Vitate, Vitawe na Visawe - Sarufi na Matumizi ya Lugha Kiswahili Notes

Share via Whatsapp


Vitate

T/D

Tata

  • hali ya kutoeleweka
    - sentensi hii ni tata.
  • fundo katika uzi
    - uzi umeingia tata/umetata.

Dada

  • ndugu wa kike

 

Tua

  • shuka kutoka angani
    - ndege ilitua uwanjani.
  • weka chini k.v. mzigo

Dua

  • maombi kwa Mungu
    - omba dua
  • piga dua – apiza/laani

 

Toa

  • ondoa kitu ndani ya kinginea
  • kinyume cha jumlisha

Doa

  • alama yenye rangi tofauti na mwili wa kitu
  • dosari/ila/walakini

Ndoa

  • arusi/makubaliano rasmi ya mwanamke na mwanamume kuishi pamoja kama mke na mume/chuo

 

 

Tundu

  • uwazi mdogo wa mviringo kwenye kitu k.v. sindano kitu maalum cha kuwekea ndege kilichotengenezwa kwa mabati, matete n.k.

Dundu

  • mdudu anayebeba uchafu
  • rundo la vitu /mtumba

 

Tuma

  • peleka kitu k.v. barua kwa njia ya posta
  • agiza mtu kufanya jambo

Duma

  • mnyama mkubwa mwenye umbo kama la paka
  • kamata, hasa katika vita

 

K/G

Kuku

  • aina ya ndege anayefugwa nyumbani

Gugu

  • mmea unaoota mahali usipotakiwa
  • mmea wa mwituni mfano wa unyasi

 

Kuni

  • vipande vya mti vya kukokea moto

Guni

  • shairi la arudhi lililokosa kutosheleza kanuni moja au zaidi ya uandishi

 

Kuna

  • kwaruza kwa kucha /kitu chenye menomeno

Guna

  • toa sauti ya kuonyesha kukataa, kutoridhika, au kuchukia jambo.

 

Kenge

  • mnyama kama mjusi mdogo

Genge

  • kundi la watu
  • pango/shimo

 

Kesi

  • daawa/mashtaka yanayosikilizwa mahakamani

Gesi

  • hewa inayotumiwa kupikia au kutiwa katika vinywaji
  • hewa ambayo haigeuki na kuwa majimaji katika joto la kawaida

CH/J

Changa

  • toa kitu ili kukusanya kwa kusudi fulani
  • isio komaa
  • chanja/pasua vipande vipande vidogo vidogo k.v. kuni

Janga

  • hatari/balaa

 

Chema

  • kizuri

Jema

  • zuri

 

Chini

  • kwenye ardhi/sakafu

Jini

  • shetani/ mtu muovu

 

Choka

  • pungukiwa na nguvu baada ya kufanya kazi

Joka

  • nyoka mkubwa sana

 

Chungu

  • chombo kinachofinyangwa cha kupikia
  • kinyume cha tamu
  • idadi kubwa (chungu nzima)
  • mdudu mdogo wa jamii ya siafu

Jungu

  • Ukubwa wa nyungu

 

Chambo

  • kinachowekwa kwenye mtego kunasia wanyama,samaki n.k.

Jambo

  • habari,tukio shughuli

 

Kucha

  • elekea asubuhi
  • ogopa

Kuja

  • hali ya kusogea karibu

 

Chuma

  • pata mali
  • madini magumu yanayotumiwa kujengea na kuundia vitu
  • tungua matunda au maua kutoka mtini

Juma

  • wiki
  • jina la mtu

 

Chenga

  • hepa kwa hila
  • mchele uliovunjikavunjika(mchele wa chenga)

Jenga

  • aka nyumba
  • fanya madhubuti/imarisha

 

Mchi

  • mti wa kupondea kwenye kinu

Mji

  • makazi ya watu wengi kulikojengwa nyumba nyingi 
  • mahali kaburini anapowekwa mauti 
  • sehemu ya kati ya chupa ya mwanamke mja mzito inayounganisha mtoto na mwili wa mama

 

Kichana

  • kitu cha kuchania nywele

Kijana

  • mtu wa makamo mwenye nguvu/mtoto wa kiume kabla ya kubaleghe

F/V

Faa

  • kusaidia
  • kuwa vizuri

Vaa

  • eneza kitu katika mwili ili kufunika sehemu fulani

 

Fua

  • safisha nguo
  • tengeneza kitu kutokana na madini
  • toa maji katika chombo
  • fua maji
  • Hakufua dafu. (hakufaulu)

Vua

  • pata samaki kwa kutumia wavu, mshipi, ndoana n.k.
  • ondoa nguo mwilini
  • nusuru, okoa, ponya
  • vua macho (tazama)

Fika

  • wasili mahali
  • bila shaka/kabisa

Vika

  • valisha

 

Fuka

  • toa moshi bila kuwaka
  • uji wowote mwepesi (uji fuka)

Vuka

  • enda upande wa pili

 

Fuma

  • piga kwa mkuki
  • ona kwa ghafla bila kutazamia mtu anayetenda jambo ovu
  • tengeneza kitu kwa kusokota nyuzi,ukindu n.k

Vuma

  • julikana kwa watu wengi k.v. habari, mtu n.k.
  • toa sauti nzito k.v. simba,.upepo mkali,.ngoma n.k.

 

Afya

  • hali nzuri ya mwili/siha

Avya

  • toa mamba
  • tumia ovyoovyo mali, pesa, n.k.

 

Fito

  • vipande vya miti au chuma vya kujengea nyumba

Vito

  • mawe ya thamani

 

 

Fuja

  • tumia vibaya
  • haribu mali, nguo ,chakula n.k.

Vuja

  • pita kwa kitu mahali penye upenyo
  • Gunia hili linavuja.

Vunja

  • fanya kitu kigumu kuwa vipande vipande
  • badilisha pesa ziwe ndogondogo
  • enda kinyume na kanuni k.m vunja sheria

 

Futa

  • pangusa
  • chomoa kisu
  • toa maji nje ya chombo/fua maji

Vuta

  • fanya kufuata/burura
  • ingiza hewa au moshi mapafuni

 

Wafu

  • waliokufa

Wavu

  • utando wa nyuzi wa kufulia samaki,kutegea wanyama,kuweka golini/kimiani n.k

CH/SH

Chaka

  • mahali penye miti iliyosongamana
  • msimu wa kaskasi/joto na ukavu wa ardhi

Shaka

  • wasiwasi
  • tuhumuma

 

Chali

  • lala mgongo juu kichwa chini
  • mtu anayechekesha watu kwa kuwatolea mkasa

Shali

  • kitambaa cha begani cha shehe

Shari

  • balaa (pata shari)


Chati

  • mchoro unaotoa maelezo Fulani

Shati

  • vazi la juu la mwili lenye mikono

Sharti

  • lazima

 

Choka

  • pungukiwa na nguvu baada ya kufanya jambo kwa muda mrefu

Shoka

  • kifaa cha kukatia na kupasulia miti

 

Chombo

  • ala ya kufanyia kazi

Shombo

  • harufu mbaya ya samaki

 

Chokoa

  • tia kitu chenye ncha kwenye tundu au shimo ili kutoa kitu k.m chokoa meno

Shokoa

  • kazi ya kulazimishwa (fanyishwa shokoa)
  • shamba lililolimwa na kuachwa kumea nyasi

 

 

 

TH /DH

Thamini

  • tia maanani, heshimu

Dhamini

  • toa pesa maakamani ili mshtakiwa asitiwe korokoroni

 

Thamani

  • kima

Dhamana

  • malipo ya kortini

 

Thibiti

  • kuwa ya kweli/kuaminika
    - Habari imethibitishwa.

Dhibiti

  • tia mkononi
    - Nikidhibiti pesa zangu kutoka kwake nitanunua baiskeli.
  • weka chini ya mamlaka

 

Ridhi

  • kubali
  • pendezwa na jambo

Rithi

  • miliki kitu kutoka kwa mtu aliyekufa ama uliye na uhusiano naye
  • pata jambo au ujuzi kutoka kwa mtu mwingine

A/H

Apa

  • tamka jina aghalabu la Mungu kuthibitisha jambo Fulani

Hapa

  • mahali karibu

 

Ama

  • au

Hama

  • toka mahali fulani ili kwenda mahali pengine kuishi (gura)

 

Adimu

  • a shida kupatikana,nadra

Hadimu

  • mtumishi (mahadimu)

 

Ajali

  • jambo la madhara au hatari

Hajali

  • kinyume cha jali

 

Auni

  • saidia

Launi

  • rangi

L/R

Lahani

  • tuni

Rahani

  • chumba maalum katika nyumba au chombo cha kuwekea vitu

 

Lea

  • tunza mtoto

Rea

  • ghadhibika

Lemba

  • nyanganya kwa hila,punja

Remba

  • pamba, rembesha

 

Fahali

  • ng`ombe dume

Fahari

  • a kujivuniwa kwa watu

 

Mahali

  • sehemu ambapo mtu au kitu huweza kukaa

Mahari

  • mali au fedha inayotolewa na mwanamme kupewa wazazi wa mwanamke anayetaka kumuoa

S/SH

Saba

  • namba inayoonyesha idadi

Shaba

  • madini yenye rangi ya manjano

 

Saka

  • tafuta,winda

Shaka

  • wasiwasi
  • tuhuma
  • kutokuwa na hakika

 

Suka

  • tikisa kitu
  • pitisha kitu kama nywele baina ya zenyewe kupata mfumo fulani

Shuka

  • enda chini kutoka juu ya kitu
  • kitambaa cha kujifunga kiunoni

 

Soga

  • mazungumzo ya kupitisha wakati

Shoga

  • jina waitanalo wanawake marafiki
  • msenge

 

Sababu

  • kinachofanya jambo kutokea,chanzo

Shababu

  • kijana

J/NJ

Jaa

  • tosha
  • tapakaa kila mahali
  • mahali pa kutupia taka

Njaa

  • hali ya tumbo kutaka kupata chakula
  • ukosefu mkubwa wa chakula

 

Chema

  • kizuri

Jema

  • zuri

Njema

  • nzuri

 

 

Jia

  • sogelea karibu

Njia

  • barabara
  • namna au jinsi ya kufanya jambo

 

Jozi

  • vitu viwili vinavyofanana vilivyo pamoja

Njozi

  • maono yatokeayo usingizini;ruia

 

Jana

  • siku kabla ya leo,mwaka kabla ya huu
  • buu la nyuki-kama kiluwiwi cha nzi

Njana

  • samaki mwenye rangi nyekundu

D/ND

Dege

  • eropleni kubwa
  • ndege mkubwa
  • ugonjwa wa watoto unaosababishwa na homa kali

Ndege

  • mnyama aghalabu anayeruka kwa mabawa
  • eropleni inayosafiri angani
  • ndege mbaya/mzuri (bahati nzuri/mbaya)

 

Duni

  • kitu chenye thamani ya chini

Nduni

  • ajabu/lisilo la kawaida

 

 

B/MB

Basi

  • gari la abiria
  • kisha

Mbasi

  • rafiki

 

Buni

  • gundua
  • unda
  • tunga

Mbuni

  • ndege asiyeweza kuruka lakini huenda mbio sana
  • mkahawa au mti uzaao kahawa

 

Bali

  • lakini
  • sijali wala sibali (kusisitiza kutojali)

Mbali

  • si karibu
  • tofauti

Mbari

  • ukoo

 

Bega

  • sehemu ya mwili juu ya mkono na chini ya shingo

Mbega

  • nyani
  • manyoya ya ndege wanayojifunga wachezaji ngoma (jifunga mbega)

 

Iba

  • chukua kitu cha mtu mwingine bila ruhusa

Imba

  • tamka maneno kwa sauti ya mziki

G/NG

Gawa

  • tenga katika sehemu mbalimbali
  • aina ya ndege wa usiku;kirukanjia

Ngawa

  • mnyama afananaye na paka

 

Guu

  • mguu mkubwa sana

Nguu

  • kilele cha mlima
  • nguru aina ya samaki

 

Goma

  • kataa kufanya jambo mpaka masharti fulani yatimizwe
  • ngoma kubwa sana
  • duwi (aina ya samaki)

Ngoma

  • ala ya mziki inayotengenezwa kwa kuwambwa ngozi kwenye mzinga (piga ngoma)
  • mchezo wa kufuata mdundo wa ngoma (cheza ngoma)

Koma

  • alama ya kituo
  • acha kufanya jambo

P/B

Pata

  • kuwa na jambo, hali au kitu
  • kuwa kali
    - Kinolewacho hupata.

Bata

  • ndege mwenye vidole vilivyotandwa aghalabu akaaye majini

 

Papa

  • samaki mkubwa

Baba

  • mzazi wa kiume

 

Pana

  • kinyume cha –embamba

Bana

  • finya

 

Bango

  • uwazi ulio ardhini,mtini au jabalini

Bango

  • kipande cha karatasi ngumu kama kadi
  • bati linalozuia matope juu ya gurudumu la gari au baiskeli

 

Pacha

  • watoto wanaozaliwa kutokana na mamba moja

Bacha

  • tundu kwenye ukuta; shubaka(closet)

Paja

  • sehemu ya mguu kati ya goti na nyonga

 

Pania

  • kazana ili kufanya jambo lililokusudiwa

Bania

  • zuia kitu bila ya kutaka kukitumia (bania pesa)

 

Pima

  • tafuta urefu, uzito n.k.

Bima

  • mkataba na shirika wa kulipa pesa ili kupata fidia mtu anapofikwa na hasara

 

Punda

  • mnyama

Bunda

  • fungu la karatasi,noti,ngozi n.k

Panda

  • enda juu
  • kifaa cha kurushia vijiwe; manati
  • baragumu
  • tia mbegu ardhini ili zimee

Banda

  • jengo kubwa la kuwekea vitu au wanyama

 

Pasi

  • fuzu/faulu
  • hati inayomruhusu mtu kusafiri nje ya nchi/pasipoti
  • chombo cha kunyooshea nguo

Basi

  • gari kubwa la abiria

Mbasi

  • rafiki

T/D

Tamu

  • enye ladha ya kuridhisha mdomo

Damu

  • maji mekundu yanayozunguka mwilini
  • ukoo

 

Taka

  • kuwa na haja ya jambo fulani
  • uchafu

Daka

  • pokea kwa mikono kilichorushwa
  • tunda bichi (nazi daka/danga)

 

Tokeza

  • fanya kuonekana

Dokeza

  • toa habari za siri kwa uchache

 

Tai

  • ndege mkubwa mwenye makucha marefu alaye mizoga (vulture)
  • kitambaa kinachovaliwa kwenye ukosi wa shati

Dai

  • taka kupewa kilicho chako
  • habari inayosemwa na haijathibitishwa

K/G

Kamba

  • uzi mnene
  • samaki mdogo
  • mnyama wa baharini mwenye miguu mingi ambaye huliwa
  • kata kamba (kimbia)

Gamba

  • ngozi kama pembe ya kasa, samaki ,kasa au kobe(scales)

 

Konga

  • kuwa mzee
  • kusanya vitu au watu mahali pamoja (kongamano)
  • meza maji kidogo ili kupunguza kiu (konga roho)

Gonga

  • kutanisha kitu kimoja na kingine kwa kuvipiganisha

Koti

  • vazi zito livaliwalo juu ya nguo

Korti

  • mahakama

Goti

  • kiungo cha mguu kinachounganisha paja na muundi

 

Mfugo

  • mnyama anayefugwa nyumbani kwa ajili ya kuliwa au biashara

Mfuko

  • kitu cha kitambaa cha kutilia vitu

 

Tegua

  • fanya mtego usifanye kazi
  • ondoa chombo kama chungu mekoni
  • fanya kiungo cha mwili kifyatuke

Tekua

  • angusha kwa kusukuma
  • ng`oa kwa nguvu k.v. mmea

 

Mkuu

  • kiongozi
  • wenye hadhi kubwa

Mguu

  • kiungo cha binadamu au mnyama cha kusimamia au kutembelea

 

Oka

  • tia ndani ya tanuu kitu ili kiive au kikauke k.v unga uliokandwa au matofali

Oga

  • safisha mwili
  • enye hofu

Pika

  • weka kitu k.v. chakula sufuriani juu ya moto ili kiive

Piga

  • kutanisha vitu kwa nguvu
  • piga chafya, maji, hodi n.k.

 

Ukali

  • hali ya kutokuwa mpole
  • hali ya uchungu (ladha)

Ugali

  • chakula kinachopikwa kwa unga wa mahindi na kusongwa na maji moto hadi yakauke


Vitawe

  • Maneno yenye maana zaidi ya moja
  1. paa :
    • kwea (enda juu)
    • mnyama wa porini anayefanana na mbuzi
    • sehemu ya juu ya nyumba
  2. shinda :
    • kaa au ishi mahali/wakati fulani
    • ongoza katika shindano
    • tupu
  3. kaa :
    • sehemu yenye moto ya kuni
    • mnyama wa majini
    • keti chini
    • kuwa mahali fulani kwa muda
  4. mbuzi :
    • mnyama anayefugwa kama ng'ombe
    • chombo cha kukunia nazi
  5. mlango :
    • ukoo au watu wenye asili moja
    • sehemu ya kuingia kwenye nyumba
    • kitu kinachotumika kifunga nyumba
  6. fua :
    • unda vyombo/vifaa mbalimbali kwa kupiga chuma
    • osha nguo
  7. vua :
    • toa nguo kutoka mwilini
    • toa samaki kwenye maji
  8. kiboko :
    • mnyama mkubwa wa baharini
    • silaha inayotumika kwa kuchapa au kupiga
  9. tembo :
    •  aina ya ndovu
    • aina ya pombe


Visawe

  • Maneno tofauti yenye maana sawa.
    1. msichana au banati : kijana wa jinsia ya kike
    2. mvulana au ghulamu : kijana wa jinsia ya kiume
    3. huzuni au majonzi : hali ya kilio na huruma
    4. mazishi au matanga : shughuli za kumzika marehemu
    5. wakati au mwia : wakati au muda
    6. mtu au mja : mnyama atembeaye kwa miguu miwili mwenye uwezo wa kuongea na kufikiri kimantiki
    7. barua au waraka : kartasi inayoandikwa na kutumwa ili kuwasilisha ujumbe fulani
    8. siri au faragha : jambo lisilopaswa kujulikana na mtu mwengine
    9. macho au maninga : sehemu za mwili zinazotumika kuangalia na kuona
    10. mwangaza au nuru : miyale inayowezesha watu kuona vitu
    11. Mungu au Mola au Rabana au Jalali au Rabuka : Majina ya Mwenyezi Mungu
Join our whatsapp group for latest updates

Download Vitate, Vitawe na Visawe - Sarufi na Matumizi ya Lugha Kiswahili Notes.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest