Kukanusha; Kinyume - Sarufi na Matumizi ya Lugha Kiswahili Notes

Share via Whatsapp


Kukanusha

  • Kukanusha ni kukataa au kukana kauli.
  • Mara nyingi tunapokanusha, tuanaongeza kiambishi 'HA-' mwanzoni mwa kitenzi. Hata hivyo, kiambishi hicho hubadilika katika nafsi ya kwanza na ya pili umoja. Angalia jedwali lifuatalo.
    KIAMBISHI MATUMIZI MFANO
    SI nafsi ya kwanza si-ku-wa-on-a
    HU nafsi ya pili hu-ni-faham-u
    HA nafsi ya tatu ha-ta-chuku-a

  • Viambishi vya wakati na vya hali pia hubadilika kama ilivyoonyeshwa katika ifuatavyo:

Kukanusha Wakati Uliopita (LI) - 'KU'

  1. Kajuta alimpigia kura. - Kajuta hakumpigia kura.
  2. Nilikupa nafasi yako. - Sikukupa nafasi yako.

Kukanusha Wakati Timilifu (Uliopita Muda Mfupi) (ME) - 'JA'

  1. Maziwa ya nyanya yamemwagika. - Maziwa ya nyanya hayajamwagika.
  2. Viwete wametembea. - Viwete hawajatembea.

Kukanusha Wakati Uliopo (NA) - '-I'

  1. Unasoma sentensi ya kwanza. -  Husomi sentensi ya kwanza.
  2. Zinafanana na nyota. - Hazifanani na nyota.

 

Kukanusha Wakati Ujao (TA) - 'TA'

  1. Jua litawaka sana. - Jua halitawaka sana.
  2. Watakaribishwa kwenye malango ya lulu. - Hawatakaribishwa kwenye malango ya lulu.

Kukanusha Wakati wa Mazoea (HU) - '-I'

  1. Polisi wa jiji kuu huchukua hongo. - Polisi wa jiji kuu hawachukui hongo.
  2. Bendera hufuata upepo. - Bendera haifuati upepo

Kukanusha Wakati Usiodhihirika (A) - '-I'

  1. Anita ampenda Kaunda. - Anita hampendi Kaunda.
  2. Chema chajiuza, kibaya chajitembeza. - Chema hakijiuzi, kibaya hakijitembezi.

Kukanusha KI ya Masharti (KI) - 'SIPO'

  1. Ukimwadhibu mtoto, atapata adabu njema. - Usipomwadhibu mtoto hatapata nidhamu..
  2. Bei yake ikishuka, nitainunua. Bei yake isiposhuka, sitainunua.

Kukanusha PO ya Wakati (PO) - 'SIPO'

  1. Ulalapo usiku zima stima - Usipo lala usiku usizime stima
  2. Mtoto aliapo mnyonyeshe. - Mtoto asipo lia usimnyonyeshe

Kukanusha Hali ya Uwezekano (NGE) - 'SINGE'

  1. Ningekuwa nakupenda ningekwambia mapema. - Nisingekuwa nakupenda nisingekwambia mapema.
  2. Zingekuwa nyingi, wangeziiba. - Zisingekuwa nyingi, wasingeziiba.

Kukanusha Hali ya Uwezekano (NGALI) - 'SINGALI'

  1. Khadija angalisoma kwa bidii angalikuwa na cheo kikubwa. - Khadija asingalisoma kwa bidii asingalikuwa na cheo kikubwa
  2. Yangalikuwa mabivu yangalianguka yenyewe. - Yasingalikuwa mabivu yasingalianguka yenyewe

Kukanusha Amri/Agizo (-a/-e) - 'SI'

  1. Peleka kikapu hiki kwa nyanya.  - Usipeleke kikapu hiki kwa nyanya.
  2. Chakula kiliwe. - Chakula kisiliwe.
  3. Mpende adui yako. - Usimpende adui yako.
  4. Waambieni watu wa mataifa yote. - Msiwaambieni watu wa mataifa yote.

Kukanusha Viunganishi vya Kujumuisha (NA, KA) - 'WALA'

  1. Bafi alikuzaba kofi na kukupiga teke. Bafi hakukuzaba kofi wala hakukupiga teke.
  2. Mama amepika chakula tukala pamoja. Mama hajapika chakula wala hatujala pamoja


Kinyume

  • Maneno ya kinyume ni maneno yenye maana inayopingana.
  • Inafaa ikumbukwe kwamba kuna tofauti kati ya kinyume na kukanusha. Kukanusha ni kukataa ujumbe wa sentensi bila kubadilisha maneno. Tunapokanusha, tunabadilisha viambishi pekee ili kupinga wazo la sentensi.
  • Maneno ya kinyume huwa maneno mengine tofauti kabisa ambayo yanapingana kimaana bila kubadilisha maendelezo ya neno.

Kinyume cha Kawaida

Hisia, hali, dhana n.k

  1. vita - amani
  2. furaha - kilio
  3. nuru - giza
  4. shibe - njaa
  5. mwanzo - mwisho

Kinyume cha Sifa

Sifa zinazopingana kimaana

  1. tamu - chungu
  2. kubwa - dogo
  3. nzuri - mbaya
  4. nyeupe - nyeusi

Kinyume cha Jinsia (Uume - Uke)

Majina ya kijinsia moja yanabadilishwa na kuwa jinsia ile nyingine.

  1. baba - mama
  2. mumewe - mkewe
  3. mjomba - shangazi
  4. kaka - dada
  5. babu - nyanya
  6. mvulana - msichana
  7. ghulamu - banati
  8. shaibu - ajuza

Kinyume cha Uhusiano

Kinyume cha vitu au dhana mbili zinazohusiana.

  1. mwalimu - mwanafunzi
  2. daktari - mgonjwa
  3. mzazi - mwana
  4. kiongozi - mfuasi

Kinyume cha Vitenzi

Tunabadilisha vitenzi kwa kuweka vitenzi vingine vyenye maana inayokinzana

  1. ongea - nyamaza
  2. penda - chukia
  3. sifu - kashifu
  4. simama -keti
  5. lia - cheka
  6. tabasamu - nuna
  7. enda - kuja

Kinyume cha Kutendua

Vitenzi vinaweka katika kauli ya kutendua ili kuvikanusha.

  1. fumba - fumbua
  2. ficha - fichua
  3. vaa - vua
  4. anika - anua
  5. kunja - kunjua
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kukanusha; Kinyume - Sarufi na Matumizi ya Lugha Kiswahili Notes.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest