Jalada na Anwani ya Tamthilia - Mwongozo wa Bembea ya Maisha

Share via Whatsapp

Menyu ya Urambazaji:

JALADA LA BEMBEA YA MAISHA

  • Jalada ya hadithi hii imechorwa watu watatu wamekumbatiana, mwanaume mmoja na wanawake wawili. Wote wamekalia bembea. Nyuma yao, kuna mwanga wa jua. Jalada na anwani ya kitabu hiki vina uhusiano wa moja kwa moja.
  • Tunaweza sema kwamba wattau hawa wamekalia bembea ili kuonyesha changamoto za maisha ya kifamilia. Maisha ya familia yana juu na chini kama vile bembea huenda mbele na nyuma. Pia, watatu hawa jinsi walivyokumbatiana inalingana na mwisho wa hadithi ambapo wahusika watatu(Yona, Sara na Neema) wanakumbatiana.
  • Jalada ni sehemu iliyoko juu ya kitabu Huwa ni mambo yaliyo muhtasari wa kile msomaji anataraji ndani. Jalada huwa kuwili yaani, jalada la mbele na la nyuma. Kunavyo vipengele muhimu hasa rangi za michoro na maandishi.
  • Jalada la tamthilia ya Bembea ya Maisha limechorwa mwanamume na wanawake wawili wakiwa wamekumbatiana. Watu hao wameketi kwenye bembea. Mwanamume huyo anawakilisha Yona na wanawake hao wanawakilisha Sara na Neema.
  • Wote wanaonekana kufunga macho kuonyesha wako katika hali ya utulivu wa moyo. Hali hii ya kukumbatiana inadhihirisha kwamba kuna upatanisho wa familia ambayo ilikuwa imeyumbishwa na bembea ya maisha.

ANWANI YA TAMTHILIA

  • Bembea ni kifaa kama vile ubao, kamba au chuma inayoninWinia baina ya chuma au mti ambacho hutumiwa kuchezea aghalabu na watoto. Bembea ni aina ya chombo cha mchezo ambacho kinachezewa kwa kuenda mbele na nyuma. Kwa hadithi hii, mwandishi anazingatia jinsi maisha yanavyoendelea kuenda mbele na nyuma kila uchao.
  • Bembea huenda juu na chini au mbele na nyuma. Ili mtoto aweze kucheza na bembea, wakati mwingine kuna anayeisukuma bembea hiyo.
  • Bembea ya maisha ni namna maisha yanavyoendesha watu.
  • Katika tamthilia hii, maisha yamesawiriwa kama bembea. Kuna wakati maisha ya wahusika yamejawa na furaha na mafanikio tele na kuna wakati maisha ya wahusika yanaenda chini, wanakumbwa na shida na matatizo.
  • Kwa kupitia wahusika, mwandishi anataka kutuonyesha kwamba maishani hakuna hali iliyo wastani au ilikwama ila mambo huenda yakibadilika, mabaya kwa mazuri na mazuri kwa mabaya. Haya ayanazingatiwa haswa na mhusika Sara, ambaye anaonekana kuwa amekubali yale yote ambayo maisha yamempa na kwa mazungumzo yake na wahusika wengine anajaribu kuwaeka kwa hali ya kuwaonyesha kwamba hii ndiyo hali ya maisha na kwamba tunapaswa kuyakubali jinsi yalivyo.

Kwa mfano, ufaafu wa anwani unazinagtiwa kupitia njia kama vile:

  • Maisha ya familia ya Sara na Yona yanaleta taswira ya bembea. Mwanzoni, ndoa ya Sara na Yona inaonekana yenye furaha. Hii ina maana kuwa, kama bembea inavyokuwa juu, maisha yao yalikuwa yenye mafanikio na furaha. Maisha yao yanaingiwa na dosari wakati wawili hao wanakosa mtoto baada ya kipindi kirefu katika ndoa. Zaidi ya hayo, wanajaliwa na watoto wa kike watatu. Hawajaliwi na mtoto wa kiume, kinyume na matarajio ya jamii. Wanachekwa, wanasutwa na kukejeliwa.
  • Bembea ya maisha yao inarudi chini. Sara anaanza kuchapwa kichapo cha mbwa na bwana yake Yona. Yona anaidharau familia yake na kuingilia ulevi, ulevi uliomfanya kupigwa kalamu kazini. Sara anasema, japo kuna wakati maisha yanabwagwa na bembea ya maisha, lazima maisha hayo yaendelee. Hata kama kamba, chuma au minyororo ya maisha inakatika, hawana budi kujiinua na kuendelea na maisha (uk. 20-21). Hivyo basi Sara anasimama na familia yake kidete akifahamu kuna siku atafanikiwa na maisha yao yatakuwa mema tena.
  • Maisha ya familia ya Yona yanabadilika kutoka kuwa maisha ya kukosa mahitaji ya kiuchumi. Bembea yao ya maisha ilionekana kuwachini. Baada ya Neema kufanikiwa na kupata kazi, bembea ya maisha yao inakuwa juu. Wanafanikiwa kujengewa nyumba, wanapata wafanyakazi wa kuwasaidia nyumbani na hata kuwa na jiko la gesi la kupikia.
  • Bembea ya maisha ya Neema inaonekana kusukumwa na Bunju mumewe. Kwanza Bunju alimsaidia Neema alipokuwa amepata ajali. Bunju alimtumia flying doctors ili aweze kupata matibabu zaidi (uk. 41).
  • Bunju anasaidia kuisukuma bembea ya maisha ya Neema kwa kumsaidia kuwasomesha dada zake. Vilevile, anamsaidia kuwajengea wazazi wa Neema nyumba.
  • Maradhi ya Sara yanaifanya bembea ya maisha ya Sara kuwa kama iliyokatika na kuwa chini. Sara anakosa matumaini ya kuishi na kutamani kufa.
  • Bembea ya maisha ya mjini huwa juu kutokana na maendeleo. Kuna maendeleo ya barabara, magari mengi, majengo mengi na hata sekta ya matibabu imeimarishwa.
  • Watu mjini wanapokea matibabu ya hali ya juu ilhali, bembea ya maisha ya kijijini huwa chini kwa sababu ya kukosa maendeleo hasa katika sekta ya matibabu na barabara nzuri. Sekta ya matibabu ya kijijini inamfanya Neema kumtafutia mamake hospitali ya mjini sababu zile za kijijini hazimpi mtu matumaini ya kutoka akiwa mzima ilhali za mjini zinampa mgonjwa matumaini ya kutoka akiwa buheri wa afya.

Dhamira ya mwandishi

Dhamira huelezwa kama lengo au shabaha ya mwandishi wa kazi ya fasihi.
Mwandishi wa tamthilia ya Bembea ya Maisha anadhamiria:

  • kuonyesha masaibu ya pombe katika maisha ya familia
  • kuonyesha kuwa ili kujenga jamii mpya, mapinduzi ni muhimu na ni lazima wanajamii wajitolee kupinga tamaduni zisizo na umuhimu wowote katika maisha ya wanajamii
  • kutuonyesha kuwa watoto wa jinsia zote ni sawa na hawafai
  • kutenganishwa kwa mila na tamaduni za jamii
  • kutuonyesha kuwa hakuna lililo na mwanzo lisilokuwa na mwisho.

Ushauri muhimu kwa mtahiniwa

  1. Mtahiniwa sharti asome kitabu husika (Bembeaya Maisha) barabara na kukielewa.
  2. Mwongozo ni kurunzi ya kumulikia njia, kwa hivyo, mtahiniwa sharti aelewe aendako.
  3. Ni muhimu kusoma na kulielewa swali lililoulizwa. Ni vyema kujiuliza swali lifuatalo: Mtahini anataka habari gani kutokana na swali hili?
  4. Usitoke nje ya muktadha wa swali na kuandaa habari ambazo hazihusiani na swali uliloulizwa.
  5. Ikiwezekana, toa mifano kutoka kwenye tamthilia inayohusiana na jambo unalolifafanua ili kuweka jambo hilo wazi.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Jalada na Anwani ya Tamthilia - Mwongozo wa Bembea ya Maisha.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?