Hadhi ya lugha, Lahaja za Kiswahili na Chimbuko la Kiswahili - Isimu Jamii Notes

Share via Whatsapp


Hadhi ya lugha

Lugha rasmi

Ni lugha inayopewa jukumu la kutumika kikazi mf katika kuendeleza shughuli rasmi k.v elimu, utawala n.k.

Sifa

  • Hutumika katika mazingira au shughuli rasmi kv. Mikutano ya mawaziri,elimu, mikutano ya machifu n.k
  • Aghalabu huwa ni lugha inayosemwa nchini na pia nje ya nchi. Mf. Kiswahili.
  • Inaweza kuwa lugha mojawapo ya wenyeji au lugha ya kigeni.
  • Yaweza kutekeleza majukumu mengine k.v kuwa lugha ya Taifa.
  • Huwa imesanifishwa na kusambazwa kupitia vyombo vya habari, vitabu na machapisho mengine.
  • Mara nyingi huwa ni lugha yenye historia ndefu.
  • Iweze kutoa fursa ya kujiendeleza kimsamiati kutokana na kuibuka kwa maneno mapya.
  • Huwa na msamiati mpana katika kila Nyanja za maisha. Isikosekane fasiri ya neno katika lugha hiyo.

 

Majukumu.

  • Kuendesha shughuli zote katika ofisi za serikali.
  • Kufundisha shuleni(msingi hadi vyuoni).

Lugha ya Taifa

Ni lugha iliyoteuliwa kama kitambulisho na ustaarabu wa taifa zima.

Sifa za lugha ya taifa

  • Ina wazungumzaji wengi.
  • Ina uwezo wa kutoa hisia za kikabila na kuwafunza watu kuhisi kuwa taifa moja.
  • Huwapa watu utambulisho katika umoja wa mataifa.
  • Huibua hisia za kizalendo miongoni mwa wananchi.
  • Ni lugha ya mama/ kwanza ya kikundi cha watu katika taifa husika
  • Ili wapokezane utamaduni, amali na historia.
  • Ili wafunze wengine
  • Iwe na muundo wa kiisimu unaofanana na ule wa baadhi ya lugha za watu katika taifa husika hivyo kujifunza ni rahisi k.m Kiswahili na lugha zingine za kibantu K.v kiluhya , Kikuyu n.k
  • Iwe lugha mojawapo asilia, isiwe ya kigeni bali ya kienyeji; isilete chuki bali ieleze hisia za uzalendo na utaifa.

Majukumu

  • Huunganisha watu wa taifa/huleta umoja.
  • Huziba mipaka ya kikabila.
  • Hukuza utamaduni wa kiafrika.
  • Hukuza uzalendo wa watu wa taifa kwa kutumia lugha kama kifaa cha kuonyesha hisia za kizalendo.
  • Hutambulisha watu wa taifa fulani kwa mfano; wimbo wa taifa n.k.
  • Huleta maendeleo ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kisayansi kutokana na umoja wa taifa zima kilugha.
  • Hufanikisha harakati za uongozi.
  • Husawazisha watu kilugha kwa sababu hisia zitakuwa sawa.

Lugha ya kimataifa

Ni lugha ambayo inaweza kutumika katika mawasiliano nje ya mipaka ya nchi husika kwa masuala ya kisiasa, kidiplomasia, kibiashara na kitamaduni.

Sifa za lugha ya kimataifa

  • Ina uwezo wa kutimiza masuala ya kidiplomasia, kiuchumi, kisiasa, kielimu na hata sera katika nchi mbalimbali.
  • Ina uwezo wa kutumika katika vyombo vingi vya habari katika pembe nyingi duniani.
  • Ina uwezo wa kutumika katika utafiti na uchunguzi kote duniani.
  • Inasemwa katika pembe nyingi za dunia na watu wengi.
  • Inatumika kuendesha mikutano na shughuli rasmi za kimataifa.

Majukumu ya lugha ya kimataifa.

  • Hufundishwa katika vyuo vikuu vingi duniani- Amerika, Ujerumani, Uswidi, Uingereza, Japani.
  • Hutumika kutangazia na idhaa nyingi duniani kuanzia hapa Afrika ya mashariki, Uingereza kuna BBC, voice of Amerika, Radio Urusi, Radio China kimataifa n.k.
  • Kinasemwa katika kila pembe ya dunia mf. Afrika nzima, Amerika, China n.k
  • Ni kati ya lugha mojawapo ya lugha zinazotumiwa kama lugha rasmi katika umoja wa Afrika(AU).
  • Hutumiwa katika kutolea magazeti mengi na majarida katika pembe tofauti za dunia.mNchi kama vile Uchina, Ujerumani na Uajemi zina majarida yanayotolewa kwa lugha ya Kiswahili.

Viziada lugha

Ni matumizi ya ishara kv za mikono na uso mtu anapozungumza ili kusisitiza jambo fulani.

Sababu za kutumia viziada lugha

  • Haja ya msemaji kutilia mkazo analosema mfano kunao walio na tabia ya kutupatupa mikono au kuwagusa wenzao wanapozungumza kwa nia ya kutilia mkazo wanachokisema.
  • Hali ya kihisia ya mzungumzaji - kwa mfano mtu akiwa na furaha au hasira huathirika kupitia uso wake
  • Haja ya kuwavutia au kuwanasa wasikizaji. Aghalabu wazungumzaji bora huweza kunasa nadhari za wasikilizaji kwa kutumia viziada lugha.
  • Ukosefu wa muda wa kutosha. Huenda ikawa mzungumzaji ana muda mfupi sana wa kusema aliyonayo. Katika hali hii mzungumzaji huona kuwa ni bora maneno yake yaandamane na ishara
  • Kudumisha siri. Ishara hutumika pale ambapo mzungumzaji anataka kusema jambo ambalo ni la siri na hataki wengine wajue mf. Wanaovuta sigara hutumia ishara kuuliza kama mwenzake ana sigara
  • Ulemavu. Vigugumizi hulazimika kuambatanisha mazungumzo yao na viziada kwa sababu ya kudodosa kwingi katika mazungumzo yao.
  • Huwa ni jambo la kawaida kwa binadamu kuambatanisha mazungumzo na matumizi ya viziada lugha.


Dhana ya Lahaja

  • Ni vilugha katika lugha moja kuu( vijilugha vidogo vidigo vya lugha moja kuu.
  • Ni tofauti za kimatamshi na maumbo pamoja na matumizi katika lugha ambayo huhesabiwa kuwa lugha moja
  • Lahaja huzungumzwa na kundi dogo ikilinganishwa na jumla ya watumizi wa lugha kuu

Asili ya Lahaja (Sababu za kuzuka Kwa lahaja)

  1. Kutawanyika kwa watu wanaotumia lugha moja ambao huenda kuishi maeneo mbalimbali ambako mazingira ni tofauti
  2. Kuingiliana na kuoana kwa watu na kwa hivyo kuathiri lugha kwa namna fulani
  3. Uhusiano baina ya watumiaji wa lugha kama vile wa biashara
  4. Utawala na mfumo wa siasa tofauti ambao huweza kupendelea namna fulani ya lugha
  5. Dini kama vile Uislamu na ukristo, huweza kusababisha kuzuka kwa lahaja
  6. Elimu husababisha kuzuka kwa lahaja ambapo aina Fulani ya lugha kama vile Kiswahili sanifu ,hutumiwa katika mafunzo
  7. Ujirani wa makabila. Makabila yanayopakana,lugha zao huweza kuathiriana kwa kiwango cha kuzua lahaja mpya inayodhihirika kimatamshi
  8. Mwachano wa kijiografia. Tofauti za kimasafa huweza kusababisha kuzuka kwa lahaja.
  9. Matabaka katika jamii. Tabaka la juu nhujizulia lahaja inayowatambulisha katika matumizi ya misamiati na vilevile tabaka la chini

 

Vipengele vinavotambulisha lahaja

  1. Matamshi- maneno hutamkwa kwa namna tofauti katika lahaja tofauti
  2. Msamiati
  3. Sauti- sauti tofauti huweza kutumika katika lahaja tofautitofauti km, chiti na kiti, moja/moya
  4. Lafudhi tofautitofauti miongoni mwa lahaja
  5. Muundo wa maneno km. mtu/ mutu
  6. Maana ya maneno- neno moja laweza kuwa na maana tofauti katika lahaja tofauti.
    Km Lahaja 1: kufura-kushiba
    Lahaja 2: kufura- kukasirika

Umuhimu/matumizi ya lahaja

  1. Hutumiwa katika kukuza lugha kwa kupanua msamiati wake kwa mfano, maneno rununu, ngamizi na runinga ni za kilahaja
  2. Hutumika katika kusanifisha lugha
  3. Hudhihirisha utajiri wa lugha kupitia mitindo mbalimbali ya wazungumzaji
  4. Hunogeza lugha kwa kutia kwa kutia ladha mazungumzo ya wasemaji mbalimbali
  5. Huwakilisha historia ya lugha

Lahaja za Kiswahili

Lahaja za kaskazini

  1. Kiamu – huzungumzwa Lamu
  2. Kipate- huzungumzwa Pate kaskazini mwa Pwani ya Kenya.
  3. Chimiini/chimbalazi- huzungumzwa Somalia katikati ya Mogadishu na kenya.
  4. Kitukuu/kibajuni- huzungumzwa kaskazini mwa Pate na Lamu.
  5. Kisiu- huzungumzwa sehemu za Pate mjini Siyu.

Lahaja za kati

  1. Kimvita- huzungumzwa Mombasa.
  2. Kijomvu- huzungumzwa Jomvu.
  3. Kingare- husemwa Mombasa(kilindini).

Lahaja za kusini

  1. Kimtang’ata- Huzungumzwa Tanga, Pangani
  2. Kipemba- Huzungumzwa Pemba.
  3. Kimgao- huzungumzwa katika visiwa vya Kilwa.
  4. Kingozi- Huzungumzwa Kismayu, Lamu kaskazini
  5. Kingazija- Huzungumzwa Ngazija (Comoro)
  6. Chichifundi/chifundi- huzungumzwa shimoni.
  7. Kiunguja- huzungumza Unguja
  8. Kimrima- huzungumzwa Tanga, Vanga, Pangani, Dar-es-Salaam
  9. Kivumba- huzungumzwa Vanga,Wasini, Kusini mwa pwani ya Kenya

Makosa katika lugha

Sababu za makosa katika lugha

  1. Athari ya lugha ya kwanza-ulefu/urefu
  2. Hali ya kiakili ya msemaji-mgonjwa au mlevi hudondosha sauti
  3. Kuhamasisha mafunzo na lugha moja hadi nyingine-katoto/kitoto
  4. Kutodhibiti mfumo n a ngeli katika lugha-ng’ombe hii/ng’ombe huyu
  5. Kujumuisha kanuni za lugha :mnyambuliko wa vitenzi. soma-somesha, penda-pendesha(kosa)
  6. Kasi ya uzungumzaji huathiri usanifu wa lugha
  7. Kosa la kimakusudi-dhamira/lengo lakuwashawishi au kuburudisha
  8. Kosa la kutoelewa maana ya neno kimatumizi au umilisi wa maneno. Kudhani neno ‘tetesi’ linalo tokana na neno ‘teta’ ilhali maana yake ni uvumi.

Sababu zinazochangia kufa kwa Kiswahili.

  1. Kiuchumi – maendeleo na ubunifu wa viwanda yanafanya watu kuhamia mijini. Watu wanapohamia mijini wanaacha kuzungumza lugha moja na kuanza kuzungumza nyingine kwa ajili ya mawasiliano
  2. Uchache wa wazungumzaji – idadi ya watu wanaozungumza lugha fulani inapopungua lugha hiyo hufifia.
  3. Kutoungwa mkono na taasisi mbalimbali k.v elimu dini na vyombo vya habari hukabiliwa na tisho la kufa
  4. Hadhi – lugha ambazo hazina hadhi kuishia kufa
  5. Ndoa za mseto – watu wanapo changanyikana kupita ndoa za mseto husababisha lugha zingine kudidima
  6. Kuhama kwa watu – kuhama kutoka sehemu moja hadi nyingine luga zao huathiriwa
  7. Hakuna sera maalum kutoka kwa serikali kuhusu matumizi ya Kiswahili.
  8. Kuna uhaba Mwingi/mkubwa wa waandishi
  9. Kuzuka kwa lugha ya sheng’†ambayo ni maarufu miongoni mwa vijana
  10. Imani potovu kuwa lugha ya Kiswahili ni duni
  11. Kuzuka kwa lugha zingine k.v Kifaransa, Kiingereza
  12. Watumizi wa Kiswahili hawajali jinsi ya kutumia lugha
  13. Ukosefu wa fedha za kufanya utafiti wa kina wa somo la Kiswahili
  14. Kuwepo kwa sheria katika shule kuwa Kiswahili kizungumzwe siku moja kwa juma.

Juhudi za serikali katika kuimarisha lugha ya Kiswahili.

  1. Kiswahili kufanywa lugha ya Taifa / rasmi
  2. Katiba ilipitisha Kiswahili kiwe lugha rasmi nchini
  3. Kiswahili kufanywa somo la lazima shule za upili / msingi
  4. Hutumika katika matangazo na taarifa za habari kupitia runinga
  5. Viongozi wa dini wanahubiri wakitumia lugha ya Kiswahii
  6. Kenya na Tanzania zimeunda mabaraza ya vyama mbalimbali vya kushughulikia maenezi k.v CHAKITA na BAKITA
  7. Lugha hii imetumiwa na wanabiashara.
  8. Lugha hii hufunzwa katika vyuo vikuu.

Mikakati inayoweza kuchapuza kukua na kuenea kwa Kiswahili nchini Kenya.

  1. Sera madhubuti - hii itaelekeza hatua za kupanga na kuendeleza lugha. Pia itabainisha nyanja na maeneo ya matumizi ya Kiswahili.
  2. Kuamrisha Kiswahili - kitumiwe kama lugha ya kufundisha baadhi ya masomo, somo la lazima n.k
  3. Ufadhili wa miradi ya utafiti.
  4. Maandalizi mema ya walimu na wataalamu wa Kiswahili.
  5. Kubuni vyombo vya kukuza Kiswahili.
  6. Kusisitiza matumizi ya lugha sanifu.
  7. Serikali kufadhili uandishi na uchapishaji wa vitabu vya sarufi.
  8. Kuingiza Kiswahili kwenye kompyuta.
  9. Kuunda jopo la kitaifa la wataalamu - lengo lao ni kutoa mwongozo kuhusu Kiswahili.
  10. Shughuli za sanaa, maonyesho na muziki
  11. Vitabu vingi kuchapishwa kwa lugha ya Kiswahili
  12. Shughuli za lazima bunge kuendelezwa kwa lugha ya kiswahili
  13. Vyombo vya mawasiliao kutumia lugha ya Kiswahili
  14. Kuunda jopo la kitaifa la wataalamu - lengo lao ni kutoa mwongozo kuhusu Kiswahili.
  15. Kuamrisha Kiswahili kitumiwe kama lugha ya kufundisha baadhi ya masomo, somo lazima.

Shughuli zilizochangia kuenea kwa Kiswahili kabla ya ukoloni.

  1. Biashara - Kiswahili kilifanywa lugha ya biashara kati ya pwani na bara.
  2. Sera ya lugha- Kiswahili kilifanywa lugha ya taifa nchini Kenya na Tanzania.
  3. Dini - Kiswahili kilitumika kusambaza dini za Uisilamu na Ukristo.
  4. Elimu - Wamishenari walitumia Kiswahili kufundisha, kuandika, kusoma, kuhesabu na kazi mbalimbali za ufundi.
  5. Utawala wa kikoloni- Sera ya lugha ya wajeremani nchini Tanganyika ilisisitiza matumizi ya Kiswahili.
  6. Vyombo vya habari- magazeti mengi ya Kiswahili yalizuka nyakati za ukoloni.
  7. Siasa- Wahusika wengi katika vita vya ukombozi nchini Kenya na Tanzania walitumia Kiswahili kama lugha ya mawasiliano.
  8. Hisia za utaifa miongoni mwa viongozi na wananchi zilichangia sana katika maenezi maana watu waliwasiliana kutumia kiswahili.
  9. Utafiti - kina Steere na Kraph walifanya utafiti wa kina kuhusu Kiswahili na hata kuandika vitabu.
  10. Tamasha mbalimbali za muziki, drama na mashairi
  11. Uchapishaji wa vitabu, magazeti na majarida ya Kiswahili mfano kamusi iliyochapishwa.

Jinsi vyombo vifuatavyo vimechangia katika kuenea kwa kiswahili.

Vyombo vya habari

  1. Hutumia Kiswahili katika matangazo.
  2. Vipindi vya mashindano ambayo hutangazwa na vyombo.
  3. Huwasilisha makala mbalimbali wakitumia lugha ya Kiswahili.
  4. Huandaa makongamano ya waalimu wa Kiswahili.
  5. Hukuza misamiati mipya ya lugha ya Kiswahili

Vyombo vya Uchapishaji

  1. Vitabu vipya ambavyo hukuza lugha ya Kiswahili vya kiada na ziada.
  2. Uchapishaji wa majarida na magazeti kuimarisha taaluma ya Kiswahili

Vyombo vya Elimu

  1. Somo la lazima katika shule za msingi na sekondari.
  2. Hufunzwa hadi vyuo vikuu.
  3. Silabasi mpya ya Kiswahili ambayo inazumgumzia masuala ibuka kama teknolojia, jinsia n.k
  4. Kuongezeka kwa waatalam na waalimu waKiswahili

Kuteuliwa kuwa lugha rasmi.

  1. Kutumika katika mikutano rasmi.
  2. Kutumika katika kuchapisha sera za serikali.
  3. Kutumika katika miktadha rasmi.
  4. kuendesha shughuli rasmi - mahakamani.
  5. Kutumika katika makongamano ya kitaifa.

Changamoto ya Maenezi ya Kiswahili Afrika Mashariki punde baada ya uhuru

  1. Uhaba mkubwa wa wataalamu wa Kiswahili
  2. Athari kutoka kwa lugha ya kwanza.
  3. Watu kuchangamka lugha nyinginezo kama vile kiingereza, kijerumani.
  4. Imani potovu – lugha ya Kiswahili ni duni
  5. Uhaba wa walimu wa Kiswahili.
  6. Uhaba wa vitabu vya Kiswahili.
  7. Kutokuwepo kwa sera ya lugha kutoka kwa baadhi ya serikali za mataifa ya Afrika mashariki.
  8. Uhaba wa pesa za kutafiti.
  9. Nchi za Afrika za kukuza na kuendeleza Kiswahili.

Hali ya lugha ya Kiswahili nchini Kenya baada ya uhuru

  1. Kiswahili kinafundishwa shuleni; kinatahiniwa kama somo la lazima katika shule za msingi na sekiondari. Pia kinafundishwa katika vyuo vikuu
  2. Kinatumika katika utangazaji katika vituo vya utangazaji
  3. Ni lugha rasmi
  4. Serikali inatumia sambamba na Kiingereza katika kusambazia hati za serikali
  5. Kinatumika kuendesha shughuli za kiutawala katika vituo vya polisi, mahakamani n.k
  6. Kinatumika katika shughuli za kidini
  7. Kinatumika katika shughuli za sanaa, maonyesho na muziki.
  8. Wanasiasa wanakiona afadhali katika mikutano ya hadhara.


Chimbuko la Kiswahili

Nadharia zinazoeleza chimbuko la kiswahili

  1. Kuwa Kiswahili ni lugha ya mseto. Kiswahili ni tukio la maingiliano ya kibiashara, kijamii na hata kindoa baina ya wenyeji wa Pwani na Waarabu. 
    • Haja ya Waarabu kuwasiliana na watumwa wao wa Kibantu ilisababisha kuchanganya kwa maneno ya lugha za Kibantu na yale ya Kiarabu ili waweze kuelewana na hivyo lugha iliyochipuka ikawa ya Kiswahili (mchanganyiko wa Kibantu na Kiarabu.
    • Shughuli za kibiashara-Waarabu walipofika kwa shughuli hizi hawakufika na wake zao hivyo kulikuwa na uhaba wa wanawake wa Kiarabu hivyo wakaanza kufunga ndoa na wanawake Waafrika na kupata watoto waliojifunza Kiarabu na Kibantu na lugha iliyozungumzwa ikawa Kiswahili(lugha chotara-mchanganyiko wa Kiswahili na Kibantu).
  2. Kuwa Kiswahili ni lahaja ya Kiarabu. 
    • Kuna idadi kubwa ya msamiati wa kiarabu katika kiswahili.
      • Ghadhabu – hasira.
      • Nadra -chache.
      • Tisa - kenda.
      • daima – milele.
    • Lugha ya kiswahili imefungama sana na mafunzo ya dini ya Kislamu (ambayo ililetwa na Waarabu toka Uarabuni). Vile vile miongoni mwa wale wanaojiita Waswahili ni wafuasi wa dini ya Kislamu. Wao hutumia majina ya Kislamu kama vile Mohammed, Rehema, Ramadhan n.k.
    • Nyimbo za taarab hapo awali zilikuwa zikiimbwa kwa mashairi ya kiarabu na baadaye zikaanza kuimbwa kwa mashairi ya Kiswahili.
  3. Kuwa Kiswahili ni lugha ya Kiafrika yenye asili ya kibantu. Mtazamo hushikiliwa na wengi. Unashikilia kwamba Kiswahili ni Kibantu kama vile Kikamba, Kizulu, Kiganda n,k.
    • Maumbo ya maneno kwa Kiswahili na lugha za kibantu yana viambishi. k.m mu-ndu. m-tu
    • Kuna mfanano wa kimsamiati katika lugha ya Kiswahili na lugha za Kibantu. k.m kuhoa, korora, kooa. Ulimi.lulimi
    • Lugha ya Kiswahili mara nyingi huwa na muundo wa silabi wazi/huru. Mfumo huu vile vile hudhihirika katika lugha nyingi za Kibantu. Kikombe/shikombe. Kitabu/shitapu.
    • Nomino hupangwa katika ngeli kama tu ilivyo katika lugha nyingine za Kibantu. A/WA Mtu anaenda. Watu wanaenda. M/A Mundu athi Andu mathi.
    • Upatanisho wa kisarufi ni sawa k.m Baba analima/Baba arima.
    • Katika lugha za Kibantu kuna uwezekano wa kuunda maneno kutokana na aina nyingine ya maneno. Mfano kuunda nomino kutokana na vitenzi.
    • Mpangilio wa maneno katika tungo ni sawa. Mtu anakuja leo/Mundu anecha juno
    • Kuna mnyambuliko wa vitenzi katika lugha ya kiswahili jinsi tu ilivyo katika lugha nyingine za Kibantu. Lia – lilia/Rira – ririra. Piga – pigwa/khupa- khupwa.


Usanifishaji

Ni uamuzi wa kuchagua lugha moja au mojawapo wa lahaja za lugha na kuifanyia marekebisho ya kimatamshi, kisarufi, kimaana, kimaandishi ili iweze kutumika katika shughuli rasmi.

Kusanifisha ni utaratibu wa kuondoa tofauti zote za lugha ambazo hutokana na kimaeneo na tabaka.

Sababu za kusanifisha Kiswahili

Kuwepo kwa lahaja nyingi za Kiswahili.

Wingi huu wa lahaja ulitatiza sana mawasiliano katika shughuli za kibiashara, kielimu, n.k. ambazo zilihitaji kuelewa kwa lahaja moja ili kueleweka na watu wote.

Kulikuwa na hati tofauti zilizotumiwa kuandika Kiswahili.

Mwanzoni kulikuwa na lahaja ya Kiarabu na baadaye Kirumi. Ni kutokana na hili ndipo kulikuwa na tofauti katika kuendeleza maneno na kukawa na haja ya kutafuta namna moja ya kuendeleza.

Shughuli za kidini.

Madhehebu mbalimbali yalijishughulisha katika shughuli za kidini na wote walijitahidi kutafsiri biblia na nyimbo. Wamishenari hawa walitumia lahaja za maneno waliojikuta. Mfano CMC walitafsiri wakitumia kimvita na University Mission of Central Africa wakatafsiri wakitumia kiunguja. Hii ilileta tofauti na ili kuondoa tofauti hii kukawa na haja ya usanifishaji.

Haja ya kusawazisha maandishi ya kitaalamu.

Wataalamu wa lugha walikuwa wameandika vitabu tofauti mfano kraph aliandika kitabu cha Swahili Grammar(1850) katika lahaja ya Kimvita vilevile Steere akaandika kwa Kiunguja. Tofauti zilizotokea kwa maendelezo ya maneno na msamiati zilizua ugomvi kwa pande zote mbili hivyo haja ya usanifishaji.

Haja ya kuwa na lugha moja ya mawasiliano na elimu.

Hili lilifanyika baada ya kuteuliwa kwa Kiswahili kama lugha ya kufundishia, hata hivyo kulikuwa na tofauti za matamshi na maendelezo hivyo haja ya kusanifishwa ili tuwe na lugha moja.

Uteuzi wa lahaja ya kusanifishwa.

Kabla ya kuchagua na kusanifisha lahaja fulani kulikuwa na mjadala mkali ulioibuka katika mkutano kule Mombasa. Lahaja ya kiunguja na kimvita ndizo zilikuwa na uzito mwingi hasa wa maandishi kuliko lahaja zile zingine.

Nguvu za Kiunguja.

  1. Ndiyo lahaja iliyokuwa imeenezwa sana na wafanyabiashara wa Unguja sehemu kubwa ya bara ya Tanzania, Kenya na Uganda.
  2. Kiunguja kilitumika na watu wengi.
  3. Kiunguja kilikuwa kimefanyiwa uchunguzi na wataalamu.
  4. Kiunguja kilitumiwa sana katika masuala ya elimu na kidini.
  5. Wepesi wake wa kutumika na lugha nyingine za kibantu.

Nguvu za Kimvita

  1. Kilikuwa na ukwasi wa msamiati na uwezo wa kuazima maneno kwa upesi.
  2. Kilikuwa na miswada mingi ya kifasihi, ushairi na dini.
  3. Kilikuwa bora katika maandishi ya nathari na usanifishaji.
  4. Kimvita kilikuwa cha kiwango cha juu zaidi kuliko Kiunguja.

Udhaifu wa Kiunguja.

  1. Ilikuwa lugha ya biashara.
  2. Ilikuwa ya kiwango cha chini.

Udhaifu wa Kimvita.

  1. Kilitumiwa zaidi sehemu za pwani na za Mombasa.
  2. Kilihusishwa na wakereketwa.

Uteuzi wa Kiunguja

Waliounga mkono Kiunguja walikuwa na wakashinda baada ya kura kupigwa. Kiunguja kiliteuliwa kuwa msingi wa kusanifisha Kiswahili kote katika Afrika Mashariki. Ingawa Kimvita kilikuwa na utajiri, lahaja hii haikuwa imeenea.

Kamati ya lugha na shughuli zake.

Katika juhudi za kufanikisha upatikanaji wa maandishi kwa Kiswahili sanifu, nchi za Afrika Mashariki ziliunda kamati ya lugha iliyojulikana kama Inter- Territorial Language Committee mwaka wa 1930.

Malengo ya kamati

  1. Kusanifisha maandishi na kuhakikisha mtindo mmoja unazingatiwa.
  2. Kuchapisha vitabu.
  3. Kuwahimiza na kuwasaidia waandishi wa Kiswahili.
  4. Kuidhinisha vitabu vya kianda na vya ziada vinavyohitajika kufundisha shuleni.
  5. Kuwapasha waandishi, habari zozote zile kuhusu njia tofauti au mitindo ya kusomeshea katika kila nchi.

Mafanakio ya kamati.

  1. Vitabu vingi vya sarufi, kilimo na hadithi vilichapishwa kwa mfano: Modern Kiswahili Grammar.
  2. Tafsiri ilifanywa na vitabu kuchapishwa kwa Kiswahili kwa mfano: Kisima chenye Hazina.
  3. Kamusi mbili zilichapishwa: Kiswahili - Kiswahili,Kiswahili - Kiingereza h.k
  4. Vitabu vingi vya kufundishia Kiswahili viliidhinishwa.

 

Hatua za usanifishaji

  1. Kuchagua lugha au lahaja moja ya usanifishaji miongoni mwa lugha au lahaja nyingi.
  2. Kuiweka hiyo lugha au lahaja katika maandishi ambako utaratibu wa kuendeleza maneno huamuliwa na herufi zitakazotumiwa huchaguliwa.
  3. Kuipanua lahaja hiyo/lugha kimatumizi ambapo uamuzi hutolewa kuhusu mahali lugha hiyo itakapotumiwa k.m redioni, magazetini, vitabuni na hata bungeni.
  4. Kuindeleza au kuikuza hiyo lugha kwa kutumia vyombo vya habari k.v redio, runinga, magazeti n.k vile vile ikuzwe katika taasisi za elimu kwa kuiandikia vitabu kuu mf. Kamusi.

Sababu za ujenzi na upanuzi wa msamiati

  1. Kukidhi mahitaji ya mawasiliano. Mazingira yanapobadilika, huhitaji msamiati mpya ili kufanikisha mawasiliano
  2. Kupanua matumizi ya lugha katika Nyanja mbalimbali
  3. Kukuza msamiati wa lugha
  4. Kuendeleza lugha/ kikidhi hadhi ya lugha
  5. Kuzitafutia dhana mpya maneno.
  6. Kufidia msamiati unaopotea na kusahaulika.

Njia za ujenzi na upanuzi wa msamiati

  1. Kuunganisha maneno ili yaunde neon moja k.m nguvukazi, jopokazi nk
  2. Kotohoa maneno kutoka lugha za kigeni k.m charger-chaja
  3. Kuchukua maneno kutoka kwa lahaja za Kiswahili.
  4. Kuchukua maneno kutoka lugha nyingine za kibantu
  5. Kuchukua maneno kutoka kwa lugha nyingine za kiafrika
  6. Kuunganisha vipashiokwa mfano, Ukimwi- upungufu wa kinga mwilini
  7. Kwa unyambulishaji
  8. Upanuzi wa maana za maneno
  9. Kutumia tafsiri sisi kwa mfano simu ya mkono- mobile handset, mama sukari- sugar mummy
  10. Kuunda maneno kwa kutumia mbinu za kiisimu

Mbinu za kuunda maneno

  1. Kutohoa
  2. Tafsiri sisisi
  3. Kuunganisha maneno
  4. Uhamishaji wa maneno kutoka lugha mf. Ugali.
  5. Kukopa
  6. Tanakali za sauti
  7. Kuongeza viambishi / mnyambuliko.
  8. Ufupishaji / akronimu.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Hadhi ya lugha, Lahaja za Kiswahili na Chimbuko la Kiswahili - Isimu Jamii Notes.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest