Friday, 14 April 2023 08:56

Kiswahili Lugha Questions and Answers - Grade 7 End Term 1 Exams 2023 Set 2

Share via Whatsapp

SEHEMU A
Maagizo
Soma kifungu kifuatacho. Kisha andika kwa mukhtasari uk ingatia yafuatayo:

  1. Maneno 130
  2. Iwe katiaka mtiririko
  3. Panga hoja zako katika aya tofauti
  4. Tumia maneno yako mwenyewe huku ukihifadhi ujumbe kamili

Sekta ya matatu nchini Kenya ina historia ndefu na yenye mabadiliko yasiyoisha. Je, unajua chanzo cha neno matatu?

Magari haya mwanzoni yalisafimrisha abiria mijini na kulipisha nauli ya mapeni matatu safari yoyote ile. Kwa muda mrefu nauli ikawa ni hiyo hiyo wakati wowote mwendo wowote. Kwa sababu hii yakaja kujulikana kama matatu. Jina hili likakubalika miongoni mwa wakenya wa jamii zote na hutambulika katika lugha zote nchini. Linakubalika pia katika lugha ya Kiswahili.

Muda mwingi sasa,magari ya matatu yalifanya biashara bila kutilia maanani nidhamu barasteni. Wenye matatu na madereva walikuwa hawasikii la mwadhini wala la mteka maji msikitini. Walipakia abiria magarini kama bidhaa na kubeba Zaidi ya kiasi kilichotakikana. Waliendesha magari yao kasi kama umeme huku wakishindania wasafiri. Utingo au manamba waliwashawishi wasafiri kuingia magari yao na hata kuwavuta au kutwaa mizigo yao wakielekeza kwenye matatu bila ruhusa ya wasafiri. Daima wasafiri walikuwa katika tishio la kuibiwa mali yao katika vituo vya matwana.

Baadhi ya wenye matwana waliendesha magari mabovu na yasiyofaa barasteni. Askari wa trafiki nao walikuwa hawajali bora tu wapokee kile walichokiita kitu kidogo' yaani rushwa. Waliruhusu magari yaliyovunja sharia kubeba abiria. Matokeo ya mambo haya ni ajali nyingi barasteni. Maelfu ya watu waliyapoteza maisha yao na wengine wengi kujeruhiwa na kulemazwa katika ajali za magari. Kwa kweli ulikuwa usiku wa giza.

Hauchi hauchi kunakucha na hakuna marefu yasiyokuwa na mwisho. Mwanzoni mwa mwaka wa elfu mbili na nne hali hii ilibadilika kabisa. Uliokuwa usiku wa giza ukawa mchana wenye nuru na matumaini makubwa.

Serikali kupitia kwa wizara ya uchukuzi na mawasiliano ilitangaza kuwa lazima magari haya yazingatie sharia zote za usafiri. Vilevile kila matatu lazima iwe na kidhibiti mwendo ili kupunguza ajali zinazotokana na mwendo wa kasi.

Magari haya yalitakiwa pia yawe na mikanda ya usalama na kila abiria,kondakta na dereva lazima ajifunge. Jambo hili lingesaidia kuzuia matatu kubeba watu wengi kuliko inavyofaa na aidha kuzuia abiria kuumia sana wakati wa ajali. Kila matatu ilitakiwa kuandika kabisa dhahiri shahiri pembeni mwake idadi ya abiria inayofaa kubeba na sehemu zile inafika.

Madereva na makondakta nao walitakiwa wavae sare ili watambulike kwa urahisi. Vilevile walilazimika kuwa na vitambulisho vya kazi. Dereva alitakiwa aweke picha yake mahali wazi garini ili abiria waweze kuthibitisha kuwa wanabebwa na dereva afaae. Kuna leseni tofauti tofauti na stakabadhi nyingine ambazo kila matatu lazima iwe nazo kabla ya kubeba abiria. Hizi ni kama leseni ya barasteni, bima, leseni ya dereva na barua nyinginezo.

Askari wa trafiki nao walitakiwa kukoma kupokea kadhongo. Waliopatikana wakipokea mlungura walichukuliwa hatua kali na hata kupigwa kalamu. Vyombo vya mawasiliano kama vile runinga na magazeti vilichangia kutimiza haya kwa kuwatangaza askari wa trafiki walionaswa na kamera wakipokea rushwa.

Kwa viile serikali ilikuwa imara katika msimamo wake,sharia hizo zote zilianza kuzingatiwa. Matatu zilikoma kubeba abiria ovyo ovyo, zikawa na vidhibiti mwendo,mishipi ya usalama nanidhamu ikawapo katika sekta hii. Abiria sasa hufurahia safari zao na huwa hawana hofu wanapokuwa safarni kwa kuwa ajali za barabarani zimepungua kabisa. Zamani abiria walisafiri roho mkononi, lakini leo huwa wamestarehe. Si ajabu wengine hujipumzisha kwa kulala garini na hivyo kufika waendako wakiwa si
wachovu.

SEHEMU B UFAHAMU

Mtoto anapozaliwa huwa mchanga kiwango cha kutojielewa. Akili yake huwa bado changa kiwango cha kutojimudu. Kila mara kile ajuacho ni kilio tu. Kilio chake huashiria mambo mengi yakiwemo njaa,kuumwa, kuugua au kutaka kubadilishwa viwinda. Akili yake huwa kama karatasi nyeupe ambayo haijaandikwa chochote. Huwa hana habari kuhusu yanayoendelea duniani. Jambo la kushangaza ni vile mtoto hutambua mikono ya nina yake. Mtu tofauti anapombeba hulia kinyume na mamake. Mtoto hutambuaje kuwa aliyembeba ndiye mama? Mtoto hana uwezo wa kufahamu kitu anachopewa kama kizuri ama kibaya. Yeye hufurahia tu kile anachopewa na hudhania kuwa kinafaa.

Baada ya siku kadhaa,mtoto huanza kujua na kuanza kutambua watu vizuri. Mtu wa kwanza kutambuliwa ni mamake. Wakati huo yeye huwa ni bubu anayefurahia na kucheka bila sababu yoyote. Mtoto ana uwezo wa kuchekea hata makaosa. Akiona mtu analia yeye hudhani kua anamchekea.

Anapofika umri wa miezi sita,mtoto huanza kupewa uji,maziwa na vyakula viororo. Mtoto hulishwa kwa kijiko baada ya kufungwa kimori ili ngou yake isichafuke. Mama huhakikisha kuwa chakula cha mwanawe ni laini ili kisimsakame.

Kila mara tumesikia watu wakisema kuwa fulani anazungumza lugha ya mama. Mtoto hujifunza kutokana na mama yake. Mtoto humpapasa mama yake kwenye mashavu akihisi ulaini wa ngozi yake. Hapo yeye huwa makini sana akifuata jinsi mama yake anavyozungusha midomo yake. Wakati huo mtoto huyo huanza mazoezi ya kufanya jinsi mama yake anavyofanya. Hii ndiyo maana tunaambiwa kuwa mwalimu wa kwanza wa mtoto ni mama;ndiposa tunapigiwa methali kuwa asiyefunzwa na mamake hufunzwa na ulimwengu.

Wakati huo akili ya mtoto huanza kuandikwa kwa kalamu ya mate. Maandishi hayo huweza kufutika wakati wowote iwapo hatayazoea kwa muda mrefu. Wakati huo yeye hujifunza kutamka neno mama,neno ambalo kila mara huwa ndilo la kwanza kwa mtoto kulijua na kulitamka. Basi huo ndio kuaji wa mtoto. Jambo hili na hatua hizi huhutaji uangalifu mkubwa sana ili mtoto huyu awe mwadilifu. Kumbuka mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Na wimbo mui hauongoi mwana.

Jibu maswali haya

  1. Kwa nini mtoto huwa hawezi kujitegemea katika maisha yake ya mwanzo kulingana na aya ya kwanza?
  2. Mtoto huwazaje kutambua mamake au kikono chake?
  3. Jambo gani haliwezi kumfanya mtoto kulia kulingana na taarifa?
    (njaa, maradhi, akiwa ameenda haja, akibebwa na mama)
  4. Mwandishi anasema kuwa akili ya mtoto huwa kama karatasi nyeupe. Ni nini maana ya maelezo haya?
  5. Kwa nini watu hurejelea lugha ya kwanza kwa mtu kuwa ni lugha ya mama?
    (ndiyo lugha ya kwanza kwa mtoto, hufunzwa na mama, huigwa na mtoto kutoka kwa mama, lugha inayosemwa na mama)
  6. Kiwinda ni vazi gani?
    1. Vazi la mtoto
    2. Aina ya kofia umbo la pia inayovishwa mtoto
    3. Vazi analofungwa mtoto wakati analishwa ili kulinda nguo
    4. Kitambaa anachofungwa mtoto sehemu nyeti ili asichafue nguo aendapo haja
  7. Mtoto anafaa aanze kupewa maziwa, uji na vinywaji vingine ili;
    1. Vimsaidie kukua haraka
    2. Vimsaidie aimarike akili yake
    3. vimsaidie aimarike afya yake
    4. vimkomaze mifupa na kumwongeza ukubwa wa mwili
  8. Kwa nini mtu huambiwa, asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu?
  9. Kwa nini mwaandishi anasema kuwa maandishi ya kwanza kwenye akili ya mtoto huandikwa kwa penseli?
  10. Habari hii inaweza pewa mada gani bora?
    1. Akili ya mtoto
    2. Makuzi ya mtoto
    3. Mama na mtoto
    4. Hatua za kukua kwa mtoto

SEHEMU C: SARUFI (Alama 30)

Jaza nafasi zilizoachwa wazi kwenye vifungu vifuatavyo.

__11__ wengi __12__ na uandishi wa insha za methali.Hawajui iwapo ni lazima mwandishi mwandishi
__13__kwa kutoa maaana ya methali ile au la. Ukweli ni kuwa mwandishi __14__ uhuru wa kutumia __15__ wake apendavyo bora atoe kisa __16__ dhahiri shahiri ukweli wa methali inayohusika.

Hivyo basi mwandishi __17__ kuwa __18__ waziwazi maana na matumizi ya methali ile. Iwapo ataandika insha isiyoambatana na methali yenyewe atakuwa amepotoka na ataadhibiwa kwa __19__ alama __20__ maudhui.

  1. (watahiniwa, watahiriwa, watahini, wastahili)
  2. (hutakiwa, hutatizika, hukatiwa, hupatiliwa)
  3. (lanze, waanze, aanze, anaanza)
  4. (Yuko, iko, hana, ana)
  5. (uandishi, mtihani, ubunifu, kiburi)
  6. (kinachopambanua, inayopambanua, kilichopambana, kunapambana),
  7. (ana budi, hana budi, hana bundi, hana fundi)
  8. (anaeleweka, anaeleza, anaelezwa, anaelewa)
  9. (kuongezwa, kutolewa, kupokea, kupewa)
  10. (wa, cha, la, za)

Kutoka nambari 21-40 chagua jibu kulingana na maagizo.

  1. Maneno yafuatayo yatapangwaje katika kamusi ya Kiswahili.
    1. Kushoto
    2. kushona
    3. kushuka
    4. kushika
  2. Andkia sentensi hii bila amba. Mti ambao ulioandwa ni huu.
  3. Taja maneno matatu yaliyo katika ngeli ya "I-I"
  4. Neno "watakaribishwa" lina silabi ngapi? (6,8,14)
  5. Ni nini maana ya msemo "ambulia patupu"?
  6. Taja jina la mwezi wa tano.
  7. Kamilisha methali: Penye nia
  8. Ni kiunganishi kipi kilicho sahihi kujazia pengo.
    Sitaki chai (sembuse, lakini, wala, ingawa) uji
  9. Laiti ningalijua nisingalijuta. Ina maana ya;
    (najuta kwa kutojua, sijuti kwa kujua, najuta kwa kujua, sijuti kwa kutojua)
  10. Alitabasamu baada ya kupandishwa hadhi. Kinyume ni;
    (alilia baada ya kuteremsha hadhi, alilia kabla ya kushushwa hadhi alinunua kabla ya kubezwa hadhi, alikasirika baada ya kunyafurwa hadhi)
  11. Chagua kihisishi kifaacho kukamilishia sentensi hii;
    ________________________________ ! Safari yetu imekuwa salama salimini.
    (Lo, Alhamdulila, Huree, Salaale)
  12. Tulijitahidi _______________________________tuwashinde wapinzani wetu hatukuweza.
    (ili, wala, ila, lakini)
  13. Tulinyamaza _______________________________tuliposikia michakacho huko nje. (zii, pu, jii, di)
  14. Kamilisha sentensi kwa ufasaha;
    Sikujui ____________________________alikohamia. (kule, wewe, mle, hapo)
  15. Chagua kifungu sahhihi;
    Sitalitaja jambo ______________________________
    (jinginelo/yoyote, jinginelo/lolote, linginelo/lolote, ingineo/lolote)
  16. Ni sentensi ipi inayoonyesha kivumishi kimilikishi?
    (Mtoto mtiifu hupendeza, Gari hili ni jipya, Nyumbani kwao ni kuzuri, Alifurahi bali hakucheka)
  17. Iwapo jana ilikuwa Ijumaa, mtondo itakua siku ipi?
    (Jumatatu, Jumanne, Jumatano, Jumapili)
  18. Jaza pengo kwa kiwakilishi mwafaka;
    ________________________________ mnafanya mzaha. (Nao, Nawe, Nanyi, Naye)
  19. Chagua tashbihi mwafaka; Watu hao wanashabihiana kama
    (Chanda na pete, kalamu na karatasi, shilingi kwa ya pili, mbingu na ardhi)
  20. Wasichana walioolewa na mume mmoja wanaitanaje?
    (mwanyumba, wakewenza, mawifi, mashemeji)

SEHEMU C

FASIHI-USHAIRI

Soma shairi hili kisha ajibu maswali.

Kilio cha wengi waja,nchini kote chasikika,
Ajali hatwishi taja, hii dhahiri hakika,
Pasi siku hata moja, bila haya kutendeka,
Mwito tuitike jama,mwendo sote kudhibiti.

Ujumbe huu twatoa, kwenu dereva husika,
Kutojali kuondoa,muanze kuwajibika,
Wahasiri kuongoa, raha yao kutimika,
Mwito tuitike jama,mwendo sote kudhibiti.

Jongomeo wengi kenda,pasipo wao kutaka,
Kwa manani wao walipanda, masaibu kuepuka,
Waachwa hawakupenda,hali hii kuwafika,
Mwito tuitike jama,mwendo sote kudhibiti.

Wengi yatima kabaki, wengine kawa wajane,
Wamebaki kuhamaki,akilini wasipone,
Wazalendo hatutaki, hai hii ienee,
Mwito tuitike jama,mwendo sote kudhibiti.

Dhibiti mwendo tuweke,maafa kuyapunguza,
Kanda sisahaulike,usalama kuhimiza,
Kulalama kuondoke,kwa madereva hasa,
Mwito tuitike jama,mwendo sote kudhibiti.

Nauli msipandishe,donda letu kutonesha,
Shauri mkaribishe,serikali kiamrisha,
Imani tuzidishe,yenu kazi shamirisha,
Mwito tuitike jama,mwendo sote kudhibiti.

Maswali

  1. Lipe shairi hili kichwa
    (Madereva, Waja kufa, Magari barabarani, Vidhibiti mwendo)
  2. Kwa nini waja wanalia?
    (Madrereva kuwajibika, kila siku ajali kutendeka, Kuondolewe kwa vidhibiti mwendo Kupanda kwa nauli)
  3. Mwandishi anazungumza na akina nani katika ubeti wa pili? (jamaa, waja, madereva husika, watu wote)
  4. Ni nini matokeo ya kutodhibiti mwendo katika magari ya abiria?
    (waja kufa na wengine kuachwa mayatima, waja kusherehekea madereva husika, nauli kupandishwa, mwito kuitia jama)
  5. Eleza maana ya neno "jongomeo" kama ilivyotumika katika shairi.
    (kwenda mbele ya barabara, kwenda mbele ya Mungu, masaibu, kulazimishwa)
  6. Vina vya kati ubeti wa tatu ni ________________________________(ne, ka, nda, ja)
  7. Shairi hili ni la aina gani? _______________________________(tathmina, Tarbia, Tathnia, Tasdisa)
  8. Taja kibwagizo cha shairi hili.
    (Vidhibiti mwendo, Mwito tuitike jama, mwendo sote kudhibiti, Kilio cha wengi waja, nchini kote chasikika, Jongomeo wengi kenda, pasipo wao kutaka)
  9. Kanuni za shairi huitwaje?
    (kughani, sheria, kanuni, arudhi)
  10. Shairi hili lina beti ngapi?  (6, 4, 10, 3)

INSHA

Endeleza Insha ifuatayo. Ifanye iwe ya kusisimua. (alama 40)

Tuliamka asubuhi hiyo tukiwa na matumaini ya .........................................................................

MARKING SCHEME

SEHEMU A - UFUPISHO ALAMA 10

SEHEMU B - UFAHAMU ALAMA 10

  1. Akili huwa changa
  2. Huangalia jinsi Mama anavyosongesha midomo
  3. Akibebwa na mama
  4. Hakuna ajualo kuhusu elimu
  5. Huigwa na mtoto kutoka kwa mama
  6. Vazi analofungwa mtotot wakati anakula ili kulinda nguo
  7. Vimsaidie kukua haraka
  8. Akikosa kuoata masomo ya mama, atapata ya ulimwengu
  9. Yanaweza kufutika haraka
  10. Hatua za kua kwa mtoto

SEHEMU C - SARUFI ALAMA 30

  1. Watahiniwa
  2. Hutatizika
  3. Aanze
  4. ana
  5. Ubunifu
  6. Kinachopambanua
  7. Hana budi
  8. Anaelewa
  9. Kutolewa
  10. Za
  11. iv, ii,i,iii
  12. Mti uliopandwa ni huu
  13. Chumvi, sukari, mvua, ,asali, kahawa n.k
  14. 6
  15. Kukosa kitu utakacho
  16. Mei
  17. Pana njia
  18. Wala
  19. Najuta kwa kutojua
  20. Alinuna kabla ya kubezwa hadhi
  21. Alhandulillah
  22. Ili
  23. Jii
  24. Kule
  25. Jinginelo/lolote
  26. Nyumbabi kwao ni kuzuri
  27. Jumannne
  28. Nanyi
  29. Shilingi kwa ya pili
  30. Wakewenza

SEHEMU D - USHAIRI ALAMA 10

  1. Vidhibiti mwendo
  2. Kila siku ajali kutendeka
  3. Madereva husika
  4. Waja kufa na wengine kuachwa mayatima
  5. Kwenda mbele ya Mungu
  6. Nda/da
  7. Tarbia
  8. Mwito tuitike jamaa, mwendo sote kudhibiti
  9. Arudhi
  10. 6
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Lugha Questions and Answers - Grade 7 End Term 1 Exams 2023 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students