Friday, 14 April 2023 09:56

Kiswahili lugha Questions and Answers - Grade 7 Opener Exams Term 2 2023 Set 1

Share via Whatsapp

Zoezi la 1: Kusikiliza na Kuzungumza

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5.
(Mgeni anamtembelea mwenyeji. Wanazungumza kuhusu matukio ya humu nchini katika siku chache zilizopita.)
Mgeni:      U hali gani ndugu? Nimekupeza mno mwenzangu (anamwangukia kifuani).
Mwenyeji: Ah! Hali yangu shwari bwana, si waona? (Wanacheka) Familia yako yaendeleaje huko ughaibuni?
Mgeni:       Wametononoka vilivyo bwana, namshukuru Mungu. (Kimya kidogo) Vipi bwana, naskia hali ilikuwa
                 tenge tahanani tarehe ishirini Machi, kulikuwa na....
Mwenyeji: Ooh! Jiji lilifuka moshi baba! Mrengo wa upinzani ulichochea maandamano kuishinikiza serikali    
                 kutimiza matakwa ambayo ....
Mgeni:      (Kinywa wazi) Matakwa yapi hayo?
Mwenyeji: Viongozi hao walilalamikia walichokiita hali ngumu ya maisha na bei ghali za bidhaa muhimu. Licha
                 ya hayo....
Mgeni:      Hebu subiri, hali hii ilizua madhara gani kwa mwananchi mlipaushuru?
Mwenyeji: Biashara nyingi zilifungwa, barabara nyingi zilifungwa huku hali ya uchukuzi ikiyumba. Si hayo tu,
                 baadhi ya shule zilichelewa kufunguliwa baada ya likizo fupi kutokana na hali duni ya usafiri na
                 usalama wa kutiliwa shaka.
Mgeni:      (Akimkagua) Mbona wachechemea huku macho yako yakiwa mfano wa damu?
Mwenyeji: Acha tu bwana. Maafisa wa polisi walirusha vitozamachozi tulipokuwa tukichapa  kazi. Viliniwasha
                 macho nikaamua kutundika miguu mabegani bila kuona mbele vizuri. Ghafla, nilitumbukia shimoni  
                 na kuteguka mguu.
Mgeni:      Eh! Pole sana mwenzangu. Nakutakia afueni.

  1. Kulingana na mazungumzo haya, ni bayana kuwa mgeni na mwenyeji wake
    1. daima huishi pamoja.
    2. ni wahudumu katika afisi za serikali.
    3. hawaishi pamoja.
    4. wanaishi ughaibuni.
  2. Ni nini maana ya wametononoka jinsi lilivyotumika katika ufahamu?
    1. Wamenenepa.
    2. Wamewanda.
    3. Afya yao inayumba.
    4. Hali yao i shwari.
  3. Ni kweli kuwa mgeni hana subira ya usikilivu kwa kuwa
    1. anamdakiza mwenyeji wake mara kwa mara.
    2. anataka kujua mengi kuhusu ughaibuni. 
    3. anampa mwenyeji muda wa kutosha kutoa maelezo.
    4. anamsikitikia mwenyeji wake  hatimaye.
  4. Kulingana na maelezo ya mwenyeji, mrengo wa upinzani ulitaka
    1. taarifa muhimu kuhusiana na uchaguzi mkuu uliopita kuwekwa wazi.
    2. bei za bidhaa muhimu zishushwe ili wananchi waweze kumudu hali ya maisha.
    3. makamishna katika tume huru ya uchaguzi na mipaka wateuliwe upya.
    4. viongozi wao na wa serikali wakae pamoja na kupata suluhu ya hali ngumu ya maisha.
  5. Kulingana na mazungumzo haya, maandamano ya tarehe ishirini Machi hayakuathiri
    1. elimu.
    2. uchukuzi.
    3. biashara.
    4. mapigano.

Zoezi la 2: Kusoma kwa ufahamu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 10.
Tausi ni ndege wa kuvutia sana. Rangi za manyoya yake huwa tofauti. Wapo wenye rangi moja tu. Si ajabu kumwona tausi mweupe pepepe akitanua mbawa zake. Wapo pia tausi wenye rangi mseto. Tausi wengine wamejaliwa rangi nyingi mwilini. Ukiwaona utadhani kuwa unautazama upinde wa mvua. Maajabu ya maumbile.

Tausi hufikiriwa kuwa ndege mwenye maringo. Yeye hutanua mbawa zake na kuzipepeta .kama njia ya kuwatumbuiza watu. Kwa kufanya hivyo, watu husema kuwa anaringa. Je, wewe
unafikiri kuwa tausi ana maringo au ni hali ya maumbile tu?

Ukweli ni kuwa tausi anapendeza. Ni ndege mpole na anayetumiwa kupambia mazingira. Chakula chake nikama cha ndege wa kawaida tu. Anapenda kula nafaka na wadudu. Wafugaji wengine wa tausi huwapa ndege wao chakula spesheli. Chakula hiki huwawezesha kuwa na afya. Huwafanya ndege hao kuweza kuzaana kwa wingi pia. Mimi ninampenda na kumthamini tausi. Je wewe?

  1. Kwa kuzingatia kigezo cha rangi, ni makundi mangapi ya tausi yameangaziwa katika aya ya kwanza?
    1. Matatu
    2. Manne
    3. Matano
    4. Mawili
  2. Tausi wenye kuleta mtazamo wa rangi za upinde wa mvua ni wale
    1. weupe pepepe.
    2. wenye manyoya ya rangi mseto.
    3. waliojaliwa rangi nyingi mwilini.
    4. walio na rangi tofauti tofauti za manyoya.
  3. Kulingana na makala haya,
    1. tausi hupendeza.
    2. tausi ni ndege mwenye maringo.
    3. tausi wengi hawawezi kula mchele.
    4. wafugaji huwapa tausi wao nafaka ili wazaane kwa wingi.
  4. Tumeambiwa kuwa tausi hutanua mbawa ili
    1. kuwatumbukiza watu.
    2. kuwavutia wanadamu.
    3. kuonyesha maringo yake.
    4. kuonyesha rangi za manyoya yake.
  5. Chakula spesheli cha tausi
    1. huwa wadudu na nafaka.
    2. huwawezesha kukua haraka.
    3. huhusisha wadudu na mboga.
    4. huwapa afya na kuwafanya kuongezeka haraka.

Zoezi la 3: Sarufi.
Tumia maneno uliyopewa kujazia vihasho 11 hadi 15.

 bumbuazi                    nchi                   mathalani                   kina                ufanisi 

Waliposema hakuna akweaye mbuyu na viatu, waligonga ndipo. Unapotazama maendeleo ya _____11_____ nyingine  ____12____ Nigeria, Uchina na nyinginezo, utapigwa na butwaa, sikuambii ____13____isiyomithilika! Chunguza kwa ____14____ chimbuko la maendeleo na ____15____ wa mataifa hayo. Utapata kwamba uongozi murua umepewa kipaumbele. Ufisadi  ulizikwa katika kaburi la sahau kinyume na yanayofanywa na baadhi ya wenzetu humu nchini.

Kutoka swali la 16-30, jibu maswali kulingana na maagizo. 

Tambua aina za nomino zilizopigiwa mistari. 

  1. Tulishauriwa kujikakamua ili kufikia kilele cha ufanisi.
  2. Makena alinunua marashi katika duka la mzungu.
  3. Umati uliokusanyika ulisambaratishwa kwa vitozamachozi. 

Tunga sentensi sahihi ukitumia maneno uliyopewa.

  1. Upendo
  2. Usafi
  3. Hasira

Ziandike sentensi hizi katika wakati uliopita hali ya kuendelea.

  1. Tutakuwa tukiimba wimbo wa taifa.
  2. Wageni wetu wamekuwa wakisafiri kwa feri.
  3. Mwalimu atakuwa akifanyisha mazoezi uwanjani.

Pigia mistari nomino za pekee katika orodha hizi

  1. Kuchora, ufefe, Agosti.
  2. Alhamisi, meza, unga.
  3. Ujinga, Mombasa, kuimba

Viringa viambishi vya hali ya masharti

  1. Ungemwona angekusaidia.
  2. Akikuambia umuone, tafadhari usisite.
  3. Ukipanda pantosha, utavuna pankwisha.

Zoezi la 4: Kusoma kwa ufasaha.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 -35.

Kiswahili ni somo la lazima. Si katika shule za msingi tu, hata za upili. Hili latokana na dhima na umuhimu wake katika nchi yetu. Kiswahili ni lugha rasmi na ya taifa. Ni lugha ambayo imetambulika kuwa na uwezo wa kuleta mshikamano na umoja wa kitaifa. Fauka ya hayo, Kiswahili si lugha ya tabaka au kabila moja. Ni lugha ambayo kila mtu wa kila kabila na rika katika taifa zima anaweza kudai ni yake, hivyo ni yetu sote.

Kiswahili ni nguzo katika ujenzi wa nchi. Kwa kutambua haya, katiba nayo ikakitambua Kiswahili. Bungeni, Kiswahili hutumika sawa na Kiingereza, hivyo kuipandisha lugha hii hadhi.

Lugha ya Kiswahili hutumika katika uchambuzi wa maarifa ili kudumisha jamii na kuyatawala mazingira. Lugha ya Kiswahili ni kama chombo kinachoweza kuelezea mapokeo ya itikadi za jamii zetu.

Shuleni, kufundishwa kwa Kiswahili kunadhihirisha vipengele fulani vya utamaduni wa mwafrika. Kupitia mafunzo haya, mwanafunzi hupata uwezo kutathmini mambo ili kuchukua na kuzingatia yale yanayoambatana na msingi ya taifa bora.

Lugha ya Kiswahili imeonyesha cheche za udhihirisho kuwa imesaidia sana katika kueneza maendeleo ya kisiasa, kielimu na kitamaduni. Kwayo, watu wanabadilishana mawazo, jambo ambalo ni msingi wa utangamano na ushirikiano.

  1. Kulingana na taarifa hii, Kiswahili kinawezaje kumfaa mwanafunzi wa Gredi ya saba?
  2. Katika kukithamini na kukitambua Kiswahili, katiba ilichukua hatua gani?
  3. Kidokezi kilichokolezwa mwanzoni mwa aya ya pili kinatoa dhana gani?
  4. Ni kwa vipi ambapo Kiswahili huwa kama chombo cha kuelezea mapokeo ya itikadi za jamii?
  5. Kulingana na paragrafu ya mwisho, Kiswahili kimedhihirisha maendeleo katika asasi zipi?

MARKING SCHEME

  1. C
  2. D
  3. A
  4. B
  5. D
  6. A
  7. C
  8. A
  9. B
  10. D
  11. nchi
  12. mathalani
  13. bumbuazi
  14. kina
  15. ufanisi
  16. Kitenzijina
  17. Wingi
  18. Makundi
  19. Tulishauriwa kudumisha upendo
  20. Usafi ni muhimu katika kutunza afya
  21. Tulijawa na hasira tuliposhindwa
  22. Tulikuwa
  23. Walikuwa
  24. alikuwa
  25. Agosti
  26. Alhamisi
  27. Mombasa
  28. nge
  29. ki
  30. ki
  31. Humwezesha kutathmini mambo
  32. Ilikitambua Kiswahili
  33. Umuhimu wa Kiswahili
  34. Kwa kuyarithisha maarifa yaliyochambuliwa
  35. Kisiasa, kielimu na kitamaduni
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili lugha Questions and Answers - Grade 7 Opener Exams Term 2 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students