Utangulizi
- Insha inayosimulia kisa kinachoonyesha ukweli au uongo wa methali Fulani.
- Wazia methali nyingine za kutilia mkazo methali uliyopewa.
- Methali huwa na pande mbili na ni lazima insha ya methali izipe sehemu zote mbili uzito sawa.
- Upande mmoja hutoa wazo au pendekezo; na upande wa pili hutoa jibu, suluhisho au matokeo.
- Chukua kwa mfano, "Mpanda ngazi hushuka". Katika insha yako ni lazima utoe hoja za kutosha kuonyesha kwamba mhusika fulani kweli alipanda ngazi (k.v alipata cheo kikubwa, alijisifu n.k).
- Mwandishi pia anapaswa kutoa hoja za kutosha kuonyesha namna mhusika huyo aliposhuka (k.v akafutwa kazi,n.k).
- Kwa mara nyingi, wanafunzi huzingatia tu sehemu ya kwanza ya methali katika insha yote huku sehemu ya pili ikijitokeza katika aya ya mwisho pekee.
Muundo
- Kichwa
- Methali yenyewe
- Utangulizi
- Maana ya juu/wazi
- Maana ya ndani/batini
- Mwili
- Kisa kinachofungamana na methali cha kweli au cha kubuni
- Hitimisho
- Funzo/maadili
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download Insha ya Methali - Kiswahili Insha Notes.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students