- Utangulizi
- Alama ya Kikomo au Kituo Kikuu
- Alama ya Kituo, Kipumuo au Koma
- Alama ya Dukuduku
- Alama ya Kinukuu
- Alama ya Kiulizi
- Alama ya Hisi
- Alama ya Nukta-Mbili au Koloni
- Alama ya Nukta-Kituo au Semi Koloni
- Alama ya Kistari Kifupi
- Alama ya Kistari Kirefu
- Alama ya Mabano au Parandesi
- Alama ya Kinyota
- Alama ya Mlazo
- Alama ya HERUFI KUBWA
Utangulizi
- Kunazo alama kadhaa zinazotumika kuakifisha maneno na sentensi za Kiswahili.
Alama ya Kikomo au Kituo Kikuu (.)
- Kuonyesha mwisho wa sentensi.
- Huu ndio mwisho wa sentensi hii.
- Kioo kimevunjika
- Katika kufupisha maneno
- U.N, K.B.C, Y.C.S, N.Y.S
- Dkt. Maktaba, Bw. Msumari
- Kuonyesha Saa
- Misa ilianza saa 4.30 za asubuhi.
- Hivi sasa ni saa 10.20.
- Katika hesabu kuonyesha sehemu isiyo nzima
- Ukigawa tatu mara mbili, utapata 1.5
- Mtoto huyo ana uzani wa kilo 8.27
- Kuonyesha senti katika pesa
- Bei yake ni shilingi 12.50.
- Karo ya shule mwaka huu ni 80,000.00
Alama ya Kituo, Kipumuo au Koma (,)
- Kuorodhesha vitu zaidi ya mbili
- Nimenunua simu, saa, redio na viatu.
- Kina mama waliimba, wakapiga ngoma na kunengua viuno vyao.
- Kugawanya mawazo katika sentensi.
- Baada ya sala za jioni, Mzee Makosa alitoka nje na kuwasha sigara yake.
- Nilipomwuliza kama alimjua binti yule, aliniangalia tu na kucheka
- Ingawa kitabu hiki ni kizito, sina budi kukibeba.
- Kutoa maelezo zaidi.
- Shabiba, mmojawapo ya wanawake wajawazito, amejifungua mtoto wa kike.
- Shati hili, ingawa nalichukia, nitalivalia tu.
- Katika tarakimu, kugawa elfu.
- Shilingi 209, 408, 000 ziliporwa na serikali.
- Dawa hiyo iliua takribani mbu 61, 247.
Alama ya Dukuduku (…)
- Hutumika kuonyesha kuwa maneno yameachwa ya kutangulia, kati au ya mwisho. Yaweza kuachwa kwa kuwa makali
- Nyani haoni… - kukatizwa usemi/kauli
AMINA: Mama ni…
MAMA: Kwanza watoka wapi usiku huu? - maneno yanaendelea
- Alimwambia ajihadhari anapovuka barabara…
Alama ya Kinukuu (' na ")
- Kunukuu usemi halisi
- "Ukitaka kufua dafu," mama akamwambia mwanawe, "lazima utie bidii."
- Alimtazama kisha akamwuliza, "Unadhani nimechanganyikiwa kama wewe?"
- Kunukuu kichwa cha kazi ya sanaa k.v kitabu, wimbo, kipindi n.k
- Saumu na Neema ni wahusika katika riwaya "Hamu ya Sumu Tamu".
- Rose Muhando ndiye aliyeimba "Mteule Uwe Macho".
- Kuonyesha maneno yasiyo ya Kiswahili unapochanganya ndimi katika sentensi
- Huyu ndiye mchezaji "number one"
- Amesema "keyboard" ya "computer" yake haifanyi kazi..
- Kuonyesha maneno yanayowakilisha maana tofauti na maana yake ya kawaida au kinaya.
- Lesi alipoenda kwenye 'maktaba' alipata mimba.
- Rais wetu 'mtukufu' amewatisha mawaziri wake.
- Moto ulioteketeza shule hiyo ulitokana na kusudi la wanafunzi la 'kumshtua' mwalimu wao.
- Kuonyesha herufi iliyoachwa nje au kufupisha maneno katika ushairi hasa kwa kusudi la kutosheleza idadi ya mizani
- 'takufuata popote wendapo,
- 'liapo ya mgambo, lazima kuna jambo
- Katika maendelezo ya sauti ya ung'on'g'o (ng')
- Ng'ombe wa Ng'ang'a wanang'ang'ania nini?
- King'ang'i anapenda kunung'unika ovyo ovyo.
Alama ya Kiulizi (?)
- Kuulizia swali
- Je, utamtembelea lini?
- Ariana anaishi wapi?
- Kuonyesha pengo lililoachwa wazi
- Ndama ni mwana wa ng'ombe ilhali ___?___ ni mtoto wa mbuzi.
- __?__ mpokee mke wako, __?__, siku ya leo umepata jiko.
Alama ya Hisi (!)
- Kuonyesha hisia kama vile hasira, mshangao, furaha n.k
- Lo! Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni.
- Pepo nyeusi! Shindwa! Chomeka! Kwenda kuzimu!
- Kuigiza Tanakali za Sauti
- Amejikwaa sasa ameanguka pu!
- Moyo ulidunda ndu! ndu!
Alama ya Nukta-Mbili au Koloni (:)
- Kutanguliza orodha
- Harusi hiyo ilihudhuriwa na watu wa wengi: wake kwa waume; wadogo kwa wakubwa; wazee kwa vijana.
- Kuna aina kadhaa za vivumishi: vivumishi vya sifa, vivumishi vya idadi, vivumishi viwakilishi na kadhalika
- Kuelezea sababu au kuonyesha matokeo ya kitu.
- Saumu a lipoingia chumbani alipigwa na butwaa: mamake alikuwa amekufa.
- Baba alinipatia zawadi nzuri sana: nilirukaruka kwa furaha.
- Kuonyesha saa
- Wimbo huo unachukua dakika 4:45.
- Aliingia saa 5:1 5
- Kunukuu ukurasa wa Bibilia
- Padre alisoma Luka 2:1-6
- Katika kitabu cha Mwanzo 5: 2-7, Bibilia inasema...
- Kuonyesha maneno ya msemaji katika tamthilia au mchezo wa kuigiza
- Mzee Mwanyati: Unafikiria mimi ni nyanyako?
- Kadogo: (akitetemeka) Tafadhali naomba unisamehe.
- Kuonyesha mada katika barua au kumbukumbu za mkutano
- KUH: Ombi Lako la Kujiuzulu.
- RE: Barua ya tarehe 3/2/1 999.
- Katika kumbukumbu za mkutano
- KUM: 2/321 /2000 Mbinu Mpya za Kunyamazisha Raia
- Ajenda 2: Kusomwa kwa kumbukumbu za mkutano uliotangulia
Alama ya Nukta-Kituo au Semi Koloni (;)
- Kuorodhesha vitu hasa vinapokuwa na zaidi ya neno moja
- Harusi hiyo ilihudhuriwa na watu wa wengi: wake kwa waume; wadogo kwa wakubwa; wazee kwa vijana.
- Wakati wa likizo tulitembelea sehemu kadhaa: Mombasa, Kenya; Dodoma, Tanzania; Kampala, Uganda na tukamalizia hapa Nairobi, Kenya.
- Kuunganisha vishazi huru viwili au kuonyesha mawazo mawili.
- Tuliwasili darasani tukiwa tumechelewa; mwalimu alitukaribisha kwa kiboko.
- Usiwe na wasiwasi; nitakuwa pamoja nawe siku zote.
Alama ya Kistari Kifupi (-)
- Kuunganisha maneno mawili
- Mbwa-koko aliuma mwana-haramu.
- Nawatuma kama wana-kondoo miongoni mwa mbwamwitu.
- Kuonyesha hadi, au mpaka
- Bei imepanda kutoka shilingi 20 - 30
- Tutasoma kitabu cha Matendo 2: 3 - 7
- Kama alama ya kupunguza au kutoa katika Hesabu
- 9 - 7 = 2
- 4 - 5 = -1
- Kuonyesha neno ambalo halijakamilika litaendelezwa katika msitari ufuatao
- Ukitaka twende kwetu nyumbani nitakupeleka ukamwone mamangu.
- Kuna migumo kumi na mitatu katika Bustani la Kuzimu.
- Kuonyesha tarehe
- Watu wengi walikufa tarehe 07-08-1 998.
- Marehemu alikufa tarehe 06-06-2006
Alama ya Kistari Kirefu (‒)
- Kutoa maelezo zaidi
- Nilipokutana na Zakido ‒ ambaye aliripotiwa kupotea miaka miwili iliyopita ‒ nilimsalimia lakini hakunitambua.
- Hatimaye nimeshinda ‒ baada ya kujaribu kwa masaa matatu.
- Kuorodhesha hoja au vitu
- Umuhumu wa fasihi simulizi:
‒ kuburudisha
‒ kuelimisha
‒ kuunganisha jamii
- Umuhumu wa fasihi simulizi:
Alama ya Mabano au Parandesi ()
- Kutoa maelezo zaidi
- Z. Anto (aliyeimba Binti Kiziwi) ametoa wimbo mpya.
- Shangazi yangu (ambaye ni naibu wa waziri) amenitumia zawadi.
- Kutoa neno jingine lenye maana sawa
- Dhamira (nia) ya mshairi huyu ni kutushauri tusikimbilie maisha.
- Mabanati (wasichana) hao hutembea uchi jijini usiku wa manane.
Alama ya Kinyota (*)
- Kuonyesha neno ambalo litaelezewa zaidi chini ya ukurasa(foot note)
- Alipopata nafasi ya kuingia shule ya upili ya Starehe*, mwanafunzi huyo alijawa na furaha tele.
*Starehe ni mojawapo ya shule zinazofanya vizuri zaidi barani Afrika.
- Alipopata nafasi ya kuingia shule ya upili ya Starehe*, mwanafunzi huyo alijawa na furaha tele.
- Kuficha herufi/silabi katika neno ili kupunguza ukali wa maneno yasiyo na nidhamu.
- Ra is aliwaita wananchi m**i ya kuku.
- Aidha, alisema kwamba nyote ni wapu***vu.
Alama ya Mlazo (/)
- Kuonyesha 'au'
- Mkutano huo utahutubiwa na Rais/Waziri Mkuu.
- Wazungumzaji wengi wa Kiswahili wanatoka Kenya/Tanzania.
- Kuonyesha neno au fungu la maneno lenye maana sawa.
- Sheila amepewa cheo cha katibu/mwandishi.
- Hawa ndio wanaotapatapa ovyo/wasio na mbele wala nyuma.
- Katika hesabu kuonyesha kugawanya au akisami.
- 5/7 ya siku za juma ni siku za kazi.
- 12/6 = 2
- Katika tarehe
- Shule zilifunguliwa tarehe 08/01 /201 2
- Kamati hiyo ilikubaliana kwamba, Mwokozi alizaliwa tarehe 25/12
Alama ya HERUFI KUBWA
- Kuanzisha sentensi'
- Fisi hula mizoga.
- Huu ndio mwanzo wa sentensi hii.
- Kuonyesha Nomino za Kipekee
- Bi Rangile anatoka Vikwazoni.
- Nchi ya Tanzania imebarikiwa na Mlima Kilimanjaro unaowavutia wageni kutoka Ulaya.
- Kuonyesha Kichwa au Mada
- ALAMA ZA UAKIFISHAJI
- UFAHAMU
- Njia Tano za Kuua Mbu
- Kuonyesha maneno yaliyofupishwa
- UKIMWI ni Ukosefu wa Kinga Mwilini.
- TUKI ni Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download Alama za Uakifishaji - Sarufi na Matumizi ya Lugha Kiswahili Notes.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students