
Istilahi za Kishairi
1. Arudhi
- Sheria za jadi zinazofuatwa na watunzi wa mashairi:
- kugawa shairi katika beti
- beti kugawika katika mishororo inayolingana kiidadi
- mishororo kugawika katika vipande
- mishororo kuwa na mizani zinazolingana kiidadi (urari wa mizani)
- kuwa na vina vya kati na vya mwisho vinavyotamkika kwa namna sawa (urari wa vina)
- mtoshelezo wa beti au beti kutoa wazo kamili
2. Bahari
- Aina tofauti tofauti za mashairi k.m. ukara
3. Ubeti/beti
- Kifungu katika shairi kinachojitosheleza kimaaa
4. Mshororo
- Mstari katika ubeti
5. Mwanzo
- Mshororo katika ubeti
6. Mloto
- Mshororo wa pili katika ubeti
7. Mleo
- mshororo wa tatu katika ubeti
8. Kimalizio
- Mshororo wa mwisho ambao haurudiwi katika kila ubeti
9. Kibwagizo/mkarara/kipokeo/kiitikio
- Mshororo wa mwisho ambao hurudiwarudiwa katika kila ubeti na hubeba maudhui au kiini cha shairi.
10. Kipande/mgao
- Sehemu katika mshororo ambayo huonyeshwa na koma na huwa na kina
11. Ukwapi
- Kipande cha kwanza katika mshororo
12. Utao
- Kipande cha pili katika mshororo
13. Mwandamizi
- Kipande cha tatu katika mshororo
14. Mizani
- Silabi zinazotamkika katika mishororo
15. Urari wa mizani
- Kuwepo kwa idadi sawa ya mizani katika mishororo
16. Kina/vina
- Silabi zinazotamkika kwa namna sawa zinazopatikana katikati na mwishoni mwa sentensi.
17. Urari wa vina/vue
- Kuwepo kwa silabi zinazotamkika kwa namna sawa

Aina za Mashairi
- Mashairi ya arudhi/Ushairi wa kijadi
- Ambayo huzingatia sheria za jadi za utunzi wa mashairi.
- Mashairi huru
- Ambayo hayazingatii sheria za jadi za utunzi wa mashairi.
Mashairi ya Arudhi
- Aina
- tathmina (mshororo mmoja katika kila ubeti)
- tathnia (miwili)
- tathlitha (mitatu)
- tarbia (minne)
- takhmisa (mitano)
- tasdisa (sita)
- ushuri (kumi)
- Bahari
- mtiririko (mfanano wa vina vya kati na vya mwisho katika shairi zima)
- ukara (vina vya mwisho kufanana na vya kati kutofautiana)
- ukaraguni (vina vya kati na vya mwisho kutofautiana katika shairi zima)
- kikwamba (mishororo kuanza kwa neno fulani katika shairi zima)
- pindu (neno au maneno mawili ya mwisho ya kila mshororo kutumiwa kuanzia mshororo unaofuata) k.m. kicha changu wachezea. Wachezea kichwa changu.
- Tenzi/tendi (mgao mmoja, kina kimoja)
- Mathnawi (migao miwili, vina viwili)
- Ukawafi (migao mitatu, tumbuizo 8,8,8)
- Ngonjera (majibizano)
- Malumbano (kujinaki/kuonyesha ugwiji akimdunisha mshairi mpinzani ili kutaniana)
- Msuko (mshororo wa mwisho mfupi kuliko inayotangulia)
- Sakarani (mchanganyiko wa bahari)
- Dura mandhuma (kauli/swali katika ukwapi na mjalizo/jibu katika utao k.m. shida zikishinda, hazishindiki. Unalolipenda, halipendeki. Unapopaenda, hapaendeki)
- Gungu (mizani 12, kina kimoja cha mwisho)
- Upeo (mishororo inayozidiana ki mizani)
- Kikai (mizani 12, 4:8 au 8:4, hakuna ulinganifu wa mizani katika ukwapi na utao)
- Zivindo (hutoa maana tofauti za neno k.m.
- Sumbila (kila ubeti una kimalizio tofauti na beti nyingine)
- Muundo/Umbo/Sura ya Nje
- Kutaja idadi ya beti
- Mishororo mingapi katika kila ubeti
- Vipande vingapi katika kila mshororo-aina
- Mpangilio wa mizani na jumla k.m. ukwapi 8, utao 8, jumla 16.
8 8
8 8
8 8
8 8 - Mpangilio wa vina au kufanana, kutofanana katika shairi zima au vina vya mwisho kufanana na vya kati kutofautiana-bahari
na ma
na ma
na ma
ka ba
Vina na Mizani
8a 8b
8a 8b
8a 8b
8c 8b - Kibwagizo(linacho au halina. Kinakili kama kipo)
- Majibizano (ngonjera)
- Malumbano (majinaki)
- Uhuru/Idhini za Kishairi
- kibali mshairi alichonacho kukiuka sheria fulani.
- Inkisari (kufupisha ili kuwe na urari wa mizani na vina. Aghalabu huonyeshwa kwa matumizi ya ritifaa k.m. ‘sikate-usikate)
- Mazda/mazida (kurefusha neno ili kuwa na urari wa mizani na vina)
- Tabdila (kubadilisha tahajia ya neno bila kuzidisha au kupunguza mizani k.m. siachi-siati)
- Utohozi - kuswahilisha maneno kutoka lugha nyingine k.m bratha, sekretari, kompyuta
- Kuboronga/kufinyanga sarufi (kubadili mpangilio wa maneno katika sentensi k.m. upesi jielimishe)
- Kiswahili cha kikale/ujadi (mtima, ngeu, insi, mja, ,maozi)
- Lahaja k.m. ficha-fita
- Matumizi ya ritifaa
- Inkisari (kufupisha ili kuwe na urari wa mizani na vina. Aghalabu huonyeshwa kwa matumizi ya ritifaa k.m. ‘sikate-usikate)
- kibali mshairi alichonacho kukiuka sheria fulani.
- Lugha ya Nathari
- lugha ya kawaida na kimtiririko
- Kutotumia koma au vipande
- Kutumia maumbo ya kawaida ya maneno
- Ubeti kutengewa aya moja
- Kuondoa uhuru na kusanifisha lahaja na kikale
- matumizi ya lugha/fani
- matumizi ya maneno (kama yalivyotumiwa)
- ujumbe
- maudhui
- dhamira
- kusimanga, kusuta, kudharau, kusifu, kufunza, n.k.
Mashairi Huru
Sifa/Mbinu
- urudiaji
- wa neno (takriri neno)
- wa kifungu (usambamba)
Umuhimu - kusisitiza ujumbe
- kutia ridhimu/mapigo fulani katika usomaji
- mishata
- mishtari ambayo haikamiliki. Mistari toshelezi ni mistari iliyokamilika.
- sehemu za beti kuingizwa ndani
Umuhimu- ili kusisitiza
- kuzifanya zionekane wazi

Ulinganishaji wa Shairi la Arudhi na Shairi Huru
Kufananisha
- yote mawili ni sanaa ya ushairi
- mishororo kupangwa katika beti
- yametumia mbinu za lugha za namna moja
- alama za kuakifisha zinazofanana
- kufanana kimuundo
- uhuru wa kishairi
Kutofautisha
- moja ni la arudhi jingine ni huru
- mishata
- sehemu za beti kuingizwa ndani
- kuwa au kutokuwa na urari wa mizani
- kuwa au kutokuwa na urari wa vina
- tofauti kimaudhui
- idadi ya beti
- idadi ya mishororo katika beti
- vipande
- kutumia alama za uakifishi tofauti
- uhuru wa kishairi
Download Ushairi - Kiswahili Notes.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students
Join our whatsapp group for latest updates