- Utangulizi
- Kiwakilishi kuwa Kivumishi
- Kivumishi kuwa Kiwakilishi
- Kivumishi kuwa Nomino
- Kivumishi kuwa Kielezi
- Nomino kuwa Kivumishi
- Nomino kuwa Kielezi
- Kielezi kuwa Nomino
- Kitenzi kuwa Nomino
- Nomino kuwa Kiunganishi
- Kielezi kuwa Kihisishi
- Kihusishi kuwa Kielezi
- Kitenzi kuwa Kielezi
- Nomino kuwa Kihisishi
Utangulizi
- Hali ya maneno kuwa na matumizi tofauti mifano:
Kiwakilishi kuwa Kivumishi
- Huyu analia.
- Mtoto huyu analia.
Kivumishi kuwa Kiwakilishi
- Vikombe vizuri vitavunjika.
- Vizuri vitaliwa.
Kivumishi kuwa Nomino
- Mti mrefu haupandiki.
- Mrefu alikufa jana jioni.
Kivumishi kuwa Kielezi
- Viatu vibaya vitachomwa.
- Uliifanya kazi vibaya.
- Mtu mjinga ni huyu.
- Anakaa mjinga.
Nomino kuwa Kivumishi
- Tajiri alimdharau Razaro.
- Mtu tajiri huheshimiwa.
Nomino kuwa Kielezi
- Nairobi ni mji mkuu.
- Amewasili Nairobi.
- Kitoto kinalia.
- Unaongea kitoto.
- Haraka haina baraka.
- Fanya haraka tuondoke hapa.
- Sindano ya babu imepotea
- Alidungwa sindano/kwa sindano na daktari.
Kielezi kuwa Nomino
- Niliwasili jana.
- Jana yangu haikuwa nzuri.
Kitenzi kuwa Nomino
- Nataka kulala sasa.
- Kulala kwake kunaudhi.
Nomino kuwa Kiunganishi
- Ila yake imemwathiri sana.
- Watu wote ila yeye walikwenda.
- Kichwa changu kina walakini.
- Nimekula walakini sijashiba.
Kielezi kuwa Kihisishi
- Mwenda pole hajikwai.
- Pole! Usijali utapona.
- Amepaka rangi sawasawa.
- Sawasawa! Siku moja tutakutana.
Kihusishi kuwa Kielezi
- Paka amepanda juu ya mti.
- Ameingia katika choo.
Kitenzi kuwa Kielezi
- Mtoto akilia atatapika.
- Aliingia akilia.
Nomino kuwa Kihisishi
- Gege anacheza ala yake ya muziki.
- Ala! Waniwekea uchafu katika chakula?
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download Mwingiliano wa Maneno - Sarufi na Matumizi ya Lugha Kiswahili Notes.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students