- Utangulizi
- Sifa za Hadithi
- Sababu za Ngano Kutambwa Jioni/Usiku
- Majukumu ya Hadithi
- Sifa za Mtambaji/Mganaji Bora
- Aina za Hadithi
- Mambo ya Kuzingatia katika Uchambuzi wa Hadithi/Ngano
Utangulizi
- Masimulizi yanayotumia lugha ya mtiririko au nathari.
Sifa za Hadithi
- Hutumia ya lugha ya mtiririko au nathari-kueleza matukio moja kwa moja.
- Hurithishwa jamii kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
- Huwasilishwa mbele ya hadhira
- Hutambwa mahali maalum k.v. ndani ya nyumba, chini ya mti, uwanjani, n.k.
- Huweza kutokana na matukio halisi (kihistoria) au ya kubuni.
- Huwa na mafunzo fulani kwa jamii/hadhira.
- Hutumia wahusika wa aina tofauti k.v. nyumbani, wanyama, ndege, mazimwi, n.k.
- Hutumia aina nyingine za sanaa k.v nyimbo, methali, ushairi, n.k.
- Huwa na utendaji k.v. mtambaji kuiga fisi anavyokula.
- Aghalabu hutambwa jioni.
Sababu za Ngano Kutambwa Jioni/Usiku
- Ndio wakati watu walikuwa wamejumuika nyumbani baada ya kazi.
- Utambaji ulikuwa njia ya kupitisha wakati chakula kikingojewa.
- Wakati huu ulihakikisha mwanajamii hapotezi wakati wa kazi.
Majukumu ya Hadithi
- Kufunza maadili yaliyo nguzo kuu kwa wanajamii.
- Kukuza ujasiri wa kuzungumza hadharani.
- Kuburudisha baada ya kazi ya kutwa.
- Kukuza uwezo wa watoto wa kukumbuka ili kutamba baadaye.
- Kueleza asili ya mambo k.m visaviini, visasili na ngano za usuli.
- Kutahadharisha wanajamii dhidi ya kufanya mambo yasitofaa.
- Kuunganisha watu katika jamii wanapojumuika pamoja kusikiliza utambaji.
- Ngano za mtanziko hukuza uwezo wa kutathmini na kutoa uamuzi ufaao.
- Kukuza lugha hasa kwa hadhira ya watoto.
- Kuhifadhi na kuendeleza historia ya jamii k.v. mighani, tarihi, n.k.
- Kuelimisha hadhira kuhusu utamaduni wao.
- Njia ya kupokeza kizazi historia na utamaduni wa jamii.
Sifa za Mtambaji/Mganaji Bora
- Asiwe mwoga ili kuweza kuzungumza hadharani.
- Asiwe na haya ili kuweza kuzungumzia mambo ya aibu inapobidi.
- Awe na uelewa wa mazingira na masuala ibuka katika jamii ili kuweza kuwasilisha dhana zisizopatikana katika mazingira yake k.m. kutumia rais kuelezea dhana ya mfalme.
- Awe na ufahamu mpana wa lugha ili aweze kuitumia kwa uhodari na kuwasilisha kwa wepesi.
- Awe mchanganfu na mcheshi ili kunasa makini ya hadhira na kuzuia isikinai.
- Awe na ufahamu mpana wa utamaduni husika ili kuzuia kutumia maneno na ishara zinazoweza kuwaudhi au kupingana na imani za hadhira.
- Awe na uwezo wa kushirikisha hadhira k.v. kuimba, maswali ya balagha ili isikinai, n.k.
- Aweze kujua, matarajio, kiwango cha elimu na tajriba ya hadhira ili kuweza kubadilisha kwa kiwango kinachofaa.
- Awe na uwezo wa kuingiliana vizuri na hadhira ili aivutie.
- Awe na kumbukumbu nzuri ili usimulizi wake utiririke vizuri.
- Awe na uwezo wa kudramatisha ili kuonyesha picha fulani k.v. kuiga toni, sauti, na kiimbo kulingana na swala analowasilisha.
- Kubadilisha toni au kiimbo ili hadhira isikinai.
- Awe na ujuzi wa kutumia ishara za uso, mwili na miondoko kulingana na hali anayoigiza.
- Awe na ujuzi na ufasaha wa lugha ili kuwasilisha mawazo kwa njia mwafaka na inayovutia.
- Aweze kubadilisha toni na kiimbo kulingana na hali tofauti anazoigiza k.v. huzuni
- Awe na uwezo wa kushirikisha hadhira kwa nyimbo na maswali ya balagha ili kuondoa uchovu wa kutazama na kusikiliza.
- Awe na uwezo wa ufaraguzi/ kubadilisha utambaji wake papo hapo kutegemea hadhira yake na kutoa mifano inayofahamika kutoka katika mazingira ya hadhira.
- Awe na uwezo wa kutumia mtuo wa kidrama ili kuongeza taharuki, kusisitiza ujumbe na kuteka makini ya hadhira.
Aina za Hadithi
- Hadithi za Kubuni
- Hazisimulii matukio ya kweli bali ya kutungwa
- Hadithi za Kisalua/Kihistoria
- Zinazosimulia matukio yaliyowahi kutendwa na wahusika waliowahi kuishi.
- Huongezewa ubunifu ili kuvutia zaidi.
A. Hadithi za Kubuni
Ngano
- Hadithi zinazosimulia kisa chenye funzo na zenye wahusika aina ya binadamu, viumbe na vitu visivyo na uhai.
Sifa za Ngano
- Zina fomyula ya kuanzia/mwanzo maalum.
- Zina fomyula ya kumalizia/mwisho maalum.
- Zina wahusika aina mbalimbali.
- Zina matumizi ya nyimbo.
- Hutumia takriri (usambamba) ili kusisitiza k.m. zimwi likakimbia, likakimbia.
- Huwa na na maadili/mafunzo
- Hutumia maswali ya balagha kuongeza taharuki.
- Hutumia tanakali za sauti.
- Zina matumizi ya fantasia au matukio yanayokiuka uhalisi/mambo ya ajabu k.v. binadamu kuruka kama ndege, zimwi kumeza watu na baadaye kutapika wote, n.k.
Aina za Fomyula za Kuanzia/Mianzo Maalum
- Paukwa, Pakawa. Sahani. Ya mchele. Giza. La mwizi. Na kiboko je? Cha mtoto mrorofi…
- Hapo zamani za kale/za kongamawe…
- Ilitokea…
- Hadithi! Hadithi! Hadithi njoo…
- Kaondokea chenjangaa, kajenga nyumba kakaa, mwanangu mwanasiti, kijino kama chikichi, cha kujengea kikuta, na vilango vya kupita…
- Hapo jadi na jadudi…
Umuhimu wa Fomyula ya Kuanzia/Mwanzo maalum
- Kuvuta makini ya hadhira.
- Kumtambulisha mtambaji kwa hadhira.
- Kuashiria mwanzo wa hadithi.
- Kutoa hadhira kutoka ulimwengu halisi hadi ule wa hadithi.
Aina za Fomyula za Kumalizia/Miishio Maalum
- Hadithi inaishia hapo.
- Tangu siku hiyo…
- Wakaishi raha mustarehe.
- Maadili
Umuhimu wa Fomyula ya Kumalizia/Mwisho Maalum
- Kuashiria mwisho wa hadithi.
- Kutoa hadhira katika ulimwengu wa hadithi hadi ule halisi.
- Kumpisha/kumpa fursa mtambaji anayefuata.
- Kupisha shughuli inayofuata.
- Kutoa funzo la hadithi kwa muhtasari.
- Kupa hadhira nafasi ya kupumzika baada ya kuwa makini kwa muda.
Umuhimu wa Nyimbo katika Ngano
- Kushirikisha hadhira.
- Kusisimua hadhira na kuondoa ukinaifu
- Kuteka makini yao.
- Kuwasilisha mafunzo/maadili.
- Kutenganisha matukio katika hadithi.
- Kuburudisha hadhira.
- Kupunguzia hadhira mwemeo.
Umuhimu wa Tanakali za Sauti/Onomatopeya katika Ngano
- Kuongeza utamu.
- Kusaidia msomaji kupata picha kamili.
- Kusaidia kupata hisia halisi
Aina za Ngano
1. Hurafa
- Hadithi zenye wahusika wanyama na ndege.
- Hurafa za kijanja ni hadithi ambapo wanyama wadogo hutumia ujanja wa hali ya juu ili kujinasua na hali ngumu au mitego wanayotegewa.
Sifa
- Wahusika ni wanyama au na au ndege.
- Wanyama na ndege hupewa sifa za binadamu
- Ni kazi ya ubunifu.
- Hutoa mafunzo kwa njia ya kuchekesha na isiyoumiza.
- Huwa na ucheshi mwingi.
- Hutumia mbinu ya uhuishi.
- Huwa na sifa zinazohimizwa na zinazoshutumiwa.
- Ujanja au uongo hujitokeza katika hurafa za kijanja.
- Ushindi hujitokeza katika hurafa za kijanja.
Umuhimu
- Kutahadharisha watu dhidi ya kuwa wa danganyifu/kudanganyika kwa urahisi.
- Kuonyesha jinsi tabia ya udanganyifu inavyoweza kujitokeza na kuathiri watu.
- Hurafa za kijanja hufunza jinsi ya kupampana na hali ngumu.
2. Hekaya/Ngano za Kiayari
- Hadithi zinazomsawiri mhusika anayetumia ulaghai kupata matilaba yake kutoka kwa wengine (Abunuwasi).
Sifa
- Wahusika wakuu ni binadamu.
- Huwa na ubunifu mkubwa.
- Hustaajabisha na kuchekesha.
- Ujanja na uongo hujitokeza.
- Ushindi hujitokeza.
- Ni za kubuni.
Umuhimu
- Hutahadharisha watu dhidi ya kuhadaika kwa wepesi.
- Huonya dhidi ya matokeo yanayoweza kuwapata wanaojinyakulia mali kwa udanganyifu.
- Kuonya dhidi ya usaliti.
- Kukashifu viongozi dhalimu na matendo maovu.
- Kukejeli wanaotumia nguvu badala ya akili/hekima.
3. Visasili
- Hadithi zinazoeleza asili ya matukio fulani katika jamii k.m. kifo, jua, lugha, zilizala n.k.
Sifa
- Husimulia mambo ya kiimani na kidini.
- Huwa na misingi ya kihistoria.
- Hueleza asili ya matukio katika jamii.
- Wahusika ni wanyama na binadamu.
- Huwa na maadili.
- Hurithishwa kizazi hadi kingine.
Umuhimu
- Kueleza asili ya mambo kama vile kifo, utamaduni n.k.
- Kueleza utaratibu wa kutekeleza desturi k.v. mahari.
- Kuhalalisha baadhi ya mila na desturi za jamii k.v. ulipaji mahari, uabudu miti, n.k.
- Kukitisha mizizi imani fulani ya watu.
- Kupunguza athari za majanga kama vile kuhalalisha kifo.
- Kutambulisha jamii kwani kila jamii ina aina yake ya visasili.
- Kuhifadhi historia na utamaduni wa jamii
4. Ngano za usuli
- Hadithi zinazoeleza asili ya hali, tabia, mahusiano au wasifu. k.v. asili ya kuku kuchakura, asili ya kinyonga kwenda kwa tahadhari, n.k.
Sifa
- Wahusika ni wanyama na binadamu
- Ni kazi ya kubuni.
- Hueleza kuhusu asili ya sifa, tabia au hali.
- Hutumia mbinu ya uhuishi.
- Huwa na maadili.
Umuhimu
- Kueleza sababu ya tabia, hali au sifa Fulani.
- Kuonya dhidi ya tabia hasi kama vile ulafi.
5. Ngano za mazimwi
- Hadithi ambazo wahusika ni mazimwi.
Sifa
- Wahusika ni mazimwi
- Mazimwi huwakilisha sifa hasi za binadamu k.m ulafi, ukatili, uovu n.k.
- Hujaa uharibifu.
- Huwa na matumizi mengi ya fantasia.
- Kipengele cha safari hujitokeza k.v. kwenda nchi za mbali kutafuta suluhisho.
- Ushindi hujitokeza (mazimwi hushindwa).
- Ni kazi ya kubuni.
- Huwa na maadili.
- Mazimwi huwa na sifa zinazokiuka mipaka ya binadamu k.m. kinywa kisogoni, jicho moja kubwa, n.k.
Umuhimu
- Kukashifu tabia ya uovu, ulafi, na ukatili.
- Kutahadharisha dhidi ya kuwa na ulafi, ukatili n.k.
- Kutia moyo waliodhulumiwa kuwa waliowanyanyasa wataadhibiwa siku moja.
6. Ngano za Mashujaa
- Ambazo zinazohusu watu waliotenda matendo ya kishujaa katika jamii zao kama vile kuokoa jamii.
Sifa
- Kipengele cha motifu au kusafiri nchi za mbali, kupigana na mazimwi kuokoa jamii.
- Husawiri mapigano kati ya wema (lila) na ubaya (fira).
- Uovu huwakilishwa na mazimwi au viongozi dhalimu
- Hatimaye wema hushinda uovu kwa juhudi za mashujaa
- Ngano za mashujaa ni za kubuni ilhali katika mighani, mashujaa wanaaminiwa waliishi.
Umuhimu
- Kuhimiza uzalendo na ujasiri miongoni mwa vijana.
- Kuhimiza ujasiri miongoni mwa vijana.
- Kusifu mashujaa katika jamii
- Kuelimisha jamii kwa kuwapa maarifa ya kukabiliana na changamoto, inda na ila.
- Kuhimiza uzalendo kwa kuhimiza watu kuiga mashujaa na kupigania jamii.
- Kuonya dhidi ya matendo hasi k.v. ukatili.
- Kuhimiza watu kutokata tamaa
7. Ngano za mtanziko
- Hadithi ambapo mhusika hukabiliwa hali ngumu ya kuamua baina ya mambo wawili au zaidi yanayomkabili.
Sifa
- Wahusika ni wanyama au binadamu.
- Ni kazi ya kubuni.
- Mhusika hulazimika kufanya uteuzi mgumu.
- Hali mbili au zaidi zinazotatanisha huwepo.
Umuhimu
- Hutuerevusha jinsi ya kupambana na hali ngumu.
- Kuonya/kutahadharisha dhidi ya kujiponza.
- Kukuza uwezo wa kupima mambo na kuteua lililo muhimu.
- Kuonya dhidi ya kutenda bila kuwaza kwa kina.
8. Ngano za Kimafumbo
- Ambazo huwa na maana ya ndani/iliyofichika.
- Istiara
- Hadithi ambayo maana yake huwakilisha maana nyingine iliyofichika k.v. hurafa ambapo wanyama huwakilisha binadamu. - Mbazi
- Hadithi fupi inayotolewa inayotolewa kama mfano kumkanya au kumwelekeza mtu k.v. katika biblia.
- Istiara
B. Hadithi za Kisalua/Kihistoria
Mighani
- Hadithi za mashujaa/majagina wa jamii fulani k.m. Rwanda Magere wa Waluo, Fumo Liyongo wa Wapate, Koome Njue wa Wameru, Wangu wa Makeri wa Wakikuyu na Syokimau wa Wsakamba.
Sifa
- Huhusu mashujaa wa jamii fulani.
- Wahusika hupambana na hali ngumu inayosababishwa na maadui.
- Wahusika hupewa sifa na uwezo usiokuwa wa kawaida k.v. ukubwa wa ajabu, nguvu katika kivuli, nguvu katika nywele, kutoulika n.k.
- Wahusika hupigania haki za wanyonge.
- Mhusika hukomboa jamii yake dhidi ya maadui.
- Mhusika hufa kifo cha huzuni (tanzia) kwa kusalitiwa na mtu wa karibu k.v. mwanamke au jamaa zao.
- Mashujaa huuliwa kwa njia ya ajabu kama vile kunyolewa nywele, kivuli kuchomwa mkuki, kuchomwa shindano ya shaba kitovuni
- Mighani huzungumzia matukio ya kihistoria.
- Kuna tabia ya kupiga chuku matukio yaliyo hadithini.
- Mighani hurithishwa jamii kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
- Huchukuliwa na jamii kama hadithi zenye ukweli na jamii hujinasibisha na mighani hiyo.
- Husimulia mambo ya kiimani na kidini.
Umuhimu
- Kutambulisha jamii kwani kila jamii ina aina yake ya mighani.
- Kuhifadhi na kumbusha historia yajamii.
- Kusifu mashujaa katika jamii.
- Kuhimiza ujasiri miongoni mwa vijana.
- Kuelimisha jamii kwa kuwapa maarifa ya kukabiliana na adui au changamoto.
- Kukuza uzalendo kwa kuhimiza watu kuiga mashujaa na kupigania jamii.
- Kuonya dhidi ya matendo hasi kama vile usaliti.
- Kuhimiza watu kutokata tama.
Tofauti Kati ya Mighani na Visasili
mighani | visasili |
Husimulia kuhusu mashujaa. | Husimulia asili ya vitu. |
Husimulia historia ya jamii. | Husimulia mianzo ya vitu au mambo |
Wahusika wakuu ni majagina. | Wahusika ni k.v. binadamu, miungu, wanyama, n.k. |
Hueleza sifa za majagina. | Hueleza mianzo ya desturi. |
Visakale
- Masimulizi ya matukio yaliyotendeka zamani k.v. vita, majanga kama njaa na magonjwa na hamahama za jamii k.v. waisraeli kutoka misri.
Visaviini
- Hadithi zinazoeleza chimbuko la jamii Fulani
Mapisi
- Maelezo ya kihistoria yasiyo na ubunifu wowote k.v. chimbuko la kundi la wabantu kutoka Afrika ya Kati na kuenea sehemu mbalimbali za Afrika.
Tarihi
- Maelezo kuhusu matukio ya kihistoria kulingana na yalivyofuatana ki wakati
Kumbukumbu
- Maelezo ya kitawasifu kuhusu mtu au jamii inayotambulika kwa kutoa mchango fulani mkubwa.
Vipera Vingine vya Hadithi
Soga
- Hadithi fupi za kuchekesha zinazolenga kutania au kudhihaki.
Sifa
- Wahusika ni wa kubuni.
- Hutaja ukweli unaoumiza.
- Hutumia vichekesho kupunguza ukali wa dhihaka.
- Hutumia chuku kupita kiasi.
- Huhusu tukio moja.
- Ni fupi.
Umuhimu
- Kukashifu matendo hasi kwa njia ya ucheshi
- Kuonya na kutahadharisha dhidi ya matendo hasi k.v. ulaghai.
- Kufunza maadili.
- Kuburudisha kwa kuchekesha.
Vigano
- Hadithi fupi zinazosimulia kuhusu matendo mabaya katika jamii na wakati uo huo kuonya na kuelekeza dhidi yayo.
- Aghalabu huandamana na methali kwa lengo la kufafanua linalokusudiwa au kudhibitisha funzo la methali fulani.
Sifa
- Huwa vifupi.
- Husimulia kisa kimoja tu.
- Wahusika ni binadamu na wanyama.
- Hufunza maadili kutokana na methali.
Kisa
- Masimulizi mafupi yenye tukio moja lenye funzo kwa njia ya kufurahisha.
Mambo ya Kuzingatia katika Uchambuzi wa Hadithi/Ngano
- Kueleza aina ya ngano kwa kuzingatia wahusika na maudhui
- Ngano yaweza kuwa ya mazimwi na ya mashujaa kwa wakati mmoja.
- Ngano yaweza kuwa hurafa, ya usuli na ya kiayari.
- Kutaja wahusika
- Kufafanua sifa za wahusika wakuu
- Maadili/mafunzo yanayojitokeza katika hadithi
- Kubainisha sifa za ngano/hurafa/hekaya, n.k. zinazojitokeza katika hadithi.
- Kueleza umuhimu wa fomyula ya kuanzia/wimbo uliotumiwa katika hadithi.
- Kubainisha tamathali za usemi zilizotumiwa katika hadithi fulani
- Kuonyesha jinsi ngano inavyoshughulikia maudhui fulani.
- Kufafanua ufaafu wa methali fulani zilizotumiwa katika hadithi.
- Katika ngano ya mtanziko, ungekuwa mhusika mkuu ungefanya nini?
- Kubainisha matumizi ya mbinu ya fantasia
- Kufafanua maswala ibuka/maudhui yaliyoshughulikiwa k.m. usaliti, ujinga, ulaghai, n.k.
- Kuchanganua utungo kifani-ploti, wahusika, mbinu za lugha, fantasia, nyimbo, n.k.
- Kueleza majukumu ya hadithi.
Download Hadithi/Ngano - Tanzu za Fasihi Simulizi Kiswahili Notes.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students