
Utangulizi
- Wasifu ni insha inayosimulia maisha ya mtu fulani tangu kuzaliwa kwake, elimu yake, kazi, ujuzi wake n.k. Anayeandika wasifu ni tofauti na anayezungumziwa katika wasifu huo.
- Kuna aina tatu za wasifu:
- Wasifu wa Kawaida
- Tawasifu
- Wasifu-Kazi

Wasifu
- Wasifu wa kawaida ni masimulizi ya maisha ya mtu fulani yanayosimuliwa na mtu mwengine.
Kwa mfano, Wasifu Wa Siti Binti Saad ulioandikwa na Mwalimu Shaaban Robert.
Katika insha, mwanafunzi anawezaambiwa aandike wasifu wa:- mtu mashuhuri- anayejulikana kama vile Nelson Mandela, Julius Nyerere au Mzee Jomo Kenyatta n.k
- mtu yeyote anayemjua - kama vile mzazi, rafiki, somo(kielelezo), mwalimu wake n.k
- mtu wa kubuni - mwanafunzi anaweza kubuni mtu na asimulie maisha yake

Tawasifu
- Katika tawasifu, mwandishi huwa anasimulia maisha yake mwenyewe. Hivyo basi, tawasifu huandikwa na kusimuliwa katika nafsi ya kwanza.
- Katika insha, mwanafunzi anaweza ulizwa asimulie:
- maisha yake binafsi
- maisha yake, miaka kadhaa ijayo
- maisha ya mtu fulani kama yake binafsi k.m ajifanye kuwa Rais wa Tanzania, halafu asimulie maisha yake tangu kuzaliwa hadi alipo. k.m 'Umekuwa Rais wa nchi yako kwa muda wa miaka mitano, andika tawasifu kuhusu maisha yako itakayowasaidia wananchi wako kukuelewa vyema zaidi
- maisha ya mhusika wa kubuni, kama yake binafsi
Kwa mfano, katika riwaya ya Siku Njema, mhusika Kongowea Mswahili anaandika tawasifu akisimulia maisha yake tangu kuzaliwa, maisha ya nyumbani, elimu yake, kazi alizozifanya, maono yake n.k

Wasifu-Kazi/Wasifutaala
- Wasifu-kazi (Resume/Curriculum Vitae) ni stakabadhi inayotumiwa kuorodhesha mambo muhimu katika maisha ya mtu kama vile elimu, kazi, ujuzi n.k inayotumiwa sanasana katika kuomba kazi.
- Kinyume na wasifu na tawasifu ambazo hutumia lugha natharia (ya masimulizi), wasifu-kazi hutumia muundo fulani wa orodha na/au jedwali kuwasilisha mambo muhimu tu.
- Isitoshe, wasifu kazi huwa fupi - aghalabu ukurasa mmoja.
- Tunapoorodhesha mambo fulani katika wasifu, tunaanza na yale ya hivi karibuni hadi yale ya kitambo. Kwa mfano, anza na shule uliyosomea mwisho, iliyokuwa imetangulia hiyo n.k hadi shule uliyoenda kwanza.
Muundo wa Wasifu-Kazi
Katika wasifu-kazi unahitajika kuonyesha:
- Jina lako
- Jinsia
- Umri
- Hadhi ya ndoa
- Namna ya mawasiliano (simu, anwani, barua pepe)
- Elimu
- orodhesha shule zote ulizozisomea kutoka shule uliyosomea mwisho hadi shule ile uliyoihudhuria kwanza.
- katika kila shule, onyesha miaka uliyohudhuria k.m 1996-2000
- onyesha shahada (degrees) na diploma ulizozipata
- Kazi
- orodhesha kazi zote ulizozifanya kutoka kazi ya hivi karibuni hadi kazi ulizozifanya mwanzoni
- onyesha cheo ulichokuwa nacho katika kazi hiyo na majukumu yake
- onyesha kampuni au mahali ulipofanya kazi hiyo
- onyesha miaka ambayo ulikuwa katika kazi hiyo
- taja ujuzi au taaluma uliyoipata katika kazi hiyo
- Ujuzi / Taaluma - taja ujuzi maalumu ulionao, taaluma au talanta zozote zinazokufanya
- Mapato/Mafanikio/Tuzo - taja mafanikio yoyote au tuzo zozote ulizozipata katika maisha
- Mapendeleo/Uraibu - Nini kinakupendeza katika maisha? unapenda kutumiaje muda wako wa likizo usiokuwa wa kazi
- Maono ya Kazi - una maono gani katika kufanya kazi? ungependa kufanya nini?
- Warejelewa/Wahisani - hawa ni watu wa kuulizwa maswali ju yako ikiwa maelezo zaidi yatahitajika
Mfano wa Wasifutaala
WASIFUTAALA WANGU
MAELEZO BINAFSI
Jina : Farida Almasi Juma
Tarehe ya Kuzaliwa : 7-6-1971
Umri : miaka 22
Mahali pa kuzaliwa : Voi
Jinsia : mwanamke
Hadhi ya ndoa : Nimeolewa/kapera
Nambari ya kitambulisho : 12345678
Uraia : Mkenya
Lugha : Kiswahili, Kingereza, Kikuyu
Anwani ya kudumu : S.L.P. 1600, Voi
Barua pepe : This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Simu tamba : 9876543210
ELIMU
1993 - 1997: Chuo Kikuu cha Maseno (Shahada ya Uhasibu)
1988-1992: Shule ya upili ya Shimoni (Shahada ya KCSE)
1978-1987: Shule ya Msingi ya Umazi (shahada ya KCPE)
TAJRIBA
Mpaka sasa Mhasibu katika shule chekechea ya Mtakatifu Yohana
HABARI ZA ZIADA
URAIBU
- Kusoma vitabu vya sarufi na fasihi
- Kutembelea wajane, mayatima na wagonjwa
- Kuandika mashairi
AZIMIO LANGU
- Kupaa kitaaluma kwa kuendeleza masomo yangu hadi kiwango cha uzamifu
- Kuwa mhasibu bora zaidi nchini kwa matendo na kuwapa wananchi huduma za kufaa
WAREJELEWA
- Profesa Hassan Muoso,
Chuo Kikuu Kenyatta,
S.L.P.43844,
Nairobi. - Maimuna Njavu Mukota,
Shule ya Upili ya Alliance,
S.L.P. 1 234,
Nairobi.
Download Wasifu - Kiswahili Insha Notes.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students
Join our whatsapp group for latest updates