Monday, 04 September 2023 12:05

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 7 Opener Exams Term 3 2023 Set 1

Share via Whatsapp
 1. Soma mazungumzo haya kati ya Mzee Timoo na Hamisi kisha ujibu maswali yafuatayo.
  Hamisi:        Shikamoo Mzee Timoo? Unaelekea wapi asubuhi hii yote?
  Mzee Timo: Marahaba Mwanangu! Nimeteseka sana. Jana sikupata chajio. Naelekea kuomba
                       kiamshwa kinywa mahala popote.
  Hamisi:        Samahani sana Mzee Timoo. Hebu tuandamane na wewe kwenye hoteli Juma                                             ushughulikiwe ya Mzee
  Mzee Timo:  Asante sana Mwanangu kwa kweli Akufaaye kwa dhiki
  1. Kuna uwezekano kwa Hamisi na Mzee Timo walikutana wapi?  ( al 1)
  2. Matamshi gani yaonyesha heshima ya Hamisi kwa Mzee Timoo?( al 1)
  3. Je Mzee Timoo alikuwa anaelekea wapi?    ( al 1)
  4. Kwa nini Mzee Timoo anashukuru?    ( al 1)
  5. Kamilaha methali: Akufanye kwa dhiki    ( al 1)
 2. Jaza mianya iliyoachwa wazi kwa kuchagua jina mufti zaidi kwenye kijisanduku kilichoko hapa chini
  ( al 6 )
   watu, mmomonyoko, ardhi, kupenya, kusuna mabaya, dhidi, miti, mazito, mema

  Upanzi wa a.)_______ na nyasi unasaidia kuzuia b.)_______ wa udongo. c.)______ iliyopandwa miti huwa ngumu. Ugumu huo huzuia matone ya mvua d.)_________ ardhini. Mahali penye miti kadhalika huwa pamehifadhiwa e.) ________ ya mapigoi ya matone f.)________ ya mvua. Sote tupande miti.
 3. Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali yafuatayo
  Maisha ya vijijini yalimchekiza mno Amina. Daima alilalamika ukosefu wa vyombo za kisasa kama vile barabara za lami, magari ya kifahari na majumba ya starehe yaliyokuwa mjini. Haikumpita kamwe kuwa siku moja atakinaishwa na maisha haya.

  Amina alijituma jijini mara tu baada ya kukamilisha masomo yake ya darasa la sita. Kama ghulamu yeyote yule wa umri wake, alikuwa na matamaniona ndoto za ajabu. Alijiona akiendesha mojawapo ya magari yaliyokuwa yakiendeshwa na wapita njia. Alitamani kuishi katika jumba nzuri kama aliloishi mjomba wake laiti angalilipa wazo zito shauri la babake la kuliendeleza shamba lao kubwa.

  Miezi ya mwanzo aliona raha kuuamka asubuhi kutafuta kazi bora kuliko ya shambani. Akajiunga na wenzake kupigania vibarua ambavyo vilikuwa vimeadimika katika eneo la viwanda. Mara moja moja aliambulia kibarua cha sulubu ambacho kilichakazaa viganja na akili zake. Mara  nyingi hakupata chochote na ilimbidi kula mate, jikwambii kustahimili kelele za mwenye nyumba kwa kuchelewa kulipa kodi. Amina akaanza kuhofia na kutilia shaka ufanusi aliotarajia kupata.

  Siku zilivyosonga ndivyo hali ya kukata tamaa. Ilivyomsonga. Maisha ya mji yalijaa vurumai na zogo ya kila aina. Kelele za wapiga maji, muziki wa kupasua maskio, moshi kutoka viwandani na magari makuumakuu, kelele za wachuuzi mitaani na mengine mengi. Haya yote hakuwa ameyatarajia pia kwamba ingembidi kutembea akishikilia mifuko yake ya shati na suruali asije akapoteza riziki yake. pekee ya siku.
  1. Amina alichukia maisha ya mashambani kwa sababu   (Al. 1)
  2. Neno ghulamu limepigwa mstari kinyume chake ni     (Al. 1)
  3. Amina alitembea mjini wakati upi hasa?    (Al. 1)
  4. Kibarua cha sulubu ni kazi gani?      (Al. 1)
  5. Amina kushikilia mifuko yake ya shati na suruali ni ishara kuwa kulikuwa na     (Al. 1)
  6. Taja mambo matatu ambayo Amina hakuyatarajia yatokee mjini     (Al 3)
 4. Andika wingi wa sentensi hizi.
  1. Choroto cha mawasiliano kitanunuliwa.
  2. Kifutio hiki ni cha kijana.
  3. Chamba cha mgeni kinafagiliwa.
 5. Kamilisha matumizi haya
  1. Masalkheri
  2. Sabalkheri
  3. Alamsiki
  4. Habari za kutwa
  5. Shikamoo
 6. Kamilisha methali
  1. Dua la kuku
  2. Mtaka cha mvunguni
  3. Fuata nyuki 
  4. Ulimi
 7. Kamilisha nomino za makundi
  1. Kadamnasi ya
  2. Wingu la
  3. ________________ ya ndizi.
  4. ________________ cha mtama.
  5. ________________ cha kuni.
 8. Andika majina ya maumbo haya.
  G7SwaT3OS12023Q8
  _________________        __________________       ________________________
 9. Andika sentensi hizi kwa nyakati ulizopewa katika mabano.    ( al 4)
  1. Mwalimu Waichugu analima shamba lake. ( uliopita )
  2. Mama atapika ugali. (uliopita )
  3. Wazazi watakuwa wakiwapeleka watoto shuleni. ( uliopo hali ya kuendelea )
  4. Bw. Makenzi alikuwa mtu mwongo sana. (Ujao hali ya kuendelea )
 10. Kamilisha makao ya wanyama kwa kuchagua jina mufti kwenye kijisanduku hiki.
   kombe, zizi, vidoleni, uchango, kizimba, utando, tundu
  1. Makao kasuku ya ______________________
  2. Makao ya ng'ombe ______________________
  3. Makao ya konokono ______________________
  4. Makao kuku ya ______________________
  5. Makao ya funza ______________________
  6. Makao ya buibui ______________________

MARKING SCHEME

 1.  
  1. Njiani
  2. Shikamoo
  3. Mahali popote angesaidika
  4. Aliahidiwa kununuliwa vyakula
  5. ndiye rafiki
 2.   
  1. miti
  2. mmomonyoko
  3. Ardhi
  4. kupenya
  5. dhidi
  6. mazito
 3.  
  1. Kulikuwa na uhaba wa ukosefu wa vyombo vya kisasa.
  2. Gushi
  3. Pindi tu malipomaliza masomo ya darasa la sita
  4. Kazi ngumu
  5. Kulikuwa na watu wa mikono mirefu.
  6.  
   • kukutana na wachuuzi wengine
   • wapiga mtindi kupiga kelele
   • viwanda mbalimbali kutoa wingu la moshi
 4.  
  1. vyombo vya mawasiliano vitanunuliwa
  2. Vifutio hivi ni vya vijana
  3. Vyumba vya wageni vinafagiliwa.
 5.  
  1. Masalkheri au aheri
  2. Sabalkheri
  3. Binuru
  4. Salama au sina la kuamba
  5. Marahaba
 6.  
  1. Halimpati mwanawe
  2. Sharti ainame
  3. Ule asali
  4. Hauna mfupa
 7.  
  1. watu
  2. nzige
  3. chane
  4. kipeto
  5. kitita
 8.  
  1. mche mraba
  2. mche duara
  3. mche mstatili
 9.  
  1. Mwalimu Waichuge alilima shamba lake
  2. Mama alipika ,ugali
  3. Wazazi wanapeleka watoto shuleni
  4. Bw. Makenzi atakua mtu mwongo sana,.
 10.  
  1. tundu
  2. zizi
  3. kombe
  4. kizimba
  5. vidoleni
  6. utando
Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 7 Opener Exams Term 3 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students