Tuesday, 27 June 2023 07:49

Kiswahili Activities Questions and Answers - Grade 7 Mid Term 2 Exams 2023 Set 2

Share via Whatsapp

MASWALI

SEHEMU YA A: KUSOMA

UFAHAMU WA KWANZA
Soma taarifa hii kisha ujibu maswali yafuatayo.
Ukitazama miti na mito siku hizi utadhani kuwa ibilisi alikuwa amechukua usukani. Kama ingekuwa kweli, basi angekuwa amezishikilia hatamu za uongozi mbaya bila hata kujali. Inasikitisha kuona mito ikiwa imekauka kaukau nayo miti ikiwa imechomeka mithili ya ulimwengu wa jehanamu.
Binadamu wote walikuwa wakiomba kucha kutwa Mungu airehemu nchi yao. Joto lilikuwa jingi kiasi cha kuyeyusha milima kuwa nyika. Maji na chemchemi zote zilikuwa kama hadithi tu! Asubuhi moja tulijua kuwa Mungu hamwachi mja wake. Jua lilichoma tosi na kuashiria mwisho wa uhai. Kila kiumbe kilikiri kwamba hiyo ilikuwa siku ya siku.
Mwendo wa adhuhuri anga ilijawa na giza totoro. Ukungu ulitanda na kufunika ardhi nzima. Dhoruba zenye nguvu za kusi zilivuma na kung'oa miti hafifu. Nyumba zenye paa dhaifu pia ziliachwa zikikaa mahame.
Mara ngurumo za radi na umeme zikasikika. Mito na mabonde ilijaa na kufurika maji. Watu walikimbilia vileleni vya milima mirefu. Baridi ilijaa kote, hakukuwa na pa kujificha. Ama kweli lilikuwa gharika!

Maswali

  1. Kwa nini mwandishi akafikiri kuwa ibilisi alikuwa amechukua usukani?
  2. Wanadamu waliomba kucha kutwa, kumaanisha nini?
  3. Neno 'Nyika' jinsi lilivyotumika lina maana gani?
  4. Ni msimu gani unaodhihirika mwanzoni mwa hadithi hii?
  5. Dhoruba zenye nguvu za kusi zilileta madhara gani?

UFAHAMU WA PILI
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

Mimi humhurumia sana kumbikumbi. Huyu ni mchwa aliyeota mbawa. Maskani ya mchwa ni kichuguu, kidurusi, kishirazi au kingulima. Hayo ndiyo makao ya kumbikumbi. Kumbikumbi ni mchwa.
Huruma zangu kwa kumbikumbi sijui kama ni za kweli au ni za mamba. Aghalabu mvua ikinya, yeye hutoka ndani ya kichuguu kwa fujo, mbwembwe, madaha, maringo, majivuno, mikogo na kila aina ya kujionyesha. Swali ni je, huwa wanaeda wapi?
Baada ya kutoka nje ya kichuguu, wao huruka ovyo ovyo huku na huko na kuanguka popote shaghalabaghala. Hapo mbawa zao hung'oka. Kazi kwisha! Kumbikumbi wengine wakiona. mwangaza wa taa au moto, wao huukimbilia na kutumbukia ndani. Kazi kwisha! Kumbe maringo yake ya kuruka ovyo ndiyo kuisha kwake. Maskini kumbikumbi. Namhurumia.
Wewe pia. Usipokuwa mwangalifu, maringo na kurukaruka bila tahadhari ndicho chanzo cha kuangamia kwako kama kumbikumbi. Nakuhurumia. Nawe, je, wajihurumia?

Maswali

  1. Kisawe cha neno 'maskani' kama lilivyotumika katika kifungu hiki ni
  2. Ni msimu upi ambao kumbikumbi hupenda kuruka ovyo?
  3. Maringo ya kumbikumbi humdhuru vipi?
  4. Ni kwa nini msimulizi anamhurumia kumbikumbi?
  5. Ni funzo gani unalopata kutokana na hadithi hii?

SEHEMU YA B:
Jibu swali la 11 - 15 kutokana na taarifa hii.

Wanafunzi watukutu walitoroka kutoka shuleni wakaenda hadi kwenye shamba la Mzee Fimbo kuiba maembe. Watatu wao walipanda juu ya mwembe kuyaangua matunda. Wawili wao walibaki chini kuyaokota na kuyatia mkobani. Mzee Fimbo aliwaona kwa umbali. Akaja kinyemela bila yeyote kumwona. Ghafla, aliwakamata wale wawili akawafunga mikono na miguu. Walichapwa vibaya sana! Walilia kwa sauti lakini wapi!

Kisha mzee akawageukia waliokuwa mtini kwa ukali. Yafuatayo yalikuwa mazungumzo yao.

Fimbo: (kwa ukali) Shukeni nyinyi!
Watoto: Sisi si shuka. Ni blanketi.
Fimbo: Mwanichezea eeh?
Watoto: Wewe si mpira!
Fimbo: (kwa hasira) Nani amewaambia myaibe maembe yangu?
Watoto: (kwa madharau na kejeli) Maembe haya si yako, ni yetu sisi!
Fimbo: (akikasirika zaidi) Huu mti niliupanda mimi, ni maembe yangu!
Watoto: Wewe uliupanda zamani. Sisi tumeupanda hadi sasa hivi! Angalia tumeupanda na tungali juu. Sasa aliyeupanda wa kweli ni nani kati yetu? Ni mwembe wetu na maembe ni yetu! (Mzee Fimbo alirudi chumbani akiwa na ghadhabu sana kwa utundu wa watoto wale. Keshoye alifika shuleni na kuwaripoti kwa mwalimu mkuu. Walipewa adhabu iliyowafaa.)

Maswali.

  1. Kando na utukutu, ni tabia gani ya watoto inayojitokeza katika maongezi yao?
  2. Tambua na uandike tashbihi moja iliyotumika katika kifungu hiki.
  3. Mzee Fimbo alipowaambia watoto 'shukani' alimaanisha nini?
  4. Ni nini kinachoashiria kuwa watoto katika hadithi hii hawakuwa na adabu?
  5. Ni tofauti gani iliyopo kati ya neno 'panda' aliyosema Mzee Fimbo na waliyomaanisha watoto?

SEHEMU YA C
Chagua jibu bora zaidi kati ya yale uliyopewa kujaza pengo.

.................16..........................(Kikosi, Kigaro, Timu, Kikundi) cha Kenya kiliondoka saa moja na nusu asubuhi katika uwanja wa ndege. Kilitarajiwa .................17.......................... (kutoa, kupita, kuwasili,kuelekea) jijini Lagos .................18..........................(asubuhi, jioni, macheo, mapema) hiyo kabla ya kuunganika tena jijini Abuja  .................19.......................... (ambapo, ambao, ambayo, ambamo) kingekita kambi .................20..........................(wa, la, ya,za) siku mbili kabla kizaazaa chenyewe kutokea.

SEHEMU YA D: SARUFI
Chaqua jibu mwafaka kulingana na maagizo.

  1. Jibu maagano 'buriani' ni ........................................................
  2. Sahihisha sentensi hii.
    Ningeenda ningalimwona.........................................................
  3. Je, watoto wakitaka kulala huimbiwa nyimbo gani?
  4. Andika katika ukubwa.
    Kichwa chake kina jiwe.
  5. Kanusha sentensi hii.
    Wewe umechora picha nzuri.
  6. Tambua nomino na aina zake katika sentensi ifuatayo.
    Kitabu chake kina ramani ya Kenya.
  7. Mchezo ambao wahusika huvutana kwa kamba huitwaje?
  8. Taja tanzu moja ya Fasihi andishi.
  9. Andika katika wingi.
    Kucheka kwake kuliniudhi sana
  10. Taja sifa moja ya mtambaji.

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.

Andika insha ya kusisimua kuhusu;

UMUHIMU WA LISHE BORA

......................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

MWONGOZO

  1. Kulikuwa na jua kali lililofanya miti na mito kukauka.
  2. usiku na mchana wote.
  3. sehemu kave ambayo haioteshi mimea.
  4. kiangazi.
  5. kung'oa miti hafifu na mapaa dhaifu ya nyumba. 
  6. maskani- makan. 
  7. masika. 
  8. Hukatiza maisha yake anapochomeka/mbawa zake zinapong'oka kwa kuruka ovyo.
  9. Kwa kuwa anaangamia ovyo kwa maringo bila kutahadhari.
  10. Tusifanye vitu bila tahadhari kwa kuwa ndicho chanzo cha kuangamia kwetu.
  11. wizi/hawana heshima/adabu/nidhamu.
  12. walilia kama mbuzi.
  13. wateremke kutoka mtini
  14. wanavyojibizana na Mzee Fimbo bila kujali. 
  15. Mzee alimaanisha kuwa alitia mche/mbegu za mwembe mchangani nao watoto walimaanisha kuwa waliukwea mti wa mwembe.
  16. kigaro 
  17. kuwasili
  18. mapema
  19. ambapo
  20. ya
  21. buriani dawa
  22. Ningeenda ningemwona/Ningalienda ningalimwona.
  23. nyimbo bembelezi
  24. Jichwa lake lina jijiwe
  25. Wewe hujachora picha nzuri. 
  26. kitabu-kawaida Kenya pekee. 
  27. jugwe
  28. tamthilia, novela, riwaya
  29. Kucheka kwao kulituudhi sana.
  30. mkakamavu/mcheshi/ahusishe hadhira/mweledi wa lugha husika.

Mtungo

Angazia kanuni za usahihishaji wa mtungo kama hati. mtiririko, uasilia na ubunifu.

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Activities Questions and Answers - Grade 7 Mid Term 2 Exams 2023 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students