FANI- MBINU ZA LUGHA NA MBINU ZA TAMATHALI/MBINU ZA SANAA- Mwongozo wa Chozi la Heri

Share via Whatsapp


Utangulizi

Tamathali za uandishi ni matumizi ya kwa narrina fulani ili kuifanya lugha iwe ya kuvutia na kuifanya kazi ya Sanaa iwe ya kupendeza. Mbinu hizi za uandishi zimegawika katika makundi mawili makuu: Mbinu Fani za lugha na Mbinu za Sanaa

  1. Mbinu za lugha Huu ni uteuzi wa maneno iii kuifanya lugha iwe ya kupendeza na kuvutia. Pia hujulikana kama mapambo ya lugha
  2. Mbinu za Sanaa Huu ni ubunifu wa kisanaa unaojitokeza baada ya kusoma kazi ya fasihi au kusikiliza masimulizi. Mifano ya mbinu za lugha katika riwaya hii:

 



Mbinu za Lugha

1. Jazanda.

Hii ni mbinu ya kulinganisha vitu viwili moja kwa moja bila kutumia viunganishi.

  1. Katika ukurasa wa 4 tunasoma; "Mwangeka alisema Ridhaa kupitia kwa sauti ya mawazoni mwake, kumbe wewe ni sawa na yule Mwangeka wa kihistoria ambaye kivuli chake kikitembea siku zote mbele yake, ambaye mwili wake ulikuwa kaka tu, roho yenyewe iliishi nje ya kaka hill kwa kutotaka kudhibitiwa? Umewezaje kunusurika? Kumbe wadhifa waliokupa wa kwenda u umisha Amani katika mashirika ya kati umetokea kuwa wongovu wako?" Hapa, Ridhaa anamlinganisha Mwangeka wa kisasa na yule Mwangeka wa kihistoria.
  2. Katika ukurasa wa 6 tunasoma; "Basi niambie, baba, unatumia mantiki gani kusema kuwa Sisi si watoto wa miaka hamsini? Je, miaka hamsini ya uhuru imetukuza kiuchumi au tumebaki kuwa wategemezi wa hao hao ambao walitupa uhuru?" Hapa kuna ulinganishi kati ya miaka hamsini ya uhuru wa taifa, na miaka hamsini ya kuzaliwa kwa hawa watu ambao bado hawajajikomboa kutokana na ule ukolonio mambo leo.
  3. Katika ukurasa wa 8 tunasoma; "Ardhi ya mzee Mwimo Msumbili ikawa haitoshi kuyalea madume yake ishirini " Vijana wake Mzee Mwimo wanalinganishwa na madume ishirini.
  4. Katika ukurasa wa 29 tunasoma; "Nilihisi kwamba ingekuwa bora kama tungefia katika mazingira tuliyoyazoea; huenda hata tungepata wa kutuomboleza, kuliko kufia ugenini "Sasa umeanza kufikiria kama wafuasi wa nabii Musa ambao baada ya kukosa chakula huko jangwani, walimshutumu kwa kuwatoa kule Misri. Walidai kuwa huko Misri wangekula matikitimaji yao pamoja na kuwa watumwa!" Hapa, msemewa anafananishwa na wale wana wa Israeli waliotamani kuwa ni heri wangekufia huko misri badala ya kupelekwa jangwani na Musa kufia huko.

2. Tashihisi/uhuishaji

Hii ni mbinu ya kupatia kitu kisicho uhai sifa za kiumbe mwenye uhai, au sifa za kibinadamu.

  1. Katika ukurasa wa 3 tunasoma; "Alijiona akiamka asubuhi ambayo ilizaa usiku wa jana, usiku ambao ulitandaza kiza katika maisha yake " Usiku unapewa sifa za kuwa na uhai na kupewa uwezo wa kuzaa asubuhi kama mwana.
  2. 4 tunasoma; "Familia yangu na mali yote hii kuteketea siku moja? Bila shaka hili ni zao lingine la husuda " Husuda inapewa sifa ya kibinadamu na kuwa na uwezo wa kuzaa maovu aliyotendeka.
  3. Katika ukurasa wa 7 tunasoma; "...mustakabali wa ukuaji wetu kiuchumi uligonga mwamba wakati sheria ya mkoloni ilipompa mzungu kibali cha kumiliki mashamba katika sehemu zilizotoa mazao mengi. Ukengeushi wa ardhi ukatiliwa muhuri" Tunapata kuwa hapa, mashamba yanapewa sifa ya kuwa na uhai, kwani kuna sehemu zilizozaa mazao mengi. pia ardhi inaonekana ikiwa katika hali ya ukengeushi; hivyo kupewa sifa ya kuwa na uhai.
  4. Katika ukurasa wa 8 tunasoma; "Ardhi ya Mzee Mwimo Msumbili ikawa haitoshi kuyalelea madume yake ishirini ifigawanywa hadi ikawa vikata, ikalimwa na kupaliliwa mpaka ikachoka " shamba hili linapewa sifa kuwa na uhai, kwani linachoka baada ya kufanyiwa kazi nyingi.
  5. Katika ukurasa wa 12 tunasoma; "Ridhaa hakujua alikuwa amesimama pale kwa muda gani. Miguu yake sasa ilianza kulalamika " Tunapata kufahamu kuwa miguu ya Ridhaa inalalamika. Hapa miguu imepewa sifa ya kuwa uhai na kuwa na uwezo wa kulalamika kama binadamu.
  6. Tunasoma pia; "Baada ya muda wa mvutano wa hisia na mawazo, usingizi ulimwiba " Usingizi umepewa sifa ya kibinadamu na kuwa na uwezo wa kuiba.
  7. Katika ukurasa wa 14 tunapata haya; "Tumo katika kambi fulani la, si kambi, mabanda hasa yaliyosongamana na kutazamana kwa jitimai na dhiki, vibanda vya mtomeo hasa " Vibanda hivi vinapewa sifa ya kibinadamu, kwa vinaweza kusongamana na pia kutazamana kwa jitimai na dhiki, kana kwamba vina macho na hisia.
  8. Katika ukurasa wa 15; "Naona wingu kubwa angani likitembea kwa kedi na madaha na kulifunika jua. Tukio hili linafuatwa na umeme, kasha mtutumo wa radi. Mawingu yaliyoshiba yakataka kutapika yanagooka, yanakaribiana, kupigana busu na kusababisha mwanguko wa matone mazito ya mvua; " Mawingu yanapewa sifa za kuwa na uhai kama binadamu, yanatembea kwa kedi na nadaha. Pia mawingu haya yanashiba na kuataka kutapika. Pia yanagooka, yanakaribiana na pia kupigana busu; hizi zote zikiwa ni sifa za kibinadamu.
  9. Katika ukurasa wa19; "Tunahitaji kumpa nafasi Mwekevu. Huenda hata hatukwamulia uchumi ambao unachechemea " Uchumi unapewa sifa ya kibinadamu ya, na uwezo wa kuchechemea.
  10. Katika ukurasa wa 35; "Undugu na utangamano wa wakimbizi wenzake uliyahuisha maisha yake, ukayajenga upya, ukamfunza Zaidi kuhusu maisha yake, ukayajenga upya, ukamfunza Zaidi kuhusu thamani ya binadamu " Ridhaa anakumbuka jinsi maisha yake yalivyokuwa yamekosa maana lakini baadae yakahuishwa na wakimbizi wenzake, yakajengeka upya na akaelewa Zaidi kuhusu dhamani ya binadamu.
  11. Katika ukurasa wa 76; "Walipokuja hapa, ardhi hiyo haikuwa bikira, wakatifua udongo wakailima?" Ardhi inapewa sifa kama za binadamu za kuwa bikira, hivyo basi, mbinu ya uhuishaji kujitokeza.
  12. Katika ukurasa wa 143; "Kipanga sasa ameanza kuuhuisha utu wake " Mbeleni maisha yake hayakuwa na maana lakini kwa sasa anayapa uhai, na hivyo yanapata maana, na utu wake unakuwa kamili.
  13. Katika ukurasa wa 156; "Asubuhi moja mbichi ilinipay kwenye baraste kuu; nimmeamua kutamba na ulimwengu Asubuhi inapewa sifa za kuwa na uhai na kuwa mbichi au changa. Pia asubuhi hii inampata kwenye baraste kana kwamba inatembea.

3. Semi

Semi ni fungu la maneno linalotumika kutoa maana tofauti na ile ya maneno yaliyotumika. Semi hutumika kuficha ukali wa maneno au kupamba lugha. Kwa jumla, kuna aina mbili za semi.

  1. Nahau.
  2. Misemo.

Nahau

Ni fungu la maneno lenye maana fiche, isiyotokana na maana ya maneno halisi yaliyotuimika katika uandishi.

  1. Katika ukurasa wa 2; "Wewe endelea kupiga hulu tu, lakini utakuja kuniambia "
  2. Katika ukurasa wa 3; "Angesema bibi huyu amebugia chumvi ya maisha ikamrishai "Alijihisi kama mpigana masumbwi aliyebwagwa na kufululizwa makonde bila mwombbezi"
  3. Katika ukurasa wa 6; "Na kazi zenyewe si kazi, ni vibarua vya kijungujiko tu '
  4. Katika ukurasa wa 7; "Mustakabali wa ukuaji wetu kiuchumi uligonga mwamba wakati sheria ya mkoloni ilipompa mzungu kibali cha kumiliki mashamba katika sehemu zilizotoa mazao mengi"

Misemo

Haya ni mafungu ya maneno yenye maana maalum ambayo hutoa mafundisho kwa jamii.

  1. Katika ukurasa wa 4;"Alikuwa amesafiri kwa shughuli za ujenzi wa taifa kama alivyoziita safari zake za kikazi. Uchungu wa mwanagenzi ukawa haujui simile, ukabisha hodi, naye mwangeka akazaliwa "
  2. Katika ukurasa wa 6; "Imekuwa tunaubadili ule msemo wa mtegemea nundu haachi kunona "
  3. Katika ukurasa wa 7; "Ukengeushi wa ardhi ukatiliwa mhuri, umilikaji wa ardhi na waafrika katika sehemu hizi ukapigwa marufuku "
  4. Katika ukurasa wa 9; "Mzee mwimo akaona ku moto, akaamua kuwahamishia wake wawili wa mwisho Msitu wa Heri, ama Ughaishu kama walivyouita watu wa huko "
  5. Katika ukurasa wa 10; "wewe ni mfuata mvua. Hatutaki kucheza nawe "
  6. Katika ukurasa wa 11; "Baadaye aliamua kuuasi ukapera, akapata mke; Terry "
  7. Katika ukurasa wa 16; "Wamesema wajuao kuwa simba akikosa nyama hula nyasi "
  8. Katika ukurasa wa 25; "Wakati tukitazama ubahaimu huu wa Firauni, hatukujua kuwa tulikuwa kuni kwenye uchaga, chuma chetu kilikuwa motoni"
  9. Katika ukurasa wa 71; "Rai ya wakubwa hata hivyo haikuwanyamazisha Lunga. Aliendelea kulipinga tendo hili kwa jino na ukucha "
  10. Katika ukurasa wa 92; "Lakini, lo!wanasema wajuao kuwa msitu ni mpya, ila nyani ni wale wale "
  11. Katika ukurasa wa 148; "Akiisha kutimiza maazimio yake, atajichagulia kijana mwenzake wafunge akida "
  12. Katika ukurasa wa 150; "Hata hivyo, fahamu kuwa mara zote binadamu huhitajika kujikuna ajipatapo; "
  13. Katika ukurasa wa 183; "Ule msemo maarufu wa baba yangu, usiisifu njaa ya mbwa kabla usiku haujaingia ukahakikisha kuwa mbwa amelala njaa, ukatimia "

4. Methali

Hii ni misemo ya hekima yenye maana iliyofumbwa. Mwandishi hutumia methali kupitisha ujumbe fulani.

  1. Katika ukurasa wa 12; "Kweli jaza ya hisani ni madhila?"
  2. Katika ukurasa wa 36; "Hata Ridhaa anapomfikiria Kaizari anajiambia, 'Heri nusu shari kuliko shari kamili '
  3. Katika ukurasa wa 50; "Moyoni alijua kuwa bado palikuwa na kazi ngumu ya kujenga upya ukuta ambao ufa wake ulikuwa umepuuzwa " Methali inayorejelea ni 'usipoziba ufa utajenga ukuta '
  4. Katika ukurasa wa 51; "Alimtazama baba yake kana kwamba anataka kuhakikishiwa jambo, naye Ridhaa akamjibu kwa mtazamo uliojaa Imani, "Mwenye macho haambiwi tazama "
  5. Katika ukurasa wa 53; "Akili yake ilimkumbusha methali aliyozoea kumtolea mpinzani wake darasani kila mara Mwangeka alipomshinda kuwa, 'Wino wa mungu haufutiki '"
  6. Katika ukurasa wa 55; "kumbe amekwenda kuingia kwenye mtego wa panya unaowanasa waliomo na wasiokuwemo!"
  7. Katika ukurasa wa 75; Kulikuwa pia na maskini ambao kupata kwao ahueni kulitegemea utashi wa matajari. Dau la mnyonge tangu lini likaenda joshi?"
  8. Katika ukurasa wa 113; "Kumbukeni methali isemayo, ulingo wa kwae haulindi manda "
  9. Katika ukurasa wa 183; "Msemo huu ni sawa na methali ya Kiswahili isemayo, Mungu hamsahau mja wake; au hata bora zaidi, kuregarega sio kufa, kufa ni kuoza tumbo "

5. Lakabu

Ni mbinu ya mhusika kupewa ama kubandikwa jina na wahusika wengine ama yeye mwenyewe kujibandika jina linalooana na tabia au sifa zake.

  1. Katika ukurasa wa 94, "Haikuwa ibra kumsikia nyanya akimrejelea mama kama Muki, yaani, huyo wa kuja, na kusema kwamba msichana wa bamwezi, hata akiwa na umri wa miaka tisini, ni msichana wa Bamwezi tu.
  2. Katika ukurasa wa 178; "Pongezi engineer Vuuk. Naona hili litatusaidia kumhepa Kumuku mwenye kuchungulia kutoka dirisha ndogo la kibanda chake. Kumuku ilikuwa lakabu ambayo vijana hawa walikuwa wamembandika babu yao; lakabu ambayo ilikuwa msiba wa kujitakia "
  3. Katika ukurasa wa 182; "Jumamosi hii kinyang'anyiro kilikuwa katia ya majimbi wawili wa Mwangeka akiitwa Kyenza kabisa na wa Mwangemi akiitwa Mumina (kamaliza)."

6. Ritifaa

Hii ni mbinu ya kuzungumza na mtu aliyekufa au asiyekuwepo kana kwambo yupo pamoja nawe.

  1. Katika ukurasa wa 6; "Ni kweli binti yangu, kwa kutumia falsafa hii, una haki ya kusema Sisi tu watoto wa miaka hamsini; Ridhaa sasa analiambia lima la jivu ambalo anaamil ndilo mabaki ya mwili wa bintiye 'ffunapata kuwa Ridha anazungumza na nafsi ya bintiye aliyeiaga dunia kutokana na kuteketezwa moto.
  2. Katika ukurasa wa 12; "Ridhaa hakujua majibu ya maswal haya. Alilojua ni kwamba haya siyo aliyotumaini baada miongo mitano ya maisha katika maskani haya. Alitamani kupiga ukemi kumwamsha mkewe lakini akili ilimkumbusha kuwa huyo hayupo tena katika ulimwengu huu "Ridhaa anatamani kumwamsha mkewe ambaye kwa sasa ni majivu tu, hayupo tena kwa hali halisia, bali yupo katika nafsi yake Ridhaa.

7. Utohozi

Hii ni mbinu ya kuswahilisha maneno ya lugha nyingine, yatumike kama ya Kiswahili.

  1. Katika ukurasa wa 6; "Si yule myunani ambaye amewageuza wenyeji kuwa maskwota katika vitovu vya usuli wao?" Maskwota kutoka 'squatter'.
  2. Katika ukurasa wa 13,".kupitia kwa halmashauri ya kitaifa ya barabara, ilikuwa imewapa notisi mabwanyenye wanaoyamiliki majumba haya " Neno notisi kutoka 'notice'.
  3. Katika ukurasa wa 34; "Opresheni rudi kanani " opresheni kutokana na 'operation'.
  4. Katika ukurasa wa 70; "Mkulima namba wani " Namba wani kutokana na 'Number one'.
  5. Katika ukurasa wa 189; "Najihisi kama Kurwa katika novela ya Kurwa na Doto novela kutokana na 'novel'.

8. Uchanganya ndimi.

Hii ni mbinu ya kuweka maneno yasiyo ya Kiswahili katika sentensi ya Kiswahili.

  1. Katika ukurasa wa 2; "na hata kukawa na jambo, what can
  2. Katika ukurasa wa 6; "Mara ngapi umesimama kwenye shopping mall yake ukiwa safarini
  3. Katika ukurasa wa 7; "Ama hii ndiyo ile wanayoiita historical injustice?"
  4. Katika ukurasa wa 17; "...hawa watu wamekuwa wakitusumbua na Affirmative Action, na A third should be women "
  5. Katika ukurasa wa 23; "Wewe tutakuteuwa kama Education Attache huko Uingereza "
  6. Katika ukurasa wa 86; "Alipoinua macho yake alikiona kibao kilichoandikwa church road, na mara anakumbuka ilikoelekea ile barabara "
  7. Katika ukurasa wa 86; "Poa sana sistee, we ni mnoma siku moja nitakuhelp hata mimi " "Eazie, nenda ukanunue loaf. Na promise hutanunua glue pliz pliz bratha, "
  8. Katika ukurasa wa 113; "Katika kozi zenu mmefunzwa Effective Communication and Conflict Resolution, "Vilio vya raja kuhusu kile wanachokiita extra judicial killings vimehanikiza kote "
  9. Katika ukurasa wa 114; "Watetezi wa haki wanalilia kile wanachokiita untimely deaths of innocent people, many of whom are youth "
  10. Katika ukurasa wa 159;"haikuwa Baraka yetu, mwanetu Bahati was a sickle-cell case "

9. Kuhamisha ndimi

Ni mbinu ya kuingiza hii sentensi ya lugha nyingine katika kifungu cha lugha ya Kiswahili. Kinyume na kuchanganya ndimi, (ambapo mwandishi huchanganya maneno katika tensi moja), katika kuhamisha ndimi, sentensi kamilifu lugha nyingine hutumika miongoni mwa sentensi za Kiswahili sanifu.

  1. Katika ukurasa wa 2; "Since when has man ever changed destiny?"
  2. Katika ukurasa wa 25; "As for me and my family, we will support our mother "
  3. Katika ukurasa wa 31;"Peace be with you "
  4. Katika ukurasa wa 43; "If there is no bread, let them eat cake "
  5. Katika ukurasa wa 80; "Darling, this will be your home soon after our honeymoon "
  6. Katika ukurasa wa 86;"Mum pliz, just a red!These guys are needy!"These are pretenders. They have been sent by their stinking rich relatives l cant give them even a penny "
  7. Katika ukurasa wa 159;"She did not survive her first week "
  8. Katika ukurasa wa 171; "Thank you Mummy, for reminding Daddy that there is another engineer in the family "
  9. Katika ukurasa wa 182; "Come on, Kyenza Kinyenyo, give him another one, just like the other one!"

10. Istiara

Hii ni mbinu ya kulinganisha vitu viwili moja kwa moja kwa kutumia kiungo 'ni' au 'kuwa'. Mbinu hii pia hujulikana kama sitiari au istiari.

  1. Katika ukurasa wa 1; Kunguru wanalinganishwa na jeshi. "Anakumbuka jeshi la kunguru lililotua juu ya paa la maktaba yake ya nyumbani adhuhuri ya juzi ile "
  2. Katika ukurasa wa 5;"Umekuwa kama jani linalopukutika msimu wa machipuko! Umetoweka katika ulimwengu huu ukiwa teketeke, hata ubwabwa wa Shingo haujakutoka "
  3. Katika kurasa za 8-9; Maisha ya familia ya Mzee Mwimo yanalinganishwa na ndege kwenye kiota. Anasema kuwa hata kipunga akiona kuwa wana wake wamekuwa wakubwa na bado hawataki kutoka kiotani, yeye hukifanya kiota chenyewe kukosa raha kwa kukiweka miiba. Hapo ndipo hawa vifaranga huona kuwa wakati wao wa kuondoka ushatimia. Anasema kuwa hao vifaranga hawaambiwi na mtu kuwa wakati wao wa kupambana na dunia umefika, na hivyo basi, wao hujiondokea bila kuambiwa. Vivyo hivyo, ndivyo kuko katika hii familia ya Mzee Mwimo Msumbili. Tunaambiwa kuwa kwa kuwa na wana wengi, wanao hitaji chakula kila siku, huko nyumbani kwake mzee kukatokea uhasama, na pia migogoro. Kutokana na hayo, mzee Mwimo akaamua kuwahamisha wanawake wake wawili wa mwisho. Wao walipelekwa katika msitu wa Heri kama ulivyojulikana.
  4. Katika kurasa za 14-15;Anasema kuwa ugeni uliopo ni ule wa hali, mazoea na silika. Anasema pia kuwa walipo hapo wako pamoja na matajiri na pia walio masikini. Anasema kuwa unaweza dhani kuwa kuna kiasi cha usawa, lakini binadamu husema kuwa hakuna usawa kati ya binadamu ila tu katika kifo. Anasema kuwa kile ambacho hawajui ni kuwa hata katika kifo, binadamu hawawi sawa hata kidogo. Kunao wanaoaga dunia huku wakiwa wamefishwa ganzi, kiasi cha kuwa hawatausikia uchungu wa kifo. Kuna tofauti pia kati ya mandhari wanamofia hawa binadamu. Kunao wanaokufia katika zananati huku daktari akijaribu kuwaokoa. Wengine wanakufia katika hospitali za kifahari, huku wakiliwazwa na mashine, - na kila mtu anashughulika na kuushikilia uhai wa huyu mheshimiwa. Anasema kuwa wanapokufa hawa, nyuso zao huwa huwa zimetulia, na pia wanaziachilia roho zao kwa faraja. Tunaambiwa kuwa hatuwezi kulinganisha nyuso za hawa na wale wanaofia kwenye hamaniko wakizingirwa na jamaa ambao hawana hata hela za kununulia sindano angalau ya kuwaingiza dawa mwilini. Pia kuna wale wanaokufia vitongojini, kwenye vitanda vya mwakisu baada ya kunywa pombe haramu. Hawa nao wanalinganishwa na nzi amabao hufia dondani na hiyo isiwe ni hasara. Wanalaumiwa kwa kujiingiza katika msiba wa kujitakia. Pia kuna tofauti katika mitindo ya mazishi, viviga vinavyohusishwa na sherehe za mazishi na hata mavazi ya "mwenda zake". Pia jeneza analozikwa nalo pia lina tofauti, kwani tajiri atazikwa kwa jeneza Ia dhamani kubwa kulinganisha na huyu masikini. Maelezo haya yote yanaleta tofauti kati ya matabaka mawili. Tunalinganisha matabaka haya mawili na kuona tofauti iliyokuwepo katika hali zote.
  5. Katika ukurasa wa 18; Tunaambiwa kuwa mwamu wake Ridhaa, kabla tu ya kusikia mlio wa bunduki, mitutu yake ilikuwa ishatema risasi kama bafe atemavyo mate. Utemaji wa risasi unalinganishwa na utemaji wa mate kwa bafe.
  6. Katika ukurasa wa 50; Anasema kuwa elimu yoyote bila kielelezo chema kutoka kwa wanaoitoa elimu yenyewe ni sawa tu na juhudi zile za mfa maji. Katika ukurasa wa 149; Maisha yake na Fungo yalibadilika na kuwa kama yale ya ng' ombe aliyetiwa shemere na Maisha yangu kufungwa nira pamoja na puna ambaye anakataa kusonga mbele. Maisha ya hawa wahusika wawili yanalinganishwa na huyu ng' ombe aliyefungwa pamoja na punda.

11. Taashira

Haya ni matumizi ya lugha ya ishara kuwakilisha ujumbe fulani. Jina au kitu fulani kinatumika kumaanisha kitu kingine chenye uhusiano na kile kilichotumiwa.

  1. Katika ukurasa wa 3; "Katikati ya mito hii ya machozi, Ridhaa aliileta picha ya maisha yake mbele ya kipaji chake "
  2. Katika ukurasa wa 5; "Lakini baba, wewe siwe uliyeniambia kuwa mashamba ya theluji nyeusi yalikuwa milki ya wakolo-
  3. Katika ukurasa wa 12; "Ridhaa hakujua alikuwa amesimama pale kwa muda gani. Miguu yake sasa ilianza kulalamika. Polepole parafujo za mwili wake zililegea, akaketi juu ya majivu la juu ya miili ya wapenzi wake "
  4. Katika ukurasa wa 46; "Alikuwa ameumwa na nyoka, bafe hasa, na bila shaka mwenye kuumwa na nyoka akiona ung' ongo hushtuka " Matukio yaliyokuwa yamemkumba Ridhaa yanafananishwa na nyoka ambaye alimuuma, na hivyo, hawezi kuyasahau.
  5. Katika ukurasa wa 59; "Alikuwa ametoka shuleni, siku hizo walimu walikuwa wameng'ang'ania kuwafunza Jumamosi, wanafunzi waliokaribia "ICU" kama walivyoliita darasa la nane " Darasa la nane linalinganishwa na "ICU".

12. Takriri

Hii ni mbinu ya kurudia rudia neno moja au fungu la maneno ili kusisitiza ujumbe Fulani.

  1. Katika ukurasa wa 4; "Ridhaa alirudi nyumbani na kusimama katikati mwa chumba ambacho yeye na aila yake walikuwa wamekitumia kama sebule kwa miaka na mikaka "
  2. Katika ukurasa wa 14; "Na usidhani ni mazingira mageni, kweli si mageni, si mageni kwani tu mumu humu mwetu, hatumo ughaibuni wala nchi jirani. Tu katika jimbo lile lile tulilozoea, kilichobadilika ni kijiji tu, ni kama kutoka chumba cha malazi, kwenda sebuleni!"
  3. Katika ukurasa wa 16; "Sijui kama inahalisi kumwita mke wangu kwani huyu siye subira wangu wa zamani. Siye, siye, siyeee. Tazama uso wake ulivyovamiwa na majeraha, kikwi "
  4. Katika ukurasa wa 48; "Siye!siye hata kidogo!kilichobaki lile tabasamu lake la daima, lililozoea kumhakikishia usalama siku zote, tabasamu ambalo lilidhihirisha meno meupe pepepe yenye mwanya mkubwa wa kuvutia, mwanya ambao Ridhaa alikuwa amezoea kumwambia Mwangeka kuwa mwanya huo ndio ndoana ambayo aliitumia kumvulia mama yake!"
  5. Katika ukurasa wa 138; "La!la!la mwanangu!Hayo unayoyawazia siyo, ila naona ni muhimu nihamie ile nyumba yangu ya afueni "
  6. Katika ukurasa wa 154;"Mlaani shetani' Sauna aliuambia moyo wake, 'unajua kuwa mimi sikuumbiwa ujalaana, walimwengu ndio walinifinyanga upya, wakanipa moyo wa ujabari. Fikiria u kigoli, kifua ndio kinaanza kuvuvumka, kasha unaamka usiku kumpata baba yako, ba-ba-ya-ko, kwenye chumba chako cha malazi. Anakutenda ya kutendwa. Asubuhi huna hata uso wa kumtazamia yeyote.

 

13. Uzungumzi nafsia

Hii ni mbinu inayomhusu mhusika, anapojizungumzia, ama kwa kuongea au kuwaza, bila kukusudia kusikika na yeyote.

  1. Katika ukurasa wa 4; Ridhaa kupitia kwa sauti yake ya moyoni anamwita Mwangeka, na kumwambia kuwa yeye alikuwa tu kama yule Mwangeka wa kihistoria ambaye kivuli chake kilitembea siku zote mbele yake. Mwangeka huyu pia mwili wake ulikuwa kaka tu, roho yenyewe iliishi nje ya kaka hili kwa kutotaka kudhibitiwa. Ridhaa anajiuliza ni aje mwanawe Mwangeka angeweza kunusurika tu. Anajiambia kuwa wadhifa ambao Mwangeka alipewa wa kwenda kudumisha Amani katika mashirika ya kati ulitokea kuwa ndilo jambo la kumuokoa yeye. Pia anajizungumzia kwenye mawazo yake na kujiambia kuhusu mkaza mwananwe, masikini Lily. Anajiambia kuwa amekuwa kama jani linalopukutika wakati msimu wa machipuko! Anasema kuwa Lily ametoweka katika dunia hii hata kabla ya ubwabwa wa Shingo kumtoka.
  2. Katika ukurasa wa 5; Mawazoni mwake Ridhaa anaskia sauti yake Becky ambaye alikuwa mjukuu wake ikimwita. Ridhaa anaskia sauti za mjukuu wake zikimwita akilini mwake, ilhali katika hali halisi hayupo,
  3. Katika ukurasa wa 47; Ridhaa anasema kuwa anamsikitia mwanawe kwa kuwa hakuwa na familia ya kuendea. Anajisemea kuwa wanuna wake Mwangeka waliangamia wote. Anasema kuwa mkazamwanawe na wanao aliangamizwa na moto, hivi kwamba hata mafuvu ya kuzika hayakubakia. Anaendelea kusema kuwa hata makaburi ya kuwekea makoja ya maua ambayo Mwangeka alikuwa akiyatunga akilini mwake hamna. Ridhaa anajipata katika hali hii ya kuzungumza na nafsi yake, kuhusu hisia na fikra za mwanawe kuhusiana na suala la kuangamia kwa familia yao. Mazungumzo haya yote yanajikita katika nafsi yake Ridhaa.
  4. Katika ukurasa wa 48; Mwangeka aliinua kipaji chake, akatazamana na baba yake. Aliona kuwa babake alikuwa amekonga Zaidi. Uso wake umeshamiri weusi na unyonge. Aliendelea kujisemea akilini mwake kuwa sasa babake alimshabihi babu Mwimo Zaidi, hasa kule kupwaya kwa ngozi yake.
  5. Katika ukurasa wa 78; Umulkheri aliyaambia macho yake, yatoke huko mbali yalikokuwa yametanga, akayarudisha darasani, yakatazamana na mwalimu Dhahabu bila yeye Umulkheri kumwona mwalimu mwenyewe.
  6. Katika ukurasa wa 152; "Usinitazame kana kwamba unataka nikwambie yaliyotokea baadae, 'nilijisemea kana kwamba ninajibu mtazamo wa Selume, 'nyinyi ndio wa kuniambia kwani nilijipata hapa penu, "Pete aliongeza na kukatisha ghafala usimulizi uliokuwa mawazoni mwake 'Mawio ya leo yanaelekea kuwa na kiza kisicho cha kawaida, "alijisemea kijakazi Sauna huku akijipindua kuusikiliza mlio wa king'ora unaosikika kwa mbali "
  7. Katika ukurasa wa 153; "Kwa mbali, anasikia mbisho hafifu langoni mwa jumba hili. Anatoka nje kwenda kuitika mbisho huu. Ghafla, uso wake unakumbana ana kwa ana na polisi! Mara anasikia moyo wake ukimwambia, "Yako ya arubaini imefika, "huku akijaribu kuvaa tabasamu na kuwakaribisha maafisa hawa nyumbani " Sauna ameisha kupata ujira wake kwa kazi hii pia, naye u tayari kuondoka asubuhi ya kuamkia krismasi. Hata sauna anapowazia matendo yake, hasa ya hivi maajuzi, anatamani kujisuta. Anahisi kwamba hafurahii kazi hii yake. Hata hivyo ndani ya nafsi yake anaukemea moyo wake ambao unataka kuipweza ari yake. "Mlaani shetani, "Sauna anauambia moyo wake. Anaendelea kujiambia kuwa yeye hakuumbiwa ujalaana, kuwa walimwengu ndio walimfinyanga upya, wakampa moyo wa ujabari. Fikiria u kigoli, kifua ndio kinaanza kuvuvumka, kisha unaamka usiku kumpata baba yako, ba-ba-ya-ko, kwenye chumba chako cha malazi. Anakutenda ya kutendwa. Asubuhi huna hata uso wa kumtazamia yeyote, wala kinywa cha kumwambia mamako kuhusu feli uliyotendewa. Na utamwambiaje mja huyu ambaye daima ni mwanamke taa, atakalo baba yeye hiliridhia bila swali, na ikitokea kwamba atauliza swali, anakuwa mpokezi wa makonde, vitisho na matusi? Hebu yatie haya kwenye mizani; baada ya mwezi mmoja unaanza kushikwa na kisulisuli, kichefuchefu cha asubuhi nacho kinakuandama. Fikra zako za kitoto zinakutuma kuwaza kuwa ni malaria au homa ya matumbo. Unammwambia mama yako ambaye anaonekana kushtuka kiasi. Mama anapokupeleka hospitali, anapasuliwa mbarika, nawe limbukeni hujui lolote. Mnapofika nyumbani, anakuhoji, nawe hujui kuficha lolote, unamwambia imekuwa mazoea baba yako kukuhujumu kila apatapo nafasi. Anajisemea kuwa hili haliwezi kukubalikal Kujipagaza uzazi na ulezi katika umri huu, tena mzazi mwenzio si mwingine, ila baba yako? Haya yote ni mawazo yanayoendelea katika fikra zake Sauna, na mbinu hii ndiyo uzungumzi nafsia.

14. Majazi

Hii ni mbinu ambayo mtunzi wa kazi ya fasihi hufananisha tabia za wahusika na majina yao halisi. Tabia zao na na majina waliyopewa.

  1. Mfano katika ukurasa wa 6; "Maekari na maekari ya mashamba katika eneo la Kisiwa Bora yanamilikiwa na nani?" Neno Kisiwa Bora limeturnika kimajazi kuonyesha kuwa ni mahali ambapo kulikuwa na mshamba mazuri, na labda yenye kutoa mazao kibaba, ndio maana yakanyakuliwa na yule Myunanai ili aweze kufanyia kilimo chake bora hapo.
  2. Katika ukurasa wa 9; "Mzee Mwimo akaona ku moto, akamua kuwahamisha wake wawili wa mwisho msitu wa Heri au Ughaishu kama walivyouita watu wa huko " Neno Msitu wa Heri limetumika kimajazi pia, kuonyesha kuwa msitu huu ulikuwa na fanaka na wa Baraka. Labda ndio maana Mzee Mwimo akaamua kuwahamishia wake zake huko, wakaishi kwa heri, badala ya msongamano uliokuwepo kwake nyumbani.
  3. Katika ukurasa wa 11;"Mimi binafsi nimefanya juu chini kuhakikisha kuwa kijiji kizima kimepata maji ya mabomba. Eneo ambalo awali likiitwa Kalahari, sasa limetwaa rangi ya Chani kiwiti " Jina Kalahari, kama lilivyoitwa eneo hib awali, lilitumika kimajazi kuonyesha jinsi eneo hilo ilikuwa limekauka mithili ya jangwa la Kalahari.
  4. Katika ukurasa wa 13; "Siku hiyo ambayo matrekta yakitekeleza amri ya Bwana Mkubwa, Ridhaa alitazama picha za majumba yake matatu kwenye mulishi wa runinga " Jina Bwana Mkubwa linatumika kimajazi kuonyesha cheo au nyadhifa alizokuwa nazo mtaajika huyo. Jina lenyewe linaonyesha kuwa cheo chake kilikuwa cha hali ya juu, na ndiyo maana akawa na uwezo wa kutoa amri, majumba ya watu kubomolewa, na wafanya kazi wakaweza kumtii, na kutumia matrekta kutekeleza amri hiyo. Katika ukurasa wa 15; Tunaambiwa kuwa mipaka ya kitabaka imebanwa. Kwa kweli haipo kwani hata nisemapo nang'ang'ania chakula-uji haswa-na aliyekuwa waziri wa fedha miaka mitano iliyopita. Hilo usilione dogo kwani unajua kuwa wenzetu hawa katika hali ya kawaida ni watu wenye shughuli na hali zao lla sasa inabidi waniite ndugu; hasa Ndugu Kaizari. Jina Ndugu Kaizari limetumika kimajazi kwani maana ya kaizari ni cheo cha mtawala wa zamani wa dola ya kirumi. Hivyo basi, jina hili lina maana ya mtawala wa zamani.
  5. Katika ukurasa wa 137; Ridhaa anamtazama Shamsi akipita hapa kama afanyavyo kila siku. Mtaa anakoishi Shamsi ni mbali na hapa, unaweza kusema Shamsi na Ridhaa ni majirani. Hili la kuwa jirani wa shamsi limetokea baada ya miezi mingi ya fikira na tafakuri. Kwa kweli, huu ni mwezi wa tatu tangu Ridhaa kuhamia kwenye mtaa wa Afueni. Afueni ni mtaa wa raia wenye kima cha juu kiuchumi. Mtu anapoutazama mtaa huu anasalimiwa na majengo ya kifahari ya ghorofa, yale ambayo yanaitwa katika janibu hizi town houses. Jina Ridhaa limetumika kirnajazi. Ridhaa maana yake ni hali ya kukubali jambo kwa hiari. Mhusika huyu anapewa jina hili kimajazi kuonyesha kuwa ameyakubali matukio yaliyomkumba yeye na familia yake, na hana budi ila kuyaendeleza maisha yake, ingawaje yamekumbwa na kiza cha mauti. Mhusika Shamsi pia amepewa jina hili kimajazi kwani maana yake ni jua la asubuhi linapochomoza na kuleta matumaini mapya kwa watu. Mhusika huyu kazi yake kuu katika jamii ni kutunga nyimbo ambazo zinaliwaza nyoyo za watu, na pia kutumika kupitishia ujumbe tofauti kwa hadhira. Kama miale ya jua la asubuhi, mhusika huyu Shamsi analeta furaha na matumaini mapya kwa watu, kupitia kwa nyimbo zake anazotunga. Mtaa wa Afueni pia ni jina lililotumika kimajazi, na lina maana ya ndani inayowakilisha mazingira haya halisi. Afueni ni tendo la kupungua kwa maradhi, au hali ya kupata hujambo. Hivyo basi mtaa huu ni mtaa ambao hujambo. Wanasema kuwa wanapoutazama mtaa huu, wanasalimiwa na majengo ya kifahari, ya ghorofa. Hivyo basi, watu wanaoishi katika mtaa huu ni watu matajiri watajika. Haina budi basi ila kuuita mtaa huu 'Afueni'.
  6. Katika ukurasa wa 146;"Nilizaliwa katika kijiji cha Tokosa mimi ndiye mtoto wanne kati ya watoto sita. Nina wazazi wawili, ila hawa ni wazazi tu, hawajadiriki kuwa walezi wangu, wala jina 'mlezi' haliwaafiki " Kijiji cha Tokosa kimepewa jina hili kimajazi. Kutokosa ni kupika chakula kwa kuchemsha tu boila kutia viungo vyovyote kwenye chakula hicho. Hali hii maanihirisha ukata au umaskini katika jamii, kwani anayetokosa chakula ina maana kuwa hana uwezo wa kubuni kununua hata mafuta ya kukaangia, au chumvi ya kutilia ladha, na pia viungo vingine. Kulingana na maelezo ya mwandishi, tunapata kuwa mtajwa aliyapiba masha magumu ya umasikini, kwani hata hawatambui wazazi wake kama 'wazazi',kwa kuwa hawakuwa na uwezo wa kuwalea na kuwakimu wana wao kwa njia inayofaa. Hivyo basi, jjna hili 'Tokosa' lililopewa kijiji hiki lilitumika kimajazi, kumaanisha kijiji chenye ukata.
  7. Katika ukurasa wa 149; "Basi nenda mwanakwenda, 'alisema Fungo, 'kichukue pia kijalaana hiki chako, hata kuwepo kwenu hapa hakuzidishi hakupunguzi"Mwanakwenda ni jina lililotumiwa kimajazi, kumaanisha kuwa huyu mke kazi yake ni kwenda tu. Tunapata kuwa anasema kwamba atatokomea kokote kule, Afadhali kuishi jehanamu kuliko kwenye husuni ya Fungo. Anapoamua kuenda, anaambiwa achukue hadi kitoto chake aende nacho, basi jina hili ni la kimajazi na linatuonyesha tabia hasa ya huyu mhusika.
  8. Katlka ukurasa wa 163;"Asante sana Neema kwa utu wako,'akasema Mtawa huyu, 'kitoto hiki kimepata kwao. Hapa tutakiita Nasibu, Nasibu Immaculata "Mhusika Neema anapewa jina hili kimajazi. Neno neema lina maana ya mafanikio aliyonayo mtu kutokana na majaliwa ya Mwenyezi Mungu au Udi zake. Neema ni mhusika mwenye juhudi kwani anakitoto kichanga kilichokuwa kimetupwa pipani na kukipeleka katika kituo cha polisi, na baadae wakakipeleka kwenye hifadhi ya watoto wasiokuwa na wazazi wao lngawa hakujaaliwa na wana, baadae anapanga mwana na anakuwa wa Baraka nyingi sana kwao, na wanapendana kama mamake mzazi na mwanawe. Hivyo basi, jina Neema lilitumika kimajazi kuonyesha sifa zake mhusika huyu. Mtawa Cizarina pia ni mhusika aliyepewa jina lake kima. jazi. Neno mtawa lina maana ya mtu mcha Mungu anayeishi katika makazi maalumu mbali na watu wengine. Mara nyingi huwa ni mwanamke. Sifa za Cizarina ni kuwa alikuwa rntu mwenye rehema, utu, mpole, na mwenye kukaribisha. Aliishi katika kituo cha watoto, akiwashughulikia wana walioletwa hapa baada ya kutupwa na mama zao wasio kuwa na utu wala hisia. Hivyo basi jina Mtawa alilopewa Cizarina lilikuwa na maana ya ndani, kuwa alikuwa mtu mcha mungu aliyeishi katika makazi ya kituo cha watoto, mbali na watu wengine, ili kuwatumikia watoto hao. Kitoto hiki cha kuokotwa kilipewa jina Nasibu Immaculata na Mtawa Cizarina. Jina hili 'Nasibu' lilipewa kitoto hiki kimajazi, kwani nasibu ni neno lenye maana iliyolingana na sifa za kitoto hiki. Nasibu kwanza lina maana ya jambo litokealo bila ya kutarajiiwa au kwa bahati. Pili, nasibu humaanisha kugundua au kujua ukoo wa mtu fulani. Hivyo basi, kitoto hiki kilikuwa na bahati kwani baada ya kutupwa pipani na mamake, hakikuliwa na majibwa yaliyokuwa yakichokora mapipa kutaftia mabaki ya chakula. Kitoto hiki pia hakikupatwa na magonjwa wala ajali yoyote huko mapipani, bali kilipata msamaria mwema, (Neema),aliyekichukua na kukiokoa. Hivyo basi, ni kitoto chenye bahati na Baraka pia. Kulingana na Una maana ya Pill ya neno Nasibu, tunaweza linganisha na maneno aliyosema Cizarina kuwa; "Najua itatokea familia hitaji kuja kutaka kumpanga kama mwanao. Siku hizi hata walio na watoto wao halisi hujitolea kuwachukua na kuwahalalisha wana wa wengine kuwa wao "Hili lina maana kuwa jina hili Nasibu lilitumika kimajazi kuonyesha kuwa siku moja mtoto huyu angepata ukoo wake.
  9. Katika ukurasa wa 169; "Mwaliko ndiye aliyeendesha gari siku hiyo; Birthday Boy akaambiwa apumzike. Walifika kwenye hoteli ya Majaliwa saa sita unusu adhuhuri; wakaketi mahali ambapo walikuwa wamezoea kuketi kila mara ambapo hawakutaka kughasiwa na pitapita za watu "Mwaliko alikuwa mhusika aliyepewa jina hili kimajazi. Neno lenyewe lina maana ya ujumbe wa kumwita mtu kwenye shughuli fulani kwa mfano sherehe. Katika kisa hiki, kuna sherehe ya kuzaliwa kwa Umulkheri, ambayo inaendelea kwenye hoteli ya Majaliwa. Jina mwaliko linatumika kimajazi hapa, kuonyesha kuwa anawaalika watu kuja kusherehekea siku hii ya maana kwa Umu. Hoteli ya majaliwa pia imepewa jina lenyewe kimajazi. Neno majaliwa lina maana ya mambo yafanyikayo kwa mapenzi ya Mungu. Mambo yanayofanyika katika hoteli hii ni kwa mapenzi yake Mwenyezi Mungu, kwani katika sherehe hizi, ndipo familia na mandugu hawa wote wanapopatana baada ya miaka mingi ya kutoishi pamoja. Mwaliko, Mwangemi, Mwangeka, Dick, na Neema wote wanafurahia kuwa pamoja kwa majaaliwa yake Mungu, kuwakutanisha tena wakiwa hai. Hivyo basi, hoteli hii inapewa jina 'Majaaliwa' kimajazi. Umulkheri pia anapewa jina kimajazi, na kuitwa 'BirthdayBoy Hili ni kkwa sababu ile ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa, na kwa kweli ilikuwa yake ya kuzaliwa kwani aliweza kukutana tena na ndugu zake na furaha ikawa tele.
  10. Katika ukurasa 63-64; Familia ya bwana Kangata ilikuwa miongoni mwa zilizoselelea kwenye msitu huu. Kwa Kangata na mkewe, Ndarine, hapa palikuwa afadhali. Hawakuwa na pa kwenda, kwani hata kule ambako walikuwa wakiishi awali, hakukuwa kwao. Walikuwa wamelowea katika shamba la mwajiri wao ambaye alikuwa akiishi jijini. Waliishi hapa hata watu wakadhani kuwa hii ilikuwa milki yao. Wengine hata walidhani kuwa Kangata na familia yake walikuwa akraba kindakindaki ya mwajiri wao. Kwa hakika hata watoto wa Kangata walipokwenda shuleni walijisajilisha kama wana wa tajiri baba yao! Jina Kangata limepewa mhusika huyu ambaye ni mzee mwenye familia na watoto wake wanakwenda shuleni. Jina kangata linatumika kimajazi kuonyesha sifa halisi za huyu mzee. Kangata ni neno lenye maana ya kushikilia jambo mpaka ufanikiwe kutaka ukitakacho. Kulingana na kisa hiki, tunaona kuwa Kangata anashikilia kuishi kwa tajiri wake, hadi watu wanamwona kama yeye ndiye tajiri mwenyewe. Hata watoto wake shuleni wanabadilisha majina lakiani baadae anahofia jina lake huenda likasahaulika kwani alikuwa amengata utajiri wa mkwasi huyu, hadi sifa zake zikadidimia.

15. Taswira

Haya ni matumizi ya lugha maneno yanayojenga picha ya hali au jambo fulani kwa msomaji. Ni mchoro au picha ya kitu au hali fulani inayotokea katika fikira za mtu asomapo kazi ya mwandishi.

  1. Katika ukurasa wa 7; Waafrika waliobahatika kuwa na makao yao binafsi walipata sehemu ambazo hazingeweza kutoa mazao yenyewe; na bila shaka hali yao iliweza kutabirika; kuvyazwa kwa tabaka la wakulima wadogowadogo, maskini, wasio na ardhi. Nadhani unaweza kukisia hali ilivyokuwa kwa familia nyingi za kiafrika. Kama vile baba Msumbili alivyokuwa akisema, jamii yetu iligeuka kuwa hazina kuu ya wafanyakazi ambamo wazungu wangeamua kuchukua vibarua kupalilia mazao yao. Kuna taswira inayojengeka kwenye akili za msomaji kuhusu jinsi hali ya familia nyingi za kiafrika ilivyokuwa, na jinsi waafrika walivyokuwa wakiishi baada ya mashamba yao kunyakuliwa na wakoloni.
  2. Katika ukurasa wa 15; Jua lilichomoza, halina ule wekundu wa jua Ia matlai ambao huleta haiba ya uzawa wa siku yenye matumaini. Naona wingu kubwa angani likitembea kwa kedi na madaha na kulifunika jua. Tukio hili linafuatwa na umeme, kisha mtutumo wa radi. Kutokana na maelezo haya ya mwandishi, tunajengewa taswira kuhusu mawingu makubwa angani yanayotembea kwa madaha na kufunika jua, kuna picha ya umeme inayojengeka akilini pia, na radi zinazofuata umeme.
  3. Katika ukurasa wa 47; "Nakusikitikia mwanangu, kuwa huna hata familia ya kuendea. Wanuna wako wote wameangamia. Mkaza mwanangu na maskini wanao waliunguzwa moto, wasibakia hata mafuvu ya kuzika!huna hata makaburi ya kuwekea hayo makoja ya maua unayotunga akilini ko "Kuna picha inayojengeka akilini mwa msomaji kuhusu maneno yake Ridhaa yanayojikita katika fikra zake tu. Jinsi familia yake ilivyo angamizwa na moto, makoja ya maua ya kuweka kwenye makaburi ya hawa walioangamia; .haya yote tunayachora kwenye fikra zetu tu. Pia Ridhaa mwenyewe anayachora mawazo haya akilini mwake tu, na kufikiri jinsi mwanawe anavyowaza kuhusiana na suala hilo.

16. Maswali ya balagha

Haya ni maswali yanayoulizwa na msimulizi au mhusika ambayo hayahitaji jibu. Wakati mwingine yaweza kuitwa mubalagha. Assumpta K. Matei pia amejikita katika matumizi ya maswali ya balagha katika kazi yake ya Chozi la Heri kama tunavyoona katika ukurasa wa kumi na moja.

  1. Katika ukurasa wa 12; "Je, huu si mchango tosha wa mtu kuitwa ndugu hata angawa mgeni?Kweli jaza ya hisani madhila?Vipi watu wawa hawa walioniita 'ndugu' na 'mzee',tukala na kunywa pamoja, tukazungumza ya kupwa na kujaa wananilipulia aila na kuyasambaratisha maisha yangu Ridhaa hakujua majibu ya maswali haya " Haya ni maswali aliyojiuliza Ridhaa lakini hayakuhitaji majibu, hivyo basi ikawa ni mbinu ya kutumia maswali ya mbalgha katika kazi ya kifasihi.

17. Ukinzani/tanakuzi

Hii ni mbinu ya kusisitiza ujumbe kwa kuambatanisha maneno ya kinyume au yanayokinzana. Kukinzana ni hali ya kutofautiana, au kuwa na ubishani, au yenye kutokubaliana. Mwandishi wa riwaya ya Chozi la Heri amejikita katika matumizi ya ukinzani katika kuwasilisha maudhui yake kwa njia zifuatazo.

  1. Katika ukurasa wa 14; "Na usidhani ni mazingira mageni, kweli si mageni, si mageni kwani tu mumu humu mwetu, hatumo ughaibuni wala nchi jirani. Tu katika jimbo lile lile tulilozoea, kilichobadilika ni kijiji tu, ni kama kutoka chumba cha malazi, kwenda sebuleni!"Kuna mkinzano wa mawazo kuwa mazingira yamebadilika ilhali la, ni yale yale tu ya awali, waliyozoea, ni sehemu tu wamehama wakaenda katika sehemu tofauti, ya mazingira yale yale. Anathibitisha haya kwa kufananisha hali hii na kutoka chumba cha malazi, kwenda sebuleni.
  2. Katika ukurasa wa 15; "Mipaka ya kitabaka imebanwa. Kwa kweli haipo kwani hata sasa nisemapo nang'ang'ania chakula-uji haswa-na aliyekuwa waziri wa fedha miaka mitano iliyopita " Kuna mkinzano wa mawazo tunapoambiwa kuwa kwa sasa, wanang'ang'ania chakula, la sio chakula, bali uji, na aliye kuwa waziri wa fedha miaka mitano iliyopita.
  3. Katika ukurasa wa 16; Haya ni matokeo ya ubahaimu wa binadamu kwa mbali namwona Ridhaa-mwamu hasa-akitafuna kitu fulani, nadhani ni mzizi mwitu! Ridhaa, kweli Ridhaa kula mzizi!daktari mzima!mkurugenzi mzima wa wakfu wa matibabu nchini. Wanasema wajuao kuuwa samba akikosa nyama hula nyasi. Wazo hill linaleta mkinzano Kwenye fikra za msomaji kwani si kawaida ya daktari mzima na mwenye cheo na wadhifa aina ile kua akila mizizi msituni, lakini lisilo budi hubidi, na hivyo basi, inambidi aile mizizi tu, badala ya kuangamizwa na njaa.

18. Tashbihi

Hii ni mbinu ya lugha inayolinganisha vitu au hali mbili tofauti kwa kutumia maneno ya kulinganisha; kama, mithili ya, sawa na, au pia ja. Assumpta K.Matei amejikita katika matumizi ya mbinu hii ya tashbihi katika kazi yake ya kuwasilisha maudhui kwa msomaji kwa njia zifuatazo;

  1. Katika ukurasa wa 16; "Tazama uso wake ulivyovamiwa na majeraha, kikwi. Tazama tambo lake lililoumbuka. Amevimba na kuvimbiana kama dongo la unga ngano baada ya kutiwa hamira. Lakini yeye hana la hamira!" Uso wake unalinganishwa na unga wa ngano uliotiwa hamira kwa jinsi ulivyo vimbiana kwa majeraha.
  2. Katika ukurasa wa 49; Sasa ninaamini usemi wa Tila wa kila mara kuwa: "Usicheze na uwezo wa vijana, wao ni kama nanga. Huweza kuzamisha na kuiongoa merikebu " Uwezo wa vijana unalinganishwa na nanga, ambayo iko na uwezo wa kuzamisha na kuongoa melikebu.

 

 

Mbinu za sanaa.

1. Kinaya

Hii ni mbinu inayofanya matukio katika kazi ya Sanaa kuwa kinyume na matarajio ya hadhira.

  1. Katika ukurasa wa 5; "Naona umeanza kuitia akili yangu kwenye mtihani mgumu. Unanichanganya hasa! Kwanza sijui wapi kapata moto wa miaka hamsini " Ni kinaya kuwa mototo ana miaka hamsini, kinyume na matarajio ya kawaida ya kuwa mototo ni yeyote aliye chini ya umri wa miaka kumi na minane.
  2. Katika ukurasa wa 62; Mwangeka aliajiriwa na kupanda ngazi moja baada ya nyingine hadi alipoenda kudumisha Amani kwingine, na mkewe kufa kutokana na ukosefu wa usalama nchini mwao huu ukawa mwisho wa ndoa yao ya miaka mitatu. Ni kinaya kuwa Mwangeka anaenda kuweka usalama kwenye mataifa mengine ilhali kwao bado usalama ni balaa, - na hili linasababisha kuuliwa kwa mkewe.
  3. Katika ukurasa wa 65; Alipofikiria kila asubuhi, kama alivyo_ sikika akisema, alihisi kinaya. Wanawe walipoenda kusomea Ngambo, kama wafanyavyo wana wa viongozi ambao wanaiona elimu ya humu kama isiyowahakikishia mustakabali mwema raiya wake, ... Ni kinaya kuwa viongozi wa nchi za kiafrika wanaiona elimu ya humu kuwa duni ilhali ni wao wanaoisimamia elimu yenyewe; badala, wanawapeleka Wana wao kusomea nchini za mbali ambako wanadhania kuwa kiwango cha elimu ki juu.
  4. Katika ukurasa wa 65; This country has nothing to offer. Nchi ambayo hata walio na shahada tatu bado wanalipwa mishahara ya mkia wa mbuzi!mimi sitakufa maskini acha niwekeze huku mbali ambako Sina hofu ya mali yangu kuibwa au kuchomwa na waivu wangu... Ni kinaya kuwa wana hawa wanakataa kurudi kwao nyumbani walikozaliwa kwa kuona kuwa hali ya maisha huku ni duni sana na si ya kiwango walichofikia huko ughaibuni walikoenda kupata elimu.
  5. Ni kinaya kuwa kiongozi wa dini anawaambia watu 'amani iwe nanyi'ilhali hawa watu hawana Amani kwani chakula, mavuzi na makao hawana. Wanaishi msituni kama wanyama pori; Katika ukurasa wa 28;"...haikosi alikuwa kiongozi wa kidini-alitoka na kutusalimu: peace be with you,.

2. Sadfa

Sadfa ni mgongano wa vitendo viwili vinavyohusiana kana kwamba vimepangwa, japo havikuwa vimepangwa.

  1. Katika ukurasa wa 175; "Tesi!sadfa gani hii?Unafanya nini hapa?Ulikuja lini jijini humu?Yu wapi wifi Nema?Niliskia motto wenu amehitimu chuoni!Ajabu hatujapata kukutana naye, 'Mwangeka aliyauliza maswali haya moja baada ya lingine bila kumpa mwenzake muda wa kujibu hata la kwanza wengine walimtazama wakishangaa kwa nini hata hamwachi mgeni akawasalimu "Hii ni sadfa kubwa sana mimi huwa siji hapa sana lakini mwanangu Mwaliko alingangania kunileta hapa kwa chakula cha mchana " sadfa inajitokeza wakati Mwangeka na Tesi wanakutana mahali pamoja, ilhali hawakuwa wamepanga lolote kuhusu mkutano wao. Jambo hili linatokana na uwezo wake Mungu bali si kwa mipango ya hawa wa wahusika wawili.
  2. Katika ukurasa wa 175; "Nakumbuka sana. Na kweli hii ni sadfa kwa sababu pia ni siku ya kuzaliwa kwa binti yangu Umulkheri " Inasadifu pia kuwa wote wanakutana pamoja siku ya kuzaliwa kwake Umulkheri.
  3. Katika ukurasa wa 183; "Tunawatarajia walioenda sokoni kurui. Kisadfa, wakati huo huo, babu Mwimo Msumbili akawa ndio anatoka kwenye shughuli zake za usili (ujaji)" Inasadifu kuwa wakati watu wanapotarajiwa kuwa wakirudi, wakati huohuo babu Msumbili akawa amewasili kutoka shughuli zake.

 

3. Kisengere nyuma.

Katika mbinu hii, mwandishi hurudi nyuma na kusimulia kisa kilichokuwa kimetendeka kabla ya alichokuwa anasimulia. Aidha mwandishi hubadilishawa wa masimulizi kuwa wakati wa kisa hicho. Mbinu hii hutumika sana kuonesha mhusika anapokumbuka kitu, au kutuelezea jinsi mambo yalivyoanza. Mbinu hii pia hujulikana kama mbinu rejeshi.

  1. Katika ukurasa wa 1;"Sasa anakumbuka vyema. Anakumbuka kupepesa kwa jicho lake la kuli kwa muda wa wiki mbili mtawaliwa. Anakumbuka anguko aliloanguka nalo sebuleni mwake, akatafuta kilichomfanya kujikwaa asikione. Anakumbuka mavune yaliyouandama mwili wake na kuunyongonye za kwa muda hata pasi na kuudhili kwa kazi yoyote ya haja. Anakumbuka jeshi la kunguru lililotua juu ya paa ya maktaba yake ya nyumbani adhuhuri ya juzi ile " Ridhaa anayakumbuka yaliyokuwa yametendeka ingawa ilikuwa miaka mingi iliyopita.
  2. Katika ukurasa wa 3;"Katikati ya mito hiyo ya machozi, Ridhaa aliileta picha ya maisha yake mbele ya kipaji chake. Alijiona akiamka asubuhi ambayo ilizaa usiku wa jana, usiku ambao ulitandaza kiza maishani mwake. Kwa mbali alianza kuskia sauti ya mkewe ikilia kwa kite "Anakumbuka akiskia mlipuko mkubwa, kisha kushikwa na uziwi wa muda uliofwata na sauti nyingine ya mkewe, yamekwisha!" Haya yote ni mawazo yanayomjia Ridhaa. Ni matukio yaliyotendeka zamani lakini mawazo haya bado yako akilini mwake, hayajafutikatna anayarelea kila wakati kwenye fikra zake.
  3. Kurasa 9-10; Hapa Ridhaa anayakumbuka maisha yao tangu utotoni hadi akiwa mtu mzima, mkondo ambao maisha yake yamechukua. Anakumbuka jinsi siku ya kwanza shuleni alivyotengwa na wenzake katika mchezo wao wa kuvuta, mchezo wa kusukuma vifuniko vya chupa za soda kwa ncha za vidole vyao. Anakumbuka mwanafunzi mmoja ambaye kwa kawaida aljpenda kuwachokoza wenzake akimwambia, wewe ni mfuata mvua. Hatutaki kucheza nawe. Umekuja hapa kutushinda katika mitihani yote. Wewe ndiwe unayetuibia kalamu zetu.
  4. Katika ukurasa wa 13; Siku hiyo ambayo matrekta yakitekeleza amri ya bwana mkubwa, Ridhaa alitazama picha za majumba yake matatu kwenye mulishi wa runinga. Anayatazama hata sasa katika ruya yake. Majumba haya sasa yamegeuka dongo. Anayasoma usingizini na kutoa kidoko ambacho tribu kimwamshe. Hili la sasa ni pigo la pili ambalo ni kali zaidi. Hapa pia Ridhaa anaendelea kuyawaza matukio yaliyompata nyakati zile ambazo mali yake ilipoharibiwa.
  5. Katika ukurasa wa 45; Sasa Ridhaa anapotazama picha iliyo mbele ya macho ya akili yake, anajua fika kuwa Tila wake hayupo, kilichobaki ni kumbukumbu ambazo zinang'ata kama mkia wa nge, kumbukumbu ambazo kila mara zilifungua Chemchemi za machozi, yakalovya kifua chake. Ridhaa anakumbuka mwana wake na kulia kwa machungu aliyokuwa nayo moyoni mwake.

4. Nyimbo

Ni maneno na sauti zilizopangwa na huandamana na muziki unaotokana na ala za kimuziki kama vile ngoma saut hizi za muziki pia huwa zimepangwa ili kuandamana maneno vizuri na kwa urari. Wimbo huweza kutuumika kupitisha ujumbe wa mwandishi ambao ni dhamira. Katika riwaya hii, kuna matumizi ya nyimbo katika matukio tofauti:

  1. Katika ukurasa wa 20; "Wote walikuwa wakighani rnkarara huu: Tawala Wahafidhina tawala, Mwanzi wetu tawala Waha. fidhina tawala 'Wimbo huu ulitumika wakati wa shughuli kupiga kampeni kabla ya uchaguzi kufika. Wimbo wenyewe unampigia debe kiongozi anayetakwa na wananchi.
  2. Katika ukurasa wa 49;"Mama mtu angemshika mabegani na kumwimbia mkarara mmoja wa wimbo pendwa wa kidini:
    Salama, salama
    Rohoni, rohoni
    Ni salama, rohoni mwangu"
  3. Katika ukurasa wa 60; "Wengine walijilazimisha kupiga ukemi, eti wanaomboleza kifo cha Dedan Kimathi. Walianza kulizunguka lile 'jeneza' wakiimba mbolezi. Walimwimbia Kim wao,  kwaheri
    Kwaheri we Kim wetu
    Kwaheri, kwaheri
    Kwaheri we Kim kipenzi chetu kwaheri
    Kwaheri na malaika wakungoje.
    Umewaacha wazazi kwa majonzi
    Kwaheri, kwaheri

    umewaacna nauguzo kwa ukiwa
    Kwaheri na mababu wakulaki peponi.

  4. Kurasa 129-135; Huu ni Wimbo ambao Shamsi aliuimba kuhusiana na hali ya kisiasa iliyokuwemo nchini. Haukuwa Alimwimbia Chupa ambaye alikuwa kipenzi chake.
    Alikuwa mboni yajicho lake, mwendani wake.
    Alikuwa shujaa, Hakuhisi shinikizo la majabali,
    Alimzingira kwa mahangaiko pia,
    Alimjaza kwa tuo,
    Akampa maji matamu
    Maji hayo yakawa dawa mujarabu.
    Dawa hiyo ikawa ya kuuguzia banguzi.
    Waliomsababishia mahasidi.
    Chupa yake, alijua pia walimcheka
    Wachunguliao kwenye madirisha
    Waliokwenye maroshani yao "

  5. Kurasa 136-137; Kwa sauti ya chini, Ridhaa alisema kuwa Shamsi anasikika kama amebadilisha wimbo wake. Huu wa leo unahisika kama wa kiumbe mwenye maumivu zaidi, mapigo yake hasa ni ya mbolezi, ni tofauti na yale majigambo yake ya kila siku, Akaongeza Ridhaa huku akiyaghani majigambo Ya Shamsi kwa sauti ya chini kama anayeyatia maneno ya majigambo yenyewe kwenye mizani. Anasema kuwa hawa wanaomfuata wanamwacha kwa ukoo wake mtukufu. Kwa jadi yenye majagina, wa mioyo na vitendo Wananicha kwa kuwa wa kwanza kijijini Kuvishwa taji kwa kusoma kwa bidii Kwa kuwa jogoo wa kwanza kuwika kwenye anga za elimu Idhini nikapewa ya kuendeleza utafiti, Nikapewa mamlaka ya kuwaza kwa niaba ya jamii.

5. Matumizi ya barua.

  1. Lunga anapokea barua rasmi ya kumfuta kazi. Ni fupi lakini yenye ukali na kukatisha tamaa (Uk 72;) Barua yenyewe iliandikwa na bwana Kalima ambaye alikuwa mwenyekiti wa Halmashauri ya kitaifa ya uhifadhi wa nafaka. Yeye ni mkurugenzi wa Halmashauri ya Kitaifa ya Uhifadhi wa Nafaka. Anamwandikia bwana Lunga waraka na kumwambia kuwa amestaafishwa kazi. Anastaafishwa kazi kutokana na gharama ya uzalishaji mali ambayo inaendelea kupanda kila uchao, shirika hilo limekumbwa na changamoto kubwa ya kifedha. Halmashauri inayosimamia shirika hili imeamua kupunguza idadi ya wafanyakazi katika ngazi za juu, kama hatua mojawapo ya kudhibiti gharama ya uzalishaji. Shirika hilo lilisikitika kumwarifu Lunga kuwa yeye ni mmoja wa walioadhirika na kwamba ameachishwa kazi kuanzia tarehe 31 mwezi wa Julai, mwaka huo. Shirika hili lilimshukuru Lunga kwa uwajibikaji wake alionao katika utenda kazi wake. Pia walimshukuru kwa mchango wake katika kuliendeleza shirika hilo. Shirika hilo pia lilimtakia kila laheri bwana Lunga, katika shughuli zake za kitaaluma.
  2. Lunga pia anaandikiwa waraka mwingine mfupi na mkewe Naomi (uk 81) Mkewe Naomi anamwambia kuwa ameondoka. Ameenda kutamba na ulimwengu, na huenda akaambulia cha kumsaidia mumewe kuikimu familia yaao. Anasema kuwa anasikitika kwa uchungu atakaousababisha kwa mumewe na pia wana wao. Baada ya kumwandikia waraka huu, anamwambia kwaheri. Barua hii pia inamuumiza sana Lunga moyoni, kwa aliachiwa watoto na mkewe awalee peke yake. Pia ni uchungu kwani alimdhamini na kumpenda sana mkewe Naomi ambaye sasa amemwacha katika hali ya upweke.
  3. Subira pia anamwandikia mwanawe Mwanaheri barua, akimjulisha kuwa yeye amekwenda zake na labda hawatapatana tena maishani. Barua hii pia ni ya kukatisha tamaa kwani Mwanaheri alipoisoma barua ile, alihisi kuwa imejaa ujumbe wa mauti (UK.95)Barua hii inaandikwa tarehe mbili mwezi wa sita mwaka wa elfu mbili na tisa. Inaandikwa kwa mpenzi wake Mwanaheri. Anasema kuwa, Mwanaheri atakapoisoma barua ile, labda yeye hatakuwa hapo au pia katika ulimwengu huu. Ila tu ajue kuwa imembidi kuondoka. Anasema kuwa hakudhamiria kuondoka au hata kuawaacha kwa siku moja yeye na Lime, wala hata baba yao. Lakini uvumilivu wake ulishindwa kumletea mbivu. Anasema kuwa amemeza shubira kwa miaka mingi, kubaguliwa, kufitiniwa na kulaumiwa kwa asiyoyatenda. Anaendelea kusema kuwa amechoka kukilovya kifua chake kwa machozi kila mara. Amechoka kuitwa mwizi wa mayai ambayo kuku wayatagayo amewafuga yeye. Amechoka kuitwa mwizi wa mali yake. Amechoka pia kupigania penzi la mwenzi na mavyaa na mwenzi mwenyewe haoni anampagaza machungu. Anajuta sana kwa kuwaacha wana wake. Hata hivyo, anaomba jambo moja tu kwa mwanawe Mwanaheri: kuwa amtunze Lime, na Zaidi mno wamtii baba yao na pia kuzingatia masomo yao. Anaomba pia Mwenyei Mungu aweze kuwaepusha kutokana na maovu yote. Asitokee mja akawadhulumu furaha yao jinsi tu ulimwengu ulivyomhini utulivu. Baadaye anawaambia wanawe kwaheri na kuwaambia kuwa wangeweza kupatana siku moja, inshallah. Hiyo ikawa ni barua yake Subira ambaye alikuwa mamke Mwanaheri.

6. Hotuba

Haya ni mazungumzo yanayohusu jambo maalum kwa mfano siasa ambayo hutolewa kwa hadhira na mtu mmoja.

  1. (uk 112-114), Hotuba hii inatolewa na Apondi, Alianza kwa kuiita hadhira kwa maneno, "Mabibi na mabwana"Anaendelea na kusema kuwa swala la usalama haliwezi tena kupuuzwa. Anasema kuwa usalama umekuwa mojawapo ya mahitaji ya kibinadamu. Na kwa hakika, tunaweza kusema kuwa usalama ni mojawapo ya mahitaji ya kibinadamu. Kwa hakika, usalama ni mojawapo ya mahitaji ya kimsingi. Anasema kuwa bila usalama, binadamu hawezi hata kushiriki katika shughuli za kuzalisha mali, hivyo hata mahitaji yake mengine ya kimsingi kama vile chakula, malazi na makazi hayawezi kukidhiwa. Anasema kuwa kila binadamu ana jukumu la kudumisha Amani na usalama. Hata hivyo, wafanyakazi wa umma, na hasa polisi na wanajeshi wana jukumu kubwa zaidi la kudumisha usalama na Amani kuwa kila mmoja anafaa kupakata mikono na kungoja kuliniwa, la hasha!Kila mmoja wetu anastahili kuhakikisha kuwa ameepuka vitendo vya Khalifu. Anasema kuwa pia ni vyema mtu kuwaangaza wahalifu wakati wote. Vikosi vya polisi na wanajeshi vimefunzwa maarifa ya kukabiliana na kadhia za jinai na upelelezi; Kwa hivyo,wana dhima kubwa zaidi ya kudumisha Amani. Aidha, wana ujuzi wa njia mwafaka za kutatua migogoro na kupalilia maridhiano. Wanajua ni lini watashambulia na ni lini watarudi kinyumenyume, kuepuka shambulizi la adui. Anawasihi waajibike zaidi katika kazi zao, kwa kuwa wamefunzwa effective communication and conflict resoluion.
  2. Kurasa za 68-69;Kila ijumaa wakati wa gwaride, ungemskia akihutubia kwa mhemko "Mkuu wa shule, walimu na wanafunzi, suala Ia uhifadhi wa mazingira ni jukumu la kila mmoja wetu. Tumeona jinsi misitu ilivyovamiwa na viongozi wenye mate ya fisi. Nasikia baadhi ya vinara wa taasisi mbalimbali za umma wamewaacha wanyama kama mayatima kwa kuwapoka makazi yao. Maelfu ya maekari ya misitu yamefyekwa na kujengwa viwanda. Badala ya miambakofi na miti mingine inayosafisha hewa, michai imetwaa nafasi yake. Wanaohusika na matendo haya wanapoulizwa huidai kuwa michai si adui ya mazingira!wengine wanasema kuwa misitu haina budi kukatwa ili kupanda mimea inayotoa chakula, kwani jamii lazima ijitosheleze kwa chakula. La kuhuzunisha ni kwamba hawa hawa wanaosema hivyo ndio wanaokita majengo ya kifahari katika sehemu ambazo zinastahili kutengwa upanzi wa chakula! Wengine wamediriki kunyakua hata madhabahu kwenye mlima wa Nasibu ili kujenga hoteli kubwa kitalii. Wazee wetu hata hawana mahali pa kuchomea kafara! Tunakata miti bila kupanda mingine. Tazameni shuleni humu! Hata mabustani ya maua tunashindwa kuyastawisha! Tukiendelea hivyo, bila shaka sehemu yetu itazidi kuwa jangwa "

7. Mahojiano

Hii ni mbinu ya kuuliza maswali ili kufahamu maarifa anayojua mtu. Mahojiano hutumika mtu atakapo kupata taarifa fulani kutoka kwa mtu mwingine anayehojiwa.

  1. Kuna mahojiano yanayoendelea kwenye kituo cha polisi, wakati mwanapolisi aliye katika zamu anapomdadisi Umulkheri (uk 83). "Umasema watoto walipotea?unajuaje walipotea?" "Kwanza walikuwa wamevaa vipi walipoondoka nyumbani? "Walibeba nini?walikwambia wameenda wapi?Kwanini watoto wenyewe hawajaandikisha kupotea kwao kwenye "unasema pia kijakazi wenu hayupo?"akauliza askari. "na hakukujuza alikokwenda?"aliongeza askari yule. "Jina la huyo kijakazi?"akauliza yule askari wa kwanza.
  2. Katika ukurasa wa 100; "pacha aliyeonekana kutoyaamini maneno yangu alinidadisi: ' "una hakika na unayoyasema?"

8. Taharuki

Hii ni mbinu ya kusimulia au kuandika riwaya kwa kufanya hadhira au wasomi wajawe na hamu ya kutaka kujua kitakachotokea baadaye; hamu ya kutaka kuendelea kusoma. Baadhi ya hadithi huishia kwa taharuki na kulazimisha hadhira yake ijikamilishie au ibaki ikijiuliza maswali. Taharuki pia yaweza kujitokeza katika hali ya kawaida wakati jambo fulani linatarajiwa kutendeka, aidha jambo nzuri au la kukatisha tamaa.

  1. Katika ukurasa wa 19; "Mijadala hii ilizua na kukuza migogoro isiyomithilika. Hali ya taharuki ilitamalaki, vyombo vya dola vikatumwa kudumisha usalama katika vijiji, mitaa ikajaa sisimizi walioshika bunduki. Hali hii ilileta chachawizo zaidi katika vijiji na mitaa " Katika hali hii, kulikuwa na taharuki juu ya mambo yaliyotarajiwa kutokea baada ya mtafaruku uliokuweko kwa sababu ya siasa.
  2. Katika ukurasa wa 152; "Usinitazame kana kwamba unataka nikwambe yaliyotokea baadaye, 'nilijisemea kana kwamba ninajibu mtazamo wa ndio kuniambia kwani nilijipata hapa penu, oete aliongeza na kukatisha ghafla usimulizi uliokuwa mawazoni mwake. Pete anatuacha na taharuki bila kutuambia yaliyotokea baadaye. Anakatisha masimulizi yake kwa ghafla.

9. Masimulizi

Haya ni maelezo ya jambo fulani kwa njia ya kusimulia. Mwandishi ametumia mbinu hii kuwasilisha maudhui yake kwenye riwaya hii.

  1. Katika ukurasa wa 16; "kumbe hata wewe shemeji Kaizari upo? Ridhaa ananiuliza kwa unyonge. Hili linanizindua kutoka lepe langu la muda, linanitonesha kidonda si haba 'Ndio tu hapa na wengine wengi, 'ninamjibu, kasha ninaanza kumsimulia yaliyojiri kana kwamba ni mgeni wa hali ile baada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya, kiongozi ambaye kulingana na desturi za humu mwetu hakustahili kuiongoza jamii ya wahafidhina, kisa na maana, alikuwa mwanamke, mbingu zilishuka. Watu walishika silaha kupigania na uhuru wao; uhuru ambao walidai kuwa hawakupewa, waliupigania "Anasimulia jinsi uongozi wa nchi ulivyo, na jinsi uhuru ulipiganiwa.
  2. Katika ukurasa wa 146; Pete anasimulia kisa cha maisha yake kwa marafiki zake akina Selume "Pete alifungua pazia la jukwaa la maisha yake, akaanza kuwasimulia akina Selume kisa chake mwanzoni, kimya kimya moyoni akisema kwamba huenda wakakielewa kiini chake kutenda alichokitenda 'Nilizaliwa katika kijiji cha Tokosa. Mimi ndiye mtoto wa nne katika familia yenye watoto sita. Nina wazazi wawili, ila hawa ni wazazi tu, hawajadiriki kuwa walezi wangu, wala jina mlezi haliwaafiki. Naona mnaniuliza vipi mtu kuwa mzazi na asiwe mlezi lla nataka mjue kuwa haya hutokea mara nyingi. Hamuwezi kujua haya nyinyi, yaonekana mlilelewa kwa nun na cerelac, hamjaonja shubiri ya maisha " "Maneno haya yalifunga pazia la jukwaa la mawazo ya Neema, akaanza kumsimulia mumewe, la, kuisimulia hadithi aliyoitunga yeye mwenyewe kwa matendo yake miaka kumi iliyopita 'siku hizo nilikuwa nikifanya kazi kama hasibu mwandamizi katika hazina ya kitaifa, 'alianza Neema "Asubuhi moja ya ummande ilinipata nimeshuka kutoka kwenye daladala, nashika tariki kuelekea afisini. Mzizimo wa Julai ulidhulumu ngozi yangu laini, nikalaani msongamano wa magari jijini, ukosefu wa mahali pa kuegeshea, na ada kubwa iliyotozwa walioazimia kuendesha magari yao hadi kitovu cha jiji. Laiti vinara wa jiji wangeweza kuboresha hali, ningeweza kulitumia gari langu " Neema anamsimulia mumewe Mwangemi kuhusu matukio yalivyokuwa siku hizo zilizokuwa zimepita.
  3. Katika ukurasa wa 162; "Nilimsimulia Cizarina kisa changu alikisikiliza bila kuonyesha hisia yoyote ya kushtuka ila uso wake ulitwaa vituta vilivyoficha huzuni na kuudhika " Neema anamwelezea Cizarina kwa njia ya masimulizi jinsi alivyoweza kukiokota kitoto kilichokuwa kimetupwa kwenye jaa la taka ili kiage dunia ama kipate msamaria mwema wa kukichukua kitoto kile.

10. Mazungumzo

Haya ni majailiano ya jambo fulani baina ya watu wawili au zaidi. Kila mtu huzungumza kwa wakati wake, na kumpa mwingine nafasi ya kusikiliza.

  1. Uk 38; "Tila: Shikamoo baba. Ridhaa: Marahaba mwanangu. Umeshindaje?
    Tila: (kwa uchangamfu)vyema. Baba, leo somo letu la fasihi lilivutia mno.
    Ridhaa: Kwani waliwafunza nini huko?Ama ni zile siasa zenu zisizoisha? Leo mwalimu Meli alitueleza jinsi mifumo ya uzal-
    Tila: ishaji mmali ilivyobadilika, kuanzia wakati wa ujima, ukabila, ubwanyenye, ujamaa hadi sasa tunapopambana na utandawazi. Lakini anasema ujamaa si rahisi kutekelezwa.
    Ridhaa: (kwa wasiwasi) Kipi kiini hasa cha kufunza mada hii kwa watoto wakembe kama nyinyi?siku zetu sikumbuki kuona mada hii hata katika mtalaa wa kidato cha sita! Nadhani umesahau baba. Suala hili ulisema limeshu-
    Tila: ghulikiwa katika kazi za kifasihi kama vile Mashetani, ile tamthilia ya Hussein inayoisawiri migogoro ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ya baada ya ukoloni lsitoshe, mwalimu alitaka tu kuonyesha kwamba upo uhusiano kati ya mfumo wa kiuchumi wa kislasa alituambia kwamba mfumo wa kiuchumi hudhibitiana na mfumo wa kisiasa. Utawala huteuliwa makusudi kuendeleza mfumo uliopo wa kiuchumi kwa maslaya watawala na tabaka ambalo linazimiliki nyenzo za uzalishaji mmali. (kama aliyeudhika).Naona mmeanza kuingilia
    Ridhaa: Nyanja ambazo ni michezo ya wengine na wanafaa kuachiwa wao. Lakini baba, unajua hatuwezi kuyafumbia macho
    Tila: mabadiliko yanayozikumba jamii zetu kwa mfano, kura ya maoni ya hivi maajuzi yaonyesha kwamba majimbo mengi nchini yanamuunga mkono Bi. Mwekevu Tendakazi. Ameongoza kwa asilimia sitini. Mpinzani wake wa karibu wa kiume ana asilimia thelahini. Mwalimu alisema kuwa wakati umefika kwa jamii kuacha kuacha kupima uwajibikaji wa mtu kwa misingi ya kijinsia. Wote waume kwa wake wapewe nafasi sawa. Si kwamaba napinga hili. Ningekuwa hasidi wa
    Ridhaa: usawa wa kijinsia nisingewapelekeni nyinyi shuleni. Ningemshughulikia Mwangeka tu ambaye jamii inaamini kuwa ndiye mridhi wa mali yangu. Hata hivyo, naona kwamba ni mapema mno kuanza kulitolea hukumu suala la nani anaongoza. Huku kutakuwa kukata mbeleko kabla ya mtoto kuzaliwa. (akichekacheka)Dalili ya mvua ni mawingu baba. Mara hii kama wapiga kura tumeamua kujaribu mbinu mpya za kilimo. Haya matumzi ya visagalimma yameanza kupitwa na wakati.
    Ridhaa: Tila!Kummbuka hapo ulipo hata kura yenyewe hauna!Naona wamekutia maneno ya uchokozi. Ngojea kipindi kingine cha uchaguzi kifike, utakuwa na haki ya kuchukua kura na kumpigia mwanamke umtakaye. Kwa sasa itabidi utosheke na chaguo letu!
    Tila: Lakini baba, sijasema tunataka kiongozi mwanamke. Sisi tunataka kiongozi yeyote awe mwanamke au mwamume, atakayeweza kulielekeza jahazi hili letu kwenye visiwa vya hazina. Tufikie kilele cha maendeleo pale tutakapofikia malengo ya nkimaenndeleo ya kimilenia. Kiongozi ambaye ataendeleza Zaidi juhudi za kukabiliana na na wale maadui ambao wewe daima huniambii kuhusu: umaskini, ujinga, magonjwa (akisita kumtazama baba) uhaba wa nafasi za kazi na ufisadi. Je, huu sio uliokuwa muono wa waliopigania uhuru?siyo ambayo viongozi waliochukua hatamu za uongozi kutoka kwa watu weupe waliyofanya juu chini kutekeleza?
    Ridhaa: Na nani akasema viongozi waliopo hawajajikuna wajipatapo?Huoni hata wahasiriwa wa magonjwa sugu kama vile iri na hata UKIMWI wana dawa za bei nafuu za kuwawezesha kudhibiti hali hizi?Je, serikali haijaanzisha sera ya elimu bila malipo kwa shule zote za msingi?Haijagharamia karo za shule za kutwa katika Shule za upili?kumbuka pia na ule mradi wa kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi kuanzia darasa la kwanza ana kipakatalishi chake?Ushaona?Hivi karibuni, nchi Inafikia ile vision 2030 hata kabla ya 2030 yenyewe! Je, ni tume ngapi za kuchunguza kashfa za kifisadi ambazo zimeundwa?Hizo si juhudi za kupigana na ufisadi?Serikali imetumia bilioni ngapi katika shughuli ya kuhesabiwa kwa watu mwaka jana?Unajua sababu ya shughuli hii voiongozi wanataka kupata takwimu sahihi Zaidi na za kutegemewa, zitakazowawezesha viongozi kujua mahitaji ya kiuchumi na ya kijamii ya kila jimbo. Huduma zitaweza kutolewa kwa urahisi zaidi katika kila eneo la ugatuzi.
    Tila: Na umaskini, je, baba?Mara nyingi hukuona umejishika tama ukilalamikia asilimia kubwa ya raia ambao hawamudu hata gharama ya matibabu ya kimsingi si wewe unayesema kwamba vifo vingi vya watoto chini ya miaka mitano husababishwa na magonjwa yanayotokana na ukosefu wa lishe bora, pamoja na wazazi na walezi kutopata elimu kuhusu njia za kujikinga dhidi ya baadhi ya magonjwa?
    Ridhaa: (kwa msisitizo)Kumbuka kwamba haya malengo ya kimilenia hayajaanza kupigiwa Shabaha sasa. Kilichobadilika ni istilahi ya kuyarejelea jawapo ya haki za kibinadamu ambazo wanaharakati mapinduzi walipigania ni matibabu boila malipo kwa wasioji. weza kiuchumi, na elimu ya lazima, na bila malipo kwa watoto wote, kufikia umri wa miaka kumi na mitano. Na nadhani kile ambacho mwalimu wenu angewasisitizia zaidi ni kwamba vijana wana jukumu la kuelimishana kuhusu nafasi ya kila mmoja wao katika kuuboresha uongozi uliopo sasa. Watumie vipawa vyao kwa njia endelevu ili kusaidia katika kuzalisha nafasi za kazi badala ya kungojea serikali iwatilie riziki vinywani. Nchi haijengwi kwa mihemko na papara za ujana. Na suala la umaskini?Naona hili ni tatizo la kijaamii. Mathalan, watu wanaoishi katika sehemu kame wanastahili kujitahidi kuvumbua mbinu za kuyahifahi maji ya mvua. Pia kila eneo la ugatuzi halina budi kuwashajiisha wataalamu wake kujizika katika uafiti ili kuvumbua rasilimali zinazopatiakana katika maeneo haya, hili litawawezesha maeneo yenyewe kuzitumia raslimali kwa njia endelevu. Haya yote yatasaidia kupunguzu mng'ato wa uhawinde.
    Tila: Watayahifadhi vipi maji haya kama mvua yenyewe hainyeshi? Baba, wewe mwenyewe unalalamika kiangazi ambacho kimmezikumba sehemu mbalimbali nchini lsitoshe, mwalimu asema kwamba asilimia kubwa ya wakazi wa sehemu kame haiwezi hata kumudu kula mara mbili kwa siku. Hizo hela za kununulia matangi ya kuhifadhia maji na kufanyia utafiti watazitoa wapi?
    Ridhaa: Basi watumie maji ya mabomba si lazima wahifadhi ya mvual Na huyo mwalimu naona anapanda mbegu za uhasama kati ya viongozi na vijana. Vijana hawapaswi kungojea kufanyiwa kila kitu. Tumewapa nyavu za kuvulia, nao wanaona wangoje kuletewa samaki!
    Tila: (akionyesha kuvunjika moyo)Baba!Umekuwa kama yule kiongozi wa kifaransa, unayeniambia wewe kila mara, ambaye alipoambiwa kuwa wanyonge hawakuwa na mkate alisema, "if there is no bread, let them eat cake!" Watu wengi huko mashambani hutegemea mashamba, mvua haijakubali kunyesha kwa muda. Wengi wa wanaofanya kazi za ajira, hufanya kazi za kijungujiko. Sasa mabomba yatatoka wapi?na hata kama mabomba yenyewe yangekuwepo, juzi nimeskia kwenye runinga kwamba bwawa la Fanisi ambalo ndilo lililotegemewa sana kutoa maji kwenye sehemu kame halitasambaza maji tena kwa sababu kiwango cha maji kimeshuka sana. Mabomba yenyewe yamejikaukia!
    Ridhaa: Serikali imeanzisha mpango wa kusambaza huduma za maji na umeme katika sehemu za mashambani, hususan zile kame. Wanachohitaji ni subira tu. Na nadhani mwalimu wenu alisahau kuwaambia kuwa katika baadhi ya sehemu mna machimbo ya mawe ya ujenzi, vito, na hazina za mafuta. Wenyeji wana jukumu la kutumia raslimali hizi kujiendeleza.
    Tila: Alituambia hayo pia. Lakini kuna tayari kampuni za kibinafsi ambazo zimetumwa huko kuchimbua madini haya. Isitoshe, kampuni zilioshinda zabuni za kuyachimbua madini haya ni za kigeni. Uchimbaji wenyewe unafadhiliwa na wawekezaji wa kigeni. Raiya watafaidika vipi?Fedha zinazotokana na raslimali hii yahofiwa kuwa zitaishia kwenye mifuko ya wageni. Zinatumwa kuendeleza nchi za hao hao wawekezaji wanaodaiwa kuwa wawekezaji.
    Ridhaa: Ni kweli lakini kumbuka kuwa kampuni hizi zimebuni nafasi za kazi. Wenyeji wamepata ajira!
    Tila: Ambayo mshahara wake ni mkia wa mbuzi. Baba, kile ambacho raiyaa wanahitaji ni mabadiliko ya mara kwa mara ya uongozi na sera zenyewe za uongozilNa naona awamu hii, kama asemavyo mwalimu, wingu la mabadiliko limetanda.

11. Kisengere mbele.

Hii ni mbinu ambayo mwandishi hutumia katika sanaa yake. Inahusisha mwandishi kubadilisha wakati na kusimulia mambo yatakavyokuwa siku za usoni; au kutumia isiyo moja kwa moja kutabiri yatakayojiri. Mbinu hii pia huitwa utabiri.

  1. Katika ukurasa wa 45;"Sasa anapotazama nyuma anaona kuwa ule utabiri wa 'wingu la mabadiliko' wa mwalimu ulikuja Kutumia "Ni kweli mwalimu alikuwa ametabiri kuhusu wingu hili la mabadiliko ambalo kwa sasa limetanda
  2. (uk 44) Tila: Ambayo mshahara wake ni mkia wa mbuzi. Baba, kile ambacho raiyaa wanahitaji ni mabadiliko ya mara kwa mara ya uongozi na sera zenyewe za uongozi!Na naona awamu hii, kama asemavyo mwalimu, wingu la mabadiliko limetanda.
  3. Katika ukurasa wa 70;Lunga alikuwa ameona kuwa maisha yake yalikuwa yakielekea kudidimia hata kabla ya kuhamia makao hayo yake mapya ambayo anadai kuwa jaala kampeleka huko "Ametononeka si haba katika msitu huu. Hadiriki kuwaza kwamba msitu huu unastahili kuhifadhiwa kwa matumizi ya baadaye! Kabla ya jaala kumleta hapa, lunga aliuona mstakabali wa maisha yake ukiporomoka. Alikuwa ameipoteza kazi yake "

12. Njozi au ndoto

Mwandishi hutumia njozi au ndoto kutabiri jambo litakalofanyika au kufumbua jambo lililokuwa limefumbwa.

  1. Katika ukurasa wa 2; "Anakumbuka akimwambia mkewe Terry, "Milio hii ni kama mbiu ya mgambo, huenda kukawa na jambo "Terry kwa ucheshi wake wa kawaida hakunyamaza " "Ridhaa akamwambia, "wewe endelea kupiga hulu tu, lakini utakuja kuniambia!" Ridhaa alikuwa na ndoto ya kuwa kuna jambo mbaya au lisilo la kupendeza ambalo lingeweza kutendeka, na kwa kweli, njozi lake likawa ni la ukweli wakati lilipo timia.

13. Kejeli

Hii ni mbinu ya Sanaa inayotumia maneno kudharau au kukemea kitendo au mtu fulani. Mwandishi pia anatumia mbinu hii kuwasilisha maudhui yake kwenye kazi yake ya kifasihi.

  1. Katika ukurasa wa 15; "Kuna wale ambao hufia kwenye vitanda vyao vya mwakisu vitongojini baada ya kupiga haramu. Hawa husemekana kuwa wamekuwa nzi ambao kufia dondani si hasara. Hulaumiwa kwa kujitosa katika msiba wa kujitakia " Hawa watua mabao wanakunywa pombe haramu na kufia kwao nyumbani ambako kumekithiri ukata, wanadharauliwa na kulinganishwa na huyo nzi afaye kwenye donda, kwani wanafanya jambo kwa hiari yao, huku wakijua madhara na matokeo yake ni yepi.

14. Unukuzi kutoka bibilia.

Hii ni mbinu ya kunukuu visa tofauti kutoka kwenye Biblia. As sumpta K.Matlei amejikita sana katika mbinu hii ya kunukuu Biblia, kama tunavyoona kutokana na mifano ifuatayo.

  1. Katika ukurasa wa 36; "Aliweza kuudhibiti ugonjwa wa shinikizo la damu ambao ulitokana na mshtuko wa kupoteza jamaa na mali yake dafrao moja. Awali akijihisi kama yule Ayubu kwenye kitabu kitakatifu ambaye ibilisi aliifakamia familia na mali yake takriban kutwa moja!"
  2. Katika ukurasa wa 46; "Umbali ulio kati yao, japo ni hatua tatu tu, waonekana kama upana wa bahari ya Shamu wakati Waisraeli walipokuwa wakikamia wokovu wao kutokana na dhuluma ya wamisri "
  3. Katika ukurasa wa 47; "Walishikana kukutu, kila mmoja akimwambia mmwenzake kimoyomoyo, "Ni hai!Sijafa!" Ikawa ni kama Yesu anamhakikishia "Tomaso asiyeamini","Tazama hii mikono yangu. Nipe mkono wako, utie ubavuni mwangu. Usikose kuamini tena.
  4. Katika ukurasa wa 34; "Baada ya kuishi kwenye msitu wa Mamba kwa miezi sita, Ridhaa, Kaizari na familia yake walibahatika kurudi nyumbani kufuatia mradi ulioitwa na wanaharakati wa kupigania haki za kibinadamu: Operesheni Rudi Edeni "
Join our whatsapp group for latest updates

Download FANI- MBINU ZA LUGHA NA MBINU ZA TAMATHALI/MBINU ZA SANAA- Mwongozo wa Chozi la Heri.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest