kubainisha matumizi ya KWA. (alama 2)
    8. Onyesha shamirisho kipozi na kitondo katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
      Msichana alimkaririra mgeni shairi.
    9. Tumia vitenzi hivi katika sentensi mojamoja katika jinsi ya kufanyiwa. (alama 2)
      1. nywa
      2. pa
    10. Kistari kifupi ( - ) aghalabu hutumika kuendeleza sauti hasa katika vihisishi. Onyesha matumizi mengine matatu ya alama hii akifishi. (alama 3)
    11. Tunga sentensi kubainisha tofauti kimaana kati ya vitawe: (alama 2)
      1. juha………………………………………………………………………………………
      2. jua………………………………………………………………………………………
    12. Ziandike upya sentensi hizi kwa mujibu wa maagizo uliyopewa. (alama 2)
      1. Kiyondi aliukomelea mlango alipovisikia vishindo.
        (Anza kwa :Mlango…………………..)
      2. Mvua ilinyesha sana alasiri hiyo. Wachezaji walicheza mpira vizuri tu.
        (Tumia ‘japo’)
    13. Tunga sentensi sahihi kubainisha matumizi ya KI kuonyesha: (alama 4)
      1. masharti
      2. ngeli
      3. kufanyika vitenzi viwili au zaidi wakati mmoja
      4. kielezi namna
    14. Tambua hali na matumizi ya kisarufi ya neno lililopigwa mstari katika sentensi: (alama 1)
      Mtu mzee anapaswa kuheshimiwa
    15. Andika katika usemi halisi. (alama 2)
      Mwalimu aliwaagiza wanafunzi warudi darasani, warejelee madaftari yao ya kumbukumbu na kuikosoa kazi hiyo.
    16. Andika katika umoja. (alama 2)
      Tembe ambazo tulizimeza zilikuwa chungu.
    17. Eleza maana za semi au nahau: (alama 2)
      1. kwenda mbweu
      2. shika sikio
    18. Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha jedwali (alama 4)
      Kiatu kilichonunuliwa juzi kimerejeshwa dukani.
  4. ISIMU - JAMII
    1. Eleza ukionyesha bayana tofauti baina ya lahaja na lafudhi. (alama 4)
    2. Taja sifa tatu tambulizi za lugha ya misimu (alama 3)
    3. Orodhesha sifa kuu za sajili ya siasa. (alama 3)

Mwongozo wa Kusahihisha

  1. UFAHAMU
    1. Uvutaji sigara/tumbaku.
      Madhara ya uvutaji sigara/tumbaku 1x2=2
    2.        
      1. Husababisha saratani
      2. Husababisha shida za macho na masikio.
      3. Huathiri mifupa na meno.
      4. Husababisha magonjwa ya moyo na vidonda vya tumbo. 3 x 1
    3.      
      • Madhara kwa  njia ya uzazi huifanya iwe vigumu kuhimili.
      • Ni rahisi kwao kuzaa njiti.
      • Huzaa watoto wepesi
      • Huweza kusababisha kifo cha mtoto aliye tumboni.
      • Mtoto huweza kuzaliwa akiwa na kasoro.
      • Mimba huweza kutunguka. 4 x 1
    4. Ndio:  Kwa kila sekunde nane mtu mmoja hufa duniani kwa sababu ya kutumia tumbaku/kwa siku watu 10,800 hufa. 1 x 2
    5.     
      • Ngozi ya mvutaji hukauka/fanya mtu kuonekana mzee.
      • Vidole hugandwa na kutu ya sigara.
      • Kucha za vidole hugeuka rangi vikawa vya manjano/hudhurungi.
      • Nywele hukosa nguvu
      • Nywele hung’oka mapema. Zozote 3 x 1
    6. Kwamiliwa/kataliwa. 1 x 1
  2. UFUPISHO
    1. Umuhimu
      • Ukuaji wa uchumi.
      • Kupata bidhaa kutoka nchi nyingine.
      • Masoko kwa bidhaa yake.
      • Huduma za kitaalamu.
      • Hukuza ushurikiano wa kimataifa.
      • Hukuza ushindani.
      • Ushirikiano wa kisiasa. 7 x 1 =7
    2.  
      • Masoko huru yanayoleta ushindani wa wafanyibiashara wadogo.
      • Biashara kufungwa.
      • Ucheleweshaji, wa bidhaa zilizoagizwa.
      • Bidhaa kuchukua mda.
      • Bidhaa duni huweza kupenyezwa.
      • Ulanguzi wa madawa. 6 x 1 = 6
        Mtiririko =2
  3. MATUMIZI YA LUGHA
    1.          
      • Mitume hao sio ambao tunaowajua. 4 x ½ = 2
      • Wasikilizaji sasa wanaburudika kwa muziki kutoka idhaa ya taifa. Tuza 1 x 2 = 2
    2. Angecheza kiustadi angeshinda katika mchezo ule. Zozote 4 x ½ = 2
    3. Wakati uliopita, hali ya kuendelea 1
      Wakati uliopita,hali isiyodhihirka 1
      1.       
        • Mbona hawawezi kulia wakiwa hapa/ (Kitumizi) 1
        • Mbona hawawezi kulila(tunda / boga/nk) wakiwa hapa
      2.  
        • Mbona hawawezi kula wakiwa hapa?
        • Mbona hawawezi kulia wakiwa hapa 1
    4.    
      1.  ufizi /t/ /d/, /s/z/ /n/ /l/ /r/
      2. meno /th/ /dh/
    5.   
      1. Kijidole
      2. Dole 2 x 1 = 2
    6. Sentensi idhihirishe
      Mahali
      • Sehemu ya kitu
      • ‘Pamoja na’
      • Kielezi namna / jinsi
      • Kitumizi
      • Swali Zozote 2 x 1 = 2 .Atunge sentensi
    7.  
      1. Shairi – kipozi 1
      2. Mgeni – kitondo 1
    8.         
      1. Nywewa 1
      2. Pewa 1
        Tuza sentensi sahihi
    9.  
      • Kuonyesha neno lilitokatwa
      • Kuonyesha mzizi wa neno
      • Kugawa silabi
      • Kuunganisha sentensi mbili 3 x 1 = 3
    10.        
      1.  
        • juha -mtu mjinga
          Sentensi moja sahihi – alama 1
        • Jua
          Jua linaloangaza angani
        • Fahamu Sentensi moja sahihi – alama1
    11.   
      1. Mlango ulikomelewa na Kiyondi alipovisikia vishindo. 1
      2. Wachezaji walicheza mpira tu japo mvua ilinyesha sana alasiri hiyo 1
        Japo mvua ilinyesha sana alasiri hiyo, wachezaji walicheza mpira vizuri tu.
    12.   
      1. Ya masharti / vikwazo
      2. Ngeli ya ki – vi
      3. Vitenzi viwili / zaidi kwa wakati mmoja
      4. Kielezi namna ( Kiustadi,Kishujaa, kitoto,nk) 4 x 1 = 4
    13. Kitenzi kuwa kivumishi 1 x 1 = 1
    14. “Rudi darasani mrejelee madaftari yenu ya kumbukumbu na kuikosoa kazi hii” Mwalimu aliwaagiza wanafunzi.
    15. Tembe ambayo niliimeza ilikuwa chungu. 4 x ½ = 2
    16.        
      1. Kutoa hewa mdomoni kwa nguvu 1 x 1 = 1
      2. Ujutia jambo / tendo / kujifunza 1 x 1 = 1
    17.         
        S  
        KN   KT
       N  S  T  E
      Kiatu  Kilichonunuliwa juzi  kimerejeshwa  dukani 
      Kila kitengo, alama moja 4x1=4
  4. ISIMU – JAMII
    1. Lahaja – Tofauti katika matamshi, maumbo na matumizi ya maneno zitokanazo na tofauti za kimaeneo kwa lugha yenye asili moja.
      • Husanifiwa na kupata hadhi ya kuwa lugha; K.M chimiini na Kingazija Kiswahili
      • Yaweza kuandikwa: ndoo tulale, mato yaniuma.
      • Lafudhi- Matamshi ya mzungumzaji yatokanayo na athari za lugha yake ya kwanza,lugha jirani,maumbile au hadhi katika jamii.
      • Hujitokeza kwanza kimatamshi na wala si kimaandishi:
      • Piga ugali (pika), utaguja lini? (utakuja),ndoa la mauti (doa) na kulanga kuku(kula)
        2 x 2 = 4
    2. Sifa za lugha ya misimu:
      Misimu – maneno au semi ziibukazo mahali na zidumuzo kwa muda tu; mzee, kimwana,dot-com,kusota,kupiga ngeta n.k
      1. hupendwa na kutumiwa kwa wingi
      2. huambatana na kitushi / tukio.
      3. hurahisisha mawasiliano / mazungumzo
      4. huzuka na kutoweka baada ya muda
      5. huweza kuingizwa katika maandishi zozote 3 x 1 = 3
    3. Sajili ya siasa
      • Lugha yenye mvuto / ushawishi ari na mwamko
      • Hubeba porojo na ukinzani
      • Hudokeza ahadi na utendaji bora
      • Hupumbaza na kunata
      • Hulenga kundi / watu fulani zozote 3 x 1 = 3
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Asumbi Girls High School KCSE Mock 2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest