Maigizo - Tanzu za Fasihi Simulizi Kiswahili Notes

Share via Whatsapp


Utangulizi

 • Utanzu wa fasihi simulizi unaoambatana na vitendo.
 • Sanaa ya mazungumzo yanayoambatana na vitendo.


Sifa za Maigizo

 1. Huwa na watendaji au waigizaji.
 2. Huwasilishwa mbele ya hadhira.
 3. Huwasilishwa mahali maalum k.v. ukumbini.
 4. Huwasilishwa kwa mazungumzo na matendo
 5. Waigizaji hujivika maleba yanayooana kutia uhai maigizo.
 6. Matayarisho kabambe hufanywa kabla ya maigizo.
 7. Huweza kuambatana na ngoma pamoja na uimbaji.
 8. Lugha ni yenye ufundi wa juu k.v. picha, mafumbo na tamathali.
 9. Huweza kuambatana na sherehe fulani ya kitamaduni k.v. jando, matanga, n.k.
 10. Huwasilishwa kwa lugha sahili.
 11. Hujaa taswira zinazoweza kutambulika na hadhira.


Umuhimu

 1. Kuburudisha wahusika na hadhira.
 2. Kukuza umoja na ushirikiano kwa kujumuisha watu pamoja.
 3. Kuimarisha uwezo wa kuzungumza hadharani-kupata ukakamavu jinsi mtu anapoendelea kuigiza.
 4. Kukuza umoja na ushirikiano watu wanapojumuika pamoja kutazama maigizo.
 5. Kukuza uwezo wa kukumbuka kwani mwigizaji huhitaji kukumbuka maneno halisi.
 6. Kukejeli kitendo kisichofaa/cha kijinga alichofanya mtu.
 7. Njia ya kipato/kuwatafutia riziki baadhi ya watu.
 8. Kutoa nafasi kwa watu kudhihirisha vipawa vyao.
 9. Kuonya na kutahadharisha watu dhidi ya kufaya mambo yasiyofaa.
 10. Kuelimisha watu wafahamu jambo fulani k.v. ukimwi, ufisadi, n.k.
 11. Kukosoa watu wanaofanya kinyume na matarajio ya jamii k.v. wivu, uchoyo, n.k.
 12. Kupitisha maarifa na amali za kijamii.


Ploti

 1. Utangulizi-kutambulisha mgogoro
 2. Ukuzaji wa mgogoro
 3. Kilele cha mgogoro
 4. Usuluhishaji wa mgogoro


Aina za Maigizo

 1. Maigizo Ya Kawaida
  • Maonyesho ya jadi yakiwa yameondolewa kwenye mazingira yake halisi.
 2. Sanaa ya Maonyesho
  • Matendo ya kweli yanayojitokeza katika jamii kulingana na mazingira yake halisi k.m. uganga, mazishi, unyago, ngoma, n.k.

Tofauti

Maigizo ya kawaida Sanaa ya maonyesho
Mazingira ya kuzua/maalum Hutumia mazingira halisi
Matukio ya kuiga Matukio halisi/ ya kila siku.
Huwa na wahusika na hadhira maalum Washiriki na waigizaji walio pia hadhira
Matumizi ya ukumbi na jukwaa maalum akuna haja ya ukumbi wala jukwaa
Hutumia maleba na vifaa vya kuzua mazingira maalum Hakuna vifaa maalum bali huwa mazingira yenyewe.
Hugawika katika maonyesho kutumia lugha kwa njia maalum Muundo wake hufululuza au hayajagawika katika maonyesho.
Wahusika hufanya mazoezi kabla ya igizo halisi Hawahitaji kufanya mazoezi kwani ni matukio ya kila siku.

Maigizo ya Kawaida

1. Michezo ya Kuigiza

 • Maigizo ambayo huwasilishwa na watendaji jukwaani mbele ya watu.

Sifa za Mwigizaji bora

 1. Awe jasiri ili aweze kuigiza mbele ya watu/hadharani.
 2. Awe na ubunifu ili aweze kufanya uigizaji kuvutia na kuondoa ukinaifu.
 3. Awe na ujuzi wa kutumia ishara za uso, mwili na miondoko kuonyesha picha ya hali anayoigiza.
 4. Awe na ujuzi na ufasaha wa lugha ili kuwasilisha mawazo kwa njia mwafaka na inayovutia.
 5. Aweze kubadilisha toni na kiimbo kulingana na hali tofauti anazoigiza k.v. huzuni.
 6. Awe na uwezo wa kushirikisha hadhira kwa maswali ya balagha ili kuondoa uchovu.
 7. Awe na uwezo wa ufaraguzi/ kubadilisha uigizaji wake papo hapo kutegemea hadhira yake na kutoa mifano inayofahamika kutoka katika mazingira ya hadhira.
 8. Awe anaelewa utamaduni wa hadhira yake ili asitumie maneno na ishara ambazo zinaudhi ama kukinzana na na imani zao.

2. Vichekesho

 • Michezo ya kuigiza inayokusudiwa kuzua kicheko ili kupitisha ujumbe k.m. vioja, vitimbi n.k.

Sifa

 1. Vichekesho huigizwa.
 2. Huwasilishwa kwa lugha sahili.
 3. Hujaa taswira zinazoweza kutambulika na hadhira.
 4. Hutumia mbinu ya kejeli, kunaya na tashtiti.
 5. Vichekesho huwa vifupi.
 6. Havihitaji uchambuzi wa ndani ili kuvielewa au kupata maana.

 

Jukumu

 1. Kuburudisha hadhira kwa kuchekesha.
 2. Kuelimisha kwa kuonyesha jambo la kijinga alilofanya mtu.
 3. Njia ya kuwapatia watu riziki.
 4. Hutumika katika hadithi kuifanya ivutie.
 5. Kukejeli kitendo fulani kisichofaa alichofanya mtu fulani.
 6. Kukashifu matendo hasi ya kijinga.
 7. Kuadilisha ama kutoa funzo fulani la tabia njema.

3. Ngonjera

 • Ngonjera inayoambatana na uigizaji/utendaji.

Sifa

 1. Kuweko kwa uigizaji/utendaji k.v. ishara za uso na mikono.
 2. Huwa na wahusika wawili au zaidi.
 3. Huendelezwa kwa njia ya wimbo.
 4. Mhusika mmoja huuliza jambo na mwingine hujibu.
 5. Wahusika kupingana mwanzoni.
 6. Wahusika hufikia uafikiano kufikia mwisho.

4. Michezo ya Watoto/Chekechea

 • Michezo inayoigizwa na watoto katika shughuli zao.

Aina

 1. Mchezo wa baba na mama
 2. Kuruka kamba
 3. Kujificha na kutafutana
 4. Kukimbiza kibaramwezi dhidi ya upepo ili kizunguke
 5. Mchezo wa baba na mama

Sifa

 1. Waigizaji ni watoto.
 2. Huhusu shughuli za kiuchumi na kitamaduni k.v. arusi, siasa, ukulima.
 3. Huandamana na nyimbo za watoto.
 4. Huwa na miondoko mingi k.v. kujificha, kuruka.
 5. Huwa na matumizi mengi ya takriri.
 6. Huchezwa popote.
 7. Huwa na kanuni fulani.
 8. Hukoma watoto wakichoka au wakikiuka kanuni

Umuhimu

 1. Kufunza watoto majukumu yao ya utu uzima.
 2. Kuwatanguliza watoto katika sanaa ya uigizaji.
 3. Kukuza ubunifu wa watoto kadiri wanapoendelea kuigiza.
 4. Kudumisha utamaduni wa jamii.
 5. Kuburudisha watoto.
 6. Kukuza stadi ya uigizaji miongoni mwa watoto.
 7. Kukuza utangamano miongoni mwa watoto kwa kuwajumuisha pamoja.
 8. Kukashifu matendo hasi ya watu wazima kwa watoto.
 9. Kuwapa watoto ukakamavu na kujiamini wakiwa wachanga.

5. Majigambo/vivugo

 • Uigizaji ambapo wahusika hujigamba kwa matendo ya kishujaa.

Mfano

Ndimi Kisoi, dume la ukoo mtukufu
Ulojipamba kwa mabingwa
Wachezaji hodari wa ngoma
Ndimi dume liloingia nyanjani
Makoo yakatetemeka
Yakang’ang’ania, ngozi kusakata nani
Kijiji kizima kilinijua
Wazee walilienzi
Wakamiminika kiamboni

Mabinti kunikabithi.

Sifa

 1. Aghalabu huambatana na ngoma.
 2. Hujitokeza, kujigamba na kisha kuendelea kucheza ngoma.
 3. Anayejigamba hubeba zana zake za vita kama vile mkuki na ngao kuonyesha aliyotenda.
 4. Anayejigamba huvaa maleba kuambatana na jambo analojisifia.

6. Utambaji

 • Usimulizi wa hadithi unaoambatana na uigizaji.
 • Huwa na matumizi ya vizuizui.

7. Mazingira

 • Uigizaji wa maumbile asilia yaliyozunguka jamii ya watu k.v. sauti za wanyama.
 • Kuna matumizi ya viziuzui, matawi n.k.

Sanaa ya Maonyesho

1. Ngoma

 • Uchezeshaji wa viungo vya mwili kuambatana na mdundo au miondoko maalum.

Aina

 1. Ngoma za wanawake
 2. Ngoma za tohara
 3. Ngoma za wanaume
 4. Ngoma za sherehe
 5. Ngoma za vijana
 6. Ngoma za unyago na jando
 7. Ngoma za wazee
 8. Ngoma za arusi
 9. Ngoma za kufukuza mapepo
 10. Ngoma za kuaga mwaka

Sifa

 1. Huandamana na muziki na ala ya muziki k.v. ngoma.
 2. Ngoma huchezewa mahali wazi na penye hadhira.
 3. Wachezaji huvaa maleba maalum kulingana na funzo linalonuiwa.
 4. Huwa na wahusika aina mbili; watendaji na watazamaji kwa wakati mmoja.
 5. Huweza kuandamana au kutoandamana na sherehe.
 6. Hutofautiana kulingana na jamii husika.

Umuhimu

 1. Kuburudisha kwa ufundi wa kucheza kwa kuzingatia miondoko.
 2. Kitambulisho cha jamii kwani kila moja ina aina yake ya ngoma.
 3. Kuhifadhi na kuendeleza tamaduni za jamii husika.
 4. Kukuza uzalendo kwa kuwafanya wanajamii kuionea fahari jamii yao.
 5. Kukuza umoja na ushirikiano kwa kujumuisha watu pamoja.
 6. Kuelimisha kwa kupitisha mafunzo na maarifa.

2. Matambiko

 • Utoaji wa kafara kwa Mungu, miungu, pepo au mizimu ili wasaidiwe kutatua shida, kutoa shukrani au kuomba radhi.

Sifa

 1. Hutolewa na wazee maarufu walioteuliwa.
 2. Hufanywa nahali maalum k.v. pangoni, mwituni, n.k.
 3. Huandamana na sala.
 4. Huandamana na utoaji kafara k.v. kuchinja mbuzi, n.k.
 5. Huandamana na maombi.

3. Maigizo Ya Uganga wa Ramli

Sifa

 1. Mganga hujitia kujua kwa hivyo vitendo vyake ni maigizo ya uganga wa madaktari.
 2. Mengi katika matendo ya mganga hayana mashiko.
 3. Aghalabu kafara hutolewa.
 4. Waganga wanapopiga bao huvaa maleba kama ngozi, vibuyu, pembe, n.k.
 5. Huweza kuwa na fimbo maalum.
 6. Lugha maalum anayodai kuitumia kuwasiliana na misimu.
 7. Mizimu humshauri mganga kuhusu ugonjwa na tiba inayofaa.
 8. Mganga humchanja mgonjwa na kumpa dawa za miti shamba.

Umuhimu

 1. Wakati mwingine mizizi ya mganga huponya.
 2. Huwapa watu matumaini hasa walio na magonjwa yasiyo na tiba.
 3. Dawa za mganga hupunga mashetani kwa wagonjwa wake.
 4. Hukutanisha ulimwengu wa mizimu na ulimwengu halisi.
 5. Waganga huburudisha wanapoigiza.

Hasara

 1. Mgonjwa huenda asipone kwani matendo mengi ya mganga ni ya kukisia.
 2. Dawa za uganga zaweza kumdhuru mtu.
 3. Malipo ni ghali na mtu hata aweza kufilisika akitafuta tiba ya ugonjwa usiopona.
 4. Mazingira ya uganga husheheni uchafu mwingi.
 5. Mgonjwa huridhika kwa muda mfupi halafu uhalisia hudhihirika.

4. Ngomezi

 • Uwasilishaji wa ujumbe kwa kupiga ngoma au zana nyingine ya kimziki.

Sifa

 1. Kuwepo kwa ngoma au ala nyingine kama panda.
 2. Mapigo ya ngoma hueleweka tu na jamii husika.
 3. Mapigo kufuata toni au ridhimu maalum kuwasilisha maneno fulani.
 4. Kuwepo kwa hadhira au wasikilizaji.
 5. Kueleweka kwa mapigo hayo na wanajamii husika pekee.
 6. Makini huhitajika ili kupata midundo.

Aina za ngomezi

 1. Taarifa
  • Huarifu kuhusu jambo k.m. msimu wa kuanza kutayarisha mashamba, kuitwa katika mkutano, kazi ya ujima n.k.
 2. Tahadhari
  • Hutoa tahadhari kuhusu mavamizi kama wizi wa mifugo, vita, majanga kama moto, mafuriko n.k.
 3. Uhusiano
  • Kuita watu kwa sherehe.

Umuhimu wa Ngomezi

 1. Njia ya mawasiliano kwa jamii zisizojua kusoma.
 2. Husaidia wanaokabiliwa na ugumu wa mawasiliano.
 3. Kuharakisha mawasiliano katika masafa mafupi.
 4. Kutoa taarifa kuhusu matukio fulani k.m. ndoa, kifo n.k.
 5. Husaidia kupitisha jumbe za dharura.
 6. Kutahadharisha wanajamii kuhusu tukio la hatari/dharura k.v. vita, gharika n.k.
 7. Kuficha siri kwa kuwasilisha ujumbe kwa njia isiyoeleweka.
 8. Kuhifadhi na kudumisha utamaduni wa jamii.
 9. Namna ya kudhihirisha ufundi wa kutumia zana kama ngoma.
 10. Kitambulisho cha jamii kwani kila jamii hupitisha ujumbe kwa mapigo tofauti.

Udhaifu wa Ngomezi

 • Si kila mtu anaweza kufasiri ujumbe unaokusudiwa.
 • Mapigo hayasikiki mbali na hivyo husikika na idadi dogo ya watu.
 • Mapigo yaweza kuhitilafiana na hivyo kufasiriwa kwa namna tofauti.

Ngomezi za kisasa

 1. Milio ya ambulensi, magari ya polisi na zimamoto.
 2. Kengele za kubisha hodi nyumbani zinazotumia umeme.
 3. Kengele shuleni, makanisani, n.k.
 4.  Toni za rununu zinazowakilisha aina mbalimbali za jumbe.
 5. Ving’ora vya kuashiria moto umetokea katika majumba ya horofa, benki, hospitalini, n.k.

Changamoto za Ngomezi katika Jamii ya Sasa

 1. Mwingiliano wa jamii mbalimbali unaosababisha kutofasiri ujumbe kwa njia moja inayotakikana.
 2. Viwanda na majumba marefu kusababisha kutosikika kwa sauti au milio ya ngoma.
 3. Njia nyingine za kisasa za mawasiliano zinazotumiwa kwa wingi na kwa wepesi.
 4. Uhaba wa zana kama baragumu na zumari zilizokuwa zinatumika.
 5. Mabadiliko ya maisha kuleta ubinafsi na kusababisha wengi kutoitikia wito wa vyombo.

5. Mivigha

 • Sherehe za kitamaduni ambazo hutokea katika kipindi fulani cha mwaka ambazo huonyesha mwanajamii ametoka kiwango kimoja hadi kingine.

Aina za Mivigha

 1. Sherehe za tohara
  • kutoka utotoni na kuingia utu uzimani.
 2. Sherehe za ndoa
  • kutoka kapera hadi kuoa
 3. Sherehe za kutambika
  • kutoa sadaka kwa Mungu, miungu, pepo au mizimu
 4. Sherehe kutawazwa kwa kiongozi
  • kutoka uraia na kuingia katika uongozi/utawala
 5. Shughuli za mazishi/matanga
  • kutoka uhai hadi ufu
 6. Sherehe za kuwapa watoto majina
 7. Sherehe za ulaji kiapo
 8. Shughuli za posa
 9.  ibada

Hatua

 1. Kutoa mtu rasmi kutoka kundi moja la wanajamii.
 2. Kumfundisha majukumu yanayohusiana na wadhifa mpya.
 3. Kumwingiza rasmi katika kundi jingine.

Sifa

 1. Huandamana na matendo au kanuni fulani (mivigha).
 2. Maleba maalum huvaliwa na wahusika kuwatofautisha na hadhira.
 3. Hufanyika kwa kutumia lugha maalum au kimyakimya.
 4. Kuna watu aina tatu: watendaji wanaoshiriki kuimba na kucheza, wale sherehe inafanyika kwa sababu yao na wanaoshuhudia tu.
 5. Huhusisha vitendo maalum kama kula viapo, kutoa kafara, kucheza ngoma, n.k.
 6. Huandamana na utoaji wa mawaidha.
 7. Uigizaji hujitokeza pale mwanajamii anaingizwa katika kundi fulani kutoka jingine.
 8. Huhusisha maombi.
 9. Hufanywa mahali maalum sherehe hiyo inapofanyika k.m. tambiko hufanywa porini au pangoni.
 10. Wahusika huweka ahadi za kutenda wema.
 11. Huwa na mpangilio wa shughuli kuanzia mwanzo, kati hadi mwisho.

 

Umuhimu

 1. Kuburudisha kwa vile baadhi ya mivigha huhusisha nyimbo, ngoma na uigizaji.
 2. Kutoa mafunzo ya utu uzima na elimu ya jadi.
 3. Mivigha ya mazishi huliwaza wafiwa.
 4. Kukuza utangamano miongoni mwa wanajamii kwa kuwajumuisha pamoja katika mivigha yao.
 5. Kuashiria mwanajamii ametoka kiwango kimoja cha maisha hadi kingine.
 6. Kujenga uhusiano bora kati ya jamii na miungu au mizimu.
 7. Kitambulisho cha jamii kwani kila moja ina aina yake ya mivigha.
 8. Kudumisha mila za jamii.
 9. Kuelimisha jinsi ya kukabiliana na changamoto maishani.
 10. Kuadilisha kwa kufunza tabia zinazokubalika na jamii k.v. uaminifu, utiifu, n.k.
 11. Kukashifu vitendo vya uoga.
 12. Kukuza uzalendo kwa kuhimiza wanajamii kuonea fahari tamaduni zao.
 13. Msingi wa wanajamii kujitambulisha na kuionea fahari jamii yao.

Hasara

 1. Baadhi ya mivigha huhatarisha afya na maisha k.v. kutahiri watoto wa kike.
 2. Baadhi ya sherehe hukiuka maadili kama vile kwa kuruhusu matusi hata kushiriki ngono.
 3. Baadhi yaweza kusababisha hasara kama vile kueneza ukimwi k.v. tohara kwa kisu kimoja.
 4. Huzua tofauti za kijinsia k.v. mwanamme kujiona bora kuliko mwanamke.
 5. Kuzua utabaka baina ya waliopashwa na wasiopashwa tohara.
 6. Baadhi ya mivigha hukiuka malengo ya kitaifa k.m. ukeketaji ni ukiukaji wa haki za binadamu
 7. Kunayo hujaza watu hofu k.v. kufukuza mapepo kunakohitaji kafara ya binadamu.
 8. Baadhi huhusisha ushirikina na hivyo kusababisha uhasama baina ya koo.
 9. Baadhi hugharimu kiasi kikubwa cha pesa na kuifilisi familia.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Maigizo - Tanzu za Fasihi Simulizi Kiswahili Notes.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest