Tumbo Lisiloshiba Insha Questions and Answers
Maswali ya Insha
Haya ni maswali ambayo hutoa kauli inayohitaji kujibiwa kwa kirefu na kwa kina. Swali linaweza kuwa la jumla yaani linalohusu Hadithi nzima. Pia, swali laweza kulenga sehemu ya kazi husika katika nyanja na maudhui, wahusika na hulka zao, mafunzo na fani. Maswali haya huhitaji zaidi uwezo wa kukumbuka wa mtu, kupanga hoja na kuelezea msimamo au maoni yake kuhusiana nayo. Mtahiniwa anahitajika kutoa hoja na kuziteteta kwa mifano dhabiti. Mtahiniwa asitumie vistari vistari, afafanue hoja kikamilifu akiandamisha mifano mingi kutoka kwa Hadithi.
Swali la Insha 1
- Eleza namna maudhui ya ndoa yalivyosawiriwa katika hadithi ya Masharti ya Kisasa (alama 13)
- Kwa kurejelea hadithi ya Shibe inatumaliza,eleza namna maudhui ya ufisadi yanavyojitokeza (alama 7)
Eleza namna maudhui ya ndoa yalivyosawiriwa katika hadithi ya Masharti ya Kisasa (alama 13)
- Mwanaume humposa wanamke. Dadi alienda nyumbani kwa Kidawa kumposa
- Mwanamke ndiye huamua wakati wa kuolewa na nani wa kumwoa. Kidawa alimchagua Dadi baada ya muda refu
- Ndoa huandamana na masharti. Dadi alipewa masharti na Kidawa ili akubali kuolewa naye.
- Wanandoa hufanya kazi pamoja ili kukithi mahitaji ya nyumbani. Dadi anachunza samaki na kidawa ni metroni
- Wanaume hawafurahi wake wao wanapotangamana na wanaume wengine. Kidawa anaposimama kuongea na wanaume,Dadi anadhika sana.
- Wanandoa husaidia kazi za nyumbani, Dadi anasaidia kidawa kazi za nyumbani kama vile kuosha vyombo na kufagia.
- Wanandoa wanapanga uzazi,Dadi na Kidawa wanapanga kuwa na mtoto mmoja pekee
- Mwanamke anaajiriwa. Kidawa aliajiriwa shuleni kama metroni.
- Mwanamke anajinunulia nguo na fashoni nyingine. Kidawa ananunua viatu na kanzu anayaovalia kwenda kazini.
- Ndoa imekosa uaminifu. Dadi anashuku kuwa Kidawa ana mapenzi na mwalimu mkuu.
- Kiwango cha elimu si kikwazo katika ndoa. Kidawa anaolewa na Dadi licha ya kuwa ana kisomo cha juu kuliko Dadi.
- Mwanamke amekengeuka. Kidawa anapenda fashoni
- Wote wawili. Mwanamke na mwanaume wanachangizana nyumbani
- Kuna makubaliano ya kufanya mambo kwa pamoja (13x1=13)
Kwa kurejelea hadithi ya Shibe inatumaliza,eleza namna maudhui ya ufisadi yanavyojitokeza (alama 7)
- Mzee Mambo hafanyi kazi wizarani ilhali analipwa mshahara mkubwa kuliko Sasa na Mbura wanaofanya kazi wizarani
- Mambo anatumia runinga ya taifa inayofaa kuufahamisha umma masuala yataifa lao kwa maslahi yake. Anaitumia kupeperusha sherehe inauofahamika nyumbani kwao.
- Mambo anaifilisi serikali kwa kutumia pesa za serikali kugharamia sherehe zake binafsi. DJ na wenzake wanalipwa mabilioni ya pesa za serikali kwa kusimamia sherehe hii.
- DJ anaipunja serikali kwa kutumia mtaji wa bohari kuu ya dawa za serikali kufungua duka lake la dawa.
- Dj anaifilisi serikali kwa kupokea huduma za maji,umeme na matibabu bure ilhali wananchi maskini wanazilipia.
- Wafanyakazi wa umma wanaibia serikali saa za kazi. Sasa na Mbura wanahudhuria shere zilizofanyika kwa Mambo siku nzima ilhali walipaswa kuwa kazini.
- Mzee Mambo anatumia magari ya serikali kwa maslahi yake binafsi. Kwa mfano, anayatumia kusomba maji, chakula, kuwaleta jamaa wa Mambo shereheni na mapambo. (7x1=7)
Swali la Insha 2
Ukirejelea hadithi zifuatazo, eleza jinsi maudhui ya mapenzi na asasi ya ndoa yanavyojitokeza. (alama 20)
- Mapenzi ya kifaurongo
- Masharti ya kisasa
- Ndoto ya Mashaka
- Mtihani wa maisha
Mapenzi ya kifaurongo
- Ndoa iliyotarajiwa ya Dennis na Penina ilitawaliwa na unafiki. Penina anamjia Dennis na wazo la kuwa wapenzi bila kuzingatia hali duni ya familia yake. Dennis anapokosa ajira anamfukuza
- Inatawaliwa na kuhimiliana
- Imetawaliwa na kukata tamaa - Penina anakata tamaa baada ya Dennis kukosa kazi
- Imezingirwa na utabaka wa kiasili
- Mapenzi hukua, huugua na hufa 5 x 1 = 5
Masharti ya kisasa
- Ndoa ya Dadi na Kidawa
- Ndoa inayodhibitiwa na masharti
- Ndoa ya kugawana majukumu
- Ndoa ya kupanga uzazi
- Ndoa inayoruhusu mwanamke kufanya kazi. Kidawa anafanya kazi ya umetroni usiku na kuuza bidhaa mtaani
- Baadhi ya watu huingilia ndoa za wenzao kama njia ya kuona mapenzi yamevunjika baina ya wanandoa husika 5 x 1 = 5
Mtihani wa maisha
- wazazi wa Samueli ni wenye mapenzi wanaonyesha mapenzi kwa mtoto huyu wao kwa kumpeleka shuleni akajipatie elimu
- Samuel anaonyesha mapenzi kwa Nina. Kwa muda amekuwa mpenziwe
- Nina anaamini kuwa mwanaume huyu ni bingwa kutokana na kudanganywa alikodanganywa na mwanaume huyu
- mamake Samueli ana mapenzi ya dhati kwake, baada ya Samuel kujaribu kujitoa uhai mamake anamsihi waende nyumbani “Twende zetu nyumbani mwanangu.” zozote 4 x 1 = 4
Ndoto ya Mashaka

- Kuna ndoa ya Mashaka na Waridi
- Kuna ndoa ya mtumwa na mumewe mzee Rubeya
- Tatizo la kwanza ni ndoa ya kulazimishwa. Mashaka na Waridi walitoka kwenye matabaka mawili tofauti
- Waridi - tabaka la kitajiri
- Mashaka - tabaka la maskini
- Kuna kutohusisha wanawake katika ndoa. Mamake Waridi hakuhusishwa katika harusi
- Ndoa inakumbwa na tatizo la malazi bora - upendo, kujikubali, ukosefu wa taasubi ya kiume
- Kuna changamoto zinazojitokeza baada ya kifo cha mmoja. Mashaka anawachwa yatima
- Kuna utengano katika ndoa. Waridi anatengana na mumewe kutokana na hali ngumu ya kiuchumi
Swali la Insha 3
- Eleza ufaafu wa anwani mapenzi ya kifuaurongo kwa kurejelea mhusika Penina. Al.10
- Eleza nafasi ya elimu katika maisha ya wanajamii ukirejelea hadithi: Mtihani wa maisha.
Eleza ufaafu wa anwani mapenzi ya kifuaurongo kwa kurejelea mhusika Penina. Al.10
Kifaurongo ni mmea wenye sifa ya kujifisha mara unapoguswa. Mwandishi akejeli mahusiano yaliyojengwa katika msingi wa unafiki.
- Penina anajifanya kumjali Dennis katika hali yake ya kunywa uji na kuonyesha huzuni. Anamtia Dennis mshawasha wa mapenzi ila si mapenzi kamili.
- Msimulizi anadai wavulana wengi wameangamia katika utandabui wa mapenzi baada ya kufanyiwa makuruhu na wasichana wenye tabia ya kifaurongo.
- Penina anadai atakuwa na Dennis kwa mazuri na mabaya lakini alimwacha alipokosa ajira.
- Penina asema kuwa hafanyi mzaha na kuwa hawezi kumchagua mpenzi kwa msingi wowote kama si mapenzi. Mwishowe alivunja ndoa yake kwa sababu Dennis alikuwa fukara. Hii ni tabia ya kifaurongo.
- Penina hataki kuitwa mpenzi wa Dennis na amtaka atafute msichana wa kufu yake akidai mgomba changaraweni haupandwi ukamea.
- Penina amfukuza Dennis nyumbani alipokosa kazi ilhali alikuwa ameapa hangemsaliti kwa vyovyote vile. Hoja 5 x 2 = 10
Eleza nafasi ya elimu katika maisha ya wanajamii ukirejelea hadithi: Mtihani wa maisha.
- Wanafunzi wanatarajiwa kufanya mtihani wa kidato cha nne ili kubaini hatima yao. Samueli awaza kuwa matokeao ya mthihani yangekuwa daraja ya ufanisi.
- Elimu ina daraja/viwango – Samueli anatarajia kuingia chuo kikuu anapokamilisha kidato cha nne.
- Katika masomo kuna kufeli.
- Wanafunzi wanahofia matokeo ya mtihani wa kidato cha nne k.m Samueli.
- Wanafunzi wanaojiamini kupindukia huathiriwa kisaikolojia wanapofeli.
- Wanakunzi lazima watimize matakwa Fulani kabla ya kupatiwa matokeo yao.
- Wanafunzi wengine wanaonea aibu matokeo yao.
- Jinsia ya kike inapiku jinsia ya kiume masomoni k.m Dada zake Samueli.
- Jinsia ya kike inabaguliwa masomoni. Babake Samueli ameweka matumaini yake kwa Samueli.
- Watoto wanatarajiwa kupita mtihani wanusuru familia zao.
- Wanafunzi wanaichukulia elimul na masomo kwa mzaha na kejeli.
- Samueli aliona shule kama jela. 10 x 1 = 10
Swali la Insha 4
Safari ya elimu ni kama ua la waridi ambalo licha ya upendezaji wake, huzingirwa na miiba. Jadili adha za safari hii kwa hoja tano tano kutoka kwa kila mojawapo wa hadithi fupi zifuatazo: Mapenzi ya Kifaurongo, Mame Bakari, Mwalimu Mstaafu na Mtihani wa Maisha.
Tanbihi: swali hili linamhitaji mtahiniwa kuonyesha changamoto zinazoikumba elimu.
Mapenzi ya Kifaurongo
- Ugumu wa kuelewa mambo shuleni – Dennis Machora na wenzake wanapata kugumiwa na mambo wanayofunzwa katika mhadahara chuoni. Kauli za Daktari Mabonga hazieleweki upesi.
- Utabaka shuleni – Dennis mwenye jadi ya kimaskini anatatizwa na maisha chuoni anakojipata akitagusana na wenzake kutoka familia za kitajiri.
- Kejeli za walimu – Daktari Mabonga anawajekeli wanafunzi wake kwenye mhadhara kila wanapomwuliza maswali.
- Kuchekwa na wanafunzi wengine – Wanafunzi wanamcheka sana Dennis anapomwomba Daktari Mabonga kutumia lugha nyepesi katika mhadhara.
- Kutamauka shuleni – Dennis anakatizwa tamaa na masomo anapoyaona kama madubwana ambayo hakujua yalitoka wapi.
- Utashi /Umaskini huwakumba baadhi ya wanafunzi – Dennis anajipata na uhitaji wa vitu muhimu vikiwemo malazi bora, chakula n.k. Analazimika kulalia shuka zilizozeeka na kuchanikachanika na pia kunywa uji anapokosa chakula.
- Upweke/Ubaguzi shuleni – Wanafunzi wa familia za kitajiri huona haya hujinasibisha na wenzao wasio na chochote. Dennis anajipata katika upweke kutokana na hili.
- Anasa/ Mapenzi shuleni – Wanafunzi katika Chuo cha Kivukoni wanatumbukia kwenye anasa na masuala ya mapenzi , Dennis anawaona wenzake wakitembea huku wameshikana wawili wawili.
- Kukosa kazi baada ya kusoma – Dennis anatafuta kazi bila ya mafanikio licha ya kuhitimu na shahada ya uanahabari kutoka kutoka chuoni.
Mame Bakari
- Mimba za mapema kwa wasichana – Sara anajipata na ujauzito unaomtatiza kimawazo akiwa mwanafunzi.
- Kubakwa kwa wanafunzi wa kike – Sara anabakwa na janadume asilolijua majira ya saa tatu unusu akitoka ‘twisheni’.
- Kutengwa kwa wanafunzi wajawazito – Sara anawazia kutengwa na watu wote wa kando na wa karibu.
- Wanafunzi kukosa wa kuwasikiliza wanapopatwa na balaaa mishani - Sara anawaza jinsi ambavyo hakuna mtu ambaye angemwelewa baada ya kubakwa.
- Kufukuzwa shuleni kwa wasichana wajawazito/ kukatiziwa masomo – Sara anawazia jinsi ambavyo mwalimu mkuu angemfukuza kwa kusema shule ni ya wanafunzi sio wamama.
- Msongo wa mawazo/ Shinikizo za akilini – Sara anajiwa na wazo la kujitoa uhai, hata hivyo nalikomesha wazo hilo.
- Uavyaji mimba – Wanafunzi wa kike huweza kulazimika kuavya mimba ili wafiche hali zao. Wazo hili liliwahi kumjia Sara na akalitupilia mbali.
- Kuaibishwa – Sara anawazia ambavyo mwalimu mkuu angemwita mama hadharani.
Mwalimu Mstaafu
- Ubaguanaji kwa misingi wa wepesi wa kupata mambo darasani – Jairo alibaguliwa katika sherehe ya kustaafau kwa mwalimu Mosi kwa kuwa hakuwa hodari masomoni hivyo hakutajirika baada ya shule.
- Dhana potovu ya baadhi ya wanafunzi – Jairo alikuwa na dhana ya kwamba mwalimu Mosi kwa kuendelea kumpa matumaini shuleni alikuwa anamharibia wakati.
- Mtazamo hasi dhidi ya masomo – Jairo hakupenda masomo. Kwake waliosoma na kufanikiwa ni wakora.
- Baadhi ya wanafunzi huwa na uwezo wa chini wa kuelewa mambo darasani – Jairo alipata sufuri ambazo mwalimu Mosi alimpa matumaini kwamba zingepisha mia mia.
- Walimu kupata lawama kutokana na upungufu wa wanafunzi – Jairo anamlaumu Mwalimu Mosi kwa mapungufu yake shuleni.
- Baadhi ya wanafunzi huzipuuza nasaha za walimu – Jairo alipuuza kabisa ushauri alioupata kutoka kwa Mwalimu Mosi kuhusu kuepuka ufuska, ulevi n.k.
Mtihani wa Maisha
- Wasi wasi utokanao na matokeo ya mtihani – Samueli anajipata moyo ukimtuta anapokwenda kuyapokea matokeo ya mtihani wake wa kidato cha nne.
- Walimu kuwadunisha wanafunzi – Samueli anasema vile ambavyo Mwalimu mkuu hakuwahi kumwamini.
- Dharau kutoka kwa walimu – Mwalimu mkuu anamwonyesha dharau Samueli anapoingia ofisini kuyapokea matokeo yake. Anamtupia matokeo yake badala ya kumpa kwa njia nzuri.
- Wanafunzi kupumbazwa na sifa wanazopaliwa na wenzao – Samueli alipokuwa akisoma, alipumbazika na umaarufu kutoka kwa wanafunzi wengine akasahau kutia bidi. Wenzake walimtambua kama ‘rasta’ shuleni.
- Kuvunjwa moyo na matokeo duni ya mtihani – Samueli anavunjika moyo anapopata matokeo duni ya mtihani.
- Mapenzi ya mapema – Samueli anaingilia uhusiano wa kimapenzi na msichana kwa jina Nina.
- Udanganyifu wa wanafunzi kwa wazazi wao – Samueli anamdanganya babake kuwa hakupata matokeo ya mtihani kwa kuwa hakukamilisha kulipa karo.
- Baadhi ya wanafunzi huwakosea heshima walimu- Samueli anamrejelea mwalimu mkuu kama ‘hambe’.
- Wanafunzi kwenda mbali kupata elimu – Samueli alilazimika kusomea shule iliyokuwa mbali na nyumbani.
- Kusalitika kwa wazazi – Wazazi wa Samueli wanahisi kusalitika baada ya mtoto wao mvulana, waliyemtegemea sana kufeli mtihani wa kidato cha nne.
- Elimu ya msichana kutodhaminiwa sana – Babake Samueli aliona fahari kumwona mtoto wa kiume akifanikiwa, licha ya kuwa binti zake wawili Bilha na Mwajuma walifaulu katika mtihani ya sekondari na walikuwa vyuoni.
Tanbihi: Mwanafunzi anaweza kupendekeza hoja nje ya zilizotolewa kwenye mwongozo huu. Hivyo, mtahini atathmini hoja za mwanafunzi.
Hoja tano kutoka kwa kila hadithi ( 5 × 4 = 20)
Swali la Insha 5
``Wahusika katika hadithi shibe inatumaliza wanatumia uhuru wao vibaya.’’ Onyesha ukweli wa kauli hii kwa kutoa mifano. alama 20
- Mzee mambo anatumia uhuru wa cheo chake serikalini vibaya kwa kupokea misharaha kutoka wizara mbalimbali ilhali hafanyi kazi yoyote.
- Sasa na mbura wanatumia uhuru wao vibaya kwa kupanga na kupangilia wapi kwa kudoea badala ya kushiriki katika shughuli ya ujenzi wa jamii.
- Wananchi wa taifa la Mzee Mambo wanatumia uhuru wao vibaya kwa kuzingatia kirenda kazini bila kujali kama wanfanya kazi yoyote. Muhimu si kwenda/ kazini ila kufanya kazi.
- Mzee mambo anatumia uhuru wake vibaya kwa kutumia mali na wakati wa taifa kuandaa sehere zisizo na msingi wowote. Anaandaa sherehe kubwa kwa madai ya kusheherekea kuingizwa kwa mtoto wake ``nasari’’.
- Mambo anatumia magari ya serikali kuhudumu katika sherehe yake.
- Walaji katika sherehe ya kuingizwa kwa mtoto wa kwanza wa Mzee mambo nasari wanatumia uhuru wao wa kula vibaya kwa vile hawachunguzi kile wanachokula
- Vyombo vya habari vinatumia uhuru wao vibaya kwa kupeperusha sherehe ya kibinafsi moja kwa moja badala ya kumulika mambo yanayoathiri taifa.
- Dj na wengine wenye nafasi katika taifa wanatumia uhuru kupokea mabilioni ya pesa za serikali kutumbuiza katika sherehe za mtu binafsi.
- DJ na wenzake wanatumia uhuru wao kupata huduma za maji, umame, matibabu miongoni mwa huduma nyingine bila malipo huku wananchi wakalazimika kulipia huduma hizi kwa dhiki na ufukara.
- Sasa na mbura wanatumia uhuru wao wa kula kila kitu kibaya na kizuri, wanachokijua na wasichokijua,vyao na vya wenzao hata vya kuokotwa. Hili linawaweka katika hatari ya kupatwa na maradhi kama kisukari na saratani. Hoja ( 1x 2 = 2) ( 10 x 2= 20)
Swali la Insha 6
Kwa kurejelea hadithi ya Mapenzi ya Kifaurongo, Mame Bakari, Nizikeni Papa Hapa , Mtihani wa Maisha na Mkubwa, eleza changamoto zinazowakumba vijana. (al.20)
Mapenzi ya Kifaurongo.
- Ukosefu wa karo -wazazi wa Dennis kufanya kazi kwa majirani kudunduiza karo yake.
- Ukosefu wa hela za matunzo – Dennis hana cha kupika ila uji mweupe bila sukari.
- Mapenzi shuleni – wanafunzi wa Chuo kikuu cha Kivukoni wanahusiana kimapenzi.
- Masomo magumu – wanafunzi hawaelewi anayofunza Dkt. Mabonga.
Mame Bakari
- Ubakaji – Sara anabakwa na jana dume.
- Kuavya mimba – Sara anatupilia mbali wazo la kuavya.
- Kujitia kitanzi – Sara alilikataza wazo la hili likome hata kumpitikia.
- Kutengwa –Alijiona akitengwa na jamii kwa jumla.
Nizikeni Papa Hapa
- Mapenzi ya kiholela - Otii kuhusiana na Rehema bila kujali ushauri wa mwendani wake.
- Ukimwi – Otii anaugua gonjwa lenye dalili zote za UKIMWI.
- Kuumia kazini – Otii anaumia mguu akiichezea timu yake ya Bandari.
- Kutelekezwa na waajiri wao – anapoumia timu yake haikumjali wala kumfidia.
Mtihani wa Maisha
- Kutembea kwenda shule – Samueli anatembea kilomita sita kila siku kwenda shuleni.
- Ukosefu wa karo – babake Samueli analazimika kuuza ng`ombe ili kulipa karo.
- Mapenzi shuleni – Samueli anahusiana na Nina.
- Kufeli mtihani wa kitaifa – Samueli anafeli mtihani wake.
Mkubwa
- Umaskini- Mwavuli wa Mubwa umetoka mistari mitatu.
- Matumizi ya dawa za kulevya – vijana wengi vichochoroni anakopitia Mkubwa wanatumia dawa hizi.
- Ufisadi – wanafunzi wa profesa wanahongwa kumpigia Mkubwa kura.
- Kufungwa – vijana wanaotumiwa kulangua dawa na wanaozitumia wanapokamatwa hutiwa kizuizini.
Swali la Insha 7
- “Mame Bakari”
Kwa mujibu wa hadithi hii, ubahaimu anaotendewa mwanamke unakuwa na athari mbaya kwake. Onyesha kwa mifano mwafaka. (alama 10) - “Masharti ya Kisasa”
“…mapenzi ni mateso, ni utumwa, ni ukandamizaji, ni ushabiki usio na maana.”
Thibitisha ukweli wa kauli hii kama unavyojitokeza kwenye hadithi. (alama 10)
“Mame Bakari”
Kwa mujibu wa hadithi hii, ubahaimu anaotendewa mwanamke unakuwa na athari mbaya kwake. Onyesha kwa mifano mwafaka. (alama 10)
- Tukio la kubakwa linampotesea fahamu na anaaibika sana anapozinduka na
kujipata akiwa uchi uk 47 - Mwanamke kujeruhiwa - Baada ya Sara kubakwa na janadume lile,
anaharibiwa na kuvuja damu. - Mwanamke kuvunjiwa ujanajike na utu wake.
- Maisha ya mwanamke kuingiliwa na kuharibiwa.
- Masomo yake yanakatizwa - mwalimu mkuu alimkabidhii Sara barua ya
kumfukuza shuleni (uk 49) - Mwalimu mkuu hamsikilizi wala kumhurumia - badala yake aliongoza
kumkejeli na kumweleza ile haikuwa shuke ya wazazi bali wa wasichana.
Anasema hawafundishi wanawake hapo. - Mwanamke anateseka kiakili - Sara anaingiwa na mawazo mengi jinsi
atakvyoukabili ule ujauzito. Anafikiria hata kuitoa ile mimba, kuhama kwao na hata kujiua. - Mwanamke katika umri mdogo anabebeshwa mimba jinsi Sara alivyofanysihwa. Mzigo huo ungekuwa na changamoto nyingi kutokana na umri wake mdogo.
- Kuishi adhabu ya wazazi - Sara anahofia babake angemchinja kwa ujauzito
wake. - Kuogopa kutoa taarifa ya kubakwa kwa wazazi kwa sababu wazazi hawangemwamini.
- Kuishi maisha ya kimaskini - msimulizi anaeleza kuwa Sara angekunjiwakunjiwa matambatra yake na kurushiwa nje. Kila mara mwanamke anapobakwa, anayelaumiwa ni mwanamke na hata huonwa kama shetani. Uk 48 (hoja 10 x 1 = 10)
