Jalada, Anwani, Dhamira ya Mwandishi na Muhtasari wa Nguu za Jadi - Mwongozo wa Nguu za Jadi

Share via Whatsapp


Utangulizi

Riwaya ya Nguu za jadi ni hadithi iliyoandikwa na Clara Momanyi. Hadithi hii imegawanywa kwa sura sita, kila sura ikitofautiana na ingine kwa mada iliyozingatiwa, wakati wa vitendo na wahusika wanaofuatiliwa. Sura hizi zinafikia kurasa 182.

Riwaya hii ni ya aina ya kiepiki. Hii ni kumaanisha, wahusika ambao mwandishi amewatumia ni wa kutungwa. Aidha, wahusika hawa hukabilliana na uovu mkubwa katika jamii yao na kwa ukabili huo, huo hawafi. Ni hadithi iliyoandikwa kumsisimua msomaji kuangazia yale yanayofanyika katika jamii yake.

JALADA

Jalada ya hadithi hii inatupa taswira kidogo yay ale yanayofanyika. Katika jalada tunamwona mzee aliye na mvi akimwonglesha kijana mmoja aliye mvulana. Wanaongea palipo giza. Tunaeza kuweza kubaina vitu vingine kama jinsi arghi iliyo katikatik haina mimea. Pia, kuna msitu ambao nyuma yake kuna mlima unaozuia mwangaza ulio nyuma yake.

Kulingana na jalada, tunaweza sema kwamba mzee huyo anampa mvulana huyo mawaidha. Hii inaweza kuwa taswira ya jinsi jadi na mila inavyopitishwa, kwa sababu katika kitabu kwa maelezo ya fikra za Mangwasha, wazee ndio wanaopaswa kuwalea vijana ile waweze kupata mwelekeo. Pia, kwa kuangalizia wawili hawa wameketi kwa nyasi, kuangazia kwamba pale ambapo jadi kunazo uzuri ambavyo vinapaswa kuhifadhiwa. Sio yote yaliyo katika mila ni mabaya lakini pia kulingana na nyakati, sio mengi mazuri. Mila na jadi ingawa zina mazuri yao hayaweza kuza jamii milele. Kwa maana hii, ingawa kuna nyasi, hakuna miti wa mimea mirefu hapo walipoketi.

Ardhi iliyo tupu inaweza kuwa inaonyesha ukame na ukosefu wa rasilimali ambao mwandishi anatuambia ulikuwa umekithiri nchi yote. Inaweza kuwa inaangazia ukosefu wa maadili unaokithiri watu wahusika, ambapo tunaeleza kuna wingi wa ufisadi na ukabila. Hadithi hii inatuanzia jamii hii ikiwa mahala hapa, ambapo maovu yamekithiri na mila zinazozingatiwa ni za kufilishisha watu hasa wanawake na vijana. Hakuna ukuzi wowote ulio katika jamii.

Lakini pia, kuna msitu ambao unaweza kuwa unaashiria kwamba hata kwa jangwa hili, kunao waliojitolea kukuza jamii wanavyoweza. Kwa kukwamilia maadili mema na kwa kupingana na uovu ulio kithiri kunao ukuzi wa jamii na maadili ambayo hajajifungwa kwa mila na jadi ila yanazingatia yanayotendeka. Mfano mzuri ni Mangwasha , licha ya kuwa mwanamke kujitolea kuangalia maslahi ya vijana wa mtaa wao. Pia, Lonare anajitolea kusomesha watoto wake wote hata wa kike na kwa njia hizi wanakuza jamii. 

Mlima ulioshikana na msitu unaweza kuwa unaashiria magumu ya safari hii ya kukuza maadili. Ni mlima mrefu na tunapoangazia hadithi, tunayaona yale magumu ambayo wahusika wetu wanaweza kupitia ili waweze kubadili hali zao. 

Mwanga unaoonekana nyuma ya mlima inaweza kuwa inaashiria faraja amabyo wahusika wetu wanapata baada ya kukabiliana na yale maovu wanayopitia.

ANWANI

Anwani ya Riwaya hii ni ufupisho wa 'Nguvu za Jadi'. Anwani hii inalingana na matokea ya hadithi jinsi tunavyowaona wahusika wakuu wakishirikiana kuvunja mila zilizowafunga na kuangazia kuleta mabadiliko katika Jamii yao. Hadithi hii inaangazia jinsi jadi na tamaduni zinaweza kutumiwa kuwafunga watu na kuwaeka kwa nafasi za watumwa.  Mwandishi anazingatia maudhui kadha wa kadha ambazo zinahusiana na anwani, pale anapoonyesha jinsi jadi zinapotumika vibaya na pia namna ya kuleta mabadiliko yanayofaa kwa mambo yaliyopitwa na wakati.  Mwandishi analeta swala ya kutufanya tuangazie jinsi maovu yanaweza kufichwa nyuma ya tamaduni ili yaendelee kuenezwa na pia kutufanya kuzingatia ni yapi kwa yale mambo ya kale yanapswa kuzingatiwa na yapi yanapaswa kubaidlishwa. 

DHAMIRA YA MWANDISHI

Kulingana na  mtiririko wa hadithi, tunaweza kusema kwamba nia kuu ya mwandishi ni kuonyesha msomaji kwamba kwa yote, tunapaswa kujitenga na maovu ya kijamii. Anaanza na kuonyesha jinsi jadi za kale zimetumika kwa faida ya watu kidogo kwa jamii na kwamba ingawa tunataka mabadiliko tunapaswa kuvunja jadi ambazo zimepitwa na wakati kama vile ubabedume na ambazo zinaleta dhana za ukabila na kuimarisha zile ambazo zinasaidia kuendeleza jamii kama vile kuwaangalia na kuwapa vijana mwelekeo. 

Aidha, ingawa kuna maovu katika jamii hatupaswi kujiunga nayo hata yawe yamekithiri kiasi gani. Pia, tunapojipata tunaeneza maovu haya, tunaweza jibadilisha kwa faida ya jamii nzima ili pia kupea wengineo mfano mwema wa kufuata. Nafasi yetu katika jamii na mazingira yetu haipaswi kuwa kizuizi cha kuleta mabadiliko yanayofaa ila yanafaa kuwa namna ya kujielewa na kuelewa yale mabayo tunapaswa kufanya. 



Muhktasari.

Riwaya ya Nguu za jadi inazingatia maisha ya Mangwasha ambaye ni mkaazi wa eneo la Matango, nchi ya Matuo. Mangwasha ni wa kabila ya Waketwa ambao wamekuwa wakifilisishwa na walio kabila ya Wakule. Mangwasha pia ameolewa na bwanake ni Mrima, ambaye kwa muda alipotelea ulevini na kumwacha bibi na watoto wake wawili, Kajewa na Sayore, taabani. 

Mangwasha amekuwa marafiki na mgombea kiti cha mtemi wan chi anayeitwa Lonare na wakati wa kufanyika kwa hadithi hii hi wa kukaribia Uchaguzi. Pia, anafanya kazi kwa ofisi ya Chifu, ambapo anaweza kuona na kupeleleza kuhusu yale maovu wanayopangiwa na Mtemi Lesulia ili wasiweze kuchukua uongozi. Chifu , Mtemi na rafiki yao Sagilu, wanapanga njama ya kufukuza Waketwa waliosishi matango kwa kuwachomea makaazi yao, lakini baadaye mpango wao unafeli wanaposhindwa kesi kortini n akulazimika kuwajengea makaazi yao tena. 

Lonare anarudi kugombea uchaguzi ambapo anaungwa mkono na Mangwasha na pia na wanawe Lombo , Sauni na Sagura. Pia, anaungwa mkono na watoto wa wapinzani wake Ngoswe na Mashauri na wanasaidiana kupiga kampeni. Siku ya uchaguzi unapokaribia, mambo kadhaa wa kadhaa yanaanza kufanyika. Sagilu anapoteza chanzo cha kugombea kiti na kupoteza akili zake. Bibi ya Mtemi, Nanzia, anafariki na kumwambia Ngoswe kwamba babake halisi ni Sagilu, rafikiye Mtemi. Uchaguzi unapokaribia, Lonare anapotea tena na baadaye tuanelewa kwamba alitekwa nyara na kuteswa kwa nia ya kumfanya apoteze uchaguzi.

Siku ya uchaguzi inapowadia, Lonare anatokea tena akiwa na majeraha na wafuasi wake wanajitolea kuenda kumpigia kura na anashinda uchaguzi huo. Riwaya hii inaisha kwa hotuba ya Lonare ya kwamba angepigana na ufisadi na kuiweka nchi yake inapofaa.

Mtiririko wa Hadithi

Nguu za jadi Sura ya Kwanza.

Hadithi hii inaanza Mangwasha akiwa mawazoni. Tunaelezewa kwamba Mangwasha na watoto wake wawili, Sayore na Kajewa,  pamoja na wakaazi wenziwe wa mtaa wa Matango, wamepatwa na msiba ambapo, makao yao yanateketea. Mangwasha amejifungia kanisani, ambapo watoto wake wamelala kando yake. Hajui pahali bwana yake, Mrima, yupo. Ameshindwa kulala kwa sababu ya mawazo yake, hasa kuhusu bwana yake alipo. Licha ya kuwa na uhusiano usio nzuri na bwana yake, Mangwasha anazidi kumwaza na hata anamwombea ili awe salama alipo kwa ajili ya watoto wake.

Tunaelezwa kwamba moto huo umetekeza mali yao nyingi na wamebaki na vitu vichache. Mangwasha anagutuka kwa wazo la kuzitafuta vyeti vyake vya masomo, ambavyo anaviangalia kama tumaini ya maisha yake. Hapa pia, tunapata maelezo kwamba anafanya kazi kwa ofisi ya chifu wa eneo hilo, Chifu Mshabaha. Anachokora mali yao na mwishowe anapatana na bahasha iliyo na barua lililoandikiwa Mrima. Barua hili linamtia hofu. Baadae tutaelezwa kwamba barua hili lilikuwa la kimapenzi ambalo lilikuwa limetoka kwa mwanamke mwingine.

Tunaona Mangwasha akijiwazia jinsi alibaki hohe hahe kwa sababu ya moto ule na anajiuliza mbona Mungu kamwacha matatani. Tunamwona akijipa moyo kwamba Mungu wakati mwingine huyakubali mabaya kutendeka kwa nia yake. Mwandishi anatupa mwelezo wa jinsi Mangwasha na wanawe walivyojiingiza katika kanisa lile ili waweze kujificha. Tunaelezewa walivyo jifungia humo ndani na Mangwasha kujihami ili kuweza kuwachunga watoto wake.

Mangwasha alipotulia humo ndani, anaanza kuwasikiliza wale walio nje jinsi wanavyo zungumza. Anaweza kutambua kwamba hawajui kwanini wakachomewa mali ili kufurushwa makwao. Anaweza kubaini pia kwamba Waketwa wenzake wana uchungu mwingi kwa sababu ya yale waliofanyiwa. Mwandishi pia anatueleza uhasama ulio kati ya kabila mbili za taifa hilo la Matuo, Waketwa na Wakule.

Waketwa wamefilisishwa na Wakule kwa njia nyingi, na pia wamewekewa lawama kwa yote mabaya yanayotendeka katika nchi yao. Pia, tunaelezwa kwamba Wakule ndio wanaomiliki nyadhifa za uongozi na wanazitumia nafasi zao kuwa filisisha Waketwa zaidi. Mojawapo ya njia hizi ni kuwanyima nafasi za uongozi. Pia tunaelezwa jinsi Waketwa wamefilisishwa kimali na kwa hivyo wao ndio walio wengi kwa matabaka ya chini, ilhali Wakule wako katika matabaka ya juu. Jambo  hili linadhihirishwa na mitaa wanayoishi, ambapo Wakue wanaishi mtaa wa Majuu, na Waketwa wanaishi Matango na mitaa nyingine ya chini. Mtaa wa Majuu ndipo matajiri wengi wanapoishi.

Mangwasha anazidi kusikiliza walio nje wakijaribu kutatua swali la moto ule ulipotoka. Wengi wanadhania kwamba ni mkasa mwingine wa kujaribu kuwadhulumu Waketwa ili waondoke eneo lile la Matango, njama iliyopangwa na Chifu Mshabaha. Wanajibizana na kurushiana lawama kwa Waketwa wengine ambao inasemekana wamewasaliti wenzao ili wapate pesa na kuajiriwa, jambo ambalo linamsikitisha Mangwasha kwa sababu ni uongo mtupu. Pia linamsikitisha kwa sababu yeye ni mmoja wa Waketwa wachache ambao wameweza kuandikwa kazi, ingawa ni ya kiwango kidogo, na Wakule. Tunaelezewa kwamba Waketwa pia wamegawanyika kwa sababu kiongozi wao, Lonare, hajaonekana kwa muda. Mwandishi anatueleza kwamba Lonare aliweza kusimama kupambana na Lesulia lakini wakati wa uchaguzi ulipofika, Lonare alipotea na Mtemi Lesulia aliweza kuipata cheo yake bila mapingo yoyote. Pia, tunaelezwa kwamba kulingana na Mangwasha, chanzo kubwa cha kuteswa na kufurushwa kwa Waketwa kwa kupitia moto ule ni kutokana na uchaguzi ambao ulikuwa unakaribia. Mtemi Lesulia pamoja na wenzake walitaka kuwafurusha Waketwa ili wasiweze kujisajili kupigia kura mahali pale. Kulingana na Mangwasha, Lonare pia alikuwa anatambua jambo hili na ndio sababu Mangwasha alitamani sana Lonare aje ili aweze kuwaeleza Waketwa wenzake jinsi kulivyo.

Mwandishi anatuleleza jinsi Mangwasha alikuwa anatamani kuweza kuwaeleza Waketwa, na kusimamia haki zao mpaka mbele ya Mtemi Lesulia lakini alihofia kwa sababu yeye na mwanamke na jamii yao ilikuwa imejaza ubabedume. Mwandishi anatupa maelezo ya chanzo cha kuwa na roho ya kutia bidii ya Mangwasha ambapo tunaona inatokana na malezi na mafunzo aliyopewa na wazazi wake. Ingawa hakusoma hadi kiwango cha juu, alikuwa mwenye bidii na roho isiyokata tamaa.

Nguu za jadiSura Ya Pili

Sura ya pili ya riwaya hii imeandikwa kwa mbinu ya kisengere nyuma. Badala ya kuendeleza hadithi mbele, inaturudisha nyuma kutupa maelezo zaidi kuhusu Mangwasha na uhusuiano wake na bwanake, Mrima.

Mwandishi anaanza na kutueleza kuhusu maisha ya Mangwasha ya awali.  Tunaelezewa kwamba alitamatisha masomo yake alipomaliza kidato cha nne lakini baadae akajiunga na chuo cha uhazili cha Ndengoni baada ya kumshawishi baba yake, Mzee Shauri. Baada ya kuhitimu masomo yake ndipo alianza kufanya kzai kwa Chifu Mshabaha, ambako alipendwa kwa sababu ya bidii yake. Mwandishi pia anatueleza jinsi Mangwasha alikuwa na mrembo na umbo la kuvutia, ambalo ndilo lilimfanya Mrima kumtamani. Mrima naye alikuwa akifanya kazi karibuna ofisi ya chifu, katika gorofa lililokuwa na idara kadhaa za serikali.

Pia tunaelezewa kwamba kunaye bwana mwingine kwa jina Sagilu ambaye alikuwa rafiki ya Chifu Mshabaha alimtamani Mangwasha. Sagilu alikuwa na biashara kadhaa mojawapo ikiwa hoteli ya Mponda Bure, ambapo Mrima na Mangwasha walipenda kuenda kujivinjari. Pia, alikuwa na mashamba mengi na biashara za mafuta n ahata viwanda. Sagilu pia alikuwa na urafiki ya karibu na Mtemi Lesulia. Aidha, alitambulika kuwa katili hasa ilipokuja kwa wali walioshindana naye kibiashara. Alijulikana pia kuwa mwenye mali nyingi na mwenye bibi wengi, na kwamba alikuwa akiwatumia wanawake vibaya.  Mwandishi pia anatueleza kuhusu Bi Sihaba ambaye alikuwa na uhusiano wa karibu na Sagilu. Sihaba na Sagilu walishirikiana kwa ukatili na njama zao.

Mwandishi pia anatupa mano wa ukatili na hali ya kutojali ya Sagilu mabapo anaeleza kisa cha maziwa ambayo yalisababisha ungonjwa kuenea kwa watoto wachanga ilhali hakuna lile alichofanyiwa.

Mwandishi anarudi kutueleza kwamba ilhali Sagilu alimtamani Mangwasha, Mangwasha pamoja na Mrima hawakumpenda Sagilu ng’o. Mangwasha hakumpenda kwa tabia zake zilizojulikana. Mangwasha na Mrima waliacha kuenda mkahawani wake baada ya kisa cha Sagilu kuja kujikalisha nao walipokuwa wakila. Sagilu alipoona hawezi kumvutia Mangwasha, alijaribu kumtishia Mrima, jambo lililofanya Mrima aanze kukwepa kukutana naye.

Baadae , Mrima na Mangwasha wakaanza kupanga harusi. Habari hii ilipofikia Chifu Mshabaha, alimkashifu Mangwasha, kitu kilichomtia Mangwasha hofu kwa sababu ya kazi yake. Baadae, wakiwa harusini, Mrima alimwona mwanamke aliyetumwa na Sagilu kuleta barua iliyo na vitisho ofisini akijaribu kuingia kufikisha zawadi. Mrima aliongea na walinzi ili waweze kumzuia asiingie na katika mvutano wao, kifurushi alichokuwa amekibeba mwanamke huyo kilianguka na kutoa mlipuko. Mlipuko huo uliwashtua watu na mwanamke huyo akatoweka kwa gari jekundu. Upelelezi wa polisi haukufua dafu.

Mwandishi anatueleza  baada ya ndoa yao, Mangwasha na Mrima waliweza kuwapata watoto wawili, Kajewa na Sayore. Baada ya muda, Mrima akaanza kushiriki ulevi na akaanza kuchakaa. Jambo hili lilimsikitisha Mangwasha kwani hakujua pahali Mrima angetoa fedha za kushiriki anasa na asiwashugulikie watoto wake. Mangwasha alianza kuchunguza sababu za kumfanya mumewe kuanza kulewa na akamwendea rafikiye, Bi Mbulungu  ili akapate usaidizi. Bi Mbulungu alikubali kumsaidia kufanya uchunguzi. Baadae alitembelewa na Mzee Sagilu kwake akimkejeli kwa kumkataa na sasa aliyemwoa, Mrima, ni mlevi. Jambo hili lilimtia huzuni, kumfikisha mahali aliamua kutoka kwenda kumtafuta bwanake. Alipoenda kumweleza Bi Mbulungu, alionywa kwamba wanawake hawafai kuenda kuwatoa bwana zao katika starehe zao lakini Mangwasha hakutaka kuzingatia mila zao alizoziona za kinyuma. Bi Mbulungu alikubali kumwangalilia watoto na kumwacha aende kumtafuta Mrima katika mtaa wa Ponda Mali. Aliyaona mengi lakini hakumwona bwanake. Katika hali ya kumtafuta, aliona labda amwangalie kama alikuwa kazini. Kupitia huko,alisikia watu wawili wakiongea, Mrima na Sagilu. Mangwasha alijficha na kusikiliza mazungumzo yao na baadae akaweza kuelewa kwamba ni Mzee Sagilu ambaye alimpa pesa Mrima za kumpotezea ulevini. Hapo ndipo alipoelewa kwanini Sagilu alikuja kwake kumkejeli na alivyojua Mrima alikokuwa.

Mangwasha aliamua kurudi nyumbani kumngoja Mrima kwa sababu hakuwa anaenda kazini siku iliyofuata. Kufika nyumbani kwake kuliwafurahisha watoto wake, ambao pia walianza kumkumbusha vitu ambavyo walikuwa wakitishwa vya shule. Mangwasha alimweleza Bi Mbulungu kwanini Sagilu alikuja kumtembelea na yale aliyoyaskia Mrima akitamka kwamba Mangwasha na watoto wake wajipange. Bi Mbulungu alipomwaga, Mangwasha alibaki akingoja Mrima arudi nyumbani akiwa na mawazo nyingi.

Mrima alirudi nyumbani asubuhi, huku amelewa chakari na baada ya staftahi, aliamua kumkabili mume wake. Alimwongelesha kuhusu kupotea kwake na zile pesa alizopewa na Sagilu, jambo lililotia Mrima aibu, asitake kujibu maswai za Mangwasha. Mangwasha alinena naye kwa nia ya kumkosoa tabia zake na kumwokoa kutoka mkononi mwa mahasidi wanaompa mlungula ili ajimalize taratibu. Baada ya gumzo hili, Mrima hakuenda ulevini kwa muda na ilisemekana ni kama alikuwa amebadilika.

Nguu za jadi Sura ya Tatu

Sura ya tatu ya hadithi hii inaeleza matukio yaliyofanyika baada ya sura ya pili mpaka sura ya kwanza inapoanzia. Aidha, mwandishi anatueleza kwa undani jinsi Wakule na Waketwa walihusiana katika nchi yao.

Tunaelezewa kwamba Wakule waliwaonea Waketwa kijicho kwa bidii yao. Wakule walijiweka katika nafasi za utawala na za juu za nchi yao. Kwa ukabila na ufisadi walijipa vyeo ambavyo hawakuhitimu, jambo liloweka nchi yao kwa mashaka. Waketwa nao walinyimwa kazi hata walio hitimu na wale walioangukia bahati waifanya kazi katika viwanda na mashamba iliyomilikiwa na Wakule. Wakule waliponda maliasili za kitaifa kwa vyeo vyao na kuacha nchi ikiwa maskini. Waliharibu vifaa vya taifa kama hospitali, ndege na meli. Kwa kuponda mali, Wakule wasibabisha njaa kwa kuharibu misitu, bei za bidhaa zikapanda. Wakule matajiri wakaingia katika uchimba mawe na kuharibu mazingira zaidi. Jambo hili lilisababisha nchi kuzidi kuwa mbovu kwani pia maadili yalipotea na watu wakaanza kuibiana na kupokonyana mali, kutoka kwa wadogo hadi wakubwa. Mwandishi anaeleza kwamba kwa kuibia nchi yao walijiibia pia kwa ujinga wao. Watu walikosa matumaini ya kuishi.

Katika hali hii ya kukosa matumaini, Mwandishi anatueleza kwamba Mangwasha alisikitika lakini hakukubali kufa moyo. Aliendelea kujipa moyo kwa kazi aliyofanya. Mangwasha alifahau kwamba fahari ya binadamu haitokani na kukosa kuanguka bali ni kwa kuinuka kila anapoanguka. Jambo lililo msumbua Mangwasha moyoni ilikuwa hali ya vijana ambao walikosa shughuli na walizurura bila ya kufanya, a kugeuza wasichana wadogo walio na watoto kuwa ombaomba. Jambo hili lilimsikitisha kwa sababu hakuona jinsi vijana hawa wangeweza kutunza familia zao na hali ilivyo.

Mwandishi anarudi tena kutueleza kuhusu Lonare. Anatuleleza jinsi alivyoptea uchaguzi uliopita ulipofika. Mwandishi pia anatuongezea maelezo zaidi kuhusu maisha yake. Lonare alikuwa mtu aliyependa kupigania haki za kijamii na kando na mambi ya kisiasa, alikuwa pia mwanabiashara shupavu, licha ya biashara zake kushinda zikisumbuliwa na wale walio mamlakani. Lonare alikuwa na watoto watatu, binti mmoja na wavulana wawli ambao aliwasomesha wote bila ubaguzi kulingana na maadili na fikra zake kuhusu elimu. Tunajulishwa na mwandishi pia kwamba bibi yake Lonare aliaga watoto hawa wakiwa wachanga na kwa hivyo Lonare alijitahidi kuwalea wote pekee yake.

Mwandishi pia anatujulisha kwamba wakati huu ulikuwa wakati wa uchaguzi tena. Lonare alisimama na Chama cha Ushirika ilhali cha Mtemi Lesulia na wenzake kama Sagilu ilikuwa Chama cha Mamlaka. Lonare alichukiwa sana na Wakule na pia Waketwa wengine ambao walimkejeli na kumtusi.

Lonare alikuwa ameenda kumtembelea Mangwasha kazini na katika mazungumzo yao, Mangwasha alimwarifu kwamba alihisi kuna njama iliyokuwa ikipangwa dhidi ya Waketwa. Mangwasha alimweleza Lonare kuhusu watu waliokuja kumwona Chifu ambao hakuwahi waona katika ofisi hiyo tena. Lonare alimwabia Mangwasha aendelee kupeleleza pole pole huku naye pia akijaribu kufichua njama zao.

Jioni Mangwasha alipofika nyumbani, aliitisha sera za shule na mwanawe, jambo lililomkumbusha jinsi alivyokosa pesa. Hakuwa na pesa za kununua sera. Kati ya fikra zake, Sagilu alikuja kumtembelea huku akijaribu kumwinda tena kwa kumpa pesa kwa bahasha. Lonare alimkemea Sagilu na kutupa bahasha hilo na pesa. Alilala alikwa na huzuni mwingi na katika usingizi wake akaota ndoto ya ajabu.

Mangwasha aliota akikimbizwa na jitu lililotema pesa kila lilipofungua mdomo. Akikimbia mbele akapatana na moto , asiweze kujua lile la kufanya. Aliamua kuchukua jinga la moto na kuurushia jinyama hilo na alipofanya hivyo mara ya pili, alililenga. Lilipofungua kinywa kutoa mlio, manoti mengi yalitoka mdomoni na kupeperushwa na angani. Aliweza kukimbia na kujitoa hatari , kisha akagutuka na kuamka. Alipojaribu kulala tena, alisikia mayowe yalimfanya kuamka na kufungua dirisha ambapo alipata mtaa mzima ulikuwa ukiwaka moto.

Nguu za jadiSura ya Nne

Sura ya nne ya hadithi hii inaendeleza hadithi kutoka pale sura ya kwanza ilipoishia. Mwandishi anatueleza kuhusu matukio yaliyofuata baada ya kisa cha moto ule. Kulipokucha, Mangwasha alifungua dirisha la kanisa ili kutazama nje na aliwaona watu walikuwa wamelala nje. Kajewa alikuwa ameamka pia na walizungumza kidogo, huku kajewa akimuuliza maswali mama yake yaliyoonyesha hakuelewa kilichokuwa kikiendelea kama kuuliza maswali kuhusu sera za shule na mbona mama kampa maji ya matunda badala ya chai. Watu wengine walianza kuamka na walitaka kumkemea Mangwasha kwa kujifungia ndani ya kanisa . Haya yalipojiri, Lonare alitokea pamoja na watoto wake wawili, Sauni na Sagura na askari wawili.

Watu walilalamika na kuonekana kuhuzunishwa na yale yaliyowapata. Walikuwa wakijikusanya kwa kundi ndogo ndogo na polisi waliendelea kuongezeka kuimarisha usalama. Mangwasha na Mbulungu walipatana na marafiki wao ambao walikuwa wanabiashara. Waliwasili baadae kwa sababu walilala katika bishara zao kwa sababu ya moto ule. Waliwaeleza waliyoyaona usiku ule baada ya kufunga biashara zao kuchelewa ambayo ni: Walikutana na vijana waliokuwa wamebeba petroli huku wakikimbilia gari jekundu. Gari hilo lilikuwa na mwanamke dereva lakini hawakuweza kumtambua kwa sababu ya giza iliyosababihswa na kupotea kwa stima. Mangwasha alijaribu kupeleleza zaidi kwa kuuliza kama waliona gari lilikuwa la aina gari lakini hawakuwa na majibu. Mangwasha alienda kumweleza Lonare aliyoambiwa ili wakafanye utafiti zaidi. Kabla hajamweleza, Chifu pamoja na Mkurugenzi wa Ardhi wa Taria pamoja na mwanamke aliyetambuliwa kama Mbwashu waliwasili kwa magari.

Chifu na Mkurugenzi wa Serikali walikuwa wamekuja kuwaahakikishia kwamba wangefanya uchunguzi wa kujua chanzo cha moto huo. Chifu hakufurahi kumwona Mangwasha na Lonare pale. Watu walilalamika na Chifu alianza kujibizana nao lakini Lonare akaingilia kati kutuliza watu ili Mkurugenzi wa Ardhi amalize kuongea. Mkurugenzi alijaribu kuwaeleza kwamba wangepewa usaidizi kwa kujengewa mahema na kupewa chakula cha msaada lakini watu wale hawakutaka kusikia hayo. Walitaka kujua chanzo cha moto. Pia walitoa uzushi kwamba mahema yale watakayo pewa wajenge kule Matango wala si hapo walipolala maana waliona ni njia ya kuwafurusha pole pole kutoka kwao. Mangwasha na Mbulungu waliulizana nia ya Mbwashu kuwa pale maana walielewa kwamba kuja kwake haikuwa bure. Bibi yake Mtemi Lesulia, Nanzia, pia alikuja pale, jambo lililowashangaza watu zaidi. Mahema na vitu vya msaada vililetwa pia.

Mangwasha na Lonare walikuzunguza kuhusu kisa kile. Walizungumza kuhusu Sagilu na kwa maoni ya Mangwasha, Sagilu alitaka kuwafukuza kwa sababu alitaka kusimama kwa cheo cha mwakilishi wa bunge wa eneo hilo na pia walishuku alikuwa na njama ya kugueza Matango kuwa eneo la biashara. Lonare alimwa.bia Mangwasha kwamba wangefanya upelelezi zaidi ili wajue haswa ni kilichotendeka.

Jioni ilipofika, wakaazi wa Matango waliamua kurudi makwao. Walibomoa mahema yaliyokuwa yameekezwa pale kanisani na kubeba virago kuelekea Matango kwa vishindo na kelele. Lonare alifuatana nao akiandamana na polisi ili waweze kuwalinda watu wale. Watu wale walikataa ulinzi wa polisi na baada ya majibizano, mkuu wa polisi pamoja na askari wake waliondoka.

 Mangwasha alipokita hema lake, alifungua lile barua alilopata (tazama sura ya kwanza) na kulisoma. Barua hili lilikuwa limeandikwa na mwanamke mwingine, mpenzi wa Mrima. Jambo hili lilimuumiza sana moyo.

Siku yatatu ya kupiga kambi pale, wakaazi wa Matango walimka vjikaratasi vilivyowaashiria waondoke kule ili eneo lile lijengwe soko kuu la wachuuzi. Sagilu alikuwa ametoka kuzungumza na Mtemi Lesulia kuhusu vyeti vya ardhi vya wakaazi wa Matango ambayo Sagilu alimhakikishia kwamba watu wale hawangeyapata ile mipango yao ifue dafu.

Sagilu alipokuwa akielekea matango ili akajue ipango ya Lonare, alipatana na umati ulikuwa umezingira gari jekundu lililokuwa limeteketea nusu. Dereva alikuwa amewasilishwa katika stesheni ya polisi, ambaye alikuwa Sihaba. Sagilu Alielekea huko ambapo alijua kwamba sihaba alikuwa ameshikwa na watu kwa kusambaza vile vijikaratasi kwa kuambia watu wahame. Mangwasha alipomwona Sagilu pale, alimwendea pamoja na kundi la watu, naye Sagilu akatoroka kwa garo lake. Mbulungu alimwonya Mangwasha dhidi ya kumfuata Sagilu maana alikuwa mkatili.

Watu wale waliamua kupeleka kesi ya ardhi ya Matango mahakamani. Lonare alimtafuta Mwamba ile awe wakili wa watu. Mwamba alikuwa mwanasheria mashuhuri.

Sauni na Sagura walizungumza kuhusu kujihusisha kwa Sihaba kwa maneno ya ardhi ile, ambapo Sauni alimlinganisha Sihaba na Lilith, bibi wa kwanza wa Adamu kulingana na kisaasili ya Waibrania. Kulingana na jinsi Sauni alivyoeleza Lilith alikataa masharti ya Adamu na alipepepruka angani na kumwacha. Pia alizurusha uliwmenguni akiwazaa mashetani na pepo wachafu, na kusheheni uovu ulioelezeka. Mungu alimchukua ndiyo baadae akamuumba Hawa wa Pili.

Kesi ya ardi ilikuwa bado haijasikilizwa lakini magari yalikuwa yameanza kuleta vifaa kwa ujenzi pale Matango. Pia, Mangwasha aliporejea kazini baada ya muda, alishtuka kumwona Sihaba akitoka ofisini mwa Chifu Mshabaha huku watu walidhani bado ako jela. Alimwona Chifu akirudi na bahasha kubwa. Alingoja Chifu alipotoka tena na kuenda kuutafuta bahasha. Aliupata, akaufungua na kuisoma na alipoona jinsi mambo yaliyokuwa pale yalihusuiana na kesi ya ardhi, alishtuka. Alitoka kwenda kurudufu karatasi na akairejesha bahasha lile ofisini kisha akaelekea nyumbani. Baada ya wanawe kulala, aliwaita Mbulungu na Lonare, ambaye alikuwa na Sagura. Walipowasli, aliwaonyesha yale yaliyomo. Kulikuwa na ramani ya jengo kubwa la kibiashara, lile lilikuwa lijengwe pale Matango. Waliweza kufunua njama ya Mtemi Lesulia pamoja na wenzake waliotaka kuwafurusha Waketwa kutoka Matango ili waweze kunufaika kisiasa na pia kifedha.

Lonare aliwasilisha mambo haya kwa Mwamba na yakawa ya kutoa ushahidi katika kesi ya ardhi. Siku ya kusikilizwa kwa kesi ilipofika, mahakama yalikuwa yamejaa. Mafamba ndye alikuwa wakili wa Sagilu na wale waliotaka kujenga soko kuu. Licha ya Mafamba kupambana kadri ya uwezo wake, alishindwa kesi na Mwamba na Hakimu alitoa hukuma kwamba wenyeji wa Matango wapewe vyeti vya ardhi na juu ya hayo, wajengwe nyumba zao. Baada ya kesi hiyo, Hakimu na Mafambo walinyang’anywa leseni vya uanasheria. Hakimu aliweza kupata kazi baadae kufunza chuo cha kibinfasi cha uanasheria ilhali hakuna aliyejua Mafamba alipopotelea.

Baada ya haya, Mwandishi anatueleza kwamba Mangwasha alirudi kumfikria mumewe sana na siku moja aliambiwa na Mbulungu kwamba alionekana akiwa katika hali mbaya sana. Alionekana akibebwa akielekezwa mtaa duni wa Majaani. Jumamosi ya wiki hiyo ilipofika, Mangwasha pamoja na Mbulungu, Lonare, Sauni, Sagura na Mbaji, dereva wa mabasi ya kampuni ya Lonare,  walienda kumtafuta. Walieza kumpata kati ya kundi ya walevi waliokuwa wamelala. Mrima alipelewa kupata matibabu ya kiakili na kimwili kwa majuma kadhaa. Alipopata nafuu, Mrima alikuwa amekataa kurudi nyumbani ila kwa ushawishi wa Lonare na Mangwasha uliochukua muda mrefu.

Mrima Aliporudi nyumbani, alianza biashara ya kuuza mboga na iliponawiri, aliongeza vyakula vigine na baadae kikageuka kuwa duka. Aling’ang’ana kupata leseni ya kufanya biashara na baadae aliweza kufua dafu.

Siku moja Mangwasha akiwa kazini, Sagilu alikuja kumtembelea Chifu na alinena na Mangwasha kidogo huku akijidai kwamba angeshinda uchaguzi uliokuwa unakaribia kufika. Mangwasha aliwasikia Sagilu na Chifu wakiongea wakiwa ofisini. Sagilu aliondoka na baadae Chifu pia akaondoka akiwa na bahasha kubwa na hakurudi ofisini siku hiyo. Mangwasha alielekea nyumbani na baada ya gumzo dogo na watoto wake, aiingia chumbani na akapatana na lile bahasha aliloliona Chifu akitoka nayo ofisini. Alipolifungua, aliona limejaa pesa. Alilificha na hata Mrima alipotafuta bahasha lile, Mangwasha alidai hajalioa. Mangwasha alimweleza Lonare kuhusu lile bahasha na siku moja Lonare pamoja na wanawe wawili, Sauni na Sayore, wakaja kumwongelesha Mrima. Waliweza kubaina kwamba pesa hizo zilikuwa za kuhakikisha kwamba Mrima angempigia kampeni Sagilu. Waliweza kumwonya Mrima dhidi ya kitendo hilo na wakamkumbusha maovu yote aliyowafanyia. Lonare aliweza kumhimiza Mrima wakamrudishie bahasha lile.

Walingoja siku ya mkutano wa waliosimama na Sagilu. Mkutano huo ulikuwa umejaa wapinzani wa Lonare na Wakule wengi waliohusika katika visa vya ufisadi kama vile Mbwashu, Chifu Mshabaha na Ngoswe, aliye mtoto wa Mtemi Lesulia. Walienda na Lonare akamkemea Sagilu mbele ya watu wale kila akalirusha bahasha lile na wakaondoka, huku wakiwaacha watu wale wakivurugana.

Nguu za jadi Sura ya Tano

Sura ya tano inafanyika wakati ambao wananchi wa Matuo walikuwa wanangoja uchaguzi. Inaanza kwa kumwangazia Sagilu na jinsi umaaharufu wake ulikuwa umedidimia. Mwanake Sagilu, Mashauri, alikuwa mtaalamu mkuu wa usanifu wa ujenzi wa Taria. Mashauri alikuwa amemposa binti mmoja kwa jina Cheiya na hata alikuwa amewafahamisha wazazi wake. Cheiya alikuwa yatima na kwa bidii yake alikuwa amesomea uuguzi. Mwandishi anatueleza kwamba licha ya Cheiya kuwa hana mali, alipopata kazi, alibadili maisha yake kuelekea kupenda mali na vya bure. Mashauri hakushuku jinsi Cheiya alivyo husiana  na babake kwa sababu aliona ni urafiki tu.

Siku moja Mashauri alikabiliwa na Ngoswe, ambaye alikuwa mtoto wa Mtemi Lesulia. Ngoswe alimwonya kwamba anashuku kuna mengi yanayoendelea kati ya Cheiya na Sagilu. Alimwambia ampigie Chieya amuulize alikokuwa na Cheiya alimwambia ako kazini. Ngoswe alimwambia kwamba aliwaona Cheiya na babake,Sagilu, wakiwa mkahawani na wakaenda kufanya upelelezi. Mashauri alijionea babake akiwa na Cheiya na kwa uchungu na hasira akamkana Sagilu kama baba yake hapo. 

Alienda kumwona Ngoswe na Ngoswe akampa mawaidha kwamba wanawake ni wengi na hapaswi kujikwamisha kwa mmoja. Baada ya mazungumzo, Mashauri aliona kwamba hawakubaliani kimaoni na alitoka na kwenda kumwona Lonare ofisini akiwa na machozi. Alikiri yale yote maovu aliyoyafanya. Sauni alikuwa akimshuku lakini akatulizwa na Lonare. 

Baada ya wiki, Mashauri alihamia Majengo kwa kuhofia usalama wake. Watu walishangazwa na jinsi alivyobadilika. Alipoteza kazi yake lakini yeye hakujali. Sagilu alijaribu kunyang’anya mali lakini hakufaulu kwa sababu ya utetezi wa Mwamba. 

Lesulia alipoona kwamba umaaharufu wa Lonare pia unaongezeka, aliamua kuanza njama ya kuharibu umaaharufu huo na alitaka kuwatumia vijana kuleta vurugu lakini Ngoswe alipinga yale kwa sababu wengi wa vijana wale walikuwa marafiki zake. Lesulia naye kwa hasira akamfukuza Ngoswe akidhani hataenda lakini Ngoswe alitoka na kuwaacha. 

Mwandishi pia anatueleza kwamba Chifu Mshabaha alimtenga Mangwasha akazini kwa sababu ya kutofautiana kisiasi. Mangwasha alikuwa upande wa Lonare naye Chifu alikuwa upande wa Lesulia. Mangwasha aliandamana na Mrima kuenda kumpigia Lonare kampeni ambazo ziliona mikutano iliyojaa watu. Lonare kurudi nyumbani alimpata mwanawe Lombo amerudi utoka Ulaya. Mashauri alimsalimia Lombo na walijuliana hali. Walikuwa marafiki wa kitamb kwa sababu walikuwa wamesomea shule moja ya upili. Walijuliana hali na kuzungumza kuhusu kumbukumbu za kale na pia kuhusu hali ya siasa ilivyo. Walishirikiana katika kumfanyia Lonare kampeni.

Sagilu aliamua kumwomba mwanawe msamaha. Kwanza, aliamua kunena na Ngoswe na akampata katika hoteli ya Saturn. Ngoswe alimwongelesha kwa ukali na kumwambia kwamba angemwambia Lesulia amteme.Aliondoka jamo hili liliopfeli na akaamua kumkabili Mashauri ana kwa ana na akaenda hadi nyumbani kwake. Mashauri alikataa kumsamehe na akamfungia mlango. 

Siku iliyofuata, Mangwasha alielekea kazini na kupata amefutwa kazi. Walijibizana na Chifu Mshabaha ambaye alikuwa amemvuta kwa kazi aliyofanya na kumpigia kampeni Lonare.Alilipwa marupurupu yake ya kazini baada ya wiki moja na akajiunga na Mrima katika bishara ya duka. Akiwa katika shugli ya duka, alizidi kuwaona vijana jinsi walivyopotoshwa. Aliwahurumia kwa ile hali waliyomo.

Mangwash alipokuwa akijitayarisha kuenda kumfanyia Lonare kampeni, Mbulungu alimjia akimhimiza waende waone jinsi Sihaba alikuwa akiwafanyia watoto wa kike. Alimweleza alivyoona kule Sihaba alikokuwa akieneza biashara ya kuwashirikisha userati wasichana. Mangwasha alienda kuwaeleza Lonare na Mashauri yale waliyoyaona.  Lonare na Mashauri walishikana pamoja na maafisa wa huduma za vijana na kuelekea huko ambako waliweza kujionea walivyolezwa. Sihaba aliweza kukamatwa na wasichana wale pia walieweza kusaidiwa, ingawa wengine wao hawakutaka usaidizi huo. Ilijulikana kwamba wengine walikuwa wametoroka shule na hata wengine walikuwa wamewasilishwa pale na wazazi wao. 

Waliposikia kwamba Sihaba alikuwa ameachiliwa licha ya yale maovu alikuwa mefanya, Mashauri alienda kukabiliana na baba yake na akamwambia kwamba Sihaba akishikwa tena wao ndio watamshugulikia wenyewe ila si polisi. Uchaguzi wa uteuzi ulifanyika siku hiyo hiyo na mwamba alishika ugombea wa kiti cha eneo la Matango kwa Chama cha ushirika ilhali Sagilu hakushinda hata uteuzi huo. Mke wa Sagilu alimcheka kwa kushindwa kwake akimwambia kwamba kushindwa kwake kulisbabaishwa na tabia yake ya kunyang’anya watu mali.

Ilipobakia miezi minne uchaguzi ufanyike, Sagilu aliruka kichwa. Mangwasha na Mbulungu walimwona siku moja huku akifuatwa na umati wa watoto waliomcheka kwa yale aliyoyafanya barabarani. Mangwasha alimjulisha Mashauri hali ya baba yake huku asijali.  Baadae, Mashauri walipatana na Lombo katika mkahawa mmoja na walizungumza kuhusu mambo kadhaa, moja ikiwemo Nanzia, mkewe Lesulia. Lombo alimweleza kwamba Nanzia alikuwa ameshikwa na ugonjwa wa kuchanganikiwa kwa kupokonywa mali iliyokuwa mali ya umma.Walinena kuhusu kisa cha Wafaransa walivyowakata vichwa viongozi wao walipowaudhi watu. Mfalme huyo akiwa Luois wa Kumi na Sita na mkewe Antoinette. Katika kati ya mazungumzo haya, Mashauri alipokea simu kutoka kwa Lonare aliyemeweleza kwamba hali ya babake Sagilu ilikuwa imedhoofika zaidi. Kwa ushawishi wa Lombo, Mashauri alikubali kumsaidia baba yake kwa kumpeleka hospitalini na kumwachia Lombo ashugulikie matibabu yake.

Alipopata nafuu, Sagilu aliongea na Mashauri tena na ingawa Mashauri alihisi uchungu na chuki, aliamua kumsikiliza. Sagilu alikiri kwamba alichomfanyia mwanawe ni jambo mbovu sana na jinsi kupokonywa mali kilivyomtia kichaa. Mashauri alimwaga bila kujali hisi zake. 

Chifu mshabaha alipigwa kalamu kwa kazi mbaya ya utawala aliyoufanya. Alikuwa pia akifuatwa na maafisa wa serikali kwa kukosa kulipa ushuru ipasavyo. Alienda kumtafuta Mangwasha katika ofisi yake ya kushugulikia vijana wa mitaani. Alimwomba Mangwasha usaidizi ili apate mkopo aweze kulipa ushuru lakini Mangwasha alikataa na kumfukuza na baadaye kumwelezea Mbulungu yaliyojiri.

Baadae, vyeti vya uteuzi vilipewa wagombeaji na Lonare alipoenda kuchukua cheti chake, alifuatwa na umati kubwa. Katika umati huo, Lonare aliweza kumwona dada alijaribu kumwua kwa wakati mmoja na Mashauri aliweza kumtambua dada huyo kama Cheiya. Mashauri pamoja na umati waliweza kumkimbiza Cheiya hadi akaishikwa. Katika sherehe zao, Ngoswe alipokea simu na kuelezwa kwamba Nanzia likuwa hospitaini hali mahututi. Alipoenda, Nanzia alitaka kumwongelesha yeye pekee yake. Alimweleza kwamba babake halisi ni Sagilu na akaaga dunia. Ngoswe alifululiza hadi kwa Sagilu ili kuhakikisha yale aliyoambiwa na aliambiwa kisa ya yote yaliyojiri. Lesulia hangepata mtoto na Nanzia. Mtoto wa kwanza wa Nanzia alikuwa Mhindi na walifukuzwa pamoja na baba yake. Baada ya hayo, Nanzia na Sagilu walikuwa na uhusiano wa karibu ambao baadae ulikuwa chanzo cha Ngoswe kuzaliwa. Ngoswe alienda na akumjulisha Mshauri kwamba wao ni ndugu kamili. Baada ya mazishi ya Nanzia, mashauri na Ngoswe alimpeleka Sagilu hospitalini kwa sababu hali yake ilizidi kuzorota. 

Mangwasha aliweza kujiskia redioni akitajwa kama mmoja wa wananwake walio leta mabailiko nchini mwao.

Nguu za jadi Sura ya Sita

Sura hii inaendelea kutoka sura ya tano ilipowachia. Uchaguzi ulipokaribia, Lonare anapotea tena. Hakuna aliyejua Lonare aliko. Lesulia na watu wake walianza kusherehekea wakijua kwamba hakuna upinzani. Mangwasha na Mrima waliwapata wageni wengi siku moja kabla ya uchaguzi. Watu walianza kupoteza imani kwamba angetokea tena lakini kuna waliendelea kutia watu moyo kwamba awe ama asiwe wampigie kura tu. Usiku huo, Mangwasha alikuwa amevunjwa moyo kwa sababu bado hakuna aliyejua Leonare alikokuwa. Mrima alijaribu kumtia moyo kwa kumwambia akubali ukweli ambao walikabiliana nao, kwamba kuna uwezekano Loanre hangerudi.

Asubuhi ya siku ya kupiga kura, Mangwasha na Mrima walirauka ili wasikabiliane na mlolongo wa watu wakienda kupiga kura. Walipoenda kutoka, hapo mlangoni mwao walimwona Lonare amelala chini. Walishtuka na majirani waliwasili pale kujionea yaliyomo. Watu hawakumkaribia Lonare hadi wakati ule alipojaribu kujiamsha ndipo wakaenda kumsaidia. Simu zilipigwa katika stesheni za Matuo ili kuwasilisha ujumbe kwamba Lonare alikuwa ameatikana. Wafuasi wake walijikakamua ili kwenda kupiga kura huku Lonare akipelekwa hospitalini. 

Lombo na wenzake , miongoni mwao Ngoswe walibaki pale hospitalini kumwangalia Lonare. Lonare alipomwona Ngoswe alifurahia na alinena naye na kumpa mawaidha kwamba angefaa kuwacha biashara yake ya madawa ya kulevya. Ngoswe aliahidi kwamba angewacha biashara hiyo. Lombo, Ngoswe na Mashauri walinena kuhusu jinsi madawa haya yanatumiwa kuwa filisisha watu wa nchi ndogo kwa utafiti wa kampuni kubwaza kemikali.

Lesulia alihisi kukasirishwa na habari za kupatikana kwa Lonare na alimpigia Sagilu kumtetesha kwamba vijana wake walikuwa wamefanya kazi ya upuzi. Mangwasha naye baada ya kupiga kura, alirudi kule hospitalini ambapo aliambiwa kwamba Lonare alikuwa amepata nafuu. Stesheni za kupiga kura zilifungwa saa kumi na mbili. Siku iliyofuata, matangazo yalianshiria kwamba Lonare alikuwa amekaribia ushindi. Lesulia alipofikiwa a habari kwamba angeshindwa, alianza kuwalaumu jamaa wake amabo walikuwa wamekusanyika kwake.

Sagilu alianza kubugia mvinyo aliposikia kwamba Mwamba ndio aliyeshinda ugombea wa kiti cha eneo la Matango. Alikumbwa na mawazo wengi. Baadae akaambiwa na mkewe kwamba Lonare ndiye aliyeshinda. Alijawa na hasira na hofu akawakemea Mashauri na hata Mangwasha kwa kumuunga mkono Lonare. Lesulia naye akageuka kwa kusikia habari hizi na kusema kwamba hata hakuwa anataka uongozi tena kwa sababu ulikuwa umemchosha. Wafuasi waa Lonare walionekana wakisherehekea. Walijitokeza kwa uwanja ulio karibu na maskani yake. Lonare alitoa tangazo rasmi huku akisaidiwa na Lombo na Mashauri kufika jukwaani. Alihutubia watu kuhusu jinsi alitaka kubadilisha nchi yao. Alikiri kwamba ufisadi ulikuwa umekithiri na akasema kwamba ilikuwa kazi yake kukumbana nayo na wafisadi mpaka atakapomalizana na kuisafisha nchi yao. Hotuba hiyo pia iliongelea jinsi wazee wangefaa kuheshimiwa kwa sababu ndio walio na ujuzi na uzoefu wa maisha. Aidha , pia aliongelea jinsi watu wanapaswa kujua kujiongoza kimaisha na wajue kukataa maovu katika jamii yao. Hotuba yake ilisifika hadi nchi jirani na sifa za Lonare zikaenea zaidi, hasa za tabia zake nzuri.

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Jalada, Anwani, Dhamira ya Mwandishi na Muhtasari wa Nguu za Jadi - Mwongozo wa Nguu za Jadi.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Read 28502 times Last modified on Wednesday, 24 May 2023 07:43
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?