Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Momaliche Joint Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

MAAGIZO
Jibu maswali yote kwenye karatasi hii.

UFAHAMU

  1. Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
    Macho makali ya Vuai yalipigwa na mwali mkai wa jua la asubuhi.Ilikuwa ndiyo mara ya kwanza kuuona mwanga halisi wa ombwe lijiitalo dunia tangu alipohukumiwa kifungo gerezani.Punde tu komeo la mlango wa seli lilipofunguliwa,ilimlazimu Vuai ayafumbe macho kabla ya kuyafumbua tena ili yazoee mabadiliko yake.
    Ilikuwa ndiyo siku ya Vuai kuachiliwa huru kutoka kwenye kifungo kirefu kilichoyapa macho yake mazoea ya gizaa la kaburi mle gerezani.Macho yake yalipokwishaizoea ile hali na kumhakikishia kuwa kila alichokuwa akikiona si kizuka ila uhalisia,alipiga hatua.Akatoka nje ya mlango wa seli kisha kwa kutoamini,akageuka nyuma kulitazama tena lile pango alimokuwa ametikwa katika muda huo wote.Akayafikicha macho kwa kutoamini huku machozi yakimdondoka asijue kama yalikuwa ya furaha au ya huzuni.Alipogeuka kuanza safari ya uhuru wake,macho yake yalikumbana na lengo la gereza.Hapo ,akasita kidogo,labda kuhakikisha kama kweli alikuwa huru.Bila shaka,hakuna askari wa gerez aliyemshikia bunduki au kumhanikizia sauti asimame.Walimtazama tu na kumpa tabasamu.
    Taratibu,Vuai aliendelea kupiga hatua.Mhemko aliokuwa nao kutokana hewa safi iliyompenya mapafuni uliufanya moyo wake upige kwa kasi.Ghafla ,tabasamu likapasua mashavuni pake.Akasita.Akainua pua yake iliyompa hakikisho kuwa fondogoo na uvundo wa esli haukuwa- naye tena.Ingawa mwili wake ulijaa mabaka ya uchafu na matambara yaliyouficha uchi wake kuvunda,hilo halikumkera tena.Kwa hivyo,akatia tena tabasamu .Lake kuu lilikuwa ni shukrani kwa kuepuka yale madhila ya joto na rundo la wafungwa.Na kama hilo halikutosha,aligeuka tena ili sasa kuliangalia lile gereza.Bila kutaraji,alipiga magoti,akainua mikono kupigs dua,”Ewe Mungu,niepushe na balaa nyingine”.
    Safari ya Vuai kutoka katika majengo ya gereza ilikumbwa na mseto wa mawazo.Alipokuwa katika ujia uliomwelekeza katika barabara kuu,mambo mengi yalimpitikia mawazoni asipate jawabu.Hakujua kama wazazi wake wangali hai na kama bado walikuwa wanaishi katika nyumba ile ya kukodi kwa miaka hiyo kumi aliyokuwa jela”Je,nikiwakosa nitaenda wapi?Nitaanza wapi kuwatafuta ?”Mawazo haya yalifunguamifereji ya machozi,kasha ile ya makamasi.Balagha hiyo iiyomfikisha katika kituo cha magari ya uchukuzi kwa ule aliouona kuwa muda wa kufumba na kufumbua.Aliyafuta machozi yake haraka kwa kiganja kasha akaziba tundu la pua,tayari kupenga kamasi.Hata hivyo,kabla hajafanya hivyo ,nafsi yake ilimtahadharisha kuwa hatua hiyo ingekatiza uhuru aliopewa kwa kuchafua mazingira.Kwa hivyo akaghairi Akavuta ncha ya shati lake na kuitumia kama hankachifu kutimiza azma yake.
    Hapo kituoni,matatu iliyokuwa mbele ilikuwa wa watu wachache.Vuai akaingia na kukaaa upande wa kioo ambapo tafakuri nyingi zilimjia.Akakumbuka jinsi kesi yake ilivyoendeshwa kinyume kabisa na ukweli na hukumu kutoelewa kinyume cha haki.”Mimi Vuai,toto taa tangu kuzaliwa kwangu hata mdudu sijawahi kumponda kwa udole wangu,ndi sasa nije kusingiziwa kumpoka mtu uzima?Mungu wangu!Kwa nini dunia hii haina wema?Kwa nini wanaodaiwa kuwa wasomi hata wakapewa jukumu lakuwakilisha maslahi ya raia ndi wanaowadhulumu hao raia?Hivi,hata hakimu na tajriba yake aliamua kufuatilia zile poroj za wanaojiita majasusi?Angeahirisha hukumu yake ili kufanya uchunguzi zaid,bila shaka nisingepata mapig na dhuluma hizo zote.Kwa kweli hii ni dunia ya mwenye nguvu mpishe1”Vuai alijisemea
    1. Kwa nini Vuai alifungwa jela? (alama2)
    2. Kwa kurejelea kifungu ,eleza madhila yaliyomo kwenye asasi za kurekebishia tabia (alama 4)
    3. Onyesha kinaya kinachojitokeza kwenye kifungu hiki (alama 2)
    4. Ni mambo gani yaliyomtia Vuai machugachuga alipoachiliwa huru (alama 3)
    5. Vuai anaelekea kuwa na hulka gani?Fafanua kwa kurejelea kifungu (alama 2)
    6. Msamiati ufuatao una maana gani kwa mujibu wa kifungu (alama 2)
      1. Ombwe
      2. Mhemko (1×1)
  2. UFUPISHO
    Kufufua na kuendeleza uchumi wa taifa ni jambo linalotegemea bidii na ambalo huchukua muda mrefu.Ili kufufua na kuendeleza uchumi wanchi,mbinu zifuatazo zinafaa kuchukuliwa.
    Kwanza ni bora kutegemea raslimali iliyomo nchini kwani suruali ya kuazima haisitiri matako.Ni lazima tukome kutegemea misaada kutoka ng’ambo .Wahenga hawakuwa wendawazimu waliiposema kuwa mtegemea cha nduguye hufa maskini.
    Bidhaa zinazonunuliwa kutoka ng’ambo hugharimu serikali kiasi kikubwa sana cha fedha.Tukiyatosheleza mahitaji yetu kwa kutumia bidhaa zinazotayarishwa nchini,uchumi wetu utaimarika.Raslimali ya nchi hutokan na ardhi yetu ina rtuba katika sehemu nyinngi.Tuna mito,madini,maziwa misitu na madini mbalimbali kama vile dhahabu na aina zingine ammbazo hata hazijavumbuliwa bado.
    Wakenya wengi hawaithamini kazi ya ukulima.Ukuzaji wa vyakula kwao ni kama kazi ya kijungu jiko ambayo huachiwa wasio na tegemeo lingine maishani.Mwelekeo huu ukibadilisha na tuwe na wakulima wathaminiao ukulima,uchumi wa nchi utaboreshwa kwa kiwango kikubwa.Badala ya kukopa pesa nyingi aambazo huwa vigumu kulipa,nchi yetu inafaa iombe misaada.Jambo hili likitokea,wahisani wetu katika nchi za kigeni wataelewa kwani sisi tumo katika taifa ambalo halijastawi kiuchumi.Jambo la kudai malipo kwa kutoza riba kubwa hudhoofisha mno hali ya uchumi wa mataifa yanayendelea.Riba hutatiza mataifa yanayokopa jinsi kupe afanyavyo anapofyonza damu ya ndama bila huruma wala karaha.Kuwahimiza wananchi kujitegemea kwa kila njia ni jambo ambalo linaweza kuifaidi nchi yetu.Si lazima kila mtu ajiriwe ilia pate riziki.Sekta ya jua kali ni mfano mzuri wa kuigwa ili wananchi wajitegemee.Hali hii itahakikisha serikali haitataabika ikijaribu kuwaajiri watu kazi ambazo hazipatikni kwa urahisi.
    Hatua nyingine ni utulivu nchini .Nchi yoyote yenye rabsha miogoni mwa wananchi wake haiwezi kupiga hatua mbele kiuchumi .Utulivu huwapa wananchi nafasi ya kushughulikia wajibu wao wa ujenzi wa taifa. Michafuko ikiwepo,serikali hutumia pesa kununua zana za kivita kama vile bunduki za kutolea hewa ya machozi ili kukabiliana na sokomoko kila mara itokeapo.
    Viongozi ni lazima wawe mfano bora katika harakati za kuuboresha uchumi.Mti ukifa shinale na tanzuze hukauka.Viongozi wenye nyadhifa mbalimbali nchini huwa si mfano mizuri.Wengi wao hujiingiza kwenye lindi la ufisadi ili kujinufaisha binafsi.Jambo hili huwavunja mioyo kina yahe ambao hawana nafasi ya kufisidi wenzao.Uchumi wan chi hauwezi kuendeleza kwa njia hii.
    Kazi za viwango vya juu kama vile uhandisi,urubani, unahodha na uanasheria nyakati nyingi hufanywa na wageni kutoka ng'ambo.Watu hawa hupata malipo ya hali ya juu sana.Ni bora serikali ibadili hali ili wenyeji wachukue nyadhifa hizi za kazi na kiasi cha mishahara kipunguzwe kidogo-na hapo nchi yetu itafaidika kiuchumi.Kwa kununua hisa za makampuni ya nj ,serikali itaundeleza uchumi kwa vile itakuwa na kibali cha kufaidika kutokana na faida zinazopatikana kwenye mkampuni hayo.
    Maswali
    1. Eleza mambo yanayosaidia kuinua na kuendeleza uchumi (maneno 60-70) (alama 7,1 utiririko)
    2. Eleza mambo yanayokwamiza uchumi wan nchi . (maneno 60) (alama 6, 1 utiririko)
  3. MATUMIZI YA LUGHA
    1. Huku ukizingatia jinsi hewa inavyozuiliwa,ainisha sauti zifuatazo; (alama 2)
      1. /y/………………………………………………….
      2. /sh/………………………………………………
      3. /p/………………………………………………
      4. /ny/…………………………………………….
    2. Andika neno lenye muundo ufuatao ; (alama 2)
      1. irabu,irabu,irabu……
      2. irabu,konsonanti,konsonati,konsonati,irabu
    3. Ainisha mofimu katika maneno yafuatayo (alama 2)
      1. Mwanao
      2. azingatiaye
    4. Onyesha aina za vielezi katika sentensi zifuatazo; (alama 2)
      1. Barabara ndefu zaidi ilisakafiwa barabara
      2. Kiplagat alianza kula kifisi alipoambiwa asishike chakula hivi hivi (alama 1)
    5. Andika sentensi ifuatayo kwa ukubwa; (alama 2)
      Mwanamke huyu alibeba ndoo hizi hadi sokoni
    6. Tunga sentensi yenye muundo ufuatao; (alama 2)
      KN(RN+RH)+KT(t+V)
    7. Tunga sentensi ukitumia neno alikuwa kama;
      1. Kitenzi kishirikishi kikamilifu; (alama1)
      2. kitenzi kisaidizi; (alama 1)
    8. Andika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa; (alama 3)
      Mwanasiasa alisema,”Mkinipigia kura nitawajengea zahanati kabla ya mwisho wa mwaka huu”
    9. Nomino zifuatazo ziko katika ngeli gani; (alama 1)
      1. ufizi………………………………………………………………………………………………
      2. firigisi……………………………………………………………………………………………
    10. Andika sentensi ifuatayo katika wakati ujao hali timilifu Waziri anasoma hotuba yake; (alama 1)
    11. Andika sentensi ifuatayo katika hali kanushi; (alama 1)
      Nzige wengi walikuwa wanavamia maeneo hayo kabla ya serikali kuchukua hatua
    12. Bainisha kiima na yambwa katika sentensi ifuatayo; (alama 3)
      Mama alimpikia mgeni wetu nyama ya kuku.
    13. Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo; (alama 2)
      Mwalimu aliyetuzwa jana alifundisha shairi lililotungwa na Kezilahabi
    14. Tunga sentensi moja kutofuatisha maana ya daka na taka; (alama 2)
    15. Tunga sentensi mbili kuonyesha matumizi mawili ya kiambishi ka (alama 2)
    16. Chaganua sentensi ifutayo kwa njia ya mistari; (alama 4)
      Genge la wezi lilituvamia
    17. Bainisha virai katika sentensi ifuatayo; (alama 3)
      Pikipiki iliyonunuliwa jana iliharibika karibu na mto
    18. Eleza majukumu yas sentensi ifuatayo; (alama 1)
      Nipe kalamu yangu mara moja.
    19. Andika sentensi ifuatayo upya kwa kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari katika kauli zilizo mabanoni; (alama 2)
      Kazi hii imekuwa(tendea) ngumu sana lakini siwezi kufa(tendeshwa)moyo
    20. Taja methali inayoafiki maelezo yafuatayo; (alama 1)
      Mtu anayetegemewa katika jamii akiondoka wanaomtegemea huwa mashakani
  4. ISIMU JAMII(ALAMA 10)
    “Mwenye sikio amesikia.Usiwe kama mimi .Wapurukushe wote wakupotoshao.Fuata ruwaza ya wanaokujali .Kwangu nimejishika sikio baada ya laiti nyingi .Macho yamefumbuka.Usiseme nitazeekea huku.Lengo langu ni kuwahi uzamili na hata uzamifu.Kwani kuitwa profesa ni kosa?Niwafae wengine kimasomaso na kihali”
    1. Taja na kuthibitisha sajili ya mazugumzo haya; (alama 2)
    2. Tambua mazigira ambamo mazungumzo haya yanatokea; (alama 1)
    3. Eleza sifa zozote saba za lugha zilizotumika kwenya mazungumzo haya; (alama 7)

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. UFAHAMU
    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
    Macho makali ya Vuai yalipigwa na mwali mkai wa jua la asubuhi.Ilikuwa ndiyo mara ya kwanza kuuona mwanga halisi wa ombwe lijiitalo dunia tangu alipohukumiwa kifungo gerezani.Punde tu komeo la mlango wa seli lilipofunguliwa,ilimlazimu Vuai ayafumbe macho kabla ya kuyafumbua tena ili yazoee mabadiliko yake.
    Ilikuwa ndiyo siku ya Vuai kuachiliwa huru kutoka kwenye kifungo kirefu kilichoyapa macho yake mazoea ya gizaa la kaburi mle gerezani.Macho yake yalipokwishaizoea ile hali na kumhakikishia kuwa kila alichokuwa akikiona si kizuka ila uhalisia,alipiga hatua.Akatoka nje ya mlango wa seli kisha kwa kutoamini,akageuka nyuma kulitazama tena lile pango alimokuwa ametikwa katika muda huo wote.Akayafikicha macho kwa kutoamini huku machozi yakimdondoka asijue kama yalikuwa ya furaha au ya huzuni.Alipogeuka kuanza safari ya uhuru wake,macho yake yalikumbana na lengo la gereza.Hapo ,akasita kidogo,labda kuhakikisha kama kweli alikuwa huru.Bila shaka,hakuna askari wa gerez aliyemshikia bunduki au kumhanikizia sauti asimame.Walimtazama tu na kumpa tabasamu.
    Taratibu,Vuai aliendelea kupiga hatua.Mhemko aliokuwa nao kutokana hewa safi iliyompenya mapafuni uliufanya moyo wake upige kwa kasi.Ghafla ,tabasamu likapasua mashavuni pake.Akasita.Akainua pua yake iliyompa hakikisho kuwa fondogoo na uvundo wa esli haukuwa- naye tena.Ingawa mwili wake ulijaa mabaka ya uchafu na matambara yaliyouficha uchi wake kuvunda,hilo halikumkera tena.Kwa hivyo,akatia tena tabasamu .Lake kuu lilikuwa ni shukrani kwa kuepuka yale madhila ya joto na rundo la wafungwa.Na kama hilo halikutosha,aligeuka tena ili sasa kuliangalia lile gereza.Bila kutaraji,alipiga magoti,akainua mikono kupigs dua,”Ewe Mungu,niepushe na balaa nyingine”.
    Safari ya Vuai kutoka katika majengo ya gereza ilikumbwa na mseto wa mawazo.Alipokuwa katika ujia uliomwelekeza katika barabara kuu,mambo mengi yalimpitikia mawazoni asipate jawabu.Hakujua kama wazazi wake wangali hai na kama bado walikuwa wanaishi katika nyumba ile ya kukodi kwa miaka hiyo kumi aliyokuwa jela”Je,nikiwakosa nitaenda wapi?Nitaanza wapi kuwatafuta ?”Mawazo haya yalifunguamifereji ya machozi,kasha ile ya makamasi.Balagha hiyo iiyomfikisha katika kituo cha magari ya uchukuzi kwa ule aliouona kuwa muda wa kufumba na kufumbua.Aliyafuta machozi yake haraka kwa kiganja kasha akaziba tundu la pua,tayari kupenga kamasi.Hata hivyo,kabla hajafanya hivyo ,nafsi yake ilimtahadharisha kuwa hatua hiyo ingekatiza uhuru aliopewa kwa kuchafua mazingira.Kwa hivyo akaghairi Akavuta ncha ya shati lake na kuitumia kama hankachifu kutimiza azma yake.
    Hapo kituoni,matatu iliyokuwa mbele ilikuwa wa watu wachache.Vuai akaingia na kukaaa upande wa kioo ambapo tafakuri nyingi zilimjia.Akakumbuka jinsi kesi yake ilivyoendeshwa kinyume kabisa na ukweli na hukumu kutoelewa kinyume cha haki.”Mimi Vuai,toto taa tangu kuzaliwa kwangu hata mdudu sijawahi kumponda kwa udole wangu,ndi sasa nije kusingiziwa kumpoka mtu uzima?Mungu wangu!Kwa nini dunia hii haina wema?Kwa nini wanaodaiwa kuwa wasomi hata wakapewa jukumu lakuwakilisha maslahi ya raia ndi wanaowadhulumu hao raia?Hivi,hata hakimu na tajriba yake aliamua kufuatilia zile poroj za wanaojiita majasusi?Angeahirisha hukumu yake ili kufanya uchunguzi zaid,bila shaka nisingepata mapig na dhuluma hizo zote.Kwa kweli hii ni dunia ya mwenye nguvu mpishe1”Vuai alijisemea
    1. Kwa nini Vuai alifungwa jela? (alama2)
      Alisingiziwa kumuua mtu
    2. Kwa kurejelea kifungu ,eleza madhila yaliyomo kwenye asasi za kurekebishia tabia
      1. Wafugwa hudhulumiwa
      2. Mazingira yenye uvundo/hewa si safi
      3. Watuhawaogi
      4. Kwagiza
      5. Juakali
      6. Msongamano
    3. Onyesha kinaya kinachojitokeza kwenye kifungu hiki
      Wasomi ambao wamepewa majukumu ya kuwakilisha raia ndio wanaowadhulumu {Majasusi na mahakimu}
    4. Ni mambo gani yaliyomtia Vuai machugachuga alipoachiliwa huru
      1. Hakuamini alikuwa kweli ameeachiliwa huru
      2. Alihofia kuamriwa asimame
      3. Alihofia kushikiwa bunduki
    5. Vuai anaelekea kuwa na Hulka gani?Fafanua kwa kurejelea kifungu
      1. Mwema–Anasema hajawahi kumponda mdudu
      2. Mwadilifu–Hataki kuyachafua mazingira
      3. Mkweli–Anacheza kwa uwazi sauti ya wayonge
      4. Msalihina-kupiga magoti na kuomba Mungu amwepushe na balaa nyingine
    6. Msamiati ufuatao una maana gani kwa mujibu wa kifungu
      1. Ombwe-kitu kilichowazi
      2. Mhemko-hamu kubwa ya kufurahia kitu
  2. UFUPISHO
    Kufufua na kuendeleza uchumi wa taifa ni jambo linalotegemea bidii na ambalo huchukua muda mrefu.Ili kufufua na kuendeleza uchumi wanchi,mbinu zifuatazo zinafaa kuchukuliwa.
    Kwanza ni bora kutegemea raslimali iliyomo nchini kwani suruali ya kuazima haisitiri matako.Ni lazima tukome kutegemea misaada kutoka ng’ambo .Wahenga hawakuwa wendawazimu waliiposema kuwa mtegemea cha nduguye hufa maskini.
    Bidhaa zinazonunuliwa kutoka ng’ambo hugharimu serikali kiasi kikubwa sana cha fedha.Tukiyatosheleza mahitaji yetu kwa kutumia bidhaa zinazotayarishwa nchini,uchumi wetu utaimarika.Raslimali ya nchi hutokan na ardhi yetu ina rtuba katika sehemu nyinngi.Tuna mito,madini,maziwa misitu na madini mbalimbali kama vile dhahabu na aina zingine ammbazo hata hazijavumbuliwa bado.
    Wakenya wengi hawaithamini kazi ya ukulima.Ukuzaji wa vyakula kwao ni kama kazi ya kijungu jiko ambayo huachiwa wasio na tegemeo lingine maishani.Mwelekeo huu ukibadilisha na tuwe na wakulima wathaminiao ukulima,uchumi wa nchi utaboreshwa kwa kiwango kikubwa.Badala ya kukopa pesa nyingi aambazo huwa vigumu kulipa,nchi yetu inafaa iombe misaada.Jambo hili likitokea,wahisani wetu katika nchi za kigeni wataelewa kwani sisi tumo katika taifa ambalo halijastawi kiuchumi.Jambo la kudai malipo kwa kutoza riba kubwa hudhoofisha mno hali ya uchumi wa mataifa yanayendelea.Riba hutatiza mataifa yanayokopa jinsi kupe afanyavyo anapofyonza damu ya ndama bila huruma wala karaha.Kuwahimiza wananchi kujitegemea kwa kila njia ni jambo ambalo linaweza kuifaidi nchi yetu.Si lazima kila mtu ajiriwe ilia pate riziki.Sekta ya jua kali ni mfano mzuri wa kuigwa ili wananchi wajitegemee.Hali hii itahakikisha serikali haitataabika ikijaribu kuwaajiri watu kazi ambazo hazipatikni kwa urahisi.
    Hatua nyingine ni utulivu nchini .Nchi yoyote yenye rabsha miogoni mwa wananchi wake haiwezi kupiga hatua mbele kiuchumi .Utulivu huwapa wananchi nafasi ya kushughulikia wajibu wao wa ujenzi wa taifa. Michafuko ikiwepo,serikali hutumia pesa kununua zana za kivita kama vile bunduki za kutolea hewa ya machozi ili kukabiliana na sokomoko kila mara itokeapo.
    Viongozi ni lazima wawe mfano bora katika harakati za kuuboresha uchumi.Mti ukifa shinale na tanzuze hukauka.Viongozi wenye nyadhifa mbalimbali nchini huwa si mfano mizuri.Wengi wao hujiingiza kwenye lindi la ufisadi ili kujinufaisha binafsi.Jambo hili huwavunja mioyo kina yahe ambao hawana nafasi ya kufisidi wenzao.Uchumi wan chi hauwezi kuendeleza kwa njia hii.
    Kazi za viwango vya juu kama vile uhandisi,urubani, unahodha na uanasheria nyakati nyingi hufanywa na wageni kutoka ng'ambo.Watu hawa hupata malipo ya hali ya juu sana.Ni bora serikali ibadili hali ili wenyeji wachukue nyadhifa hizi za kazi na kiasi cha mishahara kipunguzwe kidogo-na hapo nchi yetu itafaidika kiuchumi.Kwa kununua hisa za makampuni ya nj ,serikali itaundeleza uchumi kwa vile itakuwa na kibali cha kufaidika kutokana na faida zinazopatikana kwenye mkampuni hayo.
    Maswali
    1. Eleza mambo yanayosaidia kuinua na kuendeleza uchumi (maneno 60-70)(alama 7,1 utiririko))
      1. Kutegemea rasli mali iliyo nchini
      2. Kutumia bidhaa zinazotayarishwa humunchini
      3. Kuthamini kazi ya kilimo
      4. Nchi ziombe misaada badala ya mikopo
      5. Watu wahimiziwe wajitegemee(wajiajiri)
      6. Kuwa na utulivu nchini
      7. Viogozi wawe mifano bora
      8. Wenyeji wapewe nyadhifa
      9. Serikali inunue hisa za nje
    2. Eleza mambo yanayokwamiza uchumi wan nchi
      (maneno 60)(alama 6,1 utiririko))
      1. Kutegemea misaada kutoka nje
      2. Nchi kununua bidhaa kutoka ng’ambo
      3. Wakenya kutothamini kazi za ukulima
      4. Kukopapesanyingi zenye riba ya juu
      5. Kutengemea kazi ya kuajiriwa
      6. Kazi/nyadhifa za juu kupewa wageni
      7. Viongozi kutokuwa mifano bora
  3. MATUMIZI YA LUGHA
    1. Huku ukizingatia jinsi hewa inavyozuiliwa,ainisha sauti zifuatazo;(alama 2)
      1. /y/.......... kiyeyusho
      2. /sh/……kikwamizo
      3. /h/ kikwamizo
      4. /ny/....... nazali/kipua/king’ong’o
    2. Andika neno lenye muundo ufuatao ;(alama 2)
      1. irabu,irabu,irabu................................................. aoa,aua aue
      2. irabu,konsonanti,konsonati,konsonati,irabu
        ……………………ombwe,imbwa,umbwa…………………
    3. Ainisha mofimu katika maneno yafuatayo
      1. mwanao Mw-ngeli
        an-mzizi
        o- umiliki
      2. azingatiaye
        a-nafsi ya tatu umoja
        zingati-mzizi
        a-kauli
        ye-kerejeshi
    4. Onyesha aina za vielezi katika sentensi zifuatazo;(alama 2)
      1. Barabara ndefu zaidi ilisakafiwa barabara
        zaidi-kielezi cha namna hali
        barabara- kielezi cha namna halisi
      2. Kiplagat alianza kula alipoambiwa asishike chakula hivi hivi
        kifisi- kielezi cha namna mfanano
        hivi hivi- kielezi cha namna vikariri
    5.  Andika sentensi ifuatayo kwa ukubwa;(alama 2)
      Mwanamke huyu alibeba ndoo hizi hadi sokoni
      …Janajike hili lilibeba madoo haya hadi sokoni.
    6. Tunga sentensi yenye muundo ufuatao;(alama 2)
      KN(RH+RH)+KT(t+V)
      Motto wa mama ni mrefu
    7. Tunga sentensi ukitumia neon alikuwa kama
      1. Kitenzi kishirikishi kikamilifu;(alama 1)
        Mama alikuwa
      2. kitenzi kisaidizi;(alama 1)
        Mtoto alikuwa analala sebuleni.
    8. Andika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa;(alama 3)
      Mwanasiasa alisema,”Mkinipigia kura nitawajengea zahanati kabla mwisho wa mwaka huu”
      Mwanasiasa alisema kuwa iwapo wangempigia kura angewajengea zahanati kabla mwisho wa mwaka huo.
    9. Nomino zifuatazo ziko katika ngeli gani;(alama 1)
      1. ufizi……U-ZI
      2. firigisi…I-ZI
    10. Andika sentensi ifuatayo katika wakati ujao hali timilifu
      Waziri anasoma hotuba yake;(alama 1)
      Waziri atakuwa amesoma hotuba.
    11. Andika sentensi ifuatayo katika hali kanushi;(alama 1)
      Nzige wengi walikuwa wanavamia maeneo hayo kabla ya serikali kuchukua hatua
      Nzige wengi hawakuwa wanavamia maeneo hayo kabala serikali kuchukua hatua.
    12. Bainisha kiima na yambwa katika sentensi ifuatayo;(alama 3)
      Mama alimpikia mgeni wetu nyama ya kuku
      Kiima-mama
      Mgeni wetu-yambwa tendewa Nyama ya kuku-Yambwa tendewa
    13. Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo;(alama 2)
      Mwalimu aliyetuzwa jana alifundisha shairi lililotungwa na Kezilahabi
      Mwalimu aliyetuzwa jana-kishazi tegemezi
      Alifundisha shairi lililotungwa na Kezilahabi -kishazi huru
      Alifundisha shairi- kishazi huru
      Lilotungwa na Kezilahabi-kishazi tegemezi
    14. Tunga sentensi moja kutofuatisha maana ya daka na taka;(alama 2)
      Daka-shika/kamata
      Taka-uchafu,kusudia/penda
    15. Tunga sentensi mbili kuonyesha matumizi mawili ya kiambishi ka
      Ka-amri Kaeni chini! Kamwambie aje.
      Ka-kitendokitafanyika wakati ujao,km.Atakayesoma,watakaoshiriki.
      Ka-wakati usiodhihirika ,km.Waziri kajiuzulu.
    16. Chaganua sentensi ifutayo kwa njia ya mistari;(alama 4)
      Genge la wezi lilituvamia
      S-KN+KT
      KN-N+KH/KV
      N-Genge
      KH-H+N/KV-V+N
      H/V-La
      N-wezi
      KT-T
      T-lilituvamia
    17. Bainisha virai katika sentensi ifuatayo;(alama 3)
      Pikipiki iliyonunuliwa jana iliharibika karibu na mto
      RN-pikipiki iliyonunuliwa jana
      RT-iliharibika karibu na mto
      RH-karibu na mto
    18. Eleza majukumu yas sentensi ifuatayo;(alama 1)
      Nipe kalamu yangu mara moja
      Amri
    19. Andika sentensi ifuatayo upya kwa kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari katika kauli zilizo mabanoni;(alama 2)
      Kazi hii imekuwa(tendea) ngumu sana lakini siwezi kufa(tendeshwa)moyo
      Kazi hii imeniwiangumu sana lakini siwezi kufishwamoyo.
    20. Taja methali inayoafiki maelezo yafuatayo;(alama 1)
      Mtu anayetegemewa katika jamii akiondoka wanaomtegemea huwa mashakani
      Mti mkuu ukigwa wana wandegehuyumba.
  4. ISIMU JAMII(ALAMA 10)
    “Mwenye sikio amesikia.Usiwe kama mimi .Wapurukushe wote wakupotoshao.Fuata ruwaza ya wanaokujali .Kwangu nimejishika sikio baada ya laity nyingi .Macho yamefumbuka.Usiseme nitazeekea huku.Lengo langu ni kuwahi uzamili na hata uzamifu.Kwani kuitwa profesa ni kosa?Niwafae wengine kimasomaso na kihali”
    1. Taja na kuthibitisha sajili ya mazugumzo haya
      Sajili ya mawaidha/ushauri/wosia/nasaha.
      Mzungumzaji anamtolea msikilizaji nasaha asifuate mkondo mbaya wa maisha aliyofuata
    2. Tambua mazigira ambamo mazungumzo haya yanatokea
      Shuleni/chuoni/taasisi ya elimu-anaiotoa nasaha hii kwa wenzake akiwa chuoni kwa sababu anasema wasidhani atazeeka huko,lengoni kupata shahada
    3. Eleza sifa zozote saba za lugha zilizotumika kwenya mazungumzo haya
      1. Lugha iliyojaa matumini-anawania kupata uzamifu
      2. Utohozi-profesa-professor
      3. Swali balagha-kwani kuitwa professor ni kosa
      4. Lugha ya kuonya-mwenye sikio amesikia
      5. Nahau-nimejishika sikio-nimejirekebisha
      6. Lugha sanifu-Kifungu kizima kimetumia lugha ipasavyo
      7. Lugha ya maelezo-wapurukushe wote wa kupotoshao fuata ruwaza ya wanaokujali
      8. Msemi–macho yamefumbika-amezinduka
      9. Matumizi ya msamiati wa taaluma ya kiusomi-uzamifu na profesa
      10. Matumizi ya sentensi fupi fupi-Usiwe kama mimi
      11. Lugha inayotumia taswira-anapotolea nasaha anasema usiwe kama mimi picha ya pengine jinsi alivyothurika inajitokeza akilini
      12. Lugha imejaa hekima–anasema fuata ruwaza ya wanaokujali(ushauri anatoa unaongozwa na busara kwa Yule hataki msikilizaji ahasirike)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Momaliche Joint Mock Exams 2021/2022.

Tap Here to Download for 50/-

Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students

Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest