Chozi Insha Questions and Answers
Maswali ya Insha
Haya ni maswali ambayo hutoa kauli inayohitaji kujibiwa kwa kirefu na kwa kina. Swali linaweza kuwa la jumla yaani linalohusu Riwaya nzima. Pia, swali laweza kulenga sehemu ya kazi husika katika nyanja na maudhui, wahusika na hulka zao, mafunzo na fani. Maswali haya huhitaji zaidi uwezo wa kukumbuka wa mtu, kupanga hoja na kuelezea msimamo au maoni yake kuhusiana nayo. Mtahiniwa anahitajika kutoa hoja na kuziteteta kwa mifano dhabiti. Mtahiniwa asitumie vistari vistari, afafanue hoja kikamilifu akiandamisha mifano mingi kutoka kwa Riwaya.
Swali la Insha 1
Haki za watoto hazitiliwi maanani katika jamii nyingi za kiafrika. Eleza ukweli wa kauli hii kwa kurejelea Riwaya ya chozi la heri (Alama 20)
Haki ya watoto kusoma inakiukwa. Ami za Lucia na Akelo wanapinga elimu yao na kudai kuwa kuwaelimisha wasichana ni kufisidi raslimali.
Watoto wanahusishwa katika ajira. Akiwa mdogo,Sauna anaajiriwa kwenye machimbo ya mawe,kuuza maji na hata pombe baani. Vilevile Chandachema anahusishwa katika ajira ya uchunaji wa majani chai akiwa mtoto wa darasa la tano kwenye shirika la chai la Tengenea.
Kuna wizi wa watoto. Sauna anawaibia Dickson na mwaliko na kuwapeleka kwa Bi. Kangara ambaye ni Mlangunzi hodari wa watoto.
Watoto wanauawa na magari moshi kwenye mtaa wa madongoporomoa wa Sombera wanapoenda haja kwenye reli
Watoto wanahusishwa katika ulanguzi wa dawa za kulevya. Dickson anatumiwa na mzee Buda kusafirisha dawa za kulevya ughaibuni.
Baadhi ya watoto wasichana wanaolewa na vikongwe kwa lazima. Fungo anamwoa Pete kwa lazima akiwa darasa la saba kama mkewe wanne.
Kunajisiwa/kubakwa – Sauna anabakwa na babake wa kambo Bwana maya na Kutungwa mimba. Pia lime na Mwanaheri wananajisiwa na vijana wahuni.
Watoto wanapotoshwa na watu wazima. Bi. Kagara anampotosha Sauna kwa kuhadaa ajihusishe na biashara haramu ya ulanguzi wa watoto. Anapotoshwa,Sauna anahusika katika wizi wa watoto na kuwalangua
Baadhi ya watoto wanapozaliwa wanatupwa. Naomi anamwokoa mtoto aliyetupwa jalalani na kumpeleka kwenye kituo cha polisi. Matawa Cizarina anasema kwamba kuna mtoto aliyetupwa langoni mwa kituo cha watoto cha Benefactor akiwa amefungwa kijiblanketi kikuukuu.
Naomi anawahini wanawe malezi anapomtoroka mumewe. Anamtoroka Lunga baada yake kufutwa kazi na kuwa maskini jambo hili linawafanya Umu, Dickson na Mwaliko kulelewa na baba yao pekee
Sauna anapotoshwa na Bi. Kangara anapohusishwa na wizi na ulanguzi wa watoto. Bi.Kangara anamhadaa Sauna na kumwingiza katika biashara hii haramu.
Watoto wanapokea vitisho kutoka kwa watu wazima wanaopania kuwatumia vibaya. Mzee Buda anamtisha Dickson anapojaribu kukataa kujihusisha katika biashara ya ulanguzi wa dawa za kulevya. Anamwambia kwamba anamtupa nje na kumsingizia wizi. Jambo hili lingemfanya Dickson kuvamiwa na kuuawa na raia kama alivyofanywa Lemi.
Watoto wanatumiwa kama vyombo vya mapenzi. Bi.Kangara anawaiba wasichana na kuwauza kwenye mandanguro (shambiro) ili watumiwe kama vyombo vya mapenzi na wanaume katili. Fumba anajihusisha na mwanafunzi wake kimapenzi na kumringa.
Kuna ubaguzi wa watoto. Wazazi wa Pete wanamwoza kwa lazima kwa mzee Fungo kama mke wanne. Wanafanya hivi ili wapewe mahari itakaayotumiwa kuwaelimisha ndugu zake watano wa kiume.
Watoto walio mijini ya mama zao wanaavywa. Mamake Sauna anamsaidia kuavya kitoto chake. Anafanya hivi kwa kumwogopa Bwana Maya aliyemnajisi Sauna. Umulikheri kuachiwa ulezi wa Dickson na baada ya Mama yao Naomi kutoroka na baba yao kuaga.
Tuama kukumbwa na maswala ya ukeketaji wa watoto wa kike
Dick kulazimishwa kushiriki ulanguzi wa dawa za kulevya na Buda
Mwanawe Selume Sara anatengwa na mamake mzazi baada ya mumewe kumwacha Selume na kumwoa msichana wa kikwao. Anachukuliwa na babake. (Uk35)
Kairu anaeleza jinsi walipofukuzwa kwao na jinsi si kitindamimba wao anapoaga dunia kutokana na njaa.uk 91
Mwanaheri na Lime wanafanyiwa unyama-wanabakwa na vijana mbele ya baba yao. Na baadaye wanakosa penzi la Mama yao Subira anapowatoroka baada ya kupitia machungu ya kubaguliwa .Uk 97
Zohali kuhusishwa katika mapenzi mapema na kupachikwa mimba. Zohali Anadhulumiwa kimapenzi uk 98
Chandachema kutelekezwa na babake Fumba na kuachwa alelewe na Bi. Kizee ambaye anaaga akiwa darasa la kwanza. Pia hajui aliko mama yake.
Rehema, Mamake Chandachema anadhulumiwa kimapenzi kwa kuringwa mimba na Fumba mwalimu wake akiwa kidato cha tatu. Uk 103
Chandachema anaizimika kufanya kazi katika shrika la chai la Tengenea ili kujikimu akiwa darasa la pili maadamu apate nafasi ya kusoma Uk.105
Chandachema na wanawe Tenge wanalazimika kushuhudia bwana Tenge akigeuza chumba chao Danguro japo ni watoto wachanga…na kusababishiwa dhiki ya kisaikolojia. Uk 106
Swali la insha 2
Ukabila ni tatizo sugu katika nchi nyingi za Kiafrika. Tetea kauli hii ukilejelea Chozi la Heri ( al. 20)
Subira alitengwa na familia ya mume wake kwa kuwa wa kabila tofauti na lao.
Mwanaheri anatueleza kuwa mama yake alikuwa ametoka kwenye jamii ya mamwezi lakini babake alikuwa wa jamii tofauti. Kila mara subira aliitwa ‘muki’ au huyo wa kuja.
Kijana mmoja alimwita Ridhaa mfuata mvua jambo lilimuumiza sana Ridhaa.
Mzee kendi alimtendea udhalimu Ridhaa na kuiteketeza aila yake licha ya wao kuwa majirani kwa miaka hamsini. Ridhaa alifanyiwa hivi kwa kuwa alikuwa ametoka kwenye kabila tofauti na mzee kendi.
Ndoa ya Selume ilisabaratika baada ya vita vya kutawazwa kwa kiongozi mpya kuoa msichana wa kikwao.
Tulia alimsaidia kaizari kufunganya na kumsidikiza hadi njia panda. Alimkumbatia na kumwambia kuwa mwenyezi Mungu ndiye hupanga na nguvu na mamlaka pia hutoka kwake
Uongozi mpya umezua uhasama kati ya koo ambazo zimeishi kwa amani kwa karibu karne moja.
Subira aliweza kuvumilia kubaguliwa, kufitiniwa na kulaumiwa kwa asiyoyatenda, Mwishowe alihiari kujiondokea na kwenda mjini alikojinywea kinywaji kikali. (zozote 10 x 2)

Swali la insha 3
Jadili nafasi ya sehemu zifuatazo katika riwaya ya Chozi la Hari:
- Hotuba (alama 10)
- Uozo katika jamii (alama 10)
Hotuba
Hotuba ni maelezo maalumu yanayotolewa na mtu mmoja mbele ya watu. Pia huitwa hutuba. Mwandishi wa riwaya hii ametumia hutuba kwa ustadi mkuu kupitisha ujumbe mbalimbali.
Hotuba hizi ni:
Hotuba ya Racheal Apondi kwa maafisa waliohudhuria warsha kuhusu jukumu la vikosi vya askari katika kudumisha usalama, amani na maridhiano nchini (uk 112- 113). Katika hotuba hii, Racheal Apondi anasisitiza kuwa: Suala la usalama haliwezi tena kupuuzwa. Usalama umekuwa mojawapo ya mahitaji ya kibinadamu. Anasema kuwa bila usalama, binadamu hawezi hata kushiriki katika shughuli za kuzalisha mali, hivyo hata mahitaji yake mengine ya kimsingi kama vile chakula, malazi na makazi hayawezi kukidhiwa. Kila binadamu ana jukumu la kudumisha amani na usalama. Wafanyakazi wa umma, hasa polisi na wanajeshi wana jukumu kubwa zaidi la kudumisha usalama na amani. Kila mmoja wetu anastahili kuhakikisha kuwa ameepuka vitendo vya kihalifu. Ni vyema mtu kuwaangaza wahalifu wakati wote. Vikosi vya polisi na wanajeshi vimefunzwa maarifa ya kukabiliana na kadhia za jinai na upelelezi. (4×1= 4)
Hotuba ya Lunga Kiriri- Kangata kwa walimu na wanafunzi gwarideni (uk 68-69). Hotuba hii ilisisitiza umuhimu wa kuhifadhi mazingira. Anasisitiza kuwa: Suala la uhifadhi wa mazingira ni jukumu la kila mmoja wetu. Misitu ilikuwa imevamiwa na viongozi wenye mate ya fisi. Baadhi ya vinara wa taasisi mbalimbali za umma wamewaacha wanyama kama mayatima kwa kuwapoka makazi yao. Maelfu ya maekari ya misitu yamefyekwa na kujengwa viwanda. Badala ya mibambakofi na miti mingine inayosafisha hewa, michai imetwaa nafasi yake. Wanaohusika na matendo haya wanapoulizwa hudai kuwa michai si adui ya mazingira! Wengine wanasema kuwa misitu haina budi kukatwa ili kupanda mimea inayotoa chakula, kwani jamii lazima ijitosheleze kwa chakula. La kuhuzunisha ni kwamba hawa hawa wanaosema hivyo ndio wanaokita majengo ya kifahari katika sehemu ambazo zinastahili kutengewa upanzi wa chakula! Wengine wamediriki kunyakua hata madhabahu kwenye Mlima wa Nasibu ili kujenga hoteli kubwa za kitalii. Wazee wetu hata hawana mahali pa kuchomea kafara! Tunakata miti bila kupanda mingine. Hata mabustani ya maua tunashindwa kuyastawisha. Tukiendelea kuharibu mazingira sehemu yetu itazidi kuwa jangwa. (2×1= 2)
Hotuba ya Umu katika hoteli ya Majaliwasiku yake ya kuzaliwa. Umu anawashuku Mwangeka na Apondi kwa kuwa wazazi wake wema. Anawashukuru kwa kumsomesha. Anawashukuru kwa kumsaidia Dick kujiendeleza kimasomo. Mwangeka na Apondi wanamshukuru Umu kwa kuwapa furaha. Apondi anamshukuru kwa kumlea mdogo wao kwa maadili bora. (2×1= 2)
Hotuba ya Dick katika hoteli ya Majaliwa siku ya kuzaliwa kwa Umu. Dick anamshukuru Umu kwa msaada wake na ahadi ya kumlea. Anamkumbusha siku walipokutana katika uwanja wa ndege na ilivyokuwa muhimu kwake. Anamshukuru Umu kwa kumwelekeza kwa wazazi wao wale. Anawashukuru Apondi, Mwangeka na wanawe kwa ushauri wanaompa. (2×1= 2)
Mtahiniwa ataje hotuba kisha aeleze masuala muhimu yanayoibuliwa na kila moja.
Uozo katika jamii (alama 10)
Uozo ni hali ya kuzorota na kutozingatiwa tena kwa maadili mema katika jamii. Ni hali ambapo milazote na desturi njema huvurugwa na wanajamii wanaofanya mambo yaliyo kinyume nahali halisi ya maisha. Mwandishi amejadili suala hili kwa undani kama ifuatavyo;
Jamii inaendeleza ubakaji. Genge la mabarobaro watano lilifululiza hadi walipokuwa maskini Lime na Mwanaheri na kuwabaka mbele ya baba yao (uk 25).
Kuna ulanguzi wa dawa za kulevya. Dick alipotoroshwa na Sauna alipelekwa kwa tajiri mmoja aliyemwingiza katika kusafirisha dawa za kulevya kutoka nchi moja hadi nyingine (uk 119- 120).
Wanajamii wanaendeleza uporaji na wizi wa mali. Vijana wanawavamia watu, kuwaua na kupora katika maduka ya kihindi, kiarabu na ya waafrika wenzao.
Jamii inaendeleza ufuska/ ukahaba. Sauna aliiba watoto na kuwapeleka kwa mama mmoja aliyewatumia kwa biashara ya nipe nikupe (uk 84).
Biashara haramu inaendelezwa. Bi. Kangara alifanya biashara ya kuwauza watoto na vijana- Safari yake ilipata mkondo mwingine baada ya polisi kupata fununu kuhusu njama ambazo yeye na Bi. Kangara walikuwa wakiendesha. Mabibi hawa walikuwa na mtandao ambao kazi yake ilikuwa kuwauza watoto na vijana (uk 84).
Kuna tatizo la mimba za mapema. Vijana wana mazoea ya kukumbatia mtafaruku wa kuhisia unaowapata na mara hujipata wameambulia ujauzito kama alivyofanya Zohali (uk 98).
Baadhi ya wanajamii wanaendeleza uavyaji mimba. Sauna alijaribu awezavyo kuavya mimba na mwishowe, baada ya kushindwa, anaamua kujiua.
Kukiuka maadili ya kikazi. Fumba (mwalimu) anakiuka maadili ya kazi na kujihusisha kwa mapenzi na mwanafunzi wake, Rehema, na hatimaye kumpachika ujauzito (uk 102).
Wazazi wanawabaka wana wao. Babake Sauna anafanya mapenzi na mwanawe kila apatapo nafasi, na mwishowe, Sauna anapata mimba.
Starehe na anasa kwa vijana. Vijana wa vyuo vikuu wameshindwa kutofautisha usiku na mchana. Tindi anasahau kumrejesha Lemi nyumbani kutokana na muziki (uk 121).
Wazazi wanakwepa malezi na kuwatupa wanao wakiwa wachanga. Neema anampeleka mtoto aliyemwokota kwa polisi (uk 162).
Vijana kuwaiga wazee. Mwangemi na Mwangeka walikuwa na tabia mbovu ya kumuiga babu yao (uk 186). (10×1= 10)
Mtahiniwa afafanue kwa mifano kutoka katika riwaya.
Swali la insha 4
- Fafanua namna mbinu ya majazi ilivyotumiwa katika riwaya. 10
- Jadili maudhui ya nafasi ya vijana katika jamii ukirejelea riwaya ya Chozi la Heri. Al.10
Fafanua namna mbinu ya majazi ilivyotumiwa katika riwaya. 10
Ridhaa – Kukubali ama kutosheka. Mhusika Ridhaa anakubali na kutosheka na makuruhu aliyofanyiwa ya kuteketezewa mali na familia yake.
Bwana Tenge – Tenge ina maana ya fujo. Bwana Tenge anamfanyia mkewe fujo na vitimbi anamwendea kinyume mke wake, Bi. Kimai. Bwana Tenge anashiriki mapenzi na wanawake wengine.
Mzee Kedi – Neno kedi lina maana ya mambo yasiyopendeza, mambo ya hila pia ni kiburi. Mzee Kedi anamfanyia ridhaa hila kwa kuhusika katika kuiangamiza familia yake.
Bwana Mkubwa – Mkubwa ni neno lenye maana ya cheo au hadhi kubwa. Bwana mkubwa ana cheo kikubwa serikalini.
Tetei – ina maana ya kutetea. Bi. Tetei ni mwanaharakati anayetetea haki za wanaume.
Mwalimu Dhahabu ni madini yenye thamani. Mwalimu dhahabu ni mwalimu anayekuwa wa msaada kwa Umulkheri
Hazina – Hazina ina maana mali iliyohifadhiwa. Mhusika Hazina anakuja kuwa kama hazina kwa Umukheri kwani anamfaa Umu jinsi alivyomfaa kwa kimpa noti ya shilingi mia mbili.
Zohali – Neno hili lina maana ya ajizi. Mhusika Zohali anapachikwa mimba akiwa kidato cha pili ni dalili ya uzembe na kutomakinika masomoni.
Chandachema – Chandachema ni jina lililoundwa kutokana na Chanda kidole) chema ambacho huvikwa pete. Mhusika huyu ingawa anapitia changmoto tele maishani anaishia kupewa ufadhili wa masomo(kuvishwa pete) na shirika la kidini.
Bwana Mabavu – Mabavu ni nguvu. Bwana Mabavu anatumia nguvu kumpoka babake Shamsi ardhi yake.
Mzee Maarifa- anatumia maarifa na hekima kuanzisha kituo cha kupigania hakiza kibinadamu.
Neema ni mkewe Mwangemi. Neema ina maana ya Baraka. Mhusika huyu anakuwa Baraka kwa mume na pia kwa mwaliko.
Bwana Kimbaumbau ni mtu kigeugeu. Bwana Kimbaumbau anamsaliti Naomi kwa kutaka kufanya mapenzi naye.
Jadili maudhui ya nafasi ya vijana katika jamii ukirejelea riwaya ya Chozi la Heri.
vijana ni wasomi mf. Umu, tila.
Ni walanguzi wa dawa za kulevya mf. Dick.
Vijana wengine wa kike wakubali kukeketwa na wengine wanaaga dunia na kulazwa hospitalini mf. Tauma.
Vijana ni wapenda fujo.
Vijana hutumiwa na wanasiasa kutekeleza uovu na mauaji.
Ni dhihirisho kama wasio na huruma. K.m kuua wenzao bila huruma.
Wasio na msimamo dhabiti. Wanapotoshwa na wanasiasa bila kuwazia madhara waliosababisha.
Vijana ni wenye bidii katika kazi zao mf. Dick.
(Tanbihi: kadilia hoja za wanafunzi.) 10 x 1 = 10
Swali la insha 5
Jadili jinsi mwandishi wa riwaya hii alivyofaulu kutumia mbinu ya kinaya na sadfa. (alama 20)
Kinaya
- Kinaya ni maelezo ya mambo kinyume na yalivyo.
- Mwangeka anashiriki udumishaji wa amani Katika Mahariki ya kati huku familia yake ikiangamia nyumbani kutokana na ukosefu wa amani.
- Mzee Kedi anaua familia ya Ridhaa ilhali ni yeye aliyethamini masomo ya wapwaze.
- Ni kinaya wenye maduka kufunga milango wakati jumba la Ridhaa lilipochomeka badala ya kuyaacha wazi watu wotorokee .
- Ni Kinaya Lunga Kirir kuachishwa kazi baada ya kutetea wanyonge wasiuziwe mahindi yaliyokuwa na sumu.
- Ni kinaya Sauna kujifanya mzuri ilhali anawaiba watoto
- Ni kinaya Neema kupeleka mtoto kwa makazi ya watoto na mwishowe kwenda kupanga mtoto huko
- Ni kinaya Naomi kutoroka mmewe nawanawe ilhali hapo baadaye anajilaumu
- Ni kinaya nchi ambayo ¡na miaka hamsini kuonekana kama mtoto wa mika hamsini
- Ni kinaya kuwa wafrika wanakuwa wafanyikazi katika mashamba yao chini ya wakoloni
- Ni kinaya watu walioishi na Ridhaa kwa amani wanawageukia na kuchoma nyumba yake pamoja na familia yake
- Ni kinaya vijana kumbaka lime na Mwanaheri mbele ya wazazi wao
- Ni kinaya mamakwe kufukuza subira kwa kuwa hawakuwa wa jamii moja
- Ni kinaya mzee Maya kumbaka mwanawe Sauna
- Ni kinaya wazazi wa Zohali ambao ni wasomi kumtesa Zohali kwa ajili ya ujauzito
- Ni kinaya Tuama kusifu utamad uni wa tohara za kike iIhali ndio sababu ya kuwa hospitalini
- Ni kinaya watu wan chi ya Wahafidhina kumkataa kiongozi wa kike na ndiye anayewafanyia kazi
- Ni kinaya kwa pete kutaka kujia kwa kuwa na watoto watatu akiwa umri wa chini ya mia ishirini na moja Hoja zozote 10 X1=10
Sadfa
- Sadfa ni kuwaleta wahusika kadhaa pamoja bila kukusudiwa.
- Selume kufikiria kustaafu katika hospitali ya uma wakati Ridhaa alikuwa anamalizia ujenzi wa hospitali ya Mwanzo Mpya
- Umu kukutana ana Hazina alipokuwa akimtafuta.
- Safari ya Umu kuchelewa inamfanya akutane na Dick katika uwanja wa ndege.
- Mwangeka kukutana na Apondi katika karakana ni sadfa.
- Ni sadfa Umu, Dick na Mwaliko kukutana katika Hoteli ya Majaaliwa.
- Inasadifiana kuwa wakati Selume anapotaka kiacha kazi katika hospitali ya umma ndio Ridhaa anama liza kujenga hospitali ya mwanzo mpya
- Siku ya kuzaliwa kwa Umu inasadifiana nay a Mwangemi
- Inasadifiana wakati Neema akienda ofisini ana kiona kitoto kilichokuwa kimetupwa
- Umu na Dick wanakitana kisadfa katika uwanja wa ndege
- Ni sadfa Mwaliko kupangwa na binamuye mwangeka aliyempanga nduguye
- Inasadifu kuwa Dick alipokuwa akiwaza juu ya nduguye Umu alikuwa nyuma yake
- Kukutana kwa wana wa Lunga katika hoteli ya Majaliwa ni sadfa
- Ni sadfa kuwa Umu anapowaza sana juu ya maisha yake wenzake wana matatizo kumliko Hoja zozote 10 X1=10
Swali la insha 6
Tathmini umuhimu wa mbinu zifuatazo katika kuijenga riwaya ya Chozi la Heri
- Nyimbo (alama 10)
- Barua (alama 10)
Nyimbo
Wimbo wa Shamsi unaonyesha ukengeushi,
Licha ya elimu aliyo nayo, Shamsi ameshindwa kukabiliana na changamoto za maisha. Anaingilia matumizi mabaya ya pombe.
Unabainisha ukosefu wa uwajibikaji, badala ya kutafuta mbinu ya kukabiliana na hali duni ya maisha, analalamika kwamba wenye nguvu hawakumpa kazi walizoziahidi.
Unakashifu unyakuzi wa ardhi za wanyonge. Shamba la kina Shamsi linachukuliwa na Bwana Mabavu.
Unachimuza ufisadi – Bwana Mabavu anawaonyesha hati miliki bandia na kuwafukuza shambani mwao
Unaendeleza maudhui ya ukoloni mamboleo – Mabavu anamiliki shamba la Baba ya Shamsi na kuwageuza kuwa maskwota.
Unaangazia ukiukaji wa haki za binadamu – Shamsi na wenzake wanafutwa kazi kwa kuwazia kugoma.
Inaonyesha umaskini wa familia ya Shamsi – Babake Shamsi anakufa kwa kula mizizi mwitu wenye vijaasumu
Unakashifu unyonyaji wa wafanyikazi – Shamsi na wenzake wanalipwa mishahara duni.
Unasawiri tatizo la matumizi mabaya ya vileo- Shamsi anaingilia ulevi baada ya kufutwa.
Wimbo wa Shamsi unaoghaniwa na Ridhaa
Wimbo wa majigambo unaosawiri tabia ya Shamsi – anajivunia na kusema kuwa anaogopwa kwa kutoka katika jadi tukufu.
Unamfanyia tashtiti Shamsi kwa kujisifu kwa kuzua mikakati ya kukabiliana na hali ya uhitaji na hali mwenyewe ni mlevi.
Unaonyesha uovu wa jamii – wauza pombe wanatia vijaasumu ili iwe tayari haraka bila kuwazia madhara ya watumia wayo. Zozote 10 X 1 = 10
Barua
Barua ya Lunga
Barua ya kustaafishwa kwa Lunga inaonyesha dhuluma kwa wafanyikazi. Lunga anafutwa kwa kutetea wanyonge dhidi ya kuuziwa mahindi hatari kwa afya.
Inaonyesha uadilifu wa Lunga anavyosema Afisa Mkuu Mtendaji
Inakashifu ukatili wa waajiri – Lunga anafutwa bila hali yake kuwaziwa
Inaonyesha mbinu-hasi za uongozi – Viongozi wanawaangamiza wanaowapinga njama zao za kiufisadi.
Kuonyesha uongo/ unafiki wa waajiri- kusingizia kuwa shirika linapunguza wafanyikazi kutokana na changamoto za kifedha kutokana na gharama ya uzalishaji mali ilhali Lunga anafutwa kwa kukashifu kutaka kuuza mahindi yaliyoharibika. (hoja 5)
