Tumbo Lisiloshiba Dondoo Questions and Answers
Maswali haya hujitokeza kwa namna ya maneno yaliyodondolewa kutoka kwenye kazi ya Fasihi. Dondoo hunukuliwa kisha maswali yanayohusiana na dondoo hilo huulizwa. Dondoo laweza kuwa maneno ya mhusika mmoja ambaye hatatajwa au maelezo katika kazi. Maswali huenda yakarejelea matukio yaliyotokea kabla au baada ya dondoo. Katika kulijibu swali la muktadha wa dondoo, mtahiniwa huhitajika kuangazia mambo yafuatayo;
- Kumtaja msemaji wa maneno haya
- Kumtaja msemewa(anayerejelewa)
- Kueleza mahali yalikofanyika mazungumzo haya.
- Kueleza kiinisababu ya mazungumzo haya kutokea.
Swali la dondoo 1
“… Ningeondoka…..mapema niende niibe au niue ili niwe mtu wa maana”
- Eleza muktadha wa maneno haya. (Alama 4)
- Onyesha vile Kinaya kinavyojitokeza katika dondoo hili (Alama 2)
- Kinaya kimetumika kwingine katika hadithi husika. Thibitisha kwa kutumia hoja tisa. (Alama 9)
- Eleza umuhimu wa msemaji katika hadithi hii. (alama.5)
Majibu ya dondoo 1
-
- Haya ni maneno ya Jairo.
- Anahutubu katika sherehe ya kumuaga mwalimu Mosi ambaye alikuwa anastaafu kutoka kazi ya ualimu.
- Sherehe hii ilifanyika shuleni.
- Jairo anamkosoa mwalimu Mosi kumpatia atumaini ya uongo masomoni ilhali alijua hawakuwa na uwezo wa kimasomo badala ya kumruhusu aende ajaribu mbinu nyingine ya kujikimu kimaisha ili awe mtu wa maana katika jamii
- Jairo anamkosoa mwalimu kwa kumfunza na kumpa atumaini maishani badala ya kumwachilia mapema aende akaibe na kuua. Jairo analodokeza hapa ni kuwa ili mtu awe wa maana ni lazima aibe na aue.
-
- Ni kinaya kwa Jairo kudai ili mtu awe wa maana, athaminiwe na kuitwa mheshimiwa na kuwa bingwa lazima aibe, apore au aue.
- Ni kinaya kwa Jairo kuuona uelekezi na ushauri wa mwalimu wake kama upotoshi na upotezaji wa muda. Jairo anadai alipotezewa muda kwa kupatiwa matumaini ya uongo.
- Ni kinaya pia kwa mwalimu Mosi kutaka ahutubie mtu ambaye atamkosa badala ya kumsifu.
- Ni kinaya kwa Jairo kumtoa bintiye na mkewe kama zawadi kwa mwalimu wake kama shukrani ya zawadi anazompa. Ni kinaya kwa mtu kubadili mkewe kama zawadi.
- Ni kinaya kwa Jairo kudai kuwa pombe ni kiiwazo cha kimawazo kinachomsahaulisha masibu ya maisha ya kumkosoa mwalimu wake kwa kumwonya dhidi ya matumizi ya pombe.
- Ni kinaya kwa mkewe Jairo kukubali kitendo cha mumewe Jairo kumtoa kama zawadi kwa familia nyingine. Anakubali kubadilishwa na mali.
- Ni kinaya kwa Jairo kudai kuwa afuska ndio raha ya maisha na kuwa uaadilifu haufai. Anadai kuwa maisha ni bora bila nasaha za mwalimu.
- Ni kinaya kwa mkewe mwalimu Mosi,Sera kukubali na kumkaribisha mwanamke mwingine na watoto wake kwenye familia yake. (Hoja Zozote 9 Alama 9)
-
- Ni kielelezo cha utovu wa nidhamu miongoni wa wanafunzi. Anakunywa pombe na hata kujihusisha katika ufuska
- Kupitia kwake uwajibikaji wa mwalimu Mosi unajitokeza. Kama mwalimu alimkanya kunywa pombe na hata ufuska
- Ametumiwa kudhihirisha ukweli wa methali “asante ya punda ni mateke.”
Swali la dondoo 2
Shibe inatumaliza : Salma Omar Hamad
“Hiyo ni dharau ndugu yangu. Kwa nini kila siku tunakula sisi kwa niaba ya wengine ?”
- Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
- Eleza sifa za msemaji. (alama 6)
- Eleza jinsi viongozi wanavyokuwa wabadhirifu. (alama 10)
Majibu ya dondoo 2
-
- Maneno haya yanasemwa na Mbura
- alikuwa anazungumza na Sasa
- walikuwa kwenye sherehe iliyoandaliwa na mzee Mambo
- walikuwa wanazungumza kuhusu ‘kula kwao’ 4 x 1 = 4
- Sifa za Mbura
- ni mzalendo - anafanya kazi kwa bidii katika wizara yake kama njia ya kuonyesha uzalendo
- mwenye tamaa - anajaza sahani kwa chakula na kukila chote
- mwenye utu - anataka wananchi wale kwa niaba ya viongozi kama vile wao wamekuwa wakila kwa niaba yao
- ni fisadi - amepokea kazi kwa afisi ya serikali kwa njia isiyo halali
- mzembe - baada ya kula sahani tatu za vyakula kwenye sherehe analala usingizi mzito badala ya kwenda kazini
- mtetezi wa haki
- mvumilivu
- mpyoro
- msema kweli zozote 6 x 1 = 6
-
- hulipwa mishahara mikubwa sana na serikali jambo linalochangia ubadhirifu wa mali ya umma
- sherehe kubwa za viongozi wa kiserikali huchangia pakubwa ubadhirifu
- viongozi hutumia raslimali za nchi kwa manufaa yao ya kibinafsi
- magari ya serikali
- raslimali zilizotumiwa katika kuvinunua vyakula na vinywaji vingetumika katika kuendeleza asasi tofauti za kijamii
- DJ na wenzake wanapata mabilioni ya fedha kutokana na kuwatumbuiza wageni katikasherehe kama hizi
- viongozi wanawachukua baadhi ya watu wao wa karibu na kufanya juu chini kuona kwamba wanajifaidi na mali na raslimali za wananchi pasipo kuzitolea jasho kamwe
- upeperushaji wa matangazo katika vyombo vya habari ya sherehe za kiongozi binafsi ni njia ya kuendeleza ubadhirifu wa raslimali za umma
- Mbura na Sasa wanaendeleza ubadhirifu pale wanapoamua kuchukua vyakula kupita kiasi katika sherehe za mzee Mambo
- kuwaajiri viongozi wawili wenye nyadhifa sawa katika sekta tofauti za umma
- vibaraka na vikaragosi kupewa mali ambayo ingewafaidi wananchi zozote 10 x 1 = 10
Swali la dondoo 3

Ndoto ya mashaka
“Sasa nimechoka mja. Nimechoka hata naradua kufa kuliko kuishi.”
- Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
- Taja mbinu mbili za lugha katika dondoo hili. (alama 4)
- Mzungumzaji alikuwa na haki ya kuradua kufa. Thibitisha. (alama 12)
Majibu ya dondoo 3
-
- Haya ni mawazo ya Mashaka.
- Yuko chumbani mwake.
- Anakumbuka hali yake ngumu ya maisha na mashaka tele.
- Anamkumbuke mkewe, Waridi, alivyomtoroka na wanawe.
- Anayaona maisha kutokuwa na thamani tena kiasi kwamba anaona kifo kingemfaa. (4×1= 4)
-
- Takriri- nimechoka
- Uzungumzi nafsi- sasa nimechoka… (2×2= 4)
- Mashaka alikuwa na haki ya kuradua kufa kwani alikuwa amepitia matizo mengi:
- Mamake mzazi, Ma Mtumwa, aliiaga dunia punde tu baada ya kumkopoa.
- Baada ya kifo cha mamake, babake alishindwa kuvumilia naye akaaga dunia.
- Mashaka alilelewa na Biti Kidebe asiyekuwa mamake mzazi.
- Mamake mlezi, Biti Kidebe naye alihitaji kulelewa. Daima alilalamikia miguu yake.
- Mashaka alilazimika kufanya vijikazi ili kumsaidia mamake mlezi kupata chohcote cha kutumia.
- Mashaka na Biti Kidebe walipanda mabokoboko ambayo wengi waliamini si ndizi.
- Biti Kideba alienda jongomeo pindi tu Mashaka alipomaliza chumba cha nane.
- Mzee Rubeya na Shehe Mwinyimvua wanawafungisha Mashaka na Waridi Ndoa ya Mkeka bila kupenda kwao.
- Mzee Rubeya wanawakimbia Mashaka na Waridi na kurudi kwao Yemeni ili Mashaka wasije kuwaaibisha.
- Kazi ya Mashaka ilikuwa ya kijungu meko- ya kupigania tumbo.
- Mashaka na Waridi waliishi sehemu kuchafu kule Tandale, Kwatumbo, eneo la Uswahilini.
- Walikosa vyoo wakawa wanatumia karatasi kwa haja zao zote.
- Mashaka na Waridi walipata watoto wengi, saba, ambao wanawashinda kuwakimu.
- Mashaka alilazimika kuomba jikoni kwa jirana yake, Chakupewa, ili wanawe wa kiume wapate mahali pa kulala.
- Chumba chao kiliingiza maji mvua iliponyesha.
- Mashaka alifanya kazi ya usiku katika Shirika la Zuia Wizi Security (ZWS).
- Waridi anamtoroka Mashaka maisha yanapokuwa magumu. (12×1= 12)
Kila hoja ifafanuliwe kikamilifu
Swali la dondoo 4
Mame Bakari
“Una nini? Umeshtuka mwanangu! Unaogopa? Uaogopa nini?
- Weka dondoo hili katika muktadha wake. al 4
- Eleza sifa za mrejelewa. al 6
- Tambua mbinu mbili za lugha zilizotumika katika dondoo. al 2
- Eleza umuhimu wa msemaji. al 4
- Tambua maudhui yanayojitokeza katika kifungu hiki. al 1
- Fafanua maudhui katika swali la (e) kwa kurejelea hadithi nzima. al 3
Majibu ya dondoo 4
-
- Msemaji ni babake Sara.
- Akimwambia Sara.
- Wakiwa hospitalini kwenye chumba cha daktari.
- Sara alikuwa ameenda kufanyiwa vipimo vya ujauzito na Beluwa alipowakuta wazaziwe wakisubiri katika chumba hicho
- sifa za mrejelewa.(Sara)
- mpenda masomo
- ni mwoga
- mwenye busara
- mwenye mapenzi ya dhati
- mwenye utu hakutaka kuavya mimba
- ni msiri
- mwenye maadili
- mwenye majuto
- ni mvumilivu.
(kila sifa itolewe maelezo. Mwanafunzi akitaja sifa tu asituzwe)
Hoja Zozote 6 (6x 1 = 6)
-
- Swali la balagha; una nini?
- Takriri; unaogopa, unaogopa
- umuhimu wa msemaji (babake Sara)
- Kupitia kwake tunapata habari ya ukali kupita kiasi kwa wazazi kwa wanao.
- Ni kielelezo cha wazazi ambao hawako tayari kubadili msimamo wao mkali kwa watoto wao.
- Anaonyesha umuhimu wa wazazi kushirikiana katika malezi.
- Anaonyesha umuhimu wa kuweka siri katika masuala tata ya familia.
- Ni kielelezo cha wazazi wanaouenzi utamaduni wa jamii yao.
-
- Malezi
- mapenzi
-
- Malezi- Babake Sara anakuwa mkali kwa sara. Babake Sara anadalika na kumwonyesha mapenzi.
- Mapenzi - Kuna mapenzi ya dhati kati ya sarana salime. Salime anamsaidia sara anapokuwa mjamzito. Salime aidha anamsaidia sara kuweka siri ya ujauzito.
Swali la dondoo 5
“Tulipokutana Tena” (Alifa Chokocho)
Halikuwa jambo la kawaida maana maji yalikuwa hayapatikani karibu pale kijijini petu. Sharti mtu aende masafa marefu kuyatafuta. Na sabuni? Sabuni ilikuwa kitu cha anasa kwa familia yetu. Wazazi wangu hakuwa na uwezo wa kununua Sabuni. Labda mara moja moja siku za sikukuu.
- Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
- Eleza majukumu mawili ya takriri katika dondoo hili. (alama2)
- Kwa kurejelea hadithi Tulipokutana Tena jadili jinsi haki za watoto zinavyokiukwa.(alama 6)
- Jadili changamoto zinazokumba asasi ya ndoa ukirejelea hadithi zifuatazo: (alama 10)
- Masharti ya Kisasa
- Ndoto ya Mashaka
Majibu ya dondoo 5
-
- Maneno haya ni ya Bogoa.
- Anawambia msimulizi na Kazu.
- Wako katika club Pogopogo.
- Bogoa na msimulizi wanakutana baabaya miaka 41 baada ya kutoroka kwasababu ya kuwa mtumwa wa nyumbani kwa Bi. Sinai.
-
- Imetumika kuchimuza hali ya umasikini kwani hata sabuni hawangeweza kununua.
- Imetumika kuendeleza maudhui ya umasikini
- Imetumika kusisitiza wazo. Mfano kutokuwa na uwezo wa kununua sabuni isipokuwa siku ya sikukuu.
- Imetumika kuendeleza tamathali nyingine za semi mfano chuku. Kuthamini sabuni sana na hata kutokuwa na uwezo wa kununua sabuni.
-
- Kutengwa na familia- Bogoa alikuwa na umri mdogo wa miaka mitano na hakuta kakutengwa na baba,mama, ndugu, kaka na dada zake. Uk 114
- Kuamrishwa kufanya vitu bila hiari ya Bogo uk. 115
- Bogoa alitwishwa mambo yote ya nyumbani alikuwa mtoto mdogo. Uk 115
- Watoto masikini hawapaswi kusoma shuleni. Uk 116
- Bogoa hakuwa na uhuru wakucheza na watoto wa Bi. Sinai.
- Kutishiwa maisha- Bi. Sinai alimtisha Bogua kuwa angemkata ulimi kama angesema chochote kuhusu maisha yake ya ndani.
- Kuadhibiwa kwa kuchomwa- Bi. Sinai alimchoma viganja Bogoa kwa kosa la kuchoma maandazi.
- Kutoambiwa ukweli- Bogoa anawalaumu wazazi wake kwa kumdanganya Alama 6×1=6
Masharti ya Kisasa
- Masharti katika ndoa
- Ukosefu wa uaminifu
- uhuru
- Taasubi ya kiume/ utamaduni
- Wivu
- Utabaka
- Ukengeushi
Ndoto ya Mashaka
- Ndoa ya lazima
- Utabaka
- Umaskini
- Upangaji wa uzazi
- Usaliti
Swali la dondoo 6
`..........Lakini shogake................. shogake.................. shogake dada nikamwona ana ndevu’.
- Eleza muktadha wa dondoo hili. alama 4
- Bainisha sifa tatu za `shoga ‘ anayezungumziwa katika dondoo hili. alama 6
- Jadili umuhimu wa `dada’ anayerejelewa katika kuendeleza dhamira ya hadithi. alama 10
Majibu ya dondoo 6
-
- Haya ni maneno ya lulua
- Anamwambia mamake Bi. Hamida
- Wamo nyumbani mwao wakila chomcha.
- Lulua anamweleza jinsi alivyoingia katika chumba cha safia na kumkuta akiwa amelala kitandani na kimwana. (4x1=4)
-
- Msiri- Wazazi wake safia hawakuwahi kuiona sura yake kwa sababu alipenda kuvaa buibui ili asijulikane kuwa ni mwanamume.
- Mzinifu- Anazini na safia na kumpachika mimba
- Mjanja – Anajifunika buibui na kujifanya jinsi ya kike
- Dada anayerejerewa ni safia
- Ni kiwakilishi cha uoza katika jamii. Anawahada wazazi wake kuwa kimwona ni shogake kumbe ni mpenziwe na kiume.
- Ametumiwa kukosoa malezi ya wazazi. Wazazi wake Bwana Masudi na Bi Hamida walimwamini sana hadi wakawa wanamsifu tu badala ya kungumza naye ili kumpa mwelekeo ufaao maishaini.
- Kuendeleza maudhui ya elimu. Alikuwa mwerevu shuleni. Kila mtihani aliofanya aliongoza katika darasa lao.
- Ni kielelezo cha wanawake wanaoavya mimba kuuficha uovu huo. Safai anajaribu kuavya mimba ili wazazi wake wasijue lakini anakufa.
- Suala la unafiki linajitokeza kupitia kwake. Alijifanya mzuri kwa zazazi wake hhadi wakamwamini kwa kila jambo kumbe alikuwa mwovu- anawahadaa wazaziwe kuwa kimwana ni shogaye ilhali ni mpenziwe wa kiume.
- Ni kielezo cha athari za mapenzi kabla ya ndoa. Anafanya mapenzi na kimwana.Anapachikwa mimba na kwa sababu ya kuhofia matokeo yake anaamua kuiavya ile iwe siri lakini anakufa. ( 2x5=10) Taja = 1, Kueleza = 1, Jumla = 2
Swali la dondoo 7
Ndoto ya Mashaka
"...dunia imenikunjulia mikono kunifariji baada ya kunicharaza fimbo yake aushi yangu yote."
- Eleza muktadha wa dondoo hili (al.4)
- Tambua na ueleze mbinu ya lugha iliyotumiwa katika dondoo.(al.2)
- Eleza jinsi dunia ilimcharaza fimbo msemaji kwa kutolea hoja kumi na nne. (al.14)
Majibu ya dondoo 7
