Utangulizi
- Kiambishi ni silabi inayofungamanishwa na mzizi wa neno ili kuleta maana iliyokusudiwa. Viambishi havina maana kamilifu peke yake: huhitaji kufungamanishwa na mzizi wa neno. Kwa hivyo, kiambishi ni mofimu tegemezi inayoongeza maana fulani katika neno kama vile ngeli, wakati, hali, mnyambuliko wa kitendo n.k
Aina za Viambishi
- Kuna aina mbili kuu za viambishi:
- Viambishi Awali
- Viambishi Tamati
Viambishi Awali
- Viambishi hivi hutokea kabla ya mzizi ya neno/shina la kitenzi. Kuna aina kadhaa za viambishi hivi kama vile viambishi viwakilishi vya nafsi, ngeli, mahali, wakati, hali n.k
Viambishi Viwakilishi vya Ngeli
- Hizi ni silabi zinazowakilisha ngeli katika neno. Mfumo wa ngeli unaokubalika hutumia viambishi hivi kubainisha ngeli mbali mbali.
k.m:
a-me-avy-a => kiambishi kiwakilishi cha ngeli ya A-WA(umoja)
zi-ta-pasuk-a => kiambishi kiwakilishi cha ngeli I-ZI wingi
ki-li-pote-a => kiambishi kiwakilishi cha ngeli ya KI-VI(umoja)
ya-na-angaz-iw-a => kiambishi kiwakilishi cha ngeli ya LI-YA(wingi)
Viambishi Viwakilishi vya Nafsi
- Hivi ni viambishi ambavyo huonyesha nafsi katika neno. Kuna aina mbili za viambishi viwakilishi vya nafsi:
- Viambishi Viwakilishi vya Nafsi ya Mtendaji/Mtenda
- Hutumika kuonyesha aliyefanya kitendo katika neno.
- Kama viambishi vya Ngeli ya Mtendaji, viambishi hivi ndivyo vinavyotangulia viambishi vingine katika kitenzi.
NAFSI UMOJA WINGI MFANO YA KWANZA NI TU ni-na-andik-a, tu-li-shind-a YA PILI U M u-me-kasir-ik-a, m-na-pig-w-a YA TATU A WA a-li-simam-a, wa-ta-p-ew-a - Viambishi Viwakilishi vya Nafsi ya Mtendewa/Mtendwa
- Hutumika kuonyesha nafsi ya aliyeathirika na kitendo katika neno. Kama viambishi viwakilishi vya ngeli ya mtendewa, mara nyingi viambishi hivi huwekwa punde kabla ya shina la kitenzi.
- Viambishi viwakilishi vya mtendewa ni sawa na viambishi viwakilishi vya mtendaji isipokuwa:
NAFSI YA MTENDEWA KIAMBISHI MFANO YA PILI UMOJA KU zi-me-ku-fik-i-a YA PILI WINGI M, MU, WA ni-na-wa-tum-a YA TATU UMOJA M ni-ta-m-tambu-a
- Viambishi Viwakilishi vya Nafsi ya Mtendaji/Mtenda
Viambishi Viwakilishi vya Wakati/ Hali
- Hivi ni viambishi ambavyo vinapowekwa kabla ya shina la kitenzi, vinatufahamisha wakati kitendo hicho kilipofanyika.
- Viambishi hivi ni:
KIAMBISHI HUWAKILISHA: MFANO LI wakati uliopita ki-li-chom-ek-a ME wakati timilifu (uliopita muda mfupi) zi-me-anguk-a NA wakati uliopo tu-na-ku-subir-i TA wakati ujao wa-ta-ni-ju-lish-a HU wakati wa mazoea hu-som-e-a A wakati usiodhihirika a-tu-pend-a KA wakati usiodhihirika zi-ka-teket-e-a PO PO ya wakati a-li-po-wasil-i KI KI ya masharti ni-ki-zi-angali-a
Viambishi Viwakilishi vya Kukanusha Wakati
- Viambishi hivi hutumika kukanusha kitenzi katika sentensi kulingana na wakati au hali
KIAMBISHI HUKANUSHA MFANO KU wakati uliopita ha-ku-ingi-a JA wakati timilifu (uliopita muda mfupi) si-ja-ku-uliz-i-a -I* wakati uliopo na wa mazoea ha-som-i TA wakati ujao ha-ki-ta-maliz-ik-a - Tanbihi: * Tunapokanusha wakati uliopo, wakati wa mazoea na wakati usiodhihirika, tunatumia kiambishi kiishio(I) badala ya kutumia kiambishi tamati.
k.m:si-ku-ju-i, ha-pat-ik-an-i
Viambishi Viwakilishi vya Kukanusha Nafsi
- Tunapokanusha kitenzi, kiambishi cha kwanzwa hubadilika kulingana na nafsi.
KIAMBISHI MATUMIZI MFANO SI nafsi ya kwanza si-ku-wa-on-a HU nafsi ya pili hu-ni-faham-u HA nafsi ya tatu ha-ta-chuku-a
Viambishi Virejeshi vya Ngeli
- Hurejelea ngeli ya mtendewa au mtendwa na hutumika hasa katika vishazi tegemezi (vyenye o - rejeshi) k.m:
- wa-li-cho-ni-tum-i-a => kiambishi kirejeshi cha ngeli ya KI-VI
- ni-ta-ka-ye-m-salim-i-a => kiambishi kirejeshi cha ngeli ya A-WA
- u-li-ko-ji-fich-a => kiambishi kirejeshi cha ngeli ya mahali KU
- tu-li-po-pa-safish-a => kiambishi kirejeshi cha ngeli ya mahali PO
Viambishi vya ngeli
- Ni viambishi vile ambavyo husimamia ngeli katika kitenzi ili kuonyesha mtenda au mtendwa.
k.m: (vitabu) vilivyonunuliwa
(vi-li-vyo-nunul-il-w-a) => vi- na -vyo- ni viambishi vya ngeli.
Viambishi Tamati
- Viambishi tama hutokea baada ya shina la kitenzi na hutumika kutuarifu kauli au myambuliko wa kitenzi hicho.
Viishio
- Katika kauli ya kutenda, vitenzi vyenye asili ya Kibantu huishia kwa sauti "-a". Kwa mfano: a-na-omb-a, tu-li-zo-andik-a
Tanbihi: Tunapokanusha vitenzi hivi vyenye asili ya Kibantu katika wakati uliopo na wakati wa mazoea, kiishio "-a" hubadilika na kuwa "-i" Kwa mfano: Ha-pat-ik-an-i, Si-ku-ju-i - Vitenzi vyenye asili ya kigeni huchukua viishio tofauti kama vile e, i na u katika kauli ya kutenda. Kwa mfano: ha-wa-ja-tu-jib-u, a-na-tu-subir-i, ni-me-ku-sameh-e
- Hata hivyo katika kauli nyinginezo (isipokuwa kauli ya kutenda) vitenzi hivi vya kigeni huchukua kiishio "a". k.m harib-ik-a, tu-me-jib-iw-a
Viambishi Viwakilishi vya Kauli ya Kitenzi
- Hubadilika kulingana na mnyambuliko wa kitenzi.
KAULI KIAMBISHI MFANO KUTENDEA e, i omb-e-a, pig-i-a, KUTENDEANA ean, ian omb-ean-a, pig-ian-a, KUTENDWA w som-w-a KUTENDEWA ew, iw omb-ew-a, pig-iw-a KUTENDEKA ek pend-ek-a KUTENDESHA esh, ez, ish, iz kom-esh-a, ing-iz-a KUTENDANA an finy-an-a
Uainishaji wa Neno
- Kuainisha ni kugawa neno katika viambishi vyake mbalimbali. Tunapoainisha neno, tunaonyesha mzizi wa neno pamoja na viambishi vyote vilivyofungamanishwa kuunda neno hilo.
Mifano:
Ainisha maneno yafuatayo:
- nitasoma → ni-ta-som-a
ni → kiambishi kiwakilishi cha nafsi ya kwanza umoja
ta → kiambishi kiwakilishi cha waka= ujao
som → shina la kitenzi cha kusoma
a → kiishio - walipozipata → wa-li-po-zi-pat-a
wa → kiambishi kiwakilishi cha nafsi ya pili wingi
li → kiambishi kiwakilishi cha waka= uliopita
po → kiambishi kiwakilishi cha po ya wakati au cha ngeli ya mahali PO
zi → kiambishi kiwakilishi cha kitendwa, ngeli ya I-ZI wingi
pat → shina la kitenzi cha kupata
a → kiishio - vimeshikamana → vi-me-shik-aman-a
vi → kiambishi kiwakilishi cha ngeli ya KI-VI wingi
me → kiambishi kiwakilishi cha waka= uliopita muda mfupi
shik → shina la kitenzi cha kupata
aman→ kiambishi kiwakilishi cha kauli ya kutendamana
a → kiishio - mnayemkimbilia → m-na-ye-m-kimbi-li-a
m → kiambishi kiwakilishi cha nafsi ya pili wingi
na → kiambishi kiwakilishi cha wakati uliopo
ye → kiambishi kirejeshi cha nafsi ya tatu
m→ kiambishi kiwakilishi cha mtendewa, nafsi ya tatu umoja
kimbi → mzizi wa kitenzi cha kukimbia
li → kiambishi kiwakilishi cha kauli ya kutendea
a → kiishio - yakimwagika → ya-ki-mwag-ik-a
ya → kiambishi kiwakilishi cha ngeli ya YA-YA
ki → kiambishi kiwakilishi cha KI-ya masharti au au cha KI-ya kuendelea
mwag → mzizi wa neno mwaga
ik→ kiambishi kiwakilishi cha kauli ya kutendeka
a → kiishio - hawakukushibisha → ha-wa-ku-ku-shib-ish-a
ha → kiambishi kiwakilishi cha kukanusha
wa → kiambishi kiwakilishi cha nafsi ya tatu wingi
ku → kiambishi kiwakilishi cha kukanusha waka= uliopita
ku → kiambishi kiwakilishi cha nafsi ya pili mtendewa
shib → mzizi wa kitenzi cha kushiba
ish→ kiambishi kiwakilishi cha kauli ya kutendesha
a → kiishio - lililolililia → li-li-lo-li-li-li-a
li → kiambishi kiwakilishi cha ngeli ya LI-YA umoja
li → kiambishi kiwakilishi cha wakati uliopita
lo → kiambishi kirejeshi cha ngeli ya LI-YA umoja
li→ kiambishi kiwakilishi cha mtendewa, ngeli ya LI-YA
li → shina la kitenzi cha kulia
li → kiambishi kiishio cha kauli ya kutendea
a → kiishio
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download Viambishi - Sarufi na Matumizi ya Lugha Kiswahili Notes.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students