Maswali na Majibu ya Dondoo katika Tamthilia ya Kigogo

Share via Whatsapp

Kigogo Dondoo Questions and Answers

Maswali haya hujitokeza kwa namna ya maneno yaliyodondolewa kutoka kwenye kazi ya Fasihi. Dondoo hunukuliwa kisha maswali yanayohusiana na dondoo hilo huulizwa. Dondoo laweza kuwa maneno ya mhusika mmoja ambaye hatatajwa au maelezo katika kazi. Maswali huenda yakarejelea matukio yaliyotokea kabla au baada ya dondoo. Katika kulijibu swali la muktadha wa dondoo, mtahiniwa huhitajika kuangazia mambo yafuatayo;

 1. Kumtaja msemaji wa maneno haya
 2. Kumtaja msemewa(anayerejelewa)
 3. Kueleza mahali yalikofanyika mazungumzo haya.
 4. Kueleza kiinisababu ya mazungumzo haya kutokea.

Swali la dondoo 1

’Na hawa wafadhili wao nao lazima wavunje kambi zao. Sagamoyo twajiweza’’

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
 2. Kwa kutolea mifano saba kwenye tamthilia eleza jinsi kauli hii ‘’Sagamoyo twajiweza’’ ni kinaya ?    (alama 14)
 3. Mbali na kinaya tambua mbinu nyingine ya kisanaa katika dondoo hili (alama 2)

Majibu ya dondoo 1

 1.  
  • Msemaji ni Majoka
  • Akimwambia Kenga
  • Wako Ofisini mwa Majoka
  • Anarejelea wafadhili wanaofadhili wanaharakati ( k.v Tunu na Sudi) na ambao wanawapa Nguvu
 2.  
  • Viongozi,Mjoka anashindwa kulisafisha soko la chapakazi japo anatoza kodi ya juu kwa wananchi
  • Walimu na wauguzi wanalalamikia mshahara duni
  • Majoka kushindwa kuwaongezea walimu na wauguzi mshahara na badala yake kutumia mbinu ya kijanja ya kutia na kuto (kuongeza mshahara na kupandisha kodi)
  • Maandamano ya wafanyikazi katika Mojoka namd majoka company kulalamikia bei ya bidhaa za chakula katika vioski kupanda bei uk 17
  • Mapato (keki Ya uhuru) kuliwa na wachache na wanasagamoyo kubakishiwa makombo
  • Wanasagamoyo waliosoma kama Tunu na Ashua hawana ajira ya maana
  • Njaa imekithiri sagamoyo-watoto wa Ashua wanakumbwa na njaa na inamlazimu Ashua kutafuta msaada kwa Majoka
  • Majoka anampa Mamapima kibali cha Uuzaji wa pombe haramu na kuishia kuwaangamiza wengi hasa vijana
  • Uongozi wa majoka kukopa pesa ughaibuni ili kufadili miradi isiyo na maana ya kuchanga kinyago na kukiachia kizazi kijacho mzigo mkubwa wa deni.
  • Wengi wa vijana na wanasagamoyo wanaenda Mangweni kuuguza majeraha ya roho zao zinasosababishwa na kufungwa kwa soko lao
  • Mazingira ya sagamoyo kuharibiwa kwani majoka atoa idhini wa ukataji kiholela wa miti.
  • Demokrasia bado ni changa sagamoyo. Wapinzani wa Majoka kama jabali wanauawa na uongozi wa majoka
  • Uongozi wa Majoka hauzingatii sheria katika utekelezaji wa mambo yake…mfano Majoka kuamuru askari Kingi awapige Risasi wanasagamoyo wasio na hatia,Ashua kutiwa ndani bila hatia,idhini ya kuuza pombe haramu.
 3. Nahau-Wavunje kambe-waondoke/Wasitishe shughuli zao

Swali la dondoo 2

“Kubali pendekezo letu la kufungwa kwa soko……… huoni hii ni fursa nzuri ya kulipiza kisasi?”

 1. Fafanua muktadha wa dondoo hili      (alama 4)
 2. Kufungwa kwa soko ni ukatili. Mbali na ukatili huu, toa mifano mingine ya ukatili kwenye tamthilia.    (alama 9)
 3. Msemaji wa maneno haya ni mshauri mbaya. Thibitisha kutoka kwenye dondoo na kwingineko tamthiliani.

Majibu ya dondoo 2

 1. Maneno haya ni ya sauti ya mzee Kenga mawazoni mwa Majoka. Haya yanatendeka katika Ofisi ya Mzee Majoka wakati Husda na Ashua wanapigana. Majoka anakumbuka ushauri wa Kenga wa jinsi ya kumnasa Ashua kwa kusababisha fujo baina yake na Husda
 2.  
  • Kumwaga kemikali na taka sokoni licha ya kuwa wananchi wanakaa na kufanyia biashara zao katika soko.
  • Kuwatumia wahuni kunyamazisha wapinzani. Mzee Kenga anakutana na Wahuni chini ya mbuyu ambao baadaye wanamwumiza Tunu.
  • Kuruhusu dawa za kulevya na wanafunzi ambao wanakuwa makabeji
  • Kuwaua wapinzani, kama vile vijana watano walioandamana
  • Kuwatumia polisi kuwaua na kurushia waandamanaji risasi na vitoa machozi.
  • Kuwanyima wafanyakazi haki, kama vile walimu na wauguzi wanaongezewa asilimia ndogo ya mshahara kasha kupandisha kodi.
  • Utawala kuruhusu uuzaji wa pombe haramu kinyume na katiba, ambao umesababisha vifo na kufanya watu kuwa vipofu.
  • Kufungulia biashara ya ukataji miti ilhai watu wanategemea miti hiyo kuboresha mazingira.
  • Kufunga kituo cha runinga ya Mzalendo kwa kuonyesha mkutano wa Tunu na wapinzani wengine wa utawala.
  • Utawala kutumia vyombo vya dola kuwafukuza watu wanaoenda sokoni na kuweka ulinzi mkali licha ya kuwa ulikuwa uwanja wa umma.
  • Kuwarushia wakazi vijikaratasi vyenye ujumbe hasimu wakitakikana wapahame mahali ambapo wamekuwa wakiishi kwa muda wote wa uhai wao.
 3.  
  • Kenga anamshauri Majoka amwalike Ashua na Husda ili patashika itokee, naye Majoka apate jinsi atakavyolipiza kisasi kwa Sudi kwa kukataa kuchonga kinyago.
  • Anamshauri Majoka atangaze kuwa maandamano ni haramu kisha anawamuru maafisa wa polisi watumie nguvu zaidi dhidi ya umma unaondoa maandamano.
  • Majoka anakataa Suala la polisi kutumia nguvu zaidi lakini Kenga anamwambia “Acha moyo wa huruma….. Siasa na hisia haziivi kwenye chungu kimoja ndugu yangu.
  • Anakubali pendekezo la Majoka la kufunga Runinga ya Mzalendo kwa kupeperusha matangazo ya mkutano moja kwa moja.
  • Kenga alihusika katika kupanga mauaji ya Jabali kwani Majoka anamsifu kwa kupanga hilo na hata wanapigishana Konzi
  • Anaibua pendekezo la kumuua Chopi kwa kutofuata maagizo ya kumuua Tunu akisema, “Nafikiri Chopi lazima aende safari.”
  • Anamwambia Majoka kuwa si kweli kwamba watu watampigia Tunu kura na kusema, “Tunu hawezi kupigiwa hata!”
  • Anapendekea kukusanya kodi ya juu na kukataa kuitumia vyema na kwa njia halali k.v. kutoa taka.

Swali la dondoo 3

Uliona nini kwa huyo zebe wako? Eti mapenzi!

 1. Eleza muktadha wa dondoo. (al. 4)
 2. Andika mbinu za lugha zinazojitokeza kwenye dondoo hili    (al. 4)
 3. Taja hulka za mnenaji unajitokeza katika dondoo.   (al. 2)
 4. Mwanamke ni kiumbe wa kukandamizwa. Thibitisha kauli hii ukirejelea tamthilia. (al. 10)

Majibu ya dondoo 3

 1.  
  • Maneno ya Majoka
  • Anamwambia Ashua
  • Ofisini mwa Majoka
  • Ni baada ya Ashua kumkataa Majoka Kimapenzi alipokwenda kutaka msaada kwake      1 x 4   = 4
 2.  
  • Swali la balagha – uliona nini kwa huyo zebe wako? (al 2 )
  • Nidaa – Eti mapenzi!      (al 2 ) (Kutaja alama 1, Mfano alama 1)
 3.  
  • Dharau/ bezo – Eti mapenzi!
  • Mpyaro – zebe ( mjinga / mpumbavu)    1 x 2 = 2   1x 2 = 2 Mwalimu akadirie
 4.  
  • kupigwa: Ashua akiwa gerezani anapigwa na askari
  • kubezwa / kukejeliwa: Tunu anakejeliwa na Ngurumo na walevi wengine
  • Chombo cha mapenzi. Majoka anamtaka Ashuakimapenzi anapokwenda kumwomba msaada.
  • Kijakazi nyumbani. Majoka anamtuma chopi kumuagiza mkewe kumpikia kuku na nyama na kumuokea chapatti
  • Kutusiwa: Boza anamwambia Sudi kuwa asifikiri kuwa yeye anauza nyong’a kama Tunu wake.
  • Kufungwa: Ashua anafungwa na Majoka
  • Kunyimwa kura/uongozi. Nurumo anamwambia Tunu kuwa kama hampi kura Majoka ni heri ampe paka wake. Majoka lakini si mwanamke Tunu.
  • Kunyimwa ajira. Licha ya Ashua kufuzu taaluma ya ualimu, hakuajiriwa na serikali. Anaishia kuchuuza maembe sokoni la chapakazi.
  • Kuozwa bila hiari. Majoka nataka kumwoza Tunu kwa mwanawe Ngao Junior bila hiari yake.
  • Kunyimwa fidia. Majoka alitaka kumnyima Hashima fidia baada ya kifo cha mumewe

Swali la dondoo 4

“Ni laghai siwaamini. Wanasema wanakwenda huku na mara…”

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)
 2. Eleza mbinu ya lugha iliyotumiwa katika dondoo hili. (Alama 2)
 3. Eleza sifa na umuhimu wa mzungumzaji. (Alama 6)
 4. Fafanua jinsi wanaorejelewa na mzungumzaji walivyo laghai. (Alama 10)

Majibu ya dondoo 4

 1. Haya ni maneno ya Majoka. Anamwambia Babu anapokuwa amezimia. Yupo katika chumba cha wagonjwa. Majoka analalamika kuwa chombo kinaenda kinyume na matarajio yake. Babu anamtaka Majoka asilalamike kwani yeye ni mmoja wa marubani. (4×1= 4)
 2. Kinaya- Majoka analalamika kuwa hawapendi marubani ilhali yeye ni mmojawapo wa marubani. (1×2= 2)
  lazima maelezo yawe sahihi ndiposa mtahiniwa apate alama zote mbili. Moja ya kutaja na moja ya kueleza. Bila maelezo sahihi kwa jibu sahihi tuza 0
 3. Sifa za Majoka
  • Ni Katili. Anawaua wapinzani wake. Anamwangamiza Jabali na chama chake cha Mwenge kwa kuhofia upinzani. Aidha, anapanga njama za uuaji wa Wanasagamoyo wengine, kama Tunu, Chopi na hata Sudi (uk 34).
  • Mwepesi wa kushawishika. Anakubali bila kudadisi athari za ushauri mbovu wa Kenga kuwa wamwangamize Chopi. Aidha, anautumia ushauri wa Kenga wa kumnasa Ashua ili kulipa kisasi kwa Sudi aliyekataa kumchongea kinyago (uk 29).
  • Ni mwingi wa tamaa. Ana tamaa kubwa ya mali. Ananyakua shamba la soko la Chapakazi ili aweze kujijengea hoteli kubwa ya kifahari. Ana mali mengi ikiwemo Majoka and Majoka Company, Majoka and Majoka Academy, Majoka and Majoka Mordern Resort na bado haridhiki.
  • Ni mwenye uchu. Ana tamaa za kimwili. Anatamani kushiriki mapenzi na Ashua licha ya kuwa Ashua ameolewa naye mwenyewe ana mke (uk 29).
  • Mwenye taasubi. Hawathamini wanawake. Anaamini kuwa mwanamke ni mwanamke tu. Anatishia kumchafua Husda.
  • Ni fisadi. Ananyakua mashamba ya umma kwa manufaa yake mwenyewe. Anamgawia Kenga kipande cha shamba huko sokoni kwa kigezo kuwa anashirikiana vyema naye.
  • Mkware/Mzinzi. Hamwamini mkewe tu. Anataka kushirikiana mapenzi na Ashua ambaye si mke wake wa ndoa (uk 28). (3×1= 3)
   Kila hoja ifafanuliwe ndiposa mtahiniwa atuzwe alama moja
 4. Umuhimu wa Majoka
  • Ni kielelezo cha viongozi wabaya na katili wanaowanyanyasa wananchi.
  • Ametumiwa kupigia darubini viongozi wa mataifa huru ya Afrika na jinsi wanavyowanyanyasa wananchi kwa kufuata uongozi mbaya wa vibaraka wao.
  • Ni kiwakilishi cha viongozi wanaokengeuka pindi tu baada ya kupewa uongozi na wananchi ili kukidhi tama zao.(3×1= 3)
   Hoja za umuhimu ziwe na ulinganifu fulani na sifa
 5.  
  • Hawahifadhi mazingira. Maji machafu (uchafuzi wa mazingira) yalipita mtaroni na kueneza harufu mbaya kila mahali bila uongozi wa Sagamoyo kuliona hili kuwa tatizo (uk 2).
  • Wanahatarisha maisha ya wananchi. Soko la Chapakazi limebadilishwa na kufanywa uwanja wa kumwagia kemikali (uk 2).
  • Wanawadhulumu wafanyabiashara. Wafanyabiashara wanahangaishwa na wanaosanya ushuru kwa kuwaitisha kitu kidogo na wengine kitu kikubwa (uk 2–3).
  • Hawajali maendeleo ya kesho. Serikali kutangaza mwezi mzima wa kusherehekea uhuru bila watu kufanya kazi ilhali haijali watakachokula watu (uk 4).
  • Hawana sera bora za maendeleo. Serikali ya Sagamoyo haina mipango maridhawa ya kimaendeleo. Majoka anamiliki kampuni kubwa ya sumu ya nyoka badala ya miradi muhimu (uk 4).
  • Wanaruhusu na kuendeleza ufisadi. Kuna ufisadi unaomfanya Asiya kupata kandarasi ya uokaji keki ya uhuru kwa kujuana na Husda bali si kwa kufuzu na kufaulu (uk 7).
  • Wanaendeleza udikteta. Utawala wa Sagamoyo ni wa kimabavu. Kenga anamlazimisha Sudi amchongee Majoka kinyago cha Ngao licha ya kujua kuwa uongozi wa Majoka ni wa udhalimu (uk 9).
  • Wanatazama mambo nchini yakiendelea kuharibika. Kombe, mshiriki wa karibu wa Kenga anakiri kuwa mambo yameenda kombo Sagamoyo (uk 15).
  • Hawajali maslahi ya wananchi. Uongozi unafunga soko la Chapakazi. Soko hili ndilo kitegauchumi pekee kwa Wanasagamoyo (uk 25).
  • Wanawachochea wananchi kuandamana. Kuna maandamano ya mara kwa mara na yasiyotatuliwa katika jimbo la Sagamoyo, wanachi wanapigania haki zao.
  • Wanaendeleza matumizi mabaya ya asasi za kijamii. Majoka anawatumia polisi wake vibaya ili kujidumisha uongozini. Polisi wanawanyanyasa na kuwadhulumu wananchi bila Majoka kujali.
  • Wana ubinafsi mwingi. Sagamoyo kuna uongozi wa ubinafsi. Majoka anataka kuendeleza ubinafsishaji wa uongozi wa Sagamoyio kwa kumtangaza rasmi Ngao Junior kuwa mrithi wake (uk37).
  • Wanaendeleza unyakuzi wa ardhi. Kuna unyakuzi wa mali ya umma. Majoka analifunga soko na kuinyakua sehemu hiyo ili ajenge hoteli ya kifahari (uk 45).(10×1= 10)
      Kila hoja ifafanuliwe kikamilifu

Swali la dondoo 5

Tulipoanza safari hii matangazo yalikuwa bayana, dhahiri shahiri babu!

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili. Al.4
 2. Tambua mbinu za uandishi zilizotumika katika kifungu hiki. Al.4
 3. Eleza matatizo yanayokumba safari inayorejelewa. Al.12

Majibu ya dondoo 5

 1.  
  • Msemaji ni majoka
  • Alikuwa anamwambia babu katika ndoto
  • Walikuwa katika chumba cha wagonjwa
  • Hii ni baada ya majoka kupata habari ya kifo cha mwanawe  Ngao Junior.   (4x1)
 2.  
  • Jazanda – safari kurejelea uongozi
  • Msemo – Dhahiri shahiri
  • Nidaa – Dhahiri shahiri babu!    ( 2 x2 = 4)
 3.   
  • Mauaji ya jabali na uongozi
  • Kufungwa kwa soko la chapakazi
  • Njaa
  • Urisadi
  • Kufungwa jela kiholelea
  • Kuchapwa na askari
  • Uchafuzi wa mazingira
  • Migomo
  • Ulevi na matumizi ya dawa za kulevya
  • Kutowajibika kwa viongozi
  • Ubadhirifu wa mali ya umma
  • Kudhirifu wa mali ya umma
  • Kudhibiti vyombo vya habari
  • Utabaka
  • Ulipizaji kisasi
  • Usaliti

Swali la dondoo 6

“Udongo tungeliuwahi uli mbichi.  Limekuwa donda ndugu sasa.  Waliota ikakita na wakamea hata pembe.”

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
 2. Taja na kueleza tamathali moja ya usemi inayojitokeza kwenye dondoo hili. (alama 2)
 3. Eleza sifa zozote nne za msemaji wa kauli hii.   (alama 4)
 4. Dondoo hili linadhihirisha jinsi baadhi ya Wanasagamoyo walivyoshiriki kuivunja jumuiya yao.  Fafanua.

Majibu ya dondoo 6

 1.  
  • Msemaji ni Kenga
  • Anamweleza Majoka
  • Walikuwa ofisini mwa Majoka
  • Walikuwa wakizungumzia jinsi ya kuwakomesha watetezi wa haki
  • Majoka anaahidi kuwanyamazisha anaposema dawa yao anayo.
 2.   
  • Methali- udongo uwahi uli mbichi- kumaanisha wangewakomesha wapinzani walipoanza utetezi wao (kabla ya kupata nguvu zaidi)
  • Msemo- ndonda ndugu- kumaanisha tatizo ambalo haliishi (anarejelea jinsi kuna Tunu wanang’ang’ania kupigania haki za wanyonge)
  • Nahau- ota mizizi na mea pembe- nahau hizi zimetumiwa kuonyesha jinsi watetezi walivyo imara katika utetezi wao ( Ya kwanza 1x2=2) (kutambua ni alama 1, maelezoalama 1)
 3. Sifa za Kenga
  • Mbabedume/mwenye taasubi ya kiume - anaamini mwanamke hawezi kuwa shujaa Sagamoyo. Anashangaa sana Sudi anapomwonyesha kinyago cha shujaa wa kike alichokuwa akichonga.
  • Mpyaro - anamtukana Tunu kuwa yeye ni hawara.
  • Dhalimu - yeye na Majoka wanapanga vifo vya watu. Mfano ni mauajiyaJabali. Anapanga kuwaumiza watu kwa kutumia wahuni.
  • Fisadi – anajaribu kumhonga sudi kwa zawadi nyingi kutoka kwa Majoka. Aidha anapokea kipande cha ardhi ya pale sokoni alichomegewa na Majoka.
  • Mshauri mbaya - amnamshauri Majoka vibaya hasa kuhusiana na kutumia nguvu zaidi dhidi ya waandamanaji. Aidha anazua mpango wa kumtia Ashua kizuizini ili kumlazimisha Sudi kumchongea Majoka kinyago cha Ngao.
  • Mwenye majuto - anapozinduka, anakiri makosa yake ya kuwanyanyasa raia na kujiunga na wanasagamoyo
  • Msaliti - anamwacha Majoka na kujiunga na wanasagamoyo anapoona raia wanakaribia kufanya mapinduzi (Hoja 4x1=4)
 4.  
  • Ngurumo na wahuni wenzake kumshambulia Tunu na kumjeruhi vibaya.
  • Ngurumo kumsaliti Boza kwa kuzini na mkewe.
  • Kenga kumpa Majoka ushauri mbaya. Mfano, kufunga soko na kulipa kisasi dhidi ya wapinzani.
  • Majoka kumiliki kiwanda kikubwa zaidi cha kuzalisha sumu ya nyoka (dawa za kulevya zinazowahasiri vijana vibaya)
  • Majoka kuidhinisha ukataji wa miti- matokeo yake ni ukame na ukosefu wa chakula.
  • Majoka kutoa kibali kwa Asiya cha kutengeneza na kuuza pombe haramu inayowapofusha na kuwaua watu.
  • Majoka kuwafurusha wachuuzi sokoni. Ananyakua ardhi hiyo ili ajenge hoteli ya kibinafsi.
  • Majoka kuwapa wafanyakazi nyongeza ndogo ya mshahara huku akipandisha kodi
  • Uongozi wa Majoka kuwasaliti vijana kwa kutowapa ajira baada ya kufuzu mfano ni Tunu, Ashua na Sudi.
  • Viongozi kama Kenga kuwa na makundi haramu kama vile Kenga kuonekana akiwahutubia wahuni chini ya mbuyu.
  • Majoka kukopa pesa kutoka nje na badala ya kuendeleza maendeleo, anafuja pesa hizo kwa mradi wa kibinafsi wa uchongaji vinyago. Pesa hizo zitalipwa na umma kwa kipindi cha miaka mia moja.
  • Kampuni ya majoka kupandisha bei ya chakula kwenye kioski. Hii ni baada ya kulifunga soko.
  • Wizi wa kura- Majoka anazua mbinu za wizi wa kura kwa kuhofia ushindani na aendelee kusalia mamlakani.
  • Majoka kuwagawia wandani wake raslimali za umma. Mafano, Kenga anapewa kipande cha ardhi ya sokoni.
  • Ngurumo na walevi wenzake pale mangweni wanamdhalilisha Tunu. Anamweleza hawezi kumpigia kura, heri amchague paka kama si Majoka.
  • Majoka kuwatamani wanawake wengine licha ya kuwa na mke.
  • Majokma kuvitumia vyombo vya dola kudhulumu raia. Anawatumia polisi kuwaua vijana watano waliokuwa wanaandamana ili kupinga nyongeza ya bei ya chakula kwenye duka la kampuni.
  • Majoka kumchochea ashua dhidi ya mumewe Sudi- nia yake ni kuwatenganisha.
  • Majoka kupanga kukifunga kituo cha Runinga ya Mzalendo kinachowazindua wanasagamoyo kuzifahamu haki zao. (Hoja zozote 10x1=10)

Swali la dondoo 7

Utaiondoa karaha,
Usiwe kama juha,
Kujipa bure usheha,
Kutembea kwa madaha,
Eti waenda kwa staha,
Ndani kwa ndani kuhaha,
Domo mbele kama mbweha.
Dume acha mzaha,
Shika lako silaha,
Kujipa mwenyewe raha,
Iwe yako shabaha.

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
 2. Taja mtindo huu wa uandishi. (alama 1)
 3. Bainisha tamathali moja ya usemi inayojitokeza katika dondoo hili. (alama 1)
 4. Fafanua majukumu ya nafsineni katika tamthilia (alama 4)
 5. Kwa kurejelea wahusika mbalimbali katika tamthilia Kigogo. Eleza jinsi mwandishi alivyofanikiwa kutumia nyimbo kuendeleza maudhui, (alama 10)

Majibu ya dondoo 7

 1.  
  • Huu ni wimbo unayoimbwa na Asiya
  • Anawaimbia Subina Tunu
  • Anawaimbia wakiwa mangweni
  • Tunu na Sudi wanawalika waliokuwa mangweni kuhudhuria mkutano utakaofanyika mbele ya lango kuu la soko la Chapa kazi siku ya maadhimisho ya uhuru ilikushinikiza kufunguliwa kwa soko.     4×1=4Alama
 2. Wimbo
 3. Tashbihi. kwa mfano usiwe kama juha.
 4.  
  • Ametumiwa kufanikisha maudhui ya ulevi na athari zake- unywaji wa pombe haramu Imewafanya watu kuwa vipofu.
  • Ametumiwa kuonyesha udhalimu wa viongozi kwani anapewa kibali cha kuuza pombe haramu na Majoka.
  • Anachimuza changamoto zinazokumba ndoa kama ukware.
 5.  
  • wimbo wa uzalendo- wimbo unaoimbwa katika kituo cha habari cha uzalendo. Wimbo unaosifu Sagamoyo na kiongozi wake. 
  • Wimbo wa Hashima- wimbo unaoashiria kuwa mambo hubadilika, kilasiku wasema heri yalipita jana. Uk 51
  • Wimbo wa Ngurumo- Ngurumo anaimba wimbo wa kumsuta Tunu kwa kuwa yeye ni mwananke anapaswa kuolewa.
  • Wimbo waumati- umati wanaimba wimbo katika lango la soko la chapakazi. Watu wanaimba kuwa yote yanawezekana bila Majoka.
  • Wimbo wa Ashua- Ashua anaimba kuwa soko la funguliwa bila Chopi. Kumanisha vikaragosi hawananguvu dhidi ya wanamapinduzi.  5×2=10 Alama

Swali la dondoo 8

``Huu moyo wangu wa huruma nao..............................’’

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili.       alama4
 2. Fafanua sifa za msemaji.             alama 4
 3. Onyesha kinyume kinachojitokeza katika dondoo hili.        alama 12

Majibu ya dondoo 8

 1.  
  • Haya ni maneno ya majoka.
  • Anamwambia kenga
  • Walikuwa ofisini mwa majoka.
  • Wanazungumza kuhusu jinsi ya kuwaangamiza wapinzani kama walivyomwangamiza jabali. (4x1=4)
 2. Majoka
  • Mwenye taasubi ya kiume- Alisema kuwa hababaishwi na mwanamke na alimkemea kingi kwa kushindwa kukabiliana naye Tunu, mwanamke pia anamwita husda mwanamke, hamheshimu.
  • Mwenye hasira- Alitaka kumpiga kingi kwa kukaidi amri yake ya kuwapiga watu risasi. Pa alimsukuma kenga na kuanguka chini. Alikataa salamu za kenga ati alienda kumuona akijivinjari.
  • Mwenye kiburi-Alisema kuwa hawezi kuongea na upepo ilhali kulikuwa na watu wachache.
  • Mpyaro- Aliwaita wanasagamao wajinga.
  • Ana hisia za ukware – Alisema bado alimpenda ashula na alikuwa bado anamwandama lidia ya kuwa tayari alikuwa amemuoa husda.
  • Mbinafsi – Alishikanisha sherehe za uhuru na siku ya kuzaliwa kwake ili watu waisherehekee.
  • Fisadi –alisema kuwa hata wasipompigia kura moja, bado angeshida labda alinuia kuiba kura .Pia alikuwa amemtengea Kenya kipande chake sokoni.
  • Mjinga – yaonekana haelewi kuna katiba mpya anaelezwa na kingi. Hafahamu maana ya safari yake, anamuuliza babu.
  • kali – anamwambia kingi kuwa amefutwa kazi mara moja. Pia anamkaripia chopi na kumwambia asichizi na chui.
  • Mwenye moyo mgumu- Baada ya kuunda safari ya kujisafisha nafsi, hakubadilika, aliendelea kuwa katili. Alitaka watuwapigwe risasi.
  • Mwenye vitisho – Alimtishia chopi anapomletea habari ya kifo cha ngurumu. Anamwambia akishindwa na kazi kenga angeifanya kumaanisha angepoteza kazi.
  • Mwenye mapuuza- alipuuza ushairri wa Kenya wa kutoenda sokoni kwa sababu ilikuwa hatari. Afikapo huko, watu walitaka kumpiga na walimkataa kama kiongozi.
  • Muoga – Alimwambia babu asimwache peke yake. Pia alihofia watu waliolilia damu yake na kumhukumu.      (hoja 4x 1=4)
 3. mtahiniwa aonyesha kuwa msemaji ( majoka) hana huruma yaani ni katili.
  • anafunga soko la chopakazi
  • Anapanga mauaji ya jabali aliyekuwa mpinzani wake.
  • Alishirikiana na Kenya wanapanga kumwangamiza Tunu.
  • Mapanga kumu chopi kwa kutotekeleza mpango wa kumwangamiza tunu. Wanasema ni lazima aende safari.
  • Anamvumanisha ashua na husda katika ofisi yake na hatimaye kusababisha vurugu kati yao.
  • Hakumsaidia Ashua alipoenda kwake kumuomba msaada watoto walipokuwa hawana chakula.
  • Kampuni yake inawanyanyasa wafanyikazi jambo linalopelekea mgomo.
  • Wanaompinga/ wanaoandamana wanafurushwa na askari kutokana na armi yake.
  • Ingawa anaungwa mkono na ngurumo, baada ya kifo chake anasema kimba chake kifukine juu ya vingine.
  • Anaishi na husda na wakati huo huo anamtamani Ashua. Anamsababishia mkewe dhiki.
  • Anamwambia kenga kuwa atavunjwa na chatu. Anaonyesha kuwa katili na huenda akatumia vikosi vyake vya mauaji kumwangamiza.
  • Anamfuta kazi kingi baada ya kukataa kuwafyatulia risasi watu waliokuwa mkutanoni nje ya soko la chapakazi ni katili.
  • Majoka alishika ukosi wa shati lake kingi akitaka kumpiga. Alimsukuma Kenya akaanguka chini.

Swali la dondoo 9

Mmesikia? Hamtatuletea wazimu wenu hapa! Nendeni kama mmekuja kutuhasimu.

 1. Eleza muktadha wa maneno. (alama 4)
 2. Jadili umuhimu wa msemaji kwa hoja nne. (alama 4)
 3. Fafanua mbinu ya lugha iliyotumika. (alama 2)
 4. Kenga alichangia pakubwa msiba wa Wanasagamoyo. Thibitisha kwa hoja zozote kumi. (Alama 10).

Majibu ya dondoo 9

 1.  
  • Ni maneno ya Ngurumo   (al 1)
  • Kwa Tunu (al 1)
  • Wakiwa Mangweni (al 1)
  • Asiya/ Mamapima alikuwa amekasirika baada ya mteja mmoja kuondoka na kuwafukuza akina Tunu kwa kuwapa dakika moja waondoke ndipo Ngurumo akauliza Tunu iwapo wamesikia kuwa waondoke wakiwa na Sudi. Tunu alikuwa amesema hapo mbeleni kuwa ni hatia kuuza pombe haramu na kuwa katiba imezifafanua sheria za uuzaji na unywaji pombe.   (al 1)
 2.  Umuhimu wa Ngurumo
  • Anaendeleza maudhui ya ulevi; kijana anayejulikana kwa uraibu wa vileo
  • Anaendeleza maudhui ya taasubi ya kiume; kusema kuwa afadhali apigie paka kura kuliko mwamamke.
  • Anaendeleza maudhui ya uzinizu; kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mamapima ilhali ana mume.
  • Kielelezo cha usaliti ; anasaliti Wanasagamoyo kwa kuunga mkono uongozi dhalimu.
  • Anaonyesha ukatili wa Majoka; anauawa na chatu (kundi la Majoka) licha ya kuunga mkono utawala wa Majoka.
  • Anaonyesha ujinga wa Boza; Boza hagundui kuwa Boza ana uhusiano wa kimapenzi na mkewe licha ya kuwa mlevi mwenzake.
  • Kielelezo cha vijana ambao hawachangii katika maendeleo; anatumia wakati mwingi huko mangweni na hana mwelekeo.
 3.  
  • Kinaya; akina Tunu hawakuwa hasimu bali walitaka tu kuita watu kwa mkutano wa kusukuma viongozi wafungue soko na kuonyesha uvunjaji wa sheria katika kuuza pombe haramu.
  • kejeli; hamtatuletea wazimu wenu hapa.    (yoyote moja)
 4. Kenga alichangia pakubwa msiba wa Wanasagamoyo. Thibitisha kwa hoja zozote kumi. (Alama 10).
  • Kutoa ushauri mbaya kwa Majoka km kufunga soko na watu wengi walilitegemea.
  • Kuzorotesha usalama- alihutubia wahuni pale chini ya mbuyu na aliwatumia kuvuruga usalama. Alikuwa akipanga njama fulani.
  • Kupiganisha raia/ kufunga raia bure. Anamwambia Majoka aite Husda ofisini ili pakitokea vurugu kati ya Husda na Ashua, asingizie Ashua na kumtia ndani.
  • Kupendekeza wanaharakati wadhulumiwe- wanaharakati wawekewe vidhibiti mwendo na basi Majoka akawafukuza wafadhili na hivyo kulemaza upiganiaji haki.
  • Kupendekeza polisi watumie nguvu dhidi ya waandamanaji. Majoka basi akaamuru polisi watumie nguvu zaidi na kukatokea vifo.
  • Kupendekeza mauaji – ya wapinzani kama vile Jabali. Ya wanaharakati Tunu na Sudi kwa kupinga uongozi mbaya wa Majoka./ ya Chopi kwa sababu Majoka alisema Chopi anajua mengi kuliko inavyostahili.
  • Anaunga mkono udikteta- Majoka anapotaka kumrithisha Ngao Junior uongozi, Kenga anasema jambo hilo linafaa nah ii inanyima raia nafasi ya kuchaguana.
  • Kupendekeza runinga ifungwe na iadhibiwe kwa kupeperusha maandamano ya raia jambo amabalo lingeharibia sifa uongozi wa Majoka. Anasema Runinga ya Mzalendo ichukuliwe hatua lakini kituo cha Sauti ya Mashujaa kibakie.
  • Kutopinga miradi isiyo na faida na hata kuisimamia. Anafanikisha mradi wa kuchonga ambao unafilisi nchi na raia watalazimika kulipa deni kwa miaka mingi.
  • Kukubali kugawiwa ardhi ya umma. Majoka anamgawia kipande cha ardhi cha soko la Chapakazi alichonyakua.
  • Kufanikisha ubomoaji wa vibanda sokoni Chapakazi. Alisimamia ubomoaji bila kujali raia waliotegemea soko kwa mapato yao.
  • Kukubali ajira kwa njia ya mapendeleo- alikuwa binamuye Majoka na basi kuendeleza unasaba badala ya kupatia mtu ambaye angetoa ushauri mwafaka wa kuleta maendeleo.
  • Kuharamisha maandamano na basi kunyima raia haki ya kupigania haki yao ya kufunguliwa soko. Anamshauri Majoka kuyaharamisha. 10x1 (kadiria hoja yoyote nyingine ambayo ni sahihi)

Swali la dondoo 10

"Siwezi mimi, siwezi, sitaki kuwa gurudumu la akiba ..... hujayaacha hayo?"

 1. Eleza muktadha wa dondoo. (al.4)
 2. Eleza sifa nne za msemaji wa kauli hii. (al.4)
 3. Tambua matumizi 12 ya jazanda katika tamthilia. (12)

Majibu ya dondoo 10

 1.  
  • Msemaji ni Majoka
  • Msemewa ni Ashua
  • Wako ofisini mwa Majoka
  • Majoka alikuwa akimshawishi Ashua kimapenzi
 2. Sifa za Majoka
  Tazama majibu ya dondoo 8, swali la pili
 3.   
  • Bahari mchafukoge- ni jazanda ya mambo kumwendea mrama sudi. Kenga anamaanisha sudi atakumbwa na matatizo au changamoto kali za kimaisha iwapo hataacha kuingilia maswala ya uongozi mbaya wa mzee majoka.
  • Keki ya taifa - ni raslimali za nchi ambazo zinanuiwa kuwanufaisha watu wote katika jamii ya sagamoyo. Rslimali hizi zinawafaidi watu wachache kama vile majoka na vibaraka wake.
  • Makombo ya keki ya uhuru - (uk. 17) ni jazanda ya raslimali chache wanazopata watu kutoka kwa viongozi.
  • Asali - ni jazanda ya mapenzi mjo wa ashua unamfanya majoka kumwona mwanamke huyu kama mtu anayetaka maswala ya mapenzi kutoka ka majoka.
  • kutafuta nyuki - ni jazanda ya kutafuta mapenzi/mwanamume ili amkidhie mahitaji yake ya kimwili.
  • ... Ala moja haikai panga mbili....ala inaashiria. Ashua nazo, panga mbili ni sudi na majoka. Majoka anamfahamisha ashua kuwa wanaume wawili hawawezi kuwa na mwanamke mmoja. Kwa hivo ashua achague kuishi na mmoja wao.
  • Milango i wazi – (uk 23) majoka anatumia kwa ashua kama mbinu ya kumwonyesha kwamba, ingawa ameolea yuko tayari kumchukua na kukaa naye.
  • Kutoa tonge kinywani (uk. 27) - husda anatumia jazanda hii kumaanisha ........mumewe ambaye anashuku-kuwa tayari amenyakuliwa na ashua - Ni kutokana na hili ambapo yuko tayari kumshambulia mwanamke huyu.
  • Kuku na kanga (uk. 28) - Husda anatumia kama njia ya kuonyesha kuwa, kama ashua ameshindwa kumtunza mumewe kama ataweza kumtunza majoka ambaye ni wa kiwango cha juu akilinganishwa na mumewe ashua, bwana Sudi.
  • Vidhibitimwendo (uk. 33) - hii ni ishara ya kuwazua tunu na wengine wanaoongoza maandamano kukomesha tabia hii yao, na hatimaye kumaliza kabisa.
  • Kuwaweka mahalimpao (uk. 34) - hapa kenga anamaanisha yuko tayari kuwaua wote wanaoongoza maandamano na wanaopinga utawala wa majoka mmoja baada ya mwingine hadi waishe.
  • Kuota mizizi na kukita na kumea pembe (uk. 35) - kenga anatumia kumwonyesha majoka kwamba Tunu na wapinzani wengine wa mzee majika walianza mambo polepole kasha baadaye wakapata nguvu zaidi hadi sasa wanateleza vitrndo vinavyoenda kinyume na matakwa ya majoka bila woga wowote kama vile kuandaa maandamano.
  • kutotumia bomu kuulia mbu (uk. 35) - majoka anamfahamisha kenga kwamba hakuna haja ya kutumia nguvu nyingi kupambana na wapinzani wake kama vile akina tunu. Kwake anawaona wakiwa watu wadogo sana ambao wanahitaji nguvu kidogo kuwaangamiza.
  • Kucheza na simba anayenyonyesha (uk. 37) simba ni ishara ya majoka ambaye ni hatari kama simba , huku kutia mikono katika mdomo wa simba ni ile hali ya tunu kuingilia uongozi wa Majoka kwa namna ya kutaka kuuporomosha. Hapa majoka anamwonya tun kwmba ni hatari sana kuingilia utawala wake kwa njia hii.

Swali la Dondoo 11

 

“na uuchunge sana ulimi wako usikutome kwenye bahari mchafukoge usi…”

 1. Fafanua muktadha wa dondoo hili. (al 4)
 2. Eleza sifa mbili za msemaji (al 2)
 3. Eleza umuhimu wa msemewa katika kazi hii (al 2)
 4. Kwa kurejelea dondoo hili na tamthilia kwa jumla, eleza jinsi msemewa na wenzake walitiwa katika bahari mchafukoge. (al 12)

Majibu ya Dondoo 11

 1. Fafanua muktadha wa dondoo hili. (al 4)
  • Maneno haya yanasemwa na Kenga. Anamzungumzia sudi, wakiwa katika karakana yao kwenye soko la Chapakazi. Kenga anamwita Tunu hawara jambo linalomkasirisha Sudi baada ya kukataa kumchongea ngao kinyago
 2. Eleza sifa mbili za msemaji. (al 2)
  1. Katili - Anamwambia Majoka aache moy wa huruma ili polisi watumie nguvu zidi kuwatawanya waandamanaji
   • Anashirikiana na Majoka kupanga kifo cha Jabali
   • Anapanga mauaji ya Tunu.
   • Anapanga kifo cha Chopi.
  2. Kibaraka - Ni kibaraka wa Majoka. Anataka kujua kama shujaa anayechongwa na Sudi anatambuliwa na Majoka.
   • Anakubali yote anayoambiwa na Majoka.
  3. Mshauri mbaya - anamshauri Majoka kulifunga soko.
   • Anamshauri pia atangaze kuwa maandamano ni haramu
   • Anakubali pendekeso la Majoka la kufunga runinga ya mzalendo
  4. Mwenye mapuuza/asiyewajibika
   • Anasema kuwa ‘Tunu hawezi kupigiwa kura hata!’
   • Anapoona kinyango cha mwanamke kikichongwa, anasema, “Tena ni wa kike? Sagamoyo ishawahi kuwa na mashujaa wa kike kweli?” Anakataa kufuatilia ili ajue ni nani hasa anayechongwa, na anavyoathiri utawala wa Majoka.
  5. Mwenye taasubi ya kiume
   • Anauliza, “Tena ni wa kike? Sagamoyo ishawahi kuwa na mashujaa wa kike kweli?
  6. Mpyaro
   • Anamwita Tunu haware anaposema, “umelishwa kiapo na huyo hawara wako, sio?’
    (zozote mbili)
 3. Umuhimu wa sudi
  • ni kielelezo cha watu wazalendo wanaojitolea kupigania haki katika jamii
  • ni kielelezo cha watu wenye ujuzi katika jamii kwa sabu alikuwa mchongaji Hodari
  • ni kielelezo cha watu waliosoma katika jamii kwa kuwa alifanya uanasheria
 4. jinsi sudi na wenzake walitiwa katika mchafukoge
  1. Kutiwa jela- ashua anatiwa jela
  2. Kutishwa-hashima wanatupiwa vikaratasi wahame
  3. Kufungiwa soko-wasifanye biashara
  4. Kuuliwa- jabali kuuliwa na majoka na vijana kuuwawa
  5. Kuongezwa mshahara na kupandishiwa kodi-walimu na madaktari
  6. Kupewa ahadi hewa-sudi kuahidiwa kupelekwa ughaibuni
  7. Matumizi ya vyombo vya dola-polisi wanawaua vijana
  8. Kunyakuliwa ardhi- ya soko la chapakazi ili majoka ajenge hoteli ya kifahari
  9. Kuvunjwa miguu-tunu
  10. Kupigwa-tunu na waandamanaji
  11. Kusimangwa-tunu anasimagwa na walevi
  12. Fumanizi- majoka kumwita Ashua ili amfumanishe na mkewe
  13. Ubaguzi – kandarasi kutolewa kwa vikaragosi 

Swali la Dondoo 12

 

"Kutia kwa kulia na kutoa kwa kushoto".

 1. Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 4)
 2. Fafanua mbinu ya lugha iliyotumika. (alama 2)
 3. Fafanua sifa nne za msemaji wa maneno haya. (alama 4)
 4. Jadili mbinu hasi za uongozi katika Tamthilia. (alama 10)

Majibu ya Dondoo 12

 1. Maneno ya Kenga
  • Anamwambia Majoka
  • Ofisini mwa Majoka
  • Wanaongea kuhusu mshahara wa walimu na wauguzi kuongezwa na Majoka anasema wataiongeza kisha waongeze kodi ili wafanye hesabu ya kutia na kutoandio Kenga akamwambia maneno haya.
 2.      
  • kinaya- Kutia kwa kulia na kutoa kwa kushoto
  • tanakuzi- kutia na kutoa
 3. Kenga
  • Mshawishi
  • Mpyaro
  • Mwenye vitisho
  • Mwenye hasira
  • Dhalimu
  • Mwoga
  • Fisadi
  • msaliti
  • karagosi
  • nafiki
  • mwoga
  • katili
  • mshauri mbaya
 4.    
  • Kuua wapinzani. Jabali
  • Kuwapa likizo ndefu. Anataka kuwafurahisha kwani wafanyakazi hawataenda kazini.
  • Kuharamisha maandamano. Ili raia waache kupinga kufungwa kwa soko. 
  • Kufurusha wafadhili wa wapiganiaji haki. Wafadhili wa akina Tunu na Sudi wanatakikana wavunje kambi ili kudhoofisha kifedha.
  • Unafiki/hila/udanganyifu. Kuongeza walimu na wauguzi mshahara lakini anapandisha kodi hivyo hawajafaidika.
  • Kuvunja sheria. Kufuta Kenga kazi kinyume cha katiba kwa kukataa kufyatua risasi kwa raia ambao hawajafanya makosa.
  • Kufukarisha raia. Ili wamtegemee km kufunga soko ambalo ni tegemeo la raia. Ashua anakosa chakula na watoto wakala njaa na akamwendea Majoka msaada. 
  • Kutumia wahuni. Majoka kutumia wahuni kupambana na wapinzani wake km Tunu kuvamiwa na kuvunjwa mguu kwa kupinga soko kufungwa. 
  • Kujaza hofu. Bi Hashima waishi kwa hofu.
  • Kutumia jela. Kufunga Ashua ili mumewe Sudi achongee Majoka kinyago alichokuwa amekataa hapo mbeleni.
  • Kutumia askari. Polisi wanatumia vitoa machozi na risasi ili wasiendelee kupiga soko kufungwa.
  • Kutumia vishawishi na hongo. Tunu na Sudi wanapatiwa kazi katika kiwanda cha Majoka ili wamuunge mkono kisiasa lakini wanakataa. 
  • Kufunga vyombo vya habari. Runinga ya Mzalendo. Kwa kukashifu vitendo vya Majoka kwa kupeperusha maandamano moja kwa moja kupinga kufungwa kwa soko.
  • Tenga tawala. Majoka kutaka kuongea na Tunu na Sudi kando kando, mhuni mmoja kumwambia Tunu kuwa Sudi na Ashua ndio wanawinda  roho yake. 
  • Unasaba. Kuteua binamuye Kenga kuwa mshauri wake mkuu ili iwe rahisi kutekeleza maovu km kuua Jabali.

Swali la Dondoo 13

 

"Wewe ni msichana mdogo hata ubwabwa wa shingo haujakutoka ila tu umenaswa katika utandu wa kasumba na flasafa za ukoloni mambo leo".

 1. Yape maneno haya muktadha wake. (al.4)
 2. Bainisha mbinu mbili za kimtindo ambazo zimetumika katika dondoo hili. (al. 2)
 3. Kwa kumrejelea msemewa wa maneno haya; onyesha kinyume cha maneno yaliyopigiwa mstari. (al. 12)

Majibu ya Dondoo 13

 1. maneno ya Majoka.
  1. kwa Tunu
  2. Ofisini mwa Majoka.
  3. Ni baada ya Tunu kumhoji Majuka Kuhusu vijana watano waliouwawa
 2. Msemo - ubwabwa wa shingo (Hajakomaa)
  1. Taswira (mguso) naswa katika utando Wa Kasumba na falsafa za ukoloni mamboleo.
  2. Utohozi - faisafa
 3. Kukomaa kwa Tunu.
  Wakati Asiya anamwomba msamaha anamsamehe.
  1. Anajua umuhimu wa usalama - anapomwona Kenga akihutubia wahuni chini ya mbuyu anahofia usalama wa wananchi na kuwataka Kombe Bora na sudi waende Wasiklia
  2. Anakataa ujenzi wa hoteli ya kibinafsi. Kwenye uwanja wa soko. Andenda kwa Ofisi ya Majoka na kumwambia kuwa hatajenga hoteli ya kibinafsi hapo.
  3. Anawahimiza raia kususia mkutano wa majoka ili kumshinikiza kulifungua soko
  4. Anakashifu upikaji wa pombe haramu anamwambia Asiya kuwa imewauwa watu wengi
  5. Amewahi kuwa kiongozi wa wanafunzi 
  6. Anawahimiza wanasagamoyo kutowachagua viongozi wanaowatusi


Swali la Dondoo 14

 

”Mimi sili makombo kama kelbu!Nilishakunywa chai ya mke wangu nikaridhika.”

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili.(alama 4)
 2. Jadili umuhimu wa msemaji katika tamthilia hii.(alama 6)
 3. Wanasagamoyo wamefanywa kelbu kula makombo.Thibitisha kauli hii.(alama 20)

Majibu ya Dondoo 14

 1. Eleza mukatadha wa dondoo hili.(alama 4)
  • Msemaji ni Sudi
  • Msemewa ni  Boza na Kombe
  • Wakiwa katika karakana ya uchongaji  Katika Soko la Chapakazi
  • Ni baada ya Sudi kususia makombo ya keki iliyotolewa  na Kenga kwa kuwa alijua kulikokuwa keki kubwa.
 2. Jadili umuhimu wa msemaji  katika tamthilia hii.(alama 6)
  • Kuendeleza ploti-Anapotumia simu yake ya rununu kama redio kumsikiza matangazji kuhusu sherehe ya kuadhimisha uhuru
  • Kukuza maudhui ya uzalendo-pamoja na Tunu kutetea haki za wananchi
  • Kukuza sifa za wahusika wengine-Ashua ni kigeugeu anapota kumtaliki  akiwa kizuizini
  • Anaendeleza ukosefu wa kazi-baada yake kuhitimu kama mwana sharia bado hajapata kazi ya taaluma yake
  • Ni kielelezo cha wananchi wazalendo-anakataa kuchonga kinyago baada ya kuamrishwa na Kenga ili afaidike peke yake-
  • Ni kielelezo cha watetezi wa haki katika jamii- anashirikiana na Tunu kutetea haki za wanasagamoyo dhidi ya uongozi dhalimu wa Majoka.
   Hoja zozote 6*1=6
 3. Wanasagamoyo wamefanywa kelbu kula makombo.Thibitisha kauli hii.(alama 10)
  • Wanasagamoyo wanafungiwa  soko ambalo lilikuwa  adimu kwao 
  • Wanasagamoyo wanapandishiwa bei ya bidha a katika kioski ya soko
  • Vijana wanauawa wakati wa migomo
  • Wanasagamoyo wanafungiwa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii
  • Wanasagamoyo wanarushiwa vijikaratasi vya kuwataka kuhama Sagamoyo-Siti na Kombe
  • Walimu wanaongezewa mishahara na kupandishiwa kodi wakati huo huo
  • Majoka ananyakuwa soko la Chapa kazi kwa lengo la kujenga Hoteli yake ya kifahari.
  • Majoka anawagawia vikaragosi wake ardhi –Kenga
  • Majoka anafungulia  biashara ya ukataji wa miti na kusababisha ukame kwa sababu ya kukauka kwa mito na maziwa.
  • Pombe haramu inawafisha walevi baada ya mama Asiya kupewa kibali na Majoka kuiuza.

Swali la Dondoo 15

 

 1. “Ni kiwandani ninakofanyia kazi; Majoka and Majoka ...wamewaua…”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  2. Bainisha vipengele vitatu vya kimtindo katika dondoo hili. (alama 3)
  3. Fafanua sifa mbili za nafsinenewa katika dondoo hili. (alama 2)
 2. Eleza sababu tano za maandamano katika tamthilia ya Kigogo. (alama 5)
 3. Jadili umuhimu wa mandhari ya soko la chapakazi katika kuijenga tamthilia hii. (alama 6)

Majibu ya Dondoo 15

 1.  
  1. Msemaji – siti
   Msemewa – sudi
   Mahali – Ni barazani mwa nyumba ya Sudi/katika nyumba ya Sudi alitaka kufahamu sababu ya maandamano ya wafanyakazi katika kiwanda cha Majoka.
   4x1=4
  2. Mdokezo – Majoka …wamewaua
   Taswira (oni) waliokuwa wakindamana.
   Takriri – Majoka. majoka.
   Kuchanganya ndimi – Majoka and majoka. 3x1=3
  3. Sudi
   Mtetezi wa haki – anadai kuwa ni jukumu la viongozi kuhakikisha soko ni safi.
   Mwenye bidii – Anachapa kazi ya kuchonga vinyago kwa bidii.
   Jasiri – anamuambia Kenga kuwa hawezi kuchonga kinyago cha ngao wanavyotaka. (Tathmini majibu ya mwanafunzi – sifa za sudi ni nyingi) 2x1=2
 2.        
  1. Kupanda kwa bei ya chakula katika kioski cha kampuni.
  2. Mazingira chafu. soko la chapakazi ni chafu na ilhali wachuuzi wanalipa kodi ya kusafisha.
  3. Mishahara duni. Walimu, Wauguzi wanashiriki maandamano kulalamikia mazingira duni ya kai pamoja na mishahara duni.
  4. Kufungwa kwa soko la chapalazi. Wachuuzi katika soko hili wanaandamana ili soko lifunguliwe.
  5. Mauaji ya watu bila hatia. Vijana watano ,wachuuzi sokoni wanauliwa bila hatia.
  6. Pesa za kusafisha soko zimefujwa na viongozi na kusababisha soko kutosafishwa.
  7. Wachuuzi kunyimwa haki zao. Wanafungiwa soko na kushindwa kuendelea kufanya biashara zao.
  8. Ukosefu wa ajira kwa vijana. Sudi, Tunu wamesoma hadi chuo kikuu lakini wanakosa kazi ya kufanya.
  9. Ufisadi – matumizi mabaya ya fedha/mali ya umma. mfano pesa za kusafisha soko zinafujwa. 5x1=5
 3.    
  1. Yanajenga sifa za wahusika mbalimbali. Mfano sudi kuwa mwenye bidii. Anafanya kazi ya kuchonga vinyago kwa ustadi.
  2. Yanajenga maudhui mbalimbali. Mfano uchafuzi na mazingira. soko ni chafu, taka, maji machafu yanayopita mtaroni.
  3. Yanaonyesha ukosefu wa uwajibikaji wa viongozi. Kodi inalipwa lakini soko halisafishwi.
  4. Yanajenga mbinu za lugha mfano uk.2 Nidaa Do!, mdokezo uk.3.
  5. Yanajenga ufaafu wa anwani “Kigogo”. Majoka anaamuru kipindi cha mwezi mmoja kusherehekea uhuru.
  6. Yanajenga ploti. Majoka anafunga soko, mkondo wa matukio unabadilika, wanasagamoyo wanaandamana. 6x1=6


Swali la Dondoo 16

 

“Mtalipa kila tone la damu mlilomwaga sagamoyo ;wewe na watu wako.”

 1. Eleza muktadha wa maneno haya (alama 4)
 2. Eleza sifa za mzungumzaji (alama 4)
 3. Thibitisha kwa kutoa mifano kuwa maisha ya anayezungumziwa yametawaliwa na dhuluma. (alama 12)

Majibu ya Dondoo 16

“Mtalipia kila tone la damu mlilomwaga Sagamoyo ;wewe na watu wako.”

 1. Eleza muktadha wa maneno haya (alama 4)
  1. Maneno ya ni Tunu.
  2. Akimwambia Majoka.
  3. Ofisini mwa Majoka
  4. Ashua alikuwa gerezani.
 2. Eleza sifa za mzungumzaji (alama 4)
  1. Sifa za Tumu.
  2. Mwanamapinduzi
  3. Msomi
  4. Mtetezi
  5. Mwajibikaji
  6. Mwenye mlahaka mwema na wahusika wengine.
 3. Thibitisha kwa kutoa mifano kuwa maisha ya anayezungumziwa yametawaliwa na dhuluma.
  • Majoka
   1. Kutoza kodi ya juu isiwasadi wafanyi biashara sokoni.
   2. Kando ya kulipa kodi wanalazimishwa kutoa kitu kikubwa juu ya kodi – kulingana na Ashua.
   3. Anafunga soko la chapakazi bila kuwapa wafanyi biashara njia mbadala ya kukidhi mahitaji yao.
   4. Anawalazimisha raia kusherehekea uhuru kwa mwezi mmoja.
   5. Anamtaka Ashua mapenzi anapoenda kwake kumtaka usaidizi.
   6. Anamlazimisha Sudi kuchonga kinyago bila hiari yake.
   7. Anawaongeza walimu na madktari mshahara pia anaongeza ushuru ili wasifaidike na nyogeza hiyo.
   8. Ana nia ya kujenga hoteli yake ya kifahari palipo soko la Chapakazi.
   9. Aliwaua wapinzani wake - Jabali.
   10. Anapanga kumwangamiza Tunu akiendelea kumpinga.
   11. Anaendeleza ukataji wa miti kuchangia uharibifu wa mazingira / ukame na njaa .
   12. Anatumia polisi vibaya kuwapiga na kuwaumiza waandamanaji.

Swali la Dondoo 17

 

 …… kila mtu sagamoyo hafanyi kazi yakek – hata hao chatu! Kwa hivyo wataka niache raha zangu, nijishike kichwa nilie?

 1. Eleza muktadha wa dondooo hili. (alama 4)
 2. Taja na ufafanue mbinu mbili za lugha zilizotumika katika dondoo hili. (alama 4)
 3. Kwa kutolea mifano mwafaka, angazia nafasi chanya alizopewa mwanamke katika tamthilia ya Kigogo. (alama 12)

Majibu ya Dondoo 17

…… kila mtu sagamoyo hafanyi kazi yake – hata hao chatu! Kwa hivyo wataka niache raha zangu, nijishike kichwa nilie?

 1. Eleza muktadha wa dondooo hili. (alama 4)
  • Msemaji ni Majoka.
  • Alikuwa anamwambia chopi maneno haya.
  • Chopi alikuwa amemfahamisha kuwa ngurumo amenyongwa na chatu
  • Majoka alikuwa katika hoteli la kifahari la Majoka and Majoka Modern Resort akiwa na mkewe Husda.
 2. Taja na ufafanue mbinu mbili za lugha zilizotumika katika dondoo hili. (alama 4)
  • ….. hao chatu! Nidaa.
  • ….. Nijishike kichwa nilie? Swali la balagha.
 3. Kwa kutolea mifano mwafaka, angazia nafasi chanya alizopewa mwanamke katika tamthilia ya Kigogo. (alama 12)
  1. NI shujaa na mkombozi:
   • Tunu amesawiriwa kama shujaa, mwanaharakati wa ukombozi wa jamii yake. Anashirikiana na wengine kuimbia jamii kutokana na uongozi dhalimu na majuka. Anawashauri vijana Mangweni kuwacha pombe haramu kutokana na madhara yake.
  2. Mwanamke ni mtetezi wa haki.
   • Ashua na Tunu wako mstari wa mbele kutetea haki za watu. Ashua anamwambia Majoka hakufanya vyema kufunga soko. Tunu anamsuta vikali Majoka kwa sabbu ya mauaji katika kampuni ya Majoka and Majoka Company.
  3. Mwanamke ni mwenye utu
   • Tunu anamshauri siti kuwapeleka watoto wa Sudi kwao wakale na watunzwe na Bi. Hashima. Siti anafika kwa kina Tunu kumjulia hali baada ya Tunu kuvamiwa na kuumizwa na wahuni.
   • Husda anaonyesha utu kwa namna anayomshughulikia mumewe baada yake kuzirai.
  4. Mwanamke ni jasiri
   • Ashua anamkosoa majoka waziziz kwa kulifubga soko ambalo ni tegemeo la wanajamii wengi. Pia anamwambia wanafunzi katika majoka and majoka Acadeny hawafuzu na huishia buwa makabeji kwa kudungana sumu ya nyoka
   • Tunu anamkashifu majoka kwa kuhusika na vifo vya vijana watano wa Kampuni yake. Pia anamwambia mwanawe (Ngao Junior) si mume ni gugume.
  5. Mwanamke ni mcha mungu
   • Siti anakiri kuwa wanamtegemea Mungu kuwaondolea dhika waliokua wakipitia.
   • Hashima anasema ni vyema wamwombe Mungu kabla ya Tunu Kuondoka.
  6. Mwanamke ni msomi
   • Ashua na TUnu Wakesoma hadi chuo kikuu ni kupata shahada.

Swali la Dondoo 18

 

“Wewe nawe hukualikwa. Wataka kutia siasa tayari? Hamkosi kutia doa kila jambo zuri.” 

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)
 2. Eleza vipengele viwili vya kimtindo alivyotumia msemaji kufanikisha uwasilishaji wa ujumbe. (Alama 2)
 3. Fafanua sifa nne za anayeambiwa maneno haya. (Alama 4)
 4. Fafanua jinsi mambo mazuri yalivyotiwa doa katika tamthiliya hii. (Alama 10)

Majibu ya Dondoo 18

“Wewe nawe hukualikwa. Wataka kutia siasa tayari? Hamkosi kutia doa kila jambo zuri.”

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)
  • Haya ni maneno ya Boza. Anamwambia Sudi. Wapo katika karakana yao sokoni. Ni baada ya kupata habari kupitia kwa redio ya simu ya Sudi kuwa wananchi watakuwa wakisherehekea mwezi mzima kuadhimisha miaka sitini ya uhuru. Komba anataka kujua watu watakula nini
   muda huu wote bila kazi. Sudi anajibu kwa kejeli kuwa wangekula mali walizochuma miaka sitini iliyopita. Boza anaona kuwa jibu hili ni la kutia doa mambo mazuri.   
   (4×1= 4)
 2. Eleza vipengele viwili vya kimtindo alivyotumia msemaji kufanikisha uwasilishaji wa ujumbe. (Alama 2)
  • Balagha- wataka kutia siasa tayari?
  • Kinaya- anaamini kuwa mwezi mzima wa sherehe bila kazi ni jambo bora.   (zozote 2×1= 2)
 3. Fafanua sifa nne za anayeambiwa maneno haya. (Alama 4)
  Sifa za Sudi
  • Ni mwenye msimamo thabiti. Anakataa katakata ushawishi wa Kenga anayemtaka amchongee Majoka kinyago cha babake, Ngao Marara. Anashikilia kuwa yeye anamchonga shujaa halisi wa Sagamoyo, Tunu (uk 10–12).
  • Ni mzalendo. Anajitolea kwa hali ili kuikomboa Sagamoyo kutoka kwa uongozi mbaya wa Majoka.
  • Mwenye mapenzi ya dhati. Anampenda sana mkewe Ashua. Anapopata habari za kushikwa kwake anaenda moja kwa moja hadi gerezani kumwona (uk 46).
  • Mshauri mwema. Anatumia muda wake mwingi kule karakarani kuwashauri Kombe na Boza kujaribu kuona ukweli wa uongozi mbaya wa Majoka.
  • Mwenye kuwajibika. Anawajibikia jamii yake. Anafanya kazi ngumu ya uchongaji wa vinyago ili aweze kuikimu jamii yake licha ya pato duni.
   (zozote 2×1= 2- mtahiniwa ataje kuwa mwambiwa ni Sudi)
 4. Fafanua jinsi mambo mazuri yalivyotiwa doa katika tamthiliya hii. (Alama 10) 
  • Maji machafu (uchafuzi wa mazingira) yalipita mtaroni na kueneza harufu mbaya kila mahali bila uongozi wa Sagamoyo kuliona hili kuwa tatizo (uk 2).
  • Soko la Chapakazi limebadilishwa na kufanywa uwanja wa kumwagia kemikali (uk 2). ⮚ Wafanyabiashara wanahangaishwa na  wanaosanya ushuru kwa kuwaitisha kitu kidogo na wengine kitu kikubwa (uk 2–3).
  • Serikali kutangaza mwezi mzima wa kusherehekea uhuru bila watu kufanya kazi ilhali haijali watakachokula watu (uk 4).
  • Serikali ya Sagamoyo haina mipango maridhawa ya kimaendeleo. Majoka anamiliki kampuni kubwa ya sumu ya nyoka badala ya miradi muhimu (uk 4).
  • Kuna ufisadi unaomfanya Asiya kupata kandarasi ya uokaji keki ya uhuru kwa kujuana na Husda bali si kwa kufuzu na kufaulu (uk 7).
  • Utawala wa Sagamoyo ni wa kimabavu. Kenga anamlazimisha Sudi amchongee Majoka kinyago cha Ngao licha ya kujua kuwa uongozi wa Majoka ni wa udhalimu (uk 9).
  • Kombe, mshiriki wa karibu wa Kenga anakiri kuwa mambo yameenda kombo Sagamoyo (uk 15). ⮚ Uongozi unafunga soko la Chapakazi. Soko hili ndilo kitegauchumi pekee kwa Wanasagamoyo (uk 25).
  • Kuna maandamano ya mara kwa mara na yasiyotatuliwa katika jimbo la Sagamoyo, wanachi wanapigania haki zao.
  • Majoka anawatumia polisi wake vibaya ili kujidumisha uongozini. Polisi wanawanyanyasa na kuwadhulumu wananchi bila Majoka kujali.
  • Sagamoyo kuna uongozi wa ubinafsi. Majoka anataka kuendeleza ubinafsishaji wa uongozi wa Sagamoyio kwa kumtangaza rasmi Ngao Junior kuwa mrithi wake (uk37).
  • Kuna unyakuzi wa mali ya umma. Majoka analifunga soko na kuinyakua sehemu hiyo ili ajenge hoteli ya kifahari (uk 45). (zozote 10×1= 10)

Swali la Dondoo 19

 

“… binadamu ni mavumbi na mavumbini aatarejea kwa maana, kwa tamaa mtu amependa kula kuku huku nduguze wakila kama kuku. Na katika uchu huo huo amependa kukifikia kilele cha ufanisi kwa kukanyaga migongo ya wenziwe. Hatajali kufanya  ujahili uwao ule, hata kupora wafu, almradi tu aweze kulifikia dhamirio lake.’’

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4) 
 2. Eleza aina mbili za taswira zinazojitokeza katika dondoo. ( alama 4)
 3. Tambua mbinu nyingine mbili za kimtindo katika dondoo hili. (alama 2)
 4. Eleza umuhimu wa mandhari ya dondoo hili. ( alama 10)

Majibu ya Dondoo 19

 1.  
  1. msemaji ni Babu
  2. msemewa ni majoka
  3. katika chumba cha wagonjwa
  4. kuhusu maovu ya majoka (4x1)
 2.      
  1. taswira muonjo – wakila kama kuku
  2. taswira mguso – kukangaga migongo ya wenziwe ( 2x 2)
 3.      
  1. Tashbihi – wakila kama kuku
  2. msemo – kukanyaga migongo ya wenziwe
  3. jazanda – kukanyaga migongo ya wenziwe ( kunyanyasa)
  4. takriri – kuku / mavumbi n.k
 4.      
  • usaliti katika ndoa – majoka hampendi husda uk.76
  • nafasi ya mwanamke – wasioweza kutegemewa uk.76
  • ukosefu wa uwajibikaji wa uongozi – hajashika usukani uk 80
  • wanasagamoyo wamezinduka – wanalilia damu yake uk79
  • mgogoro wa kinafsi – kilio kikubwa ndani kwa ndani –uk 75
  • kudokeza hatari inayongojea majoka – mikono yangu imefungwa kwa minyororo uk 73
  • kuchimuza matokeo ya awali – kuuawa kwa jabali  uk73
  • kuonyesha sifa za wahusika – tama ya husda uk 
  • sagamoyo haipigi hatua kimaendeleo – uk 81 .
  • mgongano kati ya utawala wa Babu na ule wa Majoka – kutikisa na kuubadilisha mkondo uk8 ( zozote 5x 2 = 10)

Swali la Dondoo 20

“Nusura roho inianguke mwanangu, wametutia woga mwingi sana. Twaishi kwa hofu…”

 1. Fafanua muktadha wa dondoo hili. (al 4)
 2. Mnenaji wa usemi huu ana hofu gani? (al 2)
 3. Taja sifa tatu za mnenewa. (al 3)
 4. Bainisha mbinu moja ya lugha kutoka kwenye dondoo. (al 1)
 5. Wananchi katika maeneo haya wanapitia changamoto zipi? (al 10)

Majibu ya Dondoo 20

‘Nusura roho inianguke mwanangu, wametutia woga mwingi sana. Twaishi kwa hofu…’

 1. Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  • Ni maneno ya Hashima akimuelezea Siti.
  • Walikuwa nuymbani kwa hashima, baada ya kupokea vijikakaratasi na vitisho kwamba watawaua la sivyo wahame. 4×1= al 4
 2. Mnenaji wa usemi huu ana hofu gani ? (alama 2)
  • Kutishiwa kuhama.
  • Mwanawe tunu atawaua na vibaraka wa majoka.
  • Makaazi yake yatabomolewa. 1×2= al 2
 3. Taja sifa tatu za mnenewa (alama 3)
  • Mnenewa ni siti.
  • Mtetezi wa haki.-
  • Mdadisi. Anachunguza na kufahamu kiinI cha mauwaji ya vijana watano. 3×1= al 3
 4. Bainisha mbinu moja ya lugha kutoka kwenye dondoo. (alama 1)
  • Uhuishi – nusura roho inianguke.
  • Msemo- twaishi kwa hofu. 1×1= al 3
 5. Wananchi katika maeneo haya wanapitia changamoto zipi ? (alama 10)
  • Kupigwa na polisi wanapoandana.
  • Kuwaua wanapopinga uongozi.
  • Mazingira machafu.
  • Ukosefu wa shule nzuri ,watoto wa shule ya majoka and mojoka academy huiishia kuwa makabeji.
  • Vitisho vya kufukuzzwa kutoka sagamoyo.
  • Ardhi zao kunyakuliwa na viongozi.
  • Madeni yanayotokana na mikopo inayoombwa na viongozi na kulipwa na vizazi vingi.
  • Ahadi za uongo kutoka kwa viongozi.
  • Gharama ya Maisha kupanda kila kuchao., bei ya bidhaa kupandishwa juumara kwa mara.
  • Wafanyakazi kulipwa mishahara duni, mfano walimu na wauguzi.
  • Viongozi kupuuza malalamishi ya wananchi.
  • Wafanyabiashara kutozwa kodi ya juu.
  • Wananchi kutiwa gerezani kwa amri ya viongozi bila kupitia mahakamani kisheria.
  • Vyombo ya habari vinavyowafaa wananchi kufungwa kwa amri ya kiongomfano runinga ya mzalendo.
  • Maandamano ya wananchi kutajwa kuwa si halali ilhali wanaumia.

Swali la Dondoo 21

Na wewe! Eeeh kidudumtu, hata haya huna. Umegeuka stesheni ya udaku. Tafuta kazi ufanye, umbeya hauna posho nyanya!

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili (al. 4)
 2. Eleza vipengele viwili vya kimtindo alivyotumia msemaji katika dondoo hili. (al. 2)
 3. Fafanua sifa sita za msemaji wa maneno haya. (al. 6)
 4. Jadili mambo yanayoyumbisha asasi ya ndoa kwa mujibu wa tamthlia hii. (al. 8)

Majibu ya Dondoo 21

 1. Uk 27
  1. Husda
  2. Ashua
  3. Ofisini kwa Majoka
  4. Majoka amemfumanisha mkewe na Ashua kukazuka ugomvi 4 x 1 =4
 2. vipengele vya kimtindo
  1. nidaa/usiyani – Na wewe! Eeh!
  2. Kejeli/stihizai – kidudumtu
  3. Jazanda – stesheni ya udaku zozote 2 x 1 =2
 3. sifa za Husda (awe amemtaja)
  1. tamaa – anapenda mali
  2. mpenda anasa – anajifurahisha huko Majoka and Majoka Resort
  3. msinzi – anamtamani chopi kimapenzi
  4. Mpyaro – anamtukana Ashua
  5. wivu – hataki kumwona Majoka na mwanamke mwingine
  6. mwenye malalamiko – anadai Majoka haonekani kwake
  7. mwenye hasira – anampiga Ashua mbele ya Majoka
  8. Anamwajibikia Majoka anapozirai zozote 6 x 1 =6
 4. mambo yanayoathiri ndoa
  1. vifo – hashima ni mjane
  2. harakati za ukombozi – Sudi anasemwa kuwa mpenzi wa Tunu – Ashua halifurahii suala hili.
  3. Ukosefu wa kipato – unafanya Ashua kujipata mikononi mwa Majoka
  4. Hongo – Ngurumo analala na Asiya ili amsaidie kupata kandarasi ya kuoka keki
  5. uhaba wa chakula unafanya Ashua kumlaumu mmewe kuwa hajibidiishi
  6. Viongozi kama Majoka wanachonganisha wan ndoa. Zozote 4 x 2 =8

Swali la Dondoo 22

“Hivyo vipembe vyao niwachie mimi profesa wa siasa. Michezo ya kitoto huchezwa kitoto. Hatutatumia mabomu kuulia mbu. Hawa ni wadogo. Usiichoshe akili bure. Dawa ninayo.

 1. Fafanua muktadha wa maneno haya. (al. 4)
 2. Huku ukitoa mifano kumi na sita, jadili dawa anayoirejelea msemaji. (al. 16)

Majibu ya Dondoo 22

Muktadha uk 35

 1. Maneno ya Majoka akimwambia Kenga /ofisini kwa Majoka/ wanapanga namna ya kuwakabili wapinzani wao – akina Tunu 4 x 1 =4
 2. Dawa inayorejelewa
  1. Mauaji – akina jabali
  2. Kupigwa – akina Tunu
  3. Kufunga soko ili wateseke
  4. Kuongeza bei ya vyakula
  5. Kuongeza kodi
  6. Kuwafumanisha kama vile Ashua na Husda
  7. Kuwatia kizuizini
  8. Kuwahinga – mabaki ya keki/vipande vya ardhi
  9. Kuwatisha – vijikaratasi
  10. Kuwatenganisha ili kuwatawala – akina Ngurumo ni wafuasi wake
  11. Kufunga vituo vya habari – runinga ya mzalendo
  12. Kuwapa likizo ya mwezi mzima kuadhimisha miaka sitini ya uhuru
  13. Kusambaratisha mikutano yao ya kisiasa
  14. Kuvunja maandamano yao
  15. Kutumia propaganda kama mtangazaji wa redio anavyofanya
  16. Kurithisha hatamu za uongozi – Ngao Juniour
  17. Kupujua thamani ya elimu – kuwadhalilisha waliosoma
  18. Kutoa vibali maalum kwa shughuli ambazo ni kinyume cha sheria – Asiya
  19. Kutotaka wafadhili kuendelea kutoa misaada
  20. Udanganyifu katika upigaji wa kura
  21. Kutumia asasi kama vile askari visivyo zozote 16 x 1 =16

Swali la Dondoo 23

‘‘Dalili ya mvua ni mawingu, lazima tuwe macho’’

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
 2. Bainisha vipengele vitatu vya kimtindo. (alama 3)
 3. Fafanua umuhimu wa mzungumzaji katika kuvijenga vipengele vifuatayo vya tamthilia hii.
  1. Ploti (alama 5)
  2. Maudhui (alama 5)
  3. Wahusika wengine (alama 3)

Majibu ya Dondoo 23

 1.    
  1. Ni maneno ya Tunu.
  2. Anamwambia Majoka.
  3. Ofisini mwa Majoka.
  4. Hashima/ mamake Tunu kupigania haki za mumewe wakapata fidia baada ya kifo cha mumewe aliyefanya kazi katika Majoka and Majoka Company. (4×1=4)
 2. Sifa za Tunu
  1. Mwenye utu, anamwambia Siti awachukue watoto wa Sudi awapeleke kwa mamake.
  2. Ni kiongozi mwema- Akiwa na Sudi alionyesha uongozi mwema katika chuo kikuu.
  3. Ni mtetezi wa haki- anamwambia Majoka yeye na watu wake watalipa kil atone la damu.
  4. Ni jasiri- anakabiliana na Mjoka kuhusu kifo cha Jabali.
  5. Ni mwenye shukrani- Anamshukuru Siti kwa kuja kumtembelea.
  6. Ni mtambuzi.
  7. Ni mwenye msimamo dhabiti.
  8. Ni mwenye matumaini. (za kwanza 4×1=4)
 3. Dhuluma ni kitendo cha kumnyima mtu haki au stahiki yake; ni uonevu, ni tendo lisilo na haki. Majoka alidhihirisha dhuluma maishani mwake binafsi na katika uongozi mwake.
  1. Serikali yake hutoza wanabiashara kodi lakini wanafanyia kazi katika mazingira machafu. Uvundo umekithiri. Sudi anasema. “ni jukumu lao kuhakikisha soko ni safi si kukusanya kodi pekee...(uk3.)
  2. Bali na kulipa kodi isiyowaletea huduma yoyote wafanyakazi wa soko wanalalamika kuwa wanadaiwa pesa zaidi . kombe asema kuwa ni lazima wapate chakula na pia wawape wenye nchi kitu kidogo.
  3. Ashua asema mahali wanapofanya kazi wanadaiwa kitu kikubwa au kitu chote.
  4. Utawala wake unawahangaisha wafanyakazi. hawafanyi kazi kwa amani Ashua asema “. . . na kuhangaishwa na wenye nguvu ndiyo hewa tunayopumua...” (uk2) sudi anadhibitisha hilo anapolalamika kwamba, “si haki kuchukua kilicho chetu na kututishatisha’ (uk 3).
  5. Anadhulumu raia kwa kutumia rasilimali za Sagamoyo kujinufaisha pamoja na wachache, wanaomuunga mkono. Wao ndio hula ile keki kubwa, huku raia wakitaabika. Sudi anamwambia Boza, “hapo basi-kijikeki. Kwa nini wewe upate kidogo? Sagamoyo ni kwenu,• sherehe ni zenu... na keki kubwa ni ya kina nani” (Uk 4)
  6. Ni dhuluma pia kwa serikali ya majoka kufunga soko Ia Chapakazi mahali ambapo watu wengi hufanya biashara ili kupata chakula chao cha kila siku.
   vii. Katika kiwanda chake wafanyakazi wanapujwa. Soko la chapakazi lilipofungwa bei ya chakula kwenye kioski cha kampuni ya Majoka and Majoka ikapanda maradufu. Wafanyakazi hawawezi kugharamia chakula. Hili ni dhuluma dhidi ya wafanyakazi. Majoka kuendelea kujitayarisha huh wafanyakazi wake wakiumia(uk 17)
  7. Maandamano yanayokumba jimbo la Sagamoyo , si walimu, si wauguzi, si wafanyakazi wa soko ni ithibati tosha kuwa watu wanadhulumiwa.
  8. Ni dhuluma pia kuwaua watu. k.m alimuua jabali aliyekuwa mshindani wake katika siasa.
  9. Wale vijana watano wa Majoka and Majoka waliuawa wakidai haki yao kwenye maandamano.
  10. Tunu alikuwa auwawe kwa kukashifu vitendo vyak’e vya kidhalimu.
  11. Kingi alionywa kuwa angevunjavunjwa na chatu kwa kukaidi amri ya Majoka ya kuwapiga watu risasi.
  12. Majoka anawaua hata washirika wake wa karibu akihofia kuwa wangetoa siri zake. Kwa mfano Ngurumo aliuawa ilhali alikuwa mfuasi wake sugu. Chopi alipangiwa kuuawa pia kwa kujua ‘mengi’. Hii ni dhuluma iliyozidi. Majoka anasema anaona ziwa kubwa ajabu lililofurika damu... kuna kilio cha ndani kwa ndani na machozi mengi humo yasiyoonekana... (Uk 73) na kwamba mikono yake ilikuwa imefungwa nanga humo damuni.(uk 73).
  13. Serikali yake imewahini wananchi raha, wanaishi kwa hofu. Hashima anakiri kwamba yeye na Tunu wake wanaishi kwa hofu nyingi. Wanaogopa kwamba wanaweza kuvamiwa wakati wowote hasa akitilia maanani kuwa mwanawe nusura auawe. Tunu anapopiga nduru kwa kuota mamake anafikiri wameshambuliwa.
  14. Isitoshe serikali ya majoka inawahangaisha watu kuwatupia vijikaratasi vya kuwashurutisha wahame sagamoyo si kwao. Siti anasema,”jana walitutupia vijikaratasi . . .tuhame Sagamoyo si kwet” (uk 52-53).
   Anaamuru polisi kusambaratisha kikatili maandamano ya raia ambao hawakuwa na hatia. Walikuwa wakidai haki yao tu.

Swali la Dondoo 24

‘‘Dunia ni mwendo wa ngisi… ilikuwa haki yangu unilipie karo…

 1. Fafanua muktadha wa maneno haya. (alama 4)
 2. Eleza sifa nne za mzungumzaji. (alama 4)
 3. Thibitisha kwa kutoa mifano kumi na miwili kuwa maisha ya anayezungumziwa yametawaliwa na dhuluma. (alama 12)

Majibu ya Dondoo 24

 1.  
  1. Msemaji ni Mbura
  2. Alikuwa anazungumza na Sasa.
  3. Walikuwa kwenye sherehe iliyoandaliwa kwa mzee Mambo. (uk44)
  4. Walikuwa wanazungumza kuhusu ‘kula kwao’ Zozote4×l
 2. msemaji ni Mbura
  1. Ni mzalendo- anafanya kazi kwa bidii katika wizara yake kama njia ya kuonyesha uzalendo. ii. Mwenye tamaa- anajaza sahani kwa chakula na kukila chote.
  2. Mwenye utu- anataka wananchi wale kwa niaba ya viongozi kama vile wao wamekuwa wakila kwa niaba yao.
  3. Ni fisadi- amepokea kazi kwa afisi ya serikali kwa njia isiyo halali.
  4. Mzembe- baada ya kula sahani tatu za vyakula kwenye sherehe analala usingizi mzito badala ya kwenda kazini.
  5. Mtetezi wa haki
  6. Mvumilivu
  7. Mpyaro
  8. Msema kweli. Za kwanza 6×1
 3. Tathmini vile viongozi wanavyokuwa wabadhirifu.
  1. Hulipwa mishahara mikubwa sana na serikali jambo linalochangia ubadhirifu wa mali ya üuma.
  2. Sherehe kubwa za viongozi wa kiserikali huchangia pakubwa ubadhirifu.
  3. Viongozi hutumia raslimali za nchi kwa manufaa yao ya kibinafsi- magari ya serikali.
  4. Raslimali zilizotumiwa katika kuvinunua vyakula na vinywaji vingetumika katika kuendeleza asasi tofauti za kijamii.
  5. Dj na wenzake wanapata mabilioni ya fedha kutokana na kuwatumbuiza wageni katika sherehe kama hizi.
  6. Dj kupata huduma za maji, stima, matibabu bure.
  7. Dj kuuza dawa ambazo zilipaswa kutumika na wananchi katika hospitali
  8. Viongozi wanawachukua baadhi ya watu wao wa karibu na kufanya juu chini kuona kwamba wanajifaidi na mali na raslimali za wananchi pasipo kujitolea jasho kamwe.
  9. Upeperushaji wa matangazo katika vyombo vya habari ya sherehe za kiongozi binafsi ni njia ya kuendeleza ubadhirifu.
  10. Sasa na Mbura wanapoamua kuchukua vyakula kupita kiasi katika sherehe za mzee mambo.
  11. Kuwaajiri viongozi wawili wenye nyadhifa sawa katika sekta moja ya umma.
  12. Vibaraka na vikaragosi kupewa mali ambayo ingewafaidi wananchi.

Swali la Dondoo 25

“Ama kweli dunia gunia. Ilikumeza hindi bichi ikakuguguna, sasa inakutema guguta.”

 1. Fafanua muktadha wa dondoo hili. (al 4)
 2. Tambua tamathali mbili za usemi katika dondoo hili. (al 2)
 3. Eleza umuhimu wa mazingira waliyomo wahusika katika dondoo hili. (al 4)
 4. Wananchi katika tamthilia hii wamegugunwa na madhila kadhaa ya kisiasa. Dhibitisha. (al 10)

Majibu ya Dondoo 25

 1. muktadha wa dondoo.
  • Msemaji- Majoka
  • Msemewa- Ashua
  • mahali- wakiwa ofisini.
  • Wakati- majoka anamsimanga Ashua kwa kukamtaa kumpenda na kujihusisha naye kimapenzi. Anasema sasa Ashua amezeeza ka kuparara kwa kuolewa na maskini.
   4x1=4
 2. Tamathali za usemi
  • Nahau-dunia gunia
  • Jazanda- hindi bichi…. Guguta.
   2x1=2
 3. Umuhimu wa mazingira( ofisi ya Majoka)
  • Mazingira haya yanaonyesha tofauti za kitabaka kiuongozi pale ambapo viongozi kama Majoka wanaishi maisha ya kifahari huku wanachi kama Ashua akikosa hata pesa za kuwalisha wanawe.
  • Mazingari haya yanadhihirisha uozo ulioko katika jamii kwani Majoka anataka kusinzi lakini Ashua anakataa.
  • Pia mazingira haya yanatuonyesha jinsi ambavyo viongozi wengine ni wabinafsi. Shule ya Majoka imejaa makabeji kutoka na wanafunzi kutumia dawa za kulevya.
  • Kupitia mazingira haya pia tunakuja kujua kuwa Ashua ni mzalendo kwani anakataa kazi katika shule ya Majoka na kuiita ya kihuni.
  • Pia mazingira haya yanaweka wazi shida wanazozipitia wanachi. Watoto wa Ashua walilala njaa.
  • Ulafi na tamaa ya viongozi pia umewekwa wazi katika haya mazingira. Majoka alifunga soko lililokuwa tegemeo la pekee la wananchi kwa madai ati ni chafu.
  • Ufisadi pia na matumizi mabaya ya vyombo vya dola umedhihirika katika mazingira haya. Ashua anasema kuwa kuku hawezi pata haki kama kipanga ndiye hakimu.
   4x1=4
 4. wananchi wamegugunwa na madhila ya kisiasa.
  • Jabali mpinzani wa Majoka anauliwa kwa kuupinga uongozi wake kwa kupangiwa ajali.
  • Ashua anatiwa gerezani ili kumshinikiza Sudi mpinzani wake Majoka kumchongea kinyago.
  • Tuna anapangiwa njama ya kuuliwa na kuumizwa vibaya karibu afe.
  • Wanasagamoyo wanafungiwa soko ambalo wanalitegemea.
  • Kandarasi zinapeanwa kwa mapendeleo. Asiya anapewa kandarasi ya uokaji keki kwa kujua na Husda mkewe Majoka.
  • Vijana wengi wanaaga dunia kwa kubugia pombe haramu iliyo hararishwa na uongozi wa Majoka.
  • Ukataji wa miti unaohararishwa na Majoka unasababisha ukame.
  • Watu wanaishi kwa hofu kwa kutishiwa kuhama na uongozi wa majoka.
  • Vijana watano wanauliwa wanapoandama kutokana na kupandishwa kwa bei ya chakula kiwandani.
  • Vyombo vya habari vinafungwa kiholela kwa kupeperusha habari zinazompinga Majoka. Yeye hataki upinzani.
  • Kiwanja cha soko la Chapakazi kimenyakuliwa na Majoka ili ajenge hoteli ya kibinafsi.
  • Sagamoyo hamna ajira kwa vijana waliohitimu. Kina Sudi wanasalia kuchonga vinyago kutokana na uhaba wa kazi.
  • Majoka ako na kikosi sugu cha kuwaadhibu wapinzani wake kikiongozwa na mshauri wake Kenga. Tunu anavamiwa.
  • Chopi anapangiwa njama ya kuuliwa kwa kujua siri nyingi za Majoka. Alikuwa askari mtiifu sana.
  • Kingi anafutwa kazi kwa kukataa kupiga risasi waandamanaji kinyume cha sheria.
  • Kadiria hoja zingine.

Swali la Dondoo 26

“Ulitaka wahamie wapi siku kama hizi? Wamekuja kuuguza majeraha yao ya kufungiwa soko.”

 1. Weka maneno haya katika muktadha wake. (alama 4)
 2. Tambua mbinu mbili za lugha katika dondoo hili (alama 2)
 3. Kando na kufungiwa soko, Wanasagamoyo wanauguza majeraha yepi mengine yanayosababishwa na utawala wa Majoka. (alama 14)

Majibu ya Dondoo 26

 1.                                      
  1. Mnenaji ni Ngurumo
  2. Mnenewa ni Sudi
  3. Mahali ni Mangweni kwa Mamapima.
  4. Sudi alikuwa amemwuliza swali kuhusu watu waliokuwa sokoni iwapo wamehamia kwa Mamapima. (al 4 x 1 = al 4)
 2. Kinaya- Watu wamekuja kuuguza majeraha ilhali wengine wanakufa na kupofuka kwa pombe.
  Swala balagha- Ulitaka wahamie wapi siku kama hizi?
  Kutaja: - 1
  Mfano: - 1 (1 x 2 = al 2)
 3.                
  1. Majoka anawaua wapinzani wake kisiasa ili kuzuia upinzani: Jabali.
  2. Majoka analifunga soko la Chapakazi na kuwafanya watu wateseke: Ashua, Sudi
  3. Sumu ya nyoka inayotengenezwa na kampuni ya Majoka inapenya shuleni, wanafunzi wanaitumia na hivyo kuwafanya makabeji.
  4. Majoka anamfungia Ashua gerezani ili kumlazimisha Sudi kumchongea kinyago cha Ngao.
  5. Majoka anaagiza Ngurumo kuuliwa ili asitoboe siri ya njama yake ya kutaka kumwangamiza Tunu.
  6. Majoka anawapa watu kibali kukata miti, jambo linaloacha ardhi kuwa jangwa hivyo mazao kupungua: Hashima anasema alivuna kichele tu.
  7. Majoka analifunga soko la Chapakazi kama njama ya kumnasa Ashua ili kutimiza ashiki zake za kimapenzi.
  8. Uongozi wa Majoka unasambaza vijikaratasi kuwachochea watu kuhama Sagamoyo. Jambo ambalo linawatia watu hofu: Siti
  9. Majoka anawapa polisi kibali cha kuwashambulia waandamanaji, jambo linalopelekea vijana tano kuuliwa.
  10. Majoka anampa kibali Asiya kutengeneza pombe haramu, watu wengi wanaaga na wengine kuwa vipofu.
  11. Majoka anamfuta Kingi kazi baada ya kukaidi amri yake ya kuwafyatulia watu risasi.
  12. Majoka, Chopi na Ngurumo wanapanga njama ya kumwangamiza Tunu. Tunu anavunjwa mundu wa mguu.
  13. Majoka anaamrisha vituo vya kutangaza habari kufungwa ili kubakie tu na kimoja.
  14. Majoka anamtumia Husda ujumbe mfupi afike ofisini mwake ili kuchongea ugomvi kati ya Husda na Ashua. Jambo linalopelekea Ashua kupigwa na kupata majeraha.
  15. Majoka anaamrisha wafadhili wa upinzani kuhama kutoka jimbo la Sagamoyo.
  16. Majoka anawaongezea mishahara walimu na madaktari na pia kuongeza kodi maradufu. Jambo linalofanya bei ya vyakula kupanda.
  17. Majoka anakopa pesa kutoka mataifa ya Magharibi kufadhili miradi duni ya kuchonga vinyago. Mikopo hii ingelipwa na vizazi kwa miaka mia moja.
  18. Majoka anaagiza watu kusherehekea uhuru wa jimbo la Sagamoyo kwa mwezi mmoja. Jambo hili lingeathiri uchumi wa Sagamoyo.
  19. Kandarasi zinapeanwa kwa njia ya ufisadi. Asiya licha ya kuoleka na Boza anashiriki mapenzi na Ngurumo ili apewe kandarasi ya kuoka keki.
  20. Majoka anamlazimisha Tunu kuoleka na Ngao Junior ili kudhoofisha upinzani.
  21. Ardhi ya soko la Chapakazi inagawa na Majoka pamoja na washiriki wake wa karibu kama vile Kenga, jambo ambalo linawaathiri wachuuzi kiuchumi.
  22. Uongozi umesalia katika familia moja ya Majoka tangu uhuru ulipopatikana, jambo ambalo linaathiri upinzani: Jabali anauliwa; Tunu anaumizwa mguu.

Swali la Dondoo 27

“Dudu liuuu...ma...malo halipewi chanda, Tunu si wa hulka yako. Wachezea moto, ukiungua lilia mvunguni usichekwe.”

 1. Tambua toni inayojitokeza katika dondoo hili. (alama 2)
 2. Kwa kutolea mifano, onyesha aina nne za taswira zinazojitokeza katika dondoo. (alama 4)
 3. Jadili mbinu-ishi zinazoibuliwa na msemewa katika tamthilia Kigogo. (alama 7)
 4. Jadili umuhimu wa mazungumzo kati ya Ashua na Majoka katika kujenga tamthilia Kigogo. (alama 7)

Majibu ya Dondoo 27

“Dudu liuuu...ma...malo halipewi chanda, Tunu si wa hulka yako. Wachezea moto, ukiungua lilia mvunguni usichekwe.”

 1. Tambua toni inayojitokeza katika dondoo hili.  (alama 2)
  • Kukejeli/kudhihaki/kutania - Dudu liuuu...ma...malo halipewi chanda, Tunu si wa hulka yako
  • Kuonya/kunasihi/kukanya - Wachezea moto, ukiungua lilia mvunguni usichekwe
 2. Kwa kutolea mifano, onyesha aina nne za taswira zinazojitokeza katika dondoo.   (alama 4)
  • Taswira oni – Dudu liuuu...ma...malo, lilia mvunguni usichekwe.
  • Taswira hisi- Dudu liuuu...ma...malo
  • Taswira muonjo - Dudu liuuu...ma...malo
  • Taswira mguso - Dudu liuuu...ma...malo
 3. Jadili mbinu-ishi zinazoibuliwa na msemewa katika tamthilia Kigogo. (alama 7)
 4. Jadili umuhimu wa mazungumzo kati ya Ashua na Majoka katika kujenga tamthilia Kigogo.
  • Kufufua matukio ya awali;Majoka aliwahi kumchumbia Ashua akakataa.
  • Kusisitiza umuhimu wa kuaminiana na kujiheshimu katika ndoa;Ashua anasisitiza kuwa ameolewa.
  • Kuonyesha jinsi viongozi wanavyotumia vibaya ofisi zao
  • Kuonyesha jinsinbaadhi ya viongozi hawajathamini ndoa za wananchi;Majoka hajali kuvunjika kwa ndoa ya Ashua.
  • Kuonyesha athari za ukosefu wa chakula kwa watoto
  • Kuonyesha kuzinduka kwa wanawake katika kutetea haki zao
  • Kuonyesha ubinafsi wa viongozi.
  • Kuonyeha baadhi ya miradi duni ambazo viongozi wanashughulikia.
  • kujenga sifa za wahusika;mfano kupitia mazungumzo haya tunatambua ufuska wa Majoka kuonyesha usaliti wa viongozi
  • kuonyesha ukatili wa viongozi;ashua anakamatwa ilhali ananyonyesha
  • kuonyesha unafiki;majoka anamwambia Ashua kuwa haja zangu ni haja zako
  • kuonyesha umaskini;Ashua kugeuka omba omba kwa kukosa chakula
  • Kuonyesha maudhui ya ajira; Ashua ana shahada ya ualimu ila hana kazi.
  • kuonyesha maudhui ya elimu;Ashua amehitimu
  • Kuonyesha jinsi wanawake wanavyonyanyaswa.

Swali la Dondoo 28

“…mbio za sakafuni zimefika ukingoni. Ikiwa umekataa kushindwa, mimi nimekubali.”

 1. Kwa kurejelea hoja kumi na mbili, thibitisha namna kauli iliyopigwa mstari inavyotimia ukirejelea wahusika mbalimbali kwenye tamthilia Kigogo. (alama 12)
 2. Fafanua mchango wa msemaji wa maneno haya katika kufanikisha ploti kwenye tamthilia Kigogo. (alama 8)

Majibu ya Dondoo 28

“…mbio za sakafuni zimefika ukingoni. Ikiwa umekataa kushindwa, mimi nimekubali.”

 1. Kwa kurejelea hoja kumi na mbili, thibitisha namna kauli iliyopigwa mstari inavyotimia ukirejelea wahusika mbalimbali kwenye tamthilia Kigogo.  (alama 12)
  • Kenga anakubali kushindwa na kuungana na Wanasagamoyo dhidi ya Majoka.
  • Asiya, baada ya kugeukwa na walevi, anamwomba Tunu msamaha na kuungana na Wanasagamoyo.
  • Walevi wanachoshwa na Asiya, wanamgeukia na kumwaga pombe yake.
  • Ashua anakubali kuungana na Tunu na Sudi kupigania ukombozi wa Sagamoyo.
  • Ngurumo ananyongwa na chatu na hatimaye kuuawa anapotoka Mangweni.
  • Ngao Junior anakufa kutokana na athari ya sumu ya nyoka.
  • Babake Tunu anakufa kwa njia ya kutatanisha katika kampuni ya Majoka and Majoka.
  • Kingi anamgeuka Majoka na kuwaunga mkono Wanasagamoyo kwa kukaidi amri yake ya kuwapiga Wanasagamoyo risasi.
  • Majoka anageukwa na Wanasagamoyo na kubaki peke yake/Babu anamsuta mpaka anaingiwa na majuto.
  • Jabali anauawa na chama chake cha Mwenge kupotelea mbali.
  • Kombe na Boza wanatupiwa vijikaratasi wahame Sagamoyo si kwao licha ya kumwuunga mkono Majoka.
  • Inabainika hatimaye kuwa Ngurumo alishiriki uroda na Asiya ili kupewa kandarasi ya kuoka keki.
  • Vijana watano wanauawa atika Majoka and Majoka Company.
  • Chopi anapangiwa safari baada ya kumsaidia Majoka kuwakandamiza Wanasagamoyo.
  • Wafadhili wanapanga kufurushwa ili wasifadhili juhudi za kina Tunu za kuwapigania haki.
  • Wanafunzi wa Majoka and Majoka Academy wanadungana sumu ya nyoka na kuwa makabeji, hawafuzu hatimaye.
  • Wanasagamoyo wanachoshwa na Majoka, wanasusia mkutano wake na hatimaye kumfurusha.
 2. Fafanua mchango wa msemaji wa maneno haya katika kufanikisha ploti kwenye tamthilia (alama 8)
  • Kupitia kwake tunaelezwa kuhusu usuli wa Ngurumo kumvunja Tunu mguu.
  • Anajenga mgogoro kati ya wanamabadiliko n wanaotaka hali ibakie hivyo.Kenga anasemakuwa amekubali kushindwa.
  • Anatumiwa kujenga mgogoro wa kijinsia unaotumiwa kufanya kampeni dhidi ya utawala wa tunu.
  • Kupitia kwake, nafahamu chanzo cha kifo cha jabali.
  • Ushari wake mbaya unamfanya Majoka kufanya maamuzi mabaya kwa mambo mengi hivyo kupelekea kung’olewa kwake madarakani.
  • Kuonyesha mustakabali wa sagamoyo.Anaomba msamaha.
  • Baadhi ya matukio katika maisha ya wahusika yanaangaziwanaye moja kwa moja.Anaenda katika karakana ya Sudi.
  • Matendo yake yanampa msomaji mwao kuhusu aliyepanga na kumwuua Ngao Junior hasa baada ya kutatizika Majoka anapomtangaza Ngao Junior kama mrithi wake.
  • Kupitia kwake tunafafanuliwa kuhusu ila na hila za majoka.
  • Matukio katika ofisi ya Majoka yanatusaidia kujua kuwa ndiye aliyepanga njama ya kumfunga Ashua Jela.
  • Kuonyesha hatima ya mgogoro kati ya viongozi na wanyonge.Kuwa amekubali kushindwa.

Swali la Dondoo 29

'Wewe ni popo: Kwa ndege hupo na kwa wanyama hupo.'

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili.
 2. Taja na ueleze tamathali za usemi katika dondoo hili.
 3. Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya.
 4. Huku ukitoa mifano sita mwafaka, fafanua maudhui ya usaliti kama yalivyojitokeza katika tamthilia hii.

Majibu ya Dondoo 29

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (al 4)
  Maneno ya Boza
  Anamwambia Kombe
  Wako katika karakana yao katika soko la chapa kazi.
  Wanazungumza kuhusu Hali ilivyobadilika Sagamoyo.
 2. Taja na ueleze tamathali za usemi katika dondoo hili. (al 4)
  1. sitiari - wewe ni popo.
   Boza anamrejelea Kombe kama popo kwa kuonekana kutokuwa na msimamo wa ni nani anayemuunga
   mkono.
  2. Kejeli-Boza anamrejelea Kombe kama popo. Huku ni kumdunisha kwa kukosa msimamo.
   Kutambua tamathali al.1
   Kueleza al.1
 3. Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya. (al 6)
  1. Mbinafsi
   Anapopewa keki na Kenga, anasema kuwa ni ndogo sana hivi kwamba hangeweza kuwapelekea jamaa zake.
  2. Mjinga
   Habaini maovu yoyote ya uongozi wa Majoka. Anautetea na kmuunga mkono licha ya hali Sagamoyo kuendelea kuwa mbaya.
  3. Mwenye kiburi
   Sudi anapoizima redio ya rununu yake anaikejeli kwa kuirejelea kama kijiredio cha pesa nane.
  4. Mlevi
   Anashiriki ulevi na walevi wengine kule Mangweni.
  5. Mwenye tamaa
   Hawaelezi Sudi na Kombe kuhusu mradi wa kuchonga kinyago akitarajia kuchonga yeye ili ajifaidi.
  6. Mwenye mapuuza.
   Hakung'amua uhusiano wa kimapenzi ulioendelzwa baina ya Ngurumo na mkewe.
 4. Huku ukitoa mifano sita mwafaka, fafanua maudhui ya usaliti kama yalivyojitokeza katika tamthilia hii. (al 6)
  1. Kupigwa na kuumizwa
   Ngurumo aliyesoma na Tunu darasa moja anakubali kutumiwa na Majoka kumpiga na kumvunja muundi wa mguu.
  2. Kufungulia biashara ya ukataji miti.
   Majoka anasaliti wajibu wake wa kulinda rasilmali za nchi kwa kufungulia biashara ya ukataji miti.
  3. Kufunga soko la Chapa kazi.
   Majoka anasaliti raia anaowaongoza kwa kufunga soko hivyo kuwahini kipato chao cha kila siku.
  4. Kutosafisha soko.
   Majoka anasaliti raia wanaolipa kodi sokoni kwa kutosafisha soko. Wanafanyia biashara katika mazingira machafu yanayowasababishia ndwele zisizo majina.
  5. Kutawanya raia kwa fujo.
   Polisi wanasaliti wajibu wao wa kuhakikishia raia usalama wao kwa kutawanya kwa risasi na vitoza machozi kila wanapoandamana kutetea haki
  6. Kumwaga taka sokoni.
   Serikali ya Majoka inasaliti raia kwa kumwaga kemikali na majitaka sokoni na kuwasababishia uvundo na
   ndwele.

Swali la Dondoo 30

“Jina lako litashamiri. Utapata tuzo nyingi pia”

 1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
 2. Fafanua umuhimu wa msemaji wa kauli hii katika tamthilia. (alama 8)
 3. Eleza mbinu zingine anazotumia Majoka kuongoza Sagamoyo. (alama 8)

Majibu ya Dondoo 30

 1. MUKTADHA
  Msemaji ni Kenga
  anamwambia Sudi
  wako katika karakana sokoni Chapakazi
  Sudi amekataa mradi wa kuchonga Kinyago cha Ngao,Kenga anamweza kuwa akikubali mradi huo maisha yake yatabadilika kwani atapata tuzo nyingi pamoja na likizo ya mwezi mmoja lakini anakataa,
 2. UMUHIMU WA KENGA
  Tazama: namna ya kueleza umuhimu wa mhusika
  • Kuendeleza maudhui ya ufisadi - Baada ya Kenga kumsaidia Majoka kufunga soko na kungoa vibanda Majoka anamhadi Kenga kipanda cha ardhi sokoni
  • kuendeleza maudhui ya usaliti - Anamwambia Majoka kuwa ikiwa amekataa kushindwa yeye amekubali na anajiunga na umati na kupokelewa.
  • Kuendeleza ploti - Hatua ya Ashua kwenda Ofisini na mwa Majoka na kutiwa nguvuni ilikuwa imepangwa na Kenga.
  • Kuendeleza maudhui ya mauaji - Kenga anatoa pendekezo la Chopi kuenda safari (kuuawa) kwani anajua mambo mengi na huenda akatoboa mipangao ya kumwangamiza Tunu.
  • Ni mfano wa washauri wanaounga mkono uongozi dhalimu - Kenga anamfahamisha Majoka kuwa watawawekea kina Tunu vidhibitimwendo na hatimaye kuwakomesha.
  • Kenga ametumiwa kuonyesha mbinu anazotumia Majoka kuongoza - Anamwambia Sudi kuwa atapata zawadi nyingi iwapo atakubali mradi wa kuchonga kinyago cha Ngao.
  • Kenga ni kielelezo cha washauri wachochezi - Majoka anapomwambia kuwa wataongeza mishahara kisha wapandishe kodi Kenga anamwambia kuwa mtu hawi mwana wa shujaa bila sababu. Pia, anamwambia Majoka aache kuwa na moyo wa huruma.
  • Kenga anaendeleza maudhui ya taasubi ya kiume - Baada ya kukitazama kinyago anachochonga Sudi anasema Sagamayo haijawai kuwa na shujaa wa kike
  • Ametumiwa kukuza maudhui ya mapuuza - Anamwambia Majoka asiyapuuze maandamano yanayoendelea. Majoka anasema kuwa waandamanaji watachoka hatimaye anaondolewa uongozini.
  • Mwandishi amemtumia kuonyesha namna viongozi wananyanyasa watawaliwa - Kenga anamwambia Majoka atangaze kuwa maandamano ni haramu na awaamuru maafisa wa polisi kutumia nguvu zaidi.
 3. MBINU ANAZOTUMIA MAJOKA KUONGOZA
  • Vitisho – Siti anasema kuwa wametumiwa vijikaratasi vinavyosema wahame Sagamoyo.Hii ni baada ya jirani yao Sudi kuingilia siasa za kumpinga Majoka.
  • Mauaji– Jabali aliwauawa kwa sababu alikuwa mpinzani wa Majoka.
  • Vyombo vya dola– Polisi waliwaua vijana waliokuwa wakiandamana.Pia, wanatumia vitoza machozi kuwatawanya waandamanaji.
  • Propaganda – Kupitia redio, Majoka anawaambia Wanasagamoyo wasiwaruhusu watu wachache waliojazwa kasumba za kikoloni kuwarejesha kwenye utumwa wa kimawazo.
  • Tenga tawala– hataki kuzungumza na Tunu na Sudi wote wakiwa pamoja.Tunu anamwambia aseme nao wote anapotambua kuwa anataka kuwagawa.
  • Kukiuka sheria– Anampa mama pima kibali cha kuuza pombe haramu kwa Ngurumo na asiya wanamuunga Majoka mkono.
  • Kufuta kazi wasiomuunga mkono – Majoka anamfuta kazi kingi kwa anapokataa kuwapiga watu risasi sokoni Chapakazi.
  • Ulaghai-Majoka anasema ataongeza mishahara ya waalimu na wauguzi kwa aslimia kidogo kisha apandishe kodi kwani hesabu nzuri ni kutia na kutoa.
  • Kuwafunga watu jela– Ashua anafungwa kwa madai ya kuzua vurugu katika ofisi ya serikali. Hii ilikuwa fursa ya kulipiza kisasi kwa Sudi.

Download Maswali na Majibu ya Dondoo katika Tamthilia ya Kigogo.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest