Utangulizi - Kiswahili Insha Notes

Share via Whatsapp


Utangulizi

  • Insha ni utungo unaoundwa kwa mfululizo wa sentensi zinazozungumzia jambo, tukio au kitu fulani


Mambo ya Kuzingatia Katika Uandishi wa Insha

  1. Aina ya lugha - Zingatio kuu ni kufahamu aina ya lugha ambayo inapaswa kutumika katika kila aina ya insha hizi. Kwa mfano, katika uandishi wa ripoti au kumbukumbu, kiwango cha lugha kinachohitajika ni rasmi, bali si matumizi ya misamiati migumu migumu ambayo huenda ikawakanganya watahini.Kwa mwanafunzi, ni muhimu pia kuwa na uelewa wa kina (nje ya ufahamu wa anayosomeshwa darasani) kuhusu mazingira ambayo aina husika ya insha huwa inatokea.Kwa urejeleo, mazingira ya ripoti au kumbukumbu huwa ni rasmi na hayamhitaji kutumia msamiati mgumu kwani lengo kuu la aina hizi za insha ni kuwasilisha ujumbe fulani kwa hadhira lengwa, ambayo mara nyingi huwa inahitaji ufahamu wa haraka wa mada inayorejelewa.Hata hivyo, wanafunzi wengi huwa hawana ufahamu wa kiwango cha lugha au mazingira ambayo aina fulani ya insha inapaswa kuwepo, hali ambayo huwafanya kujikanganya kabisa, na kupoteza alama nyingi.Tatizo kuu kwa wengi huwa ni kutumia mabomu ya maneno ambayo hayapaswi kutumika kamwe katika aina hizi za insha.
  2. Urefu wa insha: Hakuna insha fupi katika mtihani wa Kiswahili. Ni mwelekeo potovu kudai kuwa baadhi ya insha kama barua rasmi, ratiba, ilani, memo, n.k ni insha fupifupi. Maagizo ya karatasi ya kwanza ya Kiswahili katika kiwango cha KCSE ni bayana: kila insha isipungue maneno mia nne (400). Kwa hivyo, huna budi kutumia ubunifu wa kiwango cha juu ili kuibua hoja za kutosha kuipa insha yako urefu unaotakikana. Unapokosa kuzingatia maagizo kuhusu urefu wa insha, unaadhibiwa alama nne (4) baada ya kutuzwa mara ya kwanza. Hata hivyo, ni muhimu sana kufahamu kuwa urefu huwiana na idadi ya hoja ulizoibua. Hivyo basi, insha yako ikiwa fupi sana, inaamaanisha kuwa umejadili hoja chache, na hapa utatuzwa kwa mara ya kwanza kulingana na idadi ya hoja zako, kisha uadhibiwe alama nne za kutozingatia urefu. Unashauriwa pia kuepuka kuandika insha ndefu kupita kiasi kwa kuwa huenda ukaadhibiwa kwa kati ya alama 2 hadi 3 baada ya utuzaji wa awali.
  3. Muundo wa insha-Insha za uamilifu huwa na sura au muundo mahususi ambao sharti uzingatiwe kikamilifu. Unapokosa kuzingatia agizo hili kwa kubadilisha au kutoshirikisha baadhi ya vipengele vya kimuundo vya insha husika unaadhibiwa kwa kupunguziwa hadi alama 5 baada ya utuzaji wa awali, lakini ikiwa utabadilisha muundo mzima wa insha (kwa mfano utumie muundo wa kumbukumbu katika insha ya ripoti), insha yako inazingatiwa kama iliyopotoka kabisa na hivyo inatuzwa alama 2 za bakshishi pekee.
  4. Njeo-kila swali la mtihani wa insha huulizwa kwa kuzingatia njeo au wakati mahususi (uliopo, uliopita, ujao, au hali timilifu). Kwa mfano, swali la pili la KCSE la mwaka 201 3 (keshatajwa), liliwasilishwa katika njeo ya hali timilifu na hivyo basi, mtahiniwa alihitajika kuzingatia hali timilifu kutunga insha yake. Unaposhindwa kuzingatia njeo mwafaka, unaadhibiwa kwa kupunguziwa lama 2 hadi 3 baada ya utuzaji wa awali.
  5. Uhusika/ nafsi: Maswali ya insha, hasa katika swali la nambari ya kwanza na ya pili, huwasilishwa kwa kuzingatia nafsi mahususi (ya kwanza, pili au tatu). Huna budi ila kuzingatia nafsi inayohitajika katika kuandika insha yako iwapo hutaki kupunguziwa alama kati ya 2 hadi 3 baada ya utuzaji wa awali. Aidha, epuka kutaja majina halisi ya viongozi, vyama vya kisiasa, dini na maswala mengine ambayo huzua mihemko na hisia kali miongoni mwa wananchi. Unashauriwa kubuni majina yako mwenyewe.
  6. Maadili: Hiki ni kigezo muhimu ambacho huhusisha matumizi ya lugha ya heshima, maudhui yanayotukuza amali za kijamii, kuwaheshimu watu wa matabaka yote yakiwemo yale ya kisiasa, kikabila na kidini. Insha yako itazingatiwa kama iliyopotoka kimaadili ikiwa itahusisha chuki za kikabila au kimbari, kuwatusi wanasiasa usiowapenda, kudunisha dini za watu wengine, kutaja majina halisi ya viongozi kiholela, na kuwadunisha watu wa jinsia fulani. Katika hali hii, utaadhibiwa kwa kupunguziwa kati ya alama 2 hadi 3 baada ya utuzaji wa awali. Labda, utafaidika ikiwa utazingatia wazo hili: kwamba unaweza kuwa unashutumu chama, dini, jinsia au kiongozi anayeshabikiwa sana na mwalimu atakayesahihisha insha yako. Utamtarajia mwalimu huyo kufumbia macho shutuma zako?
  7. Sarufi na hijai:
    • zingatia kanuni zote za kisarufi unapoandika sentensi za insha yako. Utaadhibiwa hadi alama 3 kwa makosa 6 au zaidi tofauti ya kisarufi. Katika hijai, huna budi ila kuendeleza maneno jinsi yanavyostahili. Hijai ni mtego mkubwa kwa watahiniwa kutokana na mazoea ya kufanya makosa yafuatayo:
      • Kutenganisha sehemu za neno moja kama vile: “nime kuadhibu”, “nime kusudia”, “alini juza”, na kadhalika.
      • Kuunganisha maneno ambayo hayafai kuunganishwa, kwa mfano: “kwaajili”, “kwasababu”, na kadhalika.
      • Kudondosha herufi fulani za neno, kwa mfano: “tebea” badala ya “tembea”, “doa” badala ya “ndoa”, “iba” badala ya “imba”, na kadhalika.
      • Udondoshaji wa herufi za neno Kutokana na kutokuwa mwangalifu au athari ya lugha ya mama, na ni kosa ambalo huenda likaibua neno jipya na kupoteza maana ya sentensi.
      • Kupachika herufi za ziada kwenye neno, kwa mfano: “mukutano” badala ya “mkutano”, “mutu” badala ya “mtu”.
      • Kubadilisha herufi fulani za neno, kwa mfano: “piga” badala ya “pika”, “rima” badala ya “lima”, “sigilisa” badala ya “sikiliza”.
    • Sarufi nayo sharti izingatiwe kwa kuzitilia maanani kanuni za sarufi ya Kiswahili. Huenda ukajipata matatani iwapo utazembea katika kutekeleza vipengele vifuatavyo vya sarufi:
      1. Kuakifisha sentensi zako ipasavyo.
      2. Kuzingatia upatanisho mwafaka wa kisarufi. Hapa, huna budi ila kuzingatia ngeli mwafaka katika upatanisho wako ili kuepuka kutunga sentensi kama: “Kondoo zake zitapelekwa malishoni.”
    • Siku hizi, yapo mazoea ya wazungumzaji wazembe wa Kiswahili kupatanisha takriban kila nomino kwa viambishi vya ngeli ya I-ZI. Si ajabu kuwasikia watu wakisema kauli kama: “viatu zangu”, “ng’ombe zenu”, “vitu zetu”, “vikombe zao”, “gari zetu”, “duka zake”, “vitabu zao”, n.k. Kama mtahiniwa, sharti ufahamu kuwa huu si upatanisho sahihi wa kisarufi na kuandika insha yako hivi ni kufanya makosa ya kisarufi.
    • Kuzingatia mpangilio mwafaka wa maneno katika sentensi zako. Uborongaji wa sarufi tunaoukubali katika fasihi kama uhuru wa kishairi sharti uepukwe katika kuandika insha yako. Kama mtahiniwa, huna uhuru au idhini ya kishairi ambayo waandishi wa kazi za fasihi hasa mashairi huwa nayo wanapotunga kazi zao.


Aina za Insha

  • Kuna aina tatu kuu za insha
    • Insha za kawaida
    • Tungo za kiuamilifu
    • Insha za Kisanii

Insha za Kawaida

  • Insha ya picha
  • Insha ya methali
  • Insha ya maelezo
  • Insha ya masimulizi
  • Insha ya mdokezo
  • Insha ya mjadala
  • Insha ya mawazo
  • Insha ya mazungumzo

Tungo za Kiuamilifu

  • Ambazo hutekeleza kazi maalum na huwa na muundo maalum.
    • Dayolojia
    • Mahojiano
    • Barua ya kirafiki
    • Barua Rasmi/Kwa Mhariri
    • Barua ya Gazetini Iliyohaririwa
    • Tahariri
    • Hotuba
    • Ratiba
    • Shajara
    • Onyo
    • Ilani
    • Matangazo
    • Maagizo/Maelekezo
    • Kujaza Fomu
    • Hojaji
    • Mialiko
    • Risala
    • Resipe
    • Orodha ya Mambo
    • Tahakiki
    • Meme
    • Barua za Mdahilisi/Pepe
    • Memo
    • Taarifa
    • Wasifu
    • Tawasifu
    • Wasifutaala/Wasifu Kazi
    • Kumbukumbu
    • Ripoti

 

 

Utungaji wa/insha za kisanii

  1. michezo ya kuigiza
  2. hadithi fupi
  3. mashairi
  4. mafumbo
  5. vitanza ndimi
Join our whatsapp group for latest updates

Download Utangulizi - Kiswahili Insha Notes.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Read 3334 times Last modified on Wednesday, 14 July 2021 07:54
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest