Dhana na Maudhui - Mwongozo wa Nguu za Jadi

Share via Whatsapp

 

Riwaya hii inazingatia maswala kadhaa ya jamii na kujaribu kuonyesha jinsi yanavyoathiri maisha ya wananchi kupitia wahusika wake.

Maswala haya ni kama:
  1. Ukiukaji wa mila na jadi za kijamii
  2. Usaliti
  3. Nafasi ya mwanamke katika jamii
  4. Familia na ulezi yanavyoathiri jamii.
  5. Mabadiliko
  6. Uozo wa maadili - maudhui haya yanajitokeza kwa vipengele kadhaa kama vile:
    1. Utabaka
    2. Ukatili
    3. Ukabila
    4. Ufisadi
    5. Uongozi mbaya
    6. Tamaa na ubinafsi
    7. Usherati na anasa

Ukiukaji wa jadi na mila za kijamii

Kulingana na anwani, haya ndiyo maudhui makuu ya riwaya hii. Maudhui haya yanajitokeza kwa maisha ya mhusika mkuu pamoja na wahusika wengine ambao inawabidi wakiuke jadi ili waweze kuboresha maisha yao.

  1. Mangwasha alipewa mawaidha ya kwamba anapaswa kuweza kujikimu ili asitegemee mwanaume, jambo ambalo linamfanya kutamani kusoma na hata kutafuta kazi ili aweze kujikimu kimaisha.
  2. Mangwasha pia anakataa kumwoa Sagilu na anajichagulia bwana yeye mwenyewe, jambo ambalo lisilo la kawaida kwa jamii yao. Anamkataa Sagilu na hata kujibizana naye, huku asiweze kuficha jinsi anavyomkera.
  3. Hata baada ya kutukanwa na kukejeliwa kwa kusudi la kumwoa Mrima na Chifu Mshabaha, Mangwasha anajeieleza kwa Chifu kwa ustadi na baadae juu ya kuweza kujisimamia, anahofia kwamba ata angefutwa kazi.
  4. Mangwasha anakwenda kumtafuta bwana yake licha ya kuonywa na Bi Mbulungu kwamba mke hafai kuenda kumtafuta bwanake akiwa raha zake. Swala hili linarudiwa na Mrima pale Mangwasha anapomuuliza kule alipokuwa amepotolea “….Koma hapo! Tangu lini mke kamuuliza mumewe kule aendako na atokako?...”(uk 40)
  5. Mangwasha anajihusisha na nafasi za uongozi kwa nia ya kubadilisha jamii yake. Mangwasha ana uhusiano wa karibu na Lonare na wanasaidiana na kushauriana katika mambo ya kisiasa na yanayoendelea nchini mwao. Licha ya Mangwasha kujua kwamba nchi hiyo imejazwa na ubabedume.
  6. Aidha, Mangwasha pia anaonekana kwa fikira zake kwamba anatamani kama angeweza hata kumwongelesha Mtemi Lesulia kuhusu yale yanayowakumba wananchi.
  7. Pia, Mangwasha anaonekana baadae kuanzisha vikundi ambavyo vina nia ya kuwasaidia vijana ambao wamepotea ili waweze kujikimu. Jambo la kuwapa vijana, haswa wanaume matumaini na njia ya kuishi inasemekana kuwa kazi ya baba wazazi katika jamii.
  8. Lonare anawaelimisha watoto wake wote, wa kike na wakiume bila ubaguzi, jambo ambalo lisilo la kawaida katika jamii.
  9. Mangwasha pia analazimika kuwalea watoto wake , pamoja na bwanake Mrima pale anapohitaji usaidizi wa kuwachana na ulevi. Anawalea watoto wake kivyake na watoto wake wanabaki wakimtambua kwamba yeye ndiye mzaze pekee. Tunaelezewa kwamba ilikuwa imefika kiwango ambacho hata watoto hawakuuliza kule baba yao alipo.
  10. Licha ya Cheiya kuwa yatima, amaweza kusoma na kufuzu shuleni na hata kuwa muuguzi.\
  11. Baada ya kubembelezwa kwa muda, Mrima anakubali kurudi nyumbani na kuangaliwa na bibi yake hadi atakapoweza kujikimu.
  12. Kulingana na kisaasili ya Sayore, Lilith alikikuka maagizo ya Adamu na hata kumtoroka ili kusababisha Mungu amtengeneze Hawa.

Mabadiliko/ mapinduzi

Aidha, kuna mifano nyingine nyingi ya ukikukaji na kuwaza kupambana na nguvu zilizo na mtu kuweza kufanya yale yasiyo ya kawaida. Mfano:

  1. Mrima anaweza kuachana na ulevi mara ya kwanza, na baada ya kuingia ulevini mara ya pili, anauwacha kabisa na hata kuweza kuanza na kumeesha biashara kwa bidii zake.
  2. Licha ya kuwa na adui na wahasi wengi, Lonare anaweza kufaulu kuwa Mtemi wa nchi, na hata baada ya kupigwa na kuteswa.
  3. Licha ya kuwa na uhusiano wa karibu na Mtemi, Sagilu anabaki kupoteza kila kitu, kuanzia kwa mwanawe , mali na hata fahamu zake.
  4. Mtemi Lesulia anapoteza cheo chake licha ya kupanga ukatili dhidi ya Lonare na hata kuleta vurugu.
  5. Mashauri anamgeuka baba yake baada ya kumpata na Cheiya, mwanamke ambaye alikuwa anataka kumposa. Anamgeuka kamili n ahata kuungana na adui zake kina Lonare, baada ya kukiri maovu aliyoyafanya.
  6. Ngoswe pia anamgeuka babaye, Mtemi na pia anakiri kuacha biashara ya dawa za kuelvya.
  7. Sagilu anawomba mwanawe msamaha na kukiri uovu wake, jambo lisilotarajiwa kulingana na ukatili wake.
  8. Chifu Mshabaha anapoteza kazi yake na kuongezea anaanza kusakwa kwa kuwa na deni ya kutolipa ushuru.
  9. Licha ya kuwa na nguvu ya fisidi walivyotaka, Mtemi Lesulia na wenzake wanashindwa kuweka mali yao na hatimaye, wengi wao wanapoteza yale waliyo nayo.

Usaliti

  1. Mrima anaisaliti familia yake kwa kukosa kuwalea vyema. Anapopewa pesa na Sagilu anaelekea kunywa na hata barua inapatikana kuonyesha kwamba alisaliti ndoa yake na Mangwasha kwa kuwa na mpenzi wa kando.
  2. Mrima anawasaliti Waketwa wenzake kwa kukubali kuchukua lungula ili kumfanyia Sagilu na Lesulia kampeni
  3. Sagilu anamsaliti mwanake kwa kunyemela Cheiya, huku akijua Mashauri alitaka kumposa
  4. Cheiya anamsaliti Mashauri kwa kukubali kuhusiana kikaribu na babake Sagilu, na hata baadae tuanelezwa alikuwa katika njama ya kutaka kumuua Lonare.
  5. Mashauri anamsaliti babake kwa kumwacha anapompata na Cheiya. Anakiri yote mabaya aliyofanya kwa kina Lonare n ahata kumtishia kulipua kila kitu magazetini na katika vyombo vya habari
  6. Mtemi Lesulia anawasaliti wananchi wa Taria kwa kuwacha ufisadi na uovo ukithiri nchi nzima. Anaonekana kuwa kwenye njama za ukatili na za ufisadi.
  7. Mkewe Sagilu anamtoroka pindi hali yake ya kiakili inapozorota
  8. Sagilu na mkewe Lesulia wanamsaliti Lesulia kwa kumficha kwamba Ngoswe si mwanawe. Ngoswe anaambiwa habari hii mama yake anapoelekea kufariki.
  9. Ngoswe anawasaliti baba yake na wenzio kwa kujiunga na kina Mashauri kuwafanyia Lonare kampeni.
  10. Serikali ya Lesulia inamsaliti wakili wao anaposhindwa kesi ya ardhi na kumfuta kazi. Aidha pia jaji mkuu anasalitiwa na swerikali licha ya kuwa mwenye haki na kuwapa wakaazi wa Matango ardhi yao ipasavyo.

Nafasi ya Mwanamke katika jamii/ Jadi na mila za kijamii kuhusu wanawake

  1. Mwandishi anatueleza kwamba jamii iliyo Taria ilikuwa imejaa ubabedume. Nafasi ya mwanamke ilikuwa chini ya mwanaume Dhana hii inatolea pia na fikra na uzungumzi nafsiya wa Mangwasha ambapo anajiuliza kama mwanamke kama yeye angeweza kumwongelesha Lonare ama Mtemi Lesulia.
  2. Mwandishi pia anatueleza kwamba Mangwasha alitaka kuongea na Mtemi lesulia na Alipomtajia Mrima lengo lake, alidhani mek wake karukwa na akili.
  3. Mwandishi anatueleza pia kwamba Mnangwasha alifikiria kwamba nafasi ya mwanamke ni kusikiliza na kutenda wala si kusikilizwa na kutenda (uk11)
  4. Mbulungu nanmwambia Mangwasha kwamba mwanamke haendi kumtafuta bwanake akiwa raha zake.
  5. Mrima anapokabiliwa na Mangwasha anamuuliza Mangwasha tangu lini mwamake kamuuliza mwanamke aendako wala kule atokako. Pia anamkwekelea kwamba kazi ya wanawake ni kelele tu.
  6. Lonare alijitolea kuwasomesha watoto wake wote jambo linaloonekana lisilola kawaida kwa sababu hakuna wataalamu wengi Taria wanawake. Kwa kisa chote, wanawake watatu pekee ndio walihitimu: Mangwasha katika chuo cha uhazili, Lombo kama daktari na Cheiya kama muuguzi.
  7. Wanawake pia wanaonekana kutumiwa na wanaume. Sagilu anawatumia wanwake kama vile Sihaba na Cheiya kufanya njama zake.Vile vile, Mbwashu anatumiwa na Mtemi Lesulia kufanya njama zao pia.
  8. Sihaba anawatumia wasichana wadogo kwa usherati.
  9. Mangwasha napowaangalia vijana wa mtaa wao, anawaona kwamba wasichana wadogo wamebaki kuomba omba huku wakiwabeba watoto wao mgongoni.
  10. Wamewachiwa kazi za kuzilea familia zao kivyao jinsi alivyoachiwa na Mrima awalee watoto wakekivyake kwa muda.
  11. Nanzia naposhindwa kumzalia Lesulia mtoto, Lesulia anataka kumpa talaka ila kwa ushawishi wa Sagilu.
  12. Wanawake wanatumiwa kuendeleza anasa ya wanaume ka vile Sagilu na Ngoswe.
  13. Wanawake wanapaswa kutii masharti ya wanaume. Dhana hii inaonyesha na kisa cha Lilith ambaye anasemakana kuwa mwovu kwa kukataa kutii masharti ya Adamu.

Uhusiano wa kifamilia na malezi ya watoto katika jamii

Mwandishi anazingatia jinsi familia za wahusika zilivyo.

  1. Familia ya Mangwasha.

    • Mangwasha na Mrima wana watoto wawili ambao baada ya Mrima kuingia katika ulevi, mangwasha analazimika kuwalea katika upweke. Aidha, mangwasha bado anampenda Mrima na ang’ang’ana kumtafuta ili waiweke familia pamoja.
    • Kwa mapenzi na kuangaliwa na bibi yake, Mrima anaweza kurudisha mwelekeo wake kuwa sawa na hata kuanzisha biashara ili kuikimu familia yake.
    • Malezi ambayo Mangwasha alipata kutoka kwa wazazi wake ndio yalimfanya awe jinsi alivyo, mwenye bidii. Alilelewa kujua kujitegemea na kujikimu kimaisha na hata kutaka kuwaangalia vijana wengine waweze kujikimu.
  2. Familia ya Lonare

    • Lonare anajitolea kuwalea watoto wake kiadilifu na kuwasomesha wote bila ubaguzi. Baadae , tunawaona wote wanavyokuja kuchangia katika shugli za kisiasa za baba yao na hata jinsi wanavyo waathiri wenzao vyema kama vile Mashauri na Ngoswe.
    • Kwa kujitolea kuwalea watoto wake, Lonare wamewaekea maadili yanayowafanya kuwa watu wema wanapokuwa wakubwa, nao pia wanajitolea kumsaidia baba yao kwa kampeni zake.
  3. Familia ya Sagilu

    • Sagilu anaisha kwa raha zake na kwa anasa zake. Mwandishi anaitaja familia ya Sagilu katika sura za mwisho za kitabu.Hapo awali, mwandishi anatueleza tu jinsi Sagilu alikimbizana na wanawake wengi licha ya kuwa na bibi. Hahusiani na familia yake kwa karibu. Umaarufu wa Sagilu unapopungua ndipo tunaona akihusiana na faimilia yake. Hata hivyo, si uhusiano mzuri kwa sababu anamnyemelea mwanamke aliyeposwa na mwanake Mashauri na kuleta utengano kati yao. Aidha, anapopatwa na kichaa, mke wake anamtoroka kwa muda.
    • Mwandishi hautelezi kwamba mke wake amemsaidia katika kampeni ama shughuli zake zozote ila anaposhindwa kwa ugombea wa kiti cha chama, mke wake anamcheka ingawa ni kicheko cha uchungu. Ilhali mke wake anatambua tabia zake za kibinafsi na kujinyakulia mali, hajampa mawaidha wala kumwambia awache ila tunamwona anamwambia ndio sbabu kuu yake kushindwa.
    • Kwa upande mwingine, Mashauri anamkana baba yake kwa maovu anayomtendea. Anamkana na hata kuenda kuungana na mahasidi wake. Sagilu anapokuwa mgonjwa na hata anapomwomba msamaha Mashauri, mwandishi anatueleza kwamba hisia za Mashauri hazikubadilika.
    • Baadae, mwanawe wa siri, Ngoswe, anapojua kwamba Sagilu ni baba yake anamkabili lakini jambo hili halibadilishi uhusiano wao na kuwaleta pamoja, ilhali inawaleta pamoja Ngoswe na Mashauri. Pia, tunamwona Ngoswe akiwa na tabia za anasa sawa na zile za Sagilu na baadae anabadili mwendo , sawa na Mashauri.
  4. Familia ya Lesulia

    • Familia ya lesulia imekumbwa na ubinafsi. Lesulia amejilimbikizia mali na kueneza ufisadi na ubinafsi unaokithiri moaka kwa familia yake. Tuaneleza kwamba Ngoswe alikuwa hana kazi ila alikuwa natoa pesa zake kwa zile nyumba za bab yake alizotoza kodi. Aidha, nanzia pia alikuwa mejilinyakulia mali ya serikali.
    • Familia ya Lesulia inaisha kwa umoja pia. Tunaelezewa kwamba ndugu yake mkubwa Ngoswe alikuwa si mtoto halisi wa Lesulia. Pia, Ngoswe anatambulishwa kwamba baba yake halisi ni Sagilu, na baada ya kujulishwa haya, Nanzia anafariki. Isitoshe, kabla ya haya, Lesulia alikuwa amekosana na mwanawe Ngoswe n kumfukuza.

Uozo wa maadili

Kila kipengele katika maudhui haya pia yanaweza kujisimamia kama maudhui kivyake pia. Maudhui haya yanahusiana na amovu ambayo yanafanyika katika jamii ya wahusika wa riwaya hii. 

  1. Ukabila

    1. Wakule wamejinyakulia nafasi zote za uongozi katika nchi na kuwaachia Waketwa wakiwa hohe hahe
    2. Waketwa wanafilisishwa kwa kuwa ni watu wa jamii tofauti na wakule
    3. Waketwa wanaekelewa mambo mabaya yanapofanyika katika nchi yao kama kuwa na mvua nyingi ama kidogo.
    4. Wakule wanapata kazi za kifahari ilhali hawajahitimu, huku waketwa waliohitimu kukosa kazi.
    5. Waketwa wanaandikwa katika nafasi za chini za kazi katika mashamba na viwanda vilivyomilikiwa na wakuleMtaa wa matango unateketezwa ili kusababisha waketwa wahame na kuruidhwa Ndengoni, kule ambapo wengi wa jamii yao wanapoishi.
    6. Wengi wanaohusika na Mtemi Lesulia ni Wakule wenzake kama vile Sagilu, Chifu Mshabaha, Mbwashu na wengineo.
  2. Ufisadi

    1. Tunaelezwa kwamba Sagilu aliweza kupata mali na mashamba yake kwa njia zisizofaa, za kifisadi.
    2. Wakule wengi walio katika nafasi za uongozi wanaeneza ufisadi na kujinyakulia mali ili kujiendeleza kimaisha
    3. Sihaba anatolewa jela bila kwa yeyote kujua ilhali anapaswa kuwa amefungwa. Jambo hili linafanyika mara mbili kwa riwaya hii. Mara ya kwanza,a nashikwa kwa kusambaza vijikaratasi ambavyo viliwaarifu wakaazi wa Matango kwamba wanapaswa kuhama. Mara ya pili, alishikwa kwa kuwatumia wasichana wadogo katika njia isiyo haki.
    4. Sagilu anampa Mrima mlungula ili aweze kuwafanyia kampeni lakini baada ya ushawishi, Mrima na anamgeuka Sagilu.
    5. Sagilu na Mtemi Lesulia walikuwa wamepanga njama ya kuwanyima wakaazi wa Matango vyeti vyao vya ardhi ili waweze kujenga soko kuu eneo hilo na kujiendeleza kifedha.
    6. Kwa kuwa wafisadi, Wakule waliwaandika watu wasiohitimu katika nafasi za juu za kazi kama vile madaktari, rubani na nahodha na kusababisha hasara kubwa nchini
    7. Sagilu ako huru hata baada ya kisa cha maziwa ilisababisha watoto kuwa wagonjwa.
    8. Mbwashu na Sihaba wanajulikana kueneza njama za ufisadi pamoja na wengine walio katika uongozi. Wanajulikana kuwa na mali ambayo wameipata kwa kufisidi kwa kiwango ambacho Lesulia anaposhindwa katika uchaguzi, Mbwashu anatorokea nchi nyingi ili kuukibia mkono wa serikali.
    9. Ngoswe anashiriki biashara ya dawa za kulevya na hawezi kufunguliwa mashtaka kwa sababu ya baba yake na wale anaofanya nao biashara , ambao ni watu wakubwa duniani.
    10. Kwa maagizo ya Sagilu, Mashauri anabomoa nyumba ya Lonare, jambo analokiri pale wanapokasana na baba yake na anaenda kujiunga na kikundi cha Lonare.
  3. Uongozi Mbaya

    1. Mtemi Lesulia anakubali ufisadi ukite nchini mwake. Mtemi anahushwa na njama za ufisadi na ukiatili nchini mwake. Anajulikana kuwa kiongozi katili.
    2. Chifu mshabaha alifutwa kazi kwa kueneza uongozi mbaya katika eneo lake. Anajulikana kutolipa ushuru a hata kujilimbikizia mali. Pia, anaeneza njama za kifisadi.
    3. Mrima anashindwa kuchukua usukani wa kuiongoza familia yake na kumlazimu Mangwasha kuchukua hatua ya kuwa 'baba na mama' kwa watoto wao.
  4. Utabaka

    1. Wananchi wa Matuo wamejitenga kwa matabaka. Walio tabaka la juu sana wanaishi Majuu. Kufuatia Majengo halafu Matuo. Waliojipoteza kabisa na walio kwa tabaka la chini wanaishi Ponda Mali na Majaani.
    2. Wengi wa watoto wa walio tabaka la Kati na la juu wamesoma na kuhitimu vizuri kv Mashauri, Lombo, Sauni na Sagura ilhali walio tabaka la chini wanaonekana kuwa ni kama wamepotea. Wanajihusiasha na mihadarati na kuomba omba. Hata Ngoswe asiye na kazi na anayeshiriki anasa na biashara ya dawa za kulevya, anashiriki vile lakini kwa kuwa yeye ni mtoto wa Lesulia hajafikia kiwango cha kuishi maisha ya walio Ponda Mali au Majaani.
    3. Ufisadi unawakithiri walio katika tabaka za juu. Wengi wao wakiwa katika jamii ya Wakule, wamejilimbikizia mali na kwa ufisadi na ubinafsi wao. Mashauri anapokosana na baba yake, anaondoka Majuu na kuenda kuishi Majengo kwa kuhofia maisha yake. Jambo hili pia ni taswira ya kwamba Mashauri amewacha ukatili na hali ya maisha yake ya awali.
  5. Ukatili

    1. Lesulia ni katili kwa uongozi wake. Anaongoza kwa mkono wa chuma.
    2. Sagilu anaeneza ukatili kwa biashara zake. Anawatumia watu kama Sihaba kushugulikia wale wanaoshindana naye kibiashara.
    3. Sihaba alitumwa kujaribu kulipua harusi ya Mrima na Mangwasha na nia inaweza kuwa ilikuwa kifo kwa mmoja wao.
    4. Wakaazi wa Matango wanachomewa makao yao usiku na baadae wanafukuzwa kwa njama ya kuwanyang’anya ardhi ili lesulia na wenzake wajenge soko kuu.
    5. Cheiya alitumiwa kujaribu kumuua Lonare.
    6. Lonare anateswa uchaguzi unapokaribia kwa nia ya kumfanya akose kushinda uchaguzi.
    7. Mashauri alikuwa anajulikana kama katili aliyebomolea watu nyumba jinsi alivyoweza.
    8. Chifu Mshabaha anamfuta kazi Mangwasha kwa sababu ya kutofautiana kisiasa.
  6. Tamaa na ubinafsi

    1. Cheiya anabadili maisha yake pindi anapoanza kupata pesa. Kwa maelezo ya mwandishi, hatosheki na anataka zaidi.
    2. Sagilu anazidi kujilimbikizia mali na kuwanyang’anya wengine mali yao, jambo linalomfanya kupoteza uchaguzi.
    3. Mrima hangeweza kukataa mlungula alizopewa na Sagilu kwa mara ya kwanza na hata ya pili. Nia yae ilikuwa ajiendeleze kwa anasa zake mara ya kwanza na kuikimu familia yake mara ya pili.
    4. Tamaa iliwafanya Wakule waharibu rasilimali za taifa yao bila kujali vizazi vya mbele au jinsi walivyoathiri mazingira yao.
    5. Mtemi Lesulia, Mbwashu na Sagilu walishirikiana kwa njama ya kuwanyang’anya wakaazi wa Matango makao yao ili wajenge soko kuu.
  7. Usherati na Anasa

    1. Mrima alingukia maisha ya anasa na kujitosa ulevini, jambo linamfanya kuiwacha familia yake, asitake jua jinsi walivyo. Barua lililopatikana na Mangwasha pia linaashiria kwamba Mrima alikuwa na mpenzi wa kando ulevi ulipokuwa umekithiri.
    2. Cheiya pia anabadilisha maisha na kupenda anasa, jambo linalomfanya kukosana na Mashauri kwa uhusiano aliokuwa nayo Sagilu.
    3. Sagilu pia anajulikana kupenda anasa, hasa kwa kuwatumia wanawake jinsi anavyopenda.Anashiriki usherati na wanawake wengi, jambo linalomfanya kujulikana kwa tabi yake mbovu na hata kufikia mahali anampokonya mwanawe Mashauri mwanamke aliyemposa.
    4. Ngoswe pia anaonekana kupenda anasa. Tunaelezwa kwamba hana kazi na alishindia usherati na ulevi, huku pia akifanya biashara ya kuuza dawa za kulevya.
    5. Sihaba anashikwa kwa kuwatumia wasichana wadogo visivyo. Ingawa mwandishi hatuelezi, anatoa dhana ya usherati ambayo Sihaba anaeza kwa faida yake.

Elimu 

Mwandishi anazingatia jinsi elimu na kuwa na utaalam unavyokuwa na umuhimu katika jamii. Elimu unasaidia kujenga jamii. Dhana hii inaonekana kwa mifano kama:

  1. Mangwasha aliweza kusomea uhazili ili aweze kuikimu familia yake.
  2. Nyumba yao inapochomeka, anatafuta vyeti vyake vya shule kwa sababu ndio aliaminia zingemsaidia maishani
  3. Lombo kama daktari anaweza kuwashugulikia Sagilu na Lonare.
  4. Mashauri ni mtaalamu wa usanifu wa ujenzi, jabo linalompa kazi kwa serikali ya Lesulia. Katika kazi yake anaifanya kuwa kuielewa vizuri. Aidha, anapowachana na baba yake, anawacha pia kazi yake.
  5. Cheiya anawezakuhitimu masomo na kuwa muuguzi na anaweza kujikimu kwa muda , kabla hajapendana na anasa.
  6. Mwamba ni msomi wa sheria na anaweza kuwatetea wakaazi wa Matango wabaki kumiliki ardhi yao.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Dhana na Maudhui - Mwongozo wa Nguu za Jadi.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?