- Wakati Uliopita - LI
- Wakati Timilifu (Uliopita Muda Mfupi) - ME
- Wakati Uliopo - NA
- Wakati Ujao - TA
- Wakati wa Mazoea - HU
- Wakati Usiodhihirika - A
- Wakati Timilifu Usiodhihirika - KA
Wakati Uliopita - LI
- Hutumia kiambishi 'LI' na hurejelea kitendo kilichokamilika muda mrefu uliopita.
- Ifuatayo ni mifano katika sentensi.
k.m: nilienda, tulilima, walikufukuza
- mama alienda sokoni
- Ndoto hio ilinisumbua usiku kucha
Wakati Timilifu (Uliopita Muda Mfupi) - ME
- Hutumia kiambishi 'ME' na hurejelea kitendo ambacho kimekamilika muda usio mrefu.
k.m: amepona, nimewachagua, zimechanganyika
- Tumeuona wema wake Bwana
- Dada yake amepagawa
Wakati Uliopo - NA
- Hutumia kiambishi 'NA' kurejelea jambo linalotendeka sasa hivi.
k.m: anaugua, yanametameta, unatisha
- Ninakupenda kwa yale unayonitendea
- Nyumba zote zinabomolewa mwaka huu
Wakati Ujao - TA
- Huchukua kiambishi 'TA' na hurejelea kitendo ambacho bado hakijafanyika lakini kinatarajiwa kufanyika..
k.m: atakupa, kitajulikana, utapokelewa
- Mtoto atalifunga dirisha litakalokuwa likiingiza hewa
- Je, utaenda sokoni kesho kutwa?
Wakati wa Mazoea - HU
- Hutumia kiambishi 'HU' na hurejelea kitendo ambacho hufanyika mara kwa mara au kila siku n.k.
k.m: hutembea, husoma, huzilinda
- Dkt. Matumbo hutibu wagonjwa
- mchungwa ule huzaa machungwa matamu
Wakati Usiodhihirika - A
- Hutumia kiambishi cha ngeli au nafsi pamoja na kiungo 'A' kurejelea kitendo kinachoendelea kutendeka katika wakati usiodhihirika.
k.m: achukua, zapepea, twaangamia
- Baba atusubiri nyumbani
- Vitabi vyako vyote vyachomeka
Wakati Timilifu Usiodhihirika - KA
- Hutumia kiungo 'KA' kurejelea kitendo ambacho kinakamilika katika wakati usiojulika. Pia hutumika kurejelea kitendo kifanyika baada ya kingine.
- Hutumiwa katika masimulizi.
k.m: ikawalemea, tukazichukua, likampendeza
- Latifa akaangalia juu akamwona nyoka
- Akawanyeshea mana wakiwa jangwani
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download Nyakati za Kiswahili - Sarufi na Matumizi ya Lugha Kiswahili Notes.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students