Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Kigumo Mocks 2021 Exams

Share via Whatsapp

Maagizo

  1. Andika jina lako na nambari yako ya mtihani
  2. Jibu maswali yote
  3. Majibu yote yaandikwe katika nafasi zilizoachwa katika kijitabu hiki cha maswali
  4. Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili
  5. Watahiniwa ni lazima wahakikishe kwamba kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo

Kwa matumizi ya mtahini pekee

SWALI

UPEO

ALAMA

UFAHAMU

15

 

UFUPISHO

15

 

MATUMIZI YA LUGHA

40

 

ISIMUJAMII

10

 

JUMLA

 

80

 


MASWALI

  1. UFAHAMU (ALAMA 15)
    Soma makala yafuatayo kwa makini kisha ujibu maswali yanayofuata
    Katika ofisi yake moja alimfuma mpiga taipu akimwambia karani mwingine, " kamnyoa yule yatima shilingi zake elfu mbili maskini" Lakini maongezi yalikatika kwa kutokeza Salma, na Salma hakutaka kuambiwa nani 'kinyozi'
    "Yupo?" aliuliza
    "Ke -keshaondoka, bibi," alibabaika mpiga taipu,
    "Kaelekea ofisi ya kati"
    Salma naye alielekea ofisi ya kati Huko pia mlango wa ofisi yake aliukuta umefungwa, na watu kadha wakimsubiri nje
    "Ameitwa na Mheshimiwa Waziri, tafadhali kaa umsubiri bibi," mwandishi alimwambia Salma, na Salma akapweteka juu ya kiti pamoja na wengine kumsubiri Karim
    "Je, umesikia mambo hayo?" Sauti ilinong'ona karibu na Salma, miongoni mwa watu waliokuwa wakisubiri na kumfanya Salma, atege sikio "Usifanye mzaha, mjomba wangu kafutwa shilingi mia nane ndipo alipopewa waraka wa nyumba yake Mzee mmoja jirani yangu kasumbuliwa we-e-e, hata na kutahamaki kupanguswa haki yake yote Na wangapi! Na wangapi! Basi na weye jihadhari"
    "Yatakwisha hayo! Hoja umoja wetu," mtu mmoja alieleza
    "A-a-a! Na hawa wanaodhulumiwa haki zao hufanyaje?" Sauti nyingine iliuliza
    "Wanalo?" Ilijibiwa "Labda humjui mtu huyu weye Mkuu wa Polisi nduguye kwa baba na pangu pakavu atapita wapi?"
    "Hakuna pa kupita," Salma alijibu rohoni mwake, yeye akiwa ndiye mwenye kumjua kuliko wote
    Hali kadhalika, Salma alijua kuwa pengine Karim hatarejea siku ile, na hata angerejea kauli yake isimgerudi nyuma Akiwaacha wale watu wakijadili juu ya haja iliyopo ya mabadiliko kwa nchi nzima iliyojaa dhuluma, Salma aliona afadhali aende tena kwa mama yake akamjaribu, ingawa tama haikuwapo
    Alipoingia Mbiju na gari lake jekundu, alimkuta mamake na birika mkononi akitilia maji bustani yake ya maua, kavaa kanzu nyeupe, ya kukokota, rangi ya bahari Alionesha mtu mzima tena, ingawa umaridadi ulimpa nuru
    "Karibu," alisema huku akizungusha birika katika shina la mwasumini "Leo pia hukumleta Karim"
    "Kashughulika na makazi yake," Salma alisema, mkono wake mmoja mfukoni na mwingine kashika mkoba wake uliokuwa ukining'inia chini ya ukwapa
    "Haijambo wewe unanikumbuka kuliko Samir huko Ulaya Hupita miezi sita hajaniletea barua, na anapoleta huwa kashikwa na haja Hiyo huko ndani ya barua yake, nimeipata jana, anataka shilingi elfu kumi Ikiwa barua zenyewe za kutaka mapesa tu amhonge huyo kafiri wake wa Kizungu, afadhali asiniletee," Bibi Adili alisema huku akikung'uta birika tupu chini ya shina la mwaridi Laiti angelizikata yeye mwenyewe ningempelekea japo nusu yake, lakini haja hizo zimeanza tangu kupambana na huyo kafiri wa Kizungu, anazitaka amhonge Mzungu wake, na sisi atufanye mahayawani kama yeye Sipeleki hata senti moja"
    Salma ambaye hapo kabla hakuwa na tamaa ya kupata mradi wake, sasa alivunja moyo kabisa kabisa kwa maneno ya mama yake Salma mwana mpenzi kuliko wote, atanyimwa alichotaka, seuze yeye Salma ambaye miezi miwili iliyopita alipewa shilingi elfu tatu
    (Unukuzi kutoka Nyota ya Rehema, SA Mohamed)
    1. Kwa kurejelea muktadha wa ofisini, fafanua aina sita za mabadiliko yaliyohitajika nchini kwa mujibu wa masimulizi haya (alama 6)
    2. Thibitisha kwamba Salma hakuwa mgeni katika ofisi ya kwanza aliyozuru (alama 4)
    3. 'Haijambo wewe unanikumbuka kuliko Samir'
      Fafanua jinsi kauli hii haikuwa na ukweli kwa kumrejelea Salma (alama 1)
      Taja mambo mawili yaliyomkatisha tamaa Salma kuhusu ufanisi wa ombi aliloendea kwa mama yake (alama 2)
    4. Kwa kuzingatia maana zilizo katika kifungu, andika vinyume vya matumizi ya lugha yafuatayo (alama 2)
      1. kutahamaki
      2. pangu pakavu
  2. UFUPISHO (alama 15)
    Mikopo ni njia mojawapo inayotumiwa na watu wengi kwa lengo la kujiendeleza na kujikuza kiuchumi na kwa hivyo kukopa ni jambo lisilokwepeka Mikopo inakubalika katika mataifa yote ya ulimwenguni na kwa sababu hiyo, mathalani, serikali nyingi hurasimisha ardhi za wananchi kwa ajili ya kutumika katika kukopa kutoka kwenye taasisi rasmi Kutokana na uzoefu, na labda urahisi wa namna fulani, watu wengi hupendelea mikopo isiyo rasmi inayopatikana kwenye mikoba na vikundi vya ushirika vya kuweka na kukopa
    Ikumbukwe kwamba haiwezekani kupata mkopo wa pesa kutoka kwenye taasisi rasmi bila kulipa deni Ili kuonyesha uaminifu wake na uhakika wa kurejesha fedha za wenyewe, mkopaji hulazimika kuweka rehani nyumba, hatimiliki ya ardhi, mshahara wake kama yuko kwenye ajira rasmi au mali yake nyingine yoyote kama gari Hii huwa ndiyo dhamana ya mkopo wake Dhamana hii husimama kama mbadala wa mkopo ili kulipia deni taraa mkopaji atashindwa kurudisha fedha alizokopa
    Watu wanaokopa mikopo wanaweza kukumbwa na hatari mbalimbali kutokana na kulemewa na kulipa madeni yao Kushindwa kusimamia biashara au miradi wanayoanzisha kwa mikopo hiyo ni miongoni mwa hatari hizo Wanaoshindwa kudhibiti biashara au miradi yao hukosa kupata fedha za kulipia madeni yao kwa sababu ya kuhasirika
    Aidha baadhi ya wakopaji huwekeza kwenye miradi isiyozalisha faida na kwa hivyo mtaji wao unamomonyoka na hata kumalizika kabisa na kwa hivyo wanapata hasara mara mbili ya kupoteza mtaji ambao ni mkopo na kukosa fedha za kulipia mkopo wao Kuna baadhi ya watu wanaoomba mikopo na kwenda kuitumia katika anasa na sherehe na kuishia kufilisika Hawa ni wakopaji ambao hukopa bila mipango Ole wao wanaoomba kwa njia hii!
    Kadhalika hatari nyingine ya kukosa kulipa madeni ni kwamba mali iliyowekwa rehani inaishia kwa mauzo ya kupigwa mnada Aghalabu, hii inapotokea, wanaoathirika moja kwa moja ni wakopaji, familia zao, wafanyikazi na jamii inayomtegemea mkopaji
    Kuna haja ya kutafuta namna ya kuwanusuru wakopaji kutokana na adha hii Wakopaji wanafaa kushirikishwa katika namma bora za kutumia fedha za mkopo kwa ajili ya uwekezaji endelevu Vilevile, wanafaa kuelimishwa kuhusu mbinu za kulipia madeni ili waepuke kufilisika Kwa mfano, wanaweza kushauriwa waanze kulipa mikopo mara tu biashara yao inapoanza kushika japo kidogo kidogo ilmuradi bandu bandu huisha gogo
    Baadhi ya wakopaji hushindwa kulipa madeni kwa sababu ya kukopa mikopo mikubwa sana kuliko uwezo wao wa kulipa Hawa ndio wanaostahili kutathminiwa kwa kina kabla ya mikopo yao kuidhinishwa kama njia mojawapo ya kuwaepusha kujiingiza katika jinamizi la kushindwa kulipa madeni Waama, baadhi ya mashirika ya kifedha hutoa mikopo kwa awamu kama namna ya kuwadhibiti wakopaji wasibadhiri fedha za mkopo Imedbibitishwa kwamba mbinu hii imewafaa baadhi ya wakopaji
    Kijumla basi, hamna shaka kwamba mikopo ni namna ya kujiendeleza kiuchumi na ni sharti watu wakumbatie uwajibikaji mbele ya mikopo ili kujiepusha kujiingiza katika lindi la ufukara
    1. Tumia maneno 50 kuandika mawazo yanayodokezwa katika aya mbili za kwanza (alama 5, 1 utiririko)
      Nakala chafu

      ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..

      Nakala safi

      ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..

    2. Kwa kurejelea aya za tatu hadi saba, eleza hatari zinazowakumba wakopaji na suluhisho kwa hatari zenyewe ( Maneno 75-85) (alama 8,1 utiririko)
      Nakala chafu

      ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..
      Nakala safi

      ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..

  3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
    1. Andika ufanano mmoja kati ya sauti zifuatazo (alama 2)
      1. /v/ na /th/
      2. /t/ na /l/
      3. /k/ na /f/
      4. /m/ na /z/
    2. Andika maneno yenye miundo ifuatayo (alama 2)
      1. Konsonanti, konsonanti, irabu, irabu
      2. Konsonanti, irabu, konsonanti, konsonanti, irabu
    3. Andika neno lenye mofimu zifuatazo: (alama 2)
      Kikanushi cha nafsi ya kwanza umoja, hali timilifu, yambwa, mzizi na kiishio
    4. Andika sentensi ifuatayo katika hali ya wingi (alama 1)
      Wembe alionunua kwenye duka umemsaidia kukata ukucha
    5. Geuza sentensi ifuatayo katika hali ya ukubwa (alama 1)
      Ng'ombe hawa na wale walivuka mto huo kwa utaratibu
    6. Andika sentensi zifuatazo upya kulingana na maagizo (alama 3)
      1. Mwanafunzi aliadhibiwa kwa kuwa alikosea mwalimu
        (Geuza maneno yaliyopigiwa mstari kuwa nomino)
      2. Nguo zilinunuliwa juzi Nguo ziliuzwa kwa bei ghali
        (Unganisha kuunda sentensi changamano)
      3. Mapambano baina ya mwanadamu na mazingira yalizua fasihi (Anza kwa: Fasihi)
    7. Tunga sentensi yenye kishazi tegemezi ambacho ni; (alama 3)
      1. kivumishi
      2. kiunganishi
      3. cha masharti
    8. Tunga senstensi moja yenye nomino katika ngeli ya U-I na kivumishi cha idadi(alama 1)
    9. Ainisha maneno katika sentensi ifuatayo (alama 3)
      Sahani tano safi zitatumika katika sherehe
    10. Geuza sentensi ifuatayo iwe katika hali ya mazoea (alama 1)
      Kisu kinachonolewa ndicho kinachopata
    11. Eleza matumizi ya 'kwa' katika senstensi ifuatayo (alama 3)
      Moja kwa tano ya watu waliosafiri kwa gari la moshi walikula wali kwa mchuzi
    12. Akifisha sentensi ifuatayo (alama 3)
      kahindi alipanda matatu nambari saba kisha akamuuliza dereva gari hili litanifikisha ukunda
    13. Kwa kutumia kitenzi kilicho katika mabano geuza sentensi iwe katika kauli uliyopewa (alama 1)
      Mgonjwa huyu hawezi chakula mpaka apate fahamu (pa-tendeka)
    14. Tunga sentensi yenye muundo ufuatao (alama 2)
      KN (N + RH) + KT (t + E)
    15. Nyooka ni kwa pinda,______________ni kwa dhahiri, na ____________ ni kwa hakika (alama 2)
    16. Tunga sentensi moja kutofautisha maana ya kasi na kazi (alama 2)
    17. Kanusha sentensi ifuatayo (alama 2) Viongozi wetu wazindukapo tutaacha kudhulumiwa na mataifa ya kimagharibi
    18. Ainisha yambwa katika sentensi ifuatayo (alama 3) Mwalimu aliwanunulia zawadi nzuri kwa shilingi elfu kumi
    19. Onyesha kwa kutumia sentensi mbili jinsi neno shuleni linaweza kuwa nomino na kielezi (alama 2)
    20. Yakinisha katika umoja (alama 1)
      Msipokuwa wenye bidii hamtayapata mafanikio maishani
  4. ISIMUJAMII (alama 10)
    Soma kifungu kifuatacho halafu ujibu maswali
    "Baada ya mjadala mrefu kuhusu mswada huu na kuzingatia sheria za bunge hili tukufu, kifungu cha 4, kipengele cha 6, ibara ya 3, ndugu zangu ningependa kutangaza kupitishwa kwa mswada huu na sasa utawasilishwa kwa rais kusubiri sahihi yake Kupitishwa kwa mswada huu kwa kauli moja ni tukio la kihistoria kwa bunge hili Tutaweza kufikia the two third rule"
    1. Sifa mbalimbali za sajili ya bunge zinadhihirika katika kifungu hiki Andika sifa zozote tano huku ukitoa mifano mwafaka (alama 5)
    2. Fafanua vipengele vingine vitano vya mitindo ya mawasiliano ambayo mbunge angetumia katika kufanikisha mawasiliano yake (alama 5)


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA 

  1. UFAHAMU
    1. Mabadiliko yaliyohitajika
      1. Mayatima kunyanyaswa kwa kunyang'anywa pesa.
      2. Kufunga milango ya ofisi za umma
      3. Kuwepo kwa foleni ndefu za watu wanaosubiri kuhudumiwa katika ofisi za umma
      4. Wanaostahili kuwahudumia raia kutokuwepo ofisini ili kuwahudumia.
      5. Kutoa rushwa/mlungura ili kutimiziwa haki yako.
      6. Wananchi kunyang'anywa/kuhiniwa haki zao.
      7. Mapendeleo/ubaguzi katika uajiri, kuajiri watu kwa kuangalia uhusiano na kujuana.
        (hoja chanya au hasi zikubaliwe) hoja 6 x 1 = 6
    2. Salma hakuwa mgeni ofisini hapo kwa sababu zifuatazo.
      1. Alipofika ofisini mazungumzo baina ya taipu na karani yalikatika ghafla kwani walimjua
      2. Haulizwi jina na mpiga taipu anapofika ofisini.
      3. Anapoulizwa kwa neno moja ‘yupo’ anajibiwa kwa kuambiwa kuwa ameondoka. Hamtaji mhusika.
      4. Mpiga taipu anamjibu akibabaika kwa sababu anamjua Salma ni nani.4 x 1=4
    3. Ziara za Salma Mbiju (kwa mamake) hazikuwa na lengo la kumjulia hali bali kumtaka mamake ampe msaada/pesa. 1x1=1
    4.                  
      1. Samir, ambaye alikuwa mtoto mpendwa, hangetumiwa chochote na mamake seuze yeye?
      2. Wiki mbili zilizopita alikuwa amefika hapo na kupewa shilingi elfu tatu kwa hivyo hakutarajia kupewa chochote. 2x1=2
    5. Vinyume vya;
      1. kutahamaki – kutumia ; kusahau
      2. pangu pakavu –matajiri; wakwasi. 2x1=2
  2. UFUPISHO ( ALAMA 15)
    1.                                
      1. Mikopo hutumiwa na watu wengi ili kujiendeleza kiuchumi.
      2. Mikopo inakubalika kote ulimwenguni
      3. Serikali nyingi hurasimisha ardhi za wananchi ili kutumika kukopa kutoka kwenye taasisi rasmi.
      4. Watu wengi hupendelea mikopo isiyo rasmi.
      5. Haiwezekani kukopa kutoka kwenye taasisi rasmi bila kulipa deni.
      6. Wakopaji hutumia mali yao kama rehani wanapokopa.
      7. Dhamana husimama kama mbadala wa mkopo. ( zozote 5 x 1=5)
    2. Hatari
      1. Hushindwa kusimamia biashara/ miradi wanayoanzisha kwa mikopo.
      2. Hawa hukosa kupata pesa za kulipia madeni kwa kuhasirika.
      3. Baadhi huwekeza kwenye miradi isiyozalisha faida na kupoteza kila kitu.
      4. Wengine hutumia mikopo katika anasa na kufilisika.
      5. Mali iliyowekwa rehani huuzwa (hupigwa mnada)
        Suluhisho
      6. Wakopaji wanafaa kushirikishwa katika namna bora za kutumia fedha za mkopo kwa ajili ya uwekezaji endelevu.
      7. Wanafaa kuelimishwa kuhusu mbinu za kulipa madeni ili waepuke kufilisika.
      8. Wakopaji wanastahili kutathminiwa kwa kina kabla ya mikopo yao kuidhinishwa.
      9. Mashirika yanweza kutoa mikopo kwa awamu ili kuwadhibiti wakopaji wabadhirifu.
        Hoja za kuonyesha hatari 4 x 1=4
        Hoja za kuonyesha suluhisho 4 x1
        M a -5
        b -8
        utiririko -2
        15
  3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
    1.                      
      1. vikwamizo
      2. Hutamkiwa kwenye ufizi/masine
      3. sauti sighuna
      4. sauti ghuna ½ x 4=2
    2.                          
      1. ngao , nguo
      2. tumwa, temwa, lengwa, pendwa, chapwa
        (kadiria jibu la mtahiniwa) 2 x 1=2
    3. hajampa, hajawachapa (kadiria jibu la mtahiniwa)2/0
    4. Nyembe walizonunua kwenye maduka zimewasaidia kukata kucha. 1/0
    5. Magombe haya na yale yalivuka jito hilo kwa utaratibu. 1/0
    6.                  
      1. Adhabu ilitolewa kwa mwanafunzi na mwalimu kwa kufanya makosa au Makosa ya mwanafunzi kwa mwalimu yalimfanya apewe adhabu au Mwalimu alimpa mwanafunzi adhabu baada ya kufanya makosa. ½ x 2=1
      2. Nguo zilizonunuliwa juzi ziliuzwa kwa bei ghali au Nguo ambazo zilinunuliwa juzi ziliuzwa kwa bei ghali. 1/0
      3. Fasihi ilizushwa na mapambano baina ya mwanadamu na mazingira. 1/0
    7.                
      1. Nguo zilizoraruka zimeshonwa au Nguo ambazo ziliraruka zimeshonwa. 1/0
      2. Japokuwa nilienda kwake mapema sikufanikiwa kuonana naye au Maadamu umefika mapema tutaanza mkutano. 1/0
      3. Usalama ukiimarika watalii wengi watazuru humu au Angesoma kwa bidii,angepita vizuri.
        Kadiria sentensi za mwanafunzi) 1/0
    8. Miti mitano ilikatwa. (kadiria sentensi) ½ x 2=1
    9. Sahani tano safi zitatumika katika sherehe. ½ x 6=3
          N        V     V            T       H         N
    10. Kisu kinolewacho ndicho kipatacho. 1/0
    11. kwa tano –akisami /uakifishaji wa idadi
      kwa gari –kitumizi /kifaa
      kwa mchuzi –pamoja na 3x1=3
    12. Kahindi alipanda matatu nambari saba, kisha akamuuliza dereva, “Gari hili litanifikisha Ukunda?”
      Kahindi – ½
      saba, dereva, - ½
      “ “ - ½
      Gari – ½
      Ukunda – ½
      ? – ½
    13. kupeka 1 x 1 =1
    14. Mtoto wa mwalimu angali uwanjani. (kadiria sentensi ya mwanafunzi) ½ x 4=2
    15. fiche, shaka. 2x1=2
    16. Dereva yeyote atakayeendesha gari kwa kasi atapoteza kazi yake. (kadiria) 2/0
    17. Viongozi wetu wasipozinduka hatutaacha kudhulumiwa na mataifa ya kimagharibi. 2/0
    18. yambwa tendewa/ kitondo –aliwanunulia
      yambwa tendwa/ kipozi –zawadi nzuri
      yambwa ala /kitumizi–shilingi elfu kumi 3x1=3
    19. Shuleni mwetu mna majengo mapya. (nomino)
      Mashindano ya kandanda yanafanyika shuleni. (kielezi) 2x1=2
    20. Ukiwa mwenye bidii utapata fanikio maishani. 1/0
  4. ISIMUJAMII (alama 10)
    1.                        
      1. Matumizi ya sentensi ndefu. Sentensi ya kwanza ina zaidi ya maneno 30.
      2. Matumizi ya msamiati maalum. “mswada, bunge”
      3. Vifungu vya sheria vinarejelewa. “kifungu cha 4…”
      4. Matumizi ya lugha sanifu. “sentensi ya kwanza ina lugha sanifu”
      5. Matumizi ya lugha kavu. “lugha inayotumiwa haina mapambo”
      6. Matumizi ya lugha ya heshima. “sheria za bunge hili tukufu…”
      7. Kuchanganya ndimi. “kufikia the one third rule…”
      8. Lugha ya kuibua utangamano. “ndugu zangu” (zozote tano za kwanza x1=5)
    2.                      
      1. Matumizi ya uradidi/urudiaji. “mheshimiwa spika”
      2. Matumizi ya viziada lugha au ishara za mwili au uso
      3. Kutajwa kwa wahusika kwa majina. “ Mheshimiwa Orengo”
      4. Wabunge kukatizana kalima.
      5. Matumizi ya lugha ya mzaha na kukejeliana.
      6. Lugha ya maswali na majibu
      7. Matumizi ya utohozi. “spika, bajeti”
      8. Matumizi ya lugha amrishi hasa na spika. “Mheshimiwa… keti!”
      9. Mtindo maalum wa kuanzisha na kuendeleza mjadala. “ Mheshimiwa Bwana Spika”
      10. Lugha ya kushawishi. “ndugu zangu waheshimiwa naomba” (zozote tano za kwanza x1=5)
        TANBIHI: Kila sifa iandamane na mfano au maelezo.
        Sifa bila mfano, alama nusu,mfano bila sifa sufuri.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Kigumo Mocks 2021 Exams.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest