Wahusika: Sifa na Umuhimu wao - Mwongozo wa Nguu za Jadi

Share via Whatsapp

WAHUSIKA: SIFA NA UMUHIMU WAO

Riwaya hii ya Nguu za Jadi ina wahusika kadhaa. Wahusika wengi waliotajwa wana uhusiano wa karibu na mhusika mkuu.

Mangwasha

Huyu ndiye mhusika mkuu wa riwaya hii. Mangwasha ana uhusiano na wahusika wengi kama vile Kajewa na Sayore ambao ni wanawe,bwanake Mrima, rafikize Bi Mbulungu na Lonare, Chifu Mshabaha amabaye amemwandika kazi na pia Sagilu amabye ameishi kumtamani. Kulingana na jinsi anavyo husiana na wahusika wengine tumeweza kupata sifa zake na pia za hao wahusika wengine.

Sifa:

  1. Mwenye bidii – Mangwasha anatia bidii shuleni ili na hata kazini ili aweze kujikimu kimaisha, asimtegemee mwanaume. Ana bidii pia kazini, jambo ambalo mwandishi anatueleza ilikuwa sababu kuu ya Chifu Mshabaha kushindwa kumfuta kazi.
  2. Mvumilivu - Licha ya yote ambayo Mrima anampitisha ama yale anayopitia kazini kwa mikono ya Chifu Mshabaha na hata Sagilu, Mangwasha hajafa moyo. Hata baada ya kuachwa na Mrima, anazidi kumwombea awe pema pahali alipo na hata baadae anaenda kumtafuta na kumshugulikia ili aw mwenye afya tena.
  3. Mwenye haki – Mangwasha anasimama na Waketwa wenzake na kusaidia kulilia haki zao. Anaficha pia bahasha ya mlungula ya Mrima ili asiweze kujiingiza kwa shida tena na kina Sagilu. Pia anasaidia kupata ushahidi ambao ungewasaidia wakaazi wa Matango kurudishiwa ardhi yao na kusambaritsha mipango ya kujenga soko kuu.
  4. Hana ubinafsi- Anajitolea jinsi anavyoweza kuwasaidia walio karibu na yeye. Anajitolea kumtunza Mrima, Licha ya Mrima kuwa mlevi. Anajitolea kumsaidia Lonare katika kampeni licha ya kwamba kitendo hiki kingeweka kazi yake hatarini. Anajitolea kuwasaidia vijana ambao wamepoteza mwelekeo maishani.
  5. Jasiri – haogopi kusema lile lililo akilini mwake ama kufanya lile lililo haki ingawa kitamweka matatani. Anajibizana na Chifu kuhusu kuolewa kwake. Anamkemea Sagilu kwa tabia zake na kukataa mlungula yake hata alipokuwa hana pesa. Sagilu anapotokea stesheni Sihaba alipofungwa, Mangwasha alikuwa amfuate na watu wengine wakiwa nyuma yake lakini Sagilu akatoroka. Haogopi kwenda kumtafuta Mrima katika mitaa ambayo haina usalama.
  6. Mwenye huruma – Anawahurumia vijana ambao walipotea kwa sababu ya kukosa maelekeo maishani
  7. Mwenye upendo – Anampenda Mrima na hata kuenda kumtafuta kule alipopotelea. Anawapenda Watoto wake na hata kujitolea kuwachunga vile anavyoweza. Licha ya kujibizana na Chifu kwa sababu ya harusi yake na mrima, bado anamwalika Chifu harusini.
  8. Mzalendo – anasaidiana na Lonare kupigania haki za Waketwa wenzake na pia nchi yote kwa kumpigia kampeni Lonare.

Umuhimu wake:

  1. Mwandishi anamtumia Mangwasha kuonyesha jinsi wananchi wanapaswa kuwa katika taifa lao. Mangwasha anatumiwa kuangazia yale mazuri ambayo tunafai kuyatenda licha ya yale mabaya yanayofanyika katika mazingira yetu. Anatumia kutuonyesha jinsi tunapaswa kutunza familia yetu, jamii yetu na pia nchi yetu kwa kusimama kwa haki na kuwa ujasiri kwa yale yaliyo mema.

Mrima

Mrima ni bwanake Mangwasha. Ndiye baba ya Sayore na Kajewa. Mrima anapitia mabadiliko mengi katika riwaya hii mabayo yanayotusaidia kujua sifa zake.

Sifa

  1. Mwenye bidii – Mrima anapopatana na Mangwasha , anajulikana kuwa mwenye bidii kazini. Aidha, baada ya kupata nafuu anapowachana na ulevi, anaanzisha biashara ya kuuza mboga na kwa bidii yake, biashara hiyo anaikuza hadi kiwango cha kuwa duka kubwa ya kuuza bidhaa kadha wa kadha.
  2. Mpenda anasa – Mrima anapotelea kwa ulevi pale anapoanza kuwa mlungula na Sagilu badala ya kuikimu familia yake.
  3. Msaliti – Anaisaliti familia yake kwa kuiwacha matatani na pia kuisaliti jamii yake pale anapokubali lungula kutoka kwa Sagilu kuwafanyia kampeni Sagilu na Mtemi Lesulia.
    Pia anamsaliti mpenzi wake Mangwasha kwa kuwa na mpenzi wa kando, jambo tunalolijua kupitia barua aliliandikiwa.
  4. Mbinafsi – Anakataa kuwatunza familia yake huku akisema “mimi mjinga niwache mapesza haya yote bila kujifaidi?..”(uk 37)
    Pia baadae anakiri kwamba alikubali mlungula wa Sagilu ili aweze kujiendeleza kimaisha.
  5. Mwoga – Anaogopa kukumbana na mambo yaliyomjia ana kwa ana. Baada ya kupatana na Sagilu kabla hajamwoa Mangwasha, anaanza kumtoroka ili wasipatane naye tena. Anapopata nafuu baada ya kutoka hospitalini, anaogopa kurudi nyumbani kwa sababu ya aibu ya kutunzwa na mwanamke. Anaogopa kuenda kurudishia Sagilu mlungula wake wakiwa katika mkutano.
  6. Mtamaduni – Mrima bado amekwama kufuata jadi za kikwao hata licha ya maisha kuwa tofauti. Anamuuliza Mangwasha tangu lini mke kamuuliza mume kule anakoenda na kule anakotoka. Baada ya kupata nafuu, anakataa kurudi nyumbani kwa sababu haamini kuwa mwanamume aanapaswa kuangaliwa na mwanamke.
  7. Mfisadi – anakubali mlungula wa Sagilu licha ya yote maovu aliyotenda
  8. juha/mjinga - Anakubali yale Sagilu anamwambia anapoanza kumpa lungula ila haoni kwamba Sagilu ana njama ya kumharibia familia. Hata baada ya kupitia shida kwa ulevi wake, bado anakubali mlungula kutoka kwa mara ya pili licha ya yote aliyopitishwa.

Umuhimu

  • Mrima anatumiwa kumwonesha msomaji kwamba tusipokuwa waangalifu tunaweza kujipoteza kwa ujinga na anasa zetu. Tunapaswa kuwa waangalifu kwa yale yanayofanyika kwa mazingira yetu, haswa panapohusu pesa. Si kila njia ya kutengeneza pesa iliyo halali. Aidha, ingawa tunaweza potea pia tukikubali usaidizi tunaweza kurudi kuishi maisha mazuri na kujitoa kwa uovu uliotukithiri.

Sagilu

  • Mbinafsi – anajilimbikizia mali kwa kuwa rafikiye Mtemi Lesulia. Mwandishi pia nanatuelze kuwa angempata msichana yeyote ambaye alimtaka

Sifa

  1. Katili- Alijaribu kumwua Lonare. Pia, anamtuma Sihaba kupeleka kilipuzi katika harusi ya Mrima na Mangwasha. Pia, anawatawanya wana biashara wengine ili wasiweze kushindana naye.
  2. Mfisadi – aliungana na Mtemi Lesulia kujaribu kuwanyang’anya wakaazi wa Matango ardhi
  3. Msherati – anajulikana kuwa na wananwake wengi lich ya kuwa na bibi. Pia anawanyemelea Mangwasha na hata Cheiya, msichana aliyeposwa kwa motto wake. Baadae pia mwangishi anatueleza kwamba yeye ndiye babake Ngoswe, ila si mtemi Lesulia.
  4. Sio mwaminifu – Licha ya kuwa rafikiye Metmi lesulia na kumshauri asimfukuze bibiye Nanzia, anamnyemelea Nanzia na hata wana motto naye, Ngoswe
  5. Mjeuri – Anashinda akija kumsumbua Mangwasha akimuuliza kule bwanake yuko. Baadae anamkejeli Mangawasha kwamba hawawezi shinda uchaguzi
  6. Mkabila – Anaonekana nkiwatusi Lonare, Mangwasha na hata Mrima kwa sababu ni Waketwa.
  7. Mwenye bidii – Sagilu anamiliki biashara nyingi na hata mashamba. Hata katika uovu wake, amejitolea kufikisha lengo alizojiwekea kwa jinsi anavyoweza.
  8. Mwenye chuki- anaonekana kuwa chukia wale wasiosikilizana nay eye kama vile Mangwasha, Lonare ma hata Mrima.

Umuhimu wake:

  • Sagilu anatumiwa na mwandishi kutoa taswira ya wale wanaoshikana na wale walio na nguvu au cheo ili kuendleeza ufisadi na uovu. Baadae yale maovu yote aliyoyatenda yanamrudia na kumfanya kupoteza akili hadi kiwango cha kuhutaji matibabu. Kwa sbabu ya kuwasaliti waliomwamini, pia yeye anasalitiwa.

Chifu Mshabaha

Chifu Mshabaha ndiye Chifu wa eneo la Matango. Yeye ndiye aliyemeandika Mangwasha kazi. Anaonekana poia kuwa mwendelzi wa maovu yanayofanyika mtaa huo. Sifa zake ni kama vile :

Sifa

  1. Katili – Anaonekana kuwa katika njama nyingi za kuwafilisisha waketwa kv kuwachomea manyumba, kuwafukuza na kuwanyang’anya ardhi.
  2. Mjeuri- anaonekna kumkejeli Mangwasha kwa sababu ya kabila yake.
  3. Mkabila – anawadharauy Waketwa na kuwaita wajinga.
  4. Mbinafsi – anajilimbikizia mali kwa faida yake, na baadae alianza kufuatwa na watu wa kutoza ushuru kwa sabbau ya kukosa kulipa.
  5. Mfisadi – anapanga njama na kina Sihaba, Mtemi Lesulia na hata Sagilu. Bahasha ya mlungula aliyopewa Mrima ulionekana na Mangwasha ukiwa na Chifu, kuonyesha kwamba alikuwa katika njama ya kueneza kitendo hicho cha kumfisidi Mrima.

Umuhimu

  1. Chifu Mshabaha anatumiwa tuonyesha wanaotumia vyeo vyao kuendeleza uovu wao. Amefungwa macho na ukabila kwa sababu hata ingawa Mangwasha ni mfanyikazi mzuri, Chifu bado huwa anamwonea kwa sababu yeye ni wa kabila ya Waketwa. Tunapaswa kuwaona watu kwa tabia zao binafsi ila si kwa yale ambayo jamii imetulazimu kuyaona.

Lonare

Lonare ndiye mgombea mkuu wa kiti cha urais kutoka kabila ya waketwa. Lonare anao watoto watatu: Sauni, Sagura na Lombo ambao amehakikisha kuwasomesha kwa uwezo wake. Pia ni rafiki mkuu wa mangwasha ambao wanasaidiana na kushauriana jinsi ya kufanya haki katika jamii yao.

Sifa 

  1. Mzalendo - Anataka kuingia urais ili amalize ufisadi uliokithiri nchi yao. Katika hotuba yake ya mwisho, anatoa ahadi ya kwamba anataka kurudisha haki katika nchi yao.
  2. Mwenye bidii – anajitahidi kuwalea watoto wake na kuwasomesha wote. Pia, anajulikana kuwa na bishara nyingi ambazo licha ya kusumbuliwa na maafisa Wakule, ameweza kuziendeleza bado.
  3. Mwerevu – anashauriana na Mangwasha na wanawe jinsi ya kupanga njama za kuwasimamisha wanaojaribu kufilisi mali.
  4. Mwenye hekima – katika mashauriano yao na Mangwasha, anampa mawaidha watakavyo fanya vitu ili wabaki kuwa salama. Pia anampaNgoswe mawaidha ya kihekima pale anapopatana naye baada ya kurudi kutoka alikokuwa anatesewa.
  5. Msaidizi/ Mwenye haki– anamsaidia Mangwasha kumtafuta Mrima na kumshawishi pia arudi nyumbani. Anawasaidia wakaazi wa Matango kumpata wakili ambaye angewatetea katiika kesi yao ya ardhi.
  6. Jasiri – Hata baada ya kuteswa na hata kutaka kuuliwa, Lonare anaendela kung’ang’ana na Mtemi Lesulia katika ugombea wa kiti cha urais.

Umuhimu:

  • Lonare ni taswira ya wale wanaoendelea kupigania haki hata uovu ukikithiri jamii. Anatumiwa kuonyesha kwamba si lazima mtu kuwa mwovu ili akabiliane na uovu ila anaweza kukabiliana na uovu kwa hekima na kwa haki.

Mtemi Lesulia

Ndiye kiongozi mkuu wa nchi ya Taria. Ana mtoto mmoja: Ngoswe na bibiye Nanzia. Pia, ana marafiki wakaribu ambao wanalingana kitabia kama vile Sagilu na Mbwashu.

Sifa

  1. Katili – anawaongoza wananchi kwa mkono wa chuma. Anapanga njama ya kumtesa Lonare ili ashindwe katika uchaguzi.
  2. Mfisadi – Wanapanga njama na Sagilu ya kuwanyang’anya wakaazi wa matango ardhi ili wajenge soko kuu.
  3. Mwongo – Baada ya kushindwa alianza kusema kwamba hata hakuwa anataka kiti cha uongozi na alikuwa amechoka watumikia.
  4. Mkabila – anawafilisisha Waketwa kwa kuwanyima nafasi za kazi kwa serikali yake.
  5. Mbinafsi – Kwa kutumia cheo chake, amejilimbikizia mali pamoja na wenzake .
  6. Mjeuri- Hata baada ya kushindwa, anaendelea kuongea kwa ujeuri, akiwauliza watu kama walidhani angebaki mtemi siku zote.

Umuhimu

  1. Mtemi lesulia anatumiwa kuonyesha jinsi uaongozi mbaya unavyoweza kuathiri nchini vibaya. Kwa uongozi wake, Matuo imepoteza rasilimali kwa wingi. Tunapaswa kutumia vyeo tulivyo nazo kuwahudumia watu ipasavyo wala si kuwatesa na kujifaidi sisi wenyewe.

Mwamba

Mwamba ni wakili ambaye aliwasaidia wakaazi wa matango kushinda kesi ya Ardhi yao. Ni rafikiye Lonare. Pia Alimshinda Sagilu katika ugombeaji wa kiti cha uongozi wa Matango. Sifa zake ni:

Sifa

  1. Mwenye haki – Anawasaidia Waketwa katika kesi yao ya ardhi.
  2. Msomi/Mwerevu – katika kesi hiyo anaweza kujieleza na hata kumshinda mafambo amabye alijulikana kuwa shupavu.

Umuhimu

  • Mwamba anatumiwa kutoa taswira ya wataalamu katika jamii ambao wanajitolea kwa taaluyma yao kuwasaidia watu. Anajulikana kwa werevu wake na pia kwa kuwa mtetezi.

Bi. Mbulungu 

Ni rafikiye Mangwasha na anaonkena kumsaidia kila anapohitaji usaidizi.

Sifa

  1. Ni mwenye hekima – anamshauri Mangwasha kufanya vitu kwa utaratibu amabao hautamweka matatani.
  2. Ni mtamaduni – Anaonekana kuwa amekwama katika kuitii jadi zao kuhusu nafasi ya mwanamke, huku akimkanya Mangwasha dhidi ya kumtafuta bwanake.
  3. Msaidizi- anamsaidia Mangwasha kwa kuwaangalia watoto wake anapoenda kumtafuta Mrima. Pia, kwamara ya ili ndiye anamfahamisha Mangwasha kule alikomwona Mrima.

Umuhimu

  • Bi. Mbulungu anatumiwa kutoa taswira ya wale wanaosaidia katika kupigania haki. Ingawa hayuko usukani, anaonekana kuchangia pakubwa kwa mawaidha na kwa ushirikiano pale anapohitajika.

Sihaba

Sihaba ni mmoja wa wanawake wanaohusishwa na Sagilu. Mwandishi anatueleza kwamba alihusika kuwasumbua walishindana na Sagilu kibiashara.

Sifa

  1. Katili – Alitumwa kuleta kilipuzi kwa harusi ya Mrima kwa nia ya kuwaua au kuwaumiza walioenda kusherehekea.
  2. Mfisadi- Anaachiliwa jelakila anaposhikkwa kwa maovu aliyotenda.
  3. Mbinfasi - anawatumia wasichana wadogo kwa nia ya kujiendelea kipesa ila ni kitendo kibaya.
  4. Mjeuri - anajibizana na polisi pale anaposhikwa akiwatumia wasichana wadogo.

Umuhimu

  • Mwandishi anamtumia Sihaba kuonyesha wale wanaoshirikiana na wafisadi kuendeleza uovu wao. Wale wanaoeneza uovu wanapoanguka pia hawa wanaanguka. Anatoa taswira ya kimelea ambaye anategemea wale alioshikana nao ile aweze kujiendeleza ama kuondokea/ kuhepa haki au matokeo ya matendo yake kwa njia kama vile kutolewa jela anaposhikwa.

Ngoswe

Ngoswe ni mwana wa Mtemi Lesulia na Nanzia. Mwandishi anatueleza kwamba hafanyi kazi ila anatuymia mali ya baba yake kwa anasa. Ngoswe pia anaeneza biashara ya mihadarati lakini anaahidi kuachana nayo kwa mawadha ya Lonare. Baadaye, anaambiwa na Nanzia kwamba babke halisi ni Sagilu.

Sifa

  1. Mbinafsi - Anajilimbikizia mali yabab yake na kuitumia kwa anasa
  2. Msherati - Anamshauri Mashauri amtafute mwanamke mwengine akimshawishi kuwa wanawake ni wengi. Mashauri anamwambia kwamba yeye hajui mapenzi kwa sababu ya wale wasichana wote alio nao.
  3. Mfisadi - Tunaelezewa kuwa angefanya biashara yake ya miuhadfarati vile alivyopenda kwa sababu hanegshikwa na yeyote kwa sababu ya baba yake na pia wale aliofanya nao biashara.
  4. Msaliti - Anamsaliti baba yake kwa kuenda kuungana na Lonare
  5. Mzalendo - Kwa kusikia maovu ambayo baba yake anapanga, anamtishia kwamba hatajiunga na wao na anawaacha kujiunga n Lonare. Kwa mawadiha ya Lonare, anaamua kuacha biashara ya kuuza mihadarati.
  6. Mpenda anasa - Tunalezewa kuwa anashindia ulevi na usherati kwa mali ya baba yake huku pia hafanyi kazi ila ya kuuza mihadarati.

Umuhimu

  • Licha ya kuwa mwana wa Mtemi Lesulia na kuwa mmoja wa wale wahusika waovu, mwandishi anamtumia Ngoswe kuonyesha kwamba hakuna yule aliyekithiri maovu asiyeweza kubadilika.

Mashauri

Mashauri ni mwanake Sagilu. Baada ya kumpata baba yake Sagilu na mpenziwe Cheiya mkahamwani, anamwacha babake na kumwendea Lonare ili kumsaidia na kukiri maovu aliyomfanyia.

Sifa

  1. Msomi/Mwerevu – amesomea ustadi wa ujenzi
  2. Katili - Kwa masharti ya babe yake, alimharibia Lonare majengo yake.
  3. Mwenye utu - Baadae aliweza kukiri yale maovu aliyofanya kwa hiari ya baba yake.
  4. Msaidizi - anajitolea kumsaidia lonare na wnezake kushinda uchaguzi
  5. Asiye samehe - amekataa kumsamehe baba yake kwa yale maovu aliyomtendea.
  6. Mjinga/juha - Hakuona kwamba kulikuwa na jambo kati ya baba yake na Cheiya.

Lombo

Lombo ni mmmoja wa wanawe Lonare ambaye alisomea udaktari na aliposikia babake anashiriki katika uchaguzi, alirudi nyumbani ili kumsaidia. Pia, mwandishi anatueleza kwamba walisoma na Mashauri na wailikuwa marafiki shuleni.

Sifa

  1. Mwenye utu - Anamhimiza Mashauri aweze kumsaidia baba yake ila wamekosana.
  2. Msomi/mwerevu- anaonekana kuwayatambua magonjwa mengi. Anatambua ugonjwa wa akili ambao ulimshika Sagilu na pia anatambua ugonjwa ulimshika Nanzia.

Sauni 

Ni mwanawe Lonare ambaye anasaidiana na nduguze lombo na Sagura kwa kampeni za uchaguzi.

Sifa

  1. Msomi – anatoa kisa cha Lilith kumfaananisha na Sihaba kitabia. Kisa hiki kianonyesha kwamba ana ujuzi wa visaasili ambao haupatikani ila kwa mtu kuw msomi.
  2. Msaidizi – Anamsaidika baba yake katika kampeni
  3. Mwenye hasira – Anaudhika haraka anapokatiswa akieleza asili.
    Pia, anamrukia Mrima na maneno na kumwita msaliti, na Pia kumrukia Mashauri na maneno makali anapokiri uovu wake.

Sagura

Ni mwanawe Lonare ambaye anasaidiana na nduguze Lombo na Sauni kwa kampeni za uchaguzi.

Sifa

  1. Msaidizi – Anamsaidika baba yake katika kampeni
  2. Mpole – Anamwonglesha Mrima kwa upole wanapoenda kumkabili. Anamwambia pia kwamba anapaswa kumshukuru bibi yake aliyemwokoa kutoka kwa mdomo wa chui.

Mbwashu

Ni mwanamke aliye marafiki na Sagilu na Mtemi Lesulia. Uhusiano wao unahusu kushirikiana kueneza ufisadi na kujilimbikizia mali ya umma. 

Sifa

  1. Mfisadi - Anajulikana kuwa katika njama za ufisadi wakishikirikiana na Mtemi Lesulia na Sagilu
  2. Mbinafsi - Anajulikana kuwa katika njama za ufisadi wakishikirikiana na Mtemi Lesulia na Sagilu
  3. Msaliti - Anawakwepa Lesulia kwa kutoroka nchi Lonare anaposhinda uchaguzi.
  4. Kimelea - Uhusiano wake na wa Mtemi unaonekana kuwa wa kujisaidia tu, pindi Lesulia anapopoteza cheo, Mbwashu anaondoka nchini na kutorokea kwingine.

Hakimu/jaji 

Ni mhusika mdogo anayetokea aple kortini kusikiza kesi ya wakaazi wa Matango. Anaonekana kuwa mwenye haki na kuwapa wakaazi hao ardhi yao na jambo hili linaonekana kumfanya afutwe kazi.

Sifa

  1. Mwenye haki - Anawapa ardhi yao wakaazi wa Matango kwa kuzingatia utetezi/ ushahidi wa Mwamba. Jambo hili linafanya atolewe kazini n kunyang’anywa leseni ya kufanya uhakimu.

Mbaji

Ni mhusika mdogo ambaye ni mmoja wa madereva wa basi za Lonare. Amejitolea kumfanyia kazi Lonare vizuri ingawa  yeye ni Mkule, jambo lisilo la kawaida.

Sifa

  1. Mwaminifu - Anafanyia kazi Lonare ila kujali kwamba wametoka kabila tofauti. Pia, mwandishi anatueleza kwamba alikataa mlungula wa kina Sagilu awache kumfanyia Lonare kazi
  2. Msaidizi- Anajitolea kuenda na kina Lonare, Mangwasha , Sauni na Sagura kumtafuta Mrima Ponda Mali

Umuhimu

Mbaji anatumiwa kuonyesha kwamba hata ukabila unapokithiri, tunapaswa kufanya haki. Mabji, Ngoswe na Mshauri ndio wahusika Wakule ambao wanaonekana kushirikiana na Waketwa. Aidha, yeye ndiye mhusika pekee wa kabila ya Wakule ambaye hajatajiwa maovu kwa riwaya hii. Mwandishi anamtumia kuonyesha kwamba tunaweza simama kando na yale maovu yanayohusishwa na jamii tuliyomo.

Cheiya

Cheiya ni mhusika mabaye alikuwa ameposwa na Mashauri, mwanawe Sagilu. Kwa maelezo ya mwandishi, tunapata kuelewa kwamba alikuwa yatima na licha ya hayo, aliweza kusoma kufikia kiwango ya kuwa muuguzi.

Sifa

  1. Msaliti - Alimsaliti mpenzi wake Mashauri kwa kujenga uhusiano usiofaa na baba yake Sagilu
    Pia, hata baada ya nyumba ya mayatima kumshugulikia asipokuwa na mali, alipopata mali mwandishi hatuelezi kwamba alirudisha mkono ila alibadilika na kuanzana na maisha ya anasa.
  2. Mwenye bidii -  Licha ya kuwa yatima, aliweza kutia bidii kufikia kiwango ya kuwa muuguzi.
  3. Katili - Alitumiwa kujaribu kumwua Lonare
  4. Mpenda anasa - Anajiingiza kwa maisha pindi anapoanza kupata pesa. Na hata kufikia kuanza kushiriki usherati na maovu kwa sababu ya pesa

Umuhimu

Cheiya anatumika kuangazia wale walio wabinafsi kwa jamii. Licha ya magumu aliyopitia maishani, anabaki kujiangalia yeye mwenyewe ila hawezi kurudisha mkono wa usaidizi kuwasidia wengine waliokuwa alipotoka. Kupitia kwake, tunapata kuona kwamba si wale walio na mali pekee ambao wanaoeneza uovu ila ni maovu hayaoni tabaka. Kupitia kwake tunaona jinsi ubinfasi, tamaa na anasa zinaweza kumfunga mtu macho. 

Mzee Shauri

NI mhusika mdogo amabye ndiye babake Mangwasha. Anatokea kwa riwaya kuonyesha jinsi alivyomlea Mangwasha.

Sifa

  1. Mwenye hekima - Anaonekana kumpa Mangwasha mawaudha ya busara na ya hekima ambayo Mangwasha anayatilia maanani li aweze kujikimu kimaisha.

Nanzia

Ni bibi yake Mtemi Lesulia na mama yake Ngoswe. 

Sifa

  1. Msaliti- Alimsaliti Lesulia kwa kuwa na watoto na wanaume wengine wawili.
  2. Mbinafsi- Anajilimbikizia mali ya uma
Join our whatsapp group for latest updates

Download Wahusika: Sifa na Umuhimu wao - Mwongozo wa Nguu za Jadi.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?