Kiswahili Paper 1 Pre Mock Questions and Answers - Mokasa I Joint Examination July 2021

Share via Whatsapp

 

MAAGIZO

  1. Andika jina lako na nambari ya usajili kwenye nafasi ulizoachiwa hapo juu.
  2. Tia sahihi yako kisha uandike tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
  3. Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
  4. Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
  5. Kila insha isipungue maneno 400.
  6. Kila insha ina alama 20.
  7. Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
  8. Insha zote sharti ziandikwe katika nafasi ulizoachiwa kwenye kijitabu hiki cha maswali.
  9. Karatasi hii ina kurasa 9 zilizopigwa chapa.
  10. Watahiniwa ni lazima wahakikishe kwamba kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.

Kwa matumizi ya mtahini pekee

Swali

Upeo

Alama

1

20

 

2

20

 

3

20

 

4

20

 

Jumla

40

 


MASWALI

  1. Lazima
    Wewe kama katibu wa chama cha wanahabari chipukizi shuleni mwako umepata nafasi ya kumhoji Katibu katika Wizara ya Habari na Mawasiliano nchini kuhusu athari ya mitandao na utandawazi kwa jamii. Andika mahojiano hayo.
  2. Maovu ya kijamii yamekithiri sana miongoni mwa vijana. Eleza chanzo na upendekeze hatua zinazofaa kuchukuliwa ili kusitisha maovu haya.
  3. Tunga kisa kinachodhihirisha maana ya methali ifuatayo:
    Mchuma janga hula na wa kwao
  4. Andika insha itakayomalizika kwa maneno yafuatayo:
    Tulijifunga kibwebwe kuwaopoa wahasiriwa waliokuwa wamefunikwa na vifusi vya maporomoko ya jengo lakini juhudi zetu ziliambulia patupu.


MWONGOZO

  1. Lazima
    Wewe kama katibu wa chama cha wanahabari chipukizi shuleni mwako umepata nafasi ya kumhoji Katibu katika Wizara ya Habari na Mawasiliano nchini kuhusu athari ya mitandao na utandawazi kwa jamii. Andika mahojiano hayo.
    Hii ni insha ya mahojiano. Mahojiano haya yanawashirikisha wahusika wawili. Mmoja ,mwanafunzi (ambaye ndiye mwenye kuuliza maswali) na Waziri wa Habari na Mawasiliano ambaye ndiye anayejibu.
    Majina ya wahusika yaandikwe upande wa kushoto mwa ukurasa pambizoni na kufuatwa na koloni.
    Maelekezo ya jukwaani yawe sehemu ya mahojiano ili kuelezea uhalisia wa yanayoendelea baina ya wahusika hawa
    • Kichwa cha mahojiano kiandikwe kwa herufi kubwa na kupigiwa mstari
    • Kuwe na sehemu ya utangulizi na ambayo ni sharti ibaini washiriki wa mahojiano haya

Mfano:MAHOJIANO BAINA YA KATIBU WA CHAMA CHA WANAHABARI CHIPUKIZI NA KATIBU KATIKA WIZARA YA HABARI NA MAWASILIANO KUHUSU ATHARI YA MITANDAO NA UTANDAWAZI KWA JAMII YALIYOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA SHULE

  • Katika utangulizi,mhoji na mhojiwa waamkuane.
  • Mhoji ajitambulishe na kutambulisha mada wanayozingatia
  • Mhoji amkaribishe mhojiwa na kumtaka kujitambulisha
  • Katika sehemu ya mwili,mahojiano yasitawaliwe na mhusika mmoja sana.
  • Mhoji aulize maswali ya kudadisidadisi naye mhojiwa ajibu maswali hayo; mfano

MWANAFUNZI:Hujambo Bwana Katibu…
KATIBU:Sijambo
MWANAFUNZI:Karibu katika mahojiano yetu ya leo ambapo tutaangazia athari ya mitandao na utandawazi kwa jamii. Mimi ni Salma Fuad, Katibu wa Chama cha Wanahabari Chipukizi hapa shuleni.
KATIBU:Nashukuru kukujua.
MWANAFUNZI:Hebu tuanze kwako wewe kujitambulisha na kueleza kwa kiduchu jukumu lako kama Katibu katika Wizara ya Habari na Mawasiliano
KATIBU:Mimi ni Bwana Kalume Kenge, Katibu katika Wizara ya Habari na Mawasiliano

Maudhui
Athari chanya

  • Nyenzo aula ya kupitisha Habari za taifa na kimataifa
  • Mitandao yaweza kutumiwa kuelimisha wanajamii kuhusu masuala ya afya
  • Ni jukwaa muhimu la burudani mfano vibonzo
  • Wajasiriamali na kampuni za kibiashara za humu na kimataifa hutumia mitandao hii kupitisha matangazo ya kibiashara
  • Hutoa nafasi za ajira kwa wanajamii, wauzaji na wahariri
  • Nyenzo muhimu ya mapato kwa serikali
  • Hutumiwa kutangazia nafasi za ajira
  • Huweza kutumiwa kuendeleza masuala ya elimu. Uchambuzi wa vitabu vya fasihi,mashairi na maswali ya sarufi
  • Kukuza na kudumisha umoja miongoni mwa wanajamii-fesibuku,wazapu,telegram,twita nk
  • Hurahisisha mawasiliano baina ya wanajamii
  • Husahilisha utafiti

Athari hasi

  • Makundi ya matapeli na walaghai hutumia kuendeleza uhalifu wao
  • Huchangia katika kupalilia uzembe miongoni mwa wanajamii
  • Inaishia kuwapotosha watu kimaadili
  • Pana filamu zinazohimiza watu kuwa wazinifu
  • Baadhi ya matangazo ya mitandaoni huchangia katika kupotoka kimaadili kwa wanajamii, mihadarati na vileo
  • Baadhi ya wanajamii huitumia mitandao hii kueneza jumbe na hisia za chuki na propaganda
  • Huchangia wanajamii kuiga tamaduni za kigeni na hivyo kupujua utamaduni wa wetu wa kiasili, mavazi,mienendo nk
  • Ununuzi wa nyenzo za mtandao na utumizi wake unagharimu pesa nyingi
  • Baadhi ya wanajamii huishia kuganda kwenye mitandao hii na hivyo kupoteza muda muhimu wa kufanya kazi
  • Mitandao hii imechangia katika kuvunjika kwa ndoa, uchumba na familia
  • Vifaa hivi huweza kusababisha magonjwa mfano ya macho na saratani
  • Katika kuhitimisha, mhoji amuulize mhojiwa kutoa ushauri wa kijumla kwa wanajamii kuhusu utandawazi na mitandao ya kijamii.
  • Mahojiano yahitimishwe kwa mhoji kumshukuru mhojiwa na kuagana
  • Kikao cha mahojiano kihitimishwe kwa wawili hawa kupana mikono ya kuagana

Adhabu

  • Kazi ya mtahiniwa iakifishwe vizuri
  • Mtindo wa kitamthilia utumiwe wala sio nathari…ikiwa atatumia mtindo wa kuripotibau aandike barua, atozwe 4S baada ya kutuzwa
  • Ikiwa badala ya mwanafunzi atachukua nafasi ya mhojiwa badala ya mhoji atakuwa amejitungia swali. Atuzwe D- 02/20
  • Ikiwa patakuwa na mhusika wa tatu, mchango wake usijumuishwe katika jumla ya hoja za mtahiniwa
  • Mtahiniwa atumie viwakifishi vifaavyo. Mfano, alama ya hisi (!) na alama ya kuuliza (?)Mtahiniwa asitumie alama za dukuduku(…)
  • Hoja zote zinatazamiwa kutolewa na mhojiwa,jukumu la mhoji ni kuuliza maswali tu wala si kuchangia kwa kutoa hoja.
  • Mikwaju itumiwe ili kuonyesha ukamilifu wa hoja. Mikwaju hii itiwe kushoto pambizoni mwa ukurasa kunakokamilikia hoja husika.
  • Tumia mkwaju kamilifu kwa hoja za athari chanya na mkwaju wenye kikia kwa hoja za athari hasi

Tanbihi
Ikiwa mtahiniwa atazingatia upande mmoja tu wa swali, atakuwa amepungukiwa kimaudhui. Hivyo kazi yake ihakikiwe katika kiwango cha C (6-10)

  1. Maovu ya kijamii yamekithiri sana miongoni mwa vijana. Eleza chanzo na upendekeze hatua zinazofaa kuchukuliwa ili kusitisha maovu haya.

Maovu ya kijamii

  1. Ndoa za jinsia moja
  2. Kuavya mimba
  3. Wizi wa mabavu
  4. Ubakaji
  5. Uasherati / usinzi
  6. Ndoa za mapema
  7. Wanafunzi kuchoma shule

Chanzo cha maovu ya kijamii

  1. Uhaba wa kazi
  2. Ukosefu wa maelekezi
  3. Shinikizo la hirimu
  4. Umaskini/ukata
  5. Changamoto katika ndoa
  6. Ukengeushi
  7. Matumizi ya dawa za kulevya
  8. Ukosefu wa mbinu za kufidia muda mwingi walionao vijana
  9. Uigaji wa kiholela tabia hasi
  10. Ushawishi potovu kutoka / kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii

Mapendekezo

  1. Ushauri nasaha utolewe kwa vijana kupitia asasi mbalimbali za kijamii
  2. Kuchukuliwe hatua kali za kisheria kama vile vifungo virefu, kutozwa faini
  3. Kubuniwe jopo maalum la kupambana na matumizi ya dawa za kulevya
  4. Mtalaa wa elimu uhusishe mafundisho maalum kuhusu tamaduni zenye  umuhimu
  5. Wazazi na asasi nyingine kuwaonya vijana dhidi ya kushiriki mahusiano ya kimapenzi nje ya ndoa.
  6. Kubuniwe sera za kudhibiti matumizi ya mitandao hasa miongoni mwa vijana
  7. Viongozi wa kidini waadilishe jamii kupitia mafundisho maabadini.
  8. Vyombo vya habari vidhibitiwe na kuchuja yale ambayo vinawasilisha

Utahini/utuzaji

  • Swali lina sehemu mbili. Zote zijibiwe. Atakayezingatia upande moja, asipite 10 C+
  • Hoja angalau nne kwa kila sehemu zitakuwa toshelezi.
  • Atakayetaja/rejelea hoja moja ya upande mmoja, amelijibu swali lakini amepungukiwa kimaudhui 
  1. Mchuma janga  hula na wa kwao
    • Hii ni insha ya methali
    • Chuma ni kufanya kazi na kupata faida/ tungua matunda kutoka mtini.
    • Janga-tukio la hatari linalosababisha taabu na maafa; balaa, kisanga
    • Maana ya methali: Mtu fulani asababishapo janga au taabu huishia kuwahusisha watu wake au jamaa yake.
    • Mtahiniwa asimulie kisa kitakachoafikiana na methali.
    • Asipinge methali.
    • Mwanafunzi atunge kisa kinachohusu mhusika ambaye anafanya jambo baya na hatimaye kuiletea jamii/familia yake madhara/hasara.

Mifano ya ruwaza zinazoweza kujitokeza 

  1. Mhusika kushiriki raha za kilimwengu, akaambukizwa magonjwa yasiyotibika, hatimaye      anarejea nyumbani anakougua, mzigo wa kumtunza unakuwa kwa familia yake.
  2. Mhusika aliyekuwa akifanya kazi katika kampuni au shirika fulani, Anaachishwa kazi labda kutokana na uzembe au utovu wa maadili ya kikazi, anarejea nyumbani kwa familia yake; kule hana chochote hivyo basi, anaishia kutegemea jamaa zake, huu unakuwa mzigo mkubwa kwa watu wake.
  3. Mtoto ambaye anatokea kuwa mhalifu, anafikishwa kortini na kutozwa faini kubwa. Hii inakuwa gharama kwa familia yake kwa kuwa ndio wanaotakiwa kulipia.
  4. Mwanafunzi ambaye anakosa kuwajibika masomoni shuleni , anafeli mtihani, maisha ya halafu yanakuwa  magumu kwa hivyo jamaa zake wanalazimika kuingilia kati ili kumuauni kwa mahitaji ya kila siku.
  1. Andika insha itakayomalizikia kwa maneno yafuatayo;
    Tulijifunga kibwebwe kuwaopoa wahasiriwa waliokuwa wamefunikwa na vifusi vya maporomoko ya jengo lakini juhudi zetu ziliambulia patupu
    • Mtahiniwa asimulie kisa kuhusu jumba au jengo lililoporomoka na kuwafunika watu
    • Hili pia laweza kuwa tukio la kigaidi ambapo jengo lililipuliwa kwa gurunedi au bomu
    • Lazima aonyeshe jinsi yeye na wengine walivyojituma katika mchakato mzima wa kuwaokoa watu waliokuwa wamekwama ndani ya vifusi na maporomoko ya jengo
    • Aonyeshe namna walivyokumbana na tatizo hili na namna walivyojizatiti kuwaokoa wahasiriwa lakini wakashindwa
    • Katika kubuni kisa, mtahiniwa aonyeshe sababu zilizochangia kuporomoka kwa jengo ama kwa ujenzi mbaya, mlipuko wa bomu au shambulizi la kigaidi
    • Aonyeshe jinsi ambavyo mkasa huu uliishia kusababisha maafa na hasara isiyokadirika
    • Mtahiniwa akidondoa maneno hadi kufikia maneno matatu asiadhibiwe ila hili lichukuliwe kama kosa dogo la kimtindo
    • Mtahiniwa akikosa kumaliza kwa maneno ya mdokezo huu atakuwa amejitungia swali. Atuzwe D- 02/20
    • Swali hili linatahini ubunifu na umbuji wa mtahiniwa hivyo basi mtahini atumie vipengee hivi kukadiria alama za mtahiniwa
    • Vipengele vingine vya kimsingi vya usahihishaji wa insha vizingatiwe

USAHIHISHAJI.
Karatasi hii imedhamiria kutahini uwezo wa mtahiniwa wa kuwasiliana na msomaji na kuwakilisha ujumbe kimaandishi, Mawasiliano haya yatategemea ukwasi wa lugha ya mtahiniwa, kwa mfano, kutunga sentensi; sahihi zenye utiririko mzuri kimawazo. Lugha ya (kuvutia na yenye mawazo asilia, ubunifu mwingi, na hali nadhifu. Kutegemea maagizo ya swali lenyewe na umahiri wa lugha, ni lazima kutilia mkazo mtindo. Mada na uwezo wa mtahiniwa kufuata maagizo vilivyo. Mtahini lazima aisome insha yote kwanza ili aweze kuikadiria akizingatia viwango mbalimbali vilivyopendekezwa yaani  A,B,C ama D kutengemea mahali popote pale pafaapo.

KIWANGO CHA D
MARK 01 – 05.

  1. Insha ya aina hii haieleweki kwa vyovyote ama uwezo wa mtahiniwa wa kutumia lugha ni hafifu sana, hivi kwamba mtahini afikirie kile anachojaribu kuandika.
  2. Mtahiniwa hana uwezo wa  kutumia maneno ya Kiswahili kwa njia inayofaa.
  3. Lugha imevurugika, uakifishaji haufai. Na insha ina makosa ya kila aina ya Kisarufi, kimaendelezo, kimtindo n.k.

VIWANGO  TOFAUTI  VYA D
D – (KIWANGO CHA CHINI MAKI) 01 – 02.

  1. Insha haina mpangilio maalum,na haieleweki kwa vyovyote vile. Kwa mfano kunakili swali au kujitungia swali tofauti na kulijibu.
  2. Kuandika kwa lugha isiyo Kiswahili.

D (WASTANI) MAKI 03

  1. Utiririko wa mawazo haupo.
  2. Insha haieleweki.
  3. Hoja hazikuelezwa kikamilifu/ mada haikukuzwa vilivyo.
  4. Mtahiniwa amepotoka kimandhari.
  5. Hakuzingatia urefu.
  6. Kuna makosa mengi ya kila aina.

D+ (KIWANGO CHA JUU)

  1. Insha ina lugha dhaifu ya Kiswahili na haina mpangilio.
  2. Anawasilisha ujumbe kwa njia isiyoeleweka kikamilifu.
  3. Hana uhakika wa matumizi ya lugha na hupotoka  hapa na pale.
  4. Mpangilio wa kazi ni hafifu na matahiniwa wa hujirudiarudia.
  5. Mtahiniwa ana athari za lugha ya kwanza k.m papa, badala ya baba, karamu badala ya kalamu n.k.

KIWANGO CHA C
MAKI 06-10
Kiwango hiki kina makosa yafuatayo.

  1. Mada haikukuzwa na kuendelezwa.
  2. Anawasilisha ujumbe kwa njia isiyovutia.
  3. Hana ubunifu wa kutosha.
  4. Anaakifisha sentensi vibaya.
  5. Hana msamiati wa kuvutia wala msamiati mwafaka.

VIWANGO TOFAUTI  VYA C
 C-(KIWANGO CHA CHINI) MAKI 06 – 07.

  1. Mtahiniwa ana shida ya kuwasilisha mawazo yake.
  2. Hana msamiati wa kutosha wala muundo wa sentensi ufaao.
  3. Mada haijakuzwa na kuendelezwa kwa njia ifaayo.
  4. Ana makosa mengi ya sarufi, tahajia na msamiati.

(WASTANI) MAKI  8

  1. Anawasilisha ujumbe lakini kwa njia hafifu.
  2. Hana ubunifu wa kutosha na dhana tofauti hazijitokezi wazi.
  3. Uakifishaji wa sentensi zake si mzuri.
  4. Amejaribu kushughulikia mada aliyopewa.
  5. Ana makosa ya hijia sarufi na msamiati.

C+ (KIWANGO CHA JUU) MAKI 09-10

  1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri lakini kwa njia isiyo ya mvuto.
  2. Dhana tofauti zimeanza kujitokeza kwa njia hafifu.
  3. Kuna mtiririko wa mawazo japo ufundi wa lugha unaofaa.
  4. Misemo, methali na tanakali za sauti zimetumiwa kwa njia hafifu.
  5. Anashughulikia mada aliyopewa kwa utiririko mzuri.
  6. Kuna makosa ya sarufi, msamiati na hijai lakini bado  insha inaeleweka.

KIWANGO CHA B (MAKI 11-15)

  1. Katika kiwango hiki, mtahiniwa anaonyesha kuimudu lugha vilivyo.
  2. Mtahiniwa anadhirisha kwamba anaweza kutumia lugha kwa urahisi katika kujieleza.
  3. Anatumia miundo tofauti ya sentensi vizuri.
  4. Mtahiniwa ana uwezo wa kutumia lugha kwa ufasaha kama vile kuandika sentensi kwa njia tofauti tofauti na zikaleta maana sawa.
  5. Mada imekuzwa na kuedelezwa kikamilifu.

VIWANGO TOFAUTI VYA B (MAKI -15)
B- (KIWANGO CHA CHINI) MAKI 11-12.

  1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe wake kwa kuonyesha hoja tofauti tofauti.
  2. Kuna utiririko mzuri wa mawazo.
  3. Ana uwezo wa kutumia miundo tofauti tofauti ya sentensi.
  4. Makosa ni machache ya hapa na pale.

B  (WASTANI) MAKI 13.

  1. Mtahiniwa anadhihirisha hali ya kuimudu lugha
  2. Anawasilisha ujumbe wake waziwazi kwa mawazo yanayodhihirika
  3. Matumizi ya lugha ya mnatoyamejitokeza.
  4. Anatumia mifano michache ya msamiati mwafaka.
  5. Matumizi ya tamathali za semi yanaanza kudhihirika
  6. Makosa yanaweza kutokea hapa na pale.

B+ (KIWANGO CHA JUU) MAKI 14 – 15

  1. Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika.
  2. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe wake kwa njia inayovutia na kwa urahisi.
  3. Uteuzi wake wa msamiati ni mzuri
  4. Sarufi yake ni mzuri.
  5. Uakifisha wake ni mzuri
  6. Kuna makosa ya hapa na pale.

KIWANGO CHA A
Maki 16 – 20.

  1. Mtahiniwa anadhihirisha ujuzi wa lugha yenye mnato. Ana ubunifu wa mawazo yanayodhihirika na kutiririka.
  2. Ana uwezo wa kutumia tamathali za lugha ili kutoa hisia zake kwa njia bora na kwa urahisi.
  3. Umbuji wake unadhihirisha ukakamavu wake kimawazo na mpangilio mzuri na hali ya kumvutia msomaji wake.
  4. Insha hii imezingatia urefu unaotakikana.

VIWANGO TOFAUTI VYA   A
A- (KIWANGO CHA CHINI) MAKI 16-17.

  1. Mtahiniwa hudhihirisha ukomavu wa lugha.
  2. Ana utiririko mzuri wa mawazo kulingana na mada.
  3. Anapamba lugha kwa kutumia tamathali za usemi.
  4. Anazingatia matumizi mazuri ya msamiati na sarufi.
  5. Uakifishaji wake ni mzuri zaidi.
  6. Makosa machache ya hapa na pale.

(WASTANI) MAKI 18

  1. Mawazo yanadhihirika zaidi.
  2. Anatumia lugha ya mnato
  3. Anatumia msamiati wa hali ya juu na unavutia.
  4. Sarufi yake ni nzuri
  5. Anatumia miundo tofauti ya sentensi kiufundi.
  6. Anajieleza kikamilifu
  7. Makosa machache ya hapa na pale.

A+ (KIWANGO CHA JUU) MAKI 19-20

  1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe kulingana na mada
  2. Anadhihirisha mawazo yake vizuri zaidi
  3. Anajieleza kikamilifu bila shida.
  4. Anatoa hoja zilizokomaa.
  5. Msamiati wake ni wa hali ya juu
  6. Makosa ya aina yoyote yasizidi matano.
  7. Jumla ya makosa isizidi matano.

MAKOSA  YA HIJAI.
Haya ni makosa ya maendelezo.Sahihisha huku ukiyaonyesha yanapotokea. Makosa ya tahajia huwa katika:

  1. Kutenganisha neno kama vile ‘aliye kuwa’
  2. Kuunganisha maneno kama vile ‘kwasababu’
  3. Kukata silabi vibaya kama ‘ nga-o-’
  4. Kuandika herufi isiyofaa katika neno kama ‘ mahari’ badala ya ‘mahali’
  5. Kuacha herufi katika neno kama ‘aliekuja’ badala ya ‘ aliyekuja’
  6. Kuongeza herufi isiyofaa katika neno kama ‘ piya’ badala ya ‘pia’
  7. Kuacha alama iliyotarajiwa kuwepo.
  8. Kutoandika kistari cha kuunganisha neno ufikapo pambizo na mwisho au kuandika mahali si pake.
  9. Kuacha ritifaa au kuiweka pasipofaa.
  10. Kuandika maneno, kwa kifupi mfano k.m , n.k v,v.

MTINDO
Mambo yatayochunguzwa.

  1. Mpangilio wa kazi kiaya.
  2. Utiririko wa mawazo
  3. Hati nzuri inavyosomeka kwa urahisi
  4. Namna anavyotumia methali, misemo, tamathali za usemi na mengineyo.
  5. Unadhifu wa kazi
  6. Kuandika herufi vizuri, k.m Jj,Pp, Uu.
  7. Sura ya insha.

MSAMIATI.
Jumla ya maneno yaliyotumiwa kuafikiana na mada au kichwa kilichopendekezwa.

MAUDHUI NA MSAMIATI.
Bada ya kusoma mtungo utafikiria maudhui na msamiati uliomo kwa jumla.

KIWANGO                                   ALAMA                                KI
A                                                 A+                                    19-20
                                                   A                                      18
                                                   A-                                     16-17
B                                                 B+                                    14-15
                                                   B                                      13
                                                   B-                                     11-12
C                                                 C+                                    09-10
                                                   C                                       8
                                                   C-                                     06-07
D                                                 D+                                   0-05
                                                   D                                      03
                                                   D-                                    01-02

SARUFI.
Sahihisha kwa makini sana ukionyesha makosa yote yanayotokea. Makosa ya herufi huwa katika:-

  1. Kuakifisha vibaya. Kwa mfano, vikomo, vituo, alama ya kuuliza n.k.
    • Kutumia herufi ndogo au kubwa mahali si pake.
    • Matumizi mabaya ya ngeli na viambishi, nyakati, vihusiano, muundo mbaya wa sentensi na mnyambuliko wa vitenzi na majina.
    • Kuacha au kuongeza neno katika sentensi, ‘kwa kwa.
    • Matumizi ya herufi kubwa.
  1. Mwazo wa sentensi.
  2. Majina ya pekee.
    1. Majina ya mahali, miji, nchi,
    2. Siku za  juma, miezi n.k.
    3. Mashirika, masomo, vitabu i..k.
    4. Makabila, lugha n.k
    5. Jina la Mungu.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Pre Mock Questions and Answers - Mokasa I Joint Examination July 2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest