Utangulizi
- Kuna makundi mawili ya sauti za kiswahili:
- Irabu (Vokali);
- Konsonanti;
Irabu (Vokali)
a, e, i, o, u
- Sauti ambazo hutamkwa kwa ulaini bila hewa kuzuiliwa katika ala za sauti.
Matamshi/Uainishaji wa Irabu
- a ni ya katikati na chini kinywani na midomo ikiwa imeviringa.
- e ni ya mbele na kati kinywani na midomo ikiwa imetandazwa.
- i ni ya mbele na juu kinywani na midomo ikiwa imetandazwa.
- o ni ya nyuma na kati kinywani na midomo ikiwa imeviringa.
- u ni ya nyuma na juu kinywani na midomo ikiwa imeviringa.
Konsonanti
b, ch, d, f, g, h, j, k, l, m, n, p, r, s, t, v,w, y, z
- Sauti ambazo wakati wa kutamkwa hewa huzuiliwa katika ala za sauti.
- Kuna aina mbili kuu za sauti za konsonanti:
- Sauti Ghuna - konsonanti hizi zinapotamkwa, hewa hutikisa nyuzi za sauti
- Sauti Sighuna - konsonanti hizi zinapotamkwa, hewa haitikisi nyuzi za sauti
Aina za Ala za Sauti
Ala Tuli
- Ambazo hazisogei mtu akitamka k.m. meno, ufizi, kaa kaa gumu, kaa kaa laini na koo/koromeo.
Ala sogezi
- Ambazo husogea mtu akitamka k.m. midomo na ulimi.
Matamshi/Uainishaji wa Konsonanti
- Huainishwa kulingana na inapotamkiwa, kuwepo au kutokuwepo kwa mtetemeko katika nyuzi za sauti na jinsi hewa inavyozuiliwa katika ala k.m. /p/ ni ya midomo, kipasuo na sighuna
Midomo | Midomo+ Meno | Meno+Ulimi | Ufizi | Kaakaa+ufizi | Kaakaa gumu | Kaakaa laini | Koo | Aina ya sauti | |
Vipasuo | p | t | j | k | sighuna | ||||
d | d | g | ghuna | ||||||
Vikwamizo/Vikwaruzo | f | th | s | sh | gh | h | Sighuna | ||
v | dh | z | ghuna | ||||||
Kipasuo - Kwamizo | ch | sighuna | |||||||
Nazali/Ving'ong'o | m | n | ny | ng' | ghuna | ||||
Kitambaza | l | ghuna | |||||||
Kimadende | r | ghuna | |||||||
Viyeyusho/Nusu Irabu | y | w | ghuna |
Vipasuo
- Konsonanti ambazo wakati wa kutamkwa hewa husukumwa, huzuiliwa kabisa na kuachiliwa kwa ghafla na mpasuko mdogo kutokea.
Vikwamizo/Vikwaruzo
- Konsonanti ambazo wakati wa kutamkwa hewa hupitishwa katikati ya ala kwa kukwamizwa.
Kipasuo kwamizo/kwaruzo
- Konsonanti ambayo wakati wa kutamkwa hewa husukumwa nje kwa nguvu, huzuiliwa kabisa halafu mwanya mdogo huachwa hewa ipite kwa kukwamizwa.
Nazali/Ving’ong’o
- Konsonanti ambazo wakati wa kutamkwa kuna kiasi cha hewa huachiliwa na kupitia puani
Kitambaza
- Konsonanti ambayo wakati wa kutamkwa hewa husukumwa kwa nguvu, kuzuiliwa na kuachiliwa ipite kando ya ulimi
Kimadende
- Konsonanti ambayo wakati wa kutamkwa hewa husukumwa, kuzuiliwa na kuachiliwa na kusababisha ncha ya ulimi kupigapiga ufizi mfululizo.
Nusu irabu/Viyeyusho
- Konsonanti ambazo wakati wa kutamkwa hewa hupitishwa katikati ya ala kwa ulaini kama katika utamkaji wa irabu
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download Sauti za Kiswahili - Sarufi na Matumizi ya Lugha Kiswahili Notes.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students