Ngeli za Kiswahili - Sarufi na Matumizi ya Lugha Kiswahili Notes

Share via Whatsapp


Utangulizi

  • Ngeli ni makundi ya nomino katika lugha ya Kiswahili yenye sifa zinazofanana kisarufi.


A-WA

  • Huwa na majina ya watu, vilema, viumbe, vyeo na viumbe vya kiroho, n.k.
  • Huchukua miundo kama vile M-WA, M-MI, KI-VI, n.k.
    k.m.
    - mtu - watu
    - mkulima - Wakulima
    - mtume - mitume
    - mkizi - mikizi
    - kiwete - viwete
    - kibyongo - vibyongo
    - nabii - manabii
    - kuku - kuku
    - waziri - mawaziri


U-I

  • Huwa na majina ya mimea, sehemu za mwili, vifaa, matendo, maumbile, n.k.
  • Mara mingi huchukua muundo wa M-MI.
    k.m.
    - mchungwa - michungwa
    - mkoko - mikoko
    - mkono - mikono
    - mfupa - mifupa
    - msumari - misumari
    - mgomo - migomo
    - msukosuko - misukosuko
    - mlima - milima
    - mwendo - myendo
    - mwamba - myamba



U-YA

  • Huwa na majina ya hali, matendo, n.k.
  • Huchukua muundo wa U-MA.
    k.m.
    - Ugonjwa - magonjwa
    - upana - mapana
    - uasi - maasi
    - uchungu - machungu
    - ulezi - malezi
    - uovu - maovu
    - uhusiano - mahusiano


YA-YA

  • Huwa na nomino zipatikanazo kwa wingi.
  • Hazibadiliki katika umoja na wingi.
  • Huchukua muundo wa MA-MA.
    k.m.
    - manukato
    - mauti
    - maziwa
    - marashi
    - mahubiri
    - majira 
    - maradhi
    - maafa
    - mazingira


KI-VI

  • Ni majina ya vifaa, sehemu za mwili, vitu, udogo, lugha, n.k.
  • Huchukua miundo KI-VI na CH-VY.
    k.m.
    - kisu - visu
    - kitabu - vitabu
    - chakula - vyakula
    - chanda - vyanda
    - kijitu - vijitu
    - kigombe - vigombe
    - kiguu - viguu
    - kidovu - vidovu


LI-YA

  • Huwa na majina ya sehemu za mwili, dhana, vifaa, ukubwa, n.k.
  • Huchukua muundo wa JI-MA, JI-ME, JA-MA, JE-MA n.k.
    k.m.
    - jicho - macho
    - jina - majina
    - jitu - majitu
    - jino - meno
    - goma - magoma
    - jambo - mambo
    - janga - majanga
    - jembe - majembe
    - jeneza - majeneza
    - wazo - mawazo
    - tunda - matunda
    - jua - majua
    - ziwa - maziwa
    - ua-maua


I-I

  • Huwa na nomino dhahania na vitu visivyoweza kuhesabika.
  • Hazibadiliki katika umoja na wingi.
    k.m.
    - sukari
    - amani
    - chai
    - mvua
    - Imani
    - chumvi
    - subira
    - imani
    - amani
    - furaha


I-ZI

  • Huhusisha nomino dhahania na vitu.
  • Hazibadiliki katika umoja na wingi.
    k.m.
    - nyumba
    - baiskeli
    - karatasi
    - redio
    - meza
    - dini
    - dawa
    - ndizi
    - jozi

 



U-ZI

  • Huchukua miundo W-NY, U-NY, U-F, n.k.
    k.m.
    - wayo - nyayo
    - wakati - nyakati
    - uso - nyuso
    - ufa - nyufa
    - ufunguo - funguo
    - ufagio - fagio
    - wembe - nyembe
    - uwanja - nyanja
    - ujumbe - jumbe
    - ukoo - koo
    - waraka - nyaraka
    - waya - nyaya


U - U

  • Huwa na nomino za dhahania na vitu visivyoweza kuhesabika.
  • Hazibadiliki kimaumbo.
  • Huchukua U au W.
    k.m.
    - Ujinga
    - Ulafi
    - Ulaji
    - Werevu
    - Unga
    - Uji
    - Ugali
    - udongo


KU

  • Nomino zinazoundwa kutokana na vitenzi k.m. kuomba kwake kumemsaidia.


PAKUMU

  • Ngeli ya mahali.
  • Huwa na nomino moja ‘mahali’.

PA (mahali karibu au panapodhihirika) k.m. Kitabu kipo pale.

KU (mahali mbali au kusikodhihirika) k.m. Mahali kule kunafaa.

MU (ndani ya) k.m. Mahali mle mna siafu.

 

 

  



Jinsi Ngeli Mbalimbali Zinavyotumia: "a-nganifu", Viashiria na Viashiria Visisitizi.

 NGELI A-UNGANIFU  VIASHIRIA    VIASHIRIA VISISITIZI   
    KARIBU MBALI KIDOGO MBALI KARIBU MBALI KIDOGO MBALI
 A-WA  wa  huyu  huyo  yule  yuyu huyu   yuyo huyo   yule yule 
 wa  hawa  hao  wale  wawa hawa  ao hao  wale wale
 KI-VI  cha  hiki  hicho   kile   kiki hiki  kicho hicho  kile kile
 vya  hivi  hivyo  vile  vivi hivi  vivyo hivyo  vile vile
 LI-YA  la  hili  hilo  lile  lili hili  lilo hilo  lile lile
 ya  haya  hayo  yale  yaya haya  yayo hayo  yale yale
 U-I  wa  huu  huo  ule  uu huu  uo huo  ule ule
 ya  hii  hiyo  ile  ii hii  iyo hiyo  ile ile
 U-ZI  wa  huu  huo   ule  uu huu  uo huo  ule ule
 za  hizi  hizi  zile  zizi hizi  zizo hizo  zile zile
 I-ZI  ya  hii  hiyo  ile  ii hii  iyo hiyo  ile ile
 za  hizi  hizo  zile  zizi hizi  zizo hizo  zile zile
 U-YA  wa  huu  huo  ule  uu huu  uo huo  ule ule
 ya  haya  hayo  yale  yaya haya  yayo hayo  yale yale
 YA-YA  ya  haya  hayo  yale  yaya haya  yayo hayo  yale yale
 I-I  ya  hii  hiyo  ile  ii hii  iyo hiyo  ile ile
 U-U  wa  huu  huo  ule  uu huu  uo huo  ule ule
 PA  pa  hapa  hapo  pale  papa hapa  papo hapo  pale pale
 KU  kwa  huku  huko  kule  kuku huku  kuko huko  kule kule
 MU  mwa  humu  humo  mle  mumu humu  mumo humo  mle mle


Virejeshi(-o, amba-), -enye, -enyewe, ote, o-ote, ingi, ingine n.k kulingana na ngeli mbalimbali.

 NGELI VIREJESHI   -ENYE -ENYEWE -OTE   -O-OTE -INGI -INGINE
  O-REJESHI AMBA-            
 A-WA   ye  ambaye  mwenye  mwenyewe  _  yeyote  _ mwengine
 o  ambao  wenye  wenyewe  wote  wowote  wengi  wengine
 KI-VI   cho  ambacho  chenye  chenyewe  chote  chochote  kingi  kingine
 vyo  ambavyo  vyenye  vyenyewe  vyote   vyovyote  vingi  vingine
 LI-YA   lo  ambalo  lenye  lenyewe  lote  lolote  jingi  jingine
 yo  ambayo  yenye  yenyewe  yote  yoyote  mengi  mengine
 U-I   o  amabo  wenye  wenyewe  wote  wowote  mwingi  mwingine
yo  amabayo  yenye  yenyewe  yote  yoyote  mingi  mingine
 U-ZI   o  ambao  wenye  wenyewe  wote  wowote  mwingi  mwingine
zo  ambazo  zenye  zenyewe  zote  zozote  nyingi  nyingine
 I-ZI   yo  ambayo  yenye  yenyewe  yote  yoyote  nyingi  nyingine
 zo  ambazo  zenye  zenyewe  zote  zozote  nyingi  nyingine
 U-YA   o  ambao  wenye  wenyewe  wote  wowote  mwingi  mwingine
 yo  ambayo  yenye  yenyewe  yote  yoyote  mengi  mengine
 YA-YA  yo  ambayo  yenye  yenyewe  yote  yoyote  mengi  mengine
 I-I  yo  ambayo  yenye  yenyewe  yote  yoyote  nyingi  nyingine
 U-U  o  ambao  wenye  wenyewe  wote  wowote  mwingi  mwingine
 PA  po  ambapo  penye  penyewe  pote   popote  pengi  pengine
 KU  ko  ambako  kwenye  kwenyewe  kwote  kokote  kwingi  kwengine
 MU  no  ambamo  mwenye  mwenyewe  mwote  momote  mwingi  mwengine
Join our whatsapp group for latest updates

Download Ngeli za Kiswahili - Sarufi na Matumizi ya Lugha Kiswahili Notes.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest