Mnyambuliko wa Vitenzi - Sarufi na Matumizi ya Lugha Kiswahili Notes

Share via Whatsapp


Utangulizi

  • Kunyambua kitenzi ni kukiongeza viambishi tamati ili kukipa maana tofauti.


Aina za Minyambuliko/Kauli za Vitenzi

Kutenda

  • Hali ya kawaida ya kitenzi.
    k.m
    - funika
    - choma

Kutendatenda

  • Hali ya kitenzi kurudiwa.
    km.

Kutendea

  • Kwa niaba ya
  • Badala ya
  • Sababu
  • Kuonyesha kitumizi
  • Mwendo wa kitu kuelekea kingine

Kutendwa

  • Huonyesha nomino iliyoathiriwa na kitenzi.

Kutendewa

  • Humaanisha kitendo kimetendwa na mtu badala au kwa niaba ya mtu mwingine.

Kutendana

  • Unamtenda mtu jambo naye anakutenda jambo lilo hilo.

Kutendeana

  • Unamtendea mtu jambo naye anakutendea jambo lilo hilo.

Kutendeka

  • Uwezekano wa kitendo kufanyika

Kutendesha

  • Mtu au kitu kusababisha kufanyika kwa kitendo.

Kutendeshea

  • Kusababisha kitendo kitendeke kwa niaba ya mwingine.

Kutendeshwa

  • Kusababishwa kufanya jambo.

Kutendeshewa

  • Mtu kusababishwa kitendo kitendeke kwa niaba yake.

Kutendeshana

  • Kusababisha kitendo kitendeke kwa mtu naye anasababisha kitendo kicho hicho kitendeke kwako.

Kutendesheana

  • Kusababisha kitendo kitendeke kwa niaba ya mtu naye anasababisha kitendo kicho hicho kitendeke kwa niaba yako.

Kutendesheka

  • Kitendo fulani kinaweza kusaababishwa.

Kutendama

  • Kuwa katika hali fulani bila ya mabadiliko.
    - lala-lalama
    - ficha-fichama
    - shika-shikama
    - ganda-gandama
    - chuta-chutama
    - funga-fungama
    - kwaa-kwama
    - unga-ungama
    - andaa-andama
    - saki-sakama

Kutendata

  • Hali ya mgusano au kushikanisha vitu viwili.
    - paka-pakata
    - fumba-fumbata
    - kokoa-kokota
    - okoa-okota
    - kama-kamata

Kutendua

  • Hali ya kinyume
    - choma-chomoa
    - funga-fungua

Kutenduka

  • Kuweza kufanyika kwa hali ya kinyume.
    - chomoka
    - funguka

Mifano Katika Jedwali

 TENDA TENDEA  TENDANA  TENDEANA  TENDWA TENDEWA  TENDEKA  TENDESHA  TENDESHANA
 fanya  fanyia  fanyana  fanyiana  fanywa  fanyiwa  fanyika  fanyisha  fanyishana
 lima  limia  limana   limiana  limwa  limiwa  limika  limisha  limishana
 pika  pikia   pikana  pikiana  pikwa  pikiwa  pikika  pikisha  pikishana
 lia  lilia  ?  liliana  ?  liliwa   lilika  liza  lizana
 kula  lia  lana  liana  liwa  liwa  lika  lisha  lishana
 penda  pendea  pendana  pendeana  pendwa  pendewa  pendeka  pendeza  pendezana
 omba  ombea  ombana  ombeana  ombwa  ombewa  ombeka  ombeza  ombezana
 tembea  tembelea  tembeleana  tembeleana  tembelewa  tembelewa  tembeleka  tembeza  tembezana
 abudu  abudia  abudiana  abudiana  abudiwa  abudiwa  abudika  abudisha  abudishana
 choma  chomea  chomana  chomeana  chomwa  chomewa  chomeka  chomesha  chomeshana
Join our whatsapp group for latest updates

Download Mnyambuliko wa Vitenzi - Sarufi na Matumizi ya Lugha Kiswahili Notes.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest