Sentensi za Kiswahili - Sarufi na Matumizi ya Lugha Kiswahili Notes

Share via Whatsapp


Utangulizi

  • Sentensi ni kundi la neno moja au maneno zaidi yenye kiima na kiarifa na inayofuata kanuni za sarufi.


Muundo wa Sentensi

Kiima, Kiarifa, Shamirisho na Chagizo

  • Sentensi huwa imeundwa na maneno mbalimbali. Vijenzi hivi vya sentensi ni Kiima, Kiarifa, Shamirisho na Chagizo

Kikundi Tenzi(KT) na Kikundi Nomino(KN)

  • Hizi ndizo sehemu mbili kuu katika sentensi. Kila kundi kikundi kinaweza kuwa na maneno mbalimbali.

Kikundi Nomino (Kiima): KN

  • Ni sehemu wa sentensi yenye nomino. Pia kikundi nomino kinaweza kushirikisha kikundi kivumishi au kishazi tegemezi.
    k.m:
    1. Safari zawa salama bila misukosuko.
    2. Wanafunzi waliokuwa wametoroka shuleni, wamekamatwa na kuadhibiwa.
    3. Matunda matamu huvutia sana.

Kikundi Tenzi (Kiarifa): KT

  • Ni sehemu ya sentensi yenye kitenzi. Licha ya kitenzi, kikundi tenzi kinaweza kushirikisha kikundi kielezi au kikundi kivumishi. Aidha, kikundi tenzi kinaweza kuwa na kikundi nomino kama shamirisho kipozi au kitondo.
    k.m:
    • Mvua inarutubisha vitu vyote.
    • Dunia huzunguka jua.
    • Madawati yaliyokuwa yamechafuliwa yamesafishwa.

Shamirisho/Yambwa

  • Shamirisho ni mtendwa au mtendewa katika sentensi. Ni sehemu ya sentensi inayowakilisha kitu kilichofanyiwa kitu. Kuna aina tatu za shamirisho.

Shamirisho Kipozi/Yambwa Tendwa - (direct object)

  • Ni sehemu inayowakilisha nomino inayopokea kitendo hicho moja kwa moja. Mtendwa
    • Nyanya aliwasalimia wajukuu wake.
    • Bustani la Kuzimu linawatisha watu wengi.
    • Rita alimwandikia kakake barua kwa kalamu nyeusi.

Shamirisho Kitondo/Yambwa Tendewa - (indirect object)

  • Huwakilisha ambayo kitendo kinafanywa kwa ajili yake au kwa niaba yake. Mtendewa
    1. Mama aliwapikia watoto ugali tamu.
    2. Bibi anawasimulia wasichana wadogo hadithi za kikale.
    3. Rita alimwandikia kakake barua kwa kalamu nyeusi.

Shamirisho ala/Yambwa kitumizi

  • Hurejelea ala au kifaa kinachotumika kutekeleza kitendo hicho
    1. Wetu wengine huvuna mahindi kwa panga.
    2. Mchungaji Thabiti alikufa kwa maji.
    3. Rita alimwandikia kakake barua kwa kalamu nyeusi.

Chagizo

  • Hutuelezea zaidi kuhusu kiima, kiarifa au shamirisho. Aghalabu chagizo huwa kielezi au kivumishi.
    1. Mama M alimvalisha bintiye mavazi ya kupendeza.
    2. Mumbe ni msichana hodari sana.
    3. Kinyonga hupendelea kutembea polepole.
    4. Rita alimwandikia kakake barua kwa kalamu nyeusi.


Aina za Sentensi

  1. Sentensi Sahili
  2. Sentensi Ambatano.
  3. Sentensi Changamano

Sentensi Sahili

  • Hizi ni sentensi zenye kishazi kimoja na huwakilisha wazo moja tu.
    • Sentensi sahili kutokana na kikundi tenzi pekee:
      - Ninasoma => KT(T)
      - Hajakuandikia barua => KT(T + N)
      - Tulimwona nyoka mkubwa =>KT(T + N + V)
      - Alikimbia haraka sana => KT(T + E + E)
    • Kikundi Nomino + Kikundi Tenzi
      - Sakina anaimba. => KN(N) + KT(T)
      - Latifa na Kanita wamejipamba vizuri. => KN(N + U + N) + KT(T + E)
      - Jua kali liliwaka mchana kutwa. => KN(N + V) + KT(T + E + E)
      - Runinga ya Bwana Kazito imeharibika tena. => KN (N + V + N + N) + KT (T + E)

Sentensi Ambatano

  • Sentensi ambatano ni sentensi zenye zaidi ya kishazi huru kimoja na huwakilisha mawazo mawili au zaidi.
  • Aghalabu sentensi hizi hutumia viunganishi(U) au alama za uakifishaji kama vile kituo(,) na nuktanusu (;) ili kubainisha wazo moja toka nyingine.
    • Kuunganisha Sentensi Mbili:
      - Chesi alisoma kwa bidii. Chesi alianguka mtihani. => Ingawa alisoma kwa bidii, Chesi alianguka mtihani.
      - Dadangu amerudi nyumbani. Dadangu amelala. =>Dadangu amefika nyumbani na kulala.
    • Mifano mingine:
      - Tulifika, tukaona, tukapiga na tukatawala.
      - Leo inaonekana Karimi amejipamba akapambika.

Sentensi Changamano

  • Hizi ni sentensi zinazoundwa kwa kuunganisha kishazi huru pamoja na kishazi tegemezi au sentensi mbili kwa kutumia o-rejeshi ili kuleta zaidi ya wazo moja.
    • Kuunganisha Sentensi:
      - Juma amenilitelea kitabu. Nilikuwa nimetafuta kitabu hicho kwa muda mrefu. =>Juma ameniletea kitabu ambacho nilikuwa nimekitafuta kwa muda mrefu.
      - Yeye ni mwizi. Alipigwa jana jioni. => Yeye ndiye mwizi aliyepigwa jana jioni.
    • Mifano Zaidi:
      - Nimemuona yule ninayemtafuta na neema zake.
      - Ndoto zinazotisha ni za kishetani.

Tanbihi: Ili kutofautisha sentensi ambatano na changamano kwa urahisi, sentensi changamano hutumia o-rejeshi (k.m ambacho, ambaye, niliye- , nililo- n.k)



Uchanganuzi wa Sentensi

  • Kuchanganua sentensi ni kugawa sentensi kulingana na makundi ya maneno na aina ya maneno.
  • Kuna njia tatu za kuchanganua sentensi:
    • matawi
    • jedwali
    • mishale
  • Hatua ya kwanza katika kuchanganua/kupambanua sentensi ni kutambua aina yake. Kuna aina tatu za sentensi kimuundo. 
  • Hatua ya pili ni kutambua kundi nomino (KN) na kundi tenzi (KT). Kuna miundo mingi ya KN na KT, iweze kuzingatiwa.
  • Hatua ya tatu ni kutambua aina za maneno na viambajengo vya sentensi pamoja na vifupisho vyake.

Alama Zinazotumika

Aina Za Maneno

Aina Alama 
Nomino N
Kitenzi T
Kielezi E
Kiunganishi U
Kihusishi H
Kihisishi I
Kivumishi V
Kiwakilishi W
*Kitenzi kisaidizi Ts
*Kitenzi kikuu T
*Kitenzi kishirikishi t

Sehemu za Sentensi

Sentensi  S
Kundi nomino KN
Kundi tenzi KT
*Kundi nomino kappa Ø
*kishazi tegemezi kishazi tegemezi

Alama Zingine

Kishazi tegemezi

kishazi kitegemezi

Kuchanganua Sentensi Sahili

  1. Nimefika
    • Matawi
      sahili
    • Jedwali
       S
       KT
       T
       Nimefika

    • Mishale
      S → KT
      KT → T
      T → Nimefika
  2. Jiwe Limeanguka.
    • Matawi
      sahili 2
    • Jedwali
      S
      KN KT
      N T
      Jiwe limeanguka
    • Mishale
      S → KN + KT
      KN → N
      N → Jiwe
      KT → T
      T → limeanguka
  3. Mvua nyingi ilinyesha jana usiku.
    • Matawi
      sahili 3
    • Jedwali
      S
      KN KT
      N V T KE
      N V T E E
      Mvua nyingi  ilinyesha  jana usiku
    • Mishale 
      S → KN + KT
      KN → N + V
      N → Mvua
      V → nyingi
      KT → T + KE
      T → ilinyesha
      KE → E1 + E2
      E1 → jana
      E2 → usiku

Kuchanganua Sentensi Ambatano

  1. Barua ilitumwa lakini haikumfikia Shakila.
    • Matawi
      ambatano 1
    • Jedwali
      S
      S1 U S2
      KN1 KT1 U KT2 KN2
      N1 T1 U T2 N2
      Barua  ilitumwa lakini  haikumfikia Shakila
    • Mishale
      S → S1 + U + S2
      S1 → KN1 + KT1
      KN1 → N1
      N1 → Barua
      KT1 → T1
      T1 → ilitumwa
      U → lakini
      S2 → KT2 + KN2
      KT2 → T2
      T2 → haikumfikia
      KN2 → N2
      N2 → Shakila
  2. Mwalimu alikunja shati lake na kuwachapa wanafunzi
    • Matawi
      ambatano
    • Jedwali
      S
      S1 U S2
      KN1 KT1 U KT KN3 KE
          KN2 U T N U N
      N T N V U T N U N
      mwalimu  alikunja shati  lake  na  kuwachapa  wanafunzi kwa  kiboko

    • Mishale
      S → S1 + U + S2
      S1 → KN1 + KT1
      KN1 → N
      N → mwalimu
      KT1 → T + KN2
      T → alikunja
      KN2 → N + V
      N → shati
      V → lake
      U → na
      S2 → KT2 + KN3 + KE
      KT2 → T
      T → kuwachapa
      KN3 → N
      N → wanafunzi
      KE → U + N
      U → kwa
      N → kiboko

Kuchanganua Sentensi Changamano

Hatua za Uchanganuzi

  1. Kutambua kundi nomino na kundi tenzi
  2. Ni muhimu kujua miundo mbalimbali ya KN na KT
  3. Kutambua kishazi tegemezi
  4. Kutambua iwapo kishazi tegemezi kinajitokeza upande wa KN au KT

Mifano

  1. Tarakilishi iliyonunuliwa inapendeza sana.
    • Matawi
      changamano 1
    • Jedwali
      S
      KN KT
      N kishazi tegemezi T E
      Tarakilishi iliyonunuliwa inapendeza sana
    • Mishale
      S → KN + KT
      KN → N + kishazi tegemezi
      N → Tarakilishi
      kishazi tegemezi → iliyonunuliwa
      KT → T + E
      T → watafufuka
      E → sana
  2. Wauguzi waliogoma wiki mbili watasimamishwa kazi
    • Matawi
      changamano 2
    • Jedwali
      S
      KN KT
      N kishazi tegemezi T N
      Wauguzi waliogoma wiki mbili watasimamishwa  kazi
    • Mishale
      S → KN + KT
      KN → N + kishazi tegemezi
      N → wauguzi
      kishazi tegemezi→ waliogoma wiki mbili
      T → watasimamishwa
      N → kazi
  3. Wakenya wote wameifurahia sheria iliyopitishwa jana
    • Matawi
      changamano 3
    • Jedwali
           S
      KN   KT   
       N KN2 
       N  V kishazi tegemezi 
      Wakenya  wote  wameifurahia  sheria  iliyopitishwa jana 
    • Mishale
      → KN + KT
      KN → N + V
      N → Wakenya
      V → wote
      KT → T + KN2
      T → wameifurahi
      KN2 → N + kishazi tegemezi
      N → sheria
      kishazi tegemezi→ iliyopitisha jana


Virai na Vishazi

  • Sentensi huwa na vifungu mbalimbali. Baadhi ya vifungu hivi ni vishazi na virai

Virai

  • Kirai ni fungu la maneno lisilokuwa na kitenzi.Phrase
  • Kuna aina nne za virai:

Kirai Nomino:

  • Kirai Nomino ni fungu la maneno katika sentensi lenye nomino (Kikundi Nomino/Kiima)
    1. Redio na runinga hutumika kutupasha habari.
    2. Bintiye Mchungaji Boriti anapenda kuwasaidia watu.
    3. Miembe mirefu itakatwa.

Kirai Kiwakilishi

  • Kirai Kiwakilishi ni fungu la maneno linalowakilisha nomino katika sentensi
    1. Zenyewe zimekwishaharibika.
    2. Watakaovumilia hadi siku ya mwisho wataokolewa
    3. Yeye alijitumbukiza majini na kufariki papo hapo.

Kirai Kivumishi

  • Kirai Kivumishi ni fungu la maneno katika sentensi linalotupa habari zaidi kuhusu nomino.
    1. Matokeo tuliyokuwa tukiyasubiri yametangazwa.
    2. Duka zenye bei nafuu zimefungwa.
    3. Msichana mrembo kama malaika ameolewa.

Kirai Kielezi

  • Kirai Kielezi ni fungu la maneno linaloelezea zaidi kuhusu kitenzi au kivumishi.
    1. Walevi wana mazoea ya kupayuka ovyo ovyo.
    2. Viumbe vyote vyenye uhai vinamshangilia kwa furaha milele na milele.
    3. Kwaya ya Chuo Kikuu cha Nairobi huimba kwa sauti za kimalaika

Vishazi

  • Kishazi ni sehemu ya sentensi yenye kitenzi. Kuna aina mbili za vishazi:

Kishazi Huru

  • Kishazi Huru huwa na maana kamili na kinaweza kujisimamia chenyewe kama sentensi.
    1. Amina ameanza kuimba baada ya kumaliza kusali.
    2. Watakaopatikana wakichekacheka ovyoovyo, watang'olewa meno.
    3. Nitakupatia nusu ya ufalme wangu, iwapo utanipigia magoti.

Kishazi Tegemezi

  • Kisha Tegemezi huhitaji kuunganishwa na kishazi kingine ili kuleta maana iliyokusudiwa. Aghalabu huwa na kirejeshi k.v amba-, -enye n.k
    1. Amina ameanza kuimba baada ya kumaliza kusali.
    2. Watakaopatikana wakichekacheka ovyoovyo, watang'olewa meno.
    3. Nitakupatia nusu ya ufalme wangu, iwapo utanipigia magoti.

Vishazi Viambatani

  • Vinavyoundwa kwa vishazi huru viwili vikiwa vimeunganishwa k.m.
    1. Baba analala na mama anapika.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Sentensi za Kiswahili - Sarufi na Matumizi ya Lugha Kiswahili Notes.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest