Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - 2021 KCSE Eldoret Diocese Mock Exams

Share via Whatsapp

Maswali

MAAGIZO

  •  Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
  • Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
  • Kila insha isipungue maneno 400.
  • Kila insha ina alama 20.
  •  Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.

Maswali

  1. Lazima
    Kumekuwa na visa vingi vya utovu wa nidhamu shuleni mwenu. Ukiwa katibu wa viranja, andika kumbukumbu za mkutano uliojadili vyanzo vya utovu huo na suluhisho lake.
  2. Usafiri wa pikipiki za bodaboda una manufaa zaidi kuliko hasara. Jadili.
  3. Andika insha itakayodhihirisha maana ya methali ifuatayo:
    Mpiga ngumi ukuta huumiza mkonowe.
  4. Tunga kisa kitakachomalizia maneno yafuatayo:
    …nikamtazama Marina huku machozi yakinitiririka njia mbilimbili kutokana na majuto yaliyonijaa.

Mwongozo wa Kusahihisha

  1. SWALI LA KWANZA
    Hii ni insha ya kumbukumbu. Vipengele vya:
    1. Kimuundo vya utungo wa aina hii vidhihirike kama ifuatayo:
      1. Kichwa : Kionyeshe:
        • Kundi linalokutana
        • Mahali pa mkutano
        • Tarehe ya mkutano
        • Wakati wa mkutano
      2. Waliohudhuria- vyeo na nyadhifa zidhihirishwe
      3. Waliotuma udhuru
      4. Ambao hawakuhudhuria
      5. Waalikwa / katika mahudhurio/ waliohudhuria, bali si wanachama (si lazima)
      6. Ajenda za mkutano
      7. Kumbukumbu zenyewe
        • Utangulizi
        • Wasilisho la mwenyekiti
        • Kusomwa na kuthibitishwa kwa kumbukumbu za mkutano uliopita/uliotangulia
        • Yaliyoibuka kutokana na kumbukumbu hizo
        • Maswala yanayojadiliwa leo/ masuala mapya (kulingana na ajenda)
      8. Masuala mengineyo
      9. Hitimisho
        • Sahihi, jina la Mwenyekiti na tarehe
        • Sahihi , jina la katibu na tarehe
    2. Maudhui
      • Visa vya utovu wa nidhamu vyaweza kuwa kuchelewa,kutohudhuria shule,kupigana,ulevi,kutozingatia kanuni za shule na kadhalika.
      • Mtahiniwa adhihirishe majadiliano na uamuzi ulioafikiwa na viranja kuhusu vyanzo vya utovu wa nidhamu shuleni na Suluhisho lake. Baadhi ya hoja zitakazo jitokeza ni hizi:
        1. Vyanzo
          1. Matatizo ya kiuchumi
          2. Ukosefu wa malezi mema
          3. Ukosefu wa ushauri miongoni mwa vijana
          4. Usasa na matumizi ya teknolojia
          5. Haki za watoto kutetewa sana na mashirika mbalimbali
          6. Shinikizo la rika
          7. Matumizi ya dawa za kulevya
          8. Kuvunjika kwa ndoa/ kuwepo kwa mzazi mmoja
          9. Kuvunjika kwa mifumo ya kimaadili, ya kitamaduni
          10. Mtaala wa elimu wenye masomo mengi
          11. Msongo wa mawazo
          12. Kutokuweko na michezo na shughuli za vyama
          13. Ukosefu wa vielelezo vizuri k.m Watu hutukuza viongozi wasio na nidhamu
          14. Uongozi wa shule hafifu
          15. Wazazi kuwatetea wana wao wakikosa na kadhalika
        2. Suluhisho.
          1. Kuimarisha uchumi
          2. Wazazi kuhimizwa wawaelekeza wana wao
          3. Kuimarisha ushauri- nasaha shuleni
          4. Kudhibiti matumizi ya rununu miongoni mwa wanafunzi
          5. Serikali kubuni mwongozo mzuri wa adhabu shuleni
          6. Watoto kulelewa katika misingi ya kidini
          7. Vituo vya kurekebisha tabia viimarishwe
          8. Adhabu kali itolewe kwa watumiao dawa za kulevya
          9. Kuanzisha michezo na shughuli za vyama ziimarishwe
          10. Mfumo wa elimu ufanyiwe marekebisho ili umpe mwanafunzi nafasi ya kucheza na kupumzika
          11. Kuanzisha nafasi za wachungaji shuleni na kadhalika.
      • Tanbihi
        1. Mtahiniwa akiegemea katika vyanzo pekee bila suluhu, atuzwe alama C 8/20.
        2. Atakayetaja angalau suluhu moja achukuliwe ya kwamba amejibu swali kikamilifu
        3. Akikosa baadhi ya vipengee vya kimuundo achukuliwe kuwa amekosea kimuundo.
        4. Atakayeandika sura tofauti bali na ya kumbukumbu kwa mfano ,Barua rasmi , hotuba na kadhalika aondolewe alama 4S (sura) baada ya kuwekwa katika kiwango chake
  2. SWALI LA PILI
    • Hii ni insha ya mjadala ambapo lazima pawe na mtazamo wa pande mbili za swali ,yani faida na hasara
      1. FAIDA
        1. Bodaboda zimeleta ajira kwa watu wengi, ama kujiajiri au kuajiriwa
        2. Zimeimarisha hali ya maisha kwa wawekezaji na waendeshaji
        3. Zimeimarisha usafiri wa watu wa uchukuzi wa mizigo
        4. Zimeimarisha utawala kwani hata ma chifu huzitumia
        5. Zimeimarisha matumizi ya muda au wakati kwani huhitaji tu abiria mmoja
        6. Ni usafiri wa bei nafuu
        7. Huwafikisha watu haraka na kadhalika
      2. HASARA
        1. Zimesababisha ajali nyingi, vifo na ulemavu
        2. Husababisha matatizo ya kiafya kutokana na baridi kali
        3. Wanafunzi wengi huwacha shule ili kushiriki katika biashara hii
        4. Usafiri huu unahusishwa na jinai kama vile ubakaji, wizi na kadhalika
        5. Umesababisha mimba za mapema kwa wanafunzi
        6. Zinaleta uvunjaji sheria za trafiki na kadhalika
    • Tanbihi
      Mtahiniwa aweza:
      1. Kuwa na hoja chache za faida na nyingi za hasara-atakuwa amejibu swali kikamilifu.
      2. Kuwa na hoja nyingi za faida na chache za hasara-atakuwa amejibu swali kikamilifu
      3. Akiegemea tu upande mmoja yani faida au hasara pekee achukuliwe kuwa na upungufu wa kimaudhui na alama zake zisizidi kiwango cha C
      4. Akiwa na hoja za faida sawa na za hasara achukuliwe kuwa amejibu swali ila tu ana upungufu wa kimtindo
      5. Neno jadili linamaanisha kueleza kwa mapana na marefu.
  3. SWALI LA TATU
    • Hii ni insha ya methali ambapo mtahiniwa lazima abuni kisa cha kudhihirisha ukweli wa methali aliyopewa.
      1. MAANA
        • Mpiga ngumi- Mtu yeyote anayepinga/ anayeshindana/ anayemkosea adabu mtu mwingine anayemzidi kimadaraka,kiumri,kimaumbile n.k.
        • Kuumiza mkonowe ni kupata madhara/kutofaulu/kudhurika.
        • Anayepiga ngumi ukuta atajiumiza kwani atashibuka ngozi yake.
      2. MATUMIZI
        • Anayeshindana na anayemzidi kiuuwezo atajiumiza yeye mwenyewe
        • Kisa kinaweza kuafiki hali zifuatazo:
          1. Mwanafunzi anayempinga kiranja,aadhibiwe na mwalimu au hata afukuzwe shuleni kabisa.
          2. Mwanafunzi kumkosea mwalimu heshima apate adhabu kali na hata asimalize masomo yake.
          3. Mtoto kumkosea mzazi wake heshima akapoteza mwelekeo maishani hatimaye akaharibika kabisa.
          4. Mwanasiasa kumpinga rais baadaye akose baadhi ya vitu vizuri ambavyo rais anaweza kumpa kwa Mfano.kuwa mwanachama wa kamati fulani, kuwa waziri na kadhalika.
          5. Mwajiriwa kumkosea heshima mwajiri wake baadaye afutwe kazi.
          6. Timu ndogo kujigamba itaishinda timu kubwa na baadaye ishindwe vibaya sana.
          7. Nchi ndogo ijaribu kupigana na nchi yenye uwezo mkubwa kijeshi kisha ipigwe vibaya na kushindwa.
      3. TANBIHI
        • Lazima mtahiniwa atunge kisa kudhihirisha ukweli wa methali-asipotunga kisa na atoe tu mifano na maelezo, achukuliwe kuwa amepotoka kimaudhui na atuzwe D3/20
        • Kisa lazima kidhihirishe pande mbili za methali yani kupiga ngumi ukuta na kuumiza mkonowe.
        • Akiegemea upande mmoja tu atakua amepungukiwa kimaudhui na atuzwe kiwango cha C
        • Atakayetunga zaidi ya kisa kimoja amepungukiwa kimtindo na kiwango chake kisizidi C
  4. SWALI LA NNE
    • Hii ni insha ya mdokezo ambapo lazima mtahiniwa akamilishe kwa kifungu cha meneno aliyopewa.
    • Kisa chaweza kuafiki hali zifuatazo
      1. Mhusika (yeye) alimkosea Marina, jambo hili likasababisha Marina kuwa matatani hatimaye yeye akajuta kwa kosa hilo.
      2. Marina alitaka msaada wake, yeye hakumpa, Marina akupata kwingine na akafaulu maishani.Jambo hili linamletea majuto.
      3. Yawezekana Marina alitaka amsaidie lakini yeye akakataa, jambo hili linamfanya apate matatizo mengi na akajuta kwa nini hakuuchukua msaada wa Marina.
      4. Hali nyingine zozote zinazoweza kumletea mhusika majuto zitathminiwe.
    • TANBIHI
      1. Kisa lazima kimhusishe Marina na mtahiniwa-asipowahisisha, ana shida ya kimtindo.
      2. Lazima katika kisa aonyeshe hali itakayomsababishia majuto.
      3. Kisa lazima kimalizikie kwa kifungu cha maneno aliyopewa-asipomalizia au ayaweke mahali si pake achukuliwe kuwa na upungufu wa kimtindo.
      4. Akiongezea maneno baada ya kifungu alichopewa achukuliwe kuwa na upungufu wa kimtindo.
      5. Mtahini asome insha za watahiniwa kwa makini kisha awatuze alama kulingana na mwongozo wa kudumu ulio hapa chini.

MWONGOZO WA KUDUMU

UTANGULIZI.

Karatasi hii imedhamiria kutathmini uwezo wa mtahiniwa wa kuwasiliana na msomaji na kuwasilisha ujumbe kimaandishi,akizingatia mada aliyopewa. Mawasiliano haya yatategemea ukwasi wa lugha ya mtahiniwa, kwa mfano, kutunga sentensi sahihi zenye mtiririko mzuri kimawazo, lugha ya kuvutia na yenye mawazo asilia, ubunifu mwingi na hati nadhifu. Kwa kutegemea maagizo ya swali lenyewe na umahiri wa lugha, ni lazima kutilia mkazo mtindo, mada na uwezo wa mtahiniwa kufuata maagizo vilivyo. Mtahini lazima aisome insha yote huku akizingatia sarufi, hijai, hoja, msamiati na mtindo ili aweze kuikadiria kwa kurejelea viwango mbalimbali vilivyopendekezwa. Viwango vyenyewe ni A, B, C na D kutegemea uwezo wa mtahiniwa.

VIWANGO VYA KUTATHMINIA
Vielekezi hivi ndivyo vitakavyo mwezesha mtahini kumweka mtahiniwa katika viwango mbalimbali vya kiutendaji.

KIWANGO CHA D KWA JUMLA MAKI 01-05.

  1.  Insha haieleweki kwa vyovyote vile ama uwezo wa mtahiniwa wa kutumia lugha ni hafifu sana, hivi kwamba mtahini lazima afikirie kile mtahiniwa anachojaribu kuwasilisha.
  2. Mtahiniwa hana uwezo wa kutumia maneno ya Kiswahili kwa njia inayofaa.
  3. Lugha imevurugika, uakifishaji haufai na insha ina makosa ya kila aina.
  4. Kujitungia swali na kulijibu.
  5. Insha ya urefu wa robo ikadiriwe hapa.

NGAZI MBALIMBALI ZA KIWANGO CHA D.
D- (D YA CHINI) MAKI 01-02.

  1.  Insha haina mpangilio maalum na haieleweki kwa vyovyote vile.
  2.  Kujitungia swali tofauti na kulijibu.
  3. Kuandika kwa lugha isiyo Kiswahili au kuchanganya ndimi.
  4. Kunakili swali au maswali na kuyakariri.
  5. Kunakili swali au kichwa tu.

D WASTANI MAKI 03.

  1. Mtiririko wa mawazo haupo.
  2. Mtahiniwa amepotoka kimaudhui.
  3.  Matumizi ya lugha ni hafifu mno.
  4. Kuna makosa mengi ya kila aina.

D+ (D YA JUU) MAKI 04-05.

  1. Insha ya aina hii hukuwa na makosa mengi ya kila aina, lakini unaweza kutambua kile ambacho mtahiniwa anajaribu kuwasilisha.
  2. Hoja hazikuelezwa kikamilifu/ mada haikukuzwa vilivyo.
  3. Mtahiniwa hana uhakika wa matumizi ya lugha / anajaribu kutumia lugha ila hana hakika na matumizi ya vipengele vya lugha anavyoteua.
  4.  Mtahiniwa hujirudiarudia.
  5.  Insha itakayozingatia sura lakini ikose maudhui ikadiriwe hapa.

KIWANGO CHA C KWA JUMLA MAKI 06-10.

  1. Mtahiniwa anajaribu kuishughulikia mada japo hakuikuza na kuiendeleza vilivyo.
  2. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe kwa njia isiyovutia / hana ubunifu wa kutosha.
  3. Mtahiniwa anaakifisha sentensi vibaya.
  4. Mtiririko wa mawazo unaanza kujitokeza japo kwa njia hafifu.
  5. Insha ina makosa mengi ya sarufi, ya msamiati na ya tahajia (hijai).
  6. Insha yenye urefu wa nusu ikadiriwe hapa.

Ngazi mbalimbali za kiwango cha C
C- (C YA CHINI) MAKI 06-07.

  1. Mtahiniwa ana shida ya kuwasilisha na kutiririsha mawazo yake.
  2. Mtahiniwa hana msamiati wa kutosha wala miundo ya sentensi ifaayo.
  3. Mtahiniwa anafanya makosa mengi ya sarufi, ya hijai na ya msamiati na insha yake haieleweki kwa urahisi.

C WASTANI MAKI 08.

  1.  Mtahiniwa anawasilisha ujumbe lakini kwa njia hafifu.
  2. Dhana tofauti tofauti hazijitokezi wazi.
  3. Mtahiniwa hana ubunifu wa kutosha.
  4. Mtiririko wa mawazo ni hafifu na hana ufundi wa lugha unaofaa.
  5. Anajaribu kushughulikia mada aliyopewa.
  6. Mtahiniwa ana shida ya uakifishaji.
  7. Mtahiniwa anafanya makosa mengi ya sarufi, ya hijai na ya msamiati lakini bado insha inaeleweka.

C+ (C YA JUU) MAKI 09-10.

  1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri akizingatia mada lakini kwa njia isiyo na mvuto.
  2. Dhana tofauti tofauti zimejitokeza japo kwa njia hafifu.
  3. Kuna mtiririko wa mawazo japo hana ufundi wa lugha unaofaa.
  4. Misemo na methali zimetumika kwa njia hafifu.
  5.  Ana shida ya uakifishaji.
  6. Kuna makosa ya sarufi, ya msamiati na ya hijai yanayoathiri mtiririko wa mawazo.

KIWANGO CHA B KWA JUMLA MAKI 11-15

i) Mtahiniwa anaonyesha hali ya kuimudu lugha.
ii) Mtahiniwa anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi vizuri.
iii) Mtahiniwa ana uwezo wa kutumia lugha kwa ufasaha.
iv) Mada imekuzwa na kuendelezwa kikamilifu.
v) Insha ya urefu wa robo tatu ikadiriwe katika kiwango hiki.

Ngazi mbalimbali za kiwango cha B.
B- (B YA CHINI) MAKI 11-12

  1.  Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri kwa kueleza hoja tofauti tofauti akizingatia mada.
  2.  Mtahiniwa ana mtiririko mzuri wa mawazo.
  3. Mtahiniwa anatumia mifano michache ya msamiati unaovutia.
  4. Makosa yanadhihirika/ kiasi.

WASTANI MAKI 13

  1. Mtahiniwa anadhihirisha hali ya kuimudu lugha.
  2. Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika akizingatia mada.
  3. Mtahiniwa anateua na kutumia mifano michache ya msamiati mwafaka.
  4. Sarufi yake ni nzuri.
  5. Makosa ni machache.

B+ (B YA JUU) MAKI 14-15

  1. Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika na anajieleza waziwazi.
  2. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe kwa njia inayovutia na kwa urahisi akizingatia mada.
  3. Mtahiniwa ana mchanganyiko mzuri wa msamiati unaovutia.
  4. Sarufi yake ni nzuri.
  5. Uakifishaji wa sentensi zake ni mzuri.
  6. Makosa ni machache ya hapa na pale.

KIWANGO CHA A KWA JUMLA MAKI 16-20

  1. Mtahiniwa ana ubunifu wa mawazo yanayodhihirika na kutiririka akizingatia mada.
  2. Mtahiniwa anadhihirisha ujuzi wa lugha yenye mnato.
  3. Ana uwezo wa kutumia tamathali za usemi ili kutoa hisia zake kwa njia bora na kwa urahisi.
  4. Umbuji wake unadhihirisha ukomavu na ukakamavu wake kimawazo.
  5. Insha ina urefu kamili.

Ngazi mbalimbali za kiwango cha A

A- (A ya chini) maki 16-17

  1. Mtahiniwa anadhihirisha ukomavu wa lugha.
  2. Mawazo ya mtahiniwa yanadhirika na anaishughulikia mada.
  3. Ana mtiririko na muumano mzuri wa mawazo.
  4. Msamiati wake ni mzuri/mwafaka na unavutia.
  5. Sarufi yake ni nzuri.
  6. Anatumia miundo ya sentensi kiufundi
  7. Makosa ni machache yasiyokusudiwa.

A Wastani Maki 18

  1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri kulingana na mada.
  2. Anajieleza kikamilifu akitumia lugha yenye mnato.
  3. Anatoa hoja zilizokomaa.
  4. Anatumia msamiati wa hali ya juu na unaovutia Zaidi.
  5. Anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi kiufundi Zaidi.
  6. Makosa ni nadra kupatikana.

A+ (A ya juu) – Maki 19-20

  1. Mawazo yanadhihirika Zaidi na mada imeshughulikiwa vilivyo.
  2. Anajieleza kikamilifu akitumia lugha ya mnato Zaidi.
  3. Hoja zake zimekomaa na zinashawishi.
  4. Msamiati wake ni wa hali ya juu na unaovutia Zaidi.
  5. Sarufi yake ni nzuri Zaidi.
  6. Anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi kiufundi Zaidi.
  7. Makosa yote kwa jumla hayazidi matano.

Muhtasari wa Viwango mbalimbali.

Kiwango Ngazi Alama
A+
A
A-
19-20
18
16-17
B B+
B
B-
14-15
13
11-12
 C C+
C
C-
09-10
08
06-07
 D D+
D
D-
04-05
03
01-02

 
USAHIHISHAJI NA UTUNZAJI KWA JUMLA.
Ili kuikadiria insha ya mtahniwa vyema bila kuongozwa na mtazamo-nafsi, mtahini sharti aisome insha yote akizingatia vipengee muhimu. Vipengee hivi ni maudhui, msamiati, mtindo, sarufi na hijai.

MAUDHUI.

  1. Maudhui ni hoja au mambo yanayozungumziwa, kuelezewa au kuhadithiwa kwa mujibu wa mada iliyoteuliwa.
  2. Maudhui ndio hasa uti wa mgongo wa insha yoyote ile.
  3. Ubunifu wa mtahiniwa hukisiwa kwa kutathmini uzito wa maudhui yake kulingana na mada teule.

MSAMIATI.
Msamiati ni jumla ya maneno yatumiwayo katika lugha husika. Mtahiniwa anatarajiwa kutumia msamiati unaooana na mada teule. Kutegea ukwasi wa lugha alionao, mtahiniwa anatarajiwa kuikuza mada kwa kuifinyanga lugha kiufundi. Ni muhimu kuelewa kwamba kutokana na maendeleo na ukuaji wa teknolojia na mawasiliano, maneno mapya yanaibuka kila uchao.

MTINDO.
Mtindo unahusu mambo kama vile:

  • Matumizi yafaayo ya lugha kama vile :tamathali za usemi, kwa mfano methali,misemo,sitiari na kadhalika.
  • Matumizi mwafaka ya msamiati unaohusiana na mada teule/matumizi ya sajili mwafaka.
  • Namna mtahiniwa /mwandishi anavyowaumba wahusika wake, kwa mfano kwa kuwapa majina ya majazi,kuwaua na kadhalika.
  • Matumizi ya vipengele vya kimtindo kama vile mbinu rejeshi, udokezaji na sadfa.
  • Matumizi ya vipengele vya tanzu nyingine za kimandishi /kifasihi/kisanaa, kama vile kutumia barua katika insha ya masimulizi.

MUUNDO

  • Mpangilio wa kazi kiaya.
  • Mtiririko na mshikamano wa mawazo kiaya na katika insha nzima.
  • Hati nzuri na inayosomeka kwa urahisi.
  • Kuandika herufi vizuri kwa mfano Jj, Pp, Uu, Ww na kadhalika.
  • Sura ya insha.Asiyezingatia sura ya insha katika swali la kwanza aondolewe 4S baada ya kutuzwa.
  • Unadhifu wa kazi ya mtahiniwa.

SARUFI.
Sarufi ndio msingi wa lugha. Ufanisi wa mawasiliano hutegemea uwezo wa mtahiniwa wa kutunga sentensi sahihi zenye uwiano wa kisarufi. Mtahini ataonyesha makosa yote ya sarufi yaliyo katika insha anayosahihisha. Makosa ya sarufi huweza kutokea katika:

  1. Matumizi yasiyofaa ya alama za uakifishaji.
  2. Kutumia herufi kubwa na ndogo mahali pasipofaa.
  3. Matumizi yasiyofaa ya ngeli na viambishi, viunganishi, nyakati, hali, vihusiano na kadhalika.
  4. Mpangilio usiofaa wa maneno katika sentensi.
  5. Mnyambuliko usiofaa wa vitenzi na nomino.
  6. Kuacha neno linalohitajika au kuongeza neno lisilohitajika katika sentensi.

Matumizi yafuatayo ya herufi kubwa yazingatiwe:

  1. Mwanzo wa sentensi.
  2. Majina ya pekee.
    1. Majina ya mahali, miji, nchi, mataifa na kadhalika.
    2. Siku za juma, miezi n.k
    3. Mashirika, masomo, vitabu n.k
    4. Jina la Mungu.
    5. Majina ya kutambulisha hasa wanyama wa kufugwa, kwa mfano yale ya mbwa- Foksi, Jak, Popi, Simba na mengineyo.

MAKOSA YA HIJAI/TAHAJIA.
Haya ni makosa ya maendelezo. Mtahini anashauriwa asahihishe huku akiyaonyesha yanapotokea kwa mara ya kwanza tu. Makosa ya tahajia huweza kutokea katika:

  • Kutenganisha neno kwa mfano ‘aliye kuwa’
  • Kuunganisha maneno kwa mfano ‘kwasababu’
  • Kukata silabi visivyo afikapo pambizoni kama vile ‘ngan – o’.
  • Kuandika herufi isiyofaa kwa mfano ‘ongesa‘ badala ya ‘ongeza’
  • Kuacha herufi katika neno kwa mfano ‘aliekuja’ badala ya ‘aliyekuja’
  • Kuongeza herufi isiyohitajika kama vile ‘piya’ badala ya ‘pia’
  • Kuacha alama inayotarajiwa katika herufi kama vile j I .
  • Kukosa kuandika kistari cha kuendelezea neno afikiapo pambizoni au kukosa kukiandikia mahali pasipofaa.
  • Kuacha ritifaa au kuiandikia mahali pasipofaa, kwa mfano ngombe, ngom‘be, n‘gombe, ngo‘mbe n.k
  • Kuandika maneno kwa kifupi kama vile k.v, k.m, v.v, n.k na kadhalika.
  • Kuandika tarakimu kwa mfano 27-08-2010.

Alama za kusahihishia

==== Hupigwa chini ya sehemu ambapo kosa la sarufi limetokea kwa mara ya kwanza tu.

_______ Hupigwa chini ya sehemu au neon ambapo kosa la hijai limetokea kwa mara ya kwanza tu.
✓ Hutumiwa kuonyesha hoja inapokamilika pambizoni kushoto.

˄ Hutumiwa kuonyesha kuachwa kwa neno \ maneno.

✓ Hutumiwa kuonyesha msamiati bora. Alama hii huitwa juu ya neno lenyewe.

× Hutumiwa kuonyesha msamiati usiofaa. Alama hii hutiwa juu ya neno lenyewe.

Maelezo mafupi yanahitajika kuhusu tuzo lililotolewa. Kila ukurasa uwe na alama ya √ chini katikati ili kuthibitisha kuwa mtahini ameupitia ukurasa huo

UKADIRIAJI WA UREFU WA INSHA.
✓ Maneno 9 katika kila mstari – kurasa mbili
✓ Maneno 8 katika kila mstari – kurasa mbili na robo.
✓ Maneno 7 katika kila mstari – kurasa mbili na nusu.
✓ Maneno 6 katika kila mstari – kurasa tatu.
✓ Maneno 5 katika kila mstari – kurasa tatu na nusu.
✓ Maneno 4 katika kila mstari – kurasa nne na nusu.
✓ Maneno 3 katika kila mstari – kurasa sita.

Kufikia maneno 174 Insha robo
Maneno 175- 274 Insha nusu
Maneno 275 -374 Insha robo tatu
Maneno 375 na kuendelea Insha kamili

Mapendekezo kuhusu usahihishaji wa swali la kwanza.

  • Hili ni swali la lazima kwa kila mtahiniwa. Swali hili kwa kawaida ni la kiuamilifu. Ni muhimu mtahiniwa azingatie mahitaji / masharti ya uandishi wa utungo wa kiuamilifu ambao amepewa. Kwa mfano, ikiwa ni hotuba, vipengele vya kimuundo na kimtindo vya hotuba vizingatiwe. Hata hivyo ni muhimu ikumbukwe kwamba sura au muundo wa utungo wowote ule ni kiwasilishio tu cha masuala lengwa. Kwa hivyo ni muhimu mtahiniwa azingatie maudhui/ yaliyomo. Haitoshi kuufahamu muundo wa utungo. Maudhui hasa ndicho kiunzi cha utungo. Pamoja na maudhui na muundo vipengele vingine vya kimawasiliano kama vile uteuzi wa msamiati, mtiririrko na mshikamano wa mawazo sharti vizingatiwe.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - 2021 KCSE Eldoret Diocese Mock Exams.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest