Kiswahili Kidato cha Kwanza hadi nne, Fasihi Andishi na Simulizi (92)

Durusu kiswahili katika maandalizi ya mitihani ya kitaifa KCSE.

 

Sarufi na Matumizi ya Lugha

Sarufi na Matumizi ya Lugha (17)

Sehemu hii inajumuisha sarufi na matumizi ya lugha kutoka kidato cha kwanza hadi cha nne kwa udurusu wa mitihani ya ndani na ya kitaifa. Unaweza kuipata nakala hii ya sarufi na matumizi ya lugha kama pdf.

YJ_CAT_READMORE
Mwongozo wa Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine

Mwongozo wa Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine (15)

Mwongozo huu umetayarisha hadithi zote za Lisiloshiba na Hadithi Nyingine na kuzifanya zieleweke barabara. Kuna mifano ya maswali ili kuwapa changamoto watahiniwa wote.

YJ_CAT_READMORE
Mwongozo wa Kigogo

Mwongozo wa Kigogo (7)

Sehemu hii imesheheni mwongozo wa tamthlia ya Kigogo. Uchambuzi huu wa tamthilia ya kigogo una ufupisho au muhtasari wa maonesho yote, wahusika katika tamthilia hii, na maudhui mbali mbali yanayojitokeza.

YJ_CAT_READMORE
Mwongozo wa Chozi la Heri - Chozi la Heri Notes

Mwongozo wa Chozi la Heri - Chozi la Heri Notes (8)

Pata mwongozo wa riwaya ya Chozi la Heri iliyoandikwa na Assumpta K. Matei. Mwongozo huu una sehemu zifuatazo: jadala na ufaafu wa anwani, muhtasari, dhamira na maudhui, wahusika na uhusika, fani- mbinu za lugha na mbinu za tamathali/mbinu za Sanaa, maswali na majibu ya dondoo na ya insha katika Riwaya ya chozi la heri. Unaweza kusoma bure bila malipo kwa kubonyeza viungo vilivyo hapa chini.

                                                                                                                                  chozi la heri                                                                                                                                   

Kuhusu kitabu

Chozi la heri ni kitabu kinachotahiniwa katika shule za upili chini ya karatasi ya Kiswahili 3- 102/3. Pia ni kitabu kilichowekwa cha lazima kwa shule za Sekondari za Kenya chini ya Kiswahili Fasihi. Kitabu hiki kinahusu jinsi uchoyo wa kupata mamlaka na utajiri na ukabila unavyoharibu maisha ya kawaida na maendeleo ya kijamii. Baadaye, mabadiliko yanakumbatiwa ambayo huleta hisia ya usawa katika jamii na hivyo kuwa na matumaini ya kuzaliwa upya. Wanafunzi wengi wanaona seti ya kitabu kuwa ngumu hata hivyo, mwongozo huu unasaidia kurahisisha kitabu kwa wanafunzi.

Sehemu za Mwongozo wa Riwaya – Chozi la Heri

Wahusika na uhusika
Mwongozo huu unatoa uchambuzi wa kina wa wahusika wote katika riwaya ya Chozi la Heri na familia zao. kama hujui wahusika katika riwaya hutaweza kupata alama nzuri katika swali lolote linalohusu kitabu hiki cha Chozi la Heri. Wahusika katika chozi la heri ni:

 • Ridhaa.
 • Terry
 • Mzee kedi
 • Tila
 • Becky.
 • Kangara.
 • Mzee mwimo msubili.
 • Mama ridhaa.
 • Selume
 • Billy
 • Sally
 • Naomi.
 • Lunga
 • Umulkheri (umu)
 • Sauna
 • Hazina
 • Julida
 • Kairu
 • Mzee kaizari
 • Mwanaheri
 • Lime

Sauna.Pata Uhusiana kamili wa wahusika katika riwaya ya chozi la heri na sifa zao katika mwongozo wetu hapa.
Pia pata maswali mbalimbali ya utabiri kuhusu wahusika na sifa zao.

Muhtasari
Riwaya ya Chozi la Heri ina sura kumi.
Pata muhtasari wa sura na maswali mbalimbali ya utabiri kuhusu riwaya ya Chozi la Heri hapa.

Dhamira na Maudhui

Riwaya inazungumzia masuala kadhaa yakiwemo; masuala ya ukabila, biashara haramu kama vile ulanguzi wa dawa za kulevya, na mila haribifu kama vile ndoa za utotoni, matumizi yasiyofaa ya mamlaka, ufisadi na uporaji wa rasilimali za umma.

Dhamira ya mwandishi

 • Kuupiga vita ukabila.
 • Kuvipiga vita 'vita vya baada ya kutawazwa'
 • Kuufichua uozo ulio katika jamii.
 • Kuonyesha umuhimu mapenzi katika ndoa na familia.

Maudhui.

 • Maudhui ya migogoro
 • Umasikini
 • Ushirikina
 • Ndoa
 • Mauti
 • Ukoloni mambo leo
 • Ukoloni mkongwe
 • Elimu
 • Uongozi
 • Mapenzi.
 • Teknolojia
 • Ufeministi/taasubi ya kiume
 • Umenke
 • Sheria
 • Uozo wa maadili ya jamii
 • Dini
 • Ufisadi
 • Demokrasia
 • Mabadiliko
 • Uharibifu wa mali na mazingira
 • Utamaduni
 • Utabaka
 • Utala
 • Malezi
 • Ujaala
 • Uongozi mbaya
 • Utamauishi

Pata maelezo kuhusu dhamira ya mwandishi na muhtasari wa maudhui ya riwaya hapa. Pia kuna maswali ya marudio.
Vipengee vingine katika mwongozo vinavyopatikana katika umbizo la PDF ni pamoja na fani- mbinu za lugha na mbinu za tamathali/mbinu za Sanaa, maswali na majibu ya dondoo na maswali na majibu ya insha.

Hitimisho

Mwongozo huu unatoa uchambuzi kamili wa riwaya ya Chozi la Heri ambayo hakika itawasaidia wanafunzi kupata alama nzuri linapokuja suala la maswali ya mitihani inayohusu riwaya hiyo. Zaidi ya hayo, mwongozo unatoa maswali na majibu kuhusu vipengele vyote vya riwaya kama inavyoonyeshwa hapo juu na inaweza kupakuliwa katika muundo wa PDF kwenye tovuti yetu ya easyelimu.com na Programu ya Masomo ya EasyElimu (EasyElimu Study App).

Ipate sasa!

YJ_CAT_READMORE
Isimu Jamii

Isimu Jamii (3)

Sehemu hii imesheni maelezo yote ya Isimu Jamii kuanzia utangulizi, sajili, lahaja, lafudhi n.k.

YJ_CAT_READMORE
Fasihi

Fasihi (8)

Sehemu hii inajumuisha maelezo yote katika Fasihi. Kuanzia Fasihi Andishi na Simulizi kwa udurusu wa mitihani ya ndani na kitaifa.

YJ_CAT_READMORE
Insha

Insha (33)

Sehemu hii inajumuisha maelezo yote kuhusu aina mbali mbali za insha kuanzia insha za methali, hotuba, mahojiano, barua ya kirafiki, mazungumzo, wasifu, kumbumbuku n.k

YJ_CAT_READMORE
Ushairi

Ushairi (1)

Sehemu hii inajumuisha maelezo yote kuhusu ushairi. Kuanzia aina za mashairi, istilahi za ushairi na muundo wa mashairi

YJ_CAT_READMORE
Page 5 of 5